BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MUGABE:KIELELEZO CHA UONGOZI AFRIKA? June, 30, 2008

Filed under: Editorial,Mawazo/Tafakuri,Serikali/Uongozi,Siasa,Special Interest News — bongocelebrity @ 6:29 PM

Katika anga za siasa duniani hivi leo,lipo jina ambalo dunia nzima inaendelea kulizungumzia.Hilo si lingine bali lile la Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe.Kwa wengine mtu huyu ni shujaa,kwa wengine mtu huyu ni kinyume kabisa cha neno shujaa.Kwako wewe je?Je viongozi wa Afrika wanaohudhuria kikao cha Umoja wa Afrika huko Misri(na Mugabe naye anahudhuria) wataweza kumnyoshea vidole Mugabe?Nini hatma ya siasa za Afrika?

Pichani ni Rais Mugabe akiwa na mkewe,Grace Mugabe.Wengi wanasema wakati wao wanatafuna keki,wananchi wengi wa Zimbabwe wanakufa njaa.

Photo/New York Times

Advertisements
 

36 Responses to “MUGABE:KIELELEZO CHA UONGOZI AFRIKA?”

 1. TEACHER-DENMARK Says:

  I HOPE HE WILL DIE SOON ILI WANAOKUFA NA WALIO NJIANI KUFA WAPONE JAMAAAAAAAAAAAANI DU HII KALI TANGU NATAMBAA NAMSIKIA HUYU BABA MUNGU IBARIKI AFRICA NA WATU WAKE WOOOOOOOOTE KASORO MUGABE

 2. any Says:

  huyu ni mkewe au mkamwana wake! naona wamechanganya. she is young for this old guy

 3. Matty Says:

  They are really naturo kabisa tena wanafanana,
  Mugabe unazani utaishi milele?unaenjoy kitu gani sasa wakati watu wako hawakupendi na wanakufa kwa ajili yako?unataka utawala wa mabavu?wewe baba ungetulia tu ushazeeka unatafuta kufa kabla ya siku zako, mafrasturations ya wananchi si mchezo we ng’ang’ania tu, ila iko siku tu Mungu atasema na wewe! i hate u!

 4. Ed Says:

  Mugabe proves how dumb African leaders are. He shows how our leaders entitled with leadership. This is the shame and it sucks big time.

 5. Pearl Says:

  as for me naona mugabe ni poa sana tena aendelee kuwa rais,hongera mugabe,hao wote wanaomnyooshea vidole na kumzodoa mugabe wao wamefanya mema mangapi???
  yeye hataki kuuza nchi kwa hao watoto weupe kwaninn watu wanataka kumpangia cha kufanya???
  yuko sahihi kabisa kusimama na kile anachokiamni yeye na sio kile watu wengine wanachokiamini.
  tena mugabe ni mfano wa kuigwa kuwa wakati unapofanya jambo na likawa ni kwa manufaa ya wananchi haijalishi dunia inawaza nini!!!!

 6. DUNDA GALDEN Says:

  (ZANU PF.R.MUGABE JOGOO)……..ALIKUWA MTU MMOJA SAFI SANA LAKINI UCHU WA MADARAKA NA KUTOWAAMIN WAPYA KWA KUZANI WATAKUJA KUWARUDISHA WAKOLONI AU KUMPELEKA GEREZANI HILO NDILO LINALOMSUMBUA ALIE KUWA SHUJAAA NA KUBADILIKA KUWA ADUI KWA ALIOWAKOMBOA
  WASI WASI WANGU KISIJE KIKAMKUTA KAMA………..(KUKU WA ZABANGA )BUT AFRICA STEEL CHAFOSA CHAI GODA

 7. Gervas Says:

  Ni dhahiri kwamba Land Reform kwa Zimbabwe ilikuwa inevitable, lakini alichokosea Mugabe ni kuwanyang’anya wazungu ardhi kwa 100% alipaswa awapokonye taratibu yaani km una ekari 100 unaachia zingine unabakiza 40, pia wananchi wanaopewa hiyo ardhi wawe wameandaliwa eg, mikopo, vifaa vya kilimo nk. Hivo Naona Mugabe km alikurupuka. Kwangu Mugabe amechemsha. Lakini sasa hatma ya zimbabwe ipo kwa wananchi wenyewe kumkataa kwa njia ya kura. Mambo ya ukiukwaji wa haki za binadamu, free and fair election ni wimbo wa taifa wa kila Taifa la Afrika. kumbukeni hata Marekani walilalamikia kuwa Bush alicheza rough kwenye uchaguzi uliomweka ikulu

 8. pound Says:

  mugabe is the hero,true anti-white,na wanaofanya watu wa zim. wataabike ni western countries kwa kumuwekea vikwazo.ukiambiwa chanzo ni land reform kunyanganywa wazungu kupewa wazawa,na nyinyi watanzania mnaoshabikia mnajua kinachoendelea kwet lakini?leo gazeti moja la hapa limeandika hadharani kuwa mamilioni ya pesa zikiwa ni misaada yameliwa na wajanja huku bongo kwenye kampuni moja inaitwa tanroads,tembelea http://www.vg.no

 9. hombiz Says:

  Jana niliangalia documentary iitwayo Zimbabwe undercover kwenye kipindi cha Night Line ABC News. Kwaweli huyu mzee amegeuka kuwa dikteta mkubwa. Yaani nilitibuka nilipoona jinsi askari na wafuasi wake walivyokuwa wanauwa raia wema. Yaani walikuwa wanawakimbiza na kuwalamba bakora kama vidole vyao havionyeshi kuwa hawajampigia kura Mugabe. Wangine wamepigwa na kuumizwa vibaya sana. Na mbaya zaidi, wengine wameuwawa kikatili kabisa.
  Wapo watu wengi waliopoteza maisha yao kwa upuuzi huu wa Mugabe.
  Mwenye comment # 5 hapo juu, Pearl! Sikubaliani na wewe kabisa. Kipi anachokipigania kwa ajili ya Zimbabwe? Wewe huoni madudu makubwa anayofanya mpaka dakika hii? Hakuna mtu angempinga kama angeheshimu katiba na kufuata taratibu za utawala wa ki-demokrasia. Upendo gani alionao kwa Zimbabwe kwa kutesa na kuua wananchi wake?
  AU needs to kick this guy out of the Office as soon as possible.

 10. DUNDA GALDEN Says:

  LEO JAMAA MBONA UNATAKA KURUSHA NGUMI KWENYE LANGO LA KUINGILIA MKUTANONI AU NDIO UNAMUIGA MOI KABAKI HYO NOMA SIO KILA MAHALI UBABE TUU
  CHAI GODA

 11. Mimi Says:

  Wanamponda Mzee Mugabe ni wale waliotekwa kiakili na nchi za wazungu. Habari wanazozipata ni za upande mmoja tu wa shilingi, wanapata habari zao zote kutoka kwa CNN, BBC na nyingine kama hizo halafu hawajui kuwa hawa wazungu wakiamuwa kumfanyia mtu kampeni achukiwe/apendwe kipaji hicho wanacho na kwa bahati mbaya wamefanikiwa kuwateka nyinyi nyote. Mzee ni shujaa, anawapa ukweli wao waziwazi wangu kitu ambacho hawakipendi, ndiyo maana hata hotuba za Mugabe kwa sababu zinawapa ukweli wao hawazitoi sana kwenye vyombo vyao vya habari. Mzee anajuwa maana ya uhuru sio hao viongozi wengine vibaraka wanaofuata amri za wazungu. Big Up Mugabe KWANGU MIMI NI SHUJAA.

 12. hombiz Says:

  mtoa maoni # 11(mimi) ni afadhali umeweka wazi kuwa Mugabe ni shujaa kwako wewe. Kwa watu wengi wanaopenda demokrasia ya kweli sidhani kama watamuita Mugabe ni shujaa. Jina sahihi la Mugabe ni Dikteta wa Zimbabwe. Huyu jamaa ni aibu kubwa sana kwa Afrika.

  Unaposema media ndio inayomuharibia dikteta Mugabe, mimi sikuelewi hata chembe. Hivi hizo media zinapoonyesha watu wanakimbizwa na kulazimishwa kupiga kura, kupigwa na hata kuuwawa, hayo ni makosa. Hivi Dikteta Mugabe anapotamka kuwa akishindwa uchaguzi ataingia msituni kupambana, hayo ni makosa ya media!?. Hivi Dikteta Mugabe anaponyan`ganya wakulima wa kizungu ardhi na kuwapa wazawa ambao hawana mtaji wala ujuzi ha hata uwezo wa kuendeleza hayo mashamba, hilo ni tatizo la media!?
  Dikteta Mugabe, anavuna alichopanda!. Na dalili zote zinaonyesha kuwa huyu mtu mwisho wake ni mbaya saaana. His days are numbered.
  Kwa habari zaidi juu ya ugoro anaofanya Dikteta mugabe, tembelea hapa http://www.pbs.org/frontlineworld/blog/2008/06/since_the_lates.html

 13. Ed Says:

  Mimi,
  please get a life, kusema kwamba meadia za west zina propaganda kuhusu Zimbabwe ni shame and it doesn’t make sense. Tell me what meadia you believe has a best explanation concern Mugabe nightmare?

  Waafrica wengi bado tuko kwenye colonialism era, and that is you real believe in. Get over the 1960s mentallity, let focus on the African development and not african dictotors.

 14. DUNDA GALDEN Says:

  USILOLIJUA KWELI WAKATI WA KIZA TENA KINENE.SASA WEWE NDUGU YANGU NCHI SASA INAKUWA NA NOTI YA MILION HAPO BADO KUNAUSHABIKI?KUSOMA UJUI HATA PICHA UANGALII KWELI KWELI SHUJAA KWAKO….KWETU SI SHUJAA PINDI WALE WATOTO WA ZIMBABWE WAPOTAABIKA KWA MTU MMOJA TUU
  .

 15. Matty Says:

  Hombiz kula 5, nimesoma kwenye hiyo link duu inatia uchungu sana halafu watu wanamtetea huyu chizi, anakoelekea ni kubaya sana Mugabe!yeye anajiona mjanja lakini ipo siku tu!

 16. kijiwe Says:

  kusema ukweli jamani huyu mzee amevuka mipaka kwa kuwatesa watu wa zim,kuiba pesa za wazim na kunang’ania madaraka.ni kweli kama western countries zisinge implement masharti zim wasingekuwa na uchumi mmbaya hivi.yaani hivi sasa siyo mambo ya noti tena watu wanacategorise hela in kgs.
  ila ana msimamo mkali sana kuhusu neo colonialism which i think its good and should be implemented by the AU tukiwabana hawa wazungu watapunguza kutunyanyasa kisaikolojia na kiuchumi

 17. Sem Says:

  Mugabe sucks real!..jamani, wazungu wanapotudharau it is very right; kuna ubaya gani kuwaachia wengine waongoze nchi? nadhani angekubali kushindwa labda angejiongezea heshima yake as one of the freedom fighters in Africa; lakini sasa naona anazidi kujipotezea heshima yake!

 18. masumbuka Says:

  Eti Watu wanasema mimi Mugabe sasa nimekuwa Mzee siwezi kazi?Mzee Ng’ombe Ebooo!Muulizeni Mama Mugabe aeleseee kama mimi kweli Muzee!Jogoo unajua maana yake?Mimi ndiyo Jogoo mwenyewe!Temba ukicheza karibu karibu shauri yako!

 19. tiandra Says:

  Yaliyomkuta sadam yatamkuta mugabe. bush dont fool around

 20. Mimi Says:

  Ndugu zangu amkeni, nawaonea huruma kwa kuwa mmeshaoshwa brain zenu na mmebaki kufuata mkumbo tu. Sisemi mengi ila mkitaka kujuwa unafiki wa wazungu na vyombo vyao vya habari vya nchi za magaribi, angalieni kwanza hizi video mbili hapa ingawa hazizungumzii mambo ya Zimbabwe, lakini ndivyo wanavyofanya katika kila kona ya dunia mpaka Afrika wacha Zimbabwe tu.


  Na mkifanya mchezo nitawafunguwa macho na akili zenu kwa kuwapa information zaidi za unafiki wa nchi za mgaribi na hapo ndiyo mtabaki vinywa wazi na kugunduwa kwamba bado mko nyuma.

 21. binti-mzuri Says:

  mugabe please leave zimbabwe alone!huna haya!

 22. mahamed Says:

  kweli hii ni hatari,iweje leo mugabe mmoja awadhulumu hawa wazimbabwe pote?ni wakti muafaka kwa waafrika kuwakomboa wazimbabwe ambao ni wafrika wenzetu kumtoa huyu nduli,fashti,dikteta
  wafrika amkeni

 23. karunguyeye Says:

  shetani siku hizi haji kwa sura za wanyama na madubwana ya kutisha, siku hizi ankuja kwa mtazamo mpya na anavaa suti, tie na miwani mbaya kaka ya bw robert, pia anakula keki na sio damu.

 24. Lilian (Aisher) Says:

  Mugabe Muogope Mungu umekaa sana madarakani waachie wenzako kidogo. utajibu nini kwa mungu hii ni dhambi kubwa sana.

 25. sally Says:

  Mugabe pumzika baba mbona hivyooooooooo!!!!

 26. hombiz Says:

  Mimi!?…
  you don`t get the point dude! Dikteta mugabe anan`gan`gania madaraka. Hataki kutoka madarakani. Pamoja na kuwa wananchi wanateseka saaana kupita kiasi. Yeye hilo hajali kwa jinsi alivyo mbinafsi wa kutupa. Bila shaka anataka awe Raisi hadi mauti yatakapomkuta. Vitendo vyote anavyovifanya ni vya hovyo sana. Elimu aliyonayo wala haimsaidii kabisa kuchanganua mambo. Hivi sasa anatawala kwa mabavu tu. Na wanaomfanya aendelee kuwepo madarakani ni wale watu wake waliomzunguka serikalini ambao wanafaidika na yeye kuwepo madarakani. Otherwise, wangekuwa wameshamn`goa zamani sana kwa manufaa ya Taifa. Naamini kuwa si jambo la hekima wala busara kuvilaumu vyomba vya habari vya mashariki kwa udikteta unafanywa na Mugabe huko Zimbabwe.
  Na wewe mtoa maoni # 8, unayejiita Pound itabidi ufikilie ufanye upembuzi yakinifu kabla hujasifia kuwa Mugabe ni hero kwa kuwa tu ni anti-white. Kuwa anti-white kuna faida gani?. Nadhani alichotakiwa kufanya Mugabe ni kutetea maslahi ya Taifa lake. Hao whites waliokuwa wanaendesha mashamba huko zimbabwe, waliyaendesha kwa umahili mkubwa sana. Waliifanya zimbabwe kuwa ni moja ya nchi zilizozalisha mazao mengi ya chakula na ya kutosha kukidhi matakwa ya zimbabwe na hata kuuza njie. Lakini baada ya Mugabe kuwanyan`ganya hao wazungu mashamba, Tazama mambo yalivyoharibika. Upuuzi alioufanya Mugabe, haupishani sana na wa Iddi Amini wa Ugande. Iddi Amini aliwanyan`ganya wahindi biashara zao(za maduka) na kuwafukuza. Kisha akawapa wazawa wa kiganda yale maduka. Watu waliopewa maduka yale wengi wao hawakuwa na ujuzi wala elimu ya biashara ile. Wengine sidhani hata kama waliwahi kuwa wafanyabiashara ktk maisha yao. Matokeo yake maduka yote yakikufa yakabakia kama mapango tu. Sasa afadhali Iddi Amini tunaweza kusema hana elimu. Lakini Mugabe ni msomi. Sasa inakuwaje afanye maamuzi ya kijinga na kisha kujaribu kubebesha lawama kwa vyombo vya habari vya maghalibi? Angekuwa kweli ana nia njema na wazawa kutaka wamiliki mashamba, basi angewaelimisha vya kutosha juu ya ulimu ya kilimo. Then, baada ya kujua kuendesha shughuli za kilimo kiufasaha, labda ndio angeleta land reforms. Tena hiyo sera ilitakiwa iwe ni mpango wa muda mrefu. Si wa kukurupuka na kufanya overnight and openly like that.
  Mnakumbuka ule mradi wa wajapani wa kulima mpunga kule same, Tanzania?. Wajapani walipokuwa wanalima mpunga, mradi ulikuwa unaendelea vizuri saaana. Lakini walipoondoka tu na kuwaachia wabongo, mradi wote ulikufa kifo cha mende.
  Being anti-white, is not a solution to Africa`s problems. The main solution is unification. However, this needs to be done in a constrative way!

 27. It is true Mugabe was a hero at some point, but I think right now he is just the opposite. Just because someone did something nice at some point, doesn’t exonerate them for all their future actions. Unfortunately many of our African leaders, past and present have gone that route (hero to villain).
  I must admit, I still admire Mugabe’s decision to kick out the white settlers and give land back to the blacks. It took a lot of guts to stand up to the Western powers; guts most other African leaders lack.

  However, we have to realize the land reform was not an entirely heroic and patriotic move; it had some ulterior motives. If you recall correctly, the move came about as an ad-hoc maneuver to silence the ZANU-PF veterans who were threatening to overthrow Mugabe because they got tired of being ignored for so long despite them giving their all to fight for the country’s independence.

  Either way, whatever Mugabe did in the past, he should be judged according to his actions now. As outsiders we are not best-positioned to make such a judgment. If you want to know the true story, speak to a Zimbabwean, particularly one who lives there or has close relatives who do. I have, and I can tell you, the general feeling is that Mugabe is leading his country into abyss.

  We can not deny the fact that the UK has an anti-Mugabe standing right now, does not his help his image in the Western media; but, we can not and should not always blame the West and their propaganda policies all the time. It is about time we as Africans took a firm stand and started dealing with our own problems. Not every problem is because of the colonialists or the media problem. We have managed to create plenty a problem for ourselves. We are free thinkers after all.
  Yes, the sanctions imposed by Britain and her allies does not help the economic situation in Zimbabwe. But at some point, as a true leader, Mugabe should decide what’s best for his people. But more importantly, his people should decide whether Mugabe is best for them.

  Lets us stop this idealistic anti-white, western-propaganda talk and face the reality. If you do not have a Zimbabwean friend, find one and ask them the real situation. This is not a African political science class, this is reality we are talking about.
  We should not pretend like we didn’t see the clear election violations and atrocities conducted against opposition leaders.

  Mugabe was a hero, and what he did for his country and for the continent can not be denied. But it is time to pass on the torch.

 28. oh by the way Any, kwani hukumbuki Mugabe alikuwa single muda mrefu baada ya mkewe kufa in ’92, mpaka alipomuoa secretary wake aliyekuwa amemzidi miaka 41 mwaka .

 29. Mimi you have a point in a lot of ways kuwa Western media huwa zinatumiwa kama wapambe kueneza propaganda za serikali zao. Na pia a lot of westerners as well (particularly US citizens) are stupid and they believe almost anything their government and media say. A good example ni jinsi main stream media kama FOX zilivyouza sera ya vita dhidi ya Iraq na wnanchi wakadandia treni kwa mbele bila kujua ukweli; they even believed there WMDs there. Mwafrika yeyote aliyeishi nje anajua jinsi media inavyopotray vibaya bara letu kama vile ndio mwanzo wa matatizo yote duniani. Kuna ishu nyingine nyingi, mfano suala zima la so called “axis of evil”; yaani ukipingana na Marekani basi we ndio mwovu.
  Kurudi Afrika; kuna waovu wengi kama vile Mobutu, Savimbi, n.k. waliokuwa wanakumbatiwa na nguvu za magharibi na makucha yao hayakuwekwa hadharani kwasababu nchi za magharibi zilikuwa zinafaidishwa na uwepo wao. Kuna mengi tunaweza kulaumu juu ya ubeberu wa magharibi na propaganda za vyombo vyake vya habari.

  Lakini kabla hatujatoa kibanzi katika macho ya wenzetu, tuangalie borti zilizo katika macho yetu. Hatuwezi ficha Ukweli kuwa mara nyingi sisi wenyewe tunaharibu. Nyumbani Tanzania stori zinazotawala magazeti siku hizi ni za ufisadi; sidhani kama ni wazungu walitofanya tuwe fisadi. Kuna viongozi wengi waliotawala nchi zao kwa mabavu na kunyima watu uhuru; hatuwezi kusahau jinsi mlolongo madikteta kama Babangida na Amin walivyoharibu Nigeria. Mauaji ya kikabila ya Rwanda na Burundi, n.k. Kuna mengi ambayo wote tunayajua na hatuwezi kuyaorodhesha yote hapa.

  Hivyo basi, sio kila baya tukimbilie kunyosha kidole kwa wazungu, kwani vidole vitatu vinatuelekea sisi wenyewe. Lazima tuchanganue kila jambo kwa ukweli wake. Ushujaa wa Mugabe katika miaka ya nyuma isiwe kigezo cha kufumbia macho ubabe wake sasa kwa watu wake. Kuna wengi walioanza vyema kama yeye mwishowe wakaja haribu. Nilimtaja L. Kabila katika post yangu ya mwanzo. Kuna Iddi Amin pia alitajwa na Hombiz. Ukweli ni kuwa Obote pia hakuwa Malaika kama tunavyodhania, na kwa wananchi wa Uganda wengi, Amin alikuwa kama mkobmozi alipochukua nchi. Ila wote tunajua stori yake iliishaje. Kuna watu kama kina Charles Taylor aliyeng’oa dikteta Samwel Doe ila mwishowe ye akaja kuua hata zaidi yake.

  Nakubaliana nawe ndugu yangu Mimi kuwa tusidandie kila kisemwacho na wazungu, lakini nakushauri vilevile tusiwe kama hippies huku west ambao wanadandia kila ishu na kujifanya anti-establishment; anti-imperialism; anti-media; non-comformist and idealistic bila kuangalia kuchanganua na kuangalia ukweli wa mambo. Sio lazima iwe nyeusi au nyeupe; yaweza kuwa kijivu.

 30. BB Says:

  eh!kamzidi miaka 41!?!?!?!?!?!?!daaaaaaaaaaaaaaah!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 31. any Says:

  heri mimi sijasema! POLITICS! MCHEZO MCHAFU! SIHASA!

 32. Matty Says:

  Any ni siasa sio sihasaaaaaaaaaaaaaaaaa

 33. hombiz Says:

  Wapembuzi wa mambo naomba muingie hapa chini ili muweze kuona baadhi ya viongozi wa Afrika wanavyosema juu ya Zimbabwe na Mugabe Mugabe http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7494842.stm

 34. Lily Victor Says:

  I’m not happy with you Mugabe. First of all you are very old. How dare are you!!! Pisha vijana wachape kazi who told you you will be a President forever?? Mbinguni utajibu nini na uchu wako wa madaraka??

 35. Farahani Says:

  Huyu mzee na”ssuggest’ aitwe Mubabe na sio Mugabe!Ni noma!Nafikiri hofu yake kuu akiondoka madarakani atakiona cha moto toka kwa aliowanyang’anya mashamba!

 36. Farahani Says:

  Roho Bati Mbabe!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s