BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAMBO NINAYOYAMISS KUHUSU TANZANIA. June, 24, 2008

Filed under: Burudani,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 1:13 PM

Hii ya leo ukipenda unaweza kuiita “kibwagizo”.Rafiki mmoja wa BC(Peter S.Nalitotela) hivi karibuni aliandika orodha ya vitu takribani 51 anavyovimiss kuhusu Tanzania.Hivi sasa yeye anaishi “ughaibuni”.Mara wazo likanijia, kwanini tusiwape watu wengine nafasi ya kuiendeleza orodha hii? Wewe(hususani kama uko nje ya Tanzania) unamiss nini?Kama uko nchini Tanzania hivi sasa,mambo gani unamiss ambayo hapo zamani yalikuwepo na siku hizi hayapo tena?Kwanza isome orodha ya Peter kisha…kazi kwako.Kumbuka ni Tanzania nzima na sio lazima Dar-es-salaam peke yake.

1. Samaki Samaki Bar
2. Club Maisha
3. Listening to “Power Breakfast by Masoud n Fina Mango” on the drive to work asubuhi
4. Chilling at SANAA PUB after work while waiting for the rush hour traffic to pass
5. Kiti-moto (sorry to my Muslim friends, no offence) esp Lufungira
6. Jackie’s Bar
7. Garden Bistro (always fun)
8. Mzalendo Pub
9. Ngwasuma
10. Twanga pepeta
11. La Tarverna
12. Mchemsho
13. Supu (esp ya mbuzi… and even more so after a night of drinking)
14. Chips Vumbi

15. Teksi za kukopa kwa dreva wako wa kila siku (siku mzee ukiwa uko mbaya)
16. Bills (hate it or love it.. there r tones of new clubs now, but most f us grew up with Billicanaz)
17. Mikadi Beach (and other Kigamboni Beaches) (never got to go the last 15 months I was home.. but still love it)
18. UDASA (for people who grew up or worked at or near chuo area know what I’m talking about).
19. Being able to talk your way out of almost any trouble.. and if you can’t talk, bribe your way out.
20. NO WINTERS!!!!!!!!!!
21. Nyama choma, mishkaki, kokoto..
22. Akudo Sound
23. East Africa TV
24. Watching the English Premier League at Q-Bar or Meeda on weekends
25. NO LAST CALLS
26. USUALLY NO LINE UPS AT CLUBS
27. NO BEING ID’d AT THE CLUBS
28. Clubs/Bars open till dawn
29. Irish Pub – Msasani (very nice place)
30. Kuku wa kuchoma wa Rose Garden
31. A-City (Arusha) – my adpoted 2nd home
32. Sabasaba (Hotel 77) Arusha
33. Villa Park – Mwanza (a very chill-axed place. Be sure to visit when u r in rock city)
34. Club 84 – Dodoma (only non-smocking club in Tz I have been too – good music too)
35. Kuku wa kuchoma wa Rose Garden (ya Dodoma, sio Dar).
36. Morogoro – always a party town ingawa no real classy clubs siku hizi
37. Chaggah Bite (there’s just something about the place… it’s not fancy or pretty… but somehow always manages to bring the best outta people)
38. Sweet Easy (mliokuwa ma-regular wa mitaa ya Oysterbay Hotel zamani mtapapenda hapa if u know what I mean, haha. Jovin, Xris? haha kidding bros).
39. Slipway
40. New Light Night Club, Dodoma
41. Tripple A, Arusha (has become kinda shady n full of wana-apollo of late, but deserves to be here for it’s past exploits of the clubs scene in A-City).
42. La Casa Chica, Tanga
43. Pirated/bootlegged DVDs with 15 movies in them for TZS 5,000/=
44. Seasonal interests n jumping on bandwagons – eg. Taifa Stars/uwanja mpya
45. Bongoyo Island (Paradise off the shores of Dar)
46. Bar/Club hoping culture (1 of my favorite things)
47. Mafuta hajazwi kwa tenki au liter. Ni kwa sh 500/buku (esp vihiace/taxi).
48. TGIF
49. RBA Kili League (ok.. enzi zile, maana siku hizi siufuatilii kwa sana). Go Vijana m I guess Chang’ombe n Spiders (coz of my boyz)!!!
50. Dar Es Salaam Young Africans (YANGA) a.k.a Vijana wa Jangwani!!!! 😀
51. Serengeti Lager, Kilimanjaro Premimum Lager, Konyagi

 

97 Responses to “MAMBO NINAYOYAMISS KUHUSU TANZANIA.”

  1. Bablii Says:

    BC yote tisa, kumi mie namiss vifuatavyo;

    1. Wanawake wenye shepu za kibantu (mambo flan ya transforma).

    2.Traveltine mambo ya Jahazi na Melody

    3. Supu ya pweza

    4. Masheli sheli na kombe

    5. Haluwa

  2. Celine Says:

    52. Kiti moto cha Siri yako (Hunters club) Kinondoni. Ni kizuri kwa wasiopenda mafuta maana ni ya kuchoma. Ni tamu usipime!

  3. Rodney Says:

    1. Mabinti warembo/wazuri wanaojutuma katika shuhuli husika!!!
    2. Supu ya mkia
    3. Ugali halisi na makende ya ngombe
    4. Supu ya ubongo

  4. hans Says:

    mie na-miss vi2 vingi sana, lakini kukubwa kama huna kitu unaweza ukaenda bar yako( bar uliyozoeleka) ukakopa vinywaji kiasi utakacho na jamaa akakuamini na ukamletea hela yake siku nyingine, kingine jioni ukitoka kazini unapitia kijiweni kwa washkaji mnapiga soga na kufurahi pa1, pia mademu wa kibongo wazuri sana na wakarimu sio kama wa huku (lakini na ngoma pia ipo juu sana). kwa kweli nikikumbuka nataka kutokwa na machozi

  5. any Says:

    ivi lazima viwe vya BAR, club, sexy gals/men or we can go freestyle? naona mtiririko ni mwendo wa kujirusha tu.

  6. hombiz Says:

    Mimi nina-miss mambo yafuatayo:
    1. Pesa za BOT (EPA)
    2. Ushahidi wa hayati Balali
    3. Hoja za marehemu Amina Chifupa awapo Bungeni R.I.P.

  7. baker Says:

    Ebwana always home sweet home uko na miss kila kitu!
    1.masela kupigana mizinga
    2. watu kuku beep kwenye simu
    3.kwa maparty ndo balaa apo kona bar daily apo pako full sherehe
    4.Ebwana sweety aesy ndo kabisa lovely place
    5. ebwana yako mengi!!!!!!!!!!!!

  8. lilian Says:

    oo mi na miss sana sama kanisa langu la mabati buguruni kwa malipa kwa mzee salu bwana apewe sifa

  9. fatma Says:

    Nawamiss sana wazazi,ndugu na jamaa zangu, hata majirani wetu pale Keko. Nakumbuka utani, furaha, makelele and mostly the feeling of freedom.

  10. niko Says:

    nalitolela uko wapi wewe, tupe haabri zako zaidi, na unafanya nini uko uliko, hebu tueleze sisi wenzako wa bc, tukujue zaidi.

  11. Mtu kwao Says:

    WE unafikiri usipomiss starehe vitu gani vingine utamis bongo k.m sio jua kali,matope mvua ikinyesha, fallen na kero za daladala. Mi naunga mkono washikaji hapo juu,kuongezea list na mimi namiss nyama choma na kilimanjaro baridi, viyepe yai au chips chafu hasa za uswahili na amerikan chips,kinondoni ni tamu jamani. michemsho k.m ka. na ukienda bar hukosi mtu unayemjua

  12. DUNDA GALDEN Says:

    WAZAZI NDUGU JAMAA NA MARAFIKI
    MIMI NA MISS CONGO BAR
    MCHEMSHO NA SUPU YA PWEZA KULE ILALA
    SEHEM ZA KIHISTORIA BMOYO MWAMBAO PRIMARY SCHOOL SAIGON.MAGOMEN.ARUSHA MOUNT KILIMANJARO NA KAOLE.
    MABINT WA KIBONGO NA CHACHANDU ZAO (ASHAKUM SIMATUSI) KOSA LA MAREHEM UZUNI TUPU LAKIN UKWELI NDIO HUO…
    RADIO TANZANIA NA VIPINDI VYAKE KAMA WATU NA MATUKIO.
    MWIMBO WA TAIFA MUNGU IBARIKI TZA STEEL HARD TIME..
    END OF STORY WANASIASA NA NYIMBO ZAO ZA KILA MWAKA
    MWIZI ANAPOCHOMWA MOTO KWA WIZI SIMU NA KUACHWA WAKONGWE WA UFISADI NAOMBA KUWAKILISHA WAJUMBE NDIOOO
    AMAN KWENU VIONGOZI WAADILIFU J.K,SHUKURU MSINIKOPE
    MUNGU AWAZIDISHIE UPEO ZAIDI AMIN AMIN AMIN
    CHAFOSA CHAI GODA

  13. Komredi Says:

    washikaji mimi namiss sana makonda wachafu wa kibongo wenye tabia ya kutoa vichwa nje.
    pia namiss pilikapilika za kugombania magari
    nawamiss watu wa mbagala wanaopitia madirishani kwenye daladala. namiss sana maji ya vifuko vya plastic
    pia namiss kivuko kibovu cha kigamboni. nawamiss matrafick wa kibongo wala rushwa. namiss sana dagaa kigoma. nimelimiss soko kuu la kariakoo

  14. Renee Says:

    Mimi nakosa sana raha za Radio Tanzania na kipindi chao cha kila siku alfajiri “kumbukumbu za mwalimu”, kile kilikuwa ni kipindi changu cha kuamkia na kuanza kujitayarisha kwenda kazini. Oh, na “chombeza time” wakati wa kulala toka radio one.

    HAKUNA KAMA NYUMBANI!!

  15. kekue Says:

    Kaaazi kweli kweli, ss mimi namis nini ngoja; aya na mimi namiss naniii…mbege kule machame na chakula fulani hivi kinaitwa machalari.

  16. Amina Says:

    kwahiyo sisi tulioko bongo hatuna nafasi hapa..haya

  17. pandu Says:

    Mie namiss…mananasi kule kiwangwa kwa kina JK, Urojo wa forodhani, pweza wa hamsini pale kkoo, madem wa jolly,dagaa kamba pale ferry,trinity,every sunday pale slip way, ngwasuma pale makumbusho,pantoni kunasa tukienda mikadi,kuishi mbagala miaka 20 sijawahi kukaa kwenye kiti ndani ya daladala, machizi wa roba za mbao kule minyamala,back n days coco beach na washkaji, kina zavara, drob (rip), ksingle,fresh g, sugu,sos b, willy, terry, niga j aka prof jize, machizi wangu wa lwp…..concert za avalon na madem wangu wa forodhani sec…nikiwataja itakuwa soo maana wengine mmeisha kuwa wake za watu. Mishikaki ya mombo pale liverpoll rest…kuku choma wa itigi nikienda kgm, sehem za biere kama zimbwabwe pub pale mlandizi, segera tukiwa tuna enda ta, colabus a town na kina lilly kavishe sijui kama bado yupo 88.4 ya atwn…ni raha tuuuuuuu ili mradi ujue kuzichanga

  18. Ms Bennett Says:

    mdau lilian umenena ndugu yangu, we acha tu full upako

  19. Jesse Says:

    Mimi namiss sana Msasani Beach Club,Namiss sana kitimoto cha baa moja hapo Sinza kwa Remmy.

  20. Ed Says:

    Binafsi nadhani namiss sana chips za swahili street, namiss sana dala dala, kukaa kijiweni for no reason, kucheza draft kwa kubishana, pia namiss sana bara bara za vumbi.

  21. nuru Says:

    Hi,
    Mimi na miss sanaaa
    1. chips kuku za mitaaani, kama huna mshiko wa kutosha siku hiyo basi, unachukua “chips bubu”
    2. “Young at heart club”, aerobic classes, pale ukumbi wa Tambaza sec, yakiendeshwa and Mr Mohamed Mpangala. Sijui hii bado ipo hii club ya kina mama? Ex first lady pia alikuwa member
    3. Kelele za kwenye madaladala, sio huku ughaibuni kwenye matreni, mabasi, watu wanauchuna hakuna hata kuangalia pembeni. Ni kulala au kusoma gazeti/kitabu
    4. Mchana, lunch ya ugali na sato pale break point
    5. Taarifa ya habari ya saa mbili usiku, luninga ya ITV
    etc, etc, home is best!

  22. EdwinNdaki Says:

    Namiss shughuli(sherehe) zwa kwetu uswazi zikiambatana na Segere.

    VYAKULA NINAVYOMISS:
    -Injini(vichwa vya kuku) na brake(miguu ya kuku)
    -Ngisi na mchuzi wa pweza.
    -Zege(chips mayai) ukidondoshea na ukwaju.
    -Na miss sana kwa Dan,JJ,Mzee Robert,Mbezi(Ze mdudus meat)

    VINYWAJI:
    -namiss sana supa leta nyeupe.
    -Namiss sana Chibuku na gwagwa.
    -Namiss maji ya viroba

    LAIFU
    -Namiss sana mgao wa umeme
    -Mbu wababe wenye uwezo wa kupenya kwenye chandarua.
    -Pawa breki fasti,Njia panda(Clouds),rafiki(radio one)
    -Uswazi,Bongo planet,Friday naiti live(sebo)na Ze Commedy(EATV),
    -Roba za mbao walau kwa sasa sipigwi.
    -Ambiance…kona bar
    -Namiss tafrani pale abiria anapotoa nauli ya noti ya buku 10 asubuhi jinsi konda anavyomwakia.
    -Namiss sms za Tafadhali nipigie,tafadhalie niongezee pesa..

    BURUDANI:
    -Namiss jinsi wasanii wanavyozurumiwa na “mdosi” na bado wanaenda kumpa kazi awasambazie.
    -Namiss jinsi wavyobongo wanavyojirusha monday to sunday..wakisema SHIDA TUNAZO STAREHE HATUACHI.

    Mwisho namiss majina mazuri ya kibantu mfano:-
    Siyawezi,Sikuzani,Havinitishi,Sikujua,Mazoea,Chausiku,Kurusumu,Havijawa,Madobe,Mwadawa..

    KUBWA YA YATE…Tanzania ni sehemu nzuri sana ila inaumiza sana hao Mafisa wanavyotuongezea ugumu wa maisha.

    Tutembee mwendo wa cash nchi ilisha uzwa…

    Nakupenda Tanzania kwa moyo wangu woooooote.

  23. Matty Says:

    hahahahahahahaha! jamani leo nimecheka sana maana kila mtu kasema anachomiss hapa Any rafiki yangu ni free style kwa kwenda mbele.

    Mimi namiss yafuatayo.

    -Club bilicanas kujichanganya siku moja moja

    -Miziki ya kale pale Osterbay polis mess eg.Jojina na rangi ya chungwa.

    -Namiss ile kitu Pale darajani kwa Dan….Edwin Ndaki, Amina mpo?

    -Namiss ulanzi mtogwa …Gervas upo?

    -Namiss mambo mengi kwa kweli esp.mtori pale mitaa ya kati…Kekuu wapi tena?

    ni mengi kwakweli!!!!!!!!!!!!!!!

  24. Matty Says:

    Namiss pia SENENE JAMANI NILISAHAU Chris vp hapo?

  25. SALLY Says:

    Hee jamani! itmeans humu bongo celebrity wadau karibu nusu hawapo home mi nimefurahi tu maoni yenu kuna baathi ya vitu nimemiss pia lakini nimevisoma ila bahadhi hapana, mmenifurahisha sana kwa kukumbuka home inapendeza sana.

    All the best wadau wote katika kutafuta maisha inchi za watu na mungu atujarie tufanikiwe na tuwakumbuke ndugu zetu nyumbani kwa kidogo tunachokipata.

    Mungu wabariki wadau wote

  26. Nyachikwakara Says:

    Namiss yafuatayo:-

    1. Namna ambayo mgombea feki unaweza kuukwaa uongozi kwa danganya toto za kofia, ulabu, unga wa ngano na vifanana na hayo .

    2. Wezi wa elfu moja wanalazimishwa na sheria kurejesha walichoiba, wanajulikana hadharani, wanatolewa meno kwa vipigo, huchomwa moto na au kufia rumande au gerezani wakati wale wa Mabilioni wanaombwa warejeshe fedha kwa hiyari na bila kujulikana na wanaendelea kufurahia heshima na marupurupu kadhaa kama viongozi wanaoonewawiu tu.

    3.Watu kuamka na kukaa mbele ya duka/ biashara ya mtu bila kazi maalumu na kuanza kusogoa stori kibao na kubomu rafiki wanayeonana naye kwa kauli tata ya ‘mbona unanitenga?

  27. babu Says:

    namiss sana xxL clouds fm, pia namiss sana kitimoto pale kinondoni kwa mama yule wa kinyakyusa lakini kikubwa zaidi napamiss florida pub town pamoja na masela tunaopiga nao pool table florida

  28. polisi Says:

    mimi namis sana kitimoto cha mburahati,pamoja na jam ya magari wakati wa rush hours kurudi nyumbani.bila kusahau na mashimo barabara za mjini,mahindi ya kuchomz na chios za pale american chips.zilikuwa zinatusave sana alfajiri tukitokea Billz.We acha tu nyumbani raha na mcheza kwao hutunzwa.

  29. guide Says:

    namiss sana safaris (Tours) na kuku wa sakina bar a town. napamiss lushoto na mabinti wa kitanga
    i miss my fellow guides

  30. Stephan Says:

    kweli nammiss sana Baba wa Taifa Mwl J K Nyerere,namiss uongozi wa Rais mstaafu Ben Mkapa alijitahidi sana wakati wa uongozi wake balance of payment ya tz ilikua na surplus after so long but now imerudi deficit.
    Namiss miaka ya tisini vitu vilikua bei rahisi,namisi baridi ya Arusha.
    mi ni hayo tu.

  31. solange Says:

    mie namiss starehe za A- TOWN..77 club…galaxy…mtura wa soweto garden, foil ya nick pub…hahhaha home swity home jamani.

  32. binti-mzuri Says:

    kwakweli mi nammiss konyagi,no line up at clubs,ID(hata sie wazee wanatu ID loh!),no last calls..ukizima simu bongo ndio hivo tena,hujui kama ulipigiwa au lah..lol…kuchill slipway(japo naskia siku izi pamedoda)..na supu ya mbuzi chagga bite.oh na rose garden pia..aah..bongo!

  33. dogo-GLW Says:

    mie namiss kitimoto makuna bar plae kinondoni, nikifika tu ndio sehemu ya kwanza. kachumbari malima.
    nammiss mkapa, alikusanya hela nyingi kwenye kodi halafu wakajigaia…job true true

  34. Chris Says:

    Kwanza Matty mtani wangu na hizo nsenene, huzichoki? Hahahahahahahaa!

    Aiseeee binafsi………

    -Mzalendo Pub na zile firigisi chipsi

    -Nyama choma, mishkaki, kokoto-tena kokoto ya corner bar na mbuzi choma Rose garden

    -Mbuzi choma nazifataga Dodoma mnadani-jina nimesahau kidogo

    -Glonency Morogoro for live band ya kufa mtu… nakumbuka hadi nyimbo huwa naziimba-aluuuuuuh

    -La Casa Chica, Tanga-I went once nikija ni sehemu ambazo nimeplan kwenda tena

    -Castle na Serengeti are my faves biers!

    -Brakepoint naonaga picha blogs zingine naona hapajabadilika

    -Mchemsho wa samaki na mbuzi choma laini HUGO……

    -Na mapolisi unaowapiga mkwara kidogo wanatetemeka, very weak na wasio reason.

    -Police mess na club fulani iko karibu na TANESCO (Moshi mjini)…. kwa mitura, chama choma na hali ya hewa safi… bier unakunywa nyingi sana

    Anyway, since naenda the end of this week…. aluuuuuh!

  35. kimamy Says:

    mi namiss sana bagamoyo nawamiss wote namiss gongoni ,namiss samaki wa mzee songoro pale soko jipya duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu mmenikumbusha mbali sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

  36. coco Says:

    Nyama choma ya kwa sifaa kimandolu, mtori chapati Panama Bar sakina, kuku wa sakina bar, kelele za keni garden, kuku choma kwa khan, jamani nyumbani pametulia jamani

  37. TADE Says:

    DUH MIMI NA MISS
    1…CHUO CHA SANAA
    2…UWANJA WA MWANAKALENGE PIA BAGAMOYO SCULPTURE ASS
    3…BEACH BOY.BUDA BEAST.KASSAWA.R MPILI.MACO SAWE.MANGI CHEMELA NA MSACHO BEAST DUNDA STREETS,KOLICHI
    4….MIWA YA MTONI.
    5…..KABAL ZA JANGWANI.RADIO UHURU ENZI ZA MASOUD MASOUD
    6……WASHKAJI WANGU WA CHEMCHEM MIGOMIGO
    KANYABOA SOKONI KARIAKOO
    7..NYONGLOTA YA KULE MANTEP BILA KUMSAHAU NYONGO MKALIATABU

  38. wayajua Says:

    we bablii mtu wa wapi…nimeshangaa kuwa ulikuwa unaenda hotel traventine(halafu ulikosea spelling) ni hoteli ya mama Anna Mkapa,aisee wanapiga taarabu nzuri..si ajabu tulikuwa tunapishana..mi bado nipo huku

  39. wayajua Says:

    we chris nitafute basi!

  40. Debora kiaka kizuguto Says:

    Nawamiss sana rafiki zangu namiss sana familia yangu namiss sana sana wazazi wangu kupita huku uk namshukuru mungu misosi yote ipo mpaka bamia na ngongwe isipokuwa mchunga mboga ya kibondei na papa na perege wa kuchoma lakini mihogo kande mahage maboga kila kitu hapa tunamshuru mungu.

  41. Chris Says:

    Wayajua ntakutafutaje sasa! Sema ntakavyokupata, umejiweka nusu! Friday usiku ndani ya nyumba!

  42. Chris Says:

    Babli kuna kitabu fulani tuliongea umefikia wapi ndugu yangu! Maana end of the week naiona bongo hv hv. Kama umekipata niambie nikumuvushie e-mail mkubwa!

  43. BLACKMANNEN Says:

    -Na miss sana samaki wa kukaangwa Ferry, ngisi na nyama ya mbuzi katika Bar ya Mrems-Buguruni kwa Mabaamedi waliojaza nyuma!

    -Nawa miss sana marafiki zangu akina Ustaadhi Msuya, Msoka na wengine wengi tu huko Ukonga!

    -Jolly sio pabaya pia kupatembelea nyakati za jioni!

  44. Pearl Says:

    mtura wa soweto garden Arusha naumiss sana,chips za kwa bibiii karibu na mtaa wa bondeni Arusha nazimss ile mbaya,barafu za ukwaju,ngubiti na chakula cha Maiko IAA namiss ile mbaya.

  45. any Says:

    haaa, Matty kumbe ni freestyle.
    mi namiss foleni za kwenda bafuni kuoga kwenye nyumba za kupanga. Wababa kusimama nje ya bafu wanasubiri utoke huku na miswaki yao mdomoni na apo apo wanajadili yanga ilivolala jana.
    Namiss kutuma kibakuli kwa mama wa jirani kuomba mboga nilosikia akipika kwa harufu tu.
    Namiss UDA ekarusi, unagombea hadi unakatikiwa kandambili
    Namiss wakinababa kulala mwisho saa tisa usiku masaa yaliyobaki ni kuzunguka nje kuangalia kama vibaka wamepita
    Namiss siku ya Idd watoto wanazunguka mtaani wanakusalimia then wanaomba idd yao
    Namiss kukatikiwa umeme huku ulikuwa una beki keki au una wali kwenye rice cooker
    Namiss wakaka wa kiswahili wanavosimulianaga michezo ya kwenye tv kwenye daladala, huku wengi wao unakuta tv hawana walitizama kwa jirani through dirisha.
    Namiss ukiwa umepotea njia mtaani unauliza mtu mmoja ghafla unazungukwa kila mtu anakuelekeza nenda hivi kata pale, na unakuta sio kwenyewe, mradi wamejitolea kukuelekeza, badala ya kusema hatupafahamu.
    Namiss chapati za kupikiwa barazani unatuma mtoto anaendea alafu zinafungwa na gazeti, mafuta yanayonya ile rangi nyeusi na tunakula bila kujali, alafu ukimaliza kula unaishia kusoma gazeti hilo.

    ON TOP OF THAT, I AM MISSING MY DAD WHO PASSED AWAY BECAUSE OF A VERY WRONG PRESCRIPTION. ALIPEWA DOZE YA MALARIA, HUKU ANAUMWA PNEUMONIA. R.I.P DAD AND THE PERSON WHO DID THAT SHOULD GO BACK TO SCHOOL AND GET MORE HEALTH EDUCATION ILI ASIUE WENGINE ZAIDI.
    ASANTENI.

  46. Annie Says:

    Waoh!!!nice we have an opportunity to express what we miss once outside our beautiful Tanzania. For sure there a lot that I miss. You know it is hard to note that something is precious untill you miss it. On my part I miss the Tanzanian love…People back home are so friendly and warm…here It is not like that it is just hi!! end of the story. Again Tanzania is a peaceful Country. Out here where I am you cant walk out late in evenings and feel safe sometimes you dont trust even a person u walk together along the road. Well though we are still behind and the mafisadi keep on misusing our money yet Our country is the one to treasure we just need to deal with mafisadi and help our country develop.
    Yaahh!! I also miss our food like makande (samp), ugali and rice from Mbeya, here rice is not that delicious…Anyway…it is enough to say I miss home but life has to go on outside home sometimes.
    God Bless Tanzania and its people.

  47. Chris Says:

    Pole any for the negligence of that Doctor and so the loss of ur Dad. R.I.P.

    But umenichekesha sana kwenye hizo missings nyingine, hususani ya chapati na kusoma tena gazeti… aiseee kweli kbs.

  48. Matty Says:

    Jamani Any pole sana for your loss ila sote ndo njia yetu hata mimi nammiss dad wangu ila no way out.
    Ukweli hapa pamefuka moshi ni free stlye kwa kwenda mbele!

  49. Big Says:

    Ha..ha..ha nimefurahi!! mengi yametajwa ila “any” kanichekesha sana, mambo ya chapati (ya mafuta ya transfoma) kwenye kipande cha gazeti!! Bongo tumetoka mbali!!

    Kitu ninachoki-miss ni barabara ya tatu mjini Dar! Hivi bado iko!

  50. wayajua Says:

    Chris mwambie basi bongocelebrity wakupe email yangu.. au kama vipi,tupange sehemu tukutane..si unaelewa tena mambo ya kula raha!?

  51. any Says:

    Matty pole.
    Sijui namiss nini tena huko nyumbani? ngoja nifikirie then naja`

  52. makonde Says:

    Du mie namichi chamaki nchanga na taarifa ya habari inayosomwa na Devid wakati na kipindi cha jioni njema pia mchana mwema na kipindi cha ngoma za kienyeji cha yule jamaa anasema anakuja na manyanga yake studio jina nimesahau zamani mno na pia mtangazaji wa soka maguu sita ya mtu mzima kama unajua which one am talkin about na miss watu wanao nuka vikwapa ktk daladala za temeke lol na kipindi cha phillips Radio club cha julius nyaisanga bila kusaha club raha leo aaaaah mpaka chozi linanitoka manake nimeondoka bongo enzi za mwinyi pia na mmiss mzee ruksa

  53. Maybe Says:

    Any pole kwa yalikukuta ila umenifurahisha uliposema unakula chapati halafu unaishia kusoma gazeti lako.. hapo nakuunga mkono wangu nami namiss saana hiyo kitu, na kingine ni uswazi kama kawa wachawi njenje halafu ukitoka wanakusindikiza ukirudi km kawa… umekuja na nini ukibeba rambo tu wanataka wajue umekuja na nini uswazi bwana some time poa lkn mh!! pia namiss watoto wakigombana wamama wanaingilia na kugombana halafu watoto haoooo wanaendelea zao kucheza. Job true trueeeeeeee

  54. pyupyu Says:

    Hey,nyie mmesahau mishikaki ya vumbi,pitapita pembezoni mwa barabara jioni jioni hivi yani ni shilingi hamsini yako tu.

    daa na zile chachandu zao zinawekaa kwenye vichupa hata zaidi ya wiki mbili,basi balaa tupu.

    Jamani muhogo wa nazi uweke na kijisamaki chako na vijinyanya chungu,mmmh.

    Naalia kwetu nalia kwetu,siku itafika siku ikifika nitakula……..

  55. any Says:

    Namiss
    1. Makamba na vita ya machangudoa, kwa kumkomoa macd wakatuma message kuwa vita ni ngumu maana na yeye ni mteja, kakabu kakaja juu kweli, kumbe walikuwa wanamchokoza tu.
    2. Kesi ya kwanza kuandikwa na media kuhusu kubaka watoto, kesi ya Maumba, mjini mkipita na sketi za shule wapiga debe wanaita watoto wa Maumbaaaaaaaaaaaaaa!
    3. Wakati tunasoma tukawa wadada wanamwita Mwinyi shemeji
    4. Namiss JKT, mkitoka uchaka unalala kwenye mabweni ya wanaume kwa jinsi mlivopigika na kazi hakuna hata anaekugusa.
    Namiss jeshi, maana Jumapili ilikuwa ni siku ya kuongea English, why? wengi wanakuwa wamekunywa pombe za kienyeji, ivo kiswahili kinakuwa hakipandi.
    Jeshi unasingizia kuumwa, afande akiuliza unaumwa nini unataja neno lolote la kingereza, hata ukisema unaumwa banseni bana anakupa C na anakuambia inabidi ukalale usijetufia apa buree
    Namiis mama ntilie wetu, hata kama huna hela unakula unakuja kulipa mwisho wa mwezi.
    Namiss house maids wa nyumbani, hakuna job description, anakuja primarily kwa ajili ya kulea watoto, mara anaambiwa utakuwa unapika pia, mara vyombo, mara kusafisha nyumba, akikaa kidogo anaanza kuongezewa na kuangalia na kusafisha banda la kuku uwani na kuwalisha, kumwagilia mchicha nje mwisho anakabidhiwa gudulia la ice cream anaweka barazani akiuza ndio anapata apo mshahara wake. Nawamiss kweli wale maids, huku akija ni kuangalia mtoto ni mtoto tu, ukimpa extra work means extra cash.
    Nawamiss wale wamama wa gender issues wanavopigania haki za wanawake huku wao ni wanyanyasaji wa kwanza kuanzia home, wananyanyasa housegals na kuwa underpay, huku wakiwa jukwaani wanapinga unyanyasaji.
    Namiss kuchapwa bakora shuleni ukikosea hesabu, ukimwona mwalimu badala ya kufocus anachofundisha unaogopa zile fimbo. Namiss zile fimbo maana watoto wasiochapwa wana attitude.
    Namiss shule za secondary especially boarding, maisha unawaza tu kula kusoma na kulala. huwazi rent wala nini! tena sisi shule yetu wala huwazi viwalo maana baada ya masomo ni shamba dress, na jumapili kanisani mnavaa uniform, alafu wote lazima mnyoe denge, life was good.
    Nakumbuka Sisco na mrema walivogombea ubunge Temeke, Mkapa akasema hawezi shikana mikono na upinzani, watu wakaja juu, basi jamaa akakanusha, ile siku amekanusha watu wa ITV wakavuta archive akisema Live, was good
    Namiss enzi za shida ya maji dar, hadi Sumaye akasema marufuku kumwagilia mchicha wala kusafisha gari, ukishikwa umemwagilia mchicha au gari safi utakiona. thats was funny.

  56. any Says:

    namiss enzi hizo tuko watoto mkiamka baada ya chai mnatoka nje kucheza hadi lunch time, mkimaliza lunch mnatoka tena kucheza hadi saa ya dinner, bila kujali mko wapi na nani anawaangalia. Siku hizi kila mama achunga mtoto wake maana kuna wachuna ngozi na wanyonya damu na wala vichwa vya watoto. I miss those good days, u dont have to worry about safety, sasa ivi noma, kids are not safety in this world, aidha first world or developing countries, sad eeh

  57. data-protection Says:

    we any do you work or study???

  58. doctor Says:

    mzee wa chapati umenimaliza na yule jamaa wa kutuma kibakuli cha mboga haha.do namiss mama mwenye nyumba wangu wanae vibaka nimeacha funguo nje ya mlango wameiba ili waje waniingilie nikienda kazi usiku!kumuuliza kaanza kunikoromea na kunitishia kwenda kunishtaki natembea na denti mweee,nilinywea.namiss matrafiki wanakukamata then wanakuuliza we unataka tufike kituoni.

  59. any Says:

    apo juu typos, i meant kids are not safe.lol

  60. maria Says:

    Jamani mimi namisi saana Arusha
    Kuku na mbuzi wa bugaloo
    Namisi nyama choma ya police mess na kwa sifaa kimandolu
    Namissi kwenda kungalia Ze comedy myumba ya sanaa
    Namissi kongoro la break point
    Na mwisho namisii laaziz wangu na mwanmke aliyezaa naye na vituko vyake vya kutwa kunitukana kwenye msg

  61. any Says:

    Chris, may be, na matty asanteni kunipa moyo. shukrani.

  62. any Says:

    data protectio, mambo vipi?
    I am not studying for now, done long time ago, may be in the future i may go back to school. nafanya kazi kwa sasa. kwa nini umeuliza?

  63. Mamaa(congo accent) Says:

    NA MISS SANA ENZI ZILE ZA(1.) MIAKA YA 80, KIPINDI CHA X-MASS KUPATA NGUO MPYA, KULA VIZURI NA KULINGISHIA CHUPI MPYA KWA MARAFIKI

    (2) KUKAA KIBARAZANI KUSUBIRI JIRANI MUME WA MTU APITE NA BALOON(MAZUNGU YA UNGA) KISA MTOKO WA TAZARA

    (3)KUSHINDWA KUFANYA HOME WORK KWA KELELE ZA BAA .

    (4) KUTOKUFUA UNIFOM KATIKATI YA WEEK KISA… SABUNI HAKUNA

    (5) KUKOPA MAANDAZI ASUBUHI.. NA KUOMBA CHUMVI ILI KUBANIA ELA YA TAZARA

    (6)KUSIKILIZA NYUMBA YA JIRANI WANAVYOKULA NA SAA 7 USIKU… KISA KUKOSA USINGIZI KWA SABABY YA JOTO

    (7)WALIMU WA FORODHANI SEC..WALIVYOKUWA WANAPENDA KUNIFANYA CENTER OF ATT..

  64. Hatujuani Says:

    Inafuraisha jinsi watu wanavyoandika na kutueleza vitu wanavyomiss home. Kwa kweli mimi namiss sana Shule ya muhimbili na Ndosi. Jinsi alivyokuwa anatukimbiza kupitia madirishani, anatutuma mbolea, test zetu zinasaiishwa na wanafunzi. huku si angeshafungwa kw abuse!!! Anyways nam miss Ndosi hata kama alituabuse discipline yake naikumbuka mpaka leo, but I don’t think I’ll go throught that anymore.

  65. Chris Says:

    wayajua…. find me at mc_curtisjr@yahoo.com

  66. Humu leo hapatoshi Edwin Ndaki, Any na wengine thanx u made my day, nimecheka wachangiaji wameongeza siku za kuishi kwangu kwa kunifanya nicheke. Nimemiss mengi

    Maisha kwa ujumla:
    1. nimemiss kumwagiwa maji machafu na takataka kutoka kwa watu wanaokaa ghorofa ya juu ikiwa wewe unakaa ground floor.
    2. Ukisafiri kwenda mkoani hata kama unakaa mwezi mzima huagi lakini ukienda hata Nairobi kwa siku 3 tu unaaga mtaa mzima
    3. namiss kutongozana kwa kiingereza (vitu vingine vyote kiswahili kutongoza tu ndo kizungu)
    4.Namiss maksi za chu**p* za watoto wa UDSM
    5. Namiss kupeleka ripoti ya shule kwa mdingi maana hiyo ndo siku ya kula kichapo kama umechemka na bahasha zilikuwa zilikiandikwa KWA MZAZI WA….
    6.nimemiss enzi hizo kila kitu kinakaa kwenye pochi au mfukoni ila simu inashikwa mkononi ili ionekane

    Chakula
    1. namiss supu ya makongoro kwa Octa Kinondoni Ada Estate kuna jamaa alikuwa akipika makongoro anaitwa Kimti
    2.namiss chapati za New Zahir Restaurant kule town kwa wahindi bongo daslam
    3. namiss dagaa mchele wa ferry fungu la dagaa waliokaangwa sh. 50 unanunua dagaa na pakti ya juice ya sun vita akhaaa maisha yanaenda na unashiba vilivyo
    4. namiss chips vumbi chafu pamoja na kachumbari ya jamaa alikuwa anaitwa China maskani yake nje ya shule ya sekondari Zanaki
    5. namiss kitimoto cha JJ
    6. namiss kokoto za Rose Garden Bar Dar

    Vinywaji
    namiss sana mbege, ulanzi na safari lager

    ngoja niendelee kukumbuka

  67. bonge Says:

    ooooo sasa mi namiss sana watoto wa ilala magorofani trida bar na supu ya kila jumapili asubuhi huondoki bar mpaka imefungwa namisi saluni yamamakefa kwenda kukopa namisi kituo cha polisi cha ilala mchikichini usiku kinafungwa napolisi hamna namisi maji ya 100 dum kwa ngosha namisi supu ya miguu ya kuku na vichwa mchana hujapika unalia ugali na chachandu mate yananitoka nimesahau mwisho mamisi harufu chafu ya gorofani kwetu na mjumbe wetu ma zai na msaidizi wake marehem mkuu mungu amweke mahali pema peponi amen

  68. namiss kanisa langu la mtakatifu Anna Kinondoni Hananasif kwa michango mingi ya ujenzi na inayotumika vizuri bila kuwepo kwa dalili za ufisadi adumu mwenyekiti wa Parokia mzee Mallya

  69. DUNDA GALDEN Says:

    Kazi kweli kweli
    nafikili Jeff umeona ni jinsi wabongoland walivyo miss nyumbani maana nimecheka kweli.
    Zaid ya yote mimi pia nimemiss Kombolela ndipo nilipokutana kishitobe wangu wa mwanzo. kula mbakishie baba ..
    Chandimu baada ya mechi ngumi mtu…Kula daku mwezi wa Ramadhani…pia namiss yetu ya mtaani Faru dume siku tulipocheza na Ashante Karume na mpira haukwisha kwa manakozi mechi ililudiwa baada ya siku tatu bila watizamaji Refa hadi malazimen walikuwa wanajeshi…..
    Zaid kila kheri chama letu jipya Afazali ya jana ya magomeni chemchem sasa kwisha kabisa na ile Chafosa chai goda
    mkoa wa pwani

  70. cocu Says:

    kusema kweli mie namiss usafiri wa daladala pamoja na kuwa niwashida na kubanana lakini huwezi kuona mtu mzima home akikimbia na pochi au briefcase na suti nzuri akiwahi train au bus kwavile ikimuacha itabidi asubiri kwa muda mrefu kidogo lakini home daladala likuacha linakuja lingine na unashushwa unapoomba kushushwa ‘msaada kontena” na miss sana home

  71. Wow, the responses to this piece are amazing, I guess it goes to show, no matter where you are or what you do, nyumbani ni nyumbani na wote tunapakumbuka kwa namna moja au nyingine. Mengi naona yanafanana.
    I must say, nimeipenda sana comment ya ‘Any’ juu ya chapati na magazeti haha. Personally ni mpenzi mkubwa zaidi wa vitumbua. Chapati nazizimia pia ila angalau huku niliko zinapatikana kwa wahindi, na pia mwenyewe naweza kutengeneza as do some of my friends from home. Ila vitumbua ngoma bila bila.
    So niliporudi home last time 1st morning niliagizia vitumbua vyangu jirani, vikaja ndani ya gazeti kama kawa, haha.

  72. BLACKMANNEN Says:

    -Nawamiss ndugu zangu wanapotaka pesa hunipigia simu moja kwa moja kutoka kwenye simu zao za mikononi, ambapo ni gharama kubwa mno.

    -Ninapowatumia pesa na kuingia extra gharama za kuwapa namba za “Western Union” pamoja na control question, wanaenda kuchukua pesa hizo na kukaa kimya hadi niingie gharama nyingine ya kuwapigia simu kuwauliza kama walipata pesa nilizowatumia, na wao hujibu kuwa walizipata pesa siku ile ile nilipowatumia pesa na kuwapa control namba na walipanga wangeniarifu baadaye kuwa walizipata fedha hizo!

  73. any Says:

    Nammiss Joyce wowow, (mdoli) anapitishwa mtaani basi anachezeshwa apo mnatoa sh kumi per mziki.
    Namiss Ngongoti inapita barabarani watoto mtaa mzima mnajaa hadi wengine wanapotea

  74. Matty Says:

    Any hapa ushakuwa supa star sasa kale kautaratibu ketu ka kupongezana bado kanaendelea, hii parrrrtyyyyyyyyyy itafanyika mwisho wa mwaka tutaiunganisha na parrrty ya Chris then zitakuwa two in one hhahahahahahahahah jamani Amina, Kekuu mpo?

  75. solange Says:

    pearl umenifurahisha sana…ngubiti….na chips za kwa khan wale wahindi kiboko mitaa hiyo hiyo ya bondeni….kweli home swity home.

  76. d-safy Says:

    duuuuu??????!!! home bomba sana ila viongozi sound kibao>>>>

    ELIMU.
    -ENZI ZILE ZA MZEE MASAWE PALE JITEGEMEE(JITEUTE)..FULL KUKIMBIZANA NA MAAFANDE,
    -PUSH UP KWA WINGI…UKIKAMATWA WANACHUKUA KIATU KIMOJA ..THEN SHUGHULI INAKUJA KUKICHUKUA DISPLINE OFIS…
    -DU TANGA KUNANI…PALE GALANOS.HIGH SCHOOL..SIKU YA KULA WALI KILA MTU FULL MZUKA
    -MIOGO YA KWA MAMA K…
    -UDSM MABIBO HOSTEL STAIL ZA KUWAHI LECTURE FULL KUINGILIA DIRISHANI KWENYE SHATO…DUUU

    LIFE MTAANI
    -NAIMIS TIM YANGU PALE TABATA-MAGHOROFA YA NSSF-WASHKAJ WANACHOMA BANGI NDIO WANAINGIA KUCHEZA SOKA…
    -CHAPATI….NA MAZIWA MTINDI(TANGA DAIRY)
    -KITIMOTO…..

    AMA KWELI HOME SWEET HOME…….

  77. Matty Says:

    Thanx Any!

  78. Gervas Says:

    1. Ulanzi, wanzuki, mataputapu, pingu, Gongo na mbege iliyochanganywa na bia aina ya Bingwa,
    2. Lugha za makondakta na wapiga debe hasa pale ukute wanajibizana na abiria aliyetoa noti ya elfu kumi au konda wa daladala nyingine,
    3. Msosi kwa ujumla
    4. Kule kijijini kichapo cha ngumi na mawe pale timu ya mpira ya kijiji jirani ikija kucheza football kijijini kwetu afu wawafunge wenyeji wao. kwanza refa anakuwa na kisu mfukoni.
    5. Bia za promotion kule mwanza
    6. Matty..ee Kaitaba na senene za kule migombani, mmmmh so nachuro
    7. Mishikaki ya samaki pale darajani Zanzibar (Blues restaurant)
    8. Afu mwisho namiss usafiri wa kuleee kwetu kijijini majimoto ambapo tunasafiri na mifugo kwa gari kuku bata, paka mara jogoo anawika, yaani umekalia mifuko ya humvi na Cement afu unapinda mgongo maana juu mbao zimepangwa afu safari inachukua masaa sita. I real miss home!!!

  79. KIDUME Says:

    MAKONDE kama ni kweli uliondoka Bongo zamani hivyo basi ukienda macho yatakutoka. Kipindi cha Jamaa alikuwa anaingia na Manyanga kama sikosei kilikuwa kinaitwa TUMBUIZO ASILIA mtaangazaji alikuwa MICHAEL KATEMBO(Alishaitwa Mbele za Haki) RAHA YA MILELE UWAPE EEBWANA….
    Enzi za Redio moja(labda ingine ekteno sevis!) haziwezi kurudi, 6ki hata kuzikumbuka yaani machozi yananilenga lenga

  80. Nitaongelea Viboko na adhabu za shule
    nimemiss fimbo za mwalimu wangu wa Primary Makole hukoooo Dodoma alikuwa anaitwa mwalimu Kikanya huyu mwalimu angekuwa huku angekwishafungwa kama mdau alivyosema hapo juu, alikuwa anachapa mno.

    Namiss makele ya sauti nyembamba ya da’ Rehema (afande)matron wetu tuliokuwa tukikaa hostel ya Jitegemee enzi hizo, anakuja anatuamsha kwa kusema haya haya nyie watoto, hapo wala hajakugusa usharudi kutoka kwenye likitanda lako la juu hadi chini ndani ya sekunde tu

    Nammiss mwalimu Wajadi wa Jiiteute -Jitegemee kwa fimbo zake na maneno ya utani kabla hajkunyuka”….eeh kijana nakuchapa fimbo 6 pungufu unaongea na utakula viboko leo mpaka uende haja kubwa wima…” pia tulikuwa tunamtania kwamba yeye ndo yule mtuma salamu maarufu kwamba yeye ndo yulee mtuma salamu maarufu wa redio Tanzania enzi hizo….Wajadi Fundi Wajadi wa Mahuta Shimoni Newala

  81. sally Says:

    Yani nasoma comments mpaka raha nyumbani ni nyumbani!!!!!!!!!!!

  82. masha Says:

    Mie na miss sana Namnani na Buibui!!!! 🙂 i….Home sweet home… lions club every friday nite , CBE club na Jolly pale upanga 🙂 🙂 🙂 You know what i mean… Miss home miss ma ppl..

  83. Caroline kazi Says:

    ebwanaeee mi nnachomiss sana kusema kweli kwanza uvutaji sigara mtu wangu, kwanza navuta kwa tabu afu emmbasy zenyewe hamna, cjui umenielewa?! bongo wanabana lakini hawapo advance kama mbele c unajua!! afu kili baridi duh we acha tu heineken zinaboa, basi na kanyama choma, mara chips vumbi mtu wangu machafuchafu(kitimoto) cha mwenge karibia na maryland bar, na chamwisho kabisa kutia vimeo baaaaaaassssssi zaidi ya hapo……. bongo rumba kali afu jua usilipimie mwanangu.

  84. iii Says:

    AISEE NIMEMISS SANA ROSE GARDEN. KOKOTO,MAKANGE,VIGRUPU VYA JUMAMOSI MCHANA,HAHHA
    VICHECHE NDO USISEME,KUPIGWA MIZINGA KAMA KAWA!!!!

  85. Cleopa Says:

    Namiss vituko vya Prof,Osolo pale Mlimani akitoa test ,maswali yote ni ya kuchagua;anakwambia bora ujaze namba ya mtihani na tarehe tu afu ulale mbele utaambulia C.Kila swali utakalofanya ukakosea jibu anakunyang`anya maksi 3,ina maana ukipata nusu nakukosa nusu una 0 mwe!

    Afu kuna mtandao kwa kudesa kwenye paper ilikuwa komesha!degree zingine bwana waone watu wanajenga vitambi maofisini wanajua siri za mafanikio,ndo ufisadi unakoanzia.

  86. binti-mzuri Says:

    haha cleopa nimecheka aisee..za mlimani watuachiage sie..aisee..wengine degree pale basi tu mwanawani..unashangaa mtu kwenye pepa kakazania kuangalia feni..kumbe keshaandika formula pale..mtu yupo tu anaangalia juu..haki ya mbongo..namiss shule!

  87. hombiz Says:

    Nna-miss frying termites a.k.a kumbikumbi. Hwa wakikaangwa si mchezo mazee!. Kama hauwafahamu, kongoli hapa http://www.drywoodtermitecontrol.com/swarming.html

  88. Seven Abraham Says:

    Duh!Mimi ninamiss sana michango ya kitchen Party na arusi.
    Kwani nimesave pesa kibaoooo!!!!

  89. mkate Says:

    Kweli hata mimi ingawa siko mbali sana na hoome…ts stil de best??!
    1. Namiss nlivyokuwa natoroka shule (Kibo Primary-Moshi)na kaka yangu alafu tunaenda kujifica uwanja wa mpira USHIRIKA….
    2. Namiss zile siku ukitaka kiatu kipya kama cha mtoto wa jirani unatupa cha kwako..au unakata malapa ununuliwe mapay..mbaya zaidi nipale yatakapopelekwa kwa fundi…
    3. Namiss faida za u prefect majengo Sec…moshi..kula chakula cha walimu na kukwepa foleni hasa wakati wa wali na mitihani…kweli uongozi ulinisaidia…
    4. Namiss kusafiri na baba yangu kwenda dar alafu mnapack ‘packed lunch’ ya viazi vitamu na juisi ya machinwa na maparachichi…
    5. Namiss kwenda kumtembelea bibi yangu….Kule Mwika Moshi…wengi wanapaita marangu.
    Bwana wangu nisisahau…
    6. Mwalimu Tagora na staili ya kuchapana fimbo unaingia chini ya kiti unanyayua makalio juu…au MMbaando, unaunganisha mikono yote…..
    7. namiss kwenda majengo sec. siku za mvua bwana alafu upitie pale Mary G..watoto wa kike waanze kukusumbua madirishani???
    Acha tu..nyumbani ni nyumbani…
    8. Namiss somo la omputer Mary Goreti mtu anaambiwa ‘click F8’ halafu anabonyeza F na 8…
    ni maisha tu..
    Any umenibamba sana…pole4ur dad’s death.

  90. Masha Says:

    Jamani mie namiss kugongeana milango na kuombana chumvi na moto!!! Hata mboga jamani si mnajua tena mambo ya uswazi!!

  91. mama lao Says:

    jamaniiiiiiii. tuendelee kumiss vitu jamani.
    mimi namiss majungu, siku za likizo unatoka nje asubuhi mnaanza kumjadili mtu oh, huyu kavaa hivi.
    – mi namiss maandamano ya CUF
    -namiss ugomvi wa gari kugonga kuku kesi hadi polisi

  92. wakuvanga Says:

    Namiss sana New happy Hotel iliyopo mtaa wa Rumumba Kariakoo, supu ya kuku na ndizi za kuchoma na bia aina ya Kilimanjaro. Pia namiss Que bar iliyopo Bukoba mjini, ndizi na maharage kwa nyama

  93. manka Says:

    haaaaa…kweli mtu kwao..jamani mi nawamisi kaka zetu angalau wanachunikaa kidogo..huku kupata wakumchuna kasheshe kila mkaka yuko past due…..home sweet home….

  94. Mdau Says:

    Naimisi sana Elitev Pub – Mbagala

  95. magdalene Says:

    i do miss those tyms wen we were young,2nacheza cnc monng til jion then ukibak hom nikichapo hearvy toka kwa mama then kama hujala tha whole day mam ana2lazmisha kula 1st utastat wth tea then unaenda kuruka kichura 15min thn yafata lunch unamaliza thn kichura tena hapo yn nimnalia hakuna mfano,sema 2umechoka mathe akuckie bwna mbona itakuhusu mbaya,then 2namalizia na sapa,hapo bas mpo hoy mara mwaambiwa mkaoge wakat those tymz kuoga it was a crisis as if 2megombana na maji mbaya zaid maj barid,haya bwana bt enz hizo cc ndyo 2liitwa watoto wa uswaz.com


Leave a reply to data-protection Cancel reply