BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JAMHURI JAZZ BAND-SHINGO YA UPANGA July, 31, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:43 PM

Haya tena,mwisho wa wiki ndio umeshawadia.Kama kawaida ya dunia na ubinadamu,imekuwa ni wiki nyingine yenye pilikapilika za aina yake.Pilikapilika za maisha wakati mwingine hufanya nijiulize swali moja;Hivi ilikuwa ni nia na dhumuni la muumba kwamba dunia au wanadamu tuwe na mahangaiko namna hii au sisi wenyewe tu ndio tume-complicate mambo?Kama jibu ni ndio,basi kwanini tusimpigie goti muumba na kumuomba atuonyeshe njia na kuweka mambo yawe “tambarare” kama ambavyo pengine alikusudia?Haiwezekani au?

Anyway,kwetu sisi hapa BC ni muda mwingine wa kupata burudani. Burudani kama hizi huwa zinasaidia sio tu kwa kuburudisha bali kukumbusha jinsi enzi hizo zilivyokuwa.Yumkini ukijua ulikotoka au ukikumbushwa ulikotoka basi unaweza kupata unafuu wa kupanga uelekee wapi.Shukrani kwenu wote ambao mmekuwa mkituandikia na kutuambia ni jinsi gani burudani hizi za ijumaa huifanya wikiendi iwe nzuri.Kwa bahati mbaya kuna wakati tunaweza kuweka kibao ambacho kinaweza kukumbusha mtu au watu wako ambao walishaaga dunia.Hilo linapotokea ,jua kwamba huwa sio kusudio letu.Pamoja na hayo matakwa na Muumba hatuwezi kuyapindisha kwa hiyo cha muhimu huwa ni kumshukuru tu kwa kila kitu.

Basi leo baada ya kuzunguka kidogo barani Afrika tumeona turejee nyumbani.Wimbo unaitwa Shingo Ya Upanga kutoka kwao Jamhuri Jazz Band. Jamhuri Jazz Band ni bendi iliyoanzia mkoani Tanga(picha ni mandhari kidogo kutoka Tanga) miaka ya 1950s.Ni miongoni mwa bendi zilizowahi kutamba sana enzi hizo.Baadhi ya majina makubwa ya muziki waliowahi kutamba na bendi hiyo ni Wilson Kinyonga na George Kinyonga.Kuna haja kweli ya kuishi bila huyo mwenye Shingo ya Upanga?Pata burudani.Wikiendi Njema.

Advertisements
 

MCHAGUE MISS GLOBAL PUBLISHERS 2008 July, 30, 2008

Filed under: Miss Tanzania,Sanaa/Maonyesho,Tanzania/Zanzibar,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:27 PM

Zimebaki siku chache tu kabla ya Tanzania kumpata mrembo wake wa mwaka huu (Miss Tanzania 2008). Wadau wa masuala ya urembo tayari wameshaanza kukuna vichwa wakijiuliza ni nani ataibuka mshindi mwaka huu. Mashindano ya Miss World mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 4 October huko jijini Kiev nchini Ukraine.

Sasa wakati tukisubiri kumjua atakayetuwakilisha mwaka huu huko Ukraine, kampuni ya Global Publishers,wanaendesha zoezi ambalo litakuwezesha wewe msomaji na mtembeleaji wa mitandao,kushiriki katika zoezi la kumpata Miss Global Publishers miongoni mwa warembo wanaoshiriki Miss Tanzania mwaka huu.Utakachokuwa unachagua sio Miss Tanzania bali ni Miss Global Publishers.Utakuwa unamchagua mrembo ambaye unadhani ndio mwenye mvuto wa sura kupita wenzake wote.Mshindi wa taji hilo la Miss Global Publishers atajinyakulia taji na pia kitita cha Tshs 500,000. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kupiga kura tembelea tovuti ya Global Publishers kwa kubonyeza hapa. Zoezi hili limepewa baraka na Kamati ya Miss Tanzania.Pichani ni warembo wanaowania taji la Miss Tanzania 2008.

 

SHIRIKI KUPINGA MAUAJI YA ALBINO

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 2:11 PM

Tafadhali unaombwa kushiriki katika kupinga na kulaani mauaji ya wenzetu albino nchini Tanzania.Bonyeza hapa uone ni jinsi gani unaweza kushiriki.Kumbuka kwa pamoja inawezekana.Usisahau kumtumia link na mwenzako ili naye ashiriki.

Kampeni hii inaletwa kwenu kwa ushirikiano wa BC na Mwanaharakati Pius Pius.Tafadhali shiriki.

 

ONE ON ONE WITH MARIA SARUNGI July, 29, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 2:55 PM

Fani ya urembo au ulimbwende nchini Tanzania inazidi kukua na kujipatia umaarufu siku baada ya siku.Lakini ili fani yeyote ikue au iendelee, ni lazima pawepo mtu au watu ambao wanaamini kwamba inawezekana na pia kuna sababu za kutosha za kuwepo kwa fani husika. Mtu au watu hao lazima pia wawe tayari kujitolea,kwa nguvu na mali, kuhakikisha ndoto zinatimia, malengo yanafikiwa na mafanikio yanaonekana. Miongoni mwa watu hao ni Maria Tsehai Sarungi (pichani), Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ya jijini Dar-es-salaam ambao ndio waandaaji wa Miss Universe,Miss Earth, Miss International na Miss Tourism kwa upande wa Tanzania.

Baada ya kumalizika kwa kinyang’anyiro cha kumtafuta mrembo wa Miss Universe 2008 hivi karibuni huko nchini Vietnam, tulipata nafasi ya kufanya mahojiano na Maria Sarungi ambaye sio tu anathibitisha nia na dhamira yake ya kweli katika kuwapa fursa wasichana wanaopendelea fani ya urembo,kuiletea sifa na kuitangaza Tanzania kimataifa nk bali pia anaonyesha kuwa mwanamke ambaye yuko tayari kusimama imara katika kutetea jambo ambalo analiamini.

Pamoja na hayo,dhamira tupu haitoshi.Ni lazima iendane na vitendo na wakati huo huo kuwa tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali zinaweza kujitokeza. Katika mahojiano yafuatayo Maria anaziweka bayana changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo,mwelekeo na ndoto alizonazo kuhusu fani ya urembo nchini Tanzania. Lakini pia haishii tu kwenye kuziweka bayana changamoto za sasa na hata za mbeleni, bali pia anakwenda hatua mbili tatu zaidi mbele katika kuelezea mambo ambayo anadhani yakifanyika basi Tanzania itazidi kupaa katika ramani ya dunia katika mambo mbalimbali ikiwemo fani ya urembo ambayo hivi leo yawezekana kabisa kusema kwamba ana uzoefu nayo kwa kina.

Lakini je ilikuwaje Maria akaanza kujishughulisha na mambo ya urembo?Nini kilimvutia? Anasemaje kuhusu mashindano ya mwaka huu ya Miss Universe yaliyomalizika hivi karibuni?Anatoa wito gani kwa washika dau wa fani ya urembo nchini?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

REST IN PEACE MH.CHACHA WANGWE

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 2:50 PM

Bila shaka utakuwa umeshapata taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwamba Mheshimiwa Chacha Wangwe (pichani) amefariki dunia jana usiku kufuatia ajali ya gari iliyotokea sehemu za Kongwa mkoani Dodoma. Mh.Chacha Wangwe alikuwa ni Mbunge wa Tarime kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na alikuwa miongoni mwa wabunge watetezi wazuri wa haki na usawa miongoni mwa wanajamii.

BC inatoa pole kwa watanzania wote,ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu na inaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu.

Tunawaomba radhi wasomaji na watembeleaji wetu kwa kuchelewa kuwaleteeni habari hii ili kuwapeni pia fursa ya kutuma rambirambi zenu kupitia njia ya maoni.Hiyo ilitokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.


 

YANGA WAFUNGIWA;HALALI YAO?

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 11:10 AM

Timu maarufu ya soka ya Yanga ya jijini Dar-es-salaam(pichani) imefungiwa kushiriki michezo yoyote ya kirafiki na mashindano ya kimataifa ndani na nje ya Tanzania kwa muda wa miaka miwili.

Hiyo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania(TFF), Fredrick Mwakalebela. Hali hiyo inafuatia kitendo cha timu ya Yanga, maarufu kama Watoto wa Jangwani, kuingia mitini wakati walipotakiwa kutokea uwanjani ili kucheza na watani wao wa jadi, Simba Sports Club, katika mchezo uliokuwa wa kuwania nafasi ya tatu katika mashindano ya Kombe la Kagame yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar-es-salaam. Kombe la Kagame mwaka huu limechukuliwa na timu ya Tusker kutoka Kenya waliowalaza timu ya Uganda Revenue Authority mabao 2-1.

Je ni halali kwa TFF kuwafungia Yanga?Nini faida au madhara ya kuzifungia timu? Nani anastahili adhabu zaidi? Ni viongozi walioamrisha wachezaji wasiende uwanjani au wachezaji ambao kuwafungia ni kama vile kuwanyima haki yao ya kusakata kabumbu na kuendeleza vipaji vyao?

Photo/Issa Michuzi.


 

TUNAPOWAKUMBUKA MASHUJAA;NANI SHUJAA WAKO? July, 28, 2008

Filed under: In Memory/Kumbukumbu,Jeshi,Serikali/Uongozi,Sikukuu,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 11:44 PM

Kila nchi ulimwenguni ina mashujaa wake.Lakini tafsiri ya shujaa katika nchi nyingi ulimwenguni ikiwemo yetu ya Tanzania,huwa ni wale waliopigana vita iwe ya msituni,nchi kavu,majini nk.Hivi juzi nchini Tanzania ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya mashujaa.

Kama inavyoonekana pichani,katika siku kama hiyo,huwa ni wakati wa wanasiasa kuweka pembeni tofauti zao za kisera,kiitikadi na kimtazamo na kuikumbuka siku hiyo muhimu.

Pamoja na hayo,yawezekana kabisa kwamba wewe binafsi ukawa na shujaa wako binafsi.Kwa mfano,kwangu mimi shujaa ni mama yangu,aliyenizaa na kunilea mpaka kufikia hapa nilipo.Je kwako wewe nani ni shujaa wako ukiachilia mbali “mashujaa” tuliowakumbuka juzi?

Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi,CUF, Prof. Ibrahimu Lipumba (kulia) akifurahia jambo na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, walipokutana katika maadhimisho ya siku ya mashujaa iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam juzi.