BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UZURI,UREMBO,MVUTO: NINI MAANA YAKE? July, 20, 2008

Filed under: Editorial,Majarida/Magazeti,Mambo Mseto,Mawazo/Tafakuri,Swali kwa Jamii — bongocelebrity @ 2:12 PM

Binti aliye pichani hapo juu anaitwa Megan Fox.Kwa mapana na marefu sio bongo celebrity.Yawezekana kabisa kwamba hata Bongo hajawahi kuisikia!

Kwanini basi tumemuweka hapa leo? Sababu ni kwamba binti huyu ndiye ambaye kwa mwaka huu wa 2008, jarida maarufu la FMH, lilimtaja kama mwanamke nambari wani mwenye mvuto zaidi miongoni mwa wanawake 100 iliyowaorodhesha kama wanawake wenye mvuto zaidi duniani.

Kwa bahati nzuri au mbaya,vyombo vya habari kama hivi vikishirikiana na vitu kama filamu,muziki nk ndivyo ambavyo hivi leo vina ushawishi mkubwa kuhusiana na suala zima la uzuri,urembo au mvuto.Vikisema fulani ndio mwenye mvuto zaidi basi mabilioni ya watu wanaamini hivyo.Matokeo yake ndio watu wengi(hususani wanawake) huanza safari ndefu ya kujinyima chakula ili wapunguze saizi za miili yao na kufanana na huyo aonekanaye “mzuri” kwa mujibu wa jarida fulani.Wengine hufanya kila wawezalo ili wawe na nywele,rangi ya mwili,kucha nk kama za huyo aonekanaye “mzuri” nk.Kwa bahati mbaya hata mengi ya majarida yaliyopo au yanayoanzishwa nchini Tanzania,yanafuata mkondo huo huo wa “kutafsiri” urembo,uzuri na mvuto.

Je urembo,uzuri,mvuto ni vitu gani?Ni kweli kwamba uzuri au urembo uko katika mboni ya jicho la mtazamaji au kutoka katika akili na macho ya mhariri wa jarida?Nini kifanyike ili kumfanya kila mtu aridhike na jinsi alivyo ili kupunguza mahangaiko,watu kupoteza maisha wakati wa zoezi la kujikondesha nk?

Advertisements
 

38 Responses to “UZURI,UREMBO,MVUTO: NINI MAANA YAKE?”

 1. hombiz Says:

  kula chakula bora na fanya mazoezi

 2. binti-mzuri Says:

  Clearly they’ve not seen my photo au ya mdogoangu matty..au nusu ya ulimwengu huu.ilo title lina utata,labda waseme ‘celebrity cutie of the year’ ila wakisema mst beautiful woman,wamechemsha.hawana proof,hata ivo beauty is in the eye of the beholda,n hamna rule iliyoandikwa kuashiria huyu ndio mzuri. Ila m2 tabia

 3. hombiz Says:

  kwa nje mzuri, ndani je?

 4. any Says:

  Uzuri is defined differently by different people of different locales! Wakati huko mamtoni wanaona kuwa skinny ndio uzuri, wachaga wanapenda sura ya mduara na awe mweupe pepeeee ndio mzuri apo bila kujali kama binti ana usafiri au mgogoro! kwa wachaga usafiri wa binti sio issue, akishakuwa cheupe dawa, hata kama meno ya chocolati hatujali! kwa kina Matty uzuri ni ule mshepu wa kihaya na lazima apo nyuma donati ziwe zimejaazia haswa! ukienda Kusini huko Mbeya nimesikia mwanamke mzuri lazima awe na tundevu tuwili twa kishkaji. hii nimeisikia tu mahali sina uhakika, ngoja waje wenyewe watuambie.
  Na walevi wanadefine uzuri pia kivyao! kabla hawajalewa wanadefine tofauti, na wakishalewa hata Bar maids wanageukaga kuwa ma Miss kwa wakati huo na wanaweza wakaondoka nao hadi kesho yake fahamu zikirudi wanaishia kuzimia kila wakiona kitu walichokileta chumbani! haaaaaa. ngoja nikamalizie mbege yangu mie.
  Kekue whatsup……, kutiri shonga maaa?

 5. Dunda Galden Says:

  Ahahha swali je kwanini achauliwe kuwa yeye mzuri?watu camela magazeti na Tv zimemuona kwa vigezo vingi sana kuwa kweli huyo ndio mzuri kwa mapana na marefu sio bongo celebrity ……mimi nilisha wahi kuona SBS TV , The Age pia na Foxtel siku zilizo pita mwanamke bomba ulimwenguni na aliewahi kusababisha ajali ya magari kugongana kwa jinsi alivyo mzuri
  Alie toa habari zake alikuwa ni hao hao FMH hapo jamani tusiwe wabishi DUNIANI KUNA MAMBO
  Chafosa

 6. eva moses Says:

  yep beauty is always in the eye of the beholder….so we are all beautiful…Yaaaayyyyyy!

 7. Gervas Says:

  Definition ya urembo, uzuri nk, inategemeana na jamii husika. Mfano Megan fox, ukimpeleka ktk jamii yangu ya kanda ya ziwa, ni bule kabisa wala si mrembo. urembo kwa asili ya Kiafrika lazima binti awe amejaliwa, yaani maashaallah!! Mashindano km ya miss wo wo wo yangefaa sana kumtafuta mrembo wa kitaifa. kina Lundenga naona wanachemsha tu ndo maana hatufiki mbali. Afu Any….na Binti mzuri you real made my day!!

 8. Pearl Says:

  Hivi karbuni kama mnakumbuka BC alishaweka picha ya VICTORIA MARTIN miss redds ambasador na wengi wao wali-comment kuwa “KADADA KAZURI HAKA”.Hivi tujiulize swali tulitumia vigezo gani tukasema ni mzuri maana wengine walisema ni mzuri kama mdoli kwahiyo inamaana mdoli ndo alitumika kama benchmark ya uzuri.

  Keisha alitolewa hivi karibuni watu wakasema si utani dada ni mzuri lakini referal point ilikuwa ni “MAHIPSI”,kwavile anamahipsi basi tayari ni mzuri,kwahiyo na hapa HISPI lilitumika kuuelezea uzuri.
  Swali linakuja kua sasa uzuri wa mtu tunaangalia nini hasa!!!???

  mi naona sisi hapa duniani tunahangaika tu na miili yetu isiyokuwa na shukrani,hata upake pafyumu nzuri mwisho ni masaa kumi na mbili zaidi ya hapo ni kikwapa kwa kwenda mbele hata kama watu wanakuona mzuri lakini tumebeba miili ya uharibifu.
  utaonekana unatembea vizuri lakini tumboni umebeba vitu va kupeleka chooni tena vinanuka.

 9. Saidi Sittu Says:

  Maana yake power to attract

 10. Ghalib Says:

  Uzuri huwa wa asili bila kupaka make up ya aina yeyoteUrembo ni wa kutengeneza kwa make-up,mvuto vile vile huwa wa asili Unaweza kuwa mrembo lakini usiwe mzuri,lakini unaweza kuwa mzuri na mrembo -kwa maana huyu hata kama ametoka kulala sasa hivi ukimuangalia bado anavutia siyo wengine mpaka wapake vipodozi ndio waonekane wazuri hawa ndio tunaowaita warembo-ni kitu cha muda unakuwa mrembo kwa masaa fulani lakini mzuri ni daima.Ukitaka kuwaona wasichana wazuri nenda vijijini-ndio maana wale face of africa huwa wanaenda vijijini huko utakuta watu wana ngozi ya sili haijaharibiwa kwa vipodozi.

  Thanks
  Ghalib

 11. kekue Says:

  Kaazi kweli kweli, lkn ni ngumu sn kumfanya mtu aridhike the way alivyo cha muhimu ni kushauri tu km mtu anataka kuwa namna fulani atumie njia hii coz ni safe au namna gani, lkn sio watu waridhike walivyo nani atakubali, hapa jitihada za ziada lazima zifanyike mtu achange….. Any shonga kunu nshabu kya karibu…….

 12. thanks for bringing this up BC. The portrayal of what it means to be beautiful/attractive in the western media and popular culture has caused many a problem for young girls, ranging from eating disorders to bullying and name-calling in high schools of people who are perceived to not be beautiful. Such is the depth of the problem that the modeling industry have recently resorted to barning size-0 models, who up until then were considered to be the epitomized the shape of an ideal runway lass.

  Unfortunately, this trend has been creeping up into African culture, and it has started to get to the heads of our young, urbane, female population; and I fear adverse effects in the not-too-distant future if the society does not address this problem soon. Let us take proactive action against this before our young girls start suffering from anorexia nervosa. Let us embrace what it traditionally means to be beautiful in Africa.
  It’s good to maintain a healthy diet and lifestyle, but try to stay within the recommended Body-Mass-Index range for your height.

  By the way, if you walk down the street in say, Canada, the average Canadian is not all thin and slim. In fact, obesity is a bigger problem in the west (particularly N. America and GB) than even anorexia and bulimia. What you see on TV is just a fabrication of the entertainment industry.

 13. any Says:

  Well said Nalitolela! cant agree more.

 14. thanx for the props any!!

 15. furaha Says:

  watu tunashindwa kutofautisha urembo, mvuto na uzuri
  mm kwa upande wangu ninavyojua ni kwamba: mtu anaweza kuwa mrembo na sio mzuri ni ile make up anayofanya,mzuri ni yule hata asiponawa uso anaonekana mzuri bila kuji make up,
  mvuto ni ule muonekano wa mtu labda ana hips,mguu bambataa nk.na yote hayo yanatokana na kila mtu na mtazamo wake, na hakuna mtu aliyekamilika kwa vyote kila mtu ana mapungufu yake

 16. Matty Says:

  Uzuri – mvuto ni vitu vinavyoendana mfano nikisema huyu binti ni mzuri kimtazamo wa nje nadhani kuna kitu kinavutia (mvuto) na ni kizuri kwake yaani kajaaliwa eg.macho,miguu,wowowo, hips, colour,umbo n.k

  Urembo- hapo ndo tunapoingiza mambo ya kujiremba eg.kupaka make up, kusuka,kunyoa n.k

  Sasa mimi nikimuangalia huyo shosti hapo juu sijaona kama anavutia hata ila sasa ndo pale tunaposema beauty is in the eye of the beholder…..na may be wenzetu wanapenda uwembamba zaidi kuliko kibongelaizesheni.

  Nikirudi kibongobongo nadhani kina kaka ndo mnajuaga msichana mzuri ni yupi na kila mmoja anamtizamo wake ktk hilo….ila waliowengi wanapenda kumsifu msichana aliye na shepu ya kibantu a.ka Joyce wowowo na miguu chupa ya bia!!!!

  Any hilo halina ubishi kabisa Kaitaba kuna wasichana wazuri mno mimi nikiwa mmojawapo nadhani umenipata!!
  Binti mzuri bila shaka na wewe ni mzuri kweli kama sie kina kaitaba!! ila sina hakika maana kule tanga wengi ni wazuri wa sura si umbo tetetetetetetetetete!!

  Kitu kingine nadhani hata makabila yanatofautiana ktk mtazamo wa uzuri-urembo-mvuto….mfano ni wasukuma kule mwanawane ukiwa msichana mweupe ndo unaolewa kwa ng’ombe mia sasa hapo ndo naposema kila kabila linamtizamo wake kinadharia.

 17. Matty Says:

  Kitu muhimu nilichotaka kusahau pia uzuri wa sura,umbo,lips,hips,makalio,chakula cha mtoto n.k si kitu …UZURI WA MSICHANA TABIA TU!

 18. hombiz Says:

  Matty sikubaliani na wewe kabisa ktk hilo. Ina maana gani kuwa ni uzuri wa Tabia wakati sura kama kifaru (reception nill), ziwa mtindi, usafiri mgogoro (tooth picks), makalio (pasi a.k.a Super flat?
  I don`t care how good hearted that ugly woman might be, i`m not gonna go for her! That is a buuuuull crap!
  I`m sorry for this comment, but that is just me!

 19. binti-mzuri Says:

  ai we matty dongo hilo shosti, ha ha ha… muulize chafosa chai goda wa huko bagamoyo.. pwani balaa!!! .. from head to toe,watoto wa tanga tunatisha. kaitaba nyie rangi nalo ndo tatizo,black is beauty ila …. no comment.

  we hombiz..unaeza kuwa na demu bomba kama beyonce,ila tabia… any way ngoja niachie hapo,ila like i said before,mtu tabia bwana!…afu mbona umejicontradict na posti yako ya namba 3..ha ha ha

 20. Dunda Galden Says:

  Ehhheheee umo umo
  lakini usipime hapo
  zaidi mie simo wacha nimemalizie
  likizo yangu kwa amani
  19 Binti -mzuri=CDA mtoto wa nyumbani,Dont make me
  think home brbr ya kumi na nihii zaidi Mzee wa viwango Matty na Hombizy watufahamishe zaidi
  ,,,,,,,lakini wapi mama wa kichaga tunahitaji maoni yako!

 21. ninakubaliana na point #18 ya hombiz kiasi fulani. It’s all easy to say sijui mwanamke (or mwanamume for that matter) mzuri ni tabia. Ila ukweli ni kwamba deep down inside we all have some level of shallowness (or whatever you chose to call it) inside, in a sense that kabla hujaanza kuchunguza tabia ya huyo binti/kijana ili ujue kama atakufaa, lazima uvutiwa naye kwa nje kwanza.
  Kitu gani kitakuvutia? Kama walivyotangulia wengine kusema, hiyo inategemeana na mtazamo (perception) ya unapotokea but even more importantly, inategemeana na mapendeleo yako binafsi.

  Yes tabia ya mtu is the MOST important thing. Kama alivyosema binti-mzuri (19); urembo huku tabia 0 haina maana, utaishia kulia tu, ila kwa wengi wetu (whether you admit it or not); hasa siku hizi ambapo tumejenga utamaduni wa ku-date kwanza (kuwa bf na gf) kabla ya kumtambulisha mchumba kwenu, basi lazima uvutiwe na mambo ya nje kwanza. Ukishavutiwa ndio utatafuta mahusiano ili umfahamu vizuri zaidi.

 22. hombiz Says:

  Binti mzuri mimi siji-contradict hata kidogo. Comment yangu namba tatu inahoji kuwa, Megan Fox kwa mtazamo wangu mimi naona ni mzuri wa umbo na sura. Lakini tabia yake ikoje? Kwasababu anaweza kuwa mzuri kiasi hicho halafu tabia yake ikawa ni nightmare kwa wandani wake…….! But at the same time, demu mwenye uzuri wa tabia wakati sura na umbo kimeo, hiyo inakuwa ni sooooo! Hailipi hata kidogo. Napenda mambo yake ya balance hata kama sio 100 kwa 100.
  Najua sisi binaadamu tuna mapungufu yetu na hakuna aliye 100% perfect lakini still mimi demu “HUNDE!” hiyo nasema ni HELL TO THE NO!. Na kama unasema naweza kuwa na demu bomba kama Beyonce lakini tabia….. Basi na mimi itabidi niseme BADO NIPO NIPO KWANZA!…napenda memu mzuri anayejiheshimu sio wa mkwanja na gari! I don`t believe in cheating. Can`t deal with a hooker, can`t deal with an ugly girl neither!

 23. Mtanzania Says:

  Kwa kawaida huwa sipendi kuchangia katika blog kwa sababu zangu binafsi. Lakini katika pita pita zangu humu BC nimejikuta nalazimishwa kuandika hasa kumuunga mkono mchangiaji namba 8, katika paragraph ya mwisho kabisa.
  Ni kweli kwamba hapa Duniani tunaangaika na miili yetu kwa vitu na sababu ambazo amezielezea.
  Ninachotaka kusisitiza ni kuwa mambo ya mwilini si ya muhimu, muhimu ni rohoni, yaani mahusiano yetu sisi na MUNGU wetu.
  MBARIKIWE.

 24. Matty Says:

  Hombiz, tabia ndo kitu muhimu maana unaweza kuwa na demu bomba kama alivyosema Binti mzuri (Beyonce)lakini tabia ni sufuri na ukampeleka kwa wazazi akakuaibisha sasa hapo nadhani nimeeleweka…japokuwa vijana tulio wengi hatuangalii tabia nadhani!

 25. hombiz Says:

  Matty! To be honest with you! I fail agreeing with you. Kwangu mimi hata mwanamke awe ana roho nzuri kama malaika wakati ni mbovu kwa sura ama maumbile, kwangu hana nafasi kabisa ya kuwa mke wangu. I don’t care watu wengine wanafikilia vipi, mimi kupenda mwanamke mbaya siwezi. Pia ni lazima ieleweke, sio kweli kwamba wanawake wazuri wote wana tabia mbovu. Therefore, nitamuomba MWENYEZI MUNGU anijaalie kupata mke mzuri na anayenifaa. Lakini asiwe na sura wala umbo baya because I can not deal with that! Siwezi kuwa na mwanamke ana roho boooomba kinoma lakini kila nikimtazama moyo wangu haulidhiki naye kabisa kimapenzi. Hiyo itakuwa ni sawa na kuoa jiwe. I`m so sorry about this but I’m going to stick to my point. No beauty no LOVE from me! And that is it! I’m static on this!

 26. Matty Says:

  Ok, Hombizi kakangu muombe Mungu maana mke mwema anatoka kwa bwana!!! endelea kumuomba na ukingojea mke mwema!!

 27. hombiz Says:

  thanks matty! That`s what i`m doing right now. I pray to GOD so that he can bless me with a beautiful,respectiful wife with a decent sense of humor!

 28. any Says:

  Tabia ni moja ya kigezo ila jamani si akuvutie kwanza ndio uanze movement! alafu ukishamfahamu ndio unaangalia hizo tabia? Alafu sio wote wenye sura mbaya wana tabia nzuri, mwingine anabahatika yote, sura mbaya na tabia mbaya vile vile! Sio mtu anachagua kijeba chake apo hakina mvuto basi unakuta mkaka anajiwahi aah huyu msimuone hivi ni mbaya lakini ana tabia nzuri etc.
  Na wakaka niliosoma nao chuoni Butimba, akiwa na demu mbaya anajiwahi huyu msimwone hivi mimi ndio nilimuanza, haaa. eti bikira ndio imemfanya abakie apo apo asiangaze zaidi, was funny eh ila kwangu mie kutuwahi na bikira nilikuwa naita defensive mechanism kujustify kwa nini umechagua kisichoangalika!

 29. hombiz Says:

  Ha-ha-haaa! Any!, umenichekesha na defensive mechanism ku justify kwa nini amechagua kisichoangalika! Ha-ha-ha!. Kama hakiangaliki hakifai kuwa nacho hata chembe!

 30. any Says:

  Lets be sincere on this! mtu utamjuaje ana tabia nzuri kabla hujaongea nae wala kumfahamu vizuri? apo jibu ni apana. Sasa kitakachokuvutia kwanza kwa huyu mtu ni nini ili umfahamu zaidi? Mi nadhani mvuto kwanza then usaili/interview za apa na pale zitafuata! kama hajakuvutia utamu approach vipi? Mi sina uzoefu wa ku approach maana ni mimi ni SHE! na enzi zetu nilivokuwa nakua mwanamke ku approache HE ilikuwa taboo! sasa wanaume njooni apa mtueleze! maana mimi najaribu tu kutumia common sense kuwa uvutiwe kwanza then kama ni KIBUDU au KINACHINJIKA time will tell!

 31. Matty Says:

  swali la kizushi kidogo….Any kwani wewe bado hujajicomit somewhere??hahahhahahahahahaa usijenirushia makombora!

 32. any Says:

  Aseee mi tayari mwanawane, nimejicommit 11yrs ago, plus minne ya kunikopa nikiwa chuoni! so niko nae like 15 yrs ago! niamkie Matty! sawa?

 33. truthfulness Says:

  Any umri utakua umekwenda kidogo

 34. any Says:

  truthfulness, kuhusu umri kwenda ni yes and no! kwani nani aliweka umri, its just in ur mind, unaweza kuwa na umri mkubwa lakini mwili na mind yako vinakuwa havijadepreciate kihivyo! na kuna wadogo wa umri ila wamekwenda mileage nyingi kimaisha na kifkra. Ukigoma kuzeeka utabakia kijana tu.

 35. Matty Says:

  hahahahahahahaha shikamoo dada Any…nilikuwa sijapita hapa tena, duuu safi sana sasa usikose kunialika anivesary ya 20yrs if God wishes nakuombea!

 36. any Says:

  Niombee mwaya Matty, mweee, maana navoukataa uzee kwa nguvu zangu zote, acha tu! yaani sikubaligi, uzee ni namba mi akuu niko busy na vipedo utanipenda nakwambia, hahaha, mama wa 40yrs ndani ya kipedo. hahaha.

 37. any Says:

  na wewe Matty tayari au bado upo upo tu! kama upo upo tu basi tuwasiliane, maana mi nitamwambia kakangu kama uko serious., sawa!

 38. JOHA Says:

  Uzuri,urembo na mvuto ni adimu sana kuwanavyo vyote kwa pamoja na hasa katika zama hizi zetu tofauti na zamani.Mtu anaweza kuwa mrembo lakini si mzuri halikadhalika akawa ana mvuto lakini mbaya.Pia akawa mzuri lakini si mrembo.
  UZURI unaendana na tabia kwamba mtu mzuri anaweza akapendwa nakila mtu kwasababu ya tabia yake kuwa nzuri.Mzuri anajitunza,anajiheshimu pia anajipenda.
  UREMBO unaendana na kujipodoa.Ili mtu aonekane mrembo sharti ajipodoe na make-up ili apate kuonekana mbele za watu.
  MVUTO unaendana na maungo ya mtu.Kuna wenye mawowowo makubwa,wenye mahipsi,wengine macho mazuri ya kuita,pia usafiri wa kuridhisha.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s