BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KATUNI ZA KIPANYA KWENYE MAONYESHO BERLIN August, 28, 2008

Filed under: Sanaa/Maonyesho,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 6:47 AM

Kama unaishi jijini Berlin huko nchini Ujerumani,basi leo utaweza kuona faraja pale utakapoona katuni ya KP au Kipanya(uchoraji wa Ali Masoud-pichani) itakapokuwa inaoneshwa katika njia za treni za jiji hilo(Berlin Subway System.

Kipanya inashiriki katika maonyesho ambayo yamepewa jina la Underground Exhibition ambayo yamekuwa yakiendelea jijini humo tangu tarehe 19 August 2008 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 1 September 2008.

Masoud anaungana na cartoonist wengine maarufu duniani ambao kazi zao zimo katika maonyesho hayo kama ambavyo unaweza kuona katika ratiba hii hapo chini.Tafadhali kama upo jijini Berlin itazame leo cartoon ya KP na kama inawezekana tuletee japo picha.

19/08/08 “Podium” by William Medeiros (Brazil)

21/08/08 “Auf die Plätze” by Christiane Pfohlmann (Germany)

23/08/08 “Made in China” by Herr Schewe (Germany)

24/08/08 “Skyrocketing Fuel Prices” by Prince M. Dhanta (India)

25/08/08 “Erster” by Freimut Wössner (Germany)

26/08/08 “Home Sweet Home” by Junior Lopes (Brazil)

28/08/08 “Dying” by Ali Masoud (Tanzania)

30/08/08 “Du bist Berlin” by Andreas Prüstel (Germany)

31/08/08 “Vulture Oil” by Mark Lynch (Australia)

01/09/08 “Trouble” by Pawel Kuczynski (Poland)

Advertisements
 

23 Responses to “KATUNI ZA KIPANYA KWENYE MAONYESHO BERLIN”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Ni habari njema sana.

  Nakupongeza sana mjasiriamali KP.

  pamoja …kipaji unacho

 2. EDWARD Says:

  Ali Masoud, hivyo ndivyo itakiwavyo, kulikuwa hakuna haja ya kulaza bongo zako ndani ya Radio bubu, kazana kaka mungu tu ndiye anayejuwa destination yako in life not otherwise, kuna maonyesho ya aina hiyo mengi tu duniani, hasa USA, UK, MEXICO, BRAZIL, JAPAN , FRANCE wewe search kupitia google.com na tembelea balozi zetu hapo nyumbani uwe unaomba habari ya mavituzzz kama hayo kwani wao watu wa roho safi watakusaidia tu hasa USA na CANADA.

 3. brother hugo Says:

  Hii imekaa vyema,
  KP kila la kheri katika upambabaji wako….

 4. Some more Says:

  Go on Masoud that is where u belong,though tunakumiss wewe na Fina katika Pb ile mbaya manake hawa wamezorotesha kipindi yani hata ukikosa kipindi siku hizi hata ulalamiki.Yani kipindi kiko Doroooooooooo.USIFE MOYO we endelea kufanya kazi kwa bidii tu.Sometimes nashangaa where is Kusaga?!manake sijui kwanini huwa hawasikilizi wasikilizaji tunataka nini! jamani Kusaga hawa watu hawavutii watoe kipindi kimezorota sana yani watu siku hizi tunaanza kusikilza kipindi cha Leo tena na kundelea.Why?!kwanini?!mmmhh.Gerald,Pj hamvutiiiiiiii wewe Pj kwako kwa Gadner G kusoma magazeti na habari na michezo,We Gelard bado me hata huninogei kabisa.Msinichukie niliowataja japokuwa inauma ila naamini mnakubaliana na mimi kwamba hamjafiti hapo mlipo.

 5. Majita Says:

  Salute kubwa kamanda wangu masoud.Hapo ndo PENYEWE mkubwa

 6. laila Says:

  Wewe “some more” hapo juu comments ulizotoa hazihusiana na mada….issue hapa ni kuhusu maonyesho ya KP Berlin sasa hawa wengine wa PB wanahusika vipi hapo? usitake kushangaza umati hapa kila mtu ana taste zake so kama wewe huwapendi kina Gerald basi acha kusikiliza kipindi kwani umelazimishwa?

 7. Pearl Says:

  hii imetulia.
  kila la kheri mkurugenzi.

 8. Lukamba Says:

  BIG UP CHIKUBA !!!! najua wadau wachache wanalijua hili jina,
  hili ndo jina lake la utotoni,usimwite kama hamjuani kivile,
  nakuombea kila heri bwana CHIKUBA

 9. Dada Missy Says:

  Hongera sana kaka Masoud kipanya endeleza kipaji kaka yangu… mimi binafsi naona hapo Radio clouds you dont develop at all (sorry for the harsch comment but that is my view).

  Umekaa na na kuzungukwa na watu ambao hawana vipaji, i dont want to mentioned names but wewe mwenyewe unajua ..

  well hapo radio clouds well you can still work but personal i think zingatia ushauri wa kaka Edward hapo juu na utaendelea zaidi kimaisha wewe bado kijana. so you need major developement..maana naona kaka yangu unaendeleza huo USTAR WA BONGO IS ambao ni TOO LOCAL, my bro you need to make MONEY dunia nzima and i know you can make it vitatuni vyako ni vizuri sana na ikibidi jiandikishe katika hizi short courses za cartoonist ili unjiendeleze kaka sina mengi ila nakutakia kila la kheri mungu akusaidie

 10. Edwin Ndaki Says:

  Majita wamai

  mambo vipi kaka?

  umeadimika sana.Tangu uwe kwenye timu ya kampeni ya obama umekosa muda kabisa wa kuja kuacha maoni hapa bc

  Ene wei tupo pamoja..

  ukipata muda tukutane japo mkendo kati pale bar ya mwisho kwa kalumuna japo Kemonda bar tupate kichuri na kabalimi…aa aaaa

  maana cash ingekuwa vema tungekutana penisula hotel au orange tree ila ndio hivyo tena..aaa

  siku njema kaka

 11. binti-mzuri Says:

  hongera,usitusahau na sie basii..lol

 12. Dogoboy Says:

  Hi, baba Malcom a.k.a “Kipanya”
  Nakupa shavu la kutosha katika harakati zako za kimaisha. Endelea kuwaonesha kuwa hukuwa unabahatisha bali unaweza.
  Siku zote wana wa Bongo tuko nyuma yako. Keep it up gentleman.

  Ni hayo tu

 13. kindo Says:

  Kazi nzuri KP!!!! Huu unaitwa ujasiriamali wa kweli…… hapohapo naungana na “Laila” kuwa hapa hatuzungumzii PB na what is currently going on, bali tunamzungumzia KP as a cartoonist na maonyesho yake Berlin. Pse “Some more” dont mix issues na usipende ku-divert mada. In any case wewe una mamlaka na redio yako. Wakati PB ikiwa hewani just tune off or change the station. Do you need to tell others what to do? Pleaz…..

 14. Majita Says:

  Yego Edwini Ndaki wasu,Kutiki mukaruka,
  Aisee!!!!Hili zali la kuchaguliwa kuwa kwenye kampeni ya Obama kwa kweli limefanya niwe bize sana.Yaani muda wooote nilikuwa sili wala sinywi.Hii yote ilikuwa tu ni kusubiria Chaguo la Makeini la viipii wake.Baada tu ya kutoka vipi na huyo mrembo wake sasa mimi fyuuu.Full kujiachia.Manake huyu Makopo yeye kaamua kutoka na chaguo la kudhihirisha alivyo panic na kutokuwa na uwezo kwa huyu bwana Jaluo.

  Kimsingi mimi nipo kila siku,na nahudhuria sana hapa jamvini,hadi siku ile uko golini mzee nyanda mwenyewe mimi nilikuwa nakuchungulia tuu na kushuhudia unavyokumbukia mambo ya Mjengo wa maarifa pale kwa mdau chini ya kwa mama Juma.Eee bwana ee sijasema Chumbageni wala nguvumali ila ni pale kwa mama juma.UNAPAKUMBUKA???

  Anyaway…kwa siku kadhaa hizi nimejikita sana Jamiiforum na nahisi huko unaniona sana.Ila baada ya Muungwana kukubali kuongezea muda wa kupeleleza EPA na kutufunga bao la kisigino basi ngoja tu nirudi tena manake hamu ya kukaa kule nayo imeniisha kabisa.

  Sasa Ndaki wasu hebu tukutane Palm beach Mwisenge kwa Kajanja opposite na bwalo la jeshi japo tupige stori kidogo.kama vipi tutapanga tukale Idd kule Boko bunju kwa Mkumbi pale Camp site.
  Majita

 15. Mimi Says:

  Yes Masoud keep it up Man,Kazi nzuri na juhudi zako nazo zinachangia.Mwendo huo huo wangu na 2one km utalala njaa .

  Maisha ni popote na Riziki popote,Navipenda sana Vikatuni vyako kwa kweli vinaujumbe vya kuelimisha jamii.

  Bt nakumiss sana hewani.ila aina noma chenye mwazo hakikosi kuwa na mwisho,Mie binafsi huwa sisikiliza BP mpk kwa Dina ndio naanza kufungua Radio 88.4.

  Goodbless you and Your Family.

 16. hombiz Says:

  toonz zako zimetulia kinoma mazee!. Pia zina uzito mkubwa sana hasa kuhusu mafisadi. Nitafurahi sana ukifanikiwa kupasua mawimbi ki-sawa sawa!. Kila la kheri KP
  GOD BLESS!

 17. debra Says:

  Edo Ndaki….Hehehee Majita!!
  Mweeeeeh

 18. dina Says:

  You deserve the best kaka, that ‘Kipanya’ surely deserves a world’s coverage….

 19. mkandarasi Says:

  Kipanya hata ukiwa hapa nyumbani you can still go international,mradi uwe mfuatiliaji makini tu wa ratiba za dunia! You have got what it takes to be an artist and cartoonist of international repute,boy! Jifunze lugha za kimataifa zitakupa dili babu kubwa. Some of the cartoons in kiswahili could even be in other international languages even though cartoons speak by themselves even without a caption!BIG UP SANA MANAKE! Tulisha sema wewe na FINA talent imejaa kibao! Sky is the Limit, nobody else punk! Hata Michuuz vilevile nilisha mwambiaga kwamba hata yeye anaweza kabisa kushiriki International Photo Exhibitions popote pale ulimwenguni! Kipaji anacho. Jamani onyesheni mfano ili wadogo zenu wafuate nyayo zenu. Ule wakati wa giza (kiza) ulishapita.Hata sisi watanzania tunaweza vilevile.Congratulations Kipanya! Wale ma pussy achana nao,wewe ni mbele kwa mbele!

 20. Lina Says:

  KP nakupa hongera sana hapo ulipofikia. Kipaji unacho kaka kaza buti wadau tuko nyuma yako japo kwa mawazo tuuu.

  Ila ni kweli tunakumiss sana hewani uongo mbaya bwana. PB imedororaaaaaaaa kama kuku mwenye mdondo.

  Tunapokuona lazima tunakumbukia PB kwani mlitupa mavituz ya uhakika na kusuuza nyoyo kupitia masikio yetu wewe na Fina. Na tungependa siku moja na Fina nae tumuone na atupe yake machache kuhusiana na Life after 88.4.

  Ol in ol nakutakia kila laheri katika shughuli zako na nina imani tayari utakua Balozi mzuri wa Tanzania hukoooo uendako.

  Big up KP!

 21. totolako! Says:

  Hongera sana Bro! keep it up
  uko juu sana na bado unakwenda juu,lazima ushinde nakufagilia kinoma,
  kaza buti!!!!!!!!!!!!!!!!

 22. Mama wa Kichagga Says:

  Machudi,

  Endeleza kipaji na daima fanya mambo yanayoikomboa jamii maana ndipo kipaji chako kilipo!

  Usiogope nena na kemea maovu siku zote na Bwana atakua ngao yako daima.

 23. jerry Says:

  keep it up my homeboy KP……God bless u in all ua doingz…..


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s