BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JK AKABIDHIWA RIPOTI YA EPA August, 18, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 11:48 AM

Hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekabidhiwa rasmi ripoti ya uchunguzi kuhusu upotevu wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje(External Payments Account-EPA). Rais amekabidhiwa ripoti hiyo kutoka kwa wajumbe wa tume aliyoiunda kufuatia kuibuka kwa kashfa hiyo ya matumizi mabaya au yasiyoeleweka ya fedha za umma kupitia Benki Kuu ya Tanzania(BOT)

Wajumbe wa Tume hiyo ambayo hivi leo ni maarufu kama “Tume ya EPA” walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika(Mwenyekiti wa Tume),Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini Dr.Edward Hosea. Ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo hii. Nini kimo ndani ya ripoti hiyo? Will it ever be made public? Hayo ni maswali magumu ambayo hatuna budi kusubiri tu na kuona nini kitafuata.

Pichani ni Rais JK akipitia kurasa za ripoti hiyo mara tu baada ya kukabidhiwa.

Advertisements
 

34 Responses to “JK AKABIDHIWA RIPOTI YA EPA”

 1. Bablee Says:

  Pole sana Mkuu, yaani nimejaribu kuvaa taswira yako, nimejaribu kuingia akilini mwako nakujaribu kutafakari na wewe pamoja! Dah kwa kweli ni changamoto nzito inayokukabili! Kama kuna vipindi vigumu umepitia katika uongozi, basi kipindi hiki ni babkubwa! Kuna mambo magumu na mazito ambayo yote yanasubiri maamuzi yako i.e
  1.EPA
  2. Richmond
  3. Muafaka wa zanzibar
  4. Zanzibar nchi au si nchi

  Kama haitoshi bado kuna matatizo ya kijamii, kama kuuwawa kwa maalbino, ujambazi, vita vya kikabila (Tarime) n.k.

  Bado matatizo ya kiuchumi kama vile mfumuko wa bei za vyakula, kupanda kwa nauli za dala dala (mpaka wanafunzi wanaandamana na kudai huwezi kuongoza!). Mbali na hayo yote bado kuna pressure ya wahisani inayokulazimu kufikia maamuzi kwa jinsi wanavyotaka wao..!

  Pole sana, kama Urais ndo huu Mungu chukuwa roho yako kabla sijapata wazo la kugombea urais hata wa wawacheza msewe….!

 2. Gervas Says:

  Haya tena ..akadabla-dabla a.k.a changalamacho. Ni kweli hata mtoto mdogo akiwa analia njaa afu mzazi ukajifanya unafungua fungua masefuria au fridge atajua kwamba unamwandalia chakula na atanyamaza.

 3. Binti-mzuri Says:

  Nyie kazi ya uraisi sio ndogo,kwa mtakaopenda kugombea in future..take a leaf from here.

 4. Sam Says:

  Ripoti ya Richmond ilishawasilishwa na kusomwa Bungeni, je imefanyiwa kazi? Tusije tukawa tunaunda tume tu kutuliza hasira za wananchi. Watu wakakaa kufanya uchunguzi badala ya kutekeleza majukumu yao ya kawaida ya kila siku; juu ya hapo wanalipwa per diem, etc. Halafu ripoti zikifikishwa hakuna uamuzi wowote unaotolewa.

 5. sikujua Says:

  Haya tusubiri kauli ya Rais juu ya
  EPA si fedha za serikali!
  Zanzibar si nchi!
  Ze Comedy si EATV!!!!!!!!!!!!
  CCM si mafisadi
  Mkapa si mwizi wa kiwira!!!!!!!!

 6. wabusara Says:

  Tusikie haya
  1 Vigogo wa EPA na hatua zinazochukuliwa
  2 Richmond na maazimio ya bunge,Lowasa akiwa mshiriki
  3 Muafaka wa siasa zenj
  4 Ni nchi au
  5 Kiwira na uuzwaji kwa Benny

  Hatutaki hadithi,kila kitu kipo wazi. Wezi na washirika wao wanajulikana sasa sijui utatudanganya nini.

  Muafaka, sio umuachie makamba hapana hili ni lako muheshimiwa

  Zanzibar,sio tusikie kuna wanasheria wanashughulikia,hili ni lako.
  Watanganyika,hapa kuna changa la macho,mbona hakuna issue hata moja amabyo imeshajadiliwa bungeni,sasa JK si anaenda kuwakemea wabunge!! Lakini zama hizi ni za watanganyika,wadanganyika walishakwenda baada ya uhuru.
  Tunataka kusikia substance sio ngano na hekaya

 7. ma'reen Says:

  Same old tale! Baada ya hapo rais atatoa mapendekezo, yaundiwe tume ya kuyachambua. Hiyo tume ikumbwe na kashfa ya kifisadi, na yenyewe iundiwe tume…Mwisho wa siku ulaji bongo siku hizi bora ujuane na wakubwa ili kila ‘dili’ la tume uwekwe…Tume ya Richmond, tume ya kujadili mapendekezo ya tume ya Richmond…

 8. sappy Says:

  Hii ni danganya toto kwa kamati ile ya akina Mwanyika na mwenzake Hosea haiwezi kusema ukweli wowote kuhusiana na madeni hewa yaliyolipwa ya EPA, tutabaki kuwa hivi hivi labda aje kiongozi kutoka upinzani anaweza kuteua kamati ichunguze makosa ya CCM na kuyaanika lakini si ndani ya CCM kwa CCM kuanikana, Kikwete ukiwataja wenzio lazima nao watakuanika siku moja nina imani kuwa na wewe una maovu yako.

 9. Andrew Says:

  Labda tusubiri atakayosema bungeni.

 10. Edwin Ndaki Says:

  aaa..aaaa kazi ipo Gervas..kesi ya nyani..tumempelekea ngedere..jibu unalo.

  Yaani ukimtazama tu muheshimiwa hapo anasoma tu DIBAJI tayari miwani inataka kudondoka maana ni yale yale anayoyajua ndio yamerudi.

  Kikubwa namshauri mh rais aunde wizara mpya aipe jina “WIZARA YA TUME”yaani hiyo wizara kazi yake ni kuunda tume mbalimbali.maana bongo kila wiki tume.Mara tume ya muhimbili ,tume ya ghorofa,tume ya nauli za daladala,mara tume pweza hawaonekani?

  Kila kukicha tume.Zikisha tumia pesa zetu hizo ripoti zinawekwa kapuni.Tume ya Richmond nini cha maana kilichofanyika?Sana sana tumepigwa changa la macho watu kujiuzuru wakati wezi wa kuku wanafungwa.

  Bablee bado kuna mengine yanakuja safari hii JK kazi anayo.Wiki ijayo WAFANYAKAZI wanagoma.

  Yaani kweli bongo Tambarare.JK uza nchi japo kila mtu umgawie buku tano akachachue mvinyo.

  MUHIMU:
  BC naomba umtafute Hashimu Lundenge atuambie suala la BALAZO WA KILAJI CHA REDDS imefikia wapi?Maana waandishi wetu tayari wamesahau kwamba *issue’ imebaki ‘pendingi’ wakati walisema watatoa ufafanuzi siku mbii ya tukio kutokea.Au siku mbili bado? Au ndio wanataka kutusahaulisha?

  Akigoma kutoa majibu..tumwambie mh rais aunde tume kuchunguza sakata la balozi wa ‘redisi’ kurudisha taji.

  Tutafika tu

 11. trii Says:

  nimesikia alhamisi ndo rais ataisoma bungeni,correct me if am wrong,pata kuwa hapatoshi,mmmmmm lkn navyo jua mimi watu wanajua kubebana+kuzibiana utasikai oohhh hela hazikuonyesha zilichukuliwa na nani ohhhh sijui nn yani ili mradi tuu,kwa kweli wa tz woteee tunasubiri kwa hamu,kujua ukweli wa ripoti.

 12. Matty Says:

  Pamoja na hayo yote yaliyosemwa hapo juu Sikujua ndo umemaliza zE COMEDY si EATV hahahhahahhaah!!! ila ni TBC1

  Mh nasema hivi am tired na haya mambo kwa kweli mara
  EPA
  RICHMONDULI,
  ZNZ SI NCHI BALI MKOA,
  MGOGORO WA KISIASA ZNZ

  hey bamdogo utazeeka kabla ya siku zako maana watendakazi wako wote ni bla bla tu hamna mpya!

 13. pretty girl Says:

  mmmmmmh aisee pole sn mzee JK,Nafikili miaka hii mitano kiti chako cha urais kiliacku kinawaka moto huna raha nacho hata kidogo.mara ufisadi,richmoond oo epa kidogo kichaa kaua wagonjwa wenzake mmmm kero 2pu????????

 14. msonsah Says:

  Mwanzo mwisho tutakuwa tukidanganyika hata kama akipewa riport iwe na kava la rangi gani hakuna kitakachofanyika zaidi ya mizinguo, kama unabisha wait hiyo alhamisi. mshikaji mzushi kama madaraka yote aliipa tume aliyoiunda itoe maamuzi imeshindwa sasa kuna kipi kipya labda akachekecheke bungeni
  sisi tumeshazoea hapa bongo kila mtu atakufa kivyake usitegemee kuna mtu atatutoa kwani hatuna rekodi yakuwa na manabii nchi hii.

 15. bongosamurai Says:

  Pole sana mheshimiwa rais.
  Huo ndio uongozi katika nchi maskini. Viongozi uliowaweka kukusaidia wanapogeuka (MAFISI) watoroshaji wa mali ya umma.
  Ripoti imekamilika sasa TAKE ACTION.
  Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

 16. Dunda Golden Says:

  Mkuu busara na hekima zako
  hakuna la zaidi kwetu kwako
  ni dua na nasha kwako kwenye
  kila linalojitokeza piga moyo
  konde save everything linalokuja
  chafosa chai doga

 17. kindo Says:

  He! Mizigo ilioorodheshwa hapo juu ni mizito sana. Siku hizi hata tabasamu yake haifiki machoni. Amejichokea!!! Loh!

 18. mbega Says:

  huu ni unafiki tu kwani hiyo ni babaisha toto kwa wadanganyika, anajua kila kitu kinachoendelea hapo kwani na yeye ni mmoja wapo wa hao mafisadi

 19. the ma-juuz Says:

  Si mchezo mazee! nimesoma makala hii kwenye gazeti la Raia Mwema
  HABARI
  Nakala chapishi
  Mtumie mwenzio
  Jiandikishe utaarifiwe

  Mtikisiko Serikali ya Jakaya Kikwete

  Mwandishi Wetu Agosti 13, 2008

  Hofu ya kuhujumiwa yatanda

  Vigogo kung’atuka ‘kiaina’

  MISUKOSUKO ya mfululizo inayoikumba Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inatishia kuwasukuma pembeni baadhi ya watendaji wakuu serikalini, Raia Mwema imeambiwa.

  Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kuwa, mbali na watendaji hao ambao wamekuwa wakitajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi, hatua hiyo inalenga pia kupambana na hofu ya hujuma dhidi ya Serikali, na hasa Rais Kikwete mwenyewe wakati nchi inapoelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Habari zinaeleza kwamba Rais Kikwete amekuwa kimya kwa muda mrefu akitafakari kwa makini jinsi ya kukabiliana na hali hiyo na sasa amedhamiria ‘kujivua’ baadhi ya watendaji ambao wametajwa kwa namna moja au nyingine katika tuhuma mbalimbali za ufisadi, hata kama hakutakuwapo ushahidi kamili dhidi yao.

  Lakini habari zinasema pia kwamba Rais Kikwete ameshauriwa achukue tahadhari ya kutosha katika kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutowatimua kwa aibu watendaji hao, na badala yake aache waondoke kwa taratibu tofauti zikiwamo za wao kuomba kustaafu, kuteuliwa katika nafasi nyingine au kupewa uhamisho kutoka maeneo walipo sasa.

  “Baadhi ya watendaji wanaotajwatajwa katika tuhuma mbalimbali ni watendaji wazuri na walihusishwa katika tuhuma hizo kutokana na nafasi walizokuwa nazo na walifanya hivyo kutekeleza maelekezo ama amri za wakubwa zao ikiwa ni pamoja na vikao halali vya Baraza la Mawaziri, kwa hiyo inabidi wasiondoke kwa aibu,” anasema ofisa mmoja mwandamizi serikalini.

  Pamoja na kuibuka wakati wa utawala wa sasa, sehemu kubwa ya tuhuma zilizoitikisa sana Serikali ni zile zilizorithiwa kutoka Serikali ya Rais Benjamin Mkapa. Rais Kikwete aliathiriwa kutokana na kuwashirikisha katika Serikali yake wengi wa watendaji na wanasiasa waliohusishwa ama kutajwa katika tuhuma mbalimbali.

  Miongoni mwa wanaotajwa kuweza kuondoka serikalini kwa njia ya kustaafu ama kupangiwa kazi nyingine ni pamoja na watendaji serikalini ambao walihusishwa kwa nafasi zao za zamani katika mradi tata wa dhahabu wa Meremeta, wakiwa wakurugenzi wa kampuni ya Tangold Limited iliyochukua kazi za Meremeta Gold Limited.

  Miongoni mwao yumo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Vincent Mrisho ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, wizara ambayo ilikuwa ikiwakilisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyokuwa na maslahi katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba uliokuwa ukisimamiwa na Meremeta Gold na hatimaye Tangold Limited.

  Patrick Rutabanzibwa

  Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Patrick Rutabanzibwa, ambaye wakati wa utekelezaji wa mradi huo, alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, wizara yenye jukumu la kusimamia sekta ya madini ikiwa na wataalamu wake wa madini.

  Mtendaji mwingine wa Serikali aliyetajwa kuwa mkurugenzi wa Tangold Limited ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, ambaye wakati wa utekelezaji wa mradi huo, alikuwa katika nafasi hiyo hiyo, kutokana na wizara hiyo kuhusika na usimamizi wa hisa za Serikali kupitia Msajili wa Hazina.

  Wote watatu wametajwa mara kadhaa katika kuhusika kwao na mradi huo tata na tayari imethibitishwa kwamba walikwisha kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), katika uchunguzi wake wa mradi huo ambao hadi sasa kitendawili chake kimekuwa kigumu kuteguliwa hususan baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuliambia Bunge kwamba suala hilo linahusu siri za kijeshi.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alipolizwa kama kuna watendaji wowote wa Serikali ambao muda wao wa kustaafu umefika au kama wataombwa kustaafu, alisema hajui lolote.

  “Nadhani watu wazuri wa kulizungumzia suala hilo ni DAP wa respective ministries (wakurugenzi wa utawala wa wa wizara husika), alisema.

  Raia Mwema ilifanikiwa kumpata Vincent Mrisho kwa njia ya simu yake ya mkononi, lakini alipoulizwa alikuja juu badala ya kujibu aliyoulizwa.

  “Mimi nimekwisha kuwaambia kwamba sizungumzi na waandishi wa habari kwenye simu, mpaka nionane nao, mnajifanya wajanja sana nyinyi,” alisema.

  Alipoombwa ni wapi na saa ngapi mwandishi wa Raia Mwema anapoweza kumpata kwa ajili ya kutaka kuelezwa anachokitafuta, Mrisho alizima simu yake.

  Gray Mgonja

  Pia baada ya kushindwa kumwona Gray Mgonja, Raia Mwema ilifanikiwa kumpata msemaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingiahedi Mduma, ambaye alisema hajasikia lolote kuhusu Mgonja kuomba au kuombwa kustaafu.

  “Si mnafahamu alitokea BoT na anafanya kazi kwa mkataba? Mimi ninachofahamu wakati wake wa kustaafu bado,” alisema.

  Makatibu Wakuu hao waliingia katika mradi wa Maremeta kwa kuteuliwa katika kamati maalumu iliyoundwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa, kusimamia na kumaliza matatizo ya kampuni ya Meremeta, wakati wa uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi wa Buhemba.

  Wajumbe wengine katika kamati hiyo maalum iliyoundwa mwaka 2003 ni pamoja na Dk. Daudi Balali (sasa marehemu) aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) ambaye Rais Kikwete alimfukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi uliofanyika kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Kiongozi mwingine aliyekuwapo katika kamati hiyo kwa wadhifa wake wakati huo ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa utawala wa Mkapa, Andrew Chenge, ambaye aliingia katika Serikali ya Kikwete akiwa Waziri wa Maendeleo ya Afrika Mashariki, na baadaye Waziri wa Miundombinu kabla ya kujiuzulu kutokana na kuhusishwa kwake na tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada ya kijeshi kutoka kampuni ya BAE System ya Uingereza.

  Baadhi ya makatibu wakuu hao wamepata kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakikiri kuhojiwa na TAKUKURU, lakini walielezea kushitushwa kwao na kuhojiwa huko katika mambo waliyoyafanya kutekeleza maagizo ya wakubwa, na wamekuwa wakisubiri kusafishwa baada ya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo kukamilika.

  Kampuni ya Meremeta Limited na baadaye Tangold Limited zinahusishwa na kupotea kwa zaidi ya Sh. bilioni 155 za BoT zilizobainishwa na wakaguzi waliohoji taratibu zilizotumika kulipa fedha hizo ambazo ni zaidi ya zile zilizopotea katika lile sakata la EPA. Makampuni 22 yanahusishwa na upotevu wa Sh bilioni 133 za EPA.

  Serikali imeunda timu kuchunguza upotevu wa fedha za EPA, chini ya uongozi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Hosea, lakini inakwepa kuzungumzia hadharani kuhusu Meremeta pamoja na kuichunguza.

  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, Ludovick Utouh, amekwisha kutamka kwamba ofisi yake haiitambui Meremeta kama kampuni ya umma kwa kuwa haijawahi kukaguliwa, huku baadhi ya viongozi wa serikali wakiwamo mawaziri wakidai kwamba ni ya umma.

  Pamoja na Utouh kuikana Meremeta, kuna taarifa kwamba serikali ya Mkapa kupitia Msajili wa Hazina ilitoa cheti ya kuithibitisha Meremeta kuwa kampuni ya umma tokea Oktoba mosi, 1997 baada ya kudaiwa kwamba serikali ilikuwa na hisa katika kampuni hiyo.

  Hisa zilizodaiwa kuwa za serikali zilikabidhiwa kwa waliokuwa watendaji wakuu serikalini, ambao hata hivyo hadi sasa wanaendelea kuzishikilia baada ya baadhi yao kuondolewa ama kubadilishwa nafasi zao.

  Habari zaidi zinaeleza kwamba watendaji wakuu ndani ya JWTZ na Wizara ya Ulinzi na JKT, walipata hisia za kuwapo kwa mikono michafu katika mradi wa Meremeta na hivyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa wenzao wanaochunguza sakata hilo.

  Sakata la Meremeta limeelezwa kuweza kuwa kubwa na zito zaidi kutokana na maelezo ya uwezekano wa kuwapo wahusika wanaofahamika duniani katika biashara chafu na hivyo kuibua mjadala mwingine mkubwa utakaovuka hadi mipaka ya Tanzania.

  Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi unaweza kwenda mbali kutokana na kampuni ya Nedcor Trade Services Limited ya Afrika Kusini, kuonekana kuwa na uhusiano na benki ya Nedbank ya Afrika Kusini ambayo sehemu ya fedha hizo zilielekezwa huko, zikitokea BoT, huku baadhi ya wakurugenzi wa kampuni nyingine tata ya Deep Green Finance Limited wakiwa watumishi wa benki hiyo maarufu ya Afrika Kusini.

  Deep Green Finance Limited ni kampuni iliyosajiliwa nchini na baadaye kupokea fedha kutoka BoT, kabla ya kufilisiwa bila ya kuwapo maelezo ya kutosha ya madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo katika kipindi ambacho nchi ilikuwa inaelekea katika uchaguzi mwaka 2005.

  Kashfa hiyo ya Meremeta inaelezwa kuwa zaidi ya ile ya EPA kutokana na kuwa uwezekano wa kurejesha fedha hizo ni mdogo kutokana na kuingia katika mkondo unaoihusisha zaidi Serikali yenyewe na watendaji wake wakiwahusisha wafanyabiashara wa kimataifa.

  Meremeta Ltd. ni kampuni binafsi ya kigeni iliyoandikishwa Agosti 19, 1997 katika kisiwa cha Isle of Man nchini Uingereza na kupewa namba ya usajili 3424504, ikimilikiwa na TRIENNEX (PTY) LTD ya Afrika Kusini yenye asilimia 50 ya hisa za kawaida na Msajili wa Hazina (Treasury Registrar) akiwa na asilimia 50.

  Meremeta ilipewa Hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) Oktoba, 1997 ikafilisiwa Uingereza Januari 2006 lakini kumekuwapo utata kwa upande wa Tanzania kutokana na kutajwa katika marejeo mbalimbali kuwa moja ya makampuni yanayozalisha dhahabu.

  Taarifa na takwimu muhimu kuhusu Sekta za Nishati na Madini’, ya Julai, 2007, inaonyesha kuwa Meremeta bado inafanya kazi, na inazalisha tani 2.27 za dhahabu.

  Katika mapendekezo yake yaliyokabidhiwa kwa Rais Kikwete, Kamati ya Rais iliyopitia sekta ya madini nchini, imepependekeza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusiana Meremeta na Tangold, kampuni ambazo kamati hiyo imebaini kuwapo ukiukwaji mkubwa wa taratibu.

  Wakati hayo yakiendelea, kwa zaidi ya miaka mitatu sasa serikali imekuwa ikiyumbishwa na matukio kadhaa yakiwamo tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wake wakuu ikiwa ni pamoja na zile zilizosababisha kung’oka kwa mawaziri watatu kwa mara moja akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

  Lowassa na wenzake, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, walioongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa kupishana, walijiuzulu baada ya kuhusishwa na tuhuma za ufisadi katika mradi tata wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni ya Richmond Development LLC ya Marekani na baadaye Dowans Holding.

  Mtikisiko mwingine ulioikumba serikali ya Kikwete ni ule wa tuhuma kadhaa ndani ya BoT, ambazo zilisababisha kuyumba kwa uchumi na kuhitimishwa na tuhuma za EPA zilizomng’oa Gavana Ballali, akiwa mgonjwa nchini Marekani kabla ya kufa kwake bila kujibu tuhuma hizo.

  Andrew Chenge

  Tuhuma nyingine ni zile za ununuzi wa rada ambazo zilisababisha kung’oka kwa Chenge, ambaye wakati akijiuzulu alikuwa Waziri wa Miundombinu, wizara aliyohamia akitokea Wizara ya Afrika Mashariki. Chenge aliponzwa na kuita ‘vijisenti’ zaidi ya shilingi bilioni moja anazodaiwa kukutwa nazo katika akaunti yake ya Uswisi.

  Mbali ya tuhuma hizo, hivi sasa wafanyakazi nchi nzima wanajiandaa kufanya mgomo mkubwa wiki hii, wakiilalamikia serikali kushindwa kuzingatia makubaliano yake kuhusu malipo ya mishahara mipya na malimbikizo, sambamba na mgomo wa madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Kabla ya vuguvugu la mgomo huo, serikali ilishitushwa na maandamano ya wanafunzi wa shule za Dar es Salaam, ambao walilalamikia kupanda kwa nauli ya mabasi ya daladala kutoka shilingi 50 hadi shilingi 100, wanafunzi ambao baadhi walibeba mabango kuishutumu serikali na wengine kudiriki kuzungumzia uchaguzi wa mwaka 2010.

  Wakati wanafunzi wakiandamana, askari wa JWTZ na polisi waliendelea kunung’unika chini chini na wengine kuendesha vipigo kwa madereva na makondakta wa daladala huku viongozi wao akiwamo Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk. Hussein Mwinyi, wakisema wazi kwamba hawana bajeti ya kuwalipia nauli askari wao.

  Huku hayo yakiendelea, mjadala wa hatima ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, umeibuka upya na safari hii ukielekezwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye aliliambia Bunge kwamba “Zanzibar si nchi,” kauli ambayo iliungwa mkono na kiongozi wa CCM, Tambwe Hiza, aliyesisitiza “Zanzibar si nchi.”

  Kauli hiyo pamoja na kuwa si mpya, kutokana na kuwahi kutolewa na viongozi wengine wa juu baada ya uamuzi wa mahakama kutolea ufafanuzi suala hilo, kukua kwa mjadala huo kunaashiria hali kutokuwa shwari ndani ya serikali na chama tawala katika pande mbili za muungano.

  Mjadala wa muungano unaelezwa kuchochewa na mapendekezo na mjadala wa ndani ya vikao vya CCM vilivyofanyika Butiama mkoani Mara kuhusiana na mazungumzo ya mwafaka kati ya chama hicho na mahasimu wao wakuu visiwani CUF, suala lililoshindwa kutolewa uamuzi katika vikao hivyo na kuhamishiwa kwa wananchi wa Zanzibar.

  Mbali ya mvutano kati ya CCM na CUF, imeelezwa kwamba suala la upatikanaji wa mafuta na gesi visiwani Zanzibar limechochea mvutano kati ya pande mbili za muungano pamoja na kuwa suala hilo limewekwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

 20. Saad Says:

  Namjua JK ni mtu mwenye Hekima sana. kuzidi watangulizi wake wote hata JKN. Mafisadi hakuyapanda yeye lakini yamepandwa na JKN kwa BM. Kuyangoa magugu ndani ya ngano anaweza na kishaanza. Tumpe muda tu ataweza. mzigo ni mzito ila naamini ataweza. big up JK. polepole ndio mwendo. shikilia usukani vizuri na uwazamishe wale wote wanaotukwamisha kwenda mbele.

 21. Mimi Says:

  Inashangaza kusikia kuwa ripoti inakabidhiwa tena kwa muheshimiwa, wakati alipoiunda hiyo tume aliiagiza ichunguze halafu ichukue hatuwa za kisheria kwa makampuni yote yaliyohusika na watu wote waliohusika. Hakusema kuwa akabidhiwe ripoti, sasa hiyo ripoti anakabidhiwa tena ya nini?.
  Changa la macho hilo. Wanafiki huwa wanasahau wanachokisema mwanzo na wabongo nao tuko kama mazuzu tunadanganyika tu.

 22. BLACKMANNEN Says:

  Rais Jakaya Kikwete ni mtu makini sana, anajua atakachokifanya baada ya kuipitia ripoti hii ya Tume ya EPA.

  Matakwa yenu ninyi wachangiaji wa mada hii. Mnataka Rais avunje sheria za uongozi na maadili ya urais kwa kuwahukumu wahalifu waliotajwa katika ripoti hiyo? Mnataka awe dikteta?

  Mh. Kikwete hawezi kufanya hivyo ili kuwaridhisha ninyi wakosoaji katika sakata hili, badala yake atawakabidhi wenye kazi ya kupeleleza makosa ya jinai na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika katika kufanya vitendo viovu hivyo, kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliopo.

  Kule ambapo sheria inamruhusu Rais Kikwete kufanya kitu, atafanya kile atakachokiona kinafaa kufanywa.

  Pia Rais hawajibiki kuwatajia wananchi, majina ya watu wanaohusishwa katika ripoti hiyo, isipokuwa vyombo vya sheria vinaweza kutoa majina ya watu hao, baada ya kuthibisha kuwa ni kweli wanahusika katika ufisadi huo.

  Mungu Ibariki Tanzania Na Watu Wake!

  Blackmannen

 23. kekue Says:

  Jk ni mtu anayependa maendeleo sn na anapenda wananchi wake sema tu watendaji hana, na anatamani yale yote aliyoahidi ayatekeleze lkn ndo hivyo tena, then ukichunguza ufisadi mwingi ulioteshwa cku nyingi ss ndo unachipua yy akiwa madakani yani sometime huyu baba namuoneaga huruma sn.

  Pole sn Jk cc tumeamua kuvumilia km ulivyosema.

 24. deny_all Says:

  Mhh…..sura ya rais wakati anapitia hapa hizo kurasa za EPA ripoti inaonyesha ana jambo kubwa moyoni….Tusubiri tuone.

 25. magdalena sechu Says:

  Wenye hekima kinachotakiwa ni kuiombea nchi na mungu amuongoze rais ili atende haki ,nilijualo mimi kwa imani yangu hata kama haki haitatendeka ni lazima rais ajue ipo siku kuna malipo ya kila ovu ,hivyo inabidi azingatie haki na usawa bila kuwalinda au kuwawekea kivuli maswahiba
  Kwani historia ya ufisadi haikuanzia hapa majuzi ni chembe ndogo ya rushwa na mengineyo kama hayo yalopelekea hili tunalolizungumza hapa,so Mr. presdent tenda haki mbele ya umma na mungu itakupa nafuu wewe !

  Mungu atusaidie katika kipindi hiki kigumu !

 26. maspidi Says:

  Ala, wewe ndiyo mshauri wa Rais nini?sikujua!

 27. masumbuka Says:

  Edited EPA Report or Audited EPA Report? Which is which? Tusogeze sogeze muda hadi 2010 itinge ndani, lije Zengwe lingine lituweke busy hadi 2015, upo? Au Miyeyusho Bro? Never Mind! Jamaa wanakabidhiana EPA REPORT huku wanatabasamu utafikiri WriteUp ya Mradi wa Gesi ya SongoSongo! Aiseeeeeeeeeeeeeeeeee!

 28. HALIMA Says:

  Aisee ukifanya mchezo kikwete hata gombea tena 2010 maana shughuli ni nzito halali mara Richlowasa, hajakaa vizuri eeh Epa duh mshikaji kazi unayo.Lakini hiyo ndio kazi ya uongozi baba kaza moyo usisahau kumuomba mungu wako nae atakubariki

 29. neema Says:

  kasheshe kubwa sana JK baba kaza roho natamani ningekuwa msaidizi wako nikusaidie baadhi ya majukumu ya kuwahukumu mafisadi duuu ni sooo mazeee.\

 30. magdalena sechu Says:

  Maspidi why dont you focus on your comments ?
  Thats was my comments ,add your’s, sorry !

 31. tiandra jones Says:

  MNAWIVU NA WATOTO WAWAFISADI. WAMESHABARIKIWA HAPO MAKATIBU TAWALA NA WAKUU WAWIZARA WAKIRETIRE MOJAKWAMOJA UN AU IMF AU CONSULTANT . WANAZIDISHIWA POLENI SANANNNNNNNNNNNNNNNNN

 32. binti-mzuri Says:

  the majuuz umeandika insha rafkiangu

 33. Matty Says:

  hahahahahah Ze Majuuz nimeshindwa kumaliza kusoma mhhhh nimesoma mpaka kichwa kinauma…Binti Mzuri soma kisha unisamaraizie!
  Next time try to summarize wat is important and i’ll be anxious to ready and understand your point rather than essaying as such…sorry that is my opinion!

 34. paka mkolofi Says:

  ze majuzi kuna nafasi ya kazi daly news


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s