BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NADINA/SHUKRANI KWA KUUNGANA NASI July, 17, 2008

Filed under: Burudani,Maisha,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 8:41 PM

Imekuwa ni wiki yenye mambo mchanganyiko.Wiki ilianza kwa mrembo mpya wa Miss Universe kupatikana.Kwa bahati mbaya hakuwa yule ambaye wengi wetu tungependa kuona anashinda.Taji likaenda nchini Venezuela.Hamna tabu,tutajaribu tena mwakani.

Kisha baada ya hapo likaja suala ambalo sisi hapa BC tumeona ni suala ambalo linahitaji kutokupuuziwa wala kupumzishwa kwa sababu zozote zile.Ni suala la mauaji ya albinos. Shukrani kwenu nyote mlioguswa pia na habari hizo na pia kuwa tayari kuungana nasi katika kuzidi kukemea na kujaribu kutokomeza kabisa imani hizo potofu na pia mauaji ya albinos kwa ujumla.Cha muhimu ni kuzidi kuelimishana na kuwapeleka katika mkono wa sheria wote wanaobainika kuhusika na ukatili huo.Kwa pamoja tunaweza.

Baada ya hapo likaja suala la Mtikila na mwenzake Rostam.Leo hii kila mmoja wetu anajua amuamini nani na amuache nani au la basi wote wanaingia kwenye lile kundi la politricians na wala sio politicians.Ili mradi tu imekuwa ni wiki nyingine yenye mauzamauza ya siasa.

Kama kawaida yetu,Ijumaa ni siku ya burudani na kupumzisha vichwa kidogo.Leo tumeona tuhame kidogo nchini kwetu na kuelekea Zaire(siku hizi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo).Pale tunamkuta Mbilia Bel ambaye ni miongoni mwa wanamuziki waliowahi kutamba sana barani Afrika.Kibao kinaitwa Nadina.Tunatumaini kitakukumbusha “enzi zako” au kama wewe sio wa “hapo zamani” basi pia kitakuburudisha.Tunakutakia Weekend Njema.

Advertisements
 

13 Responses to “NADINA/SHUKRANI KWA KUUNGANA NASI”

 1. hash Says:

  unajua mmenikumbusha marehem kaka yangu. Charles MAZENGO. Na machozi yananitoka. Asanteni. you made my day. its like i saw his face. du. alikua anapenda sana mziki.

 2. Naungana nanyi wana wa BC week ilikuwa taflani na hali itakuwa hivyo maana walisahau ile mrthal ukitaka kula na kipofu usimshike mkono .Mtikila na anaedai rafiki yake wamemshika mkono kipofu na kubaini kila kilicho nyuma ya pazia,
  Mwimbo unanikumbisha mbali sana bongo nyumbani kwetu
  wacha week end iende kwa amani
  wadau wote nawatakia week end njema tulio koeana tusameheane
  chai goda

 3. Matty Says:

  Asante BC na wewe pia!hakika BC Mungu awalinde mimi si wa umri uleeeeeeee wa kina mzee nanihii ila najikuta napenda radha zote i mean zilipendwa na za sasa ila zilipendwa ndo kwa sana!!Samahani sana BC nasafiri kidogo ila nitapamiss hapa na ninaomba niongee na wadau kidogo nadhani bado nitakuwa ndani ya topic tu!(usinibanie plzzz)
  Chris nitakukamatia kiwanja gani wknd hii??
  E.Ndaki sijui kama Dan kaandaa ile kitu leo!!
  Gervas vipi kwa upande wako kakangu?
  Any na wewe je wifi yangu mtarajiwa kama ndoana ikijibu inakuwaje mambo ya wknd?
  Mama wa kichaga vp wknd hii dadangu utatoka?
  Kekuu najua unapopatikanaga wknd!
  Amina hongera kwa ……..!!!nisijesutwa hapa BC
  Binti Mzuri inakuwaje upande wako shosti??? endelea kuwa mrembo kama mimi teh teh tehtetetetete!
  Sally mambo?
  Lily unaonaje warembo wa mwaka huu nani atashinda unadhani?
  Ma’reen upo?
  Hombiz ni aje mtu wangu?
  Nationella (sorry sina kumbukumbu na jina lako fresh) endelea kutuhabarisha kaka!
  Linda kanisa gani utasalia jumapili hii?
  Babli mbona kimya sana kaka?
  Mswahilina inakuwaje unawaacha watu waharibu lugha yetu ya taifa?
  Debora Kizuguto nakusalimu ktk jina la bwana!
  Jbigy hi!

  Jamani ni wengi sana wana BC nimeshindwa kuwamaliza wote ila TUPO PAMOJA INSHAALAA TUKIJALIWA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 4. Wikiendi njema wadau wa BC!
  Kibao hiki kinanikumbusha mbali kweli!
  Kinanikumbusha mpaka maswala ya kuumwa njaa kabla ugali haujaiva katika kipindi cha MCHANA mwema:-)

 5. Frateline Says:

  Hi guys, kutoka Helsinki-Finland

  Kwanza niwapongeze BC kwa kazi ya wiki hii, ninatamani kuwaita kuwa BC imekuwa ni blog ya jamii namba mbili baada ya michuzi, kwanza unakwenda na wakati, halafu mada zote za wiki hii zilikuwa ni nzuri na zenye kugusa hisia za jamii, nawapongeza, Naomba kuwauliza BC nyie ni nani kwa majina na sura? naomba hata kama hamtaki kuwa public nitumie jibu hili kwenye email yangu, kuhusu music wa ijumaa hii ni mzuri, old is gold, yakale ni dhahabu asante nimemkumbuka marehemu baba yangu mzazi alikuwa anapenda music na kuna function moja huo wimbo ulipigwa ilikuwa ni arusi ya kaka zangu wa baba mkubwa walifunga ndoa siku moja yaani mtu na kaka yake, na kwa bahati mbaya mapenzi ya mungu wote wameisha kufa, mmoja kwa ajali ya gari na mwingine kwa ugonjwa mbaya wa dunia hii ya leo, hivyo nikisikiliza ninakumbuka picha nzima mwaka 1992- it is sad and I feel really depressed & very bad because it pains me, but this is the secret behind the power of music, Mbia Abeli, ninawashukuru BC kwa kugusa hisia zangu na kuharibu Ijumaa yangu,

 6. Gervas Says:

  Matty, kumbe weye mduchu!! hiki kibao nilikuwa ndo nakisikiliza miaka ya 1987 nikiwa mduchu! tulikuwa na Bar nyumbani na mimi nilikuwa J’mosi ndo nakuwa DJ kuwaburudisha walevi. ha-ha-ha, Basi Matty, km kawaida nitakuwa kijiweni kwetu tukiburudika na the Ulanzi, mbege…..we acha tu, maana bia kila bajeti ikisomwa bungeni wamepandisha bei. sasa inabidi tunywe the natural lager.

 7. binti-mzuri Says:

  matty bwana we unataka kusutwa..lol..nalitolela leo kawa nationella..nimechekaa aisee.. ila iyo pointi yako,kwakweli mi nakujibuje…”sie ni visura na tunajitambua!”…. mwenye lake,ameze fansida.lol.ukisubiri kusifiwa bongo,utajikuta unakufa ivi ivi.

  huyo wa finland kasema kweli..apart from michuzi + bc yani sijaona kabisa.. this 2 are the best of bestest..kuna wengine nao wanajitaidi saaana..ila mi hawa ndio wamenirogaa sijui

 8. Pearl Says:

  sasa we matty unaenda pangoni!!!???? inamaana hakuna mtandao huko uendako!!!!??? bado tunahitaji sana mawazo yako hapa,fanya ufanyalo uwe mtandaoni.
  bon voyage.

 9. Edwin Ndaki Says:

  Matty mambo vipi m2 wangu.

  Yaani wiki endi hii nilikuwa misele mingi ila haina tabu natumaini tutaonana tu kwa Dan

  siku njema BC na wote

 10. ndio nimeziona hizi meseji sasa ikabidi nicheke hehe. I guess my new nickname is Nationella then. Anyways, thanx kwa 5 Matty, yeap tupo wote tunaendelea kupeana habari. And thanx binti-mzuri kwa kurekebisha jina, itabidi nikuletee zawadi toka Masasi!! Hope you all had a fun weekend (I know I did) na mmesharudi katika shughuli za maendeleo.

  PS: Nakubaliana na mliotangulia kwa kuwapa BC 5. They are doing a super good job. Mi nilichelewa kidogo to find out about BC and get on the band wagon, until I got an inside scoop from the bongocelebrity staff about the good stuff in here!!!

 11. Matty Says:

  Wapendwa ktk bwana thanks God am back!!!
  Jamani niliwamiss wote sana tu.

  Gervas na wewe duuuuuu kumbe kama DJ B. desh desh kazi unaiweza ok hongera.
  Binti mzuri, unajua mimi bado nina lafudhi ya kule kaitaba sasa jina la nanihii nilishindwa kabisa kulitaja….na hapo ndo napoamini sisi ni visura tunaojitambua!!hahahahahahahahahahahaaaha.
  Pearl asante sana, unajua nilipokuwa kuna kila aina ya access uijuayo ila muda ndo tatizo ndugu yangu.

  Pole sana Frateline kwa kuguswa na hicho kibao…RIP to your BROTHERS.

  Jamani BC OYEEEEEEEEEEEE!!

 12. Matty Says:

  E.Ndaki safi sana kaka nimekamu baki naendeleza libeneke!

 13. Matty Says:

  Nalitolela, tuko pamoja sasa jina lako nishalikamata frsh!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s