BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“APACHE WACHA POMBE”-THE NGOMA AFRICA BAND June, 23, 2008

Filed under: African Pride,Burudani,Muziki,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 2:09 PM

Bendi ya kitanzania,The Ngoma Africa Band,yenye makazi yake nchini Ujerumani hivi karibuni imetoa single yake mpya inayokwenda kwa jina Apache Wacha Pombe.Single hii tayari inatamba katika vituo mbalimbali vya radio huko Ulaya na pia Afrika Mashariki.Upo katika mahadhi unayoweza kuyaita Bongo Dance.

Kama kawaida yao,The Ngoma Africa Band,wamekuja tena na wimbo mwingine wenye kuchezeka vizuri lakini wakati huo huo kubeba ujumbe muhimu kwa wanajamii.Pombe,pombe,pombe.Apache anaambiwa aache pombe ili apate uwezo wa kuwekeza kwenye elimu ya watoto au familia.

Katika wimbo huu,Ras Makunja(kiongozi wa The Ngoma Africa Band) anaimba na Christian Bakotessa a.k.a Chris B.Usikilize wimbo Apacha Wacha Pombe kwa kubonyeza player hapa chini.Bab Kubwa The Ngoma Africa Band,endeleeni kupeperusha bendera yetu huko mlipo.

Advertisements
 

21 Responses to ““APACHE WACHA POMBE”-THE NGOMA AFRICA BAND”

 1. mwakipesile Says:

  hiiiiiii!!!!!!!!! hapa ulipo fikishwa mziki kikwetu bongo!!
  naona wanamziki wamesoma mengi nakufikia mahala
  pa kutisha na nyuzi bin nyuzi,mdundo swafi kabisa,
  ujumbe muhimu tene unafuatana na wakati,kwa kuwa sasa
  watu wengine wameweka mbele pombe kuliko elimu ya
  watoto wao.
  Bab kubwa wazee BC !?inaonekana mna Azina yenye
  wanamziki wa kutisha?

 2. John Says:

  sasa kazi hipo!naona vichaa wetu wamerudi na vijembe
  vipya kama kawaida yao! hawapitwi na jambo,washaona
  kuna watu fulani wamesahu ofisi zao kwa hajili ya pombe,
  vichaa nawakubali moto wao! na midomo yao haifichi kitu?

 3. Aruna Says:

  He!e!eh vibosile wa BC !! hizi kali mezitoa wapi?
  naona vijana wataki utani kabisa mbele ya shughuli yao,
  lakini hawa jamaa nasikia hizi ndizo zao za kurusha mawe
  ya moto,unasukiliza beat zao kali na ujumbe mzito
  wa kutisha!

 4. Salma Says:

  Chonde! Chonde !Pombe,pombe,pombe
  kuna watu pombe ndio wanafanya maji ya kunywa?
  na kujisahau kabisa kuwa wanamajukumu katika familia
  zao! yasemwayo yapo,hawa wanamziki !wameona mbali
  wanayajua matatizo ya jamii zetu,ujumbe wao una uzito
  mkubwa

 5. DUNDA GALDEN Says:

  UJUMBE MUWAFAKA MDUNDO MARIDHAWA KWELI
  ILI KUNDI LINA MIZIKI MIZURI.PEPELUSHENI BENDERA
  MNAJITAHIDI SANA
  BC MIM NATAKA CD ZAO HAWA JAMAA NITAPATAJE?
  Chai goda

 6. Annie Says:

  Yaah!!! I have given it a listen. It’s a great number…It is my first time to come accross this group but they seem to be gud in music. Wish them the best.

 7. Gracy Says:

  Haisey? hawa watu wanafanya kweli? unajua mi nilifikili utani
  nilipokuwa nasoma jarida moja kuwa mziki wa tanzania umeinyakua ulaya !hapa nimekuwa bubu sina neno!

 8. mswahili Says:

  Kaka Ras Makunja Kulikoni?
  Mbona mawe mazito wamekukera nini tena walevi?
  au wamekojolea barazani kwenu? naona mawe mazito kweli uliyo
  warushia!!!!

 9. binti-mzuri Says:

  nilikua siwajui..we salma umenichekesha though..hahahah

 10. Matty Says:

  Kaka yangu mpendwa Mswahilini ulikuwa wapi?ni kitambo sijakusikia hapa, afadhali umerejea maana lugha inachafuliwa mno siku hz!
  Haya karibu tena …tutafika tu!

 11. Mruguru Says:

  Ras Ebby Makunja !bwana kichwa ngumu na wadogo zako watoto nunda Ngoma Africa band kulikuwa kimya kiasi fulani hapa? mlikuwa wapi ? maana si kawaida kuwaga kimya kwa miezi miwili bila kusikia kuwa mshazua zogo au balaa kimziki!
  kumbe mlikuwa mnapika zogo jipya? hili sasa soo la walevi?
  duh? hapa inabidi niwapigie saluti.

 12. Swai Says:

  sasa hii! kali kuliko zote,
  hapa naona BC mmefanya kweli! inaelekea vijana hawa
  moto wao haukamatiki! kumbe BC uwa mna majeshi ya
  ziada? sasa hawa labda tuwaite republican gard? au?
  huu mziki wao sio wa kitoto kidogo hata sikumoja
  BC yinyi kweli ni wavumbuzi wa mambo

 13. Sensei Romi( Rumadha) Says:

  Ras Kunja( Makunja),
  Inapata miaka mingi sana zaidi ya ishirini tokea tutimke pale home, hongera sana na mafanikio ya kimzika wa Afrika!!.
  mimi nduguyo,
  Rumadha.

 14. MapigoSaba Says:

  wameiga wimbo wa Samba Mapangala “Vunja Mifupa Kama Meno Bado Iko”………………..hawana jipya!!!!!!!!!!!!!!!!!

 15. hombiz Says:

  Apache aache chakula tena!!? Nyie “The Ngoma African Band vipi? Apache sukuma kete hadi King!

 16. Mbasha Says:

  SAAFIII SANAAA KWA KWELI NI NZURI NA PIA ALA ZA MUZIKI ZIMEKWENDA SHULE KABISA INAFURAHISHA. NATAMANI KUONA VCD AU DVD YAO ILI NIPATE MALIZA HUONDO . MUNGU AZIDI KUWA UBUNIFU ZAIDI ALL THE BEST

 17. Ngosha Says:

  Ngoma Africa Peperusha bendera hapo msisikilize watu fitina
  kati moja sukuma kete hadi kingi wakati ndio huu

 18. Dunia Says:

  Hii! Sema Mchana Usiku Ulale Ngoma afrika hutoiweza!
  naona wanajibu shutuma zote za wale wanao usaliti miziki wa
  tanzania ,hakiwemo huyo juu mapigo saba! sikiliza wimbo na text chours na beat au tyuni kabla ujakulupuka kutoa maoni,
  wanangu fagilieni bongo wakati wenu sasa

 19. Rich Says:

  HII!!!!!!!! JAMANI HII NI FUNGA KAZI YA MWAKA!!!!
  MZIKI POA,UJUMBE NI SOMO KWA JAMII,MPANGILIO WA VYOMBO
  MAHESABU MAKALI!!!!!! HII BAB KUBWA

 20. Didy Says:

  Hey !BC
  mwe mwe ! teh! teh ewe BC nakubali tena napiga magoti nyie mwisho,hawa huu mziki wao utafikiri hawana hakili nzuri?
  namwaga manyanga

 21. R.M Says:

  Ujumbe kwa sensei Rumadha

  Kunladhi wadau hapa barazani Naomba mtoa maoni namba
  13 Sensei Rumadha (Romi) Fundi tuwasiliane,acha anuani kwa
  hapa bc. tutaipata tu
  sisi nduguzo wa uswahilini,


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s