BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA MPYA RASMI YA JK June, 26, 2008

Filed under: Photography/Picha,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 9:29 PM

Picha rasmi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete, imebadilika.Kama inavyoonekana pichani,picha ya Rais iliyoko kushoto ndio inakuwa picha rasmi mpya.Iliyopo kulia ndio iliyokuwa ikitumika mpaka hapo jana yalipotangazwa mabadiliko hayo.Haitotumika tena. Aliyezishikilia picha zote ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Kassim Mpenda. Hapo alikuwa akiwaonyesha picha hizo waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam.Kwa hiyo kama ofisi yako inahitaji au ni mojawapo ya zile ambazo kiutaratibu ni lazima ziwe na picha ya Rais fanya hima uendane na mabadiliko haya.

Photo via Yahya Charahani

Advertisements
 

25 Responses to “PICHA MPYA RASMI YA JK”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Mh. Rais, naona kisop kimekubali ndugu yangu, ni kweli picha ya zamani iliyopo kushoto kwa Mkurugenzi, inakumbusha mambo na nyakati za enzi zile. Pole kwa kazi ngumu zote ulizonazo, za kuuongoza Umma wa Kitanzania na hapo hapo ukiongoza na kutatua matatizo ya Bara letu la Afrika kama Mwenyekiti wa Au. Zimbabwe ni pagumu kaka, wakubwa wanashinikiza matakwa yao yafanikiwe, uwe makini ndugu yangu!

 2. a Says:

  Duh!!! I wud not like to meet this dude in a dark alley… forgive me yall but this dude’s face cud chase away ghost!!!!

 3. BLACKMANNEN Says:

  ………swala la Zimbabwe, ni “Mtego Wa Panya” wa kuingia waliomo na wasiokuwamo, ni mtihani mkubwa kwa viongozi wetu wa Afrika. Busara za hali ya juu na maono ya mbali zinahitajika kwa Mwenyekiti wetu wa Au. Mungu na awe pamoja nawe katika swala hili Mh. Kikwete!

 4. Kimori Says:

  Hizi picha za rais tutazibadilisha mara ngapi?…Kwani hiyo ya kwanza ina tatizo gani mpaka tubadilishe tena picha?

  Tofauti nionayo mimi ni kuwa hiyo mpya meno ya rais yanaonekana halafu kavaa miwani. Sijui kama hiyo inaweza kuwa sababu ya kubadilisha picha ya mtu yule yule kwa kipindi cha miaka miwili na nusu aliyokaa madarakani!

  Watanzania tuna vitu vingi sana vya kubadilisha na si picha ya rais!

 5. Mickey John Amos-Denmark Says:

  Mabadiliko ya picha ya kiongozi wa nchi ni sawa kabisa.

  Hata nchi zilizoendelea tumeona wanafanya hivyo mara nyingi kufuatana na mazingara ya ule wakati viongozi wanahitajika kubadilisha picha katika matumizi ya Taifa,siyo lazima kuwepo na sababu muhimu ya kuelezea mabadiliko.

  Tumeona mabadiliko ya malkia wa UK, tumeona mabadiliko ya malkia wa Denmark na nchi zingine mbali mbali ulimwenguni ni kawaida kwa viongozi wote.

  Picha ya sasa imekukubalika kama hali halisi ya kiongozi wa nchi, sawa kwa matumizi ya Taifa na kimataifa.

  mickey@mail-online.dk
  Copenhagen

 6. solange Says:

  kwani sababu ya wao kubadilisha hiyo pic ni nini haswa?mbona wanauza sura sana jamani na kuna mambo kibao ya kufanya?kwangu naona hakuna jipya na hakuna reason yoyote watakayotoa nikawaelewa…..au alisahau kuvaa miwani n now ndo katuvalia?

 7. Matty Says:

  Shavu dodo!

 8. JMbigy Says:

  DU!Leo sina la kusema kuhusu picha kubadilishwa!Nawaachia wenye exposure na uelewa waseme.Manake naskia hata huko Denmark, UK n.k wanabadilisha!Leo mtanisaidia kwa hilo sina la kusema.

 9. Kibabu Says:

  Wananchi hawana maji, dawa hospitalini hakuna, uwezo wa kupata mlo walau mmoja hawana, miundo mbinu duni…nk….nk…! Serikali iko ‘bize’ kubuni miradi ya ‘pwagu’ kama hii ya kubadilisha picha. Hapo watu ‘wameshavuta’ kamisheni yao! – Baaaado tuna safari ndefu!

 10. Ladslaus Modest Says:

  Ndugu yangu unayejiita ‘a’, yaani unamuita binadamu mwenzako “Dude”.; labda umeandika bila kukusudia, lakini kama umekusudia, basi Wewe hujaumbwa na Mungu muumba wa Mbingu na Nchi.

 11. Monii Says:

  Hiyo picha ya zamani kwani ina tatizo gani? Mimi nitabaki na hiyo ya zamani kwani huyo ndiye Rais niliyemchagua, huyu mwenye mashavu ya ufisadi simtambui!

  Na huyo bwana Mpenda mbona picha yake haionekani?! hahaha!!

 12. Monii Says:

  Oh! I didn’t realize, huyu wa sasa anavaa miwani… kusoma report za kina Mwakyembe siyo rahisi ati!

 13. Gervas Says:

  Pesa zitakazotumika kubadilisha picha hii zingeweza kabisa ku-rehabilitate Uwanja wa Fisi Manzese maana ni aibu kwa Nchi. Hii ni kuchezea fedha za kodi ya wananchi tu, sasa baada ya mwaka mmoja tena itabadilishwa? sio shida ya watanzania kuona raisi amependeza, amebadilika au amepata shavu. Hii inamaanisha kwamba itabidi picha zote zilizo kwenye ofisi zote za Serikali Tanzania, Balozi mbali mbali za Tanzania duniani nk zibadilishwe kwa gharama ya serikali. mmmh!

 14. sally Says:

  Sasa hivi madai yake mambo safi katulia ndo maana wamechange picture haya yetu macho

 15. mtz Says:

  Ladslaus Modest nduge yangu tembea uone. Neno “dude’ ambalo Marekani hutamkwa kama “dud” lina maana mwanamme. Jamaa hakusema dude (jitu) ya kiswahili. The lugha y’all.

 16. hombiz Says:

  Picha haina mpango wowote. Tunatata maisha bora kwa wananchi wote kama alivyoahidi.

 17. masumbuka Says:

  Ladies and Gentlemen!Do you see these two photos?Can you notice any difference?Asolutely.One in my left hand is a ‘PRE-EPA’ Photo.And the one in my right hand is a ‘POST-EPA’ Photo. You see! There is a Huge Difference between the two photos.This is what is called Documentation.Thats why we are recommending a change.Tanzanians got to change.You dont stay at one point all the time, you see!Ahsanteni sana mabibi na mabwana kwa kuniskiliza!

 18. bdo Says:

  ni mpango mzuri wa kubarisha picha

 19. kekue Says:

  Yani wanakaa kabisa kujadili ss jamani tubadili picha!!!!!!!! Kha jamani!!!!!! cjui mtabadilisha mpaka lini coz mwaka huu nao mashavu yakijimuvuzisha mwakani tena mtabadilisha, aya.

 20. Queen Says:

  Ladslaus no.11 umeniacha hoi kwa kweli kumbe ulidhani ‘dude’ ni jina baya ahaaaaaaaaaa haaaaaa lol
  About picha:Nilisoma ktk gazeti kuwa picha ya mwanzo ilipigwa soon after the elections na ilimwonyesha Rais akiwa na mikunjo usoni ya stress(na uzee kdg) iliyotokana na zoezi la kampeni,they also said that the pic was not professionally taken.Ndio maana wamebadili.Its true hiyo picha ya mwanzo ilikuwa hailipi Rais alionekana mzee zaidi.The new pic is good.
  Na si siri Rais ana mvuto wa Sura and believe it or not hiyo ilimwongezea kura hasa za wanawake.I also read somewhere kuwa mvuto wa sura pia unaweza kumsaidia mgombea kushinda(This happened to Bill Clinton too)
  Najua wananchi mtaniuliza kuhusu maraisi amabao hawana mvuto na wameshinda thats another topic all together

 21. binti-mzuri Says:

  hahaha ladislaus hata mie nimecheka…lol..maaan!…dude(pronounced as ‘dud’) means a guy au fella…sio tusi!!!

 22. Matty Says:

  hahahahahahahahah! Queen vp kuhusu Mugabe reception yake?? tehtehtetetetetetette!

 23. Masare Says:

  Hakuna lolote….ushetani tu na ufujaji wa mali ya umma..Nani anataka kuona picha “nzuri” ya Rais ilihali watu wanapiga miayo mchana kutwa..nashangaa sana eti mijitu na “P” zao imekaa chini na kujadili picha ya rais kubadilishwa! Msishangae mkijagundua kuwa Kikao cha kubadili picha ya Rais kilifanyikia Miami, Florida na kikao hiko kiliundwa na wajumbe 120 bila kusahau kuwa kikao kiliendeshwa kwa takriban wiki mbili! Wabongo bwana…halafu hapo hapo kuna wadau wanatoa mifano “uchwara” eti ooohh….kubadili picha ya Rasis ni jambo la Kawaida hata Malkia fulani alifanya hivyo! Our ways of doing things should not be dictated by Malkia so and so, wake up people we have to follow our instinct and live by our Principles…I am talking to you Micky John Amos from Denmark! You make me puke with your weird comments!

  masareibv@aol.com

 24. Lily Victor Says:

  Kwa kweli huo ni ufujaji wa pesa za watanzania wavuja jasho. Iko miradi mingi ya kuweza kubuniwa na ikaleta manufaa kwa wananchi wote na sio huu wa kubadilisha picha. Mimi sibadilishi ya kwangu napenda hii ya zamani cos this is original KK. wakati huu hakuna tena Mtanzania mjinga tumefungua macho yetu hatutaki ujanja ujanja wa watu wachache kujaza matumbo yao kwa pesa zetu.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s