BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUKIWEZESHWA TUNAWEZA: SURVIVAL SISTERS September, 7, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 8:20 PM

Jina lao la kisanii ni Survival Sisters. Hapo mwanzoni “walipotoka” walijiita Choka Mbaya Sisters kabla hawajaamua kubadili jina hilo.Majina yao kamili ni Irene Malekela,Lucy Samsoni na Latifah Abdallah.

Mpaka hivi sasa wameshatoa albamu mbili.Ya kwanza waliita “Yatima” na ya pili ambayo wameifyatua hivi karibuni wameiita “Tukiwezeshwa Tunaweza” ukiwa ni ujumbe muafaka kabisa kwa wanajamii kuhusiana na suala zima la watu wenye ulemavu.Jipatie kopi yako halisi tafadhali ili kuwaunga mkono na kwa maana hiyo kuzidi kuwawezesha.

Mojawapo ya nyimbo zao ambazo zinatamba ni ule uitwao Siyo Siri ambayo wamemshirikisha msanii mwingine maarufu,Dully Sykes.BC inawapongeza kwa kazi nzuri na kuwatakia kila la kheri katika kazi zao.You rock sisters!

Photo/Abdallah Mrisho

Advertisements
 

21 Responses to “TUKIWEZESHWA TUNAWEZA: SURVIVAL SISTERS”

 1. piusmickys Says:

  Huu ni mfano wa kuigwa ni bora kumuwezesha mtu kwa kumpa “Pembejeo” kuliko kumpa “Kibaba cha Unga”… duh maneno nimeyasikia siku nyingi sana hehehee!
  Hongereni kina dada kwani wao wameweza wananini na hata nyinyi mshindwe mnanini!!

 2. EDWIN NDAKI Says:

  BC ni habari njema kutuletea mtundiko mtamu kama huu kuanza nao juma hili.

  Binafsi nawapongeza pia hao wakidada..ila ingekuwa vema kuna kini moja walitoa na Juma Nature na mengineyo ungeweka japo wimbo chini yao kama unavyofanya kwa wasanii wengine hapo ungewa “UMEWAWEZESHA WATU KUTAFUTA KAZI ZAO” ila Mungu atujalie uzima natumaini utatuletea tu punde ukiipata au kuizipata kazi zao.

  Nawatakia wadau woooooooooooooote mwanzo mtamu kabisa wa juma…Kekuu natumaini ulifaidi Marashi ya pemba..

  Matty inakuwaje..mgeni ulimfungua kamba au bado anayo?

  Gervas jiandae jioni nakupitia twende kamnyonge kuna game la basketball mwembeni na Songe.

  Majita nasikia umeelekea Mgango..utarudi lini..

  Mama wa kichaga na wengine woote siku njema.

  DEBRA..HAPPY BIRTHDAY natumaini leo ni siku yako ya kuzaliwa..

 3. Dunda Galden Says:

  Safi kwa hatua mlio fikika wakina dada endelezeni kipaji chenu

 4. salama Says:

  Jamani hawa wadada wanaimba vizuri eti….sio siri.Nawakumbuka tulikuwa nao O’level pale Jangwani.Wabongo tujitahidi basi kununua kazi zao ili tuweze kuwatia moyo hawa wenzetu ili waweze kufanya vizuri zaidi.
  Salama…

 5. Mh Lukamba Says:

  Ebwana Big MASTER !!! Long Time kipindi kile cha choka mbaya !!!! Dah,nimefurahi kuwaona tena,kazeni buti,lazima mtoke tu,Ebwaneeeee,kweli mmetoka mbali !!!
  Fresh yaani kuamasisha wengine wenye upungufu kidogo mwilini,Yaani BIG UP !!!

 6. binti-mzuri Says:

  Mungu awazidishie Rehema… ukiwa kwenye condition kama hiyo ya disability,and yet you have a will to carry on.. thats like the greatest gift of all. Nothing can stop you people..you are able in every way

 7. Pearl Says:

  go girls you deserve to be on top
  all the best.

 8. mama d Says:

  du hawa wadada nawafagilia sana.kilema sio mwisho wa maisha.angalia wanavyojituma mambo yao yanakuwa mazuri hawamtegemei mtu.jamani wawape moyo na hawa vilema wengine wajitume wasiombeombe barabarani.waige mfano jamani.mungu hakunyimi kama unania ya kufanya jambo.nawatakia maisha mema dada zangu mungu awape moyo muwe ma superstar

 9. way to go sisters!! Like some like to say, you are HANDICAP-ABLE and not HANDICAPPED. Work hard and I wish you all the best!!

 10. matty Says:

  mhhh Edwin Ndaki usiseme kabisa mgeni si alipotea hahahahahaha!
  Kuhusu hawa wadada wanaimba vizuri sana na wanavipaji kwa kweli, Mungu awabariki na wakiwezeshwa ni kweli wamesimama.

 11. nifraz Says:

  good luck girls…

 12. kahindi Says:

  kama sikosei wanaishi sinza madukani…huwa nawaona mara kwa mara mitaa hiyo,na wanajua kujipamba na wanapiga pamba kwa saaaaana….big up wadada,kazi yenu naikubali sana….

 13. kokoliko Says:

  nawapa tano!
  kokoliko-koooooo!

 14. shubi Says:

  yaani mimi huwa nikikosa kuona comment ya mettey na amani naikosa,,kwani huwa nacheka sana ,,,mgeni kapoteaje??au unatuzuga?

 15. furaha Says:

  jamani ninawaonea raha sana dad zangu,mnatupa na sisi moyo wa kuwaiga mungu awazidishie zaidi

 16. matty Says:

  Shubi shosti mgeni alipotea kweli kabisa….halafu Shubi huo sasa utani,nway tuache utani shosti wewe ni shubi yupi lakini??

 17. sisterTZ Says:

  hongereni sana akina dada SURVIVAL SISTERS kujituma ni vema kuliko kukaa nyumbani na kusubiri wafadhili wawape pesa..

  ila nawashauri tafuteni promota muende angalau nje kuonyesha kazi yenu..mdau mmoja hapa kwenye BC alisema nendeni kwenye google na msearch hamuwezi jua bahati yenu ipo wapi ila jiepusheni na mapromota matapeli… otherwise God bless you all… na kumbukeni HARD WORK ALWAYS PAYS:::

 18. debra Says:

  Ahhh kweli hujafa hujaumbika!
  Mungu hakunyimi yote kabisa,kila heri wadada…
  N anyota yenu izidi kung’aa..
  Si inshu Mtafika tuuu,PamoJAH.
  Edo Ndaki senkyuuu sana!!

 19. Bob Sambeke Says:

  E bwana Big up Sisters Me Nawakubali Sana mmetulia sana tangu mpo kwenye kibao mlichompa shavu Nature kinachoitwa mashabiki c mchezo Halafu Ni Wazuri sana ukiwacheki Live! Mbona mpo Wa3 wkati mlikuwa wa4? M1 Yupo wapi? Au ndo mwaka wa shetani?

  Bob sambeke,Jr
  Moshi

 20. Hii ni safi. Inafurahisha kutambua kuwa unaweza kufanikiwa kwa kiasi ulichowezeshwa katika hali yoyote uliyopo. Nakumbuka Reginald Mengi alienda Japana akarejea akieleza juu ya milionea ambaye amepooza sehemu zote za mwili kasoro kichwa tu. Na anaongoza kampuni kwa hicho alichobaki nacho. Naliona kundi la Israel Vibration ambao wanafanya vema katika Reggae lakini linaundwa na kaka waliokutana wakati wakihudhuria kliniki ya Polio. Kwa hiyo maisha yanaweza kuwa na mafanikio kama tutatumia kile tulichonacho kwa ufasaha. Namkumbuka Philip Lucky Dube (RIP) alipoimba katika kibao Celebrate Life ndani ya albamu yake ya mwisho ya RESPECT akisema “this is a give or take world, so you gotta take what you can when you can make the best of it”
  Ndivyo mlivyofanya kinadada na nawapa HESHIMA kwa hilo na NAWATAKIA MAFANIKIO MEMA.

  http://www.changamotoyetu.blogspot.com

 21. binti-mzuri Says:

  mzee wa changamoto i love your comment..


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s