BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MORY KANTE- YEKE YEKE August, 14, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:42 PM

Mambo vipi? Wiki ilikuwaje kwa upande wako na umejiandaa vipi kwa weekend?Tunatumaini kwamba wiki ilikuwa nzuri na umejiandaa vyema kwa mwisho wa wiki muda ambao wengi huutumia kwa kupumzisha kichwa kidogo,kutembelea ndugu,jamaa na marafiki,kuhudhuria harusi au kwenda kwenye kikao cha harusi ya mshikaji kama sio kikao cha kifamilia nk.

Kwetu sisi hapa BC,mambo ni kama kawaida.Tupo kwa ajili yako huku tukiendelea kukushukuru kwa kututembelea ili kubadilishana nasi mawazo bila kusahau wasomaji au watembeleaji wenzako,kupata habari mbalimbali,kuburudika nk.Ni watu kama wewe ambao wanaifanya BC kuwa mojawapo ya blog za kitanzania zenye watembeleaji na wachangiaji lukuki na huku idadi ikiongezeka siku baada ya siku.Shukrani sana.

Kama ujuavyo,jadi ya BC ni kwamba Ijumaa huwa ni siku ya burudani.Baada ya wiki nzima ya mihangaiko isiyoisha tunadhani ni muhimu mtu ukapata japo muda wa kupumua kidogo.Leo tumeamua tukuhamishe kidogo mpaka kule Afrika ya Magharibi. Kule tunakutana na mojawapo ya magwiji wa muziki barani Afrika. Jina lake anaitwa Mory Kante.Kama utakumbuka,kunako miaka ya mwisho ya themanini,wimbo wake uliojulikana kwa jina la Yeke Yeke,ulitokea kuutikisa ulimwengu wa muziki sio tu barani Afrika bali pia barani Ulaya.Ilikuwa kila mtaa unaokatiza utasikia watu wakiimba Yeke Yeke.Raha zaidi ilikuja pale mabingwa wa “tungo” wa enzi hizo walipokuwa wanaingiza maneno yao wenyewe.Sitaki uanze kuniambia wewe ulikuwa ukitia maneno gani kwenye wimbo huu kwa sababu najua tukianza hapa patakuwa hapatoshi!Mbali na hilo la watu kutia tungo zao wenyewe, siwezi kushangaa ukiniambia kwamba wimbo unaukumbuka lakini ulikuwa hata hujui nani aliuimba achilia mbali kwamba anaimba kuhusu nini.Hapo ndipo utakubali kwamba music is the only true universal language.

Mory Kante alizaliwa tarehe 24 Februari,mwaka 1950 huko Kissidougou nchini Guinea. Hata hivyo,akiwa na umri wa miaka 7 tu alipelekwa nchini Mali ambako ndiko alikojifunzia muziki ikiwemo kutumia chombo cha muziki kiitwacho Kora. Huko Mali alikutana na kuimba pamoja na gwiji mwingine wa muziki barani Afrika,Salif Keita,ambaye waliimba pamoja katika Rail Band.Kibao chake cha Yeke Yeke ndio kibao cha kwanza kutoka barani Afrika kuuza zaidi ya kopi milioni moja barani Ulaya.Pata burudani.Wikiend Njema.

Advertisements
 

16 Responses to “MORY KANTE- YEKE YEKE”

 1. Saad Says:

  Nashukuru kwa kumuweka mtunzi wa wimbo huu!!!! Umenukumbusha mbali sana na umenikuna mno. big up mzee

 2. P Says:

  kikuku kunanukiaaa na kikuku kinanukiaaah nani kapika leo yekete shua yeke yeke, umenikumbusha mbali enzi hizo navizia soda kwenye sherehe za watu (naona hata aibu),
  nashukuru kwa kuwa leo nimejua jina la mwimbaji
  wish u a nice weekend kama mlivyoianzisha yangu leo

 3. Gervas Says:

  inanikumbusha 1987

 4. ma'reen Says:

  Kikuku kinanukiaaaaaa, kikuku kinanukiaaaa ….. yekeyeke tumoro yekeyeke!

 5. Dunda Golden Says:

  BC kibao kilivuma sana
  Mimi nakikimbuka hiki ibao na wengi wetu tulikuwa tukiimba michuzi inanukia yoyooo siemi na hilo nakwambia mwenzangu yekete michuzi yeke yeke yekete.enzi hizo Paka mkolofi ulikuwa kwenu Rufiji.Matty na Binti-mzuri Edwin Ndaki Peal Gervas Any na weni wengineo nawatakia week end njema
  BILA KUWASHAU TIMU NZIMA YA WANA WA BC VIVAAAA

 6. Matty Says:

  Edwin Ndaki wapi tena leo???kwa Dan au??
  Wknd njema wana BC wote jamani!Mungu awe kiongozi wenu popote muendapo!

 7. binti-mzuri Says:

  OMG! umenikumbusha mbali aisee 😀 ..this was my dad’s song. r.i.p

 8. Edwin Ndaki Says:

  Kama najiona vile miaka hiyoo..asikwambie mtu Dunda golden.Najiona nimeulamba ka kaunda suti na “sani gogozi”..

  Nakumbuka ukija katika uchumi ilikuwa ni kipindi cha mzee wetu..Ruksa!!!aaa aaaahaaa

  Matty leo nitachelewa kidogo kwa Dany maana nitaenda kumsalimia kidogo Gervas ingawa lazima kabisa nipitie kwa binti mzuri naye kumjulia hali.

  Nawatakia wote mapumziko mema ya juma..

  Ila duh..nipo rhumba ..sijui kama itapita salama hii wiki endi..kwii kwiiii teee teeee

 9. done Says:

  kikukukinanukiaaa kikukukinanukia aa shemeji mbayaa kanambia malaya yekeyeke tomoro yekeyeke………yani mamboya primaryschool break tim kilamtu anaimba big up bc

 10. Mnenge Says:

  Umenikumbusha Mwanaisungu Pale Tabora. Nikiwa PR. School

 11. Leila shakum Says:

  Sikujua muimbaji.Asanteni sana Bongo Celebrity

 12. Binti-mzuri Says:

  Haha,yani bc leo kapatia.kamkuna kila mtu,moto endeleza huo huo jeff. Edwin Ndaki karibu upitie mtori wa kwenu hapa. Dunda galden,my friend,salamu zikufikie wewe na wifi yangu warda. Peace to BC members

 13. the ma-juuz Says:

  yeah! Mori Kante`s YEKE-YEKE song was the B0MB!

 14. Pearl Says:

  Dunda Golden asante nawe enjoy ur weekend

 15. Mwanakijiji Says:

  Mbona kafananana na Issa Michuzi huyu?

 16. brotherkaka Says:

  thanx!!!!!!!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s