BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ODEMBA NA WANJALA August, 13, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:03 AM

Hii ilikuwa wakati yule mkali wa Dancehall,Shaggy,alipotumbuiza jijini Dar hivi karibuni.

Advertisements
 

79 Responses to “ODEMBA NA WANJALA”

 1. binti-mzuri Says:

  rashida shosti wangu,how good you look.miss u

  kwakweli wamependezaaa,no lieee….. bongo mabinti wazuri wazuriiiii….tena wanajitambua.big up

 2. any Says:

  odemba kafanana na mimi enzi nikiwa kijana!

 3. kwikwi Says:

  napenda smile ya odemba sana, bado upo juu mamii..
  rashida kama kawaida yako hukosi mishe mishe….hahhahaha

  salimia sana A….

 4. Pearl Says:

  any usiniambie na wewe ndo una weusi mzuri hivyo!!!!????
  umeshaniuzi any,kwanini hukutoka ukashiriki face of tz!!!?? mwaka huu shirika sisi wana bc wote tutakupigia kura usijali.

 5. trii Says:

  wapo natural less make-up,face colour sawa na body.

 6. Matty Says:

  Kwa kweli warembo mnawaka na mnavutia na mnajitambua kama mimi na Binti-mzuri aisee si mchezo!

  Any basi hata wewe unafanana na mimi maana nishafananishwa sana na huyu dogo!

 7. shwangwa Says:

  acha sifa uwe na sura ya odemba utambe

 8. pretty girl Says:

  mko poa mmetoka ktk bonge la pozi.safi sn inaonyesha jinsi gani mnajua kujichanganya na washkaji.nimewapendaaaaaaaa

 9. Gervas Says:

  Afu we Any kumbe mtundu!!

 10. any Says:

  Wee shangwa acha mtoto, read btn the lines nimesema nilipokuwa kijana, so not anymore, U just need to grow up al lil bit upstairs.
  Kweli Matty sio utani, alipoanzaga kuonyeshwa kwenye tv with short hair and less /no makeup, kuna watu walinifananisha nae. so sijui kama walikuwa wakweli au walijisemea, ila habari ndio hiyo!
  Matty ukute tuna ukoo! hahaha.

 11. any Says:

  Pearl sio siri nina weusi wa kutosha, no cream no nothing! nikipita Kariakoo wale vibega wananiita RANGI ADIMU MAMDOGOOO! usiiharibu. naishia kucheka tu. ila siku hizi ndio angalao tunatambulika kuwa wenye rangi yetu ni wazuri pia, zamani ukiwa mweusi hakuna anaekuangalia, hata mtu akijifungua kitoto cheusi hakabebwi na jirani, habari ndio ilikuwa iyo! sasa not anymore, watu wana appreciate black mpingo! hahah

 12. any Says:

  Pearl natamani kushiriki ila kigezo cha umri ndio kinagomba apa! kungekuwa hakuna age limit aah mngeniona.

 13. Binti-mzuri Says:

  Matty news ndio hizo,wa kumliza na limlize.Sio siri bongo mademu bomba,uzuri damu damu.

 14. Guyle Says:

  this woman is beautiful and she was the 1st in Tz to show girls they can make it to the big stages of the modelling world. Tatizo lake alikuwa mbishi, kiburi na hasikii. Not exercising enough or sticking to the healthy diet she was put on.
  Waligombana sana na marehemu Amina who was looking out for her ye akawa anaona anambana. Kaenda south only to end up losing her contract. I hope she’s settled down now and doing well. Still looking lovely!! Wish her all the best

 15. Pearl Says:

  any mi nakukubali hata kama umesema age inagomba.

 16. Matty Says:

  hahahahahahaha Any, kwakweli hizi rangi zetu ni adimu lazima tujivunie!! no mkorogo kwa kweli!lakini mimi sina ublack mpingo sana!
  Shwangwa unaumri gani??? maana nimeshindwa kukuelewa ulipohoji mtu kufanana na Odemba…kwani watu hawafanani???hata ww unaweza kuwa umefanana na mtu yyt yule haijalishi cheo,umri,uwezo n.k

  BC kuna shindano la walimbwende waliokwenda age, na inabidi tumpate mrembo mmoja ambaye atakuwa kisura kuliko wote!hala hala jamani msikatae matokeo nitakaposhinda mimi au Any teth teh teh te tetetetetette!!!!wakereketwa wanaweza shika mabango khaaaaaaaaaaaaaaa!!!

  Kekuu i hope utashiriki maana hili halitaangalia age wala umbo nadhani vigezo viwe mvuto kuliko ule uwembamba zaidi maana tulio wengi tushajiachia vya kutosha mihips na miwowo ndo balaa!
  washiriki mjitokeze jamani…Binti Mzuri uko wapi??Pearl upo?

  warembo juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!

 17. binti-mzuri Says:

  guyle na kweli,she messed up.nasikia yupo na asian contract sijui at the moment..uchina.am not even sure

 18. adakadabra Says:

  any Says: August, 13, 2008 at 5:21 pm
  odemba kafanana na mimi enzi nikiwa kijana!

  MTAACHA LINI KUJIFANANISHA NA WATU AMBAO SIO NYINYI.ACHA USHAMBA. BADALA YA KUJIELEZEA MWENYEWE,UNAJIFANANISHA NA WTAU

 19. kahindi Says:

  hata mimi mzuri bwanaaa

 20. any Says:

  Matty nimemshangaa Shwangwa! eeh huwezi kufanana na Odemba, kwani Odemba si binadamu! saa ningesema nafanana na lizard ingekuwaje.
  Matty tutashiriki, walete hizo form mi najaza, ila kusiwe tu na rushwa ili kushinda, na pls atakaeshinda ndio chaguo la kamati ya BC, NO COMMENTS, NO COMPLAIN! na mshindi akibandikwa humu BC wafunge ile option ya comments, watu wakalilie vyumbani mwao, chaaaaaaaaaa!
  Matty, kekue uchukue na Pearl mchukue form na wengineo.
  Apo ni kizaa zaaa wachaga na wahaya kwenye mashindano, bila kusahau tangakunani.

 21. Binti-mzuri Says:

  Hahaha we kahindi,binti ulipotea..mbona unaanza kuleta majungu before kambi.yani i can imagne,itakua kama episode ya americas next top model.i wonder amina nae yuko wapi.hii miss/mrs BC mbona ni bonge la opatyunite mabinti kushine. Apo shalo tina tina,2takutana boot camp matty,michelle,solange,sally,kina vibeyonce etc na bila kuwasahau wake zake dunda galden..kazi ipo. Usisahau kum2mia mama wa kichaga form,na self-adressd envelope ya majibu..lol

 22. Matty Says:

  hahaahahahahahahahah jamani sipati picha hili shindano la mlimbwende wa BC,maana ni mchuano mkali kati ya makabila makuu kadhaa sikwambii hapo unikute mtoto wa BK nikiwa na swimming cost jukwaani mguu wa bia ni balaa ukija wowowo ndo usiseme, colour sasa sikwambii mashauzu sasa hahahahahaha!wenye donge wameze wembe!
  Tukienda Moshi kwa watani zangu mh!sijui itakuwaje maana tunao walimbwende wengi sana wenye vigezo na maringo ya haja plus ung’eng’e wa kutosha kwenye kujibu maswali majaji kazi watakuwa nayo!
  Pale Tanga Kunani sasa mchuano upo kati ya Amina na Binti Mzuri maana hawa ndo hata mimi wananitisha kidogo na wengineo jamani mjitokeze!
  Upande wa pili wa pwani ya bwagamoyo wake zake Dunda Galden mpo???
  Mikoa ya Kusini,Mwanza na Kati idodomya jamani uwanja ni wenu na form zinapatikana hapa hapa BC, ni hiari yako kushiriki au kutoshiriki!
  Linda na Pearl shosti zangu vipi upande wenu???au Yesu hapendi haya mashindano???

  Na ni vema atakayeshinda asirudishe Taji, jamani pls pls warembo msikatae matokeo yatakapotoka!!!!!!!!hahahahahahahahaha ni balaa watu wataanza kuponda aliyeshindwa!

  Majaji nadhani bora wawe wanaume coz wanawake kwa kuoneana wivu ni balaaa au mnasemaje washiriki wenzangu???ndio mzeee!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Mwisho kabisa nawatakia wknd njema wote!

 23. any Says:

  adakadabra wee ndio mshamba, bado tu kujitwisha mgomba ndo ushamba wako ungekamilika! kwani Odemba Mungu? ni mtu wa kawaida tu, and for ur info hatukumtambua hadi alipotokea face of africa. Mbona kuna zaidi yake wako kijijini, sema tu hizi agencies hazipiti kijijini!
  Yes nimefanana na Odemba, kama hutaki meza piritoni zitakusaidia usingizi.
  Unataka nijieleze nini kuhusu mimi zaidi ya nilichosema kuwa kafanana na mimi!

 24. any Says:

  nyie watu mbona mme edit msg yangu kwa adakadabra! nimemaindi. mngeweka yote.

 25. any Says:

  MATTY MSAADA TUTANI, NAOMBA SUMMARY YA SAKATA LA KURUDISHA TAJI MISS REDDS! NAONA POST ZISHAFIKA TISINI NA KITU, NIPE SUMMARY, MACHO YANGU YASINZIA KUSOMA.

 26. Binti-mzuri Says:

  Heh nyie watu vipi,mbona mie nafanana na beyonce..matter of fact yeye ndo atakua kafanana na mie.i heard my behind is bigga.haya,anaejiskia ‘ataweza’ anianze. Watanzania inabidi muanze kupractice confidence and self-apreciation..eti ukijiita mzuri mara oh we kipofu,oh unajisifia,oh mshamba. Niacheni,kwani ni nyinyi?ntabakia na ushamba wangu wa lushoto na mi self esteem juu,and that my friend,is the greatest gift of all. So mwacheni huyo any,wether its true or not,shes the one living with it.

 27. Pearl Says:

  any ,matty mie ntashiriki ila nahisi mchuano utakuwa mkali,manake matty unao mguu wa bia na mie pia ninao,Mungu hakuninyima shepu upo hapo dada,nywele zinamwagikia,heheee kazi itakuwepo because na shule nayo nimeenda, any hapo unasemaje!!!!???

 28. kekue Says:

  Watt ni wazuri na ninawakubali, ss wenzangu hapa naona ni weusi tu ndo unatake place ss cc weupe tusemeje, ina mana wewe any, matty, binti mzuri,pearl na wengine mnaojitambua kuwa ni wazuri wote ni back beaty au??? coz kama ndo black wote mi sitashiriki msije sema nimependelewa. Hahahahahahahahaaa.

 29. Matty Says:

  adakadabra unaishi ulimwengu wa ngapi??? eti ushamba kufanana na mtu we vipi wewe unabahati sana BC wanabanaga baadhi ya magadhabu ya watu!

  Any ahhh hata mimi sakata la mlimbwende kurejesha taji naona lishanichosha maana watu wanamlaumu dogo na personal decision zake sijui kwanini swahili pipo!

 30. TRII Says:

  sasa mwenye pua kama ngumi inakuwaje?watakuwa na nafasi.

 31. dina Says:

  Dada Any, hizo sifa unapata Kariakoo tu? Hapo umentia mashaka!

 32. Matty Says:

  Jamani hili shindano la MISS BC a.k.a MRS BC mbona warembo hamjitokezi??? au ndo ile ishue ya mvuto not richabo??
  hahahahahahahaha warembo waliokwenda age jitokezeni bana kwani kushindwa pia ni moja ya chalenjizi hahahahahahaha
  -Michelle huchukui form???
  -Ma’reen uko wapi??
  -Tri best ni aje??
  -mama wa kichaga pls usituangushe!
  -Kekuu uko bomba pls njoo utupe changamoto
  -Any na Binti-mzuri pls msiniangushe
  -Pearl shost form ziwazi
  -Amina najua uko taiti ila usikose pls
  -sikujua Doto mamdogo usikose kushiriki
  -blackmannen beauty pls mchuano wenyewe ndo huo
  -Linda bibie ni aje ??utaparticipeti?
  -Sally jitokeze mwaya
  -Kahindi best usikose
  -Ramla natumai utatuwakilisha pale bmy

  wengine sina uhakika kama ni she/he bora mje kujiandikisha wenyewe.

  Msisitizo unabaki kuwa atakaeshindwa jamani chonde chonde asikatae matokeo hahahahahahahahaha msijeanza ohhh hana vigezo, uso mrefu,black sana mhhhhh jamani hiyo itakuwa siyo issue!

  Kwenu majaji.
  -upendeleo haufai ktk shindano hili la kiutu uzima
  -no rushwa ya aina yoyote ile

  habari ndo hiyo!

 33. Matty Says:

  hahahahahaha Dina nilikusahau best chukua form…ila wewe ni Dina yupi lakini??maana kuna kina Dina wengi ninaowajua!

  Tri, hilo shindano halina vigezo maalumu nadhani hata wenye hizo pua kama michael jakisoni wanaruhusiwa tu !

 34. any Says:

  Wee dina acha ushamba, unadhani Kariakoo wanaishi nyani au watu? wale pia ni watu regardless of their economic status! they have brain just like any other human being! unafikiri kwa vile vibega ni maskini hawawezi jua kipi kizuri na kipi kibaya? au rangi ipi nzuri au ipi mbaya? Grow up and stop judging people according to their socio-economic status! aah!

 35. binti-mzuri Says:

  wewe matty,blackmanen dume la mbegu,utaja sutwa mpenz…hahaha umenichekesha aisee…afu umejuaje sikujua doto ni mke?we una vituko walahi

 36. any Says:

  pearl wee chukua form mambo ya mguu mnene, tukiona mnakaribiana sana kwenye vigezo basi tutaweka tape measure kupiga unene wa mguu.

 37. ms Says:

  lukn gud 4 sure
  ila kwa mbaaaaali namuona mwanangu mmoja wa kitaa ebwana poa bro kweli uliruka ngoma si mchezo

 38. Leila shakum Says:

  Its good to live a fantasy world. To all of the above,be confident in your own skin, urembo,kujiachia wazi hauleti maana nzuri to minors. Be positive,sio lazima ufanye hivyo ndiyo uprove wewe ni mzuri. Kwanza kuna tofauti kati ya uzuri na mvuto.

 39. Matty Says:

  heheheheheh Leila Shakum ingia kwenye mchuano tukuone maringo yako bingili bingili mpaka chini usinichekeshe …udinilaizesheni huo!

 40. Pearl Says:

  kekuu unadhani basi hata mie ni mweusi best!!! ila ntajitokeza tu.
  Haya any nini tena mbona unapandwa na jazba kwa haraka hivyo shosti!!!?? inawezekana dina alimaanisha vingine,hebu tumsikie.

 41. Matty Says:

  mamaaa Binti-mzuri usiniambie ….niombee msamaha kabisa kabla hajashtukia mwenyewe shosti mbona nitakuwa mdogo kama piritoni!

 42. ma'reen Says:

  Matty bwana bado nambembeleza shemejio aniruhusu kuchukua form maana ana wivu si kidogo na kulazimisha asichotaka siwezi kungwi atanigomba ha ha ha! Otherwise sifa zimetulia kinoma, waosha vinywa wenyewe watakaukiwa maneno!

 43. trii Says:

  Mwenzenu naogopa kupita na kichupi,ikifika wakati wa kichupi mi sitapita au nitakuwa nimevunja kanunu???form zinzpztikana wapi???

 44. dina Says:

  any, that’s where u missed the point sweetie…..Maana ni kuwa charity begins at home, mtaani kwako ndio waanze kuona hiyo rangi, unless Kariakoo ndio unakoishi (na kama unapoishi ni Kariakoo, then I take back my words). And the message has nothing about judging people according to their socio-economic status….

 45. dina Says:

  Eeh BC nimekuheshimu, wewe kweli ni mlinda amani…ume-edit eeh..BIG UP ANYWAYS!!!

 46. any Says:

  Dina,. I didnt miss the point, umesema nakutia mashaka kama napata komment from from Kariakoo tu! apo mwenye akili ya kupambanua atajua what u meant! so hakuna kuremba ulichosema ndio ulichomaanisha na mimi nshasawazisha, so game drooo!

 47. Mama wa Kichagga Says:

  Haaaaaaaaaaaaaaaaaa nilikuwa sijapita hapa. Any umenichekesha.

  Mimi hapo kwenye mashindano “HAPANA” kwani mabinti zangu wananiwakilisha. Labda niwe jaji ila mmmmmmmmm siangalii sura wala sipokei rushwa hivyo patakuwa hapatoshi hapo.

  Mkinichagua kuwa judge mjue nitaanza kuwaengua mmoja baada ya mwingine:

  1. Aliyewahi kutukana hapa nje (hakuna kupata form)
  2. Mwenye mawazo ya mrengo wa kushoto nje
  3. Asiye heshimu makabila au dini za watu wengine nje?
  4. Shotii wao nitawaruhusu kushika vibendera na maua ya kushangilia
  5. Urefu wa kuanzia 5″+
  6. Kima kichwa imejaa uji utapata maksi 1 tuu ya kushiriki
  7. Kama huna mipango endelevu ya ulimbende wako 2
  8. Kama una minyama ilyo legalega shingoni, mikonono , miguuni na penginepo tafadhali usichukue form maana utatuharibia mtizamo wa jamii kuhusu afya (kwani nani alikudanganya kuwa mtu mzima ni kuvimbiana bila fomula?)
  9. Mengineyo kama kamati teule itakavyoamua.

  Kazi kwenu, msiponichagua basi nitakuwa mtizamaji nambari 1

 48. Matty Says:

  Kudadadeki mpambano kumbe bado unaendelea na warembo bado wanajitokeza naimani kesho ndo mwisho wa shindano na lazima mmoja awe mshindi tu piga ua!

  Ehhh Ma’reen kumbe habari yenyewe mpaka uombe ruhusa khaaaa anawivu sana bwan’shemegi yetu inaelekea!

  Trii Form zipo hapa hapa kwani huzioni??? hahahahahaha labda computer yangu inavioo viwili.

  Dina Bimkubwa tuliza kitenesi uliyeanza ni wewe Any amemalizia hahahaha habari ndo hiyo!

  Wanawake wapenda maendeleo jitokezeni nadhani mwenyewe kasikia na sms delivery.

  well, KESHO NDO KILE KINYAN’GANYIRO CHA MLIMBENDE ALIYEKWENDA AGE HAPA BC MBONA HAPATATOSHA!

  Bc pls samahani sana tuache tumalize huu mpambano wetu ili tumjue mrembo wa BC USIBANIE HII PLS.

 49. Matty Says:

  Trii mguu hauruhusu nini???hahahahahaha hata huo ruksaaa!

 50. Matty Says:

  Hahahahahahaha daima huwa naheshimu mawazo yako dadangu Mama wa kichaga na kwakuwa umetuambia wanao tutachuana nao nadhani ni vema wewe ubaki kuwa jaji mkuu hahahahahahaha usiangalie sura kama ulivosema na vigezo ndo hivyo ulivyotaja nadhani mimi ndiye mrembo wa BC nipo serious jamani!

 51. any Says:

  AMEN MATTY!

 52. dina Says:

  Hee, any kumbe unashindana! Ndio nimeuliza kama sifa zinatoka Kariakoo tu, upande unakotoka/unakoishi wewe hazitoki? sasa kilichorembwa hapo kipi? na kwa nini nirembe kama swali langu ndio hilo? anyway sis, hamna kuchajiwa kodi hapa uko huru kulonga… ila shosti kama rangi imetulia mtaani pia wangeona…uongo?

 53. kahindi Says:

  binti mzuri nilikumis sana…..nipo shost ila ubize tu wa kazi….niambie je ushachukua form?..mwambie matty nampa hi…na kwa taarifa yenu ni kwamba taji ni langu hilooo.na kigezo cha mguu kiwe cha kwanza.maana miguu yangu ni balaaa…

 54. trii Says:

  mi hadi hapo najitoa manake watu wamezidi kunitisha,na mi najua Mama wa Kichagga atapendelea tuu watoto wake,kama vipi hairisheni hadi wiki ijayo ili nipata nafasi ya kwenda bagamoyo,tanga na sumbawanga,msiulize kufanya nini.

 55. Matty Says:

  Poa Any…

  Dina unajazba ya nini mtoto wa kike???chukua form ujaze bibie mchuano ni leo!

  Kahindi poa nimekupata! nadhani mchuano ni mkali kama unavigezo basi tuwaachie majaji wafanye kazi yao…na jaji mkuu ni Mama wa Kichaga!habari ndo hiyo!
  pls pls jaji mkuu tupe matokeo maana wengine hatulali tunawaza shindano tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 56. trii Says:

  Matty ulijuaje miguu problem to me.ngoja nikupe kidogo upeo nilivyo,Nitatumia ABCDEF kama marks za shule.

  Face-B+
  Body-A
  miguu hapo sasa E
  Hips–B
  Lips A
  Mashavu–c
  Pua–C
  Nywele bila weaving B
  Kucha za mikono B za miguu D.

 57. any Says:

  Ndio maana nikasema mwanzoni kabisa kuwa ulimaanisha, kuwa kariakoo ni kwa low class ivo hata wakisifia hawaelewi kama wale wanaokaa kwenye low density areas! na hii imethibitika leo kwa saa hizi ulivojieleza (dina Says: August, 20, 2008 at 11:23 am ). Just for ur lil information ndio nitashindana, na ni kweli sifa nimezipata Kariakoo tu, is that a sin mtu wa Kariakoo kukusifia? Do you think the person from Kariakoo alieniona nina rangi nzuri is crazy simply because he doesnt belong in the so called high class residential area!
  Na kwa kumalizia na kukutoa wasiwasi, Yeah, I live in Kariakoo and I am happy to be there! Kwani ni dhambi kuishi Kariakoo? kwani wanaoishi Kariakoo wana macho mgongoni, au ni hizi kasumba za ubaguzi tulizo nazo kuwa wenye nacho wanatakiwa waishi sehemu fulani na sisi tusio nacho tuishi sehemu fulani.
  Oh my Gosh, nilidhani wabaguzi ni wazungu tu, kumbe hata sisi kwa sisi wabaguzi, mtu unabaguliwa au kufikiriwa uzuri wako depending on your socio economic status, which is VERY WRONG!
  Matty vipi bana kamati ishakaa kwani?, maana mi nataka siku ifike niingie JUKWAANI KWA RAHA ZANGU! and the good thing is form hazjaandikwa kuwa kama umetoka KAriakoo huruhusiwi kushiriki. MI NTASHIRIKI kwa HALI NA MALI!

 58. any Says:

  NDIO DINA, SIFA ZINATOKA KARIAKOO TU, MAAANA THATS WHERE I BELONG, IMPLIEDLY, BORN AND RAISED THERE. APO VIPI? APO SAWA SASA? I HOPE UTATA UMEISHA, NAONA UMESTUSHWA NA MTU KUISHI KARIAKOO, WHY? UKIPITAGA HUKO BAHATI MBAYA UNAISHIWA OXGEN KWANI? JIBU NI NO, SO KAMA KUNA OXGEN INA MAANA KUNAFAA KUISHI WANADAMU.

 59. any Says:

  PIA DINA KAMA WEWE UNAISHI MAENEO YA HIGH CLASS NA HUJASIFIWA USIKATE TAMAA, HAINA MAANA WEE SIO MZURI, WATU WANAOISHI HUKO WAKO RESERVED KUCHUNGA STATUS NA JAMII ISIMWONE MBAYA KUSIFIA WATU NJIANI ASIOWAJUE. WEE JIMUVUZISHE KARIAKOO SIKU MOJA SHASHAAAA UTAJIONEA MAMBO, WATASEMA KAMA UNALIPA MAAANA WALE WANA GUTS NA WANASEMA WANACHOKIONA RIGHT AWAY, KWENYE MA HIGH CLASS HUKO SI RAHISI MTU FROM NOWHERE AANZE KUKUSIFIA HAKUJUI WALA NINI. SI NDIO MAMBO YA CLASS TENA.

 60. Matty Says:

  HABARI NDO HIYO NA SMS DERIVELY….UNLESS OTHERWISE SHE NEED MORE CLARIFICATIONSSSSSSS!

  Tri best wala usitishike na hii miguu yangu ya bia unaweza shinda tu no matter mguu kama penseli hahahahahaha (jokes) ila umenichekesha eti upate walau chance ya kuelekea pwani na sumbawanga khaaaaaaaaaaaaaaaa hivi mpaka leo bado watu wanatumiaga zile tunguli kushindana????? enzi zetu ilikuwa hamna aiseee nio kujiamini tu!

  Any shosti,kamati nahisi ishakaa ikapanga mipangilio yake sasa mchuano ni baadae kidogo atakaeshindwa jamani pls asianze longolongo zake hapa hahahahahah

 61. binti-mzuri Says:

  kha,watu mnakeshaga humu e,sijaja siku 1,its chaos

  kahindi bibie,mi nakupigia debe, tutoke top 2.lol…gari na kitita cha fedha twende zetu kutalii hukooo kigamboni..kipepeo. sie na mista wetu… familys day out

  Leila shakum jamani my dear, have a sense of humour. you are too serious.

  ujumbe wa wiki: bora ujisifie mwenyewe,bongo nuksi nyingi

 62. dina Says:

  Any mpendwa, mbona unasema maneno mengi ambayo wala hayakuhitajika? Sio nia yangu kufanya sehemu hii kuwa ya malumbano, lakini wewe ndio unachofanya. Re-check my comment # 44 kuwa kama unakoishi ni Kariakoo, then I take back my words, kwa sababu huo ndio mtaa wako, sasa where are all those comments abouts high classes and whatever coming from? Poa moto sista, and be confident of urself, usinitake niamini kuwa you have an inferiority complex, its not good for you. And I NEVER REFERRED KARIAKOO TO BE WHATEVER U WROTE IN THIS BLOG. To make ur mind rest, siishi hata jirani na huko unakokuita high class…relax…..
  Nimehitimisha, and hopefully the subject will be closed, am sure the blog is meant to reduce our life stresses and not otherwise….friends? au bado?

 63. dina Says:

  You even got me wrong nilivyouliza unashindana? I said that from your comment # 46..something about ngoma droo…ndio nikauliza kumbe unashindana? And I never meant to criticize your participation kwenye shindano la BC, relax mpendwa, no hard feelings at all…..

 64. Matty Says:

  Mchuano umekwisha na top5 ni hii hapa.

  1.ANY
  2.MATTY
  3.BINTI MZURI
  4.PEARL
  5.MA’REEN

  Samahanini wapendwa habari ndo hiyo naomba tukubali matokeo!!

  JAJI MKUU alonga….
  -Mrembo Any alikuwa na mvuto kuliko wote hasa rangi yake ya ngozi na shepu pia.
  -Matty alipishana kidogo na Any ikabidi aende no.2
  -Binti-mzuri huyu sina usemi anavutia ila matokeo ndo hayo
  -Pearl anauwezo mzuri sana wa kujieleza hivyo kawa 5
  -Ma’reen hakuachwa mbali sana na hao warembo hapo juu

  ZAWADI
  -zitatolewa new year if God wishes

  MAJUKUMU YA WAREMBO
  -nadhani ni bora warembo walioingia 5bora wajitahidi kuwa ni mfano mzuri kwa jamii hii ya BC hasa watu wanapolumbana wao wajitahidi kuzuia sakata hilo ili kuepusha Airpollution in our ground, vile vile tutakuwa tumemsaidia hata Jeff mwenyewe kuflash some typical verbal.

  MWISHO KABISA.
  -Nawapenda wote na sorry kwa yeyote aliyekwazika ktk kipindi hiki cha mchakato wa kumpata mlimbwende wetu!

  NI HAYO TU!

  ATAKAYEPINGA HAYA MATOKEO PLS ATAJE TOP 5 YAKE NADHANI ITAKUWA YA MWAKA UJAO HIYO!!!!!!!!!!!

 65. any Says:

  Matty? haya wee. tusubiri watu waamke.
  dina, peace, i am done.

 66. binti-mzuri Says:

  matty ntakua nilichapia kujibu swali..si unanijua tena mie

 67. matty Says:

  Any, acha waamke na wakiosha kinywa TOP 5 ipo kwa ajili yao!
  Binti-mzuri eeeh mamyyy niliona ulivyochapia kujibui swali ila nakupongeza kwa kuingia top 5.
  wknd njema jamani! na hivi leo ni sabato day!

 68. Mama wa Kichagga Says:

  Nikiwa kama Jaji Mkuu nayakataa haya matokeo moja kwa moja!

  Mpambano unaendelea na bado tupo tunapokea fomu za washiriki, sasa sijui Matty kaota na kuanza kutangaza matokeo hewa? Mie sijui. Maadam mliukubali uteuzi wangu wa kuwa jaji tena mkanipa kuwa jaji Mkuu nasema hivi;

  “Mimi kama Jaji Mkuu wa mashindano haya , nabatilisha uteuzi uliofanyika na natangaza upya kuwa mchakato unaendelea”.

  Shindano litafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 30/8/2008 kuanzia saa 12 jioni pale Ubungo Plaza. Tafadhali majaji wengine 2 tuwasiliane pamaja na Matty ili tuwekane sawa maana Matty yeye huyo huyo mshindani, Jaji, msemaji na mtoa taarifa Mkuu? Tafadhali sana Matty chagua nafasi moja ili tukuelewe.

  AGIZO:
  1. Washiriki watume maombi yao upya kwa Jaji mkuu hapahapa BC
  2. Maombi yaambatane na vipengele vifuatavyo:

  a. Kwanini unagombea nafasi ya miss BC na nini malengo yako ya Sept 2008 – Aug 2008 hapa BC?

  b. Kwanini wewe upewe nafasi hiyo na sio mtu mwingine

  c. Elimu na ngazi uliofuzu

  d. Nini mtizamo wako ktk masuala ya jamii na changamoto zilizopo

  f. Uwe na wadhamini 2 mmoja wapo atoke hapa BC

  g. Toa urefu ktk cm au mita na uzito ktk kg kwa ajili ya uchambuzi wa afya (Kipimio cha BMI).

  h. Maelezo ya kutokataa taji na iwapo ukikiuka hili uwe tayari kulipia fidia ya maandalizi ya shindano.

  ANGALIZO:
  1. Elimu sio kigezo cha kushinda ila kinaongezea sifa ya mshiriki (Mangi sina hakwenda shule ila kichwa ilikuwa bongo tupu, bibi zetu hawakuona shule ila maisha yao ni bongo tupu)

  2. Kuwa na mguu sijui fito, bia, soda, sinzano, sijui urefu wa nchi tatu nk sio kigezo cha mashindano haya, ili mradi mshiriki anajiamini na anajua anachokifanya.

  3. Kama huna elimu ila unajiamini, wajua unachokifanya na unaweza kujieleza kwa lugha yoyote ile hasa Kiswahili usihofu kwani linapokuja suala la lugha ngeni kutakuwepo na wakalimani wakutosha siku hiyo. Uwezo wako wa kufikiri na uelewa wa mambo ndio utakaofikiriwa katika kuupata ushindi.

  Karibuni kumuvuzisha CV zenu za ushiriki hapa. Nasisitiza mashindano yatakuwa tarehe 30-8-2008 saa 12 jioni hapa BC na mshindi atatangazwa siku hiyo hiyo.

  Narudisha ligi kwenu washiriki ktk mchakato huu wa kumpata Miss BC 2008 na HAKUTAKUWEPO NA UPENDELEO KWA KIUMBE YEYOTE KWANI HULETA MADHARA KWA JAMII NA KUWANYIMA WENYE UWEZO NAFASI ZA KUSHIRIKI MAENDELEO KWA MOYO.

 69. Matty Says:

  mhhhh Mama wa Kichaga ulikuwa wapi lakini????sikukuona mda mrefu na ulijuaje kuwa matokeo hayo niliyaota???…anyway ngoja kwanza nikumbuke nilipoweka CV yangu kisha nakuja kuchukua form!! na pia nataka ujue kuwa mimi ni mshiriki nambari one!!
  Any,Binti-mzuri,Pearl,Ma’reen mko wapi???niliota matokeo mashosti zanguni…Jaji mkuu katanabaisha kuwa shindano ni 30th Aug jamani vigezo vimewekwa hadharani wapendwa mpo??hahahahahahaha!

 70. any Says:

  Mi na appeal.

 71. any Says:

  hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! hiyo essay apo juu imeenda shule.

 72. Matty Says:

  Kwako Jaji mkuu,hivi mfano washiriki wasipojitokeza wat do you think?maana siwaoni wakijaza form hapa zaidi yangu mimi na Any…anyway ngoja tuwaache na wao waseme!

  Any mwanawane lazima tuchuane!

 73. any Says:

  hamna aliejitokeza ivo mi na matty tumeshinda, Mi wa kwanza na matty wa pili!

 74. Mama wa Kichagga Says:

  Tutajua siku hiyo ya shindano! Maana hata nyie naona mwasubiria kuwasiliasha maombi yenu saa za majeruhi na hiyo inaruhusiwa pia.

  Washiriki wasipojitokeza , itabidi tufanye mjadala mkali ili kurekebisha mambo ili next time watu wajitokeza kushindania taji badala ya kutuzuga oooooooooo nina sura nzuri ooo mguu wangu sinzano oooooooooooo kibao! Kumbe vigezo hakuna.

  Haaaaaaaaaaaaaaa ni vijimambo tuu hivi siku zinasogea

 75. Matty Says:

  habari ndo hiyo! Any…hakuna mwenye vigezo zaidi yetu hahahahaha acha tuwakilishe BC!

 76. Matty Says:

  hahahahahahaha Mama wa Kichaga umeniacha hoi khaaaaaaaaaaaaaaa mguu sinzanooooooooooooooooooooooooooooo hahahahahah
  pls itabidi uweke hadharani email yako nikutumie picha yangu unione navyobamba mitaa ya kati aluuuuuuuuuu!

 77. Mama wa Kichagga Says:

  Kwakuwa hakuna mshiriki aliyemuvuzisha cv yake , mashindano haya hayakufanyikakama ilivyopangwa. Aidha shindano hili limesitishwa hadi mwakani kuwapa washiriki muda wa kujiandaa vema.

  Matty kajiandae na cv na hakikisha sijui mguu wa sinzano au pepsi unakuwa tayari kwa mashindano mwakani. Nakirudisha kiti kwenu salama.

  Asanteni kwa kunichagua.

 78. Amina Says:

  bwana acheni kujifagilia…nasisi weupe je watu wa tanga?namiambieni acheni kujifagilia

 79. Matty Says:

  haya tushajifagilia sasa unasemaje?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s