BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WHEN THE SMITHS MET THE KARUMES August, 30, 2008

Filed under: Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 11:54 AM

Advertisements
 

37 Responses to “WHEN THE SMITHS MET THE KARUMES”

 1. Ramsfel Says:

  kina mama wote wawili wamependeza kwa kivazi cha heshima mke wa smith anaonekana kama msichan wa kawaida wakizanzibar kapendeza sana ni kweli nguo za heshima huwahazimtupi mtu na huwa unazidi kupata heshima

 2. Mzanzibar 100% Says:

  zanzibar ni njema, atakae aje! Ukija zanzibar utapelekwa ikulu kama Willy…!

  Halafu utapata wenyeji wenye ukarimu na upendo, watakutembeza dole, mchamba wima, mnara wa mbao, soko muhogo, na malindi pia utapelekwa ukaone simba na ukali wake alivyonyweshwa chai..! Ha ha ha usiogope, kama utashindwa kukaa kwenye MKEKA utapewa KIGODA ukalie…!

  Zanzibar MINAZI tele, kuna mirefu na mifupi (twaita kitamli), minene na myembamba! Kama utapenda kula nyama ya dafu ukisha kunywa maji yake basi UTACHOKOLEWA, na ukinunuwa vocha ya simu pia UTASUGULIWA wala hupati tabu Zenji raha kila kitu wafanyiwa..!

  Kama WALI WA KUNDE ukisha iva UTAPAKULIWA (zanzibar hakuna self service), yaani kila kitu we utakarimiwa! Kama huna kazi mashaallah..utapelekwa pwani ya KIWENGWA ukapare samaki au “UTAPARA MIWA” mahonda! Huko mahonda ndo kwenye kiwanda chetu cha sukari, zanzibar miwa teleeeeeeeeeeeee!

  Matty na Watanganyika wengine (waosha vinywa) karibuni zenj mtakuja kwa meli, boti au mashuwa?

 3. Mlevi Says:

  Hivi kweli jamani, kiProtokali na kiHadhi, mtu mdogo kama huyo kulikuwa kunaulazima wa kwenda mpaka Ikulu kuonana na Rais kweli?
  Au ndio kuwadhalilisha marais wetu?
  Hakupaswa kuona na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo tu jamani?
  Hivi MASANJA MKANDAMizaji akienda Amerika atapata nafasi kama hii ya kuonana na BUSH kweli?
  Nyie Washauri – Wizara ya Mambo ya Nje na Ikulu mnafanya kazi kgani sasa?
  Wacheeeni Hizoooo!

 4. Ze Mdau Says:

  Kuna Mlevi mmoja kauliza:-

  Hivi kweli jamani, kiProtokali na kiHadhi, mtu mdogo kama huyo kulikuwa kuna ulazima wa kwenda mpaka Ikulu kuonana na Rais kweli?
  Au ndio kuwadhalilisha marais wetu?
  Hakupaswa kuona na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo tu jamani?
  Hivi MASANJA MKANDAMizaji akienda Amerika atapata nafasi kama hii ya kuonana na BUSH kweli?
  Nyie Washauri – Wizara ya Mambo ya Nje na Ikulu mnafanya kazi kgani sasa?
  Wacheeeni Hizoooo!

 5. BLACKMANNEN Says:

  Willy na Jada, jisikieni nyumbani, sisi ndivyo tulivyo, wakarimu na wapenda wageni, na “Amani” ikiwa ndiyo nguzo yetu!

  Black=Blackmannen

 6. Muh LUKAMBA Says:

  Haya !! we mzanzibar 100% tuchefue tena uone,
  Karume kwao Tabora,willy smith kwao Iringa kwa data zenye uhakika kabisaaa !!toka vizazi na vifo makao makuu,Data za mke wa will ndo tunazishughulikia.

  Kwahiyo willy,Karume wapo kwenye kisiwa cha Tanzania uko MAENEO ya zanzibar,siyo nchi ya zanzibar !!!

  Mzalendo halisi.LUKAMBA

 7. Dada A Says:

  Mimi naona ukarimu wetu umezidi kipimo yaani mtu wakawaida ndio kumeleka ikulu mhhhhhhhh no comments..

  kaka mlevi you are right in your comment..na wewe mzanzibar anza mbele nchi inaitwa Tanzania na sio Zanzibar…upo au geografia haipandi…

 8. Anonymous Says:

  Huyu mzanzibar ana hashuo la kiume hehehehe maana kangangana zanzibar nchi kweli kuna watu wana akili za kikoloni….

 9. neema Says:

  Hey nduguzanguni hapo juu wote mnayoyasema ni ya ukweli kabisa hii serikali yetu ya bongo na hao viongozi wetu wa bongo mbona washamba sana? au ndiyo kusema ukarimu umetujaa sana ? Maana mimi nipo hapa marekani mwaka wa 10 sijawahi hata kuona huyo meya hana picha na hao mastar?
  Jamani viongozi wetu huko nyumbani amkeni msiwe hivyo.Mtu gani huyo wakumfikisha ikulu au mngemuuliza kama ameshawahi kutia mguu wake White House……. And then…..
  Peace

 10. neema Says:

  Wadau wenzangu nilikuwa sijaicheck fresh picha ya hawa waungwana.. huyu Will Smith baba yake karume nini ? Mbona wamefanana sana, Au ndiyo hizo mvua alizokuwa akizimwaga karume huko nyuma sasa maury show kampatia Jada in Law…

 11. Queen Says:

  Watu wengine bwana,hivi kweli unaweza kucompare Will&Jada Smith na Masanja mkandamizaji?Hawa na masuper Star hata Karume anajua,Bush mwenyewe anajua.Na kuacha mbali umaarufu wao,hawa watu wana mapesa kibao ambayo wanaweza kutoa msaada kwa nchi zetu hizi za kimaskini.Kwa hiyo sijaona ubaya wao kumtembelea Rais wa Zanzibar nafikiri ni bahati mbaya hawajakutana na JK.Ebu fikiria mwanamama Oprah Winfrey na ile shule ya kimataifa aliyoinjenga South Africa,mbali na sababu zingine,ni urafiki wake wa karibu na Mzee Madiba ndio ulikuwa msukumo.Lets think positive people.Samahanini haya ni mawazo yangu tu,msinishambulie.

 12. trii Says:

  picha nimeipenda.

 13. Dunda Galden Says:

  kwa mbali wako kama dugu moja

 14. Muh LUKAMBA Says:

  MLEVI kweli umesema jambo la kweli kabisa,huyu jamaa pamoja na usuper stars wake lakini asitaili kuingia IKULU !!!
  Kila siku mi nasema wangi wa viongozi wetu,WALIFOJI vyeti.
  unajua kuna vitu vinafanywa na viongozi bongo,uwezi kumwambia mtu wa nchi nyingine,
  kuna ziara JK alikwenda marekani na hakuonana na BUSH !!!mpk mwisho wa ziara yake.Hii ziara aliyomaliza ndo ya kwanza Jk kukanyaga White house !!!
  sasa ukisema masanja mkandamizaji,wakati raisi wake wa nchi hana chance hiyo !!!! kweli we mlevi !!Ahaaa
  alafu wa mzanzibar 100% ebu andika matapishi tena one balaa langu !!

 15. binti-mzuri Says:

  nakubaliana na mlevi..will smith sasa ikulu kwa nini? ndio kama ile big brotha ya kwanza,eti abby wa south africa nae ivo ivo.. you people,embu nyambueni nani wa kwenda ikulu na nani wa kubaki,kama alikua anatoa charity,si angeonanana na waziri wa utalii walau..tena naibu wake..sio yeye mwenyewe.. this is bollocks!

  ka-jada kamependeza lakini..mmh…izo zimetoka americaa au zanzibari,nianze kuorder fasta fasta

 16. lailatul Says:

  mbona BC hujatuupdate nasikia Rukia Bruno kafariki

 17. Mzanzibar 100% Says:

  Nyie watanganyika aka vichogo ZANZIBAR ni chi habari ndo hiyo…! Kama mmenuna nendeni mkakaushe bahari ya hindi muje zanzibar kwa miguu…!

  Anon wa Aug31,2008 at 12:15pm, swadakta manenoyo nna hashuo lakiume tena kubwaaaaaaaaaaa…! Yawezekana we mashuwa , sharti nahodha akae nyumaaa, karibu zenji basi!

 18. Gervas Says:

  Acheni wajameni kupiga domo Will Smith sio mchezo bwana, mbona hata JK alipoenda US last time akapiga picha na Boys II men? Hawa watu wana-feel raha sana wanapokuja Africa nakukaribishwa ikulu wanafeel home and accepted. Wanafanya hivo sababu ni ngozi nyeusi. Ndo maana unaona hata Birthday ya Mandela walioalikwa wengi ni hao hao ma-black celebrities kina Lady Jaidee, Smith nk. Msisahau pia Smith ni ambasador wa UN maralia bla-bla… sijui kama mmeipata connection.

 19. Matty Says:

  Haya we mzanzibar 100% unabahati sana Jeff kaminya maoni yangu chini kwa chini, acha ujinga eti Znz ni nchi muone kwanza!
  Hizo mashua hatuna haja nazo kwa taarifa yako watu tunakodi private charter Dar/Znz & back!kalaghabao!

 20. Mchongo Says:

  Mh! Kweli Bado Watnzania tunaonyesha kutojua thamani yetu, mtu mdogo kama huyo si wa kuingia Ikulu, Rais ni Kiongozi wa Juu wa nchi huyu mtu aliyeingia Ikulu ni wakawaida tu,

 21. ma'reen Says:

  Suala la Z’bar ni nchi halitakaa lipatiwe ufumbuzi kwenye majibizano ya kisiasa/blogs…Sidhani kama issue ni kupata jibu kama kweli ni nchi au sio nchi. They (Zbar) might have grievances which might have bn ignored 4quite a long time na ili muungano udumu, lazima ziwe dealt with 2the satisfaction of both sides. We shud not percieve the union as a sacred thing which was concluded by Nyerere and Karume ambacho kukidiscuss ni kama kula 4biden fruit no! We are not stagnant, inawezekana kuna yaliyofaa wakati huo kwa sasa yanahitaji marekebisho let’s deal with them! Kuhusu Z’bar kujitenga I don take this as a wise decision…we are now speaking about unity among nations…vi-nchi kama Rwanda na Burundi vime-fight weee ili viingie East African community, unaundw umoja wa nchi zilizopakana na Mediteranean etc kujitenga itakua kurudi nyuma badala ya kusonga mbele… mawazo yangu! Otherwise comment No. 2 ya Mzanzibari imeniburudisha nimecheka mpaka basi…huyu kweli ni Mzenji 100%

 22. Muh LUKAMBA Says:

  Acheni kutuchanganyia HABARI,zanzibar ni ENEO huko kwenye visiwa vya Tanzania,
  Katika list ya nchi duniani hakuna nchi inaitwa zanzibar,check na google,ila kuna eneo linaitwa hivyo huko Tanzania.
  WILLY kwa gharama yeyote asitaili kuingia ikulu,huyo ni uvunjwaji mkubwa wa hadhi ya IKULU,
  Kwahistoria,NYERERE,MWINYI,MKAPA ajawai kuingia WHITE HOUSE
  Kama unabisha nakufungulia msaafu,
  JK ndo raisi wakwanza wa TZ kuingia White house,kama siyo wa pekee AFRICA.

 23. kahindi Says:

  hii nimeipendaaa

 24. chichemi Says:

  Acheni nyinyi. Mzee Karume akikaa barzani na kupiga stori na kila mtu sasa whats the big deal Dr Karume kuwaalika mr and mrs Smith? Huko Ikulu wameingia kina Raza na madili ndio itakuwa kina Will

 25. thms Says:

  wachangiaji wengi ni mambumbumbu hasa huyu mzanzibari%100 nadhani kichwani hayuko sawa.
  Smith na mkewa hawakuenda z’bar kama wao, bali wameenda kama mabalozi wamefadhiriwa na taasisi ya kimataifa inayojishughurisha kutokomeza ugonjwa wa malaria. z’bar ni sehemu pekee katika afrika ambayo imefanikiwa kuushinda ugonjwa wa maralia.
  sasa Smith akiwa kama balozi wa anapelekwa visiwani kwenda kujionea mwenyewe hari ilivyo na ndio maana anakutanishwa na rais ili amueleze ni mbinu zipi zimewawezesha kufika hapo walipo fika.
  akitoka hapo anarudi huko wa wafadhiri na hao wafadhiri wanaongeza misaada kwa lengo la kusaidia kutokomeza kabisa maralia
  tuwe tunafuatilia habari usilaumu tu,

 26. asmah Yahya Says:

  Kwa kweli inabidi sasa ifike wakati tupevuke, simba na panya wote ni wanyama lakini huko mwituni wote hawana hadhi sawa, hivyo ni makosa kumlinganisha will smith na masanja, na kwa taarifa tu, ni kuwa katika mara zote nne ambazo jk ameenda marekani alionana na Bush. kilichofanya rais wa zanzibar aonenane na will smith ni ile kofia yake ya balozi wa heshima wa UN na mchango alokuja kuutoa kwa jamii ya watanzania. Watanzania tupunguze lawama, let see things in positive. mkumbuke zanzibar ni nchi ndani na si katika jumuiya ya kimataifa

 27. ze news is that Says:

  Jamani kumbukeni will alikuwa kati ya waliyofanikisha shughuli ya madiba, sasa iweje mnaponda ki hivyo?

 28. Matty Says:

  anewei lets forget abaut Znz ni nchi hahahahah Mzanzibari pls usinipige ngumi ya uso….eti vichogo!!!na wewe huna kichogo unakitamani aluuuuuuuu pole weeee libeneke kama kawa Znz ni kasehemu tu kaliko Tz.

 29. binti-mzuri Says:

  wewe mh lukamba,nawe vipi tena?

  umesema hivi:

  Acheni kutuchanganyia HABARI,zanzibar ni ENEO huko kwenye visiwa vya Tanzania,

  kwani kisiwa si ndo zanzibar? pemba,mafia,unguja? na bara ndio tanganyika,so kwa pamoja ndio tz au?

 30. Mh Lukamba Says:

  Binti- mzuri samahani,Mfupa hauna ulimi,zanzibar ni ENEO la kisiwa huko Tanzania,siyo Nchi,ni ENEO tu.

  Pia visiwa ni Unguja na pemba tu,hakuna kisiwa cha zanzibar,
  zanzibar ni neno baada ya muungano,kama ilivyo Tanzania,ni neno baada ya muungano.

  ukivunja muungano unabakiwa na tanganyika na unguja na pemba.

  Kiukweli atujawai kuungana na zanzibar,tuliungana na pemba na unguja,mafia iko bagamoyo.

 31. Mh Lukamba Says:

  Jeff usinibanie hii,
  We THMS#25 unatuita mambumbumbu !!! we unaonekana ni times 5,maana kwanza tofauti ya R na L ujui.
  Pili division of labour ujui !! waziri wa afya yupo zanzibar,Raisi na balozi wa malaria wapi na wapi ???
  alafu bado umewekeza akili kwenye kuomba misaada 2222222 !!! shame upon U,
  Kwa taarifa yako,hakuna mtz asiyejua jinsi ya kijikinga na malaria,ni uzembe 2.
  Point ni willy kuingia ikulu,na siyo malaria

 32. binti-mzuri Says:

  dah umenirudisha darasani lukamba,asante kwa kuweka bayana.

 33. Joe Jr Says:

  Jamani inabidi muache ushamba ! Mimi nasupport kabisa kwa Will Smith kutembelea Ikulu… inabidi muangalie the positive side kuwa hao masupa staa wanainfluence kubwa katika kupromote utalii na kuendeleza culture za nchi. Jamani tuache kuendekeza sana heshima na kutaka kujikuza .. mbona mafisadi hamwapigii kelele wanapotembelea ikulu…
  huyu anayesema kuwa amekaa Marekani miaka kumi na hajawahi kumuona hata Meya amepiga na masupar star .. wewe acha kudanganya watu .. Marekani ni kubwa na watu wanamajukumu tofauti ..au schedule ndio zinakufanya unconclude issue bile kufayanya reserch .. wewe kama huna mda wa kuangalia news mbali mbali acha kudanya watu ambao wako Bongo.
  Mara ngapi tumeona masupa star wanaalikwaga white house?
  kila mtu anahaki ya kwenda ikulu kama Rais ameona kuna mhimu wa kukutana ana kwa ana..
  .. Wabongo tubadilike tuwe tunaangalia na positive side ya issues …. Nampongeza Rais wa Zanziber kwa kumkaribisha Willy…

 34. Lumi Says:

  Will Smith kukaribishwa na raisi Karume sio ajabu. Hamjui kama huyu bwana aliomba kukutana na raisi Karume kama hajaja Tanzania. Willy Smith kwa taarifa ni balozi na mchangiaji mkubwa wa miradi ya maendeleo barani Africa ikiwemo Malaria, visima vya maji safi, watoto (UNICEF), na huko Afrika Kusini amejenga vituo kama vitatu hivi vya michezo kwa ajili ya watoto Yatima. Hivyo wadau msibwabwaje bila kujua undani wake kwa nini alikwenda IKULU.

 35. Mh Lukamba Says:

  Dah,we JOEl,unaakili timamu kweli wewe???super star kuingia white House???4 wat big reason?
  alafu unavyosema marekani watu wana majukumu !!! ina maana Tz ndo watu awana majukumu??

  alafu unajua nini maana ya IKULU?? ukitaka kujua nini maana yake na nini thamani yake,nenda hata ikulu ya

  kigoma,bukoba,mtwara,lindi nk utakuta askari masaa 24 siku 365,na raisi anakwenda labda mara 1 kwa mwaka,

  Jk nyerere alikwenda mara 1 kigoma,mwinyi,mkapa awajeenda kabisa,lkn nenda kaangalie ikulu ya kigoma.

  Bush amekwenda mara nyingi Iraq,afghanistan nk,inamaana watalii wanakwenda iraq???maana bush ni zaidi ya willy,acha kutudangaya we !!!
  Ikulu ni zaidi ya unavyofikiria.

 36. Angel Says:

  Kwaufupi, nafkiri sisi WaTanzania are the best. Vyovyote mtakavyo chukulia… we know how to receive and be down to earth. (Thinking out loud,…..Did Jada had to think ” mhhh what will i wear” LOL) Samahanini kama nitakuwa nimewakosea!

 37. Joe Jr Says:

  Mh Lukamba itakuchukua mda sana kukuelemisha , elewa issue kabla hujaanza kujadili “alafu unavyosema marekani watu wana majukumu !!! ina maana Tz ndo watu awana majukumu??”
  Mimi nilisema “Marekani ni kubwa na watu wanamajukumu tofauti ..au schedule ndio zinakufanya unconclude issue bile kufayanya reserch .. ”
  Did i mention anything about Tanzania here?
  hii inaonesha kuwa upeo wako wa kufikiria umejawa na jaziba tupu.. Jitahidi uwe na diplomasia ya kukubali kukosolewa ili ulimike .
  Niambie kama bado unahitaji msaada kwenye tuta ili kukupatie resources za jinsi kuwa mwanablog wa karne hii ya 21.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s