BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 24 July, 20, 2008

Filed under: Burudani,Photography/Picha,Utamaduni,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:37 AM

Kwa miaka nenda rudi,watu waishio katika miji ya pwani wamekuwa na jadi ya kutumia vyombo mbalimbali vya usafiri wa majini.Vyombo kama mitumbwi,ngalawa,ma-jahazi nk ndio vimekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha shughuli za usafiri kwa watu waishio pwani na zaidi zaidi katika shughuli za uvuvi ambazo kwa wengi ndio chanzo chao kikuu cha mapato.

Lakini hivi karibuni vyombo hivyo vya usafiri vimeanza pia kuingia katika uwanja mpana wa burudani au michezo.Pameanzishwa vitu kama mashindano ya kukimbiza Ngalawa kama inavyoonekana pichani.Hapo ilikuwa ni huko Zanzibar hivi karibuni ambapo Issa Michuzi alishuhudia mbio za ngalawa(Canoe Race?).Hapo ngalawa na waendeshaji wake zilikuwa zinawekwa sawa tayari kwa shindano hilo ambalo lilishirikisha jumla ya ngalawa kumi na tisa(19)

Je unajua tofauti iliyopo kati ya Ngalawa,Mtumbwi na Jahazi?Tuelimishe.Hii ndio picha ya wiki.

Advertisements
 

3 Responses to “PICHA YA WIKI # 24”

 1. hombiz Says:

  i wish i knew!

 2. Dunda Galden Says:

  Ahsante BC
  ……Ngalawa ni ile yenye kama mabawa mawili pembeni yaani upande wa kushoto na kulia pia utumia kitambaa maalum chenye almaruff tanga iki chomba kinaweza kubeba si chini ya watu 15 zaidi ya hapo bahari hatari

  ……..Mtumbwi ni ule usio na mabawa wala mala nyingi sisi tuliopembezoni mwa bahari utumia kasia (lakini baadhi ya watu sasa utumia kaji tanga na ufunga mashine sayansi na teknolojia that why i like home)kinaweza kubeba si chini ya watu watatu tuu zaidi ya hapo Lawama Hiki chomba hakitegemei sana upepo

  …….Jahazi mwana wani ni chombo kikubwa chenye uwezo wa kubeba mizigo pia kusafilisha abilia kulingana na ukubwa wa chombo hili utumia tanga yanaweza yakawa mengi lakini ya kuwe kwetu utumia tanga moja lenye ukubwa kuliko la ngalawa,hii mala nyingi huwa kuna nahoza na mabaharia
  mwendo wa jahazi utegemea upepo kasia nk

  Huo ndio ufahamu wangu kwa hisani ya marehem babu inshallah mwenyezi amlaze mahali pema pepono Amin

 3. WARDA Says:

  HII PICHA INANIKUMBUSHA KWE2 BAGAMOYO KILA JIONI MWENYEWE NAENDA KUTEMBEA BEACH KUSHUSHA BIRIAN LA MCHANA ,,,,,,,,,,CHAIGODA


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s