BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BALOZI WA REDDS ARUDISHA TAJI August, 9, 2008

Filed under: Blogs,Mahusiano/Jamii,Miss Tanzania,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:13 PM

BALOZI wa REDDS Angela Luballa(pichani) leo aliwashangaza watu alipoamua kurejesha taji hilo wiki moja tangu avalishwe.
Luballa ambaye pia alishika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema kuwa imani yake haimruhusu kuwa Balozi wa REDDS.
“Imani yangu kwa Yesu ni kubwa mno na hainiruhusu mimi kuwakilisha REDDS, hivyo nimeamua kurejesha taji na zawadi za fedha nilizopewa,” alisema Luballa.Tembelea blog ya Lukwangule kwa undani zaidi wa habari hii ambayo kwa vyovyote vile itazua mjadala.Kipi kinakubalika kwa Yesu na kipi hakikubaliki?Imani ni nini hasa?Je ni kweli hakuna shinikizo?Bonyeza hapa.

Advertisements
 

101 Responses to “BALOZI WA REDDS ARUDISHA TAJI”

 1. Gervas Says:

  Kwa haraka haraka tu naweza sema wazazi ndo wamemshinikiza labda baada ya kuangalia future yake. Wengi wao wadada wakishakuwa ma-miss shule tena ndo inakuwa ngumu au yakubabaisha, nafikiri watakuwa wamefocus mbali zaidi. Huu ubalozi sijui hata nini kazi yake maana naona mara nyingi wanakuwa kwenye shughuli tuu basi. Swala la imani inaweza ikawa tu ni kisingizio, kwani hiyo imani yake gani inayomruhusu kupita na bikini mbele ya kadamnasi afu imani hiyo hiyo imkataze kuiwakilisha kampuni hiyohiyo iliyomfadhili kuwa miss?

 2. Joyce Says:

  Huyo mtoto ana wazimu sasa kilichompeleka kushindania huo umiss ni nini??? kuvaa vichupi mbele za watu ndio dini yake inamruhusu???sasa angeshinda Miss Tanzania angerudisha hilo taji??? mashauzi mengine bwana.

 3. Vanessa Says:

  Masikini msichana mzuri hajasoma….duh!
  Så sad!!1

 4. Vanessa Says:

  Masikini msichana mzuri hajasoma….duh!
  Soo sad!!1

 5. Frateline Says:

  Hi Guys kutoka Helsinki-Finland,
  Kwanza nakupongeza dada kwa kujirudi na kutubu na kumrudia kristo, Bwana yesu asifiwe, ni kweli biblia imeweka wazi kabisa kuhusu kileo, ktk Habakuki biblia inasema—ole wake ampaye jirani yake kilevi—ukitaka waweza kusoma biblia mwenyewe, pia swala zima la urembo limejaa mambo mengi yasiyompendeza kristo, Dada kuna faida nyingi utapata kwa kukataa kutumiwa kama balozi wa pombe, maana REDDS ni pombe, naomba nikutajie tatu tu;
  1. Kama kweli jambo hilo limetoka moyoni basi faida ya kwanza utabarikiwa maana umemkiri kristo mbele ya ulimwengu ninajua washushi wengi watakuponda lakini usijali kupitia magazeti na lakini kimtindo Yesu utakuwa umemuhuri

  2. Faida nyingine utakuwa umepunguza vishawishi vya ngono maana ukiwa balozi wa pombe-REDDS, ungetakiwa kuwa sehemu mbali mbali na muajili wako wewe ni binti mdogo ni rahisi kunasa mtego wa wakwale wa bongo ukipata bahati ni mimba au ukimwi, ni risk sana kwa binti mdogo wa miaka 20 kutembea hovyo sehemu za starehe na mabaa kutangaza pombe, wakati huo huo ni unyonyaji wewe unatumiwa tu faida wanakula wengine (kasome- Gramsci-marxist classical alienation) unapoteza utu wako kwa ajili ya mabepari,

  3. Faida ya tatu ni shule, kwa sasa unaweza kusoma na kuconcentrate na shule au kazi- maana biblia inasema huwezi kutumikia mabwana wawili yaani huwezi kuwa balozi wa pombe halafu huku wewe mwanafunzi,

  Mwisho ninakushauri achana na wapambe uamuzi wako ni wa busara wewe ni binti mdogo sana, bado mbichi unadai hivyo unaweza kuja kuwa waziri mkuu wa Tanzania miaka ijayo achana na ujinga wa kutumia pombe sasa weka mipango kabambe ya kujiendeleza kielimu na pia mshike sana huyo Yesu wako asikuponyoke.

  Nukupongeza sana maana umejitambua, kuteleza sio kuanguka, hivyo kushiriki urembo ulieleza kidogo lakini bado haujaanguka. simama na Yesu, Aminaaaaaaaaaaa

 6. sikujua doto Says:

  Huku ndiko kuchangayikiwa kwa wabongo kutokana na hizi dini wasizojua chanzo chake wala mwisho wake!!!! Kama sababu ni Yesu, ni vyema huyu binti au hao waliomshinikiza kufanya hivyo wakasoma vyema biblia. Yesu alitengeneza mvinyo murua kuliko mvinyo wote ambao umewahi kutengenezwa hapa duniani tokea binadamu aanze kuishi kama binadamu!!!!!

 7. Bablee Says:

  Hongera sana Angela, waswahili wanasema kujikwaa sikuanguka, hatimae umesimama tena na na kumrudia mungu wako! Umeonesha ni msichana wa namna gani, sio wakuweka maslahi mbele utu nyuma, bali ni msichana wa shoka!
  Laiti wasichana wote Tz wangekuwa kama wewe au angalau nusu yako wewe, basi ukimwi na umalaya tz ungekwisha.
  Ni waschana wa chache sana waliotayari kuacha fedha na misifa yakipuuzi kama hiyo (Balozi redd) kwa ajili ya mungu wao au kulinda hadhi yao! Wangapi wanapiga picha za uchi kwa sababu ya shilingi 10 ya kitanzania? wangapi wanatangaza biashara za pombe kwa malipo duni chini ya sh laki 1 ya kitanzania? wangapi wanachezewa na mapedeshee kwa malipo ya sh elfu 20? wangapi wanapewa mimba na wanaojiita masuper star wa bongo kwa gharama za lift za kwenye vi corola? Wewe unajitambuwa thamani yako!

  Angela naamini pia unajutia kitendo chako cha kwenda kwenye jukwaa ukiwa nusu uchi na umetubu kwa hilo, Mungu wetu ni mungu warehema, yeye anasamehe hata kile ambacho binaadamu anahisi hatosamehewa!
  Amin nakwambia tangu saa hii ulipokiri makosa yako mbele za mungu aliye hai, mungu asiekosea wala asie shindwa na chochote basi umesamehewa dhambi zako zote!
  Mungu azidi kukutia nguvu katika wakati huu mgumu wakuandamwa na wanywa pombe kwa kebehi na dharau za kila aina. Mungu akuongoze katika malengo yako ya baadae!

  Viva Angela viva!

 8. kijiwe Says:

  kumradhi wadau habari za thiku mingi!
  kama imani haikuruhusu kwa nini uliingia katika mchakato huo?
  pili
  umetambua kuwa imani haikuruhusu kwa nini usitoe ushuhuda live katika press instead unasema imani haukuruhusu?
  tatu
  mi naona kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe maana hizi issue za dini zipo deep kwa hiyo wanaokula bata waendelee kula bata na wanaokesha wakiomba waendelee,wanaotupiga fix na biblia,qoran waendelee ila kila mmoja wetu atafakari itakuwaje katika fainali?

 9. Doreen!! Says:

  Hongera kwa kuwa Balozi wa Redds,pili why uliamua kushiriki miss tz kuanzia kitongoji,Wilaya mpk Taifa na wakati unashiriki hukujua km utashinda au?Kwa nn unakuwa km umeradhimishwa?Sisi wadau wa kamati ya miss tz tunakuomba km kweli unaimani katangaze kuwa pombe sio dili,dili kumfuata mungu sawa ww dogo usiyekuwa na msimamo katika maisha yako na ww una miaka kuanzia kumi na nae kuendelea kwa nn unapelekeshwa?Ss tutakufunga endelea na Ubalozi wako mpk utakapo isha.Km unaimani chukua hizo pesa nenda kawape watoto yatima na watu wasio jiwezqa sawa na mungu atakubariki na kuku samehe.
  Usifanye mambo kwa kumfurahisha binadamu mwenzio fanya mambo yako ya maisha kwa kumpendeza mungu.

 10. Dogoboy Says:

  Mie nafikiri mahindi yamechangaywa na maharage+viazi+nyama+ngano+Ulezi halafu vikapikwa pamoja eti watu tunangoja mlo……mlo gani utakao tokea hapo kwenye hiyo mix.

  Angela alikiri siku alipokuwa anakabidhiwa taji hilo pale New Africa Hotel alipoulizwa (tena alikuwa pamoja na mama yake mzazi na mdogo wake) vipi dini na taji hilo na kusema “mimi ni mtu mzima nina zaidi ya miaka 18 nina maamuzi yangu, nashukuru wazazi wangu wananisapoti…” leo kageuka chatu.

  Hana ulokole wowote, tena amedhihirisha uongo na unafiki, hakuna Muumba yeyote atakayempa thawabu katika hili. Anataka kumdanganya Mwenyezi Mungu pamoja na wale Waaminio wa kweli, hadanganyi isipokuwa nafsi yake naye hatambui hilo.

  Andiko gani takatifu la Biblia yake pale Sinza Mori, World Alive Church lililomruhusu akavae chupi apite mbele ya maelfu ya wanaume, wanawake na watoto (Equitor Grill hall) na kushinda taji la Miss Temeke 2008? Andiko gani la Biblia yake lilimruhusu aende Mwanza kushiriki na kushinda huku akiwa na furaha taji la Balozi wa Redd’s? Andiko gani la Biblia yake lilimruhusu jumamosi ya Agosti 2, 2008 apande jukwaa na kichupi chake pale Leaders Club hadharani mbele ya umma wa watu kuwania taji la Miss Tanzania na kuibuka mshindi wa Tatu? Nani aliemsukuma kusema, tena mbele ya Mama yake Mzazi na Mdogo wake pale New Africa Hotel kuwa “ana miaka zaidi ya 18”, “ana maamuzi yake”, na “wazazi wake wanamsapoti…..”

  Mwenyezi Mungu, Bwana Muumba wa Mbingu na Nchi, Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka , Mungu wa Yakobo, Baba wa Mbinguni anajua yote anayofanya Angela Lubala, anajua unafiki wote anaoufanya Angela. Yeye si wa kuchezewa shere na Angela, na katika hili Angela asimsingizie Mungu kuwa alimruhusu akawe Miss Temeke, Miss Tanzania (3) halafu eti Mungu huyohuyo amkataze Angela kuwa Balozi wa Redd’s, kituko na kioja cha Mwaka (unafiki katika imani).

  Angela anamsingizia Mungu wa Haki katika Madhambi yake. Anadanganya nafsi yake na nafsi za waaminio wa kweli, ni mnafiki anauma huku na huku, anafanya kazi ya Shetani anapokea pesa na zawadi za Dunia, halafu anamdanganya Muumba wake.

  Kazi kwake Angela, Muumba na walinzi wake Malaika watakatifu wamemwona na wameona unafiki wake na wamekwisha andika wanamsubiri siku ya hukumu. Haki itajulikana na uovu utajitenga, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMEEEEEEEEEEEN

  A

 11. nus Says:

  hakuna point yoyote ya yeye kurudisha taji, kama yeye ni mcha mungu haswa, sijui mlokole wherever, ilikuwaje akaingie katika mashindano ya umiss ambayo wasichana wanakuwa nusu uchi, hilo hakuliona, au hao wazazi wake walokole hawakuliona hilo? hata wakamruhusu aingie kwenye mashindano? kwani kuwa balozi wa redds ndio kunywa pombe? bora huo ubalozi wa redds kuliko kukaa uchi mbele za watu, upuuzi mtupu!!!!!! watu wengine bwana. hovyoooooo!!!! na arudishe zawadi alizopewa katika miss Tanzania pia, hapo tutamuona kweli anaimani na YESU!!!!!!

 12. Gervas Says:

  Frateline, Mimi nakupinga hapo, unaposoma Biblia, au andiko lolote la dini usikulupukie tu kifungu kimoja, Pombe wala haijakatazwa nafikiri umempata vizuri Sikujua Doto apo juu. Tena kwa kukupanua zaidi kuna kifungu katika agano la kale (sikumbuki exactly sehem) kinaagiza kuwa …”wapeni masikini pombe (mvinyo) wasahau shida zao” na Yesu alitengeneza mvinyo swaafi kwenye harusi ya kana na watu wakaserebuka na kumtukuza bwana. Wahubiri wengi hukurupukia vifungu bila kuelewa theme nzima ya maandiko. Tunyweni pombe jamani!!

 13. raphael Says:

  Hana lolote huyo ni hasira za kukosa hiyo miss Tanzania yeye anavaa bikini na kupita mbele za watu hiyo sio dhambi eti mtoto wa pastor!!!!! alienda huko kufanya nini na kama alilijua hilo mbona keshapokea hizo zawadi halafu anarudisha later on? kama ana roho wa mungu angekataa palepale ni shinikizo tuu kutoka anakokujua mwenyewe, nenda shule ili hata maswali madogo madogo ya kutumia common sense uweze jibu kwa ufasaha zaidi na pili uweze kuwa na maamuzi yako binafsi na acha fani za watu angalia unachoweza kufanya kulingana na hiyo imani yako

 14. Ni sawa na kwenda Moshi kwa basi halafu unafika njia panda ya Himo unageuza na kusema hukuwa unaelekea Moshi sasa ulikuwa unaenda wapi chizi nini anyway Dogo boy na Sikujua Doto hapo juu mmeongea kila kitu halafu point tupu kwa ufupi mmemaliza yote, kwako wewe Angela huyo Yesu hachezewi wala kudhihakiwa kwa namna hiyo na ninaandika kwa herufi kubwa USHINDWE NA KULEGEA KABISA mwone kwanza

 15. Chris Says:

  Waosha vinywa sukutueni tu midomo! Hahahahahaaaaaa! Kazi mbona anayo huyo Angela!

 16. Saidi Situ Says:

  baki ya kupotezea watu muda kuna kitu gani umegundua sasa ambacho hukujua wakati unashinda siku tatu za nyuma?

 17. molatee Says:

  Jamani huyo mtoto anakili alivyoingia anajua yeye na wazazi wake halishiliki miss tmk sasa kashinda sijui redbull hooooo sitaki mimi nimempokea yesu.Sasa nani halikutuma hushiliki?mbona umepita na kichupi mwili wote huko nje,hitakuwa redbull mjinga mkubwa redbull sio pombe kwa taarifa yako.Tatizo huyu Angela hajui analolitaka ndio nyie mnapewa mimba baba humjui
  Usimchezeeeeee bwana Yesuuuuuu wewe na familia yako
  Sidhani kama wazazi wako na wewe mna Elimu ya kutosha hulidishe mataji yote na hela zetuuuuu ni bora tukawape maskini

 18. molatee Says:

  Jamani samahani wote nimeandika redbull baada ya redds

 19. Mama wa Kichagga Says:

  Angela kashafanya maamuzi yake binafsi na sisi wengine hatuna haja ya kupoteza muda kwa malumbano yasiyo na faida kwetu wala kwake. Keshaamua na kutolea maamuzi hivyo let us respect her decision.

  Angela be yourself and dont be moved by haters. All the best.

 20. Edwin Ndaki Says:

  Mi nampongeza huyo dada kwa maamuzialiyochukua.
  Kuwa balozi wa redds mwaka mzima alafu wanakupa huto tijisenti tudogo wao wananeemeka kwa faida kubwa haingii hakilini mwangu.

  Suala la pombe ilo kwangu ni issue nyingine.Hata kama balozi wa soda kwa kiwango kidogo sihafiki.Na kikubwa kwenye hizo promotion za pombe huko ndio maeneo ambayo mtoto kama huyo angeingia tunduni.

  hongera uamuzi mzuri

 21. Luca Toni Says:

  Nilipoona hii post kwa mara ya 1 nilijiuliza maswali ambayo baadhi ya wadau juu wameuliza. Kubwa kati ya hilo ni kuwa katika imani yake, pombe tu ndio tatizo kushiriki umiss sio tatizo? Pili, let’s say mawazo yake binafsi na imani inaruhusu umiss; ila pombe pekee ndio tatizo; in that case, kwanini alikubali kupokea taji alipokabidhiwa?

  Ukweli ni kwamba naamini kuwa uamuzi huu unaweza kuwa umechangiwa na pressure ya familia. Ila all in all, sidhani kama yeyote kati yetu anayo haki ya kumnyooshea kidole Angela na kumsema vibaya. Kwanza kuhusu suala la umiss, hutakuta kipengele chochote katika bibilia kinachoaddress 1 kwa 1 suala hili sababu enzi hizo hakukuwa na mambo haya. Hivyo unaweza kusema haijakatazwa. Lakini at the same time, kuna mahala Yesu alikuwa anasema kama mkono wako ukikufanya utende dhambi, ni bora ukkate na uutupe. Maana ni bora upoteze mkono, kuliko kupoteza roho. Na kuna mistari mingine kadhaa inayozungumzia kutoshawishi wewe mwenyewe au mtu mwingine kutenda dhambi. Kwa mantiki hiyo, unaweza ukakemea umiss kwasababu unaweza kuchochea hisia za ngono. But at the same time, maandiko matakatifu yako deep sana; wengi wetu hatujui hata nusu yake. Na lugha ni philosophical and a lot of things can be interpreted one way or another. Hivyo tusikimbilie kuachaguatafsiri inayotufaa sisi kutegemeana na argument zetu kuhalalisha mambo. Be fair and give thoughts to both sides of the argument.

  All in all, mi sio mtaalamu wa dini and I won’t pretend to be one, nataka kuargue bila kutumia sana dini. Ila tu tukumbuke kuwa wengi wetu tuna imani 1 au nyingine, lakini asilimia kubwa tunachagua kufuata vitu fulani na si vingine. Mfano wangapi wanaweza wakawa wakristo wanaofuata mambo mengi tu mazuri ktk bibilia, and yet mtu anafanya tendo la ndoa na boyfriend/girlfriend wake kabla hawajaoana? Au waislamu wangapi wanafuata mambo mengi ktk Quran, na hawali nguruwe, ila pombe wanapiga? Imani ni kitu personal na ye mwenyewe Angela kwa jinsi anavyoitafsiri imani yake moyoni, anaweza kuona kuwa kushiriki miss Tz ni okay, but kupromote pombe is not. So kama we ni mkristu pia na una tafsiri yako tofauti usimlazimishe Angela naye awe hivyo pia. Kuchukua uamuzi huo haimaanishi ni mnafiki; inamaanisha ni imani anavyoina yeye, and like Any always says, hiyo ni personal decision yake 🙂

  Kwa kumalizia pia; mliosema kuwa alishashiriki mwanzo hakuona tatizo kwanini ageuke sasa; jibu lenu ni hili: Dini, particularly dini ya ukristu inatupa fursa wote kujiredeem tunapokosa. Sawa, let’s say all that she did was wrong; kama kweli moyoni mwake amerealize ni makosa na ameamua kuachana nayo (i.e. kurudisha taji) na moyoni mwake akatubu kwa Mola then it doesn’t matter what she did before. Maria Magdalena alikuwa malaya kabla hajaokoka; Matthayo alikuwa mtoza ushuru; Paulo alikuwa Saulo; mtu aliyekuwa anawaua wakristo kabla ye mwenyewe hajaokoka. Read Mark 2:17; When Jesus heard that, he said to them, “Healthy people don’t need a physician, but sick ones do. I did not come to call righteous people, but sinners.”

  By the way, mi ni mtu anayekunywa pombe kwa kiasi sometime. Siwezi kujitia unafiki na sisemi niliyoyasema hapo juu kwasababu naichukia pombe. Ila nimesema sababu naona wengi mmemshambulia huyu dada bila sababu. Remember the following:
  1. “Do not judge, or you too will be judged” (Matthew 7:1)
  2. How can you say to your brother, ‘Brother, let me take the speck out of your eye,’ when you don’t see the beam in your own eye? You hypocrite! First remove the beam from your own eye, and then you’ll see clearly enough to remove the speck from your brother’s eye.” (Luke 6:42)

 22. Obwatasyo wa Impokochole Says:

  Angela pongezi kwa hatua hii nusu. Malizia sasa dada kwa kukana waziwazi ‘ushindi ushindwa’ mwingine wowote uliowahi kuupata na kurejesha chochote kingine ulichopewa kinachoendana na tuzo za kujileta theluthi uchi mbele ya kadamnasi.

  Ni furaha iliyoje kondoo mmoja anapoamua kurudi kundini mbinguni na duniani?

  Hakika mimi ningekuwa mchungaji na nina jimbo ninaloongoza au hata katibu wa CCT au TEC hata CSSC n.k ningechukuwa mwendo wa ghafla wa kuhamasisha maandamano ya mapokezi ya kumpongeza huyu binti toka Usharika wake kupitia nyumbani kwa wazazi wake na kuzungukia mitaa ya uwanja wa fisi, Joly club, n.k na kumalizia maandamano hayo kwa kishindo pale Leaders Club ambapo badala ya Waandamanaji kuanza ‘kutwanga na kupepeta’ wangepewa nafasi ya ; KUSUKUMA NA KUMWAMURU SHETANI AWAPISHE WAPITE’ wakiongozwa na shujaa Rose Mhando!

  Key-note speech ya siku ingetolewa na Remi Ongala na ushuhuda ungetolewa na Yvone Chakachaka.

  Baadaye sadaka ya shukrani ingetolewa kwa hamasa ya kulikumbusha Joka kuu kuwa lilishashushwa toka mbinguni na sasa hata hapa duniani linasukumwa kuwaishwa linapostahili!

  Kisha baada ya Rostam Aziz kuhesabu chagizo iliyopatikana amkabidhi Mch. Mtikila kuiombea ndipo Hashim Lundega akaribishwe ili yeye kwa mikono yake amkabidhi dada shujaa Angela huku akitangaza kiwango kilichopatikana bila vazi la ufukweni!

  Ikibainika tu kuwa kilichochangwa ni chini ya kiwango kilichotolewa X ambapo X=Tshs. 2.5 M + Ths (posho ya balozi wa Redds ya mwaka), hapo ndipo mimi Obhwatasyo mwana wa Impokochole nitakaporuka na kusema ‘ndugu Wakristo ! Mchango unaendelea na mimi naanza kwa kusema kuwa kwa Tshs. X+1, nyote msimame na kukiri Imani ya mitume iliyoharibiwa kwa kumalizia kuwa ‘Namwamini roho mchafu, na utajiri wa Redds upitao uwezo wa Kanisa Takatifu lililo moja na Ushirika wa Watakatifu, kuongezewa kwa dhambi na kifo cha milele- Amina’

  Mwingine amalizie kitakachotokea kama hatatuhabarisha kwa rejea ya ‘ile çhupa ya mwisho ya mafuta iliyotolewa na mwanamama mwenye Imani kwa nabii Elisha’

  Ndg. Wadau ni vema tuendelee kukubali na kuenzi tabia ya Mwanadamu ANAPOAMUA KUJIRUDI MBELE YA HADHARA pindi agunduapo ukiukaji wake.
  Haijalishi binti Angela alikuwa ameshajivua nguo kiasi gani! Mlandano wa swali la ‘Ni nani alikwambia ujiunge katika mashindano ya ‘vichupi’ ni sawa na swali ‘Ni nani alikwambia (wewe mwana Mpotevu) uniombe sehemu ya mali iliyo kwangukia’ swali ambalo mimi sijawahi kuliona hata kwa darubini kutoka New testament Greek !

  Tabia ya kubeza toba za WAZI ndio zinatuletea Mafisadi kurejesha fedha zetu KISIRISIRI au wengine kukaa kimya kabisa wakifikiri kuwa wataweza pia kuichanganya Mbingu kwa kuwasilisha malinganisho ya mahesabu yaliyopambwa kwa misamiati ya kiuhasibu.
  Mama wa Kichaga ubarikiwe!
  Dada Angela pole sana na karibu kundini!

 23. TEACHER-DENMARK Says:

  LAKINI HUYU NI BONGE LA MSHAMBA HALAFU NI USUMBUFU KWANI HAKULIJUA HILO TANGU MWANZO ITABIDI WAANDAJI WAAKE SHERIA KWAmf KUPIGWA FAINI, HUYU KATAKA AJULIKANE YEYE KULIKO MISS TZ NDO YALEYALEEE!!!!!!!!! YA MISS USA ALIYEJIANGUSHA

 24. komba Muhili Says:

  Mimi namshangaa huyo Dada kwanini hakujitoa tangu mwanzo sasa akaona kuwa Balozi wa pombe halamu kuliko kutembea na vichupi mbele ya watu akaona mungu anapenda vichupi ila apendi pombe.Kama yeye akaona Mungu apendi mambo kama hayo kwanini akashiriki.Mimi ninachoshauri achukuliwe hatua za kinidhamu halfu ilo Taji apewe Miss namba nne wafanye kama TFF akaondolewa Yanga akawekwa simba nafikiri hiyo itakuwa fundisho.

 25. bupe mwakatobe Says:

  mimi nampongeza sana huyu binti kwa uamuzi wake mzuri.kwani ameonyesha ni jinsi gani anamuogopa mungu wake tena hayupo tayali kumuaibisha kwa kutangaza pombe.sasa nyinyi mnaomkashifu vipi,mlitaka aitangaze pombe wakati yy ni mlokole.acheni fitina ebo.

 26. bupe mwakatobe Says:

  Angela nakupongeza sanaaaa,achana na wanadam wasio muogopa Mungu.hayo ni maamuzi yako tena ni mazuri keep it up.simama binti

 27. Mamaa G Says:

  Kwanza nampongeza sana huyu binti kwa kuwa na msimamo na kumtangaza na kumkiri Yesu mbele ya dunia ni NEEMA kubwa sana kwa binti kama yeye, umri kama wake kufanya kitendo cha namna hiyo manake watu wengi huwa wanadhani ni kitu cha kishamba lakini yeye anajua ni faida gani, vitu vya mwanzo ni kweli ndiyo amefanya lakini at the last amegundua alifanya kosa na hatimaye akatubu na kunawa mikono..

  big up angela, GOD BLESS YOU!!!

 28. TATU Says:

  Duh thatha unavunja mkataba inabidi uwalipe sasa. kwani wewe ukujua Redds ni pombe ulijua ni soda nini? maana siku ile ulifurahia sana meno thelasini na nje yote yalikuwa mbili au ulikuwa una mategemeo ya kushinda masikini maaana hata huo umiss vile vile hakuna dini inayoruhusu kutembea na vichupi hadharani au ndio mdingi wako kakupiga mkwara nini?

  Jamani kwa ushauri tu watu wenye vipingamizi vya dini iwe ni ya kiislamu au ya kikiristo msiwe mnadhiriki mashindano haswa ya umiss maana mnawaharibia watu kazi zao.
  chaoooooooo

 29. TATU Says:

  Mnashiriki sio mnadhiriki kum ladhi alafu wewe dogo kwa nini ulibana nafasi za wenzio jamani ? wewe mambo hayo inamani yako hairuhusu usingekuwepo katika horodha hiyo basi.

 30. Hili ndilo tatizo la sisi waafrika kuzirukia hizi dini za kuja.Masuala ya imani noma kweli,DogoBoy hapo juu umemaliza kabisa huu ni mseto kama ulivyosema.

  Hivi wale waliotaka kukwea pipa bila makaratasi wameishia wapi?

 31. salma Says:

  mh!!!!!! haya si madogo amina upooo!!

 32. maspidi Says:

  Angepata zawadi ya kwanza lile Gari,angelirudisha au tunadanganyana?Toka awali,kwanini alishiriki mashindano ya Urembo kama yeye ni mlokole?Na iweje abakie na taji la Miss Temeke(?),lakini Miss Redds akatae?Au kuna lingine analoficha?Si aseme tu!Ulokole maana yake nini?Mungu wetu sote ni mmoja tu!Ukitembea uchi siyo mlokole?Nani aliyezaliwa na nguo mwilini?

 33. bdo Says:

  mmh kwani hata
  kutubu dhambi ni kosa?

 34. dada Says:

  Ok Malaika kama yametoka Moyoni hongera sana
  Usisahau kutubu yotee uliyopitia mpk ukwa balozi wa Reds
  All the best Kisura

 35. Pearl Says:

  as for me, I am ok with her decision.
  halafu mi nadhani huyu dada anajua anachokifanya,maana naona kuna wengine wanamuhukumu lakini tumeambiwa tusihukumu tusije kuhukumiwa!!!.Halafu watanzania hebu tujifunzeni kuwa the past has gone we focus on the present and the future.

  My dear Angela HEAVEN IS SO REAL,keep the good work for Jesus and just hold on to him,Dont let anything or anyone ruin your relationship with God.Nobody is worth of you except the one who created you.
  People will surely talk but let them talk after all midomo iliumbwa kwa ajili ya kuongea na kula kwahiyo wacha ifanye kazi yake.
  Cha msingi dada yangu uamuzi wako uwe thabiti.

 36. aman Says:

  huyu msichana ni kama walokole tuliowazoea ambao wanatenda dhambi halafu wakishapata hela ndio wanajifanya kutubu.
  Walokole wengi wakiona dili yoyote yenye hela wamo ila wakishapata mara ooo nilikuwa dhambini
  acheni kumchezea Mungu nyie mtaungua sana

 37. Matty Says:

  Mh!hii kali sasa, Mambo ya personal decision hayo!
  Kwani hakujua kama yesu hapendi mambo hayo (kupita jukwaani nusu uchi na pombe) tangu mwanzo??? au ndo shinikizo la wazazi??
  Hongera kwa kuchagua fungu jema na endelea kumtumikia Mungu, ila ujue umetuacha midomo wazi!na majibu unayo wewe na wazazi wako!

 38. pat Says:

  ukweli ni kwamba alijua atakua miss Tanz. sasa kuwa miss redds anaona haijatulia. maana miss Tz, angepewa gari na simu kwa mawasiliano. au alikua anatafuta hela ya kuingilia chuo? maana milion 8 jamani si mchezo. na liusafiri kama lile, si mchezo.

  Akili yake ilikua ni kwenye Umiss TZila imeshatokea hivyo msameheni bure. bado mdogo.

 39. ikram Says:

  ndugu yangu mengi yamesemwa na kuandikwa, ila napenda niseme hivi ,mara zote fikiri kabla ya kutenda na usikubali kushawishika kwa vitu ambavyo mwenyewe huna uhakika navyo, iweje leo umeingia kwenye mchezo wa watu na sasa mambo yako hivyo, hivi ni kuwa wakala wa redds tu ndio hutaki au vipi, jee ungebahatika kuwa miss tanzania ingekuwaje mana ndio hivyo na kama hupendi hilo jee na yote unayokatazwa huyapendi au hilo tu, mana hata mavazi pia unayvaa ni sehemu ya makatazo, sipendi kuamini kwamba wewe huna uwezo wa kufikiri na kuamua au, huna uwezo wa kupima mambo kabla ya maamuzi na kwamba unaweza ukaamua na ukashindwa kutetea uamuzi wako, mimi sipendi kusema lolote mana uamuzi wako umegusa imani yako na eneo hilo ni gumu kwa yoyte kuliingilia mana ni sehemu ya roho na roho ni ya mtuummoja tu, wewe mwenyewe, ushauri wangu kwako, tumia mawasiliano kwanza kati ya akili, moyo na kiwiliwili. usikurupuke mana madhara yake yanaweza kuwa makubwa kwako na kwa wale wanaokuzunguka

 40. Kaka Says:

  Mamaa, we mtoto we ungepata ile Vitara na M8 ungerudisha wewe? halafu hao wanaokushauri uaiwe balozi wa pombe mbona hawakuulizi bikra yako ilitokaje?
  Acheni hizo wabopngo huyo mtoto nyuma ya pazia ni fundi kupindukia (mi nshalamba) shauri yenu!

 41. dada wa Kimahanji Says:

  Please respect her decision, uamuzi kafanya yeye. Well done Angela. Kumbuka kwa Mungu atasimama mwenyewe. Kama alikosea kupokea hiyo taji, FINE amerudisha. So WHAt do you want now? God bless you girl and keep going I personally support you and Love you.

 42. binti-mzuri Says:

  nyi watu wengine wazimu kweli..sasa mnamtukana nini dada wa watu!?mwaya Angela hongera..songa mbele

 43. jane joseph Says:

  Katika hali ya kawaida,kama kweli angela ni mlokole hakustahili kabisa kushiriki huo mchakato wa miss tz.Kwa binti aliyelelewa na kujitunza ktk maadili mema,umiss angeona sio deal kwake na badala yake angeambatana na talents au ambitions nyingine ambazo zingemuweka karibu zaidi na Mungu.Sio kama umiss ni uhuni,lah hasha.Nadhani yy hakuwa na uhakika na maana halisi ya umiss au hakujua miss ni nini?amemsaliti Mungu wake na watu wote walioudhuruia shughuli hizo.Ni vyema aite ule umati wote uliokuwepo siku alipovishwa taji ndio Mungu atamsamehe.wazuri wapo wengi ila hawakujitokeza,amepewa nafasi anaitumia vibaya.Atajuta!!!!!!!!!!!!!

 44. tatu kama moja Says:

  imani yangu hainiruhusu kupromote pombe kwani haramu na ni dhambi kubwa mno! ila naruhusiwa tu kuvaa nusu uchi, kuonesha sehemu yoyote ya mwili wangu mbele za watu hata mbele ya wazazi wangu. pombe inachochea mtu kufanya dhambi nyingi kama kuzini, kuua….lakini kuonesha uchi wa mwanamke jukwaani na midume ikishuhudia kunawapa wao tamaa ya kuwa na wake zao ili kujiliwaza kutokana na kile walichokishudia toka kwa mrembo kama (self-uncrowned Redds ambassador).wale ambao hawana wake watafanya mpango waoe.this is shiiiiit!!!

 45. Nkima Says:

  Jamani mbona mnaingilia imani za watu? Yeye imani yake haimruhusu kuitangaza pombe sasa lakini haimkatazi kushiriki miss Tanzania. Kuweni waelewa jamani. Kwa mfano watu wenye imani ya rasta huwa hawanywi pombe ila wanavuta bangi wakati bangi imo ktk kundi la madawa ya kulevya!! Ina maana inalewesha. Ninachomaanisha ni kuwa imani ya Angela haimruhusu kunywa au kujihusisha na pombe. Hawezi kuwa balozi wa pombe. Angela nakupongeza kwa uamuzi ulioufikia kama Redds wamekuelewa usihagaike na hao waosha vinywa.

 46. Aunt D Says:

  Wewe “Kaka” unajionyesha kuwa kidume sanaaa?
  Huoni aibu kuandika hayo maneno mtandaoni?
  Kaamua muache na wewe siku ukimkumbuka Mwenyenzi Mungu TUBU kivyako
  Acha Hizo!!!!!

 47. Matty Says:

  leo sina useme nawasikiliza ninyi!

 48. Anonymous Says:

  Huoni kwamba kuna mwenzio aliyestahili kupata taji hilo ila alilikosa sababu yako? Please give us a break………

 49. Mamii Says:

  mmh! jamani! hapa naona watu wanarukia suala hili bila uelewa. kwani umiss ndo nini? mtu alijivalia nguo za heshima, wala hawakupita na vichupi kama wengine mnadai. Angela alikuwa anawani taji la miss tz siyo la miss redds. alipopewa taji hilo hakulifurahia lakini hakutaka kuwaumbua akina anko lundenga hapohapo akaamua kumezea. sasa alipoona mambo yametulia amerudisha taji, na kamati imemvua mataji yote na ameambiwa arudishe zawadi zote na amekubali. sasa nyie mnaomsema mnamsema ya nini. katimiza yote mliotaka na amesema BYE. mwacheni mtoto wa watu! Angela mwaya, we songa mbele wasikubabaishe wabongo, tunapenda sana kuchonga!

 50. bdo Says:

  please this is very personal, tusichanganye “njaa” na suala la hisia/imani, ameacha yote for divinity reasons, sasa sidhani ni fair kumuhukumu….maana w’re just putting on our ideas to hers, tusiangalie background zetu ili tumuhukumu mwenzetu kuwa kachemsha,….kwangu mie nampa hongera saaaaaaaaaaaaaaaaana, wenye wivu mjinyonge!!!!!!!!!!!!!!!!

 51. Thats the problem ya watanzania. respect people choices na privacy . mmezoea mtanzania mpaka mumtie ndio mmpe kitu hautaki umiss na kama mlijua mtamtia poleni sana

 52. bdo Says:

  wewe jane, temea mate chini, kwani uanataka kusema walokole si warembo? and hawatakiwi kushindana?mmmh

 53. Ignorant Says:

  Lakini mbona REDDS ina sukari…. na akasilimia kadogo ka ulabu. hahahaha….. kanakubalika tu … Angela fikiria huu ukweli na ukane usemi wako pleaaaaaaasseeeeeee!! There is nothing wrong kuitangaza bia ya kitoto kama REDDS (for starters teh teh teh)

 54. michelle Says:

  Jamani zisi ishu izi vere simpo, wazazi wea ok wizi ti,iveni ze nite ovu ze ivent ze parents atendedi, zei wea zea tu conglatuet zea dota, iveni in heven zea wili be sachi an ivent, but zisi wili bi fo Lubala’z onli, so what izi yua problem, zei koli zemselvu’z ze bigi national. so justi shuti yua mausi endi leti zem bi hu zeia, hii ni luga ya mama wa Angela kwisha kazi!!!!!!!!!!

 55. michelle Says:

  (Tatu Laticia Aunt Lubala) unalo sasa la kusema?
  Maana ulikuwa ukiwahukumu sana akina nanihiii oh wanavaa nguo fupi sijui nini sasa unasemaje hapo, Mungu akusamehe bure, kwa wengine midomo juu kwenu sawa, tutafanya umodo huko mbinguni, na wewe ndiye utakayeongoza ibada ya sifa pamoja na la-aziz wako teh teh teh,msalimie nanihiii nitakupigia simu sawa!!!!!!!!!!!!

 56. michelle Says:

  Angela kimblia huku USA ukajifiche na mataifa yote!! teh teh teh tena uondoke usiku wakati hawakuoni au kachukue flight yako Kenya ili hao wasikuone wakati unaondoka sawa mama!!!!!!!! nipigie ukifika nitakupokea.

 57. Maua Says:

  Ignorant kwa taarifa yako Redds ina 4.5% alc v/v, sawa na Kilimanjaro.

  Mi nakubaliana na Loca Toni hapo juu; katika Ukristu kinachojalisha ni kuwa umetambua makosa kweli na ukweli ukatubu. If you are truly remorsefully God will forgive you and no human can come back and start pointing a finger at you mbona alifanya hivi au kwanini alifanya vile. It does not matter that Angela participated in Miss Tz before; what matters is she’s realized the errors of her ways and has repented.

  Isitoshe kama alivyosema mdau hapa juu; hawakuvaa vichupi katika umiss, acheni Uongo. And even if they did, imani sio uniform. Inawezekana kwa mtazamo wake yeye, umiss unaruhusiwa but pombe hairuhusiwi. Msimpangie jamani, eh!!

 58. Mwanamitumba Says:

  Haya ndo yale ya wakina Jonie Mashaka, mshikaji huko wapi siku hizi, njoo hapa changamkia hii tenda ya kilokole!

 59. anonymous Says:

  bwana asifiwe

 60. Masudi Says:

  at the end of the day kila mtu ana maamuzi yake na kila mtu anapoamua kufanya maamuzi yake binafsi yapatwa kuheshimiwa.
  Keep it on Angel u ar rok. Strong lady
  Tatizo binadamu always huwa tunakimbilia kulaumu baada ya kukaa chini na kufikiri. There is a big difference btn huo umiss na Redds embassador hao wazamini wasitufanye wajinga mara ngapi wasanii wanaibiwa kwa kutojua mikataba yao swala la mikataba still bado TZ lipo down not only Tz even in tha developed countries.
  So sioni sababu za kumsakama Angela manfact yeye na familia yake ndio wenye uamuzi wamwisho ni sio sisi, sidhani kama kuna mtu ambaye atamshauri mtoto wake ushauri mbaya thats pathetic n cruel heart which covering in our broken stink hearts
  Angela am real proud of you msikilize baba yako na sio hawa watu wamitandaoni na wakina lundenga wasikujua kiundani na maisha uliyoyapitia, kama uyo Lundenga alishawahi kukupa hata kipande cha sabuni then msikilize but if mlikutaka ktk harakati tha umiss then let talk is crap and tha end of the day hoppefully u will up baby

 61. Junior Says:

  Namnukuu Yesu’ Basi na hamna mzazi ambaye mtoto wake akimwomba MKATE atampatia JIWE’ period
  so ur dady Angel hes rite even if its not at the proper time but he still wanna see ur life shinning later
  Take 5 Angela and u hatters may keep on hatting but u gotta kno that that thingy make her feel better
  gracias

 62. HALIMA Says:

  Jamani huyu bint mimi amenichanganya sana, au hilo dhehebu lake ndilo linalovyofundisha? yaani upite mbele za watu nusu uchi halafu ashindwe ndo alete visingizio vya kitoto hapa?
  1. kwanza nataka kumuuliza kuwa aliwezaje kuwa miss kitongoji kama haitoshi bado akawa miss wa wilaya wakati wote huo hakusikia sauti ya bwana ikimuita wala hakusikia mahubiri ya baba yake akihubiri?

  2. Picha linaendelea kafunga safari kaenda mwanza huyo na kichupi chake kapanda jukwaani kwa ajili ya kushindania REDDS na anajua kabisa kuwa hiko nikilevi? maandiko anayajua na biblia kasoma sijui alikuwa anafikiria nini?

  3. Mwisho wa picha huyo karudisha makanyagio dar usiku bila hata haya na mapozi yote kapanda jukwaani watu huyo huyo kapendeza kapendeza starling anakaribia kuuwawa huyo kakurupuka ohoo nimeokoka!!!! haa!!! nampenda bwana haa!! kumbe redds nikilevi? ohoo jamani namrudia bwana,

  4. huyu sio bwana ninaemjua mimi bwana wa mabwana mungu wa majeshi hadhihakiwi hata sikumoja kaa ukijua hivo.

 63. bdo Says:

  bc, please can weigh out kuwa watu wanapenda kukuza mambo, haya ni mambo yake binfsi, natamani Yesu au mbingu zifunuke ukweli ujulikane

 64. ma'reen Says:

  That was very brave of her and I salute the girl for it. Siwezi kusema alitegemea miss tz tu kwa kuwa Mwanza walishindania miss redds na alishiriki. But who cares? Amegundua taji hilo halimfai aidha kwa matakwa yake au kwa ushauri wa wazazi au jamii ya kikristo (wana bahati kuwa na binti anaeshaurika), akaamua kujivua taji hilo na kurudisha kila kilicho chao. Ni mabinti wangapi wangeamua hivo? Si wangeishia kuzozana na wazazi/jamii…ooh it’s my right am an adult bla bla bla! Umeonyesha kuwa bado kuna mabinti wa kiafrika wenye msimamo, wanaomuogopa Mungu na wanaotii wazazi. Cheers Dear na ninaamini Mungu atakufungulia milango mingine ya baraka isiyo ya pombe. Ungeshikilia taji wanafiki hao hao wangeanza oooh mtoto wa mchungaji anauza beer, waosha vinywa hawakaukiwi maneno!

 65. Dunda Golden Says:

  DADA UKUMJUA MUNGU KABLA YA KUANZA SAFARI AU NDIO ULIKUWA UNASUBILI USHAHIDI

 66. Matty Says:

  ushuhuda hivi ni lazima uonekane au siyo????

 67. cyn Says:

  TATIZO WATU WENGI MNACHAMBUA MAMBO KWA HASIRA BILA KUANGALIA UKWELI.

  KUSHIRIKI U MISS SIO DHAMBI(DHAMBI YAKE NI NINI?) KUVAA BIKINI ALIYE KUAMBIENI NI DHAMBI NANI?KAMA NI DHAMBI BASI WASINGERUHUSIWA NA BIBLE KWENDA BEACH AU KUWA NA SWIMMING POOL NYUMBANI.

  ALICHOKUWA ANASHINDANIA ANGELLA NI U MISS TANZANIA NA SI U MISS REDDS NAOMBA MUELEWE HILO.

  BAHATI MBAYA KUNA WENGINE WALIKUWA NA SIFA ZAIDI KULIKO YEYE KWA HIYO WAKACHUKUA NAFASI ZOTE YA KWANZA MPAKA YA TATU WHICH IS FINE,NI WATANZANIA PIA.

  ALICHOKIKATAA ANGELLA NI KUWAKILISHA REDDS MKUMBUKE HILI NI TUZO LINGINE,TUZO HILO NI ZURI PIA SEMA TU KWA BAHATI MBAYA TUZO HILO LIMEANGUKIA KWA MTU AMBAYE IMANI YAKE IMESABABISHA ASHINDWE KULIPOKEA.KAMA ANGEKUWA MTU MWENYE IMANI YA KAWAIDA ANGELIPOKEA TU.MBONA VICTORIA MARTIN AMEKAA NALO MUDA WOTE.

  TATIZO SISI TUNALAZIMISHA HUYU NAE AWE VICTORIA MARTIN MWINGINE HIYO HAIWEZEKANI.HUYU NI ANGELLA AND (SHE IS SAVED).

  ACHANI KUTUMIA HASIRA,MUELEWENI MTU ANACHOKISEMA KWANZA.TATIZO KUBWA LA WATANZANIA HUWA TUNAKIMBILIA KUTOA COMMENTS BILA KUCHAMBUA TAARIFA VIZURI.

 68. binti-mzuri Says:

  mmh hivi vitimbi sasa..haya kina mujuba,fanyeni kazi za kusafisha,si tusome tuu

 69. Chris Says:

  Didn’t knew if she can be so topical!

 70. Mkate Says:

  “Usihikumu usije ukahukumiwa kwani, kipimo kilekile utakachompimia mwenzako ndicho hichohicho utapimiwa siku hiyo ikifika.”
  So..kazi kwetu na yale tunayoyasema.

 71. Mdau Says:

  Kati ya watu wote hakika CYN umechemka mno,yaani umeelezea pumba tupu….!!!!.Wewe ndiyo kabisaa huwezi hata kuchambua mambo,nina shauku ya kujua level ya elimu yako kaka/dada…!!.Haiwezekani ukatenganisha Umiss Redds na Umiss Tz…!!.
  Kitu cha msingi kwa binti huyu kutokana na msimamo wake wa kidini hangekataa tangu mwanzo akatae kuingia kwenye mashindano,Hapo angejijengea heshima kwa jamii,inaonyesha aliingia kichwa kichwa,na kama ni dhambi alishaifanya tangu mwanzo alipoanzaa kuingia kwenye haya mashindano.
  Ni kheri akatubu kabisa na kurudisha zawadi tu.
  Mpaka yeye na wazazi wake wanaudhuria sherehe ya kumpongeza kuwa miss Redds walikuwa hawajajua kuwa pombe ni dhambi…???!!!!

 72. Philip Says:

  Yaani kujianika kote pale kwenye mashindano ya miss Tanzania sio dhambi!!! Ila kuwa miss Redds ni dhambi!!!

 73. trii Says:

  kakumbuka shuka wakati kumeshakucha.

 74. Matty Says:

  caps letter means shouting! you guys no.67.wat do want to say???

 75. Mamii Says:

  we mdau! we ndo umechemsha, Ms TZ na ms redds ni vitu viwili tofauti. unaweza ukashinda taji la ms redds na usiwe hata runner up wa ms tz! mtu anaposhindana ms tz kwani anawania taji la ms redds? kama ingekuwa kitu kimoja ms tz ingekuwa ms redds tz lakini ni ms vodacom tz. na balozi wa redds anapromote kilevi wakati ms tz anapromote vodacom. au mdau, we ndo lundenga mwenyewe nini? mbona una hasira hivyo? amesharudisha zawadi sasa tatizo lako nini? kushiriki ameshiriki, kujulikana amejulikana, kushinda ameshinda, kurudisha taji amerudisha, hasira ya nini?
  Hongera Angela! wacha waseme mwisho watachoka!

 76. HALIMA Says:

  Aiseee!!!!!!! mimi nachanganyikiwa na hizi imani, kila mlokole lazima amsaliti yesu ndio atowe ushuhuda why? Naakitowa huo ushuhuda lazima atoe andiko ohhh!!! mbona yuda alimkana yesu lakini alitubu akasamehewa , ufanye kusudi utegemee malipo ya mitume waliopita hiyo hakuna, mtu na akili zako zote na wazazi wako tena wameokoka unapita mbele za watu nusu uchi mzazi yupo kwenye luninga na kichupi chako, huyo unakatiza tena usisahau wakati huo anapita baba anasoma biblia, mama huyo asubuhi kaenda kuungama, mchana kamsindikiza bint yake kupokea taji la REDDS bado tu hawajagundua hiyo ni dhambi? hao na taji lao mpaka nyumbani kwao REDDS mkononi, kuja kugundua kuwa hiyo inshu hailipi mnaanza kumsingizia mungu nyie endeleeni tu bwana!!!!!!!

 77. rob Says:

  Mimi nina muunga mkono CYN kwasababu nina kaa sinza mtaa mmoja na angella.

  Jamani kwa taarifa yetu hilo kanisa la WORL ALIVE CENTER LINALO ANDIKWA MAGAZETINI liko nyumbani kwao angella,wanaishi hapo alafu eneo kubwa lililo bakia ndio familia ya kina angella ilivyo rudi rasmi kutoka califonia wakaa amua kujenga kanisa ndani ya eneo la nyumba yao. Na hata siku nyingine ukienda kanisani kwao angella unamkuta mbele pale anaimba nyimbo za dini kwa waumini.

  Kwahiyo kwa sisi tunae kaa nae mtaa mmoja hatukushangaa alivyo vua taji hilo la pombe ambayo iko chini ya tanzania breweries.

  Wao walirudi kutoka califonia baada ya kukaa huko kwa miaka zaidi ya 19.nina uakika hata huyo angela mnaemsema sizani kama amesha anza kuzungumza kiswahili vizuri.kwasababu wana muda mfupi tu toka warudi.but true (she is saved )sijuani nae wala sina sababu ya kumtetea,lakini huo ndio ukweli wa sisi ambao ni majirani mtaani.

 78. malcolm Says:

  Napata wasiwasi na hii imani ya kilokole inavyoingia,hawa watu kila kukicha makanisa yanaibuka,ukihuliza huo uchungaji na uaskofi wameupataje au wamusomea wapi jibu sijuhi kama wanaweza kukujibu.
  Ukiangalia mchakato mzima wa Angela kuanzia u miss kitongoji hadi Taifa wazazi wake walikuwa wapi hadi wasihuone huo uchafu wa Pombe!
  Au wanataka kutuambia kutembea nusu uchi ni bora zaidi kuliko kutangaza pombe?
  Hapo inaonyesha kuna shinikizo ambalo binti kashurutishwa,bila nafsi yake kupenda hila anatutia mchanga wa macho kwa kusema ni mahamuzi yake binafsi,napatwa na wasiwasi huo uaskofu wa Mzee Luballa kuwa alikosa umakini tokea mwanzo na inaonyesha hana msimamo hata kwenye maubili yake mbele ya madhabau.
  Maandiko yako na imani si za leo ni za siku nyingi,hiweje baada ya kutawazwa ndio Angella aje na Pumba zake?
  Je anatambua Hasara aliyoisababishia Kampuni ya TBL.?
  Ni pumba kwa mtazamo wa juu juu sababu hana point ya msingi,nitamwona wa maana angesema ukweli wake tu kuwa nimeshinikizwa na kwa kuwa yeye ni mtiifu mbele ya jwazazi wake, na hilo nampongeza kwa kuwa mtii kwao kwani ndio Mungu wa pili baada ya Manani.
  Tumsamehe tu mtoto wa watu na tukumbuke hule usemi wa kuwa hajui atendalo.

 79. Fresh Says:

  Kwa kifupi huyu Angela kanobore sanaaaaaaa,hivi nani alimtuma kwenda ktk Mashindano hayo in the first place?na je kuwa balozi wa Redds ni lazima uinyweee?
  In my opinion kuokoka is about your heart and how you relate to God and others,sioni dhambi kama angeiwakilisha Redds,ya Kaisari tumpe Kaisari bwana eeh

 80. pat Says:

  mwacheni bint apumue jamani. inatosha kama taji kashalivua makelele ya nini tena? c wampe mwingine aliyekua anafatia kwa sifa za kuwa miss ulabu, kwani hakuna mshindi wa pili c yupo apewe huyo mwingine.

 81. Lina Says:

  Dah! Ama kweli mrembo huyu kachemsha saaaaana. Hapa lazima apate lawama jamani. hajatutendea haki kusema ukweli. Tumempa Taji kwa furaha zotee na alipokea mbele ya umati wa watu kwa furaha tele. Nadhani waliambiwa kabisa kama kuna Mataji yatatolewa, kama ukikosa la Umiss basi kuna la REdds & soooo sasa jamani kwani hakulitambua hiloooo??????
  Cha ajabu sijawahi kuona mlokole anayeshiriki ktk mashindano kama haya kwani wanadai ni dhambi na si vizuri kuonesha sehemu za mwili.

  Sasa najiuliza je! alienda kushiriki akitafuta nini huko?????? Hao wazazi wake ni watu wazima na wamekula chumvi kuliko yeye, Kwanini hawakumshauri mwanao asishiriki ulimbwende ili hali imani yao hairuhusuuuuuu???? Jamani hapo mimi sielewi na ametuchangaya sanaaa wapenzi wa sanaa hii.

  Yeye angeendelea kuwa balozi wa Redds tuu kwani halazimishwi kunywa na pia huo haukua mkataba wake na Redds wa mAISHA YAKE YOTEE.
  Wala kua balozi wa Redds sio kwamba ndio asingeweza kusoma tena labda wangempa sapoti nzuri tuuu ya kujiendeleza kimasomo zaidi. Au alikua anamendea lile Gari na mahela Mwanawaniiiiii, Mhhh, Hapo naweza kumfananisha na chui aliyevaa ngozi ya Kondoooo, Au tukumbuke ule msemo wa Sungura aliyekua anarukia ndizi, Baada ya kuzikosa akasema sizitaki Mbichi hizi, hahahaha……

 82. Mdau Says:

  Sasa jamani wewe Mamii,Kwani wewe hujui kuwa unaposaini form za kugombea umiss tz automatically unasaini kugombea miss Redds..??!!,Kwasababu miss Redds anatoka humo humo kwenye kambia ya miss tz na katu hatoki World Center Alive,sinza mori..!!!.
  Kwa ufupi huyu binti ameonyesha dharau ya hali ya juu,anastahili kupelekwa mbele ya sheria awalipe waandaaji wa taji la Redds,1).Pain and Suffering,2)time wasting charge,3)Humiliation charge,4)Violation of miss Tz Contest protocol.Kisha akatubu kanisani kwake kwa kuvaa kichupi na kupita mbele ya kandamnasi,kutumikia taji la Redds kwa muda wa week moja (Kwa mujibu wa Imani yake ya kidini).

 83. wales Says:

  MANENO ALIYO ZUNGUMZA DA CYN NI MAZITO SANA MIMI NA MUUNGA MKONO.

  JAMANI SIJUANI NA ANGELLA LAKINI IAM SURE KAMA ANGELLA ANGESHINDA MISS TANZANIA TARGET YAKE ILIKUWA KUBADILISHA KABISA MTAZAMO MZIMA TULIO UZOEA SISI WATANZANIA.

  KWA BAHATI MBAYA AU NZURI SIJUI HAKUWEZA KUFANIKISHA AZMA YAKE,LAKINI NINA UHAKIKA KUNA SOMETHING ALIKUWA AMEPANGA KUKI CHANGE. NA INGEKUWA USHINDI KWA GOD OF ISRAEL.

  KWASABABU KASHINDWA KWAHIYO UJUMBE WAKE HAUKUFIKA NDIO MAANA WATU WENGI WAMESHINDWA KUMUELEWA ALICHOKUWA ANAKIFIKIRIA.

  LAKINI TUKUMBUKE YEYE NDIO MSICHANA PEKEE MWAKA HUU ALIYESHINDA MATAJI MENGI KULIKO HATA HUYO MISS TANZANIA WETU NASREEN.
  YEYE NDIO MISS CHANGOMBE,MISS TEMEKE NA HUO U MISS REDDS AMBAWO AMEUKATAA.

  LAKINI WASICHANA WAKO WENGI KWANINI TUMSEME YEYE WAKATI HAUTAKI U MISS POMBE WENU,SITUWA CHAGUE HAO TUNAO WAONA WAZURI NA WANA AKILI TIMAMU.

  KAMA AMUAMINI KAMA SHE IS SAVED BASI SI MUENDE KANISANI KWAO MKASALI MSIBITISHE.

 84. michelle Says:

  Jamani hawakuwa wanaishi Califonia mbona mnarukia mambo msiyoyajua walikuwa kijiji kimoja huko south, AL!!!!!!!!!!!!!!

 85. the ma-juuz Says:

  uzuri wa huyu binti mimi siuoni. Ningekuwa judge wa shindano hilo, nisingempa maksi hata kidogo! I`m sorry to say that but that`s my opinion.

 86. Guyle Says:

  We Wales acha kutuongopea. We ndio CYN mwenyewe, eti unajifanya unamsupport CYN, haha. Angalau ungebadili badala ya caps ungetumia herufi ndogo. Na hata style yako ya uandishi mtu akisoma anajua u r 1 and the same.

  Na we Lina vipi, kwani na we ulikuwa mwamuzi? Au unahusika na Miss Tz au kinywaji cha Redds? Au TBL kwa ujumla? Maana unatuambia “Tumempa Taji kwa furaha zotee na alipokea mbele ya umati wa watu kwa furaha tele”

  Malcom uko darasa la 2 nini? Maana naona lugha inagomba kweli. Au sio mbongo? Au ulikimbia umande?
  Unaweka ‘h’ pasipotakiwa, unachanganya ‘l’ na ‘r’!? …aaahhh, job true, true!!

  ukihuliza (ukiuliza)
  sijuhi (sijui)
  wasihuone (wasiuone)
  hila (ila. Neno hila ni neno la Kiswahili lakini halina maana uliyokusudia hapo juu. You intended to say ila as in but)
  mahamuzi (maamuzi)
  maubili (mahubiri. Dah hapa ndio uliharibu kweli)
  madhabau (madhabahu)
  hiweje (iweje)
  hule (ule)
  ——————-

  haha, aisee raia wanachekesha sana humu. Watu wana hasira utadhania wana hisa TBL or something!! Get a life people. Mwacheni binti na maamuzi yake

 87. Kidalipo Says:

  Jamani nyie Redds bado mmemuachia huyo binti anaendelea kurandaranda tu hapo kanisani,sinza Mori..??!!Kwanini msimpeleke huko kwa ma-cereblity wenzie wakina T.I.D na Dogo Ramadhani awe anakuja hapo Kisutu mara moja kwa mwezi kujibu hoja…!!! Au hamna wakili wa kuwajengea hoja..???.Hiyo hasara yote mtaifidiaje sasa kuanzia mchakato wa kumpata miss Redds mpaka sherehe ya kumpongeza..???!!!

 88. Matty Says:

  Sukutueni vinywa majirani zake Angela na wataalam mimi leo nasoma tu!!!

 89. Mfakunoga Says:

  Mimi nina wasiwasi na hilo kanisani kama kweli linatumia hii Biblia tunayoitumia sisi au Biblia nyingine.Kama ni Biblia hii tunayoitumia sisi basi inabidi wajiangalie upya kwani watakuwa wanasoma “WRONG PAGE”,Waigeuze ikae vizuri.

 90. HUSTLER Says:

  Unajua ANGELLA kwa sasa amedata jamani,tumuacheni apumue manake atashindwa kusoma hata huko anapoenda
  ukweli upo wazi,mtoto alistahili u-miss TZ,sema tu yeye ni andunje kwa Nasreem.but sio issue jamani mwacheni arelax.mnaokoment upuuzi,hamna ata chembe ya ustaarabu.sasa ninyi mnatofauti gani na mafisadi.
  PUMZIKA MAMA,JIAMINI KWA UAMUZI WAKO WALA USITETEREKE..
  BIG UP N MASOMO MEMA

 91. binti-mzuri Says:

  hahahah kazi duniani.kumbe muamerica nusu nusu

 92. G Says:

  aah I m not hating ila huyu mimacho hakustahili umiss wala nini. Kwanza nilishangaa sana hata 5 bora alifikaje na huo ‘uredisi’ aliuapate

 93. lady Says:

  nasreen kwa urefu tuu poa,lakini upeo wakujibu maswali yule angela she is smart nafikiri ndio maana alishinda mataji mengi mwaka huu.

  inaoneka kana sisi watanzania mwaka huu tumeangalia sana urefu wa mtu na labda sura kidogo.

  lakini kama unazungumzia nani yuko smart kichwani basi angela kiboko,sijui kwasababu ya elimu aliyo ipata america.

  lakini mbali ya yote nasreen ndio miss wetu tuangalie atakavyo kumbana na wenzie uko kwenye u miss world.

 94. jane Says:

  lakini lady twende mbele na turudi nyuma vilevile,hawa judges wanasifa gani,mtu kama maximo kocha wa timu ya taifa anajua nini kuhusu modeling,fame,fashion e.t.c

  kwanini wasitumike ma miss wa zamani ambao ndio fani yao.mimi nili bahatika kuka na ma miss wa zamani kenye ile miss temeke ya mwaka huu, yaani wanakuchambulia mrembo mmoja mmoja kiundani mpaka wewe usiejua kitu unapata ideal fulani ya mambo ya urembo yalivyo.lakini hawamo kwenye judges team.

  nasreen alikuwa anasoma kenya,angella alikuwa anasoma america.

  angella she is smart,nasreen she is tall.time will tell

 95. Matty Says:

  Halo Dada Jane habari ni hii! amongst of the judges Shose Sinare was there didn’t u saw her?sema tu wangemuweka Maria Sarungi pia!
  Uwepo wa Judge Maximo i have nothing to say maana hata mimi sikuelewa maana jamaa anajua sana mpira sijui ilikuwa vipi!
  matokeo yashatoka lazima tukubali tu!

 96. seniordo Says:

  Hello, mimi nampongeza huyu dada. maisha yangu kwa miaka kumi nimekunywa pombe, nimeishi nchi wanazaoabudi ulevi, nimekunywa na kunywa mwisho nimejiuliza na kusema yote ni upuuzi. uaamuzi wako ni mzuri yaania kwa lugha ya kingereza (superb). sasa yakupasa ushikilie hatamu hiyo maana umeitangaza kwa ulimwengu na hivyo basi lazima utapata maadui. you are so young to represent a marely beer- Redds. you have a great life ahead of you and, to be honest, you have chosen to head to the right direction. Swala la imani ni imani tu, no one should be aloowed to question it, and those who do will be punished. Zaidi ya hayo watu wanatakiwa kuweka mipaka kati ya kungombea umiss na kuwa barozi wa beer. I think I am loving u for that one.

 97. natasha Says:

  ushauri wangu kwa nasreen kwajiri nampenda sana,aige ile comfidence kama ya angela ityamsaidia sana kwasababu tayari ni mrefu na si mbaya.

  vilevile kamati ya miss tanzania ishirikishe angella kumjenga nasreen,ndio najua angela ni mdogo sana ki umri lakini alikuwa amejenga hari ya ushindi kitu ambacho watanzania wengi hatuna hasa katika umri wa ma miss wetu hawa.

 98. Tatizo watu wengi mna toa maoni tu yakufuraishana,yule angela kwa sis ambao tulikuwa tuna mfatilia tokea miss changombe ana mambo mengi sana mazuri ya ushindi.(kujieleza,kujiamini,hari ya ushindi na mingineyo).

  kama kamati ya miss tanzania ikiyachukua mambo hayo aliokuwa nayo angella na kumjenga nayo nasreen basi atafanya vizuri sana kwenye miss world kwa sababu yeye tayari ni mrefu which is good na sio mbaya wa hivyo kwa sura.

  haya ndio mambo ya msingi ya kuyaangalia.

 99. josefini Says:

  go angella go,big up

 100. gein Says:

  big up sis angella


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s