BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

RUFAA YA KIFO-MARIJANI RAJABU August, 7, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:59 PM

Mwisho wa wiki mwingine umewadia.Siku zinazidi kuyoyoma.Mwaka 2008 unazidi kuelekea ukingoni.Ni wakati mwingine wa kufurahi na pia kutafakari mambo mbalimbali na jinsi wiki ilivyokwenda.Kwa jinsi maisha yalivyo,mwisho wa wiki unapowadia kila mtu ana mipango yake na kila mtu ana lake la kusimulia.Leo ikiwa nzuri kwako sio lazima iwe hivyo hivyo kwa mwenzako,jirani yako nk.

Kwa bahati mbaya wiki hizi mbili zilizopita(kiujumla) zimetawaliwa na habari za misiba.Imetokea ile ya watu maarufu ambao wote tumeisikia na pia ile iliyotokana na ajali mbaya za barabarani.Wengine wamepoteza ndugu,jamaa na marafiki kutokana na maradhi wakiwa majumbani au mahospitalini. Ili mradi tu anga zimekumbwa na misiba.Pamoja na kwamba hali kama hizo ndizo zinazokamilisha mkataba wa “ubinadamu”,kumpoteza ndugu,jamaa au rafiki siku zote huwa ni kitu kigumu sana.Imekuwa pia wiki ya kukumbuka mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika majiji ya Dar-es-salaam na Nairobi miaka kumi iliyopita ambapo watu wengi wasio na hatia walipoteza maisha.

Wakati nikifikiria kibao gani nitakachoweza kupiga hivi leo ili kiendane na hali halisi,mawazo yangu yalishindwa kuondoka kwenye kibao kiitwacho Rufaa ya Kifo kutoka kwake Hayati Marijani Rajabu.Ni wimbo ambao natumaini utawaliwaza wote walioondokewa na ndugu,jamaa au rafiki na wakati huo huo kutukumbusha sisi wengine jinsi gani tuutumie muda wetu na wenzetu kwani pindi wanapoondoka,hakuna muda wala uwezekano wa kukata rufaa.

BC inawapa pole watu wote waliofiwa na ndugu,jamaa na marafiki popote pale walipo.Tunawatakia weekend njema.

Advertisements
 

14 Responses to “RUFAA YA KIFO-MARIJANI RAJABU”

 1. Neema Says:

  Nimevumilia kwa muda lakini leo naomba niseme.Kwa kweli sijaona katika blog za kitanzania blog ambayo iko makini kama hii ya BC.Kwa kweli mko makini vijana na mnajua nini mnafanya.Hongereni sana na tafadhali endeleeni hivyo hivyo.Wiki hii imekuwa ngumu kwa watanzania wengi.Naungana na BC katika kutoa pole kwa wote waliofiwa.Mungu atawapa nguvu.

 2. Edwin Ndaki Says:

  Hakika Bc wiki ilikuwa na mushkeli mwingu.

  Matty mambo vipi?Tunakukosa sana rafiki,mtoto anaendeleaje?
  Tunamwombea Mungu amjalie apone haraka na wewe urejea kwenye BC yetu.Tunaku’miss’ Matty.

  Poleni wote mlipoteza ndugu,jamaa na marafiki.Najua kipindi ni kigumu kwenu ila Mungu yupo nanyi.Jipeni Moyo.

  Kwa wale ambao mwisho wa juma umewajia ukiwa na ‘ukata’ kama mimi basi msijali sio lazima kunywa “nyagi” basi unaweza kustua japo “maji”.

  Marijani nyimbo zake zote kali.

  Bc …naomba mnitafutie wimbo wowote wa washirika stars aka watu njatanjata enzi zile wakiwa na Komandoo hamza kalala,Eddy ‘sheggy’ Christian Sheggy safu ya uimbaji.

  Nawakumbuka wakina AbduSALVODO aka Father kidevu akipapasa kinanda.Nakumba vibao kama Julie n.k

 3. kindo Says:

  Naungana na Neema hapo juu. Kwa kweli nasifu umakini wa BC hasa katika utafiti na kuandika mambo ynayoendana na msimu bila kukurupuka. Congratulations and God bless you.

 4. Mama wa Kichagga Says:

  BC

  Kweli mnajua kumtupia kuku mahindi wingie ndani ili akamatwe achinjwe! Haaaa maana mie ikifika Alhamisi jioni naanza kupawazia hapa kwa hamu ya mwimbo wa Ijumaa! Asanteni sana.

  Huu mwimbo unanipa huzuni sana! Kama kweli kifo kingekatiwa rufaa basi ningewakatia wapendwa wangu wote ili warudi! Yaani ningehakikisha Nyerere anashinda rufaa arudi angalau nimnunulie shati kumshukuru kwa kazi yake nzuri ktk elimu kwani ingekuwa sasa hivi mmmmmmmm sijui hata kama ningeweza kusoma hapa.

  R.I.P. wote waliotutangulia mbele ya haki.

  Kazi ya Mungu haina makosa.

 5. binti-mzuri Says:

  😀

 6. MapigoSaba Says:

  Leo nimekumbuka mbali kidogo, sauti ya miziki yote ya kipindi hicho zimenijia. Pia kuna wimbo mmoja wa sikinde wenye mirindimo sawa na huu hapa, ulikuwa maarufu sana enzi hizo unaitwa “Selina piga moyo konde”.

 7. Gervas Says:

  Edwin, kama kawa mwalufoty weekend hii usikose maanake vibao kama hivi vya Marijani Rajab, hao watunjata njata vitacharazwa live na mzee mzima malibwa akiwa na squad yake yote ya kina mama Abel, palalaiza,Jenenge. BC Blog hii si mchezo bwana!!!

 8. Edwin Ndaki Says:

  Gervas kama utakuweo mwalufoty basi nitakuja.

  Ila itabidi nipitie kwanza mkendo kati ndio niende hadi kamnyonge then nije hapo mwalufoty.

  Nasikia leo mwana wa adamu atakuwepo yaani Balihele.Ila pia ua hatuwezi msahau mzee mzima Mtanzania na mzee keya.

  Ila kweli zilipendwa kweli tamu.

  Salaam nyingi Gervas mfikishie mwanasatu Fr Warwa..tii tiiii tii unakumbuka kiinglishi chake?Yuu jentromani..bi hambo..na kale kalafudhi ketu yaani namiss sana ng’wana satu

 9. Matty Says:

  Thanx Edwin Ndaki, lovely baby anaendelea vizuri!

  Jamani mimi ndo sina usemi ingewezekana kukata rufaa ya kifo kwa kweli ningeikata kwa gharama yoyote ile ili baba yangu mpendwa aendelee kuwepo lakini no way hakuna rufaa hapo! RIP kwa wote waliotangulia mbele ya haki!

  Hivi leo ni saturday tena jamani mbona siku zinakimbizana namna hii?

  kwa kweli BC mdumu sana.

  Haya nawatakia wknd njema BC na wapendwa wadau wote!

 10. Angelina Says:

  Huu wimbo umeniliza mno, asanteni sana BC.
  Rufaa ya kifo ingekuwepo, hiyo mahakama ingezidiwa na mawakili wangetengeneza mapesa kweli maana binafsi ningekata rufaa mara nyingi iwezekanavyo mpaka nishinde, nirudishiwe baby girl wangu…she was so cute…….lakini ndo hivyo tena, hakuna rufaa ya kifo.
  Rest in eternal peace “HOPE” my love.

 11. Edwin Ndaki Says:

  Pole sana Angelina,kazi ya Mungu haina makosa.Wewe ulimpenda na Mungu akampenda zaidi.Kikubwa ni kumbuka siku zote katika sala zako.May God rest her soul in peace.Amen

  Matty kweli inaumiza kuondokewa na mpendwa.Lakini bado tukumbuke sisi wote tu wasafari ..nasi ipo siku tutaiaga hii dunia.

  Mungu aiweke roho marehemu baba yako na wengine wote mahala pema.AMINA

 12. Matty Says:

  Thanx EDO, Pole sana Angelina MUNGU AKUPE UVUMILIVU!

 13. Mmali Anthony Says:

  BC na Issa Michuzi ndizo Blog pekee za kibongo ambazo naweza kusema zinanipa raha nikizisoma. Blog zingine zote zilizosalia ni wanna bees tu, haswa zile za vijana waliopo marekani. Maana mtu utataka kusoma habari za nyumbani unawekewa vitu vya marekani wakati wewe unaishi huko.

  Rufaa ya Kifo ni wimbo uliotungwa na Cosmas Thobias Chidumule kipindi yuko Dar Inter (1978). Miezi michache tu baada ya kurekodi huu wimbo, yeye (Cosmas), Michael Enock, pamoja na wanamuziki wengine waliondoka na kwenda kuunda Mlimani Park (Sikinde) chini ya usimamizi wake Michael Enock!

  Big up BC, leteni nyimbo za maana hatutaki mambo ya computer ama playback.

 14. Angelina Says:

  Asanteni sana Matty na Edwin, ni ngumu lakini sina jinsi nasonga mbele kiaina.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s