BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MWAKYUSA na MIGIRO July, 15, 2008

Filed under: African Pride,Kutoka Ughaibuni,Serikali/Uongozi,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 10:48 PM

Pichani ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Tanzania,Mheshimiwa Dr.David Homeli Mwakyusa(kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr Asha-Rose Migiro wakiwa katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York hivi karibuni.

Siku hizi watanzania wanaotembelea ofisi za Umoja wa Mataifa wanasema wanajisikia faraja zaidi na kuhisi wako nyumbani kutokana na kuwepo kwa Dr.Migiro ambaye amekuwa akiwapokea vizuri sana.Safi sana Mama Migiro.

UN Photo/Paulo Filgueiras

Advertisements
 

26 Responses to “MWAKYUSA na MIGIRO”

 1. Pearl Says:

  mama na elimu yake ana-enjoy life tu sasa hivi,hongera Dr.Asha uko juu,wacha na mimi nijitahidi nifike hata huko world bank.

 2. Gervas Says:

  Shavuz…..kumbe hamna mwembamba duniani. Kila wakionyesha kwa runinga makao makuu ya UN, utaiona bendera ya Tz, huwa najisikia uroda.

 3. Matty Says:

  Kweli money talks!!!!

 4. any Says:

  pesa inapohusishwa na unene, hii ni kibongo bongo tu! Wenzetu wanaiona sivyo. na mara nyingi kwenye nchi zao wale wasio na hela ndio wanene maana wanakula Junk food! au eti mtu yuko depressed ananenepa majuu, wakati tz ni vinginevyo! watu wenye hela tz wana vitambiiiiiiiiiiiii na wakipita njiani unasikia duu fulani hela imemkubali, kumbe wanakula ovyo, especially wababa hawali nyumbani, wanaongoza kwa kula bar, wala sio kwenye hoteli za maana. kwa wenzetu akuu, ukiwa na hela unakula the right food ili kuepuka obesity, na cholestrol zisizo na mpango. ni nadra sana ukute tajiri wa ulaya au US ata Japan wana manyama yameflip kila mahali, hata kiuno hujui kiko wapi.
  apa nyumbani naona kwa mbaaaaaaaaali watu wanaanza kula fruit salad for lunch ili wapungue kidogo, ila sasa ikifika jioni wanaharibu diet maana wanaenda shushia ngano za rose garden, so bidii yote ya mchana inakuwa ziro. ukimkuta mtu anakuambia mi nakula sana matunda na mboga ila sipungui! mtu anagoma kuacha bia anasubiri kukonda, sijui ni kwa miujiza au?

 5. kekue Says:

  Ss jamani sio kila anaekwenda huko awe anafika ofisini hapo kha, manake ss kila kiongozi akifika lazima aende kwa migiro kisa katoka tz; mwacheni afanye kazi.

 6. hombiz Says:

  elimu ni ufunguo wa maisha!. Now, all drop outs! Go back to school and finish what you started!

 7. Frateline Says:

  Hi guys, kutoka Helsinki-Finland

  Kwa kweli Mama, Dr. Migiro huko juu, Hongera sana, unatuwakilisha vizuri maana wazungu waliokuwa wanachonga ulipoteuliwa walie tu, dunia ya kumdharau mtu mweusi imepitwa na wakati, Kwa kweli mimi ninafarijika sana ninapoona watu weusi hususa wenye asili ya Africa wanaongoza dunia ninapata furaha sana maana historia inaonyesha mababu zetu waliteswa muno na baadhi ya matatizo ya sasa ya Africa yanatokana na historia hiyo chafu, Pia kuna wazungu wanapenda white supremacy(white mentality) na kudhani mtu mweusi uwezo wake mdogo, wapo wazungu wajinga kama Dr. Watson alihoji uwezo wa akili ya Mwa Africa na kusema ni mdogo kuliko wazungu, kitu ambacho sio kweli dunia nzima ilipinga, sasa mama kamuuuuuuuuuua mpaka wazungu wabaguzi wajinyonge, pokea salute za mataifa yote kwa niaba ya bosi wako Ban k moon , hongera sana,

 8. hombiz Says:

  any unayoongea ni kweli. Back home watu wengi bado wanadhani kunenepa ni kuwa na mambo mazuri wakati hivyo ni-ndivyo sivyo. Hata kwenye swala la mazoezi nyumbani bado ni kimeo! People needs to exercise more often!. Stop gaining too much weight! It is dangerous to your health people.
  You better make a triangle-school,work, and exercise!

 9. pound Says:

  hasikiki kimataifa,sijawahi hata kumuona kafanya ziara europe mhhh kakaa tu hajitangazi ,nilimuuliza mtoto 1 wa hapa eti naibu katibu mkuu wa UN ni nani akasema ni yule kama mchina mchina lol. huyu mama hata hajitangazi nilitegemea CNN,BBC awe ndio kichwa cha habari ampite hata condoleeza rice kwa umaarufu.

 10. Pearl Says:

  any #4 uliyosema ni kweli kabisa,tena kuna tv fulani nimeisahau jina lake hua inarusha kipindi kinaitwa “what you eat is what you are”.
  watanzania tunatakiwa tuondokane na hiyo dhana potofu ya kuona mnene ndo mweye pesa,kumbe mnene ndo mwenye kisukari,pressure n.k.

  pound #9 inawezekana kweli hajitangazi kama ulivyosema ila kumbuka kila mtu ana staili yake ya uongozi sio lazima awe au ampite Condoleeza.Uongozi uko wa aina tofautitofauti.
  Ngoja nikupe fact moja, WACHUNGUZI WANASEMA MELI YA TITANIC HAIKUANGUSHWA NA ILE ICEBERG BALI NGUVU YA MAJI YALIYOKUWA CHINI YA ILE ICEBERG.
  Back to the issue,Migiro is playing silent under the water,just wait she will shock you one day even though hajitangazi,na pia haimaanishi wale wanaojitangaza they are more powerfull kuliko wasiojitangaza.

 11. ds Says:

  pound,umeongea jambo la msingi..ni fulsa nzuri kujitangaza ingeweza hata ku boost sector ya utalii indirect..watu mataifa tofauti duniani wangeijua tanzania…au mama anagwaya kufuatwa sana na vyombo vya habari??!!

  chakushangaza hata hapa south africa-kuna watu hawaijui tanzania…kenya inafahamika sana..nilistaajabu kumuuliza raia flan(university student) hapa south africa kama anaifahamu tanzania…akasema hapana..niliposema mlima kilimanjaro akasema ndio anafahamu upo KENYA…nilitoa mimacho mie….

  ds-uj auckland park kingways campus

 12. any Says:

  true that hombiz! mtu ana 35 kitambi kama ana expect, kisa ni afisa wa masoko kampuni fulani, au afisa wa TBL kwenye bia za bure

 13. Gervas Says:

  Embu aaacheni uzushi jamani kuhusu kitambi. Kitambi heshima babake!!! waacheni wazungu wakonde! ukitembea kwa mguu tu texi kibao zinasimama kila zikipita, pia unaweza kopa bia baa ukalipa kesho. naongelea hasa kile kitambi kinachosababishwa na pombe ya kienyeji…….mnazi.

 14. binti-mzuri Says:

  mmmmhh…mtu pesa!

 15. Frateline Says:

  Hii Guys, kutoka Helsinki,

  Kwanza naomba samahani sio kawaida yangu kudandia hoja ila sipendi hoja ya kupotosha umma, Kwanza kigezo ktk mjadala wa unene na kukonda kisiwe kudhani wazungu ndiyo smart sana hii nayo ni ugonjwa wa kuwaabudu wazungu, ngugi aliwahi kusema Waafrica wamekuwa–colonized mind, kasumba ya kudhani kila kitu kizuri ni mzungu, kuna Waafrica wengi wanafanya mazoezi ni jambo zuri, lakini mimi huku finland kuna wazungu kibao wamejiachia na wala sioni hao mnaosema wamekonda, wanakula wafini kama mchwa, pia nao wengine wanakula majunk food ya kwenye masuper market, lakini wapo pia wafini ambao wanafanya diet na mazoezi, Lakini African culture sio ya kudharau kuna mambo sisi kama waafrica tunaona fahari wakati wazungu hapana, sio vizuri kujifanya sisi ni wazungu sana kuliko wazungu wenyewe, money speaks bwana, kama unapesa lazima utanawili na kama kitabi kipo ni poa, kwa WaAfrica upo juu na ni vizuri, sisi hatujazoezi watu wanaojikondesha na ukimwi wa sasa watu watakunyoshea vidole bora nenepeni achana na wazungu koko.

 16. any Says:

  Wee mtu wa Helisinki mbona unajicontradict! msimamo wako ni upi? Kitambi ni ishara ya pesa yes or no? Ukishajibu apo ndio tuendelee! Sijasema wazungu wote wanajikondesha au hawako Ob, NO! Wa US wanaongoza kwa kuwa na watu wanene na matatizo ya highblood pressure etc! Nachosema majority of people who are extra big ni maskini, ambapo kwetu tunawahusisha na kipato kikubwa, hiyo ni mbaya! hatutakiwi kuiga kila cha mzungu ila ukweli unabakia pale pale, UNENE SIO AFYA! mi mwenyewe apa ni mnene, and i am not happy about that! i am working on that~! get rid of that few extra pound, chaa.

 17. any Says:

  Nimesahau, pamoja na magonjwa yanayoambatana na unene, pia unene unazuia shughuli binafsi katika couples! mtu mnene anahema vibaya kama landrover ya zamani imeshindwa kupanda mlima!

 18. hombiz Says:

  Frateline hizo ni pumba. Kujali afya yako sio kwa kufanya mazoezi haimaanishi kutawaliwa na wazungu kiakili. Hili ni swala la muhimu na linafaa kuzingatiwa. Hata huku nchi za hawa wazungu wanawaelimisha wananchi wao kila siku ktk show, vipindi mbalimbali vya radio na television juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi.
  Na kasumba ya nyumbani kumshabikia mtu mnene au mwenye kitambi ndio mwenye maisha mazuri, hiyo bado ipo saaana. Kwa nchi hizi za dunia ya tatu kuwa mnene sana na kitambi, haimaanishi kuwa wewe una maisha mazuri. Watu wengi walionenepa sana wana matatizo ya kiafya. Wengine wanageukia chakula kama njia ya kupambana na depression. Na matokeo yake ndio hayo, kunenepa bila mpango na kujisababishia matatizo ya kiafya kama kisukari, moyo, BP na kadhalika.
  Pia kuhusu swala la kudhani wazungu wako smart sana. Naweza kusema ndio wako smart sana. Huyo Ngugi wa Thiongo mambo yalipumchachia huko Afrika, alikimbilia wapi kama si kwa wazungu hao hao aliosema wametawala akili za wa-afrika? Kwanini mambo yalipomchachia huko kwao basi asingeenda nchi nyingine ya kiafrika kama Ghana, Tanzania ama Uganda kuishi?
  Pili kama wazungu sio smart, wanawezaje kuweka viongozi vibaraka wanaowataka ktk Nchi za Afrika?
  Kama wazungu sio smart, wanawezaje kuwagawanya waafrika na kuwafanya wachukiane na kupigana kwa chuki za kidini na kikabila?
  Kama wazungu sio smart, wanawezaje kutumia wasomi(smart) waafrika kukana nchi zao na badala yake kukubali kuwa vibaraka wao ktk kuinyonya afrika?
  Hao waafrika unaosema wewe ni smart ni wangapi na ni nani anayewaunga mkono huko Afrika?
  Mimi ni mtanzania damu na nnaipenda sana nchi yangu. Lakini pale inapotokea hoja ambayo naona sikubaliana na jambo fulani kuhusu tamaduni au jambo fulani, siwezi kuliunga mkono kwa kuogopa fulani atasema nimetawaliwa na wazungu kiakili. HELL TO THE NOOOOO!
  Narudia tena! Tengeneza ratiba ya pembe tatu. Shule-kazi-na mazoezi.

 19. Mama wa Kichagga Says:

  Tunda la Weruweru.

  Mungu akujalie uishi kwa amani na ufanikiwe sana! Mwanamke kazi na kujituma, maneno ni sumu ya maendeleo!

  Asha-Rose umetupachangamoto nzuri sana hata kama nafasi yako inahitaji mtu mmoja sisi tunajisikia kama wote tupo pamoja tunawajibika.

  Mungu akubariki hadi uongoze nafasi kubwa zaidi ya hiyo.

 20. Frateline Says:

  Hi Guys, kutoka Helsinki-Finland

  Kwanza ninapenda kukubaliana na baadhi ya hoja zilizotolewa hapo juu na ndugu any pamoja na hombiz, ni kweli unene sio afya ni matatizo kwa vigezo vyote, LAKINI HUU NI ULIMBUKENI UPO SEHEMU ZOTE blacks and whites, wapo wazungu limbukeni nao wananenepeana sana , kwa hiyo sio tatizo la wa bongo tu na hii ndiyo ilikuwa hoja yangu,halafu ninakubaliana nanyi kuwa pia bongo na sehemu nyingine za Africa upo ulimbukeni wa Kitabi kuwa ndiyo ishara ya pesa, ni kweli kwa maelezo yenu nimewaelewa na ninaunga mkono hoja yenu, pili kuhusu usmart wa wazungu, ili tena ni tatizo la kifikira, kihistoria na ni pana muno siwezi kulielezea hapa maana hii ni course yenye lectures 8 kwa mwanafunzi wa chuo kikuu hivyo naomba nisikubali wala kukataa na usmart wa wazungu(ktk hili nipo neutral) ili kuweka kumbukumbu sahihi za BC kusudi historia isije kuniukumu, Lakini kwa kifupi tumeanza kuwaamusha watu jinsi hawa wazungu wanavyoendelea kulinyonya bara la Africa ni AIDUI namba moja wa MwaAfrica, Africa is not free, wazungu bado wanaingangania, tulipata uhuru wa bendera kwa masharti, sasa ni jukumu la kizazi chetu vijana kuanzisha ukombozi wa kiuchumi(economic liberation of Africa), na hii ni kazi ngumu sana maana kila kijana wa KiAfrica ndoto yake ni kuishi ulaya(Brain drain) ni tatizo kubwa kwa Africa, tusikate tamaa tupambane, maana kukili usmart wa wazungu ni ishara ya kukata tamaa, asanteni sana. ninaamini tutafanikiwa, pia ndugu zangu ANY na HOMBIZ kwa taarifa kwa sasa ninamaliza kuandika kitabu changu chenye ujumbe MAADUI wawili wakubwa wa Bara la Africa mwishoni mwa mwaka nitawatumia copy , (November, 2008) kitakuwa tiyari.

 21. Matty Says:

  Mimi narudia tena money talks kibongobongo!
  Upande wa pili wa shilingi kiuzunguni Any umeshatusaidia.

 22. any Says:

  mama wa personal decision umerudi tena! Money talks! haaa, Pesa imemkubali jamaa hadi ana kifriji!

 23. pound Says:

  HIVI NYINYI MKO SAWA SAWA KWELI MNA DISKASI UNENE BADALA MMWAMBIE HUYO MAMA YENU AITANGAZE TZ MI HAKI YA MUNGU INANIUMA HUYU MAMA MUNGU WANGU BORA NA BENARD MEMBE KAKAA TU NEW YORK KATIBU MKUU NDIYE ANAEANGAIKA KAMA NAIBU HATA MIKUTANONI HAONEKANI KAMA HAJUI MOMBO ASEME KHAAA, JAMANI AITANGAZE TANZANIA SIO KUKAA HAPO NEW YOOOOOOOORK ATEMBEE AMWANGALIE CONDOLEEZA UTASEMA YEYE NDIO KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA.PUUUUUUUUU WATZ BWANA

 24. binti-mzuri Says:

  ivi nyie watu naoo.. i know ndio aitangaze tanzania,lakini kwani ye kawa appointed kuitangaza nchi au to work for UN!?!? thats one thing she might do,as a mzalendo, but huwezi sema atembee tembee asiake new york sasa kazi zake amwachie nani wewe pound wa posti 23!!? she gets paid to do what shes appointed to do, hiyo kazi ya kwenda kuwagongea watu nyumba ‘ go to mount kilimanjaro’, etc etc haimlipi mshahara..sanasana a lot of people watapata coberage of the country coz obviously wata question mama migiro katokea wapi,and over dinner anaweza akawa anaongelea her country, just socially. mbona kofi annan wa ghana,wasnt heard talking 24/7 kuhusu ghana, he was doing his job. sometimes inabidi muwape people space to breathe.its getting too much sasa. yani iwege kuitangaza nchii tuuu… huyo balozi wenu marekani,si ndio kazi yake hiyo au

 25. binti-mzuri Says:

  ds wa posti 11,rafkiangu mie hata sishangai… nilishawai kusema hapa,watu wakanijia juu.. ‘ooh tanzaniaa inajulikana kuliko kenya’..mi nawaambieni bwana, kenya wana tourism department iliyotulia. hapa nilipo,people go on holidays huko kenya for a safari,wakirudi wananiambia ooh we went to ur continent to see mount kilimnjaro in kenya,mombasa blah blah.. unamwelezea mtu mpaka unachoka.kwanza anakushangaa unang’ang’ania uko tz na ye anasema ameuona kwa macho kenyaa..tz haijui wala haitambui..astakafurululai,ng’ombe wa maskini hanenepi

 26. Dangerous Forest Says:

  Nini kuzungumzia unene au wembamba nyie ? USA ,Helsinki ndiko wanakowafundisha mambo mnaotuandikia hapa ? Kama mnakwenda kwenye nchi za watu na kuanza kujadiri unene au wembamba wa watu ni heri mrudi Tanzania.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s