BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JAMHURI JAZZ BAND-SHINGO YA UPANGA July, 31, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:43 PM

Haya tena,mwisho wa wiki ndio umeshawadia.Kama kawaida ya dunia na ubinadamu,imekuwa ni wiki nyingine yenye pilikapilika za aina yake.Pilikapilika za maisha wakati mwingine hufanya nijiulize swali moja;Hivi ilikuwa ni nia na dhumuni la muumba kwamba dunia au wanadamu tuwe na mahangaiko namna hii au sisi wenyewe tu ndio tume-complicate mambo?Kama jibu ni ndio,basi kwanini tusimpigie goti muumba na kumuomba atuonyeshe njia na kuweka mambo yawe “tambarare” kama ambavyo pengine alikusudia?Haiwezekani au?

Anyway,kwetu sisi hapa BC ni muda mwingine wa kupata burudani. Burudani kama hizi huwa zinasaidia sio tu kwa kuburudisha bali kukumbusha jinsi enzi hizo zilivyokuwa.Yumkini ukijua ulikotoka au ukikumbushwa ulikotoka basi unaweza kupata unafuu wa kupanga uelekee wapi.Shukrani kwenu wote ambao mmekuwa mkituandikia na kutuambia ni jinsi gani burudani hizi za ijumaa huifanya wikiendi iwe nzuri.Kwa bahati mbaya kuna wakati tunaweza kuweka kibao ambacho kinaweza kukumbusha mtu au watu wako ambao walishaaga dunia.Hilo linapotokea ,jua kwamba huwa sio kusudio letu.Pamoja na hayo matakwa na Muumba hatuwezi kuyapindisha kwa hiyo cha muhimu huwa ni kumshukuru tu kwa kila kitu.

Basi leo baada ya kuzunguka kidogo barani Afrika tumeona turejee nyumbani.Wimbo unaitwa Shingo Ya Upanga kutoka kwao Jamhuri Jazz Band. Jamhuri Jazz Band ni bendi iliyoanzia mkoani Tanga(picha ni mandhari kidogo kutoka Tanga) miaka ya 1950s.Ni miongoni mwa bendi zilizowahi kutamba sana enzi hizo.Baadhi ya majina makubwa ya muziki waliowahi kutamba na bendi hiyo ni Wilson Kinyonga na George Kinyonga.Kuna haja kweli ya kuishi bila huyo mwenye Shingo ya Upanga?Pata burudani.Wikiendi Njema.

Advertisements
 

17 Responses to “JAMHURI JAZZ BAND-SHINGO YA UPANGA”

 1. EDWARD ALEX MKWELELE Says:

  NAUKUMBUKA SANA WIMBO HUU WAKATI HUO NILIKUWA MDOGO SANA MIAKA YA LATE 60’s TO 70’s, AND 80’s UKIPIGWA KARIBU NA SAA SITA HIVI AKILI YOTE INAKUWA KWENYE UGALI NA MAHARAGE YA NAZI NA UNAJUWA BABA YUKO NJIANI TOKA KAZINI KUJA KULA, MZEE WANGU ALIKUWA DAKTARI, ALIKUWA ANARUDI NYUMBANI KULA CHAKULA CHA MCHANA NA KULALA KIDOGO KISHA ANAENDA KAZINI TENA, BAND ZA ZAMANI NI BANA KWELI, I MISS THOSE TIMES MAN.

 2. EDWARD ALEX MKWELELE Says:

  Umeanza na topic nzuri sana hapo juu kwa kweli hata mimi huwa najiuliza kwa nini hali imezidi kurudi nyuma na kuwa mbaya zaidi badala ya kwenda mbele, kwani huwezi kuamini kuwa hapo zamani LINDI ilikuwa LINDI kweli, mji wa LINDI ulikuwa na lami barabara zote, taa za umeme mji mzima na za barabarani, maji ya bomba mitaa yote, kulikuwa na majumba ya cinema zaidi ya moja, majumba ya starehe for weekend dansi, kulikuwa na band ya muziki, maduka kibao ya wahindi, ni kati ya mikoa iliyokuwa na uwanja wa mpira uliojengwa kwa matofali na part kuwa na viti/jukwaa la kukaa watu, kulikuwa na bandari, ndipo makao makuu ya jimbo la kusini kuanzia KILWA, LINDI, MTWARA NA RUVUMA mkuu wa jimbo wa kizungu akikaa LINDI, ndege za aina mbili zilikuwa zinakuja, ndege za kutua majini na uwanja wa ndege, watu wakichoma mahindi kwenye streets chini nguzo ya taa usiku yaani ni burudani moja kwa moja, kulikuwa kuna timu tatu za mpira mashuhuri sana zenye umri sawa na SIMBA na YANGA na zilikuwa zinaitwa SANDERLAND NA YOUNG AFRICAN na BEACH BOYS, MAISHA YALIKUWA TAMBARARE SANA, SIKU HIZI MJI NI MCHAFU, BARABARA ZOTE VUMBI TUPU, MAJI SHIDA, NDUGU ZETU WA ASILI YA KIASIA KARIBU WOTE WAMEKIMBIA, YAANI TAABU MOJA KWA MOJA, HALI NI MBAYA, EBU KAMA NYINYI WA BC MNAWEZA KWENDA LINDI NA KUMPATA MZEE WA ZAMANI AKASIMULIYA HAYA, PATENI MZEE WA MIAKA 70 NA KUENDELA ATAKUELEZeni LINDI NI NINI, IT WAS AT PAR WITH EVEN DAR ES SALAAM AT THAT TIME.

 3. wabusara Says:

  Ni ijumaa BC lazima watese nafsi zetu.
  Jambo moja naweza kusema ni kuwa BC wanajaribu kuonyesha tofauti za vionjo vya kale na vya kisasa.Lakini hawa akina mwinjuma,Ali choki hivi hawaoni kuwa wanapiga kelele na sio muziki.Nathibitisha kauli yangu kwa kuwaomba wale wenye headphone au mziki mnene wasikilize ili wajionee namna kila chombo kinavyosikika na kina wakati wake,sio saxphone,keyboard,bass,solo na tumba vinaingiliana.Huwezi hata kuweka step uki dance.
  Huu ugonjwa wa muziki wa kizaire wa kubong’oa umetuharibia sana muziki wetu.
  Sikiliza Mbaraka,Jamhuri jazzy,tabora jazz,marehemu balisidya na Afro 70, akina marijani halafu ufananishe na hawa wa siku hizi.Hapa sina maana ya bongo fleva kwasababu bongo fleva inajitambulisha na kujitegemea,tena hata bongo fleva ni bora kuliko muziki wa dansi wa sasa.
  Tunawezatofatiana kimawazo lakini haya ndiyo yangu.

  BC keep it up!

 4. BC,KWA NIHABA YA SISI WAKAAJI WA KISANGANI,BUKAVU NA LUBUMBASHI DRCONGO SHUKRANI,HII REKODI SHINGO LA UPANGA YA JAMHURI JAZZ NA DADA ASHA YA TABORA JAZZ ZILIPENDWA SANA HAPA KONGO YA MASHARIKI KATIKA ENZI HIZO.ENDELEENI KUTUKUMBUSHA NA NYIMBO ZA MOROGORO JAZZ,TABORA JAZZ,WESTERN JAZZ,SIMBA WANYIKA,N.K…
  TULIKUA TUKISEMA HIVI; LA MUSIQUE TANZANIENNE A DES MESSAGES YAANI”MUZIKI WA KITANZANIA UNA MESEJI” AHSANTE AO AKSANTI(KONGO SWAHILI),MERCI BC.

 5. Edwin Ndaki Says:

  BC asante sana ijumaa ijyoo nyingine imewasili.

  Kwanza nawapa pole watu wote wenye misimamo dhabiti katika kudai na kutetea haki za wanyonge…RIP Mh Chacha Wangwe.

  Pole ndugu jamaa na marafiki.

  Poleni mliondokewa na ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi”albino”Poleni na mungu awatie nguvu wengine wanaoishi kwa hofu ya kuja kufanya ukatili ma mafedhuli.Washindwe na walegee.

  Pongezi wadau wote mnao pita kila siku hapa BC kuacha maoni au kusoma na kusepa.Mnamchango mkubwa sana.

  BC baada ya kusikikiliza huo wimbo na hiyo picha ya TANGA mmenikumbusha mbali sana.

  Waja leo waondoka leo…

  Ngoja nijikumbushe baadhi ya maeneo ya TANGA.

  Mjengoni kwa baba Tarimo(Eckernforde),majani mapana,mikanjinu,barabara 21,sahare,bombo,makorora,mabawa…du tanga tamu…

  ukia maeneo ya mkwakani chips kwa kaka Yohane..huku ukishushia anjari..eltho..

  Mambo ya NGOMA BAIKOKO……

  Swaiba wangu Matty ijumaa njema kama kawa tuonane Kwa DAN darajani..ze mfugos…

  Gervas nitakukuta kwa mama abel mwambie kama kawa…

  Dinah..upo mbona sikuoni siku hizi..

  pamoja

 6. Dunda Golden Says:

  HOME SICK
  ENZI IZO KUPATA DEMU MBINDE HATA UKIWA NA MASHAILI YA KUMTOA NYOKA PANGONI WAPI MUNGU HATUKUZWE NA MAMBO YALIKUWA TAMBARALEEEE,,,,,LAKINI ENZI HIZI ZETU NOMAAA USIPIME HATARI,MWIMBO UMENIKUMBUSHA MBALI SANA ENZI ZA KOMBOLA ALFAJIR WAKATI TUNATOKA SWALAT LFAJIR NA KUJIANDAA KWENDA SHULE KAMA KM 20 KWA MIGUU
  WANA WA BC,NDAKI.BINTI-MZURI,PEARL, GERVAS,MATTY,MKWAYA,ANY NA WENGI WENGINEO PAMOJA NA TIMU NZIMA BC JEFFY NAWATAKIA WEEK END NJEMA,,BILA KUSAHA WALE WOTE WALIOGUSWA NA KIFO CHA RASTA CHACHA WANGWE POLENI KWANI HIYO NDIO HALI YA DUNIA
  PEACE PUNDE TUU UKWELI UTAJULIKANA MESSAGE SANT

 7. Kisu KIkali Says:

  Yahani wazee wa BC! leo mnifanya nizaliwe umpya!
  wimbo huu uninkumbusha wakati nilipokuwa mdogo na tanzania hilipokuwa Tanzania mshahara wa wazee wetu
  labda kuanzia sh.35/= hadi 180/= na wakati huo
  mtu alikuwa ana heshimiwa katika jamii!

  Na Tanzania ndipo palikuwa chemu chemu ya Burudani
  Kuanzia Dar hadi kwa wagosi Tanga,Morogoro mjini Kasoro
  Bahari hadi Ujiji Kigoma,Visiwani Zenji(Unguja)utasikiliza Redio ya ZNZ ikitangaza kuwa POCHI NDANI LINA FEDHA
  limeokotwa! mwenye ahende kuchukua kituo cha radio!

  Mziki wenyewe ulifuatana na maisha ya watanzania tena wa
  namziki hawakuwa na kipato kikubwa lakini kazi yao walihifanya kwa uwadilifu na kujiamini!!!!
  Mungu hali hile haipo tena au tuseme Tanzania hile imezikwa
  kaburini.mungu ilaze pema peponi!
  Tanzania ya Sasa hiliyochipua kama unyoga!Utamaduni umebadlika Unyago!Unaitwa Kitchen Paty!?
  Na Mazikoni watu wanaharifiwa kwa Kadi za mwaliko,na kwa
  Sale! usikurupuke tu kwa kusikia jirani kafa ukaenda bila
  Mwaliko! Hilo ni kosa la jinai!
  Kalale pema peponi Tanzania hile ya wakati ule. Amini

 8. Gervas Says:

  BC, Edward na Kapalata de Bukavu…kwa kweli mmenikumbusha mbaali sana, miaka ile Jamhuri walitikisa sana tulikuwa tunasakata dansi jasho mpaka linakauka, nakumbuka siku moja hadi sore ya kiatu changu (Laizoni) ilichomoka ikabaki misumari tu. Halafu pia kibao kama..”chaupele mpenzi” tulikuwa tunatumia enzi hizo gramaphone na ulanzi ukiwa mezani. Zimeenda wapi siku zile??

 9. marvin Says:

  yap inabidi watu wamrudie muumba wao aliyewaumba awape uelekeo. hiyo ni kweli kabisaa nakuunga mkono.

 10. EDWARD ALEX MKWELELE Says:

  KAPALATA de BUKAVU, nyimbo za bendi zote ulizozitaja hapo juu unaweza kuzipata na kuzisikiliza katika website ya YOU TUBE, TUMIA google.com serach enginekutafuta you tube website yaani http://www.you tube.com na huku type jina la bendi yoyote au kama bado unakumbuka title ya wimbo wowote ule, utapata iko kibao, hasa SIMBA WANYIKA NI TELE TU KWA FUJO. BYE START ENJOYING THEM.

 11. AKSANTI EDWARD ALEX, YOUTUBE NIMESIKIA NA KUONA BY CLIP ZA BENDI ZOTE,WATANZANIA WENGI HAWAJUI KUWA KONGO KISWAHILI NDIO LUGHA MAJORITI,MIKOA 5 YA DRCONGO NI SWAHILIPHONE (LUNGWANA) VIRUNGA ORCH,MAQUIS ORIG,REMMY ONGALA,SUPER MAZEMBE,MANGELEPA,MAKASSY ORCH,SAFARI SOUND. PIA NI BENDI ZILIPENDWA SANA HAPA KONGO YA EAST. UNAJUA KAMA PATRICE LUMUMBA ALIKUA AKISEMA KISWAHILI YA SARUFI?

 12. Matty Says:

  Thanx BC kwa hicho kibao.E.NDAKI na DUNDA GALDEN asante kwa salamu.Kwa ujumla wknd hii imekuja viseversa to me najikuta nauguliwa na mtoto wangu kipenzi…kila kitu ni mpango wa mungu na ninamuomba amponye!!

 13. Gervas Says:

  Edwin, Bc amepiga Arua nini akasahau kurudi? maana haja-tupa update wadau wa room hii. Nakumbuka niliwaona pale kwenu darajani na Matty na BC mkitafuna raha. Dunda weekendi inogile kwa kweli, naona wadanganyika taayari wameshaanza kusahau issue ya ufisadi sijui ndo imetoka hiyo. Maisha yetu bongo nikama kitabu tu ukishafungua page basi ya nyuma unaishau. Ilikuwa Richmondi, page iliyofauata EPA, Meremeta, Balali, Zanzibar sio nchi bali ni bara, sasa tupo page ya utata wa ajali ya Wangwe, siku zinaenda, sijui next page ya kitabu chetu ni ipi

 14. Edwin Ndaki Says:

  BC habari za j3.

  vipi timu nzima mmeenda ‘vakesheni’ maana tangu mlipotuachi hii shingo ya upanga hatujawaona tena.

  Chonde chode mengi yamejiri mwisho wa juma ikiwemo mambo ya ulimwende na mustakabali wa taifa letu

  Tunawasubiri siku njema

 15. Pearl Says:

  Dunda Galden nimekupata fresh kabisa na salaam za weekend,thanx.
  wana BC wote mi nawatakia weekend njema.

 16. binti-mzuri Says:

  ebwana ndio…tanga ndio yenyewe!

  bc tuwekee basi picha za mamissi tusafishe macho

 17. pyupyu Says:

  Hello there,

  BC upo mbona kimya hivyo,tupe mambo.

  Pole kwa majukumu ya kila siku.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s