BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NAPE NNAUYE NA UONGOZI WA VIJANA CCM July, 16, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Special Interest News — bongocelebrity @ 10:19 PM

Hivi majuzi Umoja wa Vijana wa chama kinachotawala nchini Tanzania,CCM,umeanza safari ya kumtafuta Mwenyekiti wake mpya.Miongoni mwa vijana waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Nape Nnauye(pichani) ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania,Marehemu Moses Nnauye.

Nape Nnauye ameanza kampeni zake kwa kasi ya aina yake akianza na kuwashutumu wanasiasa wengine maarufu nchini kama vile Edward Lowassa na Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo,Dk.Emmanuel Nchimbi.

Pamoja na tuhuma ambazo hizo ambazo tayari zimeshaanza kuleta gumzo mbalimbali za kisiasa na kijamii,ni wazi kwamba yapo maswali mengi ambayo vijana wangependa kumuuliza Nape Nnauye.Kumbuka kwamba Umoja wa Vijana CCM ni mojawapo miongoni mwa nguzo muhimu za chama hicho tawala ambacho sio siri kwamba katika siku za hivi karibuni kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nzito nzito hususani kwa upande wa ufisadi.Je ungependa kumuuliza nini Nape Nnauye? Tutumie maswali yako aidha kwa kutumia e-mail bongocelebrity at gmail au kwa kutumia sehemu ya maoni hapo chini.BC ipo mbioni kufanya mahojiano rasmi na Nape Nnauye.

Advertisements
 

21 Responses to “NAPE NNAUYE NA UONGOZI WA VIJANA CCM”

 1. binti-mzuri Says:

  be careful kijana…hicho kiti hakina historia nzuri sana,nadhani mwajua

 2. Gervas Says:

  Hivi nani kawaambia wanaccm kuwa CCM ni chama cha ukoo??? babu, baba sijui mjukuu hebu pisheni huko wengine nao waongoze. Kilishakuwa chama cha kinafiki tu, yaani Kanzu mpya shekhe yuleyule. Simjui lakini ni walewale tu kina Nchimbi.

 3. hombiz Says:

  hawa watoto wa wanasiasa wameona ni fashion kugombea UFISADI siku hizi!

 4. Frateline Says:

  Hi Guys, Kutoka Helsinki-Finland,

  Kwanza ninawapongeza BC kwa kutuwezesha sisi wanachama wa umoja wa vijana na watanzania kwa ujumla ambao tuko mbali na Bongo. Kwanza ninapenda kumuuliza nape mnawiye lakini ajue hatutamchagua kwasababu ya baba yake, mungu amuweke pahala pema peponi, Je anajua kuwa chama chetu cha CCM nimejaa watu wengi ambao wanatiliwa mashaka na Watanzania na wengi ni vigogo, yupo tiyari kujitoa muhanga kusafisha uchafu, na kuwaanika wachafu kama ulivyoanza na Lowasa na Nchimbi au hiyo ni nguvu ya soda unataka kura na labda na hao hawakutaki kwahiyo na wewe unapambana nao kimtindo , na wewe lengo lako ni ulaji tu, je wewe Nape unatofauti gani na waliokutangulia, eleza mambo unayoona ni tofauti, je unamkakati gani na nchi iliyozama kwenye bahari kubwa ya ufisadi na rushwa toka ngazi ya kijiji mpaka taifa, Vipi unamkakati gani wa kupambana na wenye fedha za ufisadi kwa kununua kura na kuiba kura, CCM ni mali ya wenye pesa na sisi wanyonge hatuwezi hata kugombea udiwani kinyume na enzi za Nyerere pesa kilikuwa sio kigezo lakini sasa hivi umoja wa vijana na CCM kwa ujumla vimebinafsishwa kwa wafanya biashara na mafisadi, je kijana Nape unamkakati gani wa mambo yote haya, je wewe sio fisadi mtarajiwa, maana wengi walikuja kama wewe kwa kelele, na majina ya mr. Clean, Uwazi na ukweli, kumbe ni waongo na mafisadi wa kutupwa, na wametuuza kwa kuugeinisha yaani uchumi umewekwa mikononi mwa wageni, umoja wa vijana umeshindwa kuwa sauti ya vijana kwa sababu viongozi wote ni vibaraka, ukipiga kelele utateuliwa na rais ubunge au ukuu wa wilaya, je utakataa au utatumikia mabwana wawili? Eleza kwa ufasaha wewe unataka kuifanyia nini nchi yetu kupitia ngazi hiyo muhimu. asante sana ninasubiri majibu.

 5. Mr Tom Says:

  Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi kwa BC kwa kutoa kuandaa utaratibu wa mahojiano maalumu na Bwana Nape Mnauye (MNEC) kuhusiana na tuhuma nzito sana, alizoumwagia Umma wa Watanzania kupitia vyombo vya habari, tuhuma zinazomlenga Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa UVCCM Mhe. Edward Lowassa, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mhe. Dr.Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa UVCCM Bwana Francic Izack. Ninawapongeza BC kwani mimi binafsi nikiwa kada wa UVCCM na CCM kwa ujumla nilikuwa nikitafuta namna ya kumuuliza baadhi ya maswali ambayo yananisumbua akilini mwangu kufuatia tukio hilo ambalo shaka limetushtua wanaCCM wengi. Kwa hiyo BC,nawapongezeni sana kwa hatua hiyo!

  Bwana Nape Mnauye, natambua wewe kuwa ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa. Na katika maelezo yako siku unatoa shutuma hizo, ulisema kuwa wewe na wenzako mliupinga ndani ya kikao cha Baraza Kuu mchakato mzima wa namna mkataba wa mradi huo ulivyofikiwa. Nadhani hilo ni sawa kabisa. Ni kawaida kabisa kupingana kwenye vikao halali kama kuna jambo ambalo mjumbe hujajiridhisha nalo.Hata hivyo, kwa uzoefu wangu wa namna maamuzi ya vikao yanavyofikiwa, inaonekana kwamba ninyi mlioupinga mradi huo kutokana na udhaifu uliopo kwenye mkataba wenyewe hamkuwa wengi kiasi cha kuamua mradi usitishwe. Bila shaka ni kwamba waliounga mkono pendekezo la mradi walikuwa wengi. Na ndio maana Baraza Kuu likaubariki mradi huo. Sasa basi, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za vikao, hata kama kuna mtu/watu hawakuunga mkono hoja, mwisho wa siku yanakuwa ni maamuzi ya kikao na ni halali.Na ikibidi kura hutumika kufikia maamuzi.

  Sasa hoja zangu ni hizi zifuatazo!
  (1) Je, baada ya wewe kutoridhika na maamuzi ya Baraza Kuu ambalo wewe pia ni mjumbe, ulichukua hatua yoyote kwa mfano kupeleka hoja zako mbele ya vikao vya juu vya Chama kama vile NEC ambako wewe pia ni mjumbe?

  (2)Natambua kwamba agenda za NEC huandaliwa na Kamati Kuu. Naelewa pia kwamba ili uweze kutoa hoja yoyote ndani ya NEC ambayo iko nje ya agenda husika, unapaswa kupewa idhini na Mwenyekiti katika agenda ya mengineyo(Kama ipo). Sasa kama hayo yote kwa namna moja ama nyingine hayakuwezekana, Je, uliweza kufikisha hoja zako hizo kwa viongozi wa Kitaifa wa Chama? Kama vile Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Katibu Mkuu? Nina amini kabisa kuwa, kwa nafasi yako kama NNEC una fursa na uwezo kabisa wa kufanya hivyo, iwe ni kwa njia ya barua au hata kwa kuwaona viongozi hao, ana kwa ana.

  3.Shida yangu nyingine ni namna ambavyo umewasilisha tuhuma hizo kwa kuwalenga baadhi ya viongozi. Ninavyofahamu ni kwamba, maamuzi ya kuwepo kwa mradi huo ni dhahiri kwamba yalipendekezwa na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu. Siamini kwamba maanuzi hayo yalifikiwa na Mwenyekiti na Katibu Mkuu peke yao hata kama wazo hilo lilitoka kwao. Sasa je, kwa kuwashambulia Mwenyekiti na Katibu Mkuu badala ya Kamati nzima ya Utekelezaji huoni ni sawa na kutowatendea haki?

  4.Hali ni hiyo hiyo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mhe. Lowasa. Kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM, mwenye dhamana ya kulinda mali za jumuiya ni Baraza la Wadhamini na sio Mwenyekiti wa Baraza peke yake. Je, huoni kwamba kumshambulia Mwenyekiti peke yake pia ni kutomtendea haki pia? Na je, uliwahi kumuona Mhe. Lowasa kama mwenyekiti wa baraza na kumueleza kutoridhika kwako na namna utaratibu mzima wa mkataba wa mradi ulivyofikiwa?

  5.Kama sasa hivi wakati wa kuchukua fomu za kuomba kugombea uongozi umeweza kuwa na ujasiri wa kumwaga tuhuma hizo nzito mbele ya waandishi wa habari, ulishindwa nini kufanya hivyo hivyo kwa kuweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa shutuma hizo mara tu baada ya mradi huo kuanza au kupitishwa? Huoni kama kwa kufanya hivyo sasa, wakati wa mchakato wa uchaguzi inaweza Kutafsiriwa kama ni mbinu na mkakati maalumu wa kuvuta hisia za wapiga kura pindi ukibahatika kuteuliwa na vikao husika kuwa miongoni mwa wagombea?

  6.Kwa maslahi ya Chama, ningependa kupata maoni yako juu ya njia uliyotumia kutoa shutuma hizo. Ukiwa kama kiongozi wa ngazi ya juu katika Chama kama mjumbe wa NEC, bila shaka utakubaliana nami kuwa chama chetu sasa kinapita kwenye changamoto nyingi kufuatia tuhuma za ufisadi zilizowaandama baadhi ya makada. Sasa, je, kwa uamuzi wako wa kupasua jipu mbele ya umma kupitia waandishi wa habari huoni kama ni kuzidi kukizorotesha chama chetu na kutoa mwanga kwa upinzani kupata agenda ya kuendelea kukishambulia chama chetu?

  Mwisho kabisa, napenda ieleweke kwamba sina nia ya kutetea udhaifu wa kimaadili katika mradi huo (Kama ni kweli upo). Hapana, siungi mkono hata kidogo. Hata hivyo, tatizo langu ni utaratibu uliotumia kutoa tuhuma hizo. Siamini na haiingii akilini mwangu hata kidogo kwamba njia uliyotumia ilikuwa ndio muafaka. Na siamini pia kama kuna mwana CCM mwenye nia njema na chama chetu aliyeridhika na njia uliyotumia.

  Nitafurahi sana kama nitapata kujibiwa hoja zangu.

  Ahsanteni sana!

  Kidumu Chama cha Mapinduzi.
  Mwenyekiti mstaafu wa UVCCM(W).
  Bowling Green State University
  Ohio-USA.

 6. Mama wa Kichagga Says:

  Kwanza kabisa nampa Hongera Ndg Mnau kwa kuwa mstari wa mbele na kuamua kujitokeza kugombea nafasi ya urais wa vijana TZ (ila isiwe umeshauriwa chukua fomu alafu utatupeleka pabaya utakaposhinda uchaguzi).

  Mimi binafsi ningependa kumuuliza mgombea maswali yafuatayo:

  1. Je, mgombea amejiandaaje kuchukua nafasi anayoiwania (kielimu, kiutandawazi na kiteknolojia?)

  2. Je, ana sera gani kwa vijana ktk eneo la ushirikishwaji shughuli za chama (ilivyo sasa hivi lazima uwe na shina la mzazi au ndugu kuwa kwenye huo mkondo na hakuna utaratibu unaoeleweka hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi)?

  3. Nini sera zake za elimu na ajira kwa vijana ktk kukabili chamgamoto za maendeleo na mabadiliko ya kimfumo ya taifa?.

  3. Ningependa kujua mikakati yake ktk swala zima la ufisadi nchini

  4. Je, mgombea anasera gani ya kuwakomboa vijana wenzetu walio ktk mazingira magumu mfano CDs, wapiga debe nk ambao ni matokeo ya mfumo uliopo?

  Maoni:
  Sidhani kama ni sahihi kuomba kura kwa kuwakosoa waliokutangulia maana unanishawishi kuwa wewe si mtendaji bali mzungumzaji. Tanzania ya leo hasa sisi vijana tunahitaji vitendo na matokeo kuliko kuendelea kutupotezea muda kwa lawama na maneno yasio na msaada kwetu. Tuambie wewe utatufikishaje tunakotaka kwenda bila kututangazia mapungufu ya mtu maana kila mtanzania anaujua wimbo wa ufisadi sasa hivi hivyo tusingependa kutuzungumzia mambo tunayoyajua. Hapa tungependa kusikia ni mikakati gani aliyonayo mgombea ambayo itahakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake na sio blaa blaaa.

  Namtakia kila la kheri na mafanikio!

 7. Makwafya wa Manyamunyamu Says:

  kwa vile Vijana ndiwo TAIFA la Leo na kesho,

  Ni suluhisho gani la Muundo wa Serikali litakalojenga TAIFA lenye maendeleo katika kusuluhisha mgogoro wa CCM& CUF visiwani Zanzibar na kubwa zaidi juu ya mahusiano tete kati ya Tz bara & Visiwani juu ya Muungano wetu?

  (samahani sihitaji majibu marefu ya kisiasa jibu kwa mujibu wa maswali madogo yafuatayo:-)

  a. Je wewe binafsi unaunga mkono pendekezo la kuwepo kwa serikali mseto au ya umoja wa kitaifa Zanzibar? Kwa nini
  b. Je Muungano wetu (Bara) na Visiwani uwe wa muundo gani?
  i. Serikali mbili kama ilivyo sasa
  ii. Serikali mbili (Bara na Visiwani)
  iii. Serikali Tatu (Bara, Visiwani na ya Muungano)
  iv. Serikali moja ya Muungano
  v. Serikali tofauti na zote tajwa hapo juu (ielezee)
  vi. Pasiwepo na Muungano wowote

 8. Dunda Galden Says:

  Du BC kubwa

  (1) Swali je kunak itu gani kipya atachoweza kuwambia wana CCM na kuonyehsa mabadiliko pindi akibuka mshindi?

  (2)…Hatua gani atachukua kukiwa na maovu aidha kwa kuambiwa au kusikia na kubaini kweli je nini atafanya?

  (3)Ahadi zilizotolewa na chama tawala ni nyingi zilizotekelezwa kidogo yeye anajua je yuko teyali kueleza wana ccm au wananchi kama azijatekelezwa aseme kwa hiyari yake chama akifai au bora kuwe na serikali ya kiswati?
  hizi nioja zangu binafsi ikiwa nzuri zibaki mbaya mniachie lakini mnaweza kusawazisha ikiwa haziko sawa
  kazi bado ndefu

 9. Matty Says:

  We are tired of that bwana kila siku sura zile zile tu babu/bibi/kaka/binamu/dada khaaaaaaaaaa bora vyama vingine havinaga undugulaizesheni kama ccm jamani!

 10. binti-mzuri Says:

  mh hoja za humu ndani…. sijui ingekua vipi,si ndio tungekua bunge

 11. ED Says:

  Hahahaha, naanza na kucheka kwanza. Naona wengine mnamaswali mengi.
  Swali ni moja tuu, Kwa nini UVCCM wakuchague wewe na wasiwachague wengine.
  What is ur standing concern JK and EPA and Rostam. Can you separate them? If not do you believe in consitution of republic of Tanzania? If yes do you believe JK is illigemate president because EPA money put him in position.

  Then asked him about Chenge and his millions which he didnt declared them katika bunge. Will he push CCM kumnyanganya chenge kadi?

  I think hawa watoto hata shule awana, wanatafuta pesa ya kula na kununua vi range rover.
  Muandishi i wish niusike kwenye kumuhoji, nitajitolea kubiga simu and i will review my name kabla sijaanza kumuinterogate.
  Hawa wototo ni empty head tuu, wapo hapo kufull fill dream za baba zao.

  Ed

 12. wetu Says:

  i agree with ed,hawa ni warithi wa dynasty za kulindanakwa maslahi yao.toka huyu njoo huyu.babu ,mjukuu,tumuulize huyu dogo je anaweza kuikosoa ile dream team ya [bot]ambao wote ni watoto wa vigogo?na majina ninayahifadhi….tanzania kamwe haitakua na mabadiliko ya kimaendeleo kama….mizizi ya kiufisadi kukatwa.na mizizi mikubwa ya ufisadi ipo kwenye ccm….[chama cha mafisadi..ccm)na bado wana warithisha watoto wao kukalia viti vya kuzidi kuhujumu nchi

 13. Naanza kwa kumpongeza bwana Nape Nnauye kwa uamuzi wake wa kugombea nafasi ya uenyekiti UVCCM, nikiwa kada wa CCM nina maswali na hoja zifuatazo kwa mgombea:-
  1. je amejiandaa vipi kukiimarisha chama kama mwenyekiti wa UVCCM hasa wakati huu ambapo zimwi la ufisadi linataka kukitafuna chama
  2. je anafikiri kuwa kasi yake ya kukemea mafisadi itamsaidia kutimiza ndoto zake? je hizo ndoto ni zipi? na kama haitamsaidia ni njia gani mbadala atatumia
  3.je anatoa maoni gani kwa wagombea wengine katika nafasi yake?

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

 14. Matty Says:

  Ingekuwa vizuri wewe mgombea uje hapa ujibu hoja za wananchi wako plzzzzzzzz!

 15. MR HKN Says:

  Mimi nilisha wahi kuwa mjumbe katika shule ya sekondari niliyokuwa nasoma wakati huo. Nanilipata bahati ya kuhuzulia chaguzi kama hizi katika ngazi ya mkoa (Morogoro) kama mjumbe katika kumchangua mwenyeketi wa umoja huo wa mkoa.
  lakini kutokana na maswala ya shule nikaweka pembeni kidogo maswala hayo, lakini mpaka sasa napenda kufatilia sana maswala ya siasa hasa katika nchi yetu (Tanzania).

  Kwanza kabisa napenda kumpongeza bwana Nape kwa kufikia uamuzi wa kugombea nafasi ya uwenyekiti. Ninavyo fahamu mimi
  kuwa chama chochote cha siasa nguzo yake ni vijana katika mawsala yote ya kuendeleza chama. Kwa maneno uliyo tamka kwa ajili ya mkataba wa ukarabati wa jengo la umoja huo yana maana sana na yana ukweli ndani yake. Kwa sababu haiwezikani mkataba hauja sainiwa na wahusika wameaza ujenzi sehemu ya nyuma ya jengo hilo.

  1. Sasa ndugu Nape utatuhakikishia vipi? kauri uliyo towa ni dhati kutoka moyoni kwa ajili ya kutetea masirahi ya vijana? na sio giya ya kuombea kura?

  2. Je una mkakati gani hasa mawsala ya uchumi (miradi) kwa ajili ya umoja huo, kama ukibahatika kuchaguliwa?

  3. Je uko tayali kunywa maji ya bahari kwa kila tonge moja la ugari?

  Mwisho kama kweri unadhamila zuri nakuhakikishia utashinda tu uchaguzi huo, ingawa kutakuwa na rabisha za hapo na pale lakini ndo maswala ya siasa hatu huo nje rabisha hizo katika siasa hujitokeza ila wezetu si mafisadi na kama wapo wanaogopa makucha ya serikali.

 16. pwc Says:

  Hapo sasa

 17. Ed Says:

  Mr HKN.
  Maswali yako ni mazuri sana, lakini haya maswali walishaulizwa viongozi wote Watanzania. Na majibu yao ni mazuri tuu, sema wanapokwenda madarakani hapo ndio wanapofanya kisa cha Ndio Mzee.

  Hakuna maswali ya kubaby sitting anymore, just ask him challange questions kama sio controversial ili kujua real standing yake.
  JK alishasema ooohh nitapunguza umasikini, ooohh nitaongeza kazi, oohh haki sawa kwa wote or blah blah. Lakini kama waandishi wangepinga political correctness na kumuuliza maswali kama hili ” Jee kwenye cabinent yako utamuweka Lowassa mtu ambae Mwalim Julias K. Nyerere alimnyoshea kidole?”, maswali haya yangutuweka kwenye picha ya kufahamu nini muelekeo wa JK. Sasa tumeshaishia kwenye chicken egg situation, and JK is no where to be found while majority of Tanzania are stucking in the middle.

  Hawa watoto wanataka kuarchive dream za baba zao, hakuna time hata moja kuuliza simple question. Swali ni moja, jee will you protaste against Rostam? Do you believe Rostam cripple Tanzanian fortune?
  What is your standing concern Mkapa? Do you think he is axis of evil? If He move left right then he is part of blood sucker, he just came with different skin.

 18. mbk Says:

  Alipoanzia bwana mdogo si pabaya. Anaonesha anaweza kusimamia kile anachoamini kwa uwazi. Hiyo ni sawa.

  Tatizo langu ni kwamba kwa hali ilivyo (kwa miongo mingi karibu miwili sasa) kila anyetaka tumpe nafasi ya kuongoza anakuja na maneno mazuri sana. Kuna waliotuahidi maisha bora lakini walipoulizwa kwanini hatuna maisha bora walijibu hata wao hawajui kwa nini.(sasa kama hujui umefikaje hapo ulipo, utawezaje kutoka!!!!!!!!)

  Naomba atuhakikishie ni kwa vipi yeye si kama wale tuliowaamini mwanzo? Na amejipanga vipi kupambana na ubinafsi + mmomonyoko wa uzalendo= ufisadi. (Akumbuke manahodha wakuu watatu imewashinda-confirmed!!)

  Ni hayo tu.

 19. Mama wa Kichagga Says:

  Hata swali moja na angalau ku-appreciate maoni hakuna.

  Hivyo natoa hitimisho kwa kumuunga mjumbe hapo juu kuwa jamaa analengo la “ku-archieve” sera za mzazi bila kuwa na mwelekeo. Simply mi naona bado hayuko tayari kuongoza hiki kizazi cha nyoka!

 20. ikram Says:

  NAPE HOJA ZAKO NI NZITO NA NAKUBALIANA KWAMBA JUMIYA YETU SASA HAINA TOFAUTI NA CCM YENYEWE, IMEZONGWA NA WALAFI NA WEZI WA KILA AINA, MASHAKA YANGU KWAMBA HAWA JAMAA HAWATAKUFANYIA MIZENGWE MANA KILA DALILI ZINAONYESHA JK YUKO NA MAFISADI WENZAKE NA KUMTENGANISHA FISI NA MFUPA NI SAWA NA KUSEMA BINADAMU ANAWEZA KUISHI BILA YA KUPUMUA, JK NA MAFISADI NI KITU KIMOJA NA KWA HILI HATA UFANYE NINI HAWEZI KUTENDA HAKI, WOTE WANAOSEMA HUKUTUMIA PLATFORM HUSIKA WANAJIDANGANYA NA HAWAIJUI CCM, MANA HATA UNGEKWENDA NDANI YA VIKAO VYA CCM BASI UNGEAMBIWA AJENDA HIYO ISUBIRI MUA WAKE, NA USHAHDI ULIOTOA KWAMBA ULIKATAA WEWE NA WENZAKO KWENYE VIKAO VYA JUMIYA NA MLIMTAKA NCHIMBI NA TIMU YAKE WALETE KWENU ILA WALIAMUA KUTUMIA NJIA YA MKATO, KWA MANA HAKUNA KIKAO WALA NINI, NI MAAMUZI YAKE NA SHOGA ZAKE, HHI NI KWA SABABU TOKEA BARAZA KUU LA MWAKA 2007 MWANZONI HAKUNA KIKAO CHA KAMATI YA UTEKELEZAJI, BARAZA KUU WALA SECRETARIET ILIYOKAA KULIONGELEA HILI WALA JENGINE LA JUMUIYA, HAPO INA MANA JUMUIYA NI NCHIMBI NA SHOGA ZAKE TU NDIO WAAMUZI NA HAKUNA JUMUIYA KWA MAANA HIYO, HIVYO JIANDAE KWA MAWIMBI MAKUBWA HAWA JAMAA UMEWAKAMATA PABAYA NA UFISADI NDIYO STYLE YA WANA MTANDAO, KILA MTU KAPEWA ENEO LA KUJIFARAGUA ILI IWE NDIYO FADHILA ZA JK KWAKE, HATUTARAJII MEPESI ZAIDI NI KUKUTAFUTIA MAOVU, ILA SISI VIJANA WENZAKO TUKO NA WEWE NA TUTASHINDA VITA YA MAFISADI, HIYO BODY YA WADHAMINI TUMEITEUA SISI NA HAINA MAMLAKA YA KUPITISHA MAAMUZI AMBAYO HATUJAKUBALIANA NAYO NA WALA YENYEWE HAINA MAMALAKA YA KUPELEKA LOLOTE MBELE YA KAMATI KUU YA CCM BILA YA SISI KUKUBALIANA NAYO NA SISI NDIYO WAPELEKAJI SIYO BODY. SASA TUJIANDAE KUWAWEKA SAWA ANGALAU WAELEWE NINI KANUNI NA MAMALAKA YAKE NA MIPAKA YAKE NA WAELEWE NANI KAMTEUA NANI KWA MADHUMUNI GANI.
  KAZA BUTI HAPO HAKUNA HOJA YA FORUM ULIYOTUMIA, CCM NI WABABE HAWANAKANUNI WALA VIKAO, YALE WANAYOYATAKA WAO WATAYAFANYA BILA YA LOLOTE NA HAKUNA WA KUWAULIZA NA YALE WASIYOYATAKA HATA UKITUMIA NJIA GANI BADO UTAKUWA MKOSA TU, NA WEWE MBELE YA JK NA WENZAKE HUTAPATA JEMA LOLOTE, SIO WEWE TU HATA WENGINE WA AINA YAKO AMBAO HAMKUKUBALI KUWA SEHEMU YA UCHAFU WAO WA KUWAPELEKA IKULU, MANA NJIA ZAO ZAKWENDA IKULU ZILIKUWA ZA KURUKA.
  TUKO NAWE NA NCHIMBI ATAONDOKA KWA AIBU KUBWA SANA HAJAWAHI KUIPATA MAISHANI MWAKE NA SIASA ATAIONA CHUNGU KWAAIBU YEYE NA WOTE WANAOMZUNGUKA AKIWEMO MKUU WA MAFISADI MWENYEWE MR JACK.

 21. Amina Says:

  we mtoto angalia mdomo wako huo angalia sana….halafu wwe wa kutoka finland ni lazima ujitambulishe?makubwa


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s