BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAMBO BADO-MAKASSY September, 4, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:29 PM

Ile kufumba macho na kufumbua, wikiendi imeshawadia. Kwa wale wanaoishi ughaibuni katika zile nchi ambazo hupatwa na wazimu fulani yanapokuja majira yaitwayo “summer”, karibuni watajikunyata tena kwa baridi (winter). Ajabu ukiwaambia warudi nyumbani Bongo ambako kila siku ni summer,wanakuangalia na jicho fulani hivi ambalo litakupa majibu elfu kidogo kabla hata hawajasema kitu.Ukiwauliza zaidi wanakwambia Mambo Bado! Mpaka lini?Hata hivyo siwalaumu sana.Mambo yenyewe si mnajua yanavyokwendaUkitaka kuwin lazima ujiunge na lile kundi.Usipofanya hivyo,basi ujiandae.Unaleta wema wakati wema ulishazikwa? Kinachotakiwa hivi sasa ni kama vile anavyosema Prof.Jay kwamba ukimwaga ugali namwaga mboga,ngoma droo.Bahati nzuri tuna watu kama Ndaki ambao kila kukicha wao wanatukumbusha kwamba Tutafika Tu!Lini?

Naam kwetu sisi hapa BC,Ijumaa ni kama kawaida.Ni siku ya kupata burudani kidogo kutoka katika yale makasha yetu ya “Zilipendwa”.Burudani ya leo inatoka kwa Makassy.Wimbo unaitwa…Mambo Bado. Pata Burudani,Wikiendi Njema.

Advertisements
 

36 Responses to “MAMBO BADO-MAKASSY”

 1. mkandarasi Says:

  Mambo Bado ni composition ya mwanamuziki Tshimanga Kalala ASOSA wakati huo akiwa na kundi la Mzee Mackassy! Heshima Mkuu kwa burudani tosha!

 2. rahma Says:

  mambo baaado mambo bado…………………magoma motmoto dalisalamaeeee.

 3. Muh LUKAMBA Says:

  Imenikumbusha mbali sana,na upara wako makassy !!!
  bab kubwaa !!! kweli mambo badooooooo.
  Tunazeeka hiv unatuambia mambo bado???

 4. matty Says:

  Wknd njema wote! mambo bado hahahahahaha ni kama bado nipo nipo kwanza!!naupenda huu wimbo sana!
  Any uwapi weye mbona kimya shosti???
  Binti Mzuri na wewe vipi upande wako umetingwa na nini bibie??
  Pearl & M’areen,Mama wa Kichaga natumaini mtaenjoy wknd hii!
  Kekuu shosti this wknd tutakuwa wote if God wishes hahahahaha lazima tukamue na Ramadhani hiiiiii balaaaaaaaaaaa
  E.Ndaki, Gervas,Chris, Nalitolela,na wengineo mpoje??bila kumsahau mh.Lukamba natumai mtaenjoy wknd hii.
  Mzanzibar 100% ramadhani inasemaje???swaumu kali au??

  wknd ni njema all of you!

 5. EDWIN NDAKI Says:

  Yaani kweli BC napendezwa sana na ze burudani ya kila ijumaa.

  hakika kweli mida kama hii…mibovu kwani hali ya weza inazidi kubadilika.Kajua ka kubip na kagiza ka kumwaga..hapo bado kamufindi hakajashika nafasi yake.

  Nawatakia kila la kheri mapumziko mema ya mwisho wa juma.

  Tupo pamoja watu wangu…

  naamini tu tutafika ..si mnaona leo “Baraka obama” kalamba “joker” ..hapo mwanzo watu hawakuamini itawezekana ila Luther alisema anayondoto…

  Tukaze buti..tutafika tu

 6. majita Says:

  Hapo ndo penyewe.Jamani mbali na ka wimbo aka kazuri ka magoma motomoto ya Nairobi mimi nimepata jirasi kwa kweli.Yaani hadi hapo hakuna aliyenitakia wikinenda njema,haya Ndaki na Matty poa tuu,sisemi kama tutafika tuu…

  Eeeh ebwana eeh BC leo wakati najikumbusha kawimbo aka ka zamani kidogo,mara nikakumbuka taarabu moja hivi, ebu kama mtaweza mnifanyie uungwana neksti taimu mniwekee. Taarabu yenyewe ni ile ya “Nyama ya Bata”.Kuna beti moja nilikuwa nalipenda SANA nalo lilisema

  Chakula alacho bata na ndicho alacho kuku,kuku,kukuu
  Tofauti nimepata Bata kazidi shauku,uku,ukuuu,
  (Bata mlo na kwa kunona,Na masalo umpakeex2)
  Nyama ya bata ni tamu nyama ya bata nitamuuuuuuuuu…
  Kwa chapati,Kwa matonge (ya wajita),kwa pilau…..

  Hahahahahahahahah,kwikwikwi yaani nakumbuka sana enzi hizo nikiwa shule huku miziki ya kitanzania ikiwa imefunikwa na bolingo type ya kina mzee Boziboziana and the like huku tukibishana maana ya nyama ya bata.Shhhhhhh!!!wasikusikie ubishi ulikuwaje tazafali.

  Nzawisaa,e mama nzawisa..
  Watoto wabata wote paka kawalaa,kawala na mikia,kashushia na soda, eeeh,na wale wasukuma wasio kunywa soda eeeehh alisukuma ndagala asalamaleikhumu andagalaa,Nzawisa ,e mama nzawisa,mtoto akinya mnawishe,akija juu mrukie…..

  Matty malizia basi au umenyanyuka kuanza kulisakata bolingo??

 7. ma'reen Says:

  Much respect 2u BC, unajua kukonga nyoyo za watu. Matty week-end poa ndo tushaianza na mialiko ya futari ishaanza kumiminika hahaha mimi inabidi nipige work ya nguvu coz kila jioni tunaalikwa mahanjumati ya futari,very tempting misosi unasahau diet basi tu ilimradi burudani! Mungu ametubariki sana watanzania and we have to be very thankful for this…udugu na urafiki regardless imani na kabila la mtu…Mungu ibariki Tanzania, nawatakia waislam wote mfungo mwema!

 8. Matty Says:

  ohhhh jamani kakangu mpendwa Majita nilikusahau unajua mimi bwana ikifikaga ijumaa huwa najiuliza kabla ya kuingia BC kuna songi gani? sasa nikilipata tu naanza kulicheza mwenyewe aluuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu burudani ya nguvu mno.
  WKND NJEMA MAJITA & OTHERS!!!
  hapo sasa nzawisa we mamamaaaaaaa nzawisaaaaaaaaaaa au ile pepekale na mwana shikaaaaaaaaa ma …. ya …mwana…he jamani BC nibabkubwa inshaalah mbarikiwe!

  ALL THE BEST JAMANI!

 9. rahma Says:

  mmmh! majita is so fan,umenifanya nimalize siku yangu kwa kucheka leo thanx.

 10. EDWIN NDAKI Says:

  Majita..

  aaa aaahaaa lol..

  nasikia motoo motooooo..

  umenikumbusha mbalia sana wa mai MAJITA.mambo ya nzawisa..nakumbuka sana mambo ya nyama ya bata..

 11. EDWIN NDAKI Says:

  Majita..

  aaa aaahaaa lol..

  nasikia motoo motooooo..

  umenikumbusha mbalia sana wa mai MAJITA.mambo ya nzawisa..nakumbuka sana mambo ya nyama ya bata..

  Matty nashukuru nakutakia mwisho mwema wa juma..
  kila la kheri wapenzi wote wa BC..

  MAMBO BADO..Tutafika tu

 12. Muh LUKAMBA Says:

  Matty asante sana kwa salam za wiki end,
  Ma`reen,majita,ndaki,rahma na mkandarasi saluti kubwa makamanda wangu,bila kusahau wadau wengine wengi Big Up masela !!Mzanzibar 100% naona swaumu imekamta mkondo wake,Kimyaaaa,mungu akupe nguvu mwenetu

 13. EDWARD ALEX MKWELELE Says:

  Unanikumbusha zama za mbali sana wakati huo nilikuwa mwanafunzi, MZUMBE PRIMARY, BAADAYE TENA MZUMBE SECONDARY, TENA MAZENGO HIGH SCHOOL, niliishi Mzumbe na bro wangu, RICHARD ALEX- BARRY WHITE, GOAL GATE, KADO, bahati nzuri nilifanikiwa kuziona bendi zote za Tanzania ambazo mara nyingi zilialikwa na MISO = MZUMBE INSTTITUTE STUDENT ORGANISATION hii ni miaka ya 1976 to 1982, wakati huo chuo kilikuwa kinafadhiliwa na Scandinavian Countries walimu wote walikuwa wazungu tupu toka USA, CANADA na SCANDINAVIAN countries, nawakumbuka rafiki zangu wengi sana wa wakati ule akiwa pamoja na MEJA KAHEMA JUNI MZIRAY WA JKT. bendi zote za Tanzania mzijuwazo zilifika MZUMBE/IDM kwa mwaliko wa wanafunzi na akina sisi tukizamia tu.

  THANKS,
  EDWARD ALEX MKWELELE

 14. Matty nashukuru kwa salamu.. ingawa nimezipata muda huu na ilihali wikiendi ishakwisha. Kama alivyosema BC, kiangazi limefika ukingoni, jotoridi linashuka kwa kasi isiyofariji, kipupwe kinakuja. For me that means it’s back to class this week and back to tutoring the kids (undergrads)!!

  Majita umenifurahisha na rap yako ya Nzawisa… mi nilikuwa naimba: Mayai ya kuku bata kayala, kayala na ugali, kashushia kwa soda…

  PS: Aisee wimbo wa wiki hii uliniacha hoi sana; umenikumbusha enzi zangu tunasikiliza santuri na kanda za mzee na kucheza!! Good times, good times

  Wiki njema kwa wote!!

 15. by the way Edo, Obama anaweza kawa kalamba joka halafu mtu wa kushoto kwake kalia kadi na hakuna mwenye namba 8 ageuze mchezo. Sasa hapo inakuaje?

 16. Dunda Galden Says:

  HOME SICK IN THE RAMADANI JAPO TUKO MBALI NA NYUMBANI LAKINI KWA BONGOCELEBRITY (BINTI MZURI) INATUWAWEZESHA TUWE KARIBU JAPO HAPA FTUTARIII ZA KAMA BONGO NYUMBANI NIMEZIMISS
  KINOMA.NAWATAKIA MWEZI MTUKUFU MWEMA NDANI YA WIKI END….NA WALE SI WAFUNGAJI MUWE NA SUBIRA MPAKA SIKUKUU YA WAKINA NDAKI.MATTY WIKI NJEMA

 17. Mh Lukamba Says:

  MKWELLE mbona unajieleza sana bwana,we MKWELE( Jamii ya wazaramo) kweli nini???Maana nyie swali moja majibu mia,Ulifaulu kweli mitihani yako wewe???
  Uliishi na nani ?? siyo sehemu yake,ulikuwa na akina nani siyo sehemu yake,Waalimu walikuwa wazungu ndo nini hiyo??? chuo kufadhiliwa inatuhusu nini humu ndani???
  Si tumefundishwa na walimu wa UPE,una maana atukuziona hizi bendi za zamani???

 18. Pearl Says:

  matty shosti asante kwa salaamu za week end japo nimechelewa kuzipata.
  BC big up sana wimbo huu ulibamba sana those days,yaani ukipita mitaani vitoto vinacheza rede huku vinaimba “mambo bado mambo bado magoma motomoto yanaingia”
  wana bc mi nawatakia mwanzo mwema wa wiki.

 19. hi ni rekodi ya kwanza y’afrika mashariki na kati ambayo imetolewa na kampuni ya kimataifa “virgin records” ya uingereza,shukran assosa na kundi nzima la makassy,vijana fwateni nyayo za wazee wenu, ahsante bc.

 20. matty Says:

  haya jamani mliochelewa kuzipokea salamu za wknd haina kwere ilimradi ujumbe umefika!

 21. binti-mzuri Says:

  mh lukamba we nawe mheshimiwa wa bunju au wa wapi…mbona maneno mengi ivo..pointi za kuhesabu. embu mwache mkwelele wa watu

 22. binti-mzuri Says:

  hehehe dunda galden..mbona umenichekesha aisee… sasa mie ndo bongo celebrity au?maana naona niko kwenye mabano… njoo mida mida (ileeeee) tufuturu.

  matty njaa zilitubanaa,ndo mana tukawa hatuonekani

 23. Mwalimu Zawadi Says:

  BC kweli mambo badooooooooooooooooooooooooo kabisa hata ifike lini mambo bado, unajua hii ni theory bomba sana mambo bado!

 24. matty Says:

  halo halo kidole juuu (waosha vinywa hayawahusu) Binti-Mzuri ehhh njaa ??? swaumu??? bora mimi sifungagi maana siyawezi!
  Tutafika tu!

 25. none none Says:

  BC owner you are a Hypocrite, you talking like you not one of them!

 26. binti-mzuri Says:

  none none unataka kushushuliwa wewe

 27. binti-mzuri Says:

  matty we kobe tu mwanawane..hahaha…. mambo bado

 28. Mswahilina Says:

  Ninapendaga sana nyimbo za Makassy, asante sana BC

 29. matty Says:

  no Binti-mzuri shosti mimi si kobe bwana najua hata nikifunga nitakuwa nacheat.

 30. Mh Lukamba Says:

  Bint mzuri mi nacheka tu,mi mh wa bunju !!! nitake radhi !!!

 31. Binti-mzuri Says:

  Haha mh lukamba niwie radhi,my kaka..hizi zingne dhambi za kujitakia,ila nimecheka..kumbe wa bunju.

 32. Dunda Galden Says:

  BINT_MZURI
  FUTARII YENYEWE UANIKARIBISHA KIUCHOYO
  HALI UNAJUA UKU HAKUNA FUTARII ADIMU ZA KAMA
  KULE KUNANI…MATTY KWELI WEWE KOBE?

 33. matty Says:

  no pls Dunda Galden mimi ni mkristo safi kabisa kama MCHUNGAJI MTIKILA nadhani umenipata aiseee msalimie mama Ramla, cHA FOSA CHAIGODDDDDDDDDDDDDDDAAAA hapo sasa hata maana yake siijui!!!!!!!! tutafika tu!

 34. binti-mzuri Says:

  hahahah umenichekesha matty, mtikila tena

 35. Matty Says:

  Ndio Binti-mzuri mtikila huyu huyu mr.politician.

 36. Hombiz Says:

  Dude-limetulia!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s