BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JENNIFER MGENDI August, 26, 2008

Filed under: Dini,Muziki — bongocelebrity @ 9:10 PM

Ushasikia kwamba muziki wa gospel(injili) siku hizi unatamba sana nchini Tanzania.Mmojawapo ya wasanii wa muziki huo wa injili wanaotamba ni Jennifer Mgendi(pichani).Mbali na kuwa muimbaji wa nyimbo za injili, Jennifer pia ni mtunzi mzuri wa hadithi za filamu.Baadhi ya filamu alizowahi kutunga ni kama ile ya Pigo la Faraja na Joto la Roho.

Mgendi alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 1995 na albam yake ya kwanza iliitwa ‘Nini?’. Baada ya hapo alitoka tena na albamu zake zilizokwenda kwa majina ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu Nakupenda’,’Nikiona Fahari’ na ya hivi karibuni zaidi inayoitwa Mchimba Mashimo.

Photo/Global Publishers

Advertisements
 

38 Responses to “JENNIFER MGENDI”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Hongera sana Jennifer Mgendi kwa kutupa kiburudisho cha mziki wa Injili na hapo hapo kutulisha neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.

  Kitu ambacho naweza kukuambia wazi ni kwamba, umepanda haraka haraka katika fani hii ya muziki na kufikia hapo ulipo sasa, ni kutokana na sauti na uimbaji wako wa “Saida Karoli” wanna be!

  Jennifer, kama kungekuwa na “Haki Miliki” ya sauti, kwa kweli Saida Karoli ungemlipa japo kidogo, kwani moja ya kigezo cha mafaniko yako ni hiyo, copy write ya sauti yako na yeye.

  Hata hivyo, Jennifer, nakutakia kila la kheri katika shughuli zako za kutuburudisha na kutupa neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.

  Blackmannen

 2. naila Says:

  huyu dada nampenda,ana sauti nzuri,mrembo na kind of exposed!

 3. Wakuvanga Says:

  Praise the lord

 4. mama jj Says:

  kweli nimeamini kuwa kipaji kipo, hongera sana jeny kwani wewe ni mzuri,unakipaji sana si cha kuimba tu bali cha utunzi. Kazi zako zinanibariki sana. Mungu azidi kukulinda uendeelee kutunga nyimbo zinazonibariki.

 5. Jose Jose Says:

  kwani wewe kabila gani?

 6. BABA DORIE Says:

  Bwana YESU kristo asifiwe

 7. solange Says:

  jamani huyu mdada ana sauti ya kipekee, napenda sana sauti yako haaa na nyimbo zako ni nzuri sana, mungu akubariki ma dia.

 8. any Says:

  Jamani huyu mdada mzuri,anajua ku act, nimemwona kwenye joto ya roho, hadi raha, mi mwenyewe nikapata joto ya roho kwa kuangalia. haaaaaaaaaaaaaaaaaa

 9. Matty Says:

  Huyu dada naye ni kisura jamani anavutia, ubarikiwe dada kwa kumuimbia Mungu na pia nakupongeza kwa sauti nzuri uliyojaliwa na mwenyezi Mungu!
  Naupenda wimbo wako “shimo wamenichimbia eee watatumbukia wenyewe humo”

 10. edgar Says:

  Hi jenipher , nakuaminia kwa kutunga nyimbo tamu sana za kanisani,

  nakuzimia sana

 11. binti-mzuri Says:

  ameen!

 12. Ze Mdau Says:

  Sasa kutuwekea huco kidole cha mkono wa kushoto tukione manake ndo KUTUPIGA STOP au?

  Sasa Dada TUMEKUSOMA.

 13. michelle Says:

  Bado kana sauti ya kitoto inabidi aweke msisitizo anapo imba
  otherwise kazi ya Mungu iendelee, all the best!!!!!!!!!!!

 14. Matty Says:

  AMEN wapendwa! hapa hawajaja wenyewe wakasema tupunguze ukristolaizesheni hahahaha hata hivyo Tumsifu yesu Kristo!

 15. ma'reen Says:

  Beautiful and God fearing…what more can one ask for? Mungu akubariki dada. Huyu dada kaanza muziki wa injili siku nyingi na wala sauti yake hajaiga kwa Saida Karoli coz Saida kaingia mjini na kujulikana huku Jennifer kashakaa sokoni kitambo. Sidhani kama kuna kuigana sauti hapo! She’s simply blessed na sauti yake ameitumia kwa mema.

 16. debra Says:

  U mrembo dada mpendwa!!
  Bwana Yesu asifiwe !!
  Ubarikiwe mpendwa ktk bwana!!
  Amen

 17. adili Says:

  BWANA ASIFIWE DADA UNANIBARIKI SANA NYIMBO ZAKO NAOMBA MUNGU AKUBARIKI PIA KWANI NYIMBO ZAKO NI NZURI.

 18. prety girl Says:

  nampenda sn huyu mdaa coz yupo smart kimwili na kiroho pia,kwa kawaida mimi huwa napenda kusikiliza nyimbo zake kiukweli anaimba vzr sn.pia moja kati ya hizo filamu zake nimeiona kwakweli amejitaidi sn.keep it up my dia na MUNGU atakubaliki zaidi.Mwanakondoo ameshinda?2mfuate, AMEN

 19. kingo Says:

  wakti dada Jeny anaanza kuimba saida karoli nadhani hata kiswahili alikua hajui achilia mbali kuiona maiki!!!!!Mungu akubariki dada,kazi yako ni njema.

 20. gppmie Says:

  jamani mtu anaimba vizuri,hayo mambo ya kusema ameiga sauti ya mtu imetoka wapi? she is cute and humble to God. Big up sister Jeny and stay blessed.

 21. mkaku Says:

  Jamani Jennifer alikuwa anapenda muziki tangu yuo kisutu akingia kwenye muziki wa injili pia ni mwenyeji wa Singida na sauti yake ni ile aliyobarikiwa na Mungu haimbi kitoto ndio sauti yake ilivyo na anavaa vizuri sana i love her pia alikuwa room mate wangu ni mkarimu sana

 22. michelle Says:

  Jamani tukisema kwamba anaimba kama mtoto si tatizo ila ni maoni tu,kwamba ajaribu kuweka msisitizo atakuwa better than that, ni mzuri tunaamini anamsimamo wa kiroho, God bless you sister, all the best!!!!

 23. Jennifer Mgendi Says:

  Nawashukuru woooooote kwa maoni yenu na yanatutia moyo, yanatuonya na kutujenga. Mbarikiwe na Bwana!! Huyu anayesema ni roommate wangu ni nani huyu Mkaku, ni “Leah the Unshaken….?

 24. Matty Says:

  Afadhali dada Jennifer umejitokeza kutushukuru kwa maoni yetu,Mungu akubariki na wewe amen!
  Michelle umemsikia Jenniffer???anasema tubarikiwe na bwana!

 25. mambo Says:

  waibaji wengi wa injili wamejaa kashifa kibao, Lakini Jennifer yuko siku nyingi katika huduma na hatujasikia songombingo lolote. HONGERA SANA DADA. may God bless you

 26. mambo Says:

  I mean WAIMBAJI

 27. michelle Says:

  Matty,shost nimeipata sana hiyo baraka ya Jennifer, basi ndugu yangu Matty ubarikiwe na Bwana aishiye juu mbinguni!!!!!!!!!

 28. matty Says:

  hahahahah thanks ma dear Michelle AMEN!

 29. Daines Shartiel Says:

  Nakupa tano yaani nyimbo zako (tiki kubwa)

  Pia kila wimbo wako ni point huwa ninapata faraja sana ninaposikian wimbo wako wa “MOYO”

  Ninakuombea usiishie kuimba dunia tu bali uimbe hati mbinguni.

 30. Dory Says:

  Mimi nimempenda sana Jenifer kwa jinsi anavyoimba Mungu azidi kumbariki na kumuinua zaidi tunangoja kibao kingine cha nguvu kushinda kilichopita. Keep it up!!!!!!!

 31. Mama wa Kichagga Says:

  Jenny,

  Sikufahamu ila nyimbo zako zina upako! Ubarikiwe sana na Bwana na endeleza kipaji cha kumwinua Bwana siku zote.

  Amina.

 32. hs Says:

  Ubarikiwe sana dada “J” Ninabarikiwa sana na uimbaji wako kwani Mungu kaweka kitu cha pekee ndani yako
  Jehova akubariki na kukupigania ktk huduma yako

 33. Mary Mkwaya Malamo Says:

  bravo

 34. kwibisa seleman Says:

  nyimbo zako ni nzuri dada yangu na zinanibariki sana.

 35. CHANTAL MUKESHIMANA Says:

  Dadangu Jennifer hongera sana nyimbo zako zinanijenga kiroho Mungu akubarik na akuzidishie kipaji hicho cha kuimba.

 36. jeanine memba Says:

  Sister jennifer God bless you.
  I love you so much, I like to sing too when I was in Africa I was a singer (mwana kwaya) I like to praise LORD in songs.
  Just keep going to praise LORD!! Please E-mail me any time you want, I would like to have more informations from you.
  Thanks. Good luck.
  Yours jeanine from U.S.A(CoLORADO).

 37. kissa Says:

  jenifa ubarikiwe na bwana kwa kalama yako nzuri,kipawa ulichopewa kitumie sasa,mungu akubariki sana na udumu katika maombi na mungu akubariki maana kazi uliyopewa yahitaji maombi sana.barikiwa


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s