BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ILIVYOKUWA CHICAGO SUMMER BREEZE BBQ July, 28, 2008

Filed under: Burudani,Kutoka Ughaibuni,Mambo Mseto,Watu na Matukio,Weekend Special — bongocelebrity @ 1:08 PM

Kwa sababu tulikuletea matangazo kuhusu BBQ iliyofanyika jijini Chicago mwishoni mwa wiki iliyopita,tunadhani ni busara kukuletea pia picha kidogo ili kama hukupata nafasi ya kuhudhuria,basi japo uone jinsi mambo yalivyokuwa.Here we go;

Bingwa wa DanceHall kutoka Chicago,Bantuman,akiwapa burudani waliohudhuria.

Panapofuka moshi mara nyingi huwa pana chakula.

Ilipofika jioni mambo yalikuwa kama unavyoona pichani.

Kwa picha zaidi bonyeza(more) hapo chini.

Joy and fun of the BBQ

Full shangwe.

Chinga Boi,msanii wa bongo flava mwenye makazi jijini Detroit akiwakilisha kikamilifu.

You definitely recognize some of these faces,right?

Raha Kamili.

It was a family day as well.

Its always joy to meet a friend.

It was time to go!!

Advertisements
 

70 Responses to “ILIVYOKUWA CHICAGO SUMMER BREEZE BBQ”

 1. pyupyu Says:

  kwa kweli ni kujipopochoa na kujiachia kwa kwenda mbele

  Huyu chinga boy anafanana na jamaa mmoja alisoma pale Tambaza miaka ya 1996-98,kama kweli ni yeye amejitahidi kwamana amekata kilo kimtindo.

 2. Dunda Galden Says:

  Afadhali hakukuwa na longolongo wadau
  naona mambo yalikwenda kama mlivyo
  panga hamana tabu wengine watafuatia

 3. mama weee Says:

  du siku hizi salum ndolanga unaimba bongo flava makubwa kweli kweli haya sasa nendeni nyumbani (bongo )usiku umeingia duuu na magari ya kukodisha hivi bado mnaakili za kitoto sasa ukikodisha gari sio lako umelipa hela nyingi just for the ride to spean someone else wheels.

 4. Dunda Galden Says:

  JEFF LETE HABARI ZA CHACHA WANGWE RADIO INTENET HAPA INATANGAZA AMEFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI
  POLENI SANA WAFIWA

 5. V8V Says:

  Thanks Chicago for the BBQ and the party, we had so much fun.

 6. KingKong Says:

  Tangu lini ukaona Range Rovers kwenye rental cars places hayo magari yatakuwa yao binafsi.

 7. Matty Says:

  Any ni wewe pichani??? maana ulisema utahudhuria hilo parrrtyyyyy!! naona ilikuwa full kujiachia!!

 8. Jenny Says:

  Party ilikuwa nzuri na wote tuliokuwepo tulifurahia yaani nilifurahi baada ya kwenda columbus na kupatwa na mahasira, asanteni Chicago na inabidi mfanye nyingine tuje tena.

 9. binti-mzuri Says:

  hahaha ‘mama wee’ umenichekesha mie… mimi no comment..maana ukistaajabu ya musa,ya firauni yatakuumbua

 10. Heavyweight Says:

  KingKong..mbona hata Ferrari watu wanakodisha iwe range rover??Sasa na ndege watu wanakodisha siku hizi..Anyway,i was trying to make a point.kuhusu magari kama ni yao au la…mimi siingilii….LOL

 11. KingKong Says:

  Wewe Heavyweight nionyeshe public rental place ipi inayokodisha watu Ferrari au Range Rover? Magari kama Ferrari ukikuta yanakodishwa basi ni kwa VIPs na vibopa wenye fweza zao na sio walalahoi kama wewe na mimi, usije kuigonga gari ya watu bure na insurance yako ya dola 10 ambayo haitocover hata side mirror.

 12. Samchecks. Says:

  Chicago ule ushibe!!! Watu hawakodi magari,njoo Chi’ town ujionee,wakristu wame-settle..

 13. koshkov Says:

  kama we kingkong uko worried na insurance tu then it seems life is hard huh? hahahah njoo chitown uone the same rovers everyday……u will see em rovers with the same plate numbers everywhere from columbus to dc to houston , they r covered too…dont hate

 14. binti-mzuri Says:

  we KingKong uko USA ya wapi..mbona unakua mshamba… juzi juzi tu hapa,tumeenda central london walikua wanakodisha lamborghini kuanzia masaa,mpaka wiki.. sembuse range rover…

 15. big sex Says:

  mie napenda kusema kwamba mie sioni mabishano ya kuwa na range au nini kama ni yamsingi sana kubishania kwa maana hata hao wanao sema kwamba eti wanyamiliki ukiwauliza hapa marekani walikujaje utaambiwa kule bongo walichangiwa nauli ya kuja hapa marekani,,,,,,,,,,,,,,,!alafu ukiangalia thamani ya hizo gari wanazozushia wanazimiliki hata huku marekani kwenye kwa wamarekani wazaliwa ni ngumu manake mambo huku hayaendi kama bongo huwezi kumiliki haya magari eti kwa kibarua cha kufanya laundry au housekeeping ambazo wabongo wengi wanakomaa nazo hapa marekani sio rahisi,,,,,,,,,,,,,,,,,!sasa hao wabongo wanaosema hayo magari ni yao waulize ni kazi gani walizonazo hapa marekani za kuwapa magari kama hayo?ni uzushi mtupu kabisa nyie mnakopi na kupesti magari kwenye internet kwenye web za kuuzia magari mnasema yakwenu acheni ulimbukeni utawauwa kabisa sio siri,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!mie kwa maisha ninayowaona watz wanyoishi hapa marekani sio rahisi kumiliki magari kama hayo ,,,,,,,,,,,,,,!huo ni ujinga tu mnabishana wala hausaidii chochote kwanza hawa watu jinsi ninanyo waona wengiwao mmesha droppiwa mashuleni na kurepotiwa kwenye internationa student kwa jili ya kudipotiwa muache uzushi kabisa

 16. koshkov Says:

  damn!!! kumbe maisha ya wengi magumu hapa mtoni huh? hata wewe big sexy kumbe u broke as hell? i didnt know b4 kama maisha yenu ni magumu kiasi hiki……damn!! kwa hiyo wewe bado unafanya kazi za kishenzi mtoni hii? pole sana karibu chitown tutakuprovide na shelter

 17. anon Says:

  big sex Says: July, 30, 2008 at 7:53 pm
  samahani ngoja nikufahamishe kwa komenti yako inaelekea ulikaa marekani miaka ya zamani sana kama bado upo hapa basi huja-catch up.
  wabongo wanaong’ang’ania status ya shule kuogopa droppiwa mashuleni kwa kipindi hiki ni wale wanaotoka vijijini au washamba kwa msemo mwingine, siku hizi hatuishi hivyo wajanja wengi tayari wanaishi kihalali na kufanya kazi nzuri tu kihalali ndo maana wana-afford hizo range na magari mengine ya kifahari
  sasa mjanja ni yupi? yule alekuja na mamilioni kibao ya wazazi wake kayamaliza kaishia kufanya kazi ya $7 hata hawezi kurudisha faida kweo au mjanja ni yule aliyechangiwa nauli karudisha nauli kwa wanaomdai, sasa hivi anasaidia ndugu zake na anaendesha range?
  ni sawa majority ya wabongo wanapiga box, wanafanya laundry au housekeeping kama unavyosema ila few blessed ones wako kwenye corporate america na wana-live american dream.
  moja ya hiyo range mwenye nayo namjua na nadhani anailipia kihalali kwa mshahara wa kazi na biashara halali sio dili za mkato kama unavyofikiria. uliza utaambiwa tuacheni kuoneana wivu wabongo!
  ni hayo tu.

 18. Matty Says:

  Kazi mnayo!!

 19. Fogo Says:

  E bwana kingkong ni kimeo anashangaa kuona vogue! LOL e bwana ebu rudi bongo uone wa2 wanavogue za kukinga na zao binafsi! Mimi mwenyewe nipo bongo natembelea vogue sports! sasa we inaonekana kutafuta hata USD 89,000 Kununulia umeshindwa Mimi yangu nilinunua Mil.180! Acha Ushamba

 20. mkereketwa bongoz Says:

  sis huku bongo tunashangazwa na hayo maubishano yenu..naona vijana mnafurahia kukaa katika miji ya wenzenu.mababu zao walifanya kazi kubwa ya kuendeleza nchi.acheni ulimbukeni huku ni ugenini na kutabakia kuwa hivyo milele.tulitegemea muwe mfano kwa vijana wenzenu huku bongo mtuambiwe mnamiliki biashara kubwa ili iwe changamoto kwa wabongo wengine ila naona mnabishania magari.huo ni umaskini wa kifikra..uwe umekodisha,liwe la kwako hiyo sio concern yetu ila mtuambie mmefanikiwa vipi kimaisha hiyo ndo changamoto kwetu.hizo party hata sisis huku tunazo tena nyingi sana..ni hela yako tu.hizo rovers hata huku zipo vijana wanaendesha ni hela yako tu…kupitia mitandao tuambiane ukweli na sio kudanganyana .bongon ya miaka ya 80 sio kama ya leo…mkifiwa mnashindwa kurudi kuzika wazazi wenu halafu mnatuambia mnamiliki magari huo ni ufinyu na usakala wa mawazo
  salamuuuuuuuz

 21. IZZO UoN Says:

  DA! BILA SHAKA SHOW MOJA BOMBA NIMEDATISHWA NA HAO MABINTI WA KIBONGO MZUKA MNENE

 22. Heavyweight Says:

  Kingkong ngoja nikumegee website moja basi ukasafishe macho..siku nyingine tumia searching engine(google) ..and then utapata jibu…..www.bhrentacar.com

 23. cutie Says:

  du watu mnahate, poleni watu wa chi, mi nawajua wenye hizo rovers na hawabebi box wanafanya kazi za kawaida ambazo wako confortable, kitu kingine ni kwamba watu wanasaidiana kama mtu na demu wake wote wana kazi bomba kwa nini wasiendeshe rover bwana, acheni kuhate kama huna appreciate kwani ukihate haitokusadia wala nini mnaohate wote mnabeba box dizaini nyie, poleni kwa maisha magumu ombeni msaada mtasaidiwa sio kuhate, mbona bongo zipo kibao hizo rover na watu hamuwaulizi? inaonyesha nyie mnaohate maisha yashawachapa poleni sana na mrudi makwenu, for your info Chi kuna magari mengi tu ya thamani sio hayo mawili tu ulizeni mtaambiwa, watu wako confortable sio nyie mnaohemea juu juu,

 24. cutie Says:

  not only Chi kwenye migari ya ajabu ni kote tu hapa USA mi nimeenda Huoston nimebaki mdomo wazi migari hiyo na unajua mahater (wasiokuwa nayo) wamasemo ambao ni vere common, “magari yamekodishwa” damn people, sema wewe hater umeshachoka na maisha na unajiona huna basi kila alienacho unaona kaazima au kakodi, sio issue ndugu yangu, mi nipo bongo hapa na mshkaji wangu anasukuma range kali kama hizo za hapo juu, he got it with 0 miles on it sasa utamhate umwambie ni mkodisho? masikini wee nawaonea huruma sana fanyeni kazi kwa bidii labda na nyie mwaweza pata at least used Range mkishapata tujulisheni wadau ili tuwape hongera coz cos watu hatuhate tunacongratulate,

  By the way hongereni wenye magari yenu hapo juu, nunueni hata Lamborghini mkiweza, achanieni na wabongo mahater njaa tu zawasumbua wakishiba hamtowasikia hawa……

 25. anon Says:

  mkereketwa bongoz Says: July, 31, 2008 at 8:41 am
  naomba nikufahamishe kuwa marekani ni nchi ya wahamiaji kama unafatilia news hata rais mtarajiwa baba yake alihamia ingawa hakuuweka sana.
  pili sio kila mtu ni naturally mfanyabiashara ingekuwa kila mtu anafungua business sijui kazi nyingine angefanya nani, people do better on what they are better on doing! kuna topic moja ya specialization somo la commerce form 3, kama ulibahatika kwenda secondary labda itabidi ui-review
  kufiwa na kushindwa kurudi ni matatizo ya mtu na mtu watu wengi tu wanafiwa wanaweza kurudi, hata wewe sidhani kwamba una solution ya matatizo yako yote, kuna matatizo ambayo yako nje ya uwezo wako

 26. Heavyweight Says:

  Well…Cute umesema watu wana-hate kuhusu hizo range..can u at least mention two individuals ambao wamesema au wameonyesha wana-hate kwenye hii topic besides mama wee…pliz

 27. trii Says:

  nasikia huwa wanalia kwenye simu.litakaye mgusa ndo huyo huyo.

 28. trii Says:

  tusidanganyane,mtu kweli utafiwa na mzazi wako ushindwe kuja eti unamatatizo?may be if u are in ICU nitakuelewa,ukifiwa na ndugu ok unaweza usije,lakini sio WAZAZI.

 29. trii Says:

  ku miliki gari is ok it doesnt matter how expensive it is,kama vijisenti vipo why not,raha jipe mwenyewe.hamna mtu anaye penda maisha ya shida basi tu,nyie endeleeni kubeba mabox kama inalipa is ok,kazi ni kazi.kila mtu na mipango yake ,ni sawa na mtu anamiliki simu kali lakini ana kuomba umpunguzie salio ni maisha.

 30. Matty Says:

  hahahahaahahahahahahahaha nikipitisha siku bila kucheka am sure the next day nitacheka tu jamani hii kali hapa!!

  Tri, mtu ana simu kali kisha anadonea voucher!! hahahahahahahahahahah

 31. KingKong Says:

  Wewe heavyweight naona haulewi, issue unayoambiwa hapa ni kwamba hizo gari huna pesa ya ku-rent wewe hebu angalia kidogo hapa uone ni kiasi gani ku-rent Ferrari. Una uwezo wa kulipa $1800 kwa siku wewe? Una Insurance ya maana? Utakuta kwenye hiko ki-honda chako kwa mwaka 1988 huna hata insurance oooops nimesahau kumbe unatumia public buses http://www.bhrentacar.com/searchvehicleresult.htm

 32. Leila shakum Says:

  nyinyi watu wenye ufinyu wa akili mnanichekesha sana. I am in washington D.C na nina miliki gari bomba tu. kazi ninayo nzuri, nyumba ya mortgage tena bomba and am living the life. na wala sio mimi pekee, wapo watu wengi sana tu Marekani tunaonufaika na benefits za nchi hii. nyinyi walalhoi mtaendelea kuponda,watu tunazidi kupanda.ovyo

 33. truthfulness Says:

  wewe cutie acha pumba..sasa boyfriend wako yuko ulaya anasukuma wheels za nguvu wewe unajitapa,NUNUA LA KWAKO!!!!… yani bongo akili ndogo sana, utakuta mtu anasema tajiri kisa eti anko yako ana hela. strive and work for your sweat,then ujitape,because utakua ume earn that respect.

  kukodisha gari doesnt mean huna hela, mbona hata kina pdiddy wanakodisha magari sometimes,actually most of the times kuwapeleka kwenye events kama awards etc

  HAYO MAGARI HAPO JUU 90% YAMEKODISHWA

 34. truthfulness Says:

  halafu fogo,mbona na wewe unatuchekesha..sasa unasema una gari la mil. 180, unakuta hapo nyumba huna wala hamna savings.. HA HA HA.. wabongo mnasukumwa sana na peer pressure, just because pdiddy drives a pontiac,kila mtu anataka. sometimes think first

 35. cutie Says:

  We Heavy weight, whatever!!, iwe huyo mama wee au wengine, mi sio kazi yangu kukumbuka majina ya watu thast why i didnt bother kuandika who was hating, ni wazi kuwa aliehate anahate tu kama angekuwa ahate mabishano yasingekuwepo……………
  ili mradi ujumbe umefika wheather kwa mama wee au kwa mtu yoyote mwenginea anae hate!

 36. kessy Says:

  jamani wabongo mnatia aibu,kujadili mambo yasiyo na msingi,kila mtu na maisha yake mwenyewe,wengine wanafanikiwa na wengine hawafanikiwi,sasa hamna aja ya kujajiana,wengine ni wivu unawasumbua,that is my advice.

 37. KingKong Says:

  Jeff acha kubania comments zangu mshikaji, bwana hawa haters lazima tuwaambie ukweli kama wao wanashindwa kununua magari makali wanadhani hata wenzao ni hivyo hivyo.

 38. big sex Says:

  nyie acheni kutuyayusha kama hayo magari yangekuwa yakwenu jinsi ninavyo wajua wabongo si mgepiganayo picha kutuonyesha niyenu masurayenu yangekuwepo au hata kukaa ndani jinsi mnavyopenda masifa wabongo,,,,,,,,,,!upumbavu mtupu wewe unakuja kuishi american dream marekani na wakati watu tumeenza kuishi hevean dream toka tupo bongo itakuwa amerikani dream,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!lahasha inaamana nyie raha mmekuja kuzianzia marekani mmmmmh nanchekesha kwa ulimbukeni nyie ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!kanza hayo magari yanaonyeshwa yanauzwa hata jinsi yalivyo egeshwa sio kama yanatumika acheni ujinga kabisa kama ni picha wekeni na sio kuleta ulimbukeni………………….!wabongo huku marekani wanasubiriaga mpk snow ianze kumwagika ndio wanapiga picha ila wawa chengue watu wako mtoni ita kuwa mbele ya range rover bull shit damn,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!madoctar tu wa marekani kuyapata hayo marenji mpk wazichange itakuwa mzushi tu katokabongo kwa nauli za kuchanga aje atese nchi zenye heshima yake hii marekani acheni uzushi ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!ukisikiliza hata mamziki ya kibongo jinsi mapromotar wanavyopenda kurushwa hewani kwenye nyimbo ili kujipatia majina kijinga jinga tu ita kuwa una range rover eti usipige nalo picha watu wakakuona nalo wapuuzi nyie acheni ulimbukeni wenu,,,,,,,,,,,,,?

  wabongo kwa kupenda umaarufu wa kijinga na ujinga ndio wenyewe,bongo mtu anakuwa maarufu kwa kutoka tu kwenye tangazo la TIGO na ukimuona mtaani anatembea kenchi zote kaziweka juu na anakula ngozi anavyotaka umuelezi kitu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!nyie wote wazushi tu huko,,,,,,,,,,,,,,,,huku marekani hata chizi wabongo tu anaweza kuendesha magari kama hayo manake vitu vingi vinaenda kwa mikopo na vilvelie ni ngumu bado kwa mjinga tu kukopa range kirahisi

 39. anon Says:

  hapa nimestukia wengi ni wala vumbi(wako tz) ndo maana mjadala unakuwa hauishi
  naona wanaleta stories just to fit in the conversation
  mfano: truthfulness Says: August, 1, 2008 at 11:37 am
  anasema “just because pdiddy drives a pontiac,kila mtu anataka. sometimes think first”
  WHAAAAT??????????????
  PDIDDY anaendesha Pontiac?????? R U serious?
  Pontiac siku hizi wametoa executive luxury car? au anaendesha pontiac G6??? LOL
  sijawahi kusikia/kuona pdiddy anaendesha pontiac, somebody please prove me wrong please

 40. mjuaji Says:

  kwa uchumi wa sasa hivi sio hatari kumiliki gari kama hilo! mimi naishi chicago na sina hata mkokoteni! ila i can assure you nikitaka range nalipata kesho… ukienda kwa dealers wanakulazimisha kuchukua truck maana yamedoda na kama kuna mtu anasoma wall street journal, GM Motors wametangaza kupunguza production za truck ili kukwepa hasara. marekani ni mchi ya mikopo as long as u got good cedit na sasa hivi with this RECESSION bad credit is good credit. so yall do the math……. and just for the record hayo magari niya kwao!!!!!!! by mjuaji

 41. MZIWANDA Says:

  WEWE LEILA NA MADEMU WENGINE MNAOJISIFU KUMILIKI MIGARI YA THAMANI MNADHANI BILA KUTOROKA NA VIBABU VYA KIZUNGU BONGO KAMA MWANA F.A ALIVYOSEMA MNGEKUWA WAPI KAMA SIO KUFANYA KAZI ZA HOUSE KEEPING AND LAUNDRY
  NA HIZO NYUMBA NI ZA HIVYO VIBABU VYENU MSUBIRI HIVYO VIBABU VIFE NDIO MUANZE KUONGEA

 42. cutie Says:

  oke, king kong umeshinda, kuna marange ya rental nimeyaona humo kwenye http://www.bhrentacar.com, haya mie simo tena humu ndani goodluck everyone!!

 43. cutie Says:

  sore nilimaanisha heavy weight

 44. KingKong Says:

  cutie, hivi nani atatoa $3,000 kwa wiki ili akodi Range Rover?Huyo Heavyweight anatembea na bus pass.

 45. cutie Says:

  Haha, King Kong umeniuwa mbavu mwenzio, hata mi naona Heavy Weight anatembelea bus pass huyo, ndio maana ana hasira mpaka kwenda kutuwekea website ili amake point, hata mi nimekubali but pia its true like you said hamna mtu ataetoa $3000 ili arenti range kuendea kwenye BBQ, please, i didnt think of that, Heavy weight kanunue Pontiac na wewe Uwe kama Pdiddy kama alivyokushauri mdau mwenzio Truthfulness, Damn sikuiona hiyo, PDIDDY PONTIAC????????please!! labda alikuwa kwenye comercial ndo Truthfulness akadhani ukweli, Pole!!

 46. cutie Says:

  Anon, usijali hata mie nakusupport, Truthfulness ni mla vumbi tu huyo, sijui hiyo habari ya Pdiddy kuendesha pontiac kaipata wapi? huyu atakuwa one of those people ambao haelewi ung’enge, so labda alisikia habari flani alafu katika paragraph nzima mzee akaibuka na Pdiddy and Pontiac tu maana mengine yote yalimpita kwa umaimuna wake, basi masikini ya mungu mwenzetu aka conclude kwamba Pdiddy anaendesha pontiac?!! LOL

 47. cutie Says:

  Mziwanda, hiyo inaonyesha ni jinsi gani unahate a sucessful sister, i dont care how she gets her money but the most inporntant thing is that she has money, so wewe ukianzisha hizo story zako kama watu wana magari ya kifahari kwa ajili ya vibabu vya kizungu poa tu at the end of the day we ndo unahangaika na michuma ( mabasi and Train) wenzio twala viyoyozi kwenye ma Escalade!, tena na jua hili ya bongo babu, lo pole sana, goodluck with michuma, watu hatuko interested kujua how a sister got her money watu tuko interested kujua how big she is living, love it or hate it!!!

 48. cutie Says:

  alafu Truthfulness wewe unajulikana kwa ubishi huko madongo kuinama kwenu, well kama vipi njoo nikupe ride, ukipanda gari langu utakataa kushuka mwenyewe, so dont sit here and talk about nunua la kwako, ungeuliza kwanza kama nnalo au sina, kwa taarifa yako siringii cha mtu yoyote naappreciate what someone has because i know how hard they work to get those, sio wewe ambae hujui kitu, ningekushauri unyamaze tu ndugu yangu!!

 49. shey Says:

  Its sad.. jamani someni elimu haina mwisho.. and it is never too late!

 50. trii Says:

  kila mtu aliye na gari anajua mwenyewe jinsi gani alivyo lipata–wengine ni urdhi,wengine kupitia bahati na sibu/bingo,wengine gift,wengine through mikopo,wengine walihongwa,wengine kwa kuuza unga,wengine kwa kutoa mgongo,wengine kwa kufanya kazi kwa bidii+kuchanga pesa,hapa la maana watueleze tuu technique ipi walitumia ili wale wasio naye wajua njia ipi wataona inafaa kutumia.

 51. trii Says:

  cutie waambie kuwa mwanamke is an advantage,ipi bora kuwa na kibabu kizee tajiri au kuwa na kijana maskini?basi na wanaume tafuteni na sugar mummy yenye pesa muambulia magari+majumba.tusidanganyane kila mtu anatamani maisha mazuri.nani hapa asiyependa kuwa na gari kali+nyumba???

 52. trii Says:

  tena raha kulia msiba kwenye jumba lako,kuliko kulia msiba uswahili nyumba ya kupanga,baada ya msiba unaambiwa uhame,utakoma ubishi.hapo ndo ukute hauna kazi uliye kuwa unamtegemea ndo kasha tangulia mbele ya haki.

 53. babe Says:

  watu kwa mashauziiiiii ovyooooooo

 54. Pakacha Says:

  Wabongo wa ughaibuni hamna pesa za kununua Range Rovers hizo gari lazima mmekodisha halafu mnakuja kutudanganya kuwa ni zenu. Mmezikodisha ili mzipige picha hizo gari kutudanganya kuwa ni zenu halafu mkarudi kwenye vi-corolla vyenu vilivyochoka teh tehe teh teh teh teh teh teh.

 55. Anon Says:

  G and N I think y’all should shut them haters up by a visit to Jesse White’s office and personalize those Rovers…plate suggestions:- Hi Haters, Bye Haters.

 56. binti-mzuri Says:

  mi naisupport namba 47 …. mademu wawaaaaa!!

 57. Jacqueline Says:

  Mimi namjua sana mmoja wa mwenye range rover hizo na najua anaendesha range toka miaka ya zamani na si mtu mwenye makuu wala majivuno, he is such a nice guy.

 58. Matty Says:

  ahahahahahahahahahahahahahaha no. 47 Cutie unapatikana wapi maana daaa si mchezo…. maendeleo first mengine chini ya carpet!!
  Trii &Binti-mzuri hayo ndo maneno a.k.a habari ndo hiyo!

 59. any Says:

  Matty huyo mwenye kishati cha njano na kipedo cheupe ni mie, umeona hicho kitako cha kishikaji?

 60. Matty Says:

  hahahahahahaaa!!!!!!!!!! nimekuona Any mh! tumbizane ukweli wewe ni mchaga kweli???au upande mhaya???maana hizo shepu adimu mara nyingi zipo BK! lakini sasa huonekani reception!! i hope nayo inavutia!!!

 61. any Says:

  Wee Matty mbona unahoji “my reception yangu”? hahaha Reception ni kama ya Odemba kabla hajaanza kujipaka makeup nyingi. so u can imagine! alafu hicho kishepu umekiona lakini! wachaga ndio ivo ila ukikuta waliobarikiwa kama Machame na Marangu! unaweza dhani uko kwa wanyarwanda au wasomali/ethiopians. ambao hawakubarikiwa wanakuwa hawajabarikiwa haswa, kinachotusaidia ni ile ari ya kutafuta pesa na kusoma kwa bidii, so hiyo inafunika machungu yote ya tumiguu twa penseli. upo apo Matty? Niamkie kwanza, sawa? haa.

 62. Matty Says:

  hahahahahahahahahahahaaaaaa Shkamoo dada Any…Anithaaaaa au nimekothea??
  Jamani umeniacha hoi khaaa tumiguuu twa penseli tena? sio cokacola?? ila huwa najiulizaga sana sipati jibu mbona moshi na bk sote twala matoke ila bk tunaongoza kwa miguu na makalio, au ninyi wenzetu mbege inawaleteaga aleji???jokes mwaya!

 63. any Says:

  Sisi tunakula matoke lakini wazazi wengine wanayatia magadi ndio maana ndizi zinashuka zikifika kiunoni haziendi miguuni, ndio shida ilipo! alafu hatuli samaki kina Sato na Sangara! Sisi tunakula samaki wa nyumba ya Mungu na wengi wa hao samaki wanakuwaga na minyoo, so u can imagine, protini lazima igomee kwenye manyonyo na kitambi, haishuki zaidi ya apo! Sawa Matty!

 64. any Says:

  Alafu Matty umeona hiyo picha nilivotegesha kiwowo kiuchokozi fulani, mweee! hadi raha, yaani ilikuwa makusudi.

 65. Matty Says:

  hahahahahahah wewe sema tu ngoja akusikie bimkubwa unakandia chakula chenu, siunajuaga alivyo na hulka za hasira hahhahaahahha
  halafu kiwowo ulikitega si mchezo aaah uliwatega mno wapigajipicha ni hatari!
  nice wknd!

 66. any Says:

  Haaaa, habari ndio hiyo, mi mchaga bwana, pamoja na hayo bado nakubali kuna vitu tunalipa vingine hatulipi! kama ilivo kwenu Matty, kwani wahaya wote wana tuwowo na miguu ya mgomba? si kuna wengine wamebarikiwa na wengine wamenyimwa! ndio ivo ivo hata Moshi.

 67. any Says:

  Hulka za hasira mi hazinihusu Matty, i am here to have fun bana, hasira za nini huku mtandaoni, apa nakuja kurelease stress then maisha yanasonga mbele, ndio siri ya mafanikio. Sura inatakiwa ibakie na mng’ao japo umri umeenda! na Nani alileta mambo ya umri ni wazungu au ni nani hakyanani! ingekuwa hakuna manamba namba haya, tungekuwa mateenagers hadi tunatembea na mikongojo! colonialism noma sana.

 68. any Says:

  haaaa, Ivi ni nani huyo mwenye hulka ya hasira, unajua sikuwa nimeinyaka, duu. akija humu Matty unae, mi niko off leo, shauri yako, haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! nicheke mie pacha wake Odemba.

 69. Matty Says:

  hahahahahah Any bana hata hujanistua kama umeandika kitu hapa! mimi nilijua topic imeisha nikajimuvuzisha topic zijazo.

  mhhh kumtaja noma naogopa kusutwa ila ushamjua na habari ndo hiyo!

  Ni kweli kule BK wengine no mvuto, no hips dont lie, no reception,no mguu sema tu ndizi za BK ni noma kwa utamu bana kuliko za Moshi! haaa na senene sasa uwapate mhhhh balaaa i miss BK.

 70. POPO Says:

  HEBU ACHE NI KUHATE JAMANI, JUST BE HAPPY FOR THIS CHI-TOWN PLAYERS. I LOVE YOU MY PEOPLE DO YOU AND LET HATERS DO THE HATE. HI HATERS BYE HATERS I SEEEEEEEEEE YOUUUUUUUUU


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s