BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UNAWAKUMBUKA HAWA?WAKO WAPI? August, 31, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 10:19 PM

 

WHEN THE SMITHS MET THE KARUMES August, 30, 2008

Filed under: Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 11:54 AM

 

DAWA YA MAPENZI-MBARAKA MWINSHEHE August, 28, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 11:55 PM

Natumaini kwamba u-mzima na tayari kabisa kuukabili mwisho wa wiki.Kwa upande wetu sisi hapa BC,tupo tayari kabisa hususani baada ya kushuhudia historia mpya kwa mtu mweusi Barack Obama kuchaguliwa rasmi kuwa mgombea wa Chama cha Democrat nchini Marekani.Yawezekana Obama asije kuwa chochote wala lolote jipya kwa Afrika au ulimwengu lakini kwa namna yoyote ile,if you are black you gotta be proud of him and actually give him the credits he deserves.Zaidi ya hapo utaonekana mpika “majungu”.Au?

Turudi kwenye shughuli yetu ya Ijumaa.Burudani.Hivi dawa ya mapenzi ni nini?Swali hili,hata baada ya miaka chungu nzima ya wajuzi kujaribu kulipatia majibu,bado linaendelea kuulizwa mpaka leo.Sababu?Mapenzi yangalipo na yataendelea kuwepo.Bado mapenzi yanaua,yanatesa,yanafurahisha,yanatia wazimu na wengine wanasema ndio chanzo cha kila vita iliyopo duniani.Sina uhakika na hilo.Nasikia tu.

Lakini je,unaweza kukubali kwamba kwa “karumanzila” kunaweza kupatikana dawa ya mapenzi?Si ushawahi kusikia hadithi za “limbwata” nk?Inawezekana kweli ukalipata penzi chini ya mkeka?Msikilize Hayati Mbaraka Mwinshehe akiimba kuhusu Dawa ya Mapenzi katika wimbo huu.Wikiendi Njema.

Pichani ni Mbaraka Mwinshehe na mkewe Amney Shadad siku ya ndoa yao tarehe 17/3/1972 huko mjini Morogoro.

 

KATUNI ZA KIPANYA KWENYE MAONYESHO BERLIN

Filed under: Sanaa/Maonyesho,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 6:47 AM

Kama unaishi jijini Berlin huko nchini Ujerumani,basi leo utaweza kuona faraja pale utakapoona katuni ya KP au Kipanya(uchoraji wa Ali Masoud-pichani) itakapokuwa inaoneshwa katika njia za treni za jiji hilo(Berlin Subway System.

Kipanya inashiriki katika maonyesho ambayo yamepewa jina la Underground Exhibition ambayo yamekuwa yakiendelea jijini humo tangu tarehe 19 August 2008 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 1 September 2008.

Masoud anaungana na cartoonist wengine maarufu duniani ambao kazi zao zimo katika maonyesho hayo kama ambavyo unaweza kuona katika ratiba hii hapo chini.Tafadhali kama upo jijini Berlin itazame leo cartoon ya KP na kama inawezekana tuletee japo picha.

19/08/08 “Podium” by William Medeiros (Brazil)

21/08/08 “Auf die Plätze” by Christiane Pfohlmann (Germany)

23/08/08 “Made in China” by Herr Schewe (Germany)

24/08/08 “Skyrocketing Fuel Prices” by Prince M. Dhanta (India)

25/08/08 “Erster” by Freimut Wössner (Germany)

26/08/08 “Home Sweet Home” by Junior Lopes (Brazil)

28/08/08 “Dying” by Ali Masoud (Tanzania)

30/08/08 “Du bist Berlin” by Andreas Prüstel (Germany)

31/08/08 “Vulture Oil” by Mark Lynch (Australia)

01/09/08 “Trouble” by Pawel Kuczynski (Poland)

 

NZELA-B BAND August, 27, 2008

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 11:14 PM

Tumekuwa tukipokea maombi mengi kutoka kwa baadhi yenu wasomaji kuhusu wimbo wa B-Band inayoongozwa na B-Band.Katika kuitikia maombi hayo,hiyo hapo chini ni video ya wimbo Nzela kutoka kwao B-Band.Swali la kizushi kwa B-Band;kwani mpiga debe si mtu au hastahili penzi?Au?

Hata hivyo hongera sana kwa wana B-Band na wote walioshiriki kwenye wimbo huu.Umetulia.

 

JENNIFER MGENDI August, 26, 2008

Filed under: Dini,Muziki — bongocelebrity @ 9:10 PM

Ushasikia kwamba muziki wa gospel(injili) siku hizi unatamba sana nchini Tanzania.Mmojawapo ya wasanii wa muziki huo wa injili wanaotamba ni Jennifer Mgendi(pichani).Mbali na kuwa muimbaji wa nyimbo za injili, Jennifer pia ni mtunzi mzuri wa hadithi za filamu.Baadhi ya filamu alizowahi kutunga ni kama ile ya Pigo la Faraja na Joto la Roho.

Mgendi alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 1995 na albam yake ya kwanza iliitwa ‘Nini?’. Baada ya hapo alitoka tena na albamu zake zilizokwenda kwa majina ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu Nakupenda’,’Nikiona Fahari’ na ya hivi karibuni zaidi inayoitwa Mchimba Mashimo.

Photo/Global Publishers

 

WILL AND JADA IN TANZANIA

Filed under: Filamu/Movie,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 3:24 PM

Siku hizi inaelekea Tanzania inakuwa ndio chaguo la superstars wengi kutoka Marekani linapokuja suala la kupumzika au kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ingawa wengi bado wanapenda kuingia na kutoka kimya kimya pengine kwa kuogopa “paparazzi wa kibongo”

Kuthibitisha hayo hivi leo waigizaji mashuhuri kutoka nchini Marekani,Will Smith na mkewe Jada Pinkett(si unawaona pichani?), leo hii wameonekana jijini Dar-es-salaam wakiwa wanatoka ndani ya The Kilimanjaro Hotel Kempinski tayari kuelekea visiwani Zanzibar.Kabla ya hapo Willy na Jada walikuwa wametoka Bagamayo mkoani Pwani ambapo walitoa msaada wa vyandarua katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo.

Shukrani Jiachie kwa picha hii.

 

WHEN WE REMEMBER COMPLEX August, 25, 2008

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 11:25 PM

Hivi majuzi pale katika ukumbi wa Afri Centre,Ilala jijini Dar-es-salaam palifanyika tukio la kumkumbuka aliyewahi kuwa miongoni mwa wasanii na producer mahiri wa Bongo Flava/Hip Hop,Marehemu Saimaon Sayi au maarufu kwa jina la Complex. Complex alifariki dunia August mwaka 2005 kwa ajali ya gari.Katika ajali hiyo alifariki pia rafiki yake Vivian Tilya aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM.

Pichani kutoka kushoto ni mtangazaji wa Clouds FM,B-12,msanii A.Y na Prof.Jay wakiwa wameshikilia mishumaa kama kumbukumbu ya kifo cha Complex.Tukio hilo liliitwa Remember August.R.I.P Complex and Vivian Tilya.

Photos/Abdallah Mrisho


 

LATOYA NDIYE MWAKILISHI WA TZ BIG BROTHER AFRICA August, 24, 2008

Filed under: Bongo Reality TV,Television — bongocelebrity @ 3:21 PM

Kama tulivyoahidi,huyu hapa ndio mwakilishi wetu huko South Africa katika shindano la Big Brother Africa III. Jina lake anaitwa Latoya.Ana miaka 21.Ni Katibu Muhtasi.Ukitaka kuwaona washiriki wenzake bonyeza hapa.

 

MRITHI WA RICHARD KUANZA KUSAKWA LEO

Filed under: Bongo Reality TV,Television — bongocelebrity @ 1:43 PM

Lile shindano maarufu lijulikanalo kama Big Brother Africa linaloendeshwa na kituo maarufu cha televisheni cha Afrika Kusini(M-Net) linaanza tena leo nchini Afrika Kusini huu ukiwa ni msimu wa tatu tangu kuanzishwa kwake.

Jumla ya washiriki 12 wataingia leo kuanzia saa moja jioni tayari kuishi ndani ya jumba la Big Brother kwa siku 91 huku kila wanachokifanya kikirekodiwa kwenye kamera.Mshindi anatarajiwa kupata dola za kimarekani laki moja.

Kama mtakumbuka mshindi wa mwaka shindano lililopita alikuwa Richard Bezuidenhout (pichani) kutoka Tanzania.Majina au sura za washiriki wa mwaka huu bado ni siri ya waandaji na watajulikana pindi shindano litakapokwenda “live”.Pamoja na siri iliyopo kuna habari kwamba safari hii Tanzania inawakilishwa na msichana.Nani atamrithi Richard? Mwakilishi wa Tanzania ni nani?Tutawapasha punde.