BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HASIRA SIKU ZOTE NI HASARA? July, 4, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ni wiki nyingine tena, ni mwisho mwingine wa wiki.Mwaka 2008 unazidi kuyoyoma.Kwa wengi waliopo ‘ughaibuni” ni majira maarufu ya summer.Hapo ni mwendo wa watu kujianika juani kama vile hawajawahi kuona jua.Kwa wengi summer ndio maisha,ndio raha ya kuwepo duniani.Ni mwendo wa bikini na vilazia vyenye kuonyesha maungo yote.Majaribu.

Kwetu sisi wengine,kila siku ni summer.Hiyo ndio bahati tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.Kwetu jua halikomi.Fukwe nzuri nzuri tunazo.Tushindwe wenyewe tu.Au sio?

Kama ilivyo ada,hapa kwetu mwisho wa wiki ni muda wa kukumbushana kulee tulikotoka.Wengi tunasema enzi zile zilikuwa nzuri kuliko enzi hizi.Kuna wengine wanakataa.Wanasema hivi sasa ndio mambo yote.Kuna mitandao,kuna ipod,maendeleo makubwa ya sayansi na tekinolojia.Wanasema dunia yao ni kama kijiji haswa.Wa zamani nao wamesimama waliposimama.Wanasema kwanza wao ndio wameandaa mazingira haya ya leo kwa hiyo vijana wa leo wasijitape kupita kiasi.Basi tu ni mijadala kila siku.Tena mirefu isiyo na hata dalili ya kikomo.Sijui wewe unasemaje.

Ngoja nikatize maneno mengi.Leo tunao tena “Nginde” yaani si wengine bali Mlimani Park Orchestra.Wimbo unaitwa Hasira.Je ishawahi kukutokea ukamuacha mama watoto wako au la azizi wako wa karibu kutokana tu na hasira halafu baadaye ukajutia kitendo chako?Halafu huyoo ukaamua kwenda kuomba msamaha kabla hujakuta kumbe kuna gharama kubwa za kurudiana?Sikiliza wimbo Hasira hapo chini.Wikiendi njema.

Advertisements
 

7 Responses to “HASIRA SIKU ZOTE NI HASARA?”

 1. Mswahilina Says:

  Ama kweli Hasira hasara,
  Aksanteni BC kwa kutukumbushia Enzi zetu.

 2. Edwin Ndaki Says:

  Ijumaa ipo pale pale..

  asante sana BC kwa kutukumbusha enzi hizooo…

  Yaani kweli “songi” limetulia sana.Nasikia tu sauti za wazee wazima.

  Matty…badaye basi tuonane Knyama darajani kwa Dan.
  Gervas ..tuonane mwarufote au kwa mama abel..

  wadau wengine tutaona kwenye tingisha..tuone kama imekwisha…

  Ijumaa njema

 3. DUNDA GALDEN Says:

  BC NA TIMU NZIMA WAKINA JEFF SAFI SANA
  THIS WE CALL HOME SICK MA MAN ….
  UNASEMA CHA NINI KUMBE BADO UNAKIROHO PAPO
  SASA UKIMKUTA WATU WAMEULIZIA CALL UTAJINYONGA
  WAJAMAN NAWATAKIA WEEK END NJEMA
  CHAFOSA

 4. Panjee Says:

  Dah kwa kweli mimi nasema DDC ni zaidi ya Msondo hebu sikia hilo songi inanikumbusha miaka ya 84 85 nikiwa kule nyumbi bombi hii kuna mshkaji wangu akiitwa Aidan alikuwa anaupenda sana huu wimbo tuwekee nyingine mazee za hao wazee wa Ngoma ya Ukae napagawa sana nikiwakumbuka magwiji kama Beno Villa anthony, marehemu mwanyiro, Chidumule, huyu nadhani sauti yake haijawahi kupatikana hapa bongo HASSAN REHANI BICHUKA.hivi hawa jamaa hawawezi faidika na kazi zao maana zina thamani kubwa sana

 5. Michael Mloka Says:

  BC tafadhali muwe mnaweka nyimbo zaidi ya moja. This is really TZ at its best, yaani hapa hakuna mfanooooo. Duh kweli nyimbo za Bongo mali. It’s a pitty vijana turned into useless flava, then again siwalaumu kwani hawana vipaji ndio maana wanajiingiza kwenye flava.

 6. Matty Says:

  Jamani huwa natamani wknd ifike nipate kipoza roho hapa bc..ukweli mnatupa miziki mororo aluuuuuuuuuuuuuu E.Ndaki sasa Dan sikuhizi haweki pilipili nimehama kiwanja huwa naenda kuifata ile kitu Mwenge kona Bar kwa chini kidogo kwa mama mmoja hv wa kichaga!

 7. bdo Says:

  imebidi nirudi ijumaa hii ili kujikumbusha enzi zangu, maana hii ya leo mzee mbaraka imezidi uzito


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s