BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NIHURUMIE WANGU-RAY C August, 19, 2008

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 7:46 PM

Inapotokea msanii fulani maarufu wa muziki akakaa kimya kwa muda,maneno mitaani huwa ni mengi. Kuna ambao huwa wanasema amefilisika kisanii au kajiengua kwenye “game” nk.Jambo moja ambalo huwa linakuwa gumu kwa watu wengi kutambua ni kwamba wakati mwingine huwa ni muhimu kwa msanii kukaa kimya ili sio tu kupata muda kupumzisha akili bali pia kusoma jinsi muziki pamoja na soko lake linavyokwenda.

Hivyo ndivyo inavyoelekea kuwa kwa msanii Ray C(jina halisi Rehema Chalamila) ambaye hivi karibuni ameibuka na nyimbo mpya kadhaa ukiwemo huu wa “Nihurumie Wangu”.Yote hii ni katika maandalizi yake ya kufyatua albamu yake mpya ambayo anasema tayari imekamilika na kinachosubiriwa ni taratibu tu kabla haijaingia sokoni.Albamu yake ameipa jina la “Touch Me”(wimbo uliobeba albamu) na inatarajiwa kuwa na nyimbo kama huu wa Nihurumie wangu, My Love, Nalazimisha Penzi, Moyo Unaniuma na nyingine.

Katika wimbo huu Nihurumie Wangu,Ray C amemshirikisha msanii mwingine maarufu wa Bongo Flava,Chid Benz.Wimbo umepikwa na Said Comorien kutokea pale Big Time Records jijini Dar-es-salaam.Usikilize hapo chini.Pata burudani.


Advertisements
 

43 Responses to “NIHURUMIE WANGU-RAY C”

 1. Ras Twin Says:

  Kazi ni nzuri kiasi chake na naamini ataweza kufanya vema. Kwa ujumla waimbaji wamekwenda na beats na hata uwiano wa sauti za waimbaji na muziki naona ziko njema. Pia style alorejea nayo Ray C nimeipenda. Big Up
  Lakini pia nikizungumzia muziki huu wa bongo flava kwa ujumla ni kwamba kumekuwa na mapungufu ya utengenezaji na ama uzalishaji wa muziki hapo nyumbani upande wa vifaa. Inasikitisha saana kuona tuna zana nyingi za muziki na wataalamu wengi saana wachezao zana hizi (nyingi zikiwa za asili) lakini bado wazalishaji ama watengenezaji muziki (Ma-producers) wanaendelea kuwa wategemezi wa midundo na mirindimo iliyojazwa kwenye vinanda ambayo mingi kati yayo haitoi sauti halisi zistahilizo. Pia wanapunukiwa “percussions” ambazo wataalamu wa muziki watakubali kuwa hujaza saaana katika ala. Kwa wale waliohudhuria ama kusikiliza kwa umakini nyimbo za wasanii maarufu kama Oliver Mtukudzi watakubaliana nami kuwa percussions ni msaada mkubwa kutunza utambulishi (identity) ya muziki na pia kuujaza ki-ala. Ni vema kama ma-Producers wangeligeukia hilo na kushirikisha wacheza ala za asili toka vikundi mbalimbali vya sanaa kama Simba Theatre, Sisi Tambala, Parapanda Arts na wengine wengi walioko huko kuweka hadhi na ladha halisi a muziki wetu. Lazima tukubali pia kuwa hata kama mtayarishaji ana kipaji kiasi gani (na nasema kipaji maana sina hakika na elimu) hatakuwa mtaalamu wa zana zote muhimu na ndio maana wote wanakimbilia kinanda.
  Pia washairi ama waimbaji (maana wengi wafanyao Bongo flava si wanamuziki) wahariri maneno yao kutoweka utata wa yale wasemayo. Mfano ni ktk kibao hiki aliposema “MIMI NA WEWE KAMA KIDEVU NA MUSTACHI” napata utata wa kama mustachi hukaa kidevuni (hapa ni kwamba sina hakika na kama yuko sahihi then ni mimi niliyeelimika na naamini wadau wengine watachangia hili).
  Kila la kheri katika kila jema mfanyalo kuendeleza sanaa na maisha kwa ujumla.
  Blessings

 2. michelle Says:

  Ray C, mdogo wangu bado sana unajitahidi lakini mmm, halafu hao waliokuback up wamekuharibia kabisa, maana mnasound kama kwaya za kijijini, ila endelea mamii b,cause i know if you determin you can do something much better, than what you’ve done this time. All the best!!!!!!!!!!

 3. juma mhando Says:

  Good!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 4. pretty girl Says:

  i love u my csta Ray C, I dont know why??but ua cute then unamvuto,mmm?bt all in all unajua kuimba sn nategemea one day utastop music wa kidunia na utaanza kuimba nyimbo za kumsifu MUNGU.Keep it up but pls ufanyie kazi ushauri wangu,Mungu akubaliki sanaaaa

 5. mambo Says:

  Umeharibu Ray C!! Beat mzuri, Rethim Mzuri, Sauti yako sina maneno. Lakini hao uliowashirikisha sauti zao mbaya na haziwiani kabisa na sauti yako. Ni kama watia flate fulani hivi!!! .Naomba fanyia marekebisho huu wimbo kabla hujaingiza katika album. ulifuata vigezo gani kuwashirikisha hawa? sauti, umaarufu,au majina?

 6. Matty Says:

  Yap yap shepu ya kike hiyoooooooooooo!

 7. baker Says:

  Hapo nafikiri kajitahidi ila Sauti ya mzee wa HipHop apo naona kama, imepoteza ladha fulani ivi! ningewashauri wasanii wawe waangalifu katika featuring kwani unaweza uka featuring na sauti ambayo haiendani na nyimbo yenyewe ila haina noma big up ray c, Ngoja tule buku kwanza siku tukitua bongo tunakuja kuwafanyia mziki wa ukweli,
  All the best.

 8. Phill Says:

  wimbo mzuri! Ila its the same ol Ray C songs! Nothin’ new!!!

 9. Bablee Says:

  Dah Rayc nakupa 5 mtu wangu..!

  Mashairi mazuri, sauti muruwa,vina vimetulia, ujumbe usipime, featuring babkubwa, unaenda na beat, mziki unabamba ile mbaya, vocal yakufa mtu na pozi lakichokozi!!!!

  Ntaomba featuring na wewe mamaaaaaaaaa!

 10. sponge bob squire pants Says:

  Mmmmm! sijasikiliza wimbo…mi naangalia tu! pajazz!

 11. star Says:

  jamani kiukweli kwa upande wngu,haka kadada kanajua kuimba but hakajui kuvaa,kama uktoa video mpya jitahd kwa hilo mamii

 12. eva Says:

  badilisha kabisa mpangilio wa kila kitu kwenye huo wimbo. ukiwa solo inakuwa bomba zaidi.otherwise kama hiyo ndiyo single am sorry, lets face it.

 13. eva Says:

  you look cute though, ila hiyo theme sijaikubali. tafuta mtaalam wa photo shoot.

 14. binti-mzuri Says:

  HAHAHAHH namba 10,mi hoii

  nimeappreciate God’s creation

 15. wabusara Says:

  Mchangiaji wa kwanza Ras twin kasema maneno mazuri sana.
  I concur wth you 100%

 16. Ras Twin Says:

  Thanx Wabusara. Heshima kwako na kila mwenye mema na maendeleo ya “muziki wetu”
  Blessings

 17. brayan Says:

  mmmmmmmhhhh kazi kwelikweli yani from there to ………………….

 18. imzzotz Says:

  u hav to change kidogo…..its olwayz tha same. n abt ft..i think uliteleza kumchukua hyo chi.chi..chi..d beeenz, n way nice try!

 19. Sally Says:

  Maneno mazuri hata bit si mbaya. Ila Bezi limezidi kwa huyo mtu aliye mshirikisha

  Sally

 20. Frateline Says:

  Hi guys kutoka Helsinki-Finland

  Kazi zako nzuri, keep it up!

  Best wishes

  Frateline

 21. da lily Says:

  hongereni sana safi sana sana we chid wa makwilo nakufagilia sana na watoto wote wa magorofani kwa mjumbe bi shida wape hi la fam wote haswa modi

 22. MapigoSaba Says:

  mwe! kama vile bambio, lakini hata mapambio ni mazuri zaidi kuliko huu wimbo.

 23. wakuvanga Says:

  LISONGI BADO SIJALISIKILIZA ILA HAYO MAPOKEZI DUUUU………YANANINANIIII………PAJAZIIIIII…………BILA SHAKA SONG LITAKUWA LIMETULIA MAKE NAMUAMINI SANA HUYO MLEMBO

 24. kindo Says:

  I concur with Ras. As for sauti ya Chid nadhani walimanisha iwe hivyo…yaani different. Otherwise amejitahidi but more focus is required.

 25. msumari mwembamba Says:

  Shabaaaaaaash, Totooooooz limeshiba manake! Ningekuwa na uwezo japo niwe ‘Underwear’ yako tu Ray C, sitaki makubwa zaidi, aaaaaaiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!

 26. any Says:

  Mi nimependa zaidi viatu vyake!

 27. Wakiume Says:

  Chid umeharibu huu wimbo!
  Itabidi ulpie rimiks…then urap tuu

 28. Vyonne Says:

  wimbo sio mbaya umejitaidi sana…

  my person advice:

  try to bring a song which will stand out from the all other artist…

  indiviuality is needed inorder to make it in the international chats

 29. EDWARD Says:

  Wimbo huu si mbaya, ala, yaani vyombo vimipigwa vizuri na theme nzima ni bomba, kasoro ni moja tu, nayo ni wale watu wanaomsaidia tu ni kama wavivu hivi wanachelewa kwenda na pamoja pale wanapoimba chorus naye, NAOMBA WAFANYIE MAREKEBISHO KIDOGO YA UIMBAJI KABLA HAWAJAPELEKA SOKONI, CHID, KUHUSU SAUTI YAKE SI TATIZO KABISA KWANI HIVYO NDO ILIVYOPANGWA IWE, CHA MSINGI NI KUNA GAP/MWANYA FULANI HIVI WANAPOANZA KUINGIA KUIMBA KUMSAIDIA RAY C, WAJARIBU KULIONA HILO NA WAFANYE MAREKEBISHO KIDOGO, WAO WENYEWE WAKAE CHINI WASIKILIZE HUO WIMBO MARA NYINGI KIDOGO NA WATAONA KASORO HIZO NA WATAREKEBISHA, PIA CHA MSINGI NI KWAMBA WATENGENEZEE VIDEO NZURI YA KISASA INAYOENDANA NA MANENO YASEMWAYO. BC JARIBU KUWAPELEKA MAONI YA WATU YATAWASAIDIA KUTOA KITU BOMBA KITAKACHOUZIKA SOKONI. CHA MSINGI SAUTI ZA HAO WASAIDIZI ZINOLEWE NA WAJITAHIDI KU-INGIA PAMOJA NA WAZINOWE WAONDEWE U-FLAT FULANI HIVI

 30. b Says:

  Ras Twin ameongea mengi yenye kupewa uzito. Ni kweli kabisa huu mziki hauna uhalisi kwasababu viunjo vyote vinatoka kwenye vinanda, wakati waandaaji wangeweza kutumia ala za asili kuongeza utamu wa viunjo kwenye milindimo.
  Kuhusu uhakiki wa mashairi ya hawa wanamziki ni kitu muhimu pia. Ras Twin ametoa mfano mzuri, mustach na kidevu wapi na wapi. Mustach ni zile nywele zinazoota chini ya pua, wakati kidevu kiko chini ya mdomo, hapo hakuna uwiyano kabisa, nadhani hata kama maana ya alichotaka kukiwasilisha kwa halaiki kimeshindikana, bali kuleta mkanganyiko zaidi ya maana ya msingi iliyotarajiwa. Kiswahili kigumu, na usanii na sanaa nadhani ni vitu viwili tofauti. Nadhani wanamziki wengi wa bongo flava ni wasanii lakini si wanasanaa kutokana na upeo wa mdogo kwenye utengenezaji wa kazi zao. Kujua kuandika mashairi ni kitu kimoja, kujua namna ya kuyawakilisha kwa walengwa bila kuchanganya halaiki ni kitu kingine. La mwisho ni jinsi milindimo itakavyoweza kuchochea utamu wa hilo linaloimbwa. Ala zilizomo kwenye beat ziwe kama a vehicle to help carry through your words in an interesting way. Somo la sanaa bado sana. ..

 31. EDWARD Says:

  NIMESIKILIZA TENA WIMBO NI BOMBA, AWEKE VIONJO KABAMBE KWENYE VIDEO, UTAKUWA BABU KUBWA, HASA DANCERS ATAFUTE WAZURI WA KUDANCE, HASA MAUNO NA WAZURI WREMBO WA SURE, PIA IENDANE NA THEME YA WIMBO WENYEWE. APATE DANCERS WAZURI

 32. winnie udsm Says:

  Everything is gud keep it up gal

 33. EDWARD Says:

  It is like JA-RULE and JLO waliwahi kuimba wimbo wa aina hii wenye sauti za aina hiyo si mbaya sana kunatakiwa marekebisho kidogo tu, watu wataupenda na utauzika, watafute mtaalamu tu wa ku-create mandhari ya video inayoendana na wimbo/lyrics, na hivyo ndivyo alivyofanya MICHAEL JACKSON always in his career, nyimbo zake watu zilikuwa zinawakosha sana kupitia video zake ambazo nyingi zilikuwa zimeenda shule, angali THRILLER, hata uki-watch today huwezi kuhisi kuwa ilitoka zaidi ya 25 years ago. Watafuta mtu mzuri wa video creation and production wampe huo wimbo ausome na kuusikiliza kwa makini, na afanye mahojiano na waimbaji na mtunzi wa shahiri ili wafikie common ground how to make a killer video.

 34. the king Says:

  MIMI SINA MANENO ILA MWENYE EMAIL YA HUYU DADA NINAOMBA NINASHIDA NAE SANA

 35. louis Says:

  the song was beautifully and let her keep it up.
  thanks
  iam from melb_Australia.

 36. Dunda Galden Says:

  KIUNO BILA MFUPA
  BINTI KATIKA KUKIACHIA KIUNO
  SI MCHEZO ONGERA SANA PIGA HATUA

 37. adnan says;august,26,2008. Says:

  wimbo kusema ukweli uko juu ishu ni kuongeza vionjo kabambe kwenye video.naomba e.mail yako mtu wangu.

 38. EDWARD Says:

  KUHUSU KIDEVU NA MUSTACHI/MUOSTACHE, ORIGINALLY THIS WORD CAME FROM THE WORD MOUTH-TOUCH, according to the definition of this word from the Longman Dictionary of the English language page 1044, the four word from top, defines moustache as “the hair growing or allowed to grow on somebody’s upper lip of the mouth, and sometimesdown the sides of the face, framing the mouth or a growth of hair or bristles round the mouth of a mammal” na kidevu ni nywele zinaota chini ya mdomo wa mtu. KWA MAANA HIYO BASI MUSTACHI NA KIDEVU NI VITU VINAVYOOTA KWENYE USO WA BINADAMU HUSUSANI KUZUNGUKA MDOMO VINAISHI SEHEMU MOJA KAMA VILE MTU NA MPENZI WANAVYOISHI NDANI YA NYUMBA MOJA AU NDANI YA PENZI MOJA NDANI YA MIOY YAO. KWA MANTIKI HIYO HAPA HUU WIMBO HAUNA MAKOSA YOYOTE YALE YA KIFASIHI.

 39. kahindi Says:

  ni kweli Ray C,ati umebomu supu arusha?

 40. Innocent Says:

  hiyo face mmetubania..

 41. Amina Says:

  Acha kujichubua ray c

 42. Matty Says:

  hahahahahahaha Kahindi besti hata mimi hiyo niliisikia somewhere!.
  Amina na wewe mwanawane mbona unamuingilia na personal decision zake?

 43. richard Says:

  nyimbo imetulia maana chid na ray humu wameendana.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s