BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SALAMU ZANGU-IRENE SANGA ft MRISHO MPOTO na ELIDADI MSANGI July, 24, 2008

Filed under: Bongo Reality TV,Burudani,Mahusiano/Jamii,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:05 PM

Irene Sanga(kushoto) akiwa jukwaani na Elidadi Msangi.

Kama ikitokea ukawa umechoshwa na kusikiliza nyimbo au miziki inayoelemea upande mmoja tu(mara nyingi upande wa mapenzi) basi hutojutia kubadilisha frequency na kusikiliza wimbo uitwao Salamu Zangu ukiwa ni utunzi mahiri wa msanii Irene Sanga ambaye ameuimba wimbo huo kwa kuwashirikisha msanii maarufu wa mashairi,Mrisho Mpoto na Elidadi Msangi. Salamu Zangu ni mojawapo ya vibao ambavyo vilitokea kupendwa sana nchini Tanzania na kimebakia kuwa gumzo mpaka hivi leo.

Akiongea na BC hivi karibuni, Irene Sanga,alisema aliamua kutunga au kuandika mashairi kama unavyoweza kuyasikia katika wimbo huu,baada ya kukerwa na jinsi ambavyo wasanii wengi wa muziki wanavyokuwa wameegemea zaidi upande wa nyimbo za kimapenzi peke yake na hivyo kusahau kabisa pande zingine za maisha ya jamii kwa mfano umasikini,uonevu nk.Kwake yeye,anasema, muziki au sanaa sio chombo cha kuburudisha tu bali kuonya,kukosoa,kukumbusha nk.

Mshairi Mrisho Mpoto akituma Salamu zake kwa mjomba.

Wimbo huu umo ndani ya albamu iitwayo “Utandawazi” ambayo Irene anasema bado hajaamua kuitoa rasmi sokoni kutokana na sababu mbalimbali.Nyimbo zingine ndani ya albamu hiyo ni kama vile Utandawazi(inayobeba jina la albamu), Pangisheni,Maureen,Usivunje,Ndoto,Afrika Yote na huu Salamu Zangu/Salamu kwa Mjomba.Albamu hiyo imetengenezwa ndani ya Mawingu Studio jijini Dar-es-salaam.

Wimbo huu ambao leo ndio unatupa burudani ya wiki ni ombi rasmi kutoka kwa Pius Mikongoti.Pata Burudani.Wikiendi Njema.

Picha zote na Bob Sankofa.

Advertisements
 

27 Responses to “SALAMU ZANGU-IRENE SANGA ft MRISHO MPOTO na ELIDADI MSANGI”

 1. any Says:

  EEh, haya bwana, personal decision nyingine, haya wee.

 2. […] Blog ya Bongo Celebrity kama kawaida ijumaa hukupatia wimbo mmoja kwa ajili ya kukupoza na mchakamchaka wa weekend nzima, weekend hii wamekuja na kibao Salamu Zangu tokakwake Irene Sanga akimshirikisha Mrisho mpoto na Elidadi Msangi ikiwa ni ombi langu rasmi, Bofya hapa […]

 3. Pearl Says:

  mashavu ya MPOTO tu ndo huwa yananiacha nimechoka.

 4. Edwin Ndaki Says:

  Hapa sasa leo kwa mara nyingi mutima wangu umeburudika sana.

  Kuna kipindi wimbo ulileta utata kwamba nani mtunzi wa songi.Ila kwa tuliojua ukweli tuliendelea kuamini kuwa mashairikatunga Irine.

  ´Gervas na Matty yaani kwenye wimbo huu napenda pale “pa shoka hapaingii kisu”

  Any,Michelle,Angelina,Dinah,Warda,Dunda Galden,Ed Hombizi,Hans …nyie nawapa hii..”mkifunga mkanda matanga yataisha upesi”.

  Chris,Pearl,mtoto mzuri,mama wa kichaga,kekue,Lina…”pepo haina maana pasipokuwepo jehanamu…”

  Debra swahiba..najua tumetanganishwa na ukuta..lakini pokea salamu zangu…

  BC nanyie..vibwaya..mviweke hadharani tucheze ngoma zetu wanazosema ni za kishenzi…a aaaa

  Dinah..”visima vya kale havifukiwi” umeidaka hiyo…

  hizo ni salaama zangu kwa wadau wote wa BC..

  maneno mengi haya jengi ghorofa.

  salaaaaam zangu kwanu eee heeeee..ijumaa tamu watu wangu.

  tutafika tu..nawapenda sana

 5. Mkwaya Says:

  Mi namkubali sana Irene na Mrisho.. wamekaa na kufikiri sio kama wasanii wettu wa ubongo wa fleva…
  Mkipta za Maembe tafadhali mziweke maana hawa vijana wamekaa chini wakafikiri…

 6. Matty Says:

  Any, haya mambo ni kama Ngonjera kimtindo ..ila huyu dada ni black byute!!!!

 7. mambo Says:

  Nawapa bg up bwana mpoto na irene nyimbo zenu zina nigusa sana hasa ule wa watoto yatima wa njombe nyimbo zenu ni za ki Tanzania sana mnastahili pongezi sana kwa hilo maana wasanii wengi wenye majina makubwa wana copy nyimbo za wamarekani kwa kuzitafsiri kama zilivyo na wengine kuishia kuiba hata mashairi na melody nchi za jirani.Ongezeni ubunifu zaidi tuendelee kupata vitu halisi kutoka kwetu.

 8. BabyGirl Says:

  Aisee hii nyimbo huwa inanikuna sana Maneno yake
  Hivi kweli viongozi wetu huwa wanasikiliza kweli huu wimbo na kama wanasikiliza halafu hawafuatilii kweli vichwa vyao vimejaa Uwendawazimu.

  Anyway Ndio Bongo yetu hiyo.

 9. Dunda Galden Says:

  Salam zimefika mjomba BC
  mwimbo mzuri wenye ujumbe unaoendana na nyakati
  Mrisho songa mjomba salam zitawafikia wahusika
  (Taja magogo yote la mbuyu si la mvule)
  ( Lisilo kuwasha haujailmba)
  (Wamulike mapolisi wanaohukumu kwa makofi kabla hakimu hajasoma hukumu)
  Inabidi uwe makini pindi unapisikiliza salam.huu mwimbo utasikilizwa kwa miaka mingi ijayo na utakuwa unamgusa kila mtu,(SIKUFUNDISHI MJOMBA HIZI NI SALAM ZANGU)
  Chafosa mwana wa pangu pakavu

 10. michelle Says:

  Hii ndo nyimbo sasa, so mapenzi na viuno tuuuuuuuuu tumechoka bwana

 11. warda Says:

  MRISHO MPOTO HAYO MAJASHO NA HIZO RASTA HATARI KWELKWEL.ANY WAY NDIO MAMBO YA BURUDANI HAYO.

 12. mzee msuya B Says:

  sikiliza vyombo,halafu mashairi! hawa kweli ni wanamuziki.
  Huu ni muziki hata mimi mzee nausililiza sana.

 13. GEORGE Says:

  Shem Irene nakupa shavu.Endelea kuwapa somo wajomba.
  Vipi ile sinema yako umekwisha anza kuiuza rasmi.

 14. Pearl Says:

  Edwin Ndaki salaam zako nimezipata fresh.

 15. Matty Says:

  E.Ndaki…thanks God wknd ilikuwa njema upande wangu….natumaini ilikuwa njema kwa wana BC wote!! pamoja na BC wenyewe!
  Jamani na mimi nataka kuweka rasta kichwani kuna anayejua niaje kwenye suala la usafi????pls msaada tutani!

 16. any Says:

  Wimbo na yeye wanatofauti kubwa sana. Ni mtazamo! Matty hizi salam anapewa nani? Huyo mjomba asiposikia tena basi bwana.

 17. kekue Says:

  Jamani hizo rasta du!! Matty ni hizo za rasta hapo zimekuvutia mpaka unataka na ww zikutembelee au nini? Nashukuru kwa salam mzee wa tutafika tu.

 18. Matty Says:

  hahahaahahhaaah Any mjomba asiposikia hata shangazi pia atazipokea kwa niana nadhani hiyo huwaga imo!
  Any sasa mbona hujasema kitu kuhusu rasta???msaada tutani pls au na wewe ni mgeni wa hayo mambo?

 19. Matty Says:

  heee!! hapo juu ulimi hauna mfupa (niana = niaba)

 20. Ras Uhuru Says:

  Mashairi yametuliia hasa,kazi nzuri sana Mpoto.
  Ni mashairi ya kuaamsha akili za wananchi.
  Na kuwaonya na kuwakosaa walaji wachache wa taifa letu.
  Enough Respect!

 21. any Says:

  matty sasa unamwingilia personal decision zake, mi hizo nywele na mashavu are not my cup of tea! ila bado inabakia kuwa personal decision yake! haaa,
  alafu alivopozi apo kwenye picha kama anachungulia, au kama ana usongo fulani! eeeh. wenye kujua luha za picha waje waseme.

 22. Matty Says:

  Kekuu unajua mimi nywele zangu za asili not reachable kabisa sasa nataka nitest hii staili ya rasta may be nitafanikiwa, maana mambo ya kalikiti na mawiving yamenichosha, ikishindikana basi nitaenda miss universe styl.
  Any huyu kaka anaonekana kama hana mazoezi ndo maana shavu dodo namna hii!

 23. Dunda Golden Says:

  Edwin Ndaki salam zimefika mjomba
  Lakin majanga yanapozidi roho uwota kutu

 24. binti-mzuri Says:

  Edwin ndaki nimekupata sawia..ila mie sio mtoto mzuri,ni binti mzuri kaka…nshavunja nanihiii

 25. any Says:

  Unene nauhusishaga na uzembe kwenye kila kitu! sasa sijui apa nisemeje! mazoezi basi hata ya kukaza misuli ya mashavu! shavu inamwaika mtoto bado mdogo, khaa.

 26. trii Says:

  Any-umenifurahisha.kweli yana waka waka,hayo mashavu kwa kufichia nyama ukiiba kwenye sufuria ndo yenyewe.mama hawezi kugundua.

 27. Amina Says:

  haya kilichowafanya muanze kugombana kuhusu huu wimbo ni nini?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s