BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MCHAGUE MISS GLOBAL PUBLISHERS 2008 July, 30, 2008

Filed under: Miss Tanzania,Sanaa/Maonyesho,Tanzania/Zanzibar,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:27 PM

Zimebaki siku chache tu kabla ya Tanzania kumpata mrembo wake wa mwaka huu (Miss Tanzania 2008). Wadau wa masuala ya urembo tayari wameshaanza kukuna vichwa wakijiuliza ni nani ataibuka mshindi mwaka huu. Mashindano ya Miss World mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 4 October huko jijini Kiev nchini Ukraine.

Sasa wakati tukisubiri kumjua atakayetuwakilisha mwaka huu huko Ukraine, kampuni ya Global Publishers,wanaendesha zoezi ambalo litakuwezesha wewe msomaji na mtembeleaji wa mitandao,kushiriki katika zoezi la kumpata Miss Global Publishers miongoni mwa warembo wanaoshiriki Miss Tanzania mwaka huu.Utakachokuwa unachagua sio Miss Tanzania bali ni Miss Global Publishers.Utakuwa unamchagua mrembo ambaye unadhani ndio mwenye mvuto wa sura kupita wenzake wote.Mshindi wa taji hilo la Miss Global Publishers atajinyakulia taji na pia kitita cha Tshs 500,000. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kupiga kura tembelea tovuti ya Global Publishers kwa kubonyeza hapa. Zoezi hili limepewa baraka na Kamati ya Miss Tanzania.Pichani ni warembo wanaowania taji la Miss Tanzania 2008.

Advertisements
 

32 Responses to “MCHAGUE MISS GLOBAL PUBLISHERS 2008”

 1. Pearl Says:

  mi mwenzenu naona hawa mamiss kama vile baadhi yao ni wafupi.

 2. Matty Says:

  I need to vote, lakini sasa BC hujatuwekea picha zao kwa ukaribu zaidi tukawaona vizuri…pls anayejua wapi naweza kuwaona vizuri zaidi ya kwa father kidevu naomba nijulishwe ili nitimize haki yangu ya kimsingi na kikatiba!nimejaribu global publishers naona majina tu without sura zao sasa imeniwia vigumu kuchagua kwakweli.

  Pia nimesikia kocha wetu wa Taifa stars MAXIMO amechaguliwa kuwa mmoja wa majaji wa hili shindano sasa hapo sijui nisemeje maana daaaaa!! E.ndaki unasemaje hapo sasa???

 3. ninamkali Says:

  naona bora uyo mwenye kibrauzi cheusi alowacha mdomo wazi naona ni mzuri kuliko wote

 4. Chala Says:

  queen anafaa pia mwenye orange alochuchumaa, kisha nafuata , huyo mwenye top nyeusi na kitagomago (kishort)cha jeans huyo kama nashangaa hivi…

 5. salome Says:

  mim naona huyo mwenye top nyeusi ambaye anashangaa ndo anafaa kuwa miss

 6. sara Says:

  Am very sure that nelly kamwelu will win. wa pili kutoka kushoto kwa hao waliosimama huyo mwenye TOP nyeupe

 7. sara Says:

  mimi naona huyo mwenye top nyeupe wapili kutoka kushoto ndo anafaa kuwa miss ,coz anavigezo vyote

 8. sada Says:

  mim binafsi nampendekeza engel ingwa haonekani hapo kwenye picha anafaa kuwa mic

 9. kekue Says:

  Matty hujui km kuna timu ya mpira wa miguu ya wanawake may b anaweza kwenda kuona wenye vipaji vya uchezaji mpira wa miguu kule… hahahahahahahahahaaaaaaaa. Du jamani

 10. Gervas Says:

  Mmmh! labda safari hii Lundenga angebadili taste kidogo…yaani apeleke miss mwenye wowowo afu anavigimbi mguuni, maana ataonekana japo “unique”

 11. jonas Says:

  kweli dada zetu mvuto mnao ,je vigezo vipi isiwe mnadanganywa na vioo vya cm 4 hebu liangalieni hili

 12. Pearl Says:

  BC sasa hizo kura ndo tunapigaje!!!!????

 13. trii Says:

  sawa tumewaona lkn siku zote miss ana toka Dar,naomba ufafanuzi.

 14. Matty Says:

  Hhahahahahahahahahahahah we Kekuu MAXIMO natafuta wachezaji haswa nakubali watakaoshindwa wakajiunge na Taifa stars.
  Gervas na wewe ushasikia wapi miss ana wowowo??? na vigimbi tehtetetetetetetetetet!! labda miss bantu!!miss anatakiwa awe na kawowo ka kishkaji na miguu ya bia kiaina si sana na mvuto-uzuri unaoonekana mengine chini ya kapert.umenipata?

  Hivi huyo mnaemuongelea Nelly kumwelu mbona kama mhindi ???? au mamcho yangu???

  PLs pls mwaka huu msifanye kosa ohhhhh tutabaki na labda kila mwaka ukiondoa mwaka wa Nancy Sumary!

  Pearl ni kweli kabisa kimo cha wengi hapo naona ni warefu kuelekea chini though siyo sababu, mimi ningekuwa jaji ningewapa ushindi kama ifuatavyo japo siwaoni vizuri.
  1.aliyelala chini nadhani no.8kiunoni simjui jina
  2.mrembo no. 20 kiunoni
  3.mwenye top ya njano na trouser ya light blue
  4.anayeshangaa na top nyeusi
  5.binti wa kitanga mwenye top ya maroon na maroon shoes na kipedo cheupe

  Habari ndo hiyo!

 15. solange Says:

  kwlei hako kenye kitop cheusi kana mvuto, sijui ndio Fay huyo., mie namtabiria sana Fay nadhani hata miss TZ yenyewe ndio muwakilishi.

 16. zubedacelena Says:

  uyo aloachama mdomo ni mzuri kwa mvuto

 17. semwa Says:

  mimi naona huyo mwenye top nyeusi anafaa kuwa mic ila hao wenzangu na miye tubaki nyumbani kuwa mamaic mtaa tu hapo tutashinda,kidogo labla huyo anaye shangaa ,kila la kheri mamic wetu waTZ

 18. simon Says:

  jamani mimi nina swali mbona engel hatuoni picha yake huo ni uonevu au mtotonmzuri kama yule mnaficha kwanini ?co vizuri ,ila yote sawa kikubwa kushida co kuonekana kwenye internet namtakia engel mafanikio makubwa pamoja na hayo yote AMEN

 19. Edwin Ndaki Says:

  Matty sasa mbona hujatuambia tukupigie kura?

  maana nakuona kwenye huo mstari umepozi kiBC…lol..

  jamani nawaomba wadau wote kura tumpigie matty.yeye kati ya hao warembo ni huyo dada mnayemuona kavaa nanii ya nanii…

  Safari hii Maximo kaitwa kuwa Judge mwakani watamchukua Afande mstaafu mh Afred Tibaigana…aa aaaa

 20. Gervas Says:

  Mmmh, Haya Matty !! ngoja niwaaachie wenyewe bwana, Kwa ufupi tu warembo tunao tena wengi sana, ila tatizo huwa linakuja pale kwenye vigezo vingine ziada na urembo. Inabidi uandaaji uanzie kuleee Primary school au sec, na sio tu miezi sita hii ya kujipaka poda na gwaride la miondoko bagamoyo.

 21. binti-mzuri Says:

  ivi jamani queen gupta nae anashiriki u-miss tZ!!!- am shocked..goodluck. alieachia mdomo wazi ana kajiumbo kazuri,angalau huyo

 22. truthfulness Says:

  mwenye top ya pinki na viatu vya pinki

 23. sinzia Says:

  huyo aliyesemwa zaidi na wadau hapo juu kuwa anakitop cheusi na amewacha mdomo wazi ni FAY ANTONY.
  Namimi namfagilia kuwa ana mvuto zaidi ya wenzake.

 24. pandu Says:

  Ushauri kwa waandaaji wa Miss Tz…haya ni mashindano ya 15 ya kumtafuta mwakilishi wetu kwenye mashindano ya mrembo wa dunia. Kadri siku zinavyoenda mi nadhani waandaaji mnabuni njia za kuongeza kipato na si kuboresha mashindano, nachelea kusema ivyo coz hawa mabinti ni wazuri but hawana vigezo vyote vya urembo, kwa mfano angalia urefu wa hawa mabinti ambae anazidi ft 5 hawazidi 3ambao kwa mtazamo wangu kuingia tano bora itakuwa mbinde…kuna watoto wa ilala kina wapo bomba kinoma lkn wafupi, ivi Unc Hashim unategemea nini kupeleka washindani kama hawa?? ni ndoto kupata nafasi tuliyoipata kwa Nancy kwa machaguzi yasiyo makini kama haya.
  Nilikushauri upunguze wigo wa kutafuta warembo, mikoa michache uruhusiwe kufanya mashindano ya vitongoji na wilaya, mikoa mingine kama pwani, moro, dodoma, ruvuma nk ifanye mashindano ya mkoa tu…na kuwe na vigezo kama walivyofanya Tanzani Beauty Agency kumtafuta kisura wa Tanzania kabla ya kufika kilele cha fainali. Tunataka mashindano yenye tija siyo kila siku mnafanya maandalizi ya zimamoto huku mkiweka viingilio kwa mtazamo wa kimaslahi zaidi wakati mashindano yanadhaminiwa 100%.
  Kwa mwenendo huu kuna kipindi Tanzania hii wasichana kuanzia miaka 16 na kuendelea wote watakuwa mamiss, kama nimekosea niambie, miss utalii, universe, miss lundenga nk. Najua kabisa wandaaji wa mashindano ya vitongoji wanalipa ada kubwa ambayo inawanufaisha but si lengo, warembo hawana vigezo jamani.

 25. hanny Says:

  mamiss wako poa sana majaji kazi mnayo

 26. Finah Says:

  Mmmh, huyo aliyeshangaa ndio anafaa kuwa miss global publisher na kuwa miss tanzania ni mzuri kama Nancy sumary acha nimpe sifa yake kapendeza sana!!! all the best (uliyeshanga )

 27. Matty Says:

  Hahahahahahahahaha!Jamani nimecheka sana E.NDAKI nilisha kuwa mrembo wa mkoa fulani chini ya carpet zamani na bado ninadai,hao pichanì hawanipati kwa uzuri,hivyo mimi ni kisura ninaejitambua!!

 28. babe Says:

  aliyefagiliwa na wengi ndo alishika nafasi ya tano

 29. binti-mzuri Says:

  matty kumbe wewe ulikua miss i-come-to bukoba… kama nakukumbuka vileeee.. hahaha iwe bojoo

 30. binti-mzuri Says:

  hapo alieshinda ndio huyo mwenye skinny jeans ya blue na kitop cha yellow..kazi mnayo

 31. Matty Says:

  iwe Binti-mzuri unasemaje sasa? ndio nilikuwa mrembo na hata sasa bado mimi ni mrembo tu!!

 32. eric Says:

  mi naona kama wa pili kulia kutoka usawa wa mnazi mwenye cjui kijishati cheusi anafaa somehow


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s