BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

THERE SHE GOES…OFF TO SOUTH AFRICA June, 29, 2008

Filed under: African Pride,Breaking News,Fashion,Urembo — bongocelebrity @ 12:20 PM

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata, ameondoka leo mchana nchini akielekea Johannesburg, nchini Afrika Kusini ambapo atafanya kazi na kampuni kubwa ya uanamitindo ya Ice Model Agency ya huko Afrika Kusini, kufuatia mkataba wa mwaka mmoja aliosaini kupitia kampuni yake mama Compass Communications.

Flaviana alipata umaarufu mkubwa wa kimataifa katika mashindano ya Miss Universe mwaka jana ambapo alishika nafasi ya sita katika mashindano haya makubwa ya urembo, na alisaini mkataba wake na Ice Models jijini Dar-es-Salaam hivi karibuni baada ya majadiliano kati ya Compass Communications na Ice Models kukamilika. “Hii ni mara ya kwanza kwa mrembo anayeshikilia taji la kimataifa hapa nchini kupata nafasi kama hii,” alieleza mkurugenzi wa Compass Communications Maria Sarungi Tsehai ambaye alisimamia majadiliano na mkataba wa mrembo huyu.

“Ingawa tunajua kuwa warembo wengine wamepata mikataba lakini wote ili wabidi wasafiri na kuhangaika kutembelea agencies mbalimbali mpaka walipobahatika. Flaviana amepata mkataba huu bila kukanyaga Afrika Kusini.” Flaviana ambaye wakati anashikilia taji la Miss Universe Tanzania alitimiza kazi mbalimbali za kijamii na kutembelea nchi mbalimbali kufuatia mialiko kama vile Ufaransa, Hungary na Denmark. “Flaviana ameweka tayari historia nzuri na ya kipekee lakini tulijua ya kuwa alikuwa ana uwezo wa kuendelea kutuwakilisha kikamilifu huko nje.” alieleza Maria Sarungi “Mafanikio yake yanatokana na utiifu wake, jina kubwa la kimataifa la Miss Universe na jina zuri la Compass Communications katika nyanja hii ya urembo na uanamitindo huko nje ya nchi.”

Flaviana ambaye amepokelewa na kampuni yake mpya ya Ice Models alipotua airport anatarajia kuanza rasmi Jumatatu tarehe 30 Juni 2008, ambapo anategemewa kuonyesha mavazi katika maonyesho mbalimbali Afrika Kusini ikiwa ni pamoja na Fashion week mjini Johannesburg na Capetown.

“Tumefurahia sana hatua hii, kwani Flaviana amekuwa mfano wa kuigwa kwa warembo wenzake wa Miss Unvierse Tanzania, na sisi tutaendelea kuwainua akina dada ili waweze kutimiza ndoto zao. Na ndani ya mwaka mmoja mimi binafsi nina uhakika tutakuja kumwona Flaviana katika jukwaa zote kubwa za kimataifa na Mungu akimjali na akiendelea na moyo huu aliouonyesha hapa nchini, atakuwa ni super model wa kwanza wa Tanzania.” alieleza mkurugenzi wa Compass Communications.

Flaviana ni mrembo wa kwanza kuwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa kupita yote ya urembo ya Miss Universe, mwaka jana katika nchi ya Mexico na alifanikiwa kuingia katika kumi Bora (Top10) katika mashindano hayo akishika nafasi ya sita, mashindano haya yalishirikisha warembo 77 kutoka nchi mbali mbali duniani.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Compass Communications: Tel: 2182405/ 2182596 au 0784 305122

Advertisements
 

22 Responses to “THERE SHE GOES…OFF TO SOUTH AFRICA”

 1. DUNDA GALDEN Says:

  Wakilisha binti.nimeipenda hii picha
  safi sana mgongo wa nguvu na hiyo
  ngozi ya ngombe
  chafosa

 2. Gervas Says:

  Go ,go girl! big up for taking your carrier to another level. Hii ni proof kwa wazazi wasio amini kuwa urembo/modeling ni profesion pia. Pongezi zisiishie kwa Flavian pekee, nampongeza kwa nafasi ya pekee Maria Sarungi, ambaye amemsimamia kama dada/mzazi tokea aanze kushiriki mashindano. Sijasikia kashfa nyingi kama zinazoibuliwa na warembo wengine. Nafikiri hata warembo wengine wawe na watu wa kuwasimamia km guardian otherwise wakishakuwa ma-staa wanaharibiwa na offer za wakware. maana wengi wanakuwa mastaa wakiwa umri wao mdogo, uwezo wao wa kufanya maamuzi safi unakuwa mdogo pia, and they just end up in the bin and being used!

 3. hombiz Says:

  kila la kheri bibie!

 4. iii Says:

  HONGERA…MAKE US PROUD!!!

 5. Annie Says:

  Waoh!!!Great Flaviana! Congrats a million…
  Karibu Mzantsi Afrika (South Africa). Wish you the best!!!
  Go girl…You’ve made a step forward just get determined you’ll make it for urself and Tanzania as well.
  Goodluck…

 6. Mickey John Amos-Denmark Says:

  WISHING YOU ALL THE BEST FLAVIANA,YOU ARE ON TOP OF THE MOUNTAIN ALMOST REACHING THE STARS,YOU ARE WEALTH AND YOU DISERVE IT.

  All Credits goes to Maria Sarungi & Compass Communication for Creating a “road of Succes” for Flaviana our “natural Super model”

  With no doubt in my mind, competitive challenges from other sponsors, modelling agencies ahead of you to follow.

  Competitive challenges against Compass & Communication will nothing less than inspire your organisation “widely” in creating a huge “wave of succes” for our comming natural talented models at the International level.

  mickey@mail-online.dk
  Copenhagen

 7. Pearl Says:

  huyu ndo mtu na kipaji chake sasa,sio tu kushika nafasi ya sita ndo iishie hapo ila leo ameonyesha watanzania kua kweli anakipaji cha modelling mpaka nchi za watu wanatambua hilo,kweli nampongeza sana.
  pia nampongeza Maria Sarungi,kweli amefanya kazi nzuri kwa huyu dada.
  Lundenga hili ni fundisho kwako kua sio uwapeleke huko washike nafasi za miss world africa tu ila wapate nafasi kwenye modellling agency ili wazidi kuinua vipaji vyao.

 8. Matty Says:

  Hongera Flaviana, halafu mtoto umetulia ile mbaya sijasikia kashfa juu yako.Mungu akubariki!

 9. Edwin Ndaki Says:

  Daima tupo wote mdogo wangu.

  mafanikio mema.

 10. tanzanitefc Says:

  Habari yako,
  pole na shughuli nzito ya kuwakilisha jamii.Sisi Vijana wa Tanzanite fc Ya Atlanta Ga tunasikitika na habari tuliyosoma juu ya mchezaji wetu aliyewakilisha timu yetu ya taifa huko Cameroon kwa kuadhibiwa kwa kulipia jezi ya timu ya taifa aliyobadilishana na mchezaji mwenzie wa Cameroon(Etoo)tumeona kwamba ni swala la aibu kwa chama cha soka cha Tanzania kumdai mchezeji huyo hasa ukizingitia mchango wake kwa Taifa.
  Sisi Tanzanite fc tungependa kujitolea kulipa deni hilo la huyo mchezaji. Je ni utaratibu gani tuutumie kuwakilisha mchango huo, na je ni kiasi gani?Tunatanguliza shukrani zetu kwa msaada wako kutufanikishia swala hili.
  Wako
  Tanzanite fcAtlanta,GA.
  USA

 11. tanzanitefc Says:

  we realy need to solve this problem.

 12. Matty Says:

  Tanzanitefc, nimesikia president wa TFF katangaza kuwa ni Ruksa kwa wachazaji wa Taifa Star kubadilishana jezi na kuanzia sasa kila mchezaji atakuwa anamiliki ile jezi anayokuwa amevaa na anauwezo wa kuigawa au la!
  umenipata?hivyo Canavaro sijui nani nani tena hana kosa kabisa!

 13. kekue Says:

  Songa mbele mamaa!!!! Na mwenyenzi Mungu akujalie mpendwa ktk bwana.

 14. Kenny Says:

  Mbona mnatuchanganya nyie???? Tunamuongelea falaviana mnaleta mambo ya jezi apa…muulizeni mwakalebela utaratibu atawaelekeza…hamna TFF hapa

 15. Matty Says:

  Sasa Kenny, usaidiweje?achana na sisi kama unaona hutuelewi!

 16. Kenny Says:

  Sasa nyie subirini mada ya Taifa stars hapa ndio mlete ivyo vitu…wanaochangia hapa hawako interested na mambo ya TFF ukizingatia kua kila mara tuki concetrate na hayo mambo tunaambulia maumivu tu……..bora tumuunge flaviana tu sasa tufanyaje

 17. glory Says:

  heheheh falviana Excellent goooooooo up my girl.good luck love

 18. Matty Says:

  Kenny are u sure???

 19. Kenny Says:

  Matty…Tenga ameshamsamehe Nadir Haroub ” Cannavaro”..harudishi tena jezi wala hela….. na kamuambia Kaijage aache tabia yake ya ajabu… Cannavato kaonyesha kitendo cha kishujaa na chakuigwa hivyo wachezaji wote waige mfano wake” mwisho wa kumnukuu bosi wa TFF……kwaiyo usiwe na wasiwasi kashasamehewa iyo hela

 20. binti-mzuri Says:

  flaviana mwaya,usisikilize ndomondomo…

 21. Matty Says:

  Thanks Kenny, no comment!

 22. sally Says:

  Hongera sana Flavia


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s