BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JENERALI ULIMWENGU September, 30, 2008

Filed under: Magazeti,Uandishi — bongocelebrity @ 10:03 PM

Pichani ni Jenerali Ulimwengu.Huyu ni miongoni mwa waandishi wa habari nchini Tanzania walio na uwezo wa aina yake katika kujenga na kubomoa hoja iwe ni katika maandishi au maongezi.Makala zake siku hizi zinapatikana katika gazeti la Raia Mwema.

Photo/Bob Sankofa

 

SIKUKUU NJEMA

Filed under: Sikukuu — bongocelebrity @ 10:43 AM

Tunawatakieni nyote sikukuu njema.

 

WANAMUITA MR.BLUE September, 28, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 10:58 PM

Wimbo uliomtoa ulikuwa ni ule uliokuwa ukiinadi rangi ya blue.Pengine ndicho chanzo cha yeye baadaye kuja kujulikana kama Mr.Blue.Pamoja na hayo wimbo wake ulioitwa “Mapozi” ndio ulikuja kutamba kwa staili ya aina yake.Baada ya hapo ikawa ni mapozi nawe,mapozi nawe.Lakini kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya anabakia kuwa Mr.Blue.Hivi karibuni alikuwa katika ziara ya muziki nchini Uingereza.Ni miongoni mwa vijana walioko katika fani ya burudani kupitia muziki nchini Tanzania ambao wanaweza kusema “wanafanya vizuri” katika wanachokifanya.

Mcheki hapa chini katika wimbo wenye ahadi nzito nzito za kurejea kulifuata penzi.

Photo courtesy of Abdallah Mrisho

 

NGAPULILA-VIJANA JAZZ BAND September, 25, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:33 PM

Jinsi miaka inavyokwenda ndivyo hata mipangilio ya mwisho wa wiki inavyobadilika. Kuna nyakati watu walitumia muda mwingi wa mwisho wa wiki wakiwa feri wakijipanga vyema kwa mipango kabambe kuhusu namna ya namna ya kuzamia melini wakaibukie Greece kusaka maisha.

Hizo ndio nyakati ambazo nchi kama Marekani zilionekana za wazee na wenye pesa (kama alivyosema Sugu) huku vijana wakiamini kuwa maisha yanaanzia kwenye nchi ambazo zinafikika kwa meli hasa Greece. Bahati mbaya wapo walioishia majini na wengine kuteseka mpaka kufa kwa kukosa chakula. Unakumbuka nyakati hizo? Nyakati za kuamini kuwa huwezi ku-win maisha Bongo?

Hapa tunao Vijana Jazz Band enzi za “Pambamoto Shambulia” wakiwa na safu kamili na stadi ya kina Hayati Hemedi Maneti “Chiriku” , Eddie Sheggie “Fast Mover”, Shabani Yohana “Wanted”, Super Sax Rashid Pembe na wengineo wakielimisha jamii juu ya athari za uzamiaji kama aliokuwa akitaka kuufanya Ngapulila.Wimbo unaitwa Ngapulila.Pata Burudani,wikiend njema.

Ujumbe na burudani ya leo imeletwa kwenu na blogger mwalikwa,Mubelwa Bandio, anayeblog kupitia www.changamotoyetu.blogspot.com.Mtembelee.

 

ALLY REHMTULLAH’S LONDON FASHION WEEK LAUNCH September, 23, 2008

Filed under: Fashion Designer,Photography/Picha,Sanaa/Maonyesho,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 9:57 PM

It is every designers dream to be part of the London Fashion Week, and this year Ally Rehmtullah, a 22 year old Tanzanian designer was given this honour. On the 19th of September Ally Rehmtullah launched his new African Couture at the Museum of London during the London Fashion Week. Ally was also part of fashion diversity whereby as an established designer he was an inspiration to the young and upcoming designers in London. Ally Rehmtullah’s couture was modelled by MAHOGANY MODELS from London.Here are some images.

(more…)

 

NANI ATAIBUKA MWANAMITINDO BORA EAST AFRICA? September, 22, 2008

Filed under: Fashion,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 10:25 PM

WALIMBWENDE 13(pichani) wamefuzu kutinga kwenye fainali za kinyang’anyiro cha michuano ya kumsaka mwanamitindo bora wa Afrika Mashariki kitakachofanyika Novemba 29 jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa waratibu wa kinyang’anyiro hicho Judy Felician alisema leo kuwa walimbwende hao 13 wataingia kambi mwezi ujao pamoja na washindi wengine kutoka nchini za Kenya Uganda, Rwanda na Burundi kupata washindi wanne ambao watakwenda kushiriki kwenye shindano jingine la uanamitindo nchini Ugiriki.

Judy alisema nchi za Kenya Uganda, Rwanda na Burundi zitatoa walimbwende watatu kila moja ambao wataungana kambini na walimbwende 13 wa hapa nchini katika kambi ambayo itaanza Oktoba 25 jijini Dar es Salaam. (more…)

 

USHAURI WA BABU KUHUSU TALAKA!

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 10:22 PM

Raha ya BC ni pamoja na kuburudika na pia kuelimika.Kuna mtu katutumia hiki kipande cha “ushauri wa babu” kuhusu talaka na akatusihi tukiweke hapa ili nawe msomaji upate kumsikia babu.Ni kuhusu talaka.Tunaomba kuwakilisha.Halafu hakuna kucheka!Asante.

 

UNATAKA KUJISHINDIA BENZ?

Filed under: Tangazo/Matangazo — bongocelebrity @ 10:15 PM

Piga picha hii.Unanunua gazeti,unapata habari mbalimbali,unaburudika,kuelimika na kufahamu mengi yanayoendelea nchini Tanzania na hata sehemu zinginezo za ulimwengu.Kwa wengi hilo ni jambo muhimu na linalojitosheleza kabisa.Lakini je ungepewa pia nafasi ya kujishindia zawadi kama gari aina ya Mercedez Benz kwa ununuzi na usomaji wako huo huo wa gazeti/magazeti ungechangamkia tenda?

Basi hilo linawezekana kupitia promosheni kabambe inayoendeshwa na kampuni ya uchapishaji magazeti ya Global Publishers.GP ndio wachapishaji wa magazeti ya Uwazi,Championi,Ijumaa,Risasi,Amani,Ijumaa,Wikienda,Bongo Sun na Jarida la School & College.Kwa habari zaidi na jinsi ya kushiriki kwenye promosheni hii,bonyeza hapa.Kazi kwenu,Benz sio kwa ajili ya kina nani hii tu kumbe!

 

LATOYA NJE YA BIG BROTHER AFRICA! September, 21, 2008

Filed under: Burudani — bongocelebrity @ 8:12 PM

Mwakilishi wa Tanzania katika shindano maarufu la Big Brother Africa,Latoya, amekuwa mshiriki wa kwanza kuondolewa ndani ya jumba la Big Brother Africa!Kwa maana hiyo Tanzania safari hii imeambulia patupu baada ya kuonekana kuwa tishio katika misimu miwili iliyopita ya shindano hilo.Kama mtakumbuka Mwisho aliibuka mshind wa pili na Richard akaibuka namba moja.

Nini kimetokea?Unadhani kwanini Latoya ameishia hapa?Kuna yepi ambayo Mwisho Mwampamba na Richard Bezuidehout waliyafanya ambayo Latoya hakuyazingatia?Mjadala u-wazi.

 

JK ZIARANI MAREKANI

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 8:09 PM

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini jana (Jumamosi, Septemba 20, 2008) kwenda New York, Marekani, ambako atahudhuria na kuhutubia kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).

Rais amepangiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne ijayo, Septemba 23, 2008 katika nafasi yake pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu, Rais Kikwete amepangiwa kuhudhuria mikutano mingine muhimu kuanzia ule ambao utaangalia Mahitaji ya Maendeleo ya Afrika. Mkutano huo, utajadili ahadi za nchi tajiri kwa Afrika na Maendeleo ya Bara hilo, na kuona ahadi hizo zinatekelezwa namna gani.
Rais pia atahutubia kikao cha ufunguzi cha viongozi ambao watajadili maendeleo ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s). Baada ya kuwa amehutubia kikao hicho, Rais atashiriki katika mijadala kuhusu afya ya Mama na Mtoto, na pia mjadala kuhusu ugonjwa wa Malaria, masuala yote mawili yakiwa sehemu muhimu ya MDG’s.

Ijumaa, Septemba 26, Rais atakwenda mjini Washington, ambako atatoa hotuba muhimu ya ufunguzi kwenye Kikao cha Mwaka cha Wabunge Wenye Asili ya Afrika katika Bunge la Marekani, na pia kuhutubia mkutano wa viongozi wa shughuli za biashara katika Marekani.

Mbali na mikutano ambayo amepangiwa kuhutubia ama kushiriki, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wengi wa shughuli za kisiasa, kibiashara na kiuchumi duniani na katika Marekani.

Miongoni mwa viongozi ambao Rais Kikwete atakutana nao na kufanya mazungumzo nao ni pamoja na Rais wa Iran, Mheshimiwa Ahmedinajad; Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Mheshimiwa Javier Solana; na mfanyabiashara maarufu duniani wa shughuli za kompyuta na teknolojia ya mawasiliano, Bill Gates.

Rais Kikwete pia atakutana na Waziri Mkuu wa Denmark, Mheshimiwa Anders Fogh Rasmussen; na Katibu Mkuu wa Shirika la Kazi Dunia (ILO), Juan Somavia.

Rais Kikwete pia atafanya kikao cha pamoja kati yake, Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon na Makamu wa Rais wa Sudan, Ustaz. Ali Osman kuzungumzia mgogoro wa eneo la Darfur nchini Sudan.

Wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika Sudan mwanzoni mwa mwezi huu, Mwenyekiti huyo wa AU, alimwahidi Rais Omar El Bashir wa Sudan kuwa angefanya kikao kati yake, Katibu Mkuu wa UN, na mwakilishi wa Sudan kuhusu hali ya Darfur wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Kikao hicho kitaangalia jinsi gani ya kuharakisha zoezi la kupeleka askari wa kulinda amani wa UN na AU katika Darfur, na pia jinsi ya kuahirisha, kwa angalau mwaka mmoja, hati ya kukamatwa kwa Rais Bashir iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC).
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.