BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MONALISA July, 21, 2008

Filed under: Filamu/Movie — bongocelebrity @ 9:41 PM

Jina lake halisi ni Yvonne Cherry.Ila ukitaka watu watambue haraka kwamba unamuongelea nani basi huna budi kumuita “Monalisa” kwani ndio jina ambalo wengi wamelizoea kutokana na fani yake ya uigizaji filamu kitu ambacho binti huyu amebobea.Monalisa aliwahi kuwa mke wa prodyuza maarufu wa filamu aitwaye George Otieno almaarufu kama Tyson kabla mambo hayajakwenda ndivyo visivyo.

Advertisements
 

46 Responses to “MONALISA”

 1. Gervas Says:

  kako-nachuralle byutifu.

 2. Matty Says:

  Msichana mzuri huyu, hapa sasa ndo mimi naona niseme uzuri wake nauona macho yake, rangi ya ngozi na uso wake ulivyo mrefu…Gervas umenipata?? sura ya kitusi kimtindo ili kuongeza uzuri wa msichana.
  Anajua kuigiza fresh sana kwa kweli.
  halafu kuna udaku nilisikia eti yy na Thea ni ndugu wa baba mmoja kweli si kweli???? anayejua pls!

 3. any Says:

  Ehe, baada ya apo ikawaje? hadithi itaendelea wiki ijayo. LOL!

 4. Lina Says:

  Ama kweli ivumayo haidumu. Nilitegemea Superstar kama wewe ungeonesha mfano mzuri kwa jamii kudumisha ndoa yenu ikawa mfano mzuri wa kuigwa. Sasa mara mmeshaachana jamani mhhh!! Mbwembwe zoooote zile za kuchuana kwa Harusi na Marehemu AC ndio zimefika tamati? WWWWHYY jamani. kwani wasuluhishi si wapo?

  Mimi inaniuma sana kuona wasanii wanaoana na kuachana yani imekua ndio fasheni ili mradi uonekane uliolewa au ulioa.
  Tatizo la wasanii hakuna anayetaka kujishusha kwa mwenziwe kila mtu anajiona yeye zaidi. Kwa staili hii ndoa hazitadumu kamwe.

  Anyway nakutakia kila la heri jaribu kutafuta chanzo cha kuachana na mumeo, na kama inawezekana msameheane mrudiane mlee mtoto wenu.

 5. Dunda Galden Says:

  Almarufuu bint kujilusha.
  hiyo ndio adha ya kuoa wanjiona masuper star
  lakini si wote Ashakum maiwayfuu!adha na shida
  aswa mfuko ukiwa una kajiupenyo basi penzi limekwisha
  ….si freash tabia ya kuoa au kuolewa na kuachwa au kuwachwa
  sasa wewe utakuwa wa kuolewa kuachwa na kila mtalak ana mtoto je wakifika saba kila mtoto ana baba yake,,,,,,,
  kama kuna gozi gozi timua la msamehane na kuwafikilia watoto
  chai goda

 6. binti-mzuri Says:

  yes yes mama sonia..nambie!

  alianzaga kama mchezo vle,saivi yuko mbalii…

 7. Lizzy Says:

  Jamani tafuteni chanzo wacheni matatizo ya watu sio mnajudge kwa vyombo vya habari eleweni watu wanatafuta kujaza matumbo ya watoto wao kupitia umaarufu wa hawa masuper star nikimaanisha hivi sio Michuzi,Michuzi jr,Haki ngowi,Mjengwa ,Mpoki na Father kidevu na wengine wachache hizo mmoja kati ya blogs mnaweza kuamini wakirusha kitu hewani lakini wengine na magazeti hakuna kitu kabisa waongo sana elewa njaa ni kitu kibaya sana sasa wao ili washibe ni lazima wawadanganye nyie na mimi.sasa nyie hapa Michuzi jr amesema wameachana na wengi wao mmeanza kumtupia lawama huyu binti chanzo chake mnakijua lakini kwahiyo kama jamaa yake alitaka kumchoma kibiriti au kumbaka mlitaka avumilie tu au labda yeye pia ndio mwenye makosa sisi wote hapa we are just naive so tuache mambo ya watu tujaribu kuwa mifano sisi wenyewe tusitegemee wengine ndio wawe mifano

  kazi njema
  miss england

 8. hombiz Says:

  Lina! Mimi napinga kabisa hii dhana ya mtu kuwa maarufu basi awe ni mfano kwa jamii. Watu maarufu nao ni binaadamu kama wengine. Hivyo hawawezi kuwa sasa eti tu kwakuwa ni maarufu. Kukosea ni sehemu ya maisha. We always learn through mistakes! Kuwa mfano kwa jamii ni jukumu la kila mwanajamii na sio celebrities tu!. Everybody needs to play his/her part.
  Wakati huo huo, mimi binafsi nasikitishwa sana kuona ndoa nyingi za siku hizi hazidumu, ukilinganisha na zile za zamani. Hii sio kwa watu maarufu tu, bali jamii yote kwa ujumla. Sasa sijuwi tatizo ni nini!?. Sijuwi wanandoa wanakuwa wamekurupuka na kufunga ndoa kabla hawajafahamiana vya kutosha na kuhakikisha wote wana malengo sawa ktk maisha? Ama wanandoa wanashindwa kuepuka vishawishi vingi vinevyowatokea wakati wa ndoa zao na kupelekea kusalitiana hasa kimapenzi!. Au labda maisha ya sasa na mwendo kasi wake ambapo tamaa za material things zinaongezeka zaidi kulingana na mapinduzi ya sayansi na teknolojia wakati uchumi kumudu tamaa hizo haupo! Au labda pengine, wanandoa kuruhusu watu wa pembeni( ndugu, jamaa, na marafiki) wa aidha mume au mke kuingilia mahusiano yao kwa uchochezi,wivu, na tamaa zao ili wavuruge ndoa halafu baadae wacheke! Maaaaaaaaan! I just don’t know. But all I can say is that, I hate too see most modern marriages last only few years if not months!

 9. any Says:

  Wee Lina ni KE/ME! Stop judging, coz u were not there when they loved each other, got married and end the marriage! you dont know the reason behind this mess kam alivosema mmoja apo juu! DONT JUDGE HER! KIatu hujavaa wewe ivo hujui kimembana kiasi gani hadi akakivua! kwa vile superstar ndio abakie kwenye ndoa ata kama ananyanyasika? na umejuaje yeye ndio alimkataa mume, kama mume ndio alimkataaje? hatukuwepo na hatujui! mhusika kaona yamemshinda akaondoka, so its up to her ndio maisha aliyochagua! Respect her decision na sio kumkandia kwa nini hukuvumilia! kuna mengine hayavumiliki na hata bible/vitabu vingine vitakatifu vinayapinga, mfano kama alikuwa anatakwa kinyume cha maumbile nako avumilie tu in the name of NDOA!! aah umenichosha sijui ata nianzie wapi maana u have a long way to go! kama umeolewa/oa hongera mwenzetu kwa ku keep ndoa and the ring, walioachika pole zao ila wanaweza kuwa in a better situation kuliko wenye ndoa zao! Maana wadada wengi huotaga makunyanzi immediately baada ya ndoa! sasa sijui kunakuwaga na nini, ni siri yao. thats my opinion, msinitoe macho.

 10. kijiwe Says:

  mie nimemtamani na sijui nitampataje,kuna anayeweza nisaidia?

  kijiwe

 11. mpendwa Says:

  wala usijali msichana mzuri watu wanakuonea wivu urefu wako mwanamke mrefu unaonekana sehemu yoyote utakosa mwanaume ulvyp bompa

 12. Pearl Says:

  nakumbuka alifanya mahojiano hapa BC na moja ya swali aliloulizwa ni kuhusu kurudiana na mumewe,alijibu “haitakaa itokee” kwanza tayari ana mtoto mwingine tena nadhani baba wa huyo mtoto ni chotara hivi.
  kwahiyo nadhani huyu dada siri kubwa ya ndoa yake anayo mwenyewe,sidhani kama anaona ni fahari kuachana na mumewe ila imetokea labda hawaizi tena chungu kimoja kwahiyo inabidi watengane.

 13. Pearl Says:

  jamani kabla sijasutwa hayo mahojiano hayakuwa hapa BC nimesahau sikumbuki ni wapi niliyapata,ila hizo ndo nyepesinyepesi.

 14. Matty Says:

  Muachen jamani na personal decision zake…hv niwaulizeni kama nimeolewa na jamaa mlevi kila siku akija ananipiga mateke niendelee kung’ang’ania tuuuuuuuuu for wat???Binti Mzuri unasemaje hapo?

 15. sikiliza nikwambie yvone sisi wajaluo uaga hatuachagi tena tunajua kulea wewe kama umesikia ya watu shauri lako lakini sisi jaluo obama tupo highclass sanaaa, tunajua kulea sijawai kuona kakangu kuachana achana ovyo lazima wewe una matatizo basi, jirekebisheni muendelee mbele

 16. dina Says:

  Lina ndugu yangu ndoa hazina formula, hao mmeyasikia ya kwao kwa sababu ya umaarufu wao. Huko mchangani hayo mambo yapo na yanaendelea na yataendelea kuwepo, kama unayo ndoa kazana kuipalilia kwa jinsi yako huku ukimuomba Mungu. Wala usinyanyue pua kwenye issue ya ndoa ya mtu mwingine…kwa sababu the details hutazijua kamwe ni za wao wawili ndio wanajua kama the differences btwn them ni za usuluhishi or not!
  Kama huna ndoa, omba Mungu vilevile akupatie mwenza mwema….

 17. CATHERINE Says:

  adhabu ya maiti aijuay ni kaburi, hv usupastar ndo usababishe apate shida tu ndani ya ndoa kisa nini? aku dada mona bora umejianzia kivyako. Hizi nyumba watu hawajui uchungu wake, na uchungu wake umetofautiana. Sitaki kumlaumu mona wala tyson, hiyo ni siri yao na tuwaache tu kwani mungu anawasaidia na maisha yanaendele. Sisi hatupaswi kutoa hukumu kwani hata wao hakuna aliyesimama akamlaumu m wenzie kwa hiiivyo kama sisi tulivyoshikilia bendera. Big up MONA

 18. MOUREEN Says:

  tyson alisomea upadre, so kipindi hicho akawa hajui mambo ya wanawake sana hadi akamwoa dada yetu mona, kumuweka ndani akajaribu na nje ya ndoa, akapata yale ya ajabu ambayo mke hastahili kumpa hata siku moja. Si mnajua mijishangingi ya kinondoni? basi ikamchanganya kaka wa watu hadi akaona ndoa ni mbaya na akajuta kusomea upadri. matokeo yake ni hayo.

 19. angel Says:

  u r so beutifull ma dia mona

 20. kibaso Says:

  wewe mzuri tu MONA huyo mkenya asikutishe kitu. Kwani umeshindwa nn wewe? Maisha yako wayaweza sis mi nakufagilia kinoma

 21. trii Says:

  ndoa siku hizi ni kama bahati nasibu,yani balaaaa tupu,lkn sio zote baadhi,wazazi wetu wana siri kubwa sana walivyo weza kudumu kwenye ndoa miaka na miaka,Mwenyezi Mungu tushushie hekima+upendo wa kweli.

 22. kekue Says:

  Tatizo ni mawifi zake na mume wake sometime alikuwa anawasikiliza ndugu zake, so mona akaona bora arudi kwao maadam ana wazazi wanaompenda bado na istoshe ni mtt pekee, kwa nn apate shida, jamani wana BC nyumba nyengine ukiolewa ni balaa tupu…..

 23. sugu Says:

  bwana mtuweni toto wa susy ngatwika yy sio wa kwanza kuachwa kwa iyo msimjadili bure

 24. any Says:

  INAELEKEA LINA NI DADAKE TYSON IVO ANA DATA ZA KUTOSHA NDIO MAANA KAMSHIKIA WIFI YAKE (MONA) BANGO

 25. warda Says:

  mimi nampenda huyu dada kwa jitu vingi kwanza akiongea kama mtoto mdogo vile pili hajichubui.

 26. babe Says:

  nimesoma gazeti la this week kuwa na yule mwarabu aliyemuoa tena wameachana nae na amerudi nyumbani kwa mama yake na katoto kake kachotara. labda tuiangalie hii kwa jicho lingine la tatu

 27. Matty Says:

  Christine Apiyo, wewe mjaluo wa wapi unasema mnajua kupenda,,,, kama unapenda ww si wote wanapenda ebo!!!muacheni Mona ajiamulia anachotaka kufanya bwana siri ya kutengana anaijua yy na Tyson!

 28. Samuel Says:

  Lina did not comment anythig so bad to the extent of being abused. It is her opinion, let us comment on main event/character and not abusing each other. Monalisa is a matured Lady so her decision should be respected according to her philosophy, also she still have a lot to perform in her life. “MONA p’se proceed with you life, life is not a marriage but marriage is a part of life.

  Samuel

 29. any Says:

  Na nyie BC kwa nini mmemweka huyu dada na personal life yake! mbona hamkuongelea anafanya nini na kama mlikuwa na mahojiano nae muyaweke apa kama ambavyo mliwafanyia ma celeb wengine kina Mango na Kipanya and the rest! huyu hamjampa interview

 30. any Says:

  huyu Mona hamjampa interview na jinsi gani ana mchango katika jamii through kipaji chake! sana sana mmetuelekeza tujadili nini apa maana badala ya kumjadili kama msanii/mwigizaji discussion kubwa apa imelenga kuachika kwake zaidi ya kipaji kazi yake, hamjamtendea haki dada wa watu.

 31. yusuph Says:

  Vyonne Cheryl a.k.a Monalisa nakupenda sana sis sababu ni mzuri sana hapo katika hiyo picha una watoto 2 lakini ndio kama umemaliza shule.Anyway naomba nkwambie hivi YOUR BEAUTIFUL NO MATTER WHAT THEY SAY WORDS NEVER BRING YOU DOWN.

 32. Chris Says:

  I didn’t knew if people cud be caring about this chick!

 33. Jossy Says:

  Ndoa siyo mchezo ukiona mtu ameamua kuachia ngazi jua mambo yamekuwa makubwa so monalisa asiraumiwe kwa kutokuvumilia. You never know why aliamua kutimua zake. Ndoa zingine karaha tu! Monalisa we mzuri but jiheshimu.

 34. Mtukwao Says:

  Kwakweli nawasifu wale wote walio sema “thats her personal decision let us respect it”!!!

  -“Christine apiyo” ulichokiongea ni upuuzi!!. Hata mimi ni mjaluo, sikatai wajaluo kuachana ni very rare but angalia wanake wakijaluo wanavyo dhalilishwa nwa waumezao, but wanakaa tu just for the stutus of kuolewa??

  “life is all obout your own happyness”, sasa watu wanashangaa kwanini ndoa za zamani zilikuwa zinadumu kuliko za sasa, is bcoz wanawake wengi wa kizamani walikuwa -:
  1. wanafiki, hawakujali furaha zao, walifikiri ndoa is all abt furaha ya mwanaume. so all the time waliworked very hard kuwafurahisha waumezao na sio wao.

  2. walifikiri ndoa ndo maisha, hivyo kukaa kwenye ndoa kwa mda mrefu hatakama unanyanyaswa kwao ilikuwa sawa yani ndo ufahari, kumbe wahakujua ni ujinga.

  3.ndoa ilikuwa just for the public pic, ilimradi furani naye kaolewa, hivyo kuachana ilikuwa ni kitu haramu. Then kama wakiachana hata km mwanaume ndo anamakosa sikuzote mwanamke alionekana ndo mwenye makosa, na pia anaonakama maka”muhuni” kisa kaachana na mumewe.

  4. man was the only house provider, so mwanawake hawakuishi their dreams’ waliishi vile apendavyo mwanaume. yani they didn’t have a say at all!!

  lakini sikuizi wanawake wengi tumeelimika, na lazima tubadilishe huu mtazamo wa jamii kuhusu mwanamke particularly khs “ndoa”. mimi kwakweli sipendi watu wanaposema eti “ndoa ni ngumu inaitaji uvumilivu”, nani kasema ndoa nilazima iwe ngu?? ni bible/quran gani inayosema hivyo?? au ni watu tu wenye frastrurations zao za maisha au ndo zao zimewashinda, then all they can do is scare the hell aout of young couples??

  2me ndoa inatakia iwe yafuraha kupita kiasi coz ni “watu wawili waliopenda wameamua kushare their happyness for a life long” sasa km wote mnapendana na wote mko happy they why mnasema “ndoa ni ngumu”???????jama tuachane na maneno hambayo hayajengi jamii bali kubomoa!!

  mm tatizo ambalo naliona ni kwamba, watu wengi wanakurupuka tu kuowana pila kuwa “marafiki wa dhati” yani watu inabidi wawe marafiki kwa muda mrefu kabla ya kuowana, ili wakuane vizuri. Pia wasichana wenzangu hii tabia ya kung’ang’ania mwanume kwanguvu sio nzuri!! yani utakuta mtu ana BF ambaye amesha mwonyesha dalili zote kw hana mapenzi ya dhati naye, lakini msichana atang’ang’a mpaka avikwe pete nakisha ndo, sijui wanafikiri kwamba huyu mtu kesho atakupenda, sasa km hakupendi leo hii mchana wa jua kali sasa kesho kwenye usiku wa giza nene ndo atakupenda???

  wengine mpaka wanaamua kubeba mimba ilimradi tu aolewe. jamani km watoto wanaleta upendo ndani ya ndoa basi ndoa nyingi zisingekuwa na matatizo!!

 35. Mtukwao Says:

  vilevile wengine wanaolewa kuiga mkumbo, coz maswahiba wake kaoolewa sasa nayeye anataka kuowa..mmmhh! mama usiige kunya kwa tembo………….!!

  nakama ikatokea mtu ambaye umeowana naye kabadilika sio yule uliye mjuwa miaka 10 iliyo pita, hakuana ubaya wowote kuachana naye kwani kuendelea kushi naye ni kama kuolewa na wanaume wamili, yani the man/woman before and after sasa yanaini kuteseka?? Uvumilivu kila mtu anakiwango chake, sio kwbabu mwenzako kavumilia kupigwa na mumewe basi nawe uvumilie, hapana!
  Watu wansema Mona anamtoto na tyson, so wat!!!!!!!!!!!!, hivi mjawakusikia kunawatu wanaitwa “yatima”???? wana baba wala mama wale?? nani anawalea??? basi kama wanakuwa hata huyo waMona atakuwa 2!! hamna tatizo!!

  tatizo letu wasichana wengi tunajidanyanya na kitu kina itwa “hope”, tunahope kuwa tunauwezo wakubadilisha tabia ya mtu especialy wenzi wetu! hivi wewe huyu mtu ambaye haujui “Mungu” alimuumba kwa chemistry gani, alikombine nini kumtengeneza, wewe leo utaweza kumbadilisha kweli???

  Pili wasichana wengi tunafikiri “we can afford love” if we could afford love then “Jesus wouldn’t have to die in Calvery!!!

  Kunawatu wengi ambao wako single and very successful and their enjoying their life. unaweza kuishi maisha ya kudhalilishw a, kukavumilia kisa uwonekane umeolewa, matokokeo yake “raha ya duniani uikose na mbinguni vivile usende” wat a sad thing that will be???????? think abt it.

  “we all live ones not twice, and life have no rewind button, so live ur life now to the fullest”

  mwacheni Mona wawatu, that is her life all we need to do it ro respect her as who she is!!! ataka kama akiend up having seven kids with different dadies, wats wrong with that?? its her life and let us not be judges her!!!

 36. kwere Says:

  naomba namba yake ya cm kwa mwenye nayo plz nina shida naye..

 37. kwere Says:

  jamani niambieni kama ana skendo yoyote?????nampenda sana jamani, napata

 38. Mchome Says:

  Mimi naona kama mnakosea, Mona sio wa kwanza kuachana na mumewe, na wala hamjui tatizo ni nini kati yao. So ni better mkawaachia wenyewe na mjue yenu maana hata ninyi mnaochangia katika blog hii yawezekana ndoa zenu zinamatatizo au zimekufa kabisa so sioni sababu ya kumsakama mona kisa tu eti superstar. What is superstar anyway!

 39. sally Says:

  i wish u all the best,

 40. Matty Says:

  Sally, niliwahi kukuuliza kama wewe ni dada/kaka hukujibu, sorry sikuwa na nia mbaya ni just kujua!

  Any, wats wrong with swanglish no.34/35….hapa sijui kama sitashambuliwa!! ila habari ndo hiyo!!

 41. Debora kiaka kizuguto Says:

  Mambo gani hayo monalisa Ndoa sio fasion Ndoa sio kuoneka umevaa pete, Maamuzi ni kitu muhimu sana na maamuzi ukiyatumia vizuri ni mazuri mno, na ukiyatumia vibaya ni mabaya sana, Unapoolewa kataa kuachana na usitamani, kwani kwa umri wako ni mdogo sana sana itafika mahali na huo pia utamuona hafai utamuacha, Ndoa is not easer, Unafundisha nini jamii kumbuka wewe ni kioo cha jamii mona, Maana kulikuwa na vishindo mno katika ndoa yako, na AC.
  Debora

 42. Matty Says:

  Hey Debora sijakupata vizuri, unasema nakunukuu”unapoolewa kataa kuachana na usitamani” how???
  hv kama jamaa ananirudia usiku wa manane daily na ananidunda without reason nifanyeje hapo????na usizani kuna anayependa kuachika/kuachwa, no ndoa inapofikia sehemu inakuwa ndoana kwanini mtu usipishe jengo????muacheni na personal decision yake, kwani imeandikwa wapi ndoa ilivuma sana na isidumu???inaweza vuma sana na ikadumu yu never know!

 43. any Says:

  Matty Habari ndio Hiyo, maana 34 & 35 naona mchangia kote, katumia zote mbili na sio fasaha!
  na wewe Debora stop your judgemental mentality! Kioo cha jamii unakijua wewe? Kioo cha jamii kinamtaka mtu ateseke kisa alishaamua kuolewa? Kuwa Kioo cha Jamii ni pamoja na kukataa kuishi kwenye ndoa isiyo na furaha in the name of Ndoa. Mimi nampongeza kwa uamuzi wake, maana kaona hapafai na kaondoka. msikae kwenye ndoa kisa sijui watoto itakuwaje! remember those kids need a sober mom! sio mama mwenye depression na mangeu usoni! mwanzo mgumu kwenye kuachana ila in the future una stabilize tu na maisha yanaenda. Mi nashauri wanawake msingoje sana, the sooner the better! haya shauri zenu.

 44. Alice Says:

  Mbona comment yangu mumeitowa jamani?sio mambo hayo.
  Basi kama hamtaki watu wachangie hoja bora mfunge hii BC tujue moja.

 45. Lulu Says:

  Jamani maisha ya Mona hayanatofauti na maisha ya binadamu yoyote hata weye so kama usivyopenda kuyaanika maisha yako hadharani si vema pia kulazimisha kuyajua ya Mona.

  Big Up sana Monalisa
  I adores U

 46. esromchris Says:

  whatever do they say,she is very beatifuly, and she looks like house wife to me.
  regards
  uk


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s