BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NDEGE MJANJA HUNASWA NA… July, 15, 2008

Filed under: Magazeti,Mambo Mseto,Mfanyabiashara,News,Siasa — bongocelebrity @ 3:54 PM

Ukiweza kumalizia kichwa cha habari hapo juu utakuwa umepata mwangaza wa mtizamo wangu kuhusu vuta nikuvute inayoendelea kati ya Mchungaji Christopher Mtikila na Mbunge wa Igunga,Rostam Aziz.Kwa msaada zaidi wa kinachoendelea(kama bado hujafuatilia kinachoendelea) bonyeza hapa.Mwananchi amuamini nani?

Advertisements
 

21 Responses to “NDEGE MJANJA HUNASWA NA…”

 1. Frateline Says:

  Hi guys, kutoka Hlsinki-Finland

  Wanasiasa bongo wote ni wasanii, hakuna msafi wote wanatakiwa kutubu, tatizo hili la rushwa na ufisadi limelitafuna bara zima la Africa, Ni lazima watu waache unafiki wa kujifanya wao ni wasafi kumbe ni wachafu wataumbuka kama mtikila, hakuna mwanasiasa alikuwa machachari na makini kama mtikila, sasa mtikila kwisha maji yakimwagiga hayazoleki, ndiyo maana CCM itadumu sana bongo kwa sababu hakuna mbadala. Halafu tatizo la ufisadi ni kubwa sana kuanzia kwa mwenyekiti wa kijiji mpaka taifa, kila idara ya serikali imejaa mafisadi ripoti za mkaguzi wa serikali za miaka mitano ya hivi karibuni zinaonyesha hivyo hakuna hatua inayochukuliwa wala sasa hivi watu hawaogopi hati chafu maana mpaka ofisi nyeti za wakubwa zina hati chafu hivyo tatizo sio kubadili kiongozi mmoja wa juu swala ni kubadilisha mfumo mzima wa jamii kwa toba ya kitaifa hakuna msafi. Mashuleni, vyuoni , mahakamani na mahospitalini rushwa imekuwa sehemu ya maisha, rushwa iko kwenye damu ya Waafrica, kenya wanatisha zaidi lakini na sisi bongo tumo. TOBA YA KITAIFA BILA KUNYOSHA VIDOLE MAANA VITAKURUDIA KUMI KAMA MTIKILA.

 2. Mswahilina Says:

  B.C. Hahaha haaaa
  Ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bovu.
  PIA: Vyote ving’aavyo si dhahabu.

 3. DUNDA GALDEN Says:

  ((MUNGU IBARKI TANZANIA ITABALIKIWA VIPI BAADHI YA WATU VIGEU GEU HASWA VIONGOZI))
  MIMI SINA NENO KWANI MREMA ALIMALIZIA NA MWL NYERERE ALISEMA TUKUMBUKE SASA ZIE ALAMA ZA NYAKATI ZINAJIONYESHA MBIVU NA MBICHI
  (KWELI BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA TUSEME NA SHIDA ZETU)
  HATUKATAI KAMA FISADI AU LAH NANI ANAJUA?KIASI CHA PESA ALICHOKUWA NACHO KARITH TOKA KWA MABABU ZAKE HIYO MADA NZITO MIMI SIMO KAZI KWENU..
  …..LEO UNASEMA FISADI UNAKWENDA KUKOPA PESA KWA FIKLA UNAWAZA NA KUWAZUA HATO PASUA JIPU ULIKWENDA KUOMBA KAMA MATONYA MLIO MFANYIA KAMPEN YA KUFUKUZWA ETI KATIKA JIJI LINALOITWA BANDARI SALAMA SASA HUO USALAMA UKO WAPI?GOLOFA LINADONDOKA HALI YA KUWA LINAJENGWA NEVER SEE LIKE THIS THINGS MIMI VOTE YANGU NITAMPA YULE NITAKAE MUONA HASWA SAFIII
  CHAI GODA

 4. Frateline Says:

  Hi guys,
  Nimemsikiliza Bwana Rostam Aziz akihongea na waandishi wa habari kupitia ”KLH News International kijiji leo” kwa kweli Mtikila ni mnafiki, maana this is the rise and the fall of Mtikila, Mchungaji ni cheo cha kujipachika, mtu wa mungu hawezi kuwa ndumila kuwili, kuongea chuki, majungu na fitina, hata kama ungekuwa ni mkopo , mtu wa kweli wa mungu hawezi kumugeuka mkopeshaji, yaani mimi nikukopeshe pesa halafu wewe kesho unituhumu hadharani, je huu ni uungwana? sasa hivi dunia imefika pabaya, wachungaji feki na matapeli ni wengi, mungu endelea kuwaumbua, kweli ndege mnjanja unaswa kwenye tundu bovu.

 5. what’s even more ironic about this is the fact that Mtikila rose to “fame” with his anti-Asian stand, a.k.a Gabacholi policy. Now he goes and asks for money from someone he considers a Gabacholi.

 6. Ghalib Says:

  Sasa imebainika maneno yote anayongea mtikila hayatoki moyoni mwake isipokuwa ni msukoma wa “nJaa”.Inastaajabisha mtanaganyika halisi akakope pesa kwa ‘Gabacholi”_Ukistaajabu ya Musa …………………

  Ghalib

 7. Matty Says:

  ya kaisari mpe kaisari na yangu mpe mungu!

 8. anisa Says:

  fratelina umesame ukweli kabisa,mambo ya kifisadi yapo kila sehemu.Ila lake limevuja ndio anatafuta njia ya kujikosha.

 9. Pearl Says:

  mi yangu macho na masikio.

 10. Debora kiaka kizuguto Says:

  Na wewe umezidi umepewa kazi ya kuchunga kondoo wa bwana inaelekea inakushinda kila siku kwenye ulingo wa siasa kumbuka mungu wetu hachangamani na kitu chochote acha kujichanganya wewe kazi yako ni kuwaelekeza watu safari ya kwenda mbinguni na kuvua samaki yaani kuleta watu kwa yesu wasimjua yesu wamjue, lakini kila siku uko ulingoni katika siasa lazima usisike kumbuka mungu hadhihakiwi chochote apandacho mtu. na mshahara wa dhambi ni mauti sio lazima uchimbiwe kaburi cha kwanza ni kutegwa mbali na uso wa mungu na kuumbuliwa kama hivyo be carefully mtumishi kumbuka wokovu sio lelemama ni kujikana nafsi na kujitwika msalaba.
  Debora

 11. kipanya1 Says:

  HABARI WADANGANYIKA WENZANGU
  Namshukuru Mungu.
  Naamini nanyi ni wazima kama mimi, poleni nanyi wagonjwa Mungu awaponye haraka ili tuendelee kujenga hili taifa la Wadanganyika.

  Nikweli Rev.Mtikila ni maarufu katika nchi hii ila hakuna aliyeweza dhani kama na yeye ni FISADI na yupo pamoja nao kwa kipindi kirefu; ila MUNGU kwa uwezo wake ameamua kutufunulia Ufunuo Mwingine sisi WADANGANYIKA.

  Nikweli tumewaona wengi sana kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja na hii ni mwanzo kwao wote MAFISADIS. Siasa ya Bongo tatizo njaa yani huwezia amini watu wanakuwa hawana mili ya kupigia picha ila wakikaa kidogo madarakani na Wadanganyika wasipo sumbua wananenepa wanabadili picha.

  Wapo wengi sana wanajifanya wanasiasa ila siku ikifika mtawaona wanakula nao sana, ndiyo maana wanadhulumiwa KURA wanapiga kelele wakionjeswa Asali ya Nyuki waitwao WADANGANYIKA pasi hukaa kimya nakubaki wakisubili Redio mamba mara CHENGE mara JK BOYs na Kameruni, EPA mara kimya Gumzo mitaa ya Wadanganiyi.

  Namshukuru Mungu kwa kutufunulia ufunua mpya na huu ni mwaka wa Shetani kwa MAFISADs

 12. Swordfish Says:

  NJAA, NJAA, NJAA. Someone please tell this man to shut up.

 13. piusmickys Says:

  Mtikila anasema: Even if he gives me more money i will take it. Religiously, i am forbidden from having enemies. Christianity wants me to love even my enemies. hahahahaaa

 14. hombiz Says:

  waarabu wa pemba hujuwana kwa vilemba!

 15. Debora kiaka kizuguto Says:

  Mtawatambua kwa matendo si utani.
  Debora

 16. ma'reen Says:

  Hata mimi nashindwa kuelewa mazingira yaliyopelekea Mtikila kwenda kukopa hela kwa Rostam, anaemuita fisadi, ‘si raia’ etc. I am tempted kuamini kuwa jamaa alimuendea na faili lake la uhamiaji…na kumtishia kuwa anajua A to Z kuhusu uraia wake.Jamaa kaona noma ikabidi wapange terms za kumziba mdomo…ikabidi amkabidhi jamaa mzigo.Au nyie mnaonaje? Otherwise senario nyingine ni kwamba jamaa kweli alimuendea kuomba msaada kwa “kanisa”.Akakabidhiwa mzigo ila akautia ndani hakuwakilisha kanisani.Sasa kukwepa soo la washiriki inabidi azushe ulikua mkopo…ha ha ha I LOVE THIS…sisi kimya wenyewe kwa wenyewe wanaanza kuumbuana!

 17. binti-mzuri Says:

  haha at swordfish!

  akiya baba mtikilaa huyu mchungaji wa kanisa gani,lake nini..maana simuelewagi huyu baba

 18. Mama wa Kichagga Says:

  Hii ni noma!

  Hiki kijiti kizuri sana!
  Sijui Rostamu na Mtikila watampasia nani anayezungumza Kiswahili maana hili darasa mwl kasema lugha ya mawasiliano ni Kiingereza tuu. Ijumaa ikifika watu wakaanza kuitwa kwa ajili ya fimbo za kijiti haaaaa mimi simu bora nimeamua kuwa bubu. Inafurahisha kwa kweli.

  Mafisadi wote watajikamatisha wenyewe kwa wenyewe hapa ama kweli huu ni mwaka wao wa shetani! Hapa bado wenye vijiti waanze kuwataja waliozungumza na hawajapewa kijiti haaaa.

 19. Matty Says:

  Hhahahahahaahahahahha Ma’reen mh! faili la uhamiaji tena?? kwani huyu nae ndo wale kina nanihii waliochanganya damu mama afghanistan na baba tz?? lazima kieleweke mwaka huu MAFISADI MTALIJUA JIJI!

 20. george Says:

  hivi huyu mtikila anayo akili kweli,atawezaje kwenda kukopa pesa halafu baadaye aanze ksema rostam ni fisadi?kama sisa imemshinda aende kijijini akalime tumemchoka na longolongo zake,

 21. kingo Says:

  ka-movie kazuri haka!!!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s