BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MASHAKA ANA KWA ANA NA AFANDE KOVA September, 8, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 9:31 PM

Kama wewe ni msomaji mzuri wa BC,bila shaka jina John Mashaka halijakutoka kichwani.Tulipofanya naye mahojiano mwezi April mwaka huu,mahojiano yale yaliingia kwenye lile kundi la mahojiano ambayo yalizusha mjadala mikali zaidi na hivyo kupata maoni tofauti tofauti chungu mbovu.Wengi walimuunga mkono.Wengi walimpinga na kumkatisha tamaa kwa kila namna walivyoweza.Wengine walibaki katikati wakisubiri afanye kitu ili wajue jinsi ya kumuunga mkono au vinginevyo.Kama hukupata bahati au nafasi ya kuyasoma mahojiano yetu na John Mashaka,unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa.

Kwa bahati nzuri au mbaya,yaelekea John ni mtu anayejua anapotaka kufika,anachojaribu kukifanya na haelekei kuyumba katika nia yake.

Hivi majuzi,John Mashaka(yupo Bongo hivi sasa) aliandaa kongamano lililoitwa Tuwajali Wenzetu.Kongamano hilo lilifanyikia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar-es-salaam.Je kongamano hilo lilihusu nini?Mashaka aliongea nini?Ni yepi yalijiri katika tamasha hilo?Kupata undani wa kongamano hilo na picha kadhaa mtembelee Ahmad Michuzi JR kwa kubonyeza hapa. Habari njema ni kwamba,kama inavyoonekana pichani,Kamanda wa Polisi wa Dar-es-salaam,Afande Suleiman Kova amekubali kuunga mkono jitihada za John Mashaka.

Advertisements
 

24 Responses to “MASHAKA ANA KWA ANA NA AFANDE KOVA”

 1. Wakuvanga Says:

  Mimi kwa upande wangu nasubiri majibu ya huyo kaka siwezi kumuhunga mkono make wapo wengi wa namna hiyo(dealer man) kila la heri na mungu akutangulie make kuna road block nyingi

 2. MAMA QUEEN Says:

  keep it up son!God will bless u always.

 3. Hongera ! B.C kwa hii blog yenu inayozidi kuwakilisha sana katika lugha la kiswahili.Nawatakia Kila la heri kwa uandishi wenu bora!

 4. binti-mzuri Says:

  hehe nimesoma mpaka nikasinziaa…kweli ulizua mjadala

 5. Mama wa Kichagga Says:

  Ni mfano mzuri wa kuigwa.

  Wakiwepo watu 5000 kama Mashaka hakika watawagusa wengi kwani naamini hapo Mashaka kagusa sii chini ya watu 1000 na watoto 500.

  Mola akutie ujasiri na moyo wa kujitolea utimize malengo yako bila kukatishwa tamaa.

 6. matty Says:

  heee hii mupya!! God bless u!

 7. Mwenye Wivu Nijinyonge? Says:

  1. “ngoma ikilia sana ……..”

  2. Mashaka, uzoefu unanielekeza nione kuwa hii misaada inatolewa sanjari na ndoano fulani ya kutafuta umaarufu.

  3. kama nimekuhukumu vibaya nisamehe sana na hata hivyo naendelea kukushauri kuwa huna haja ya kuwa kwenye ‘masi- midia’ kila nukta unapotoa msaada. Vyombo vinavyokunyanyua huwa ndivyo baadaye vinavyokumaliza!

 8. pandu Says:

  Kipindi kile John alikuwa anaonekana mwenye busara, msomi aliyobea na kuelimika . Mbona hapa jamaa anaonekana kama Bongoflava flani ivi?? Mcheck kweny michuzijr…bluetooth huku anasoma hotuba kwenye laptop…kwani angeiweka hotuba yake kwenye karatasi ingekuwa vp?? au ndo mambo ya mbele? sunglasess ili mradi manjonjo flani…aya John kama unatafuta ubunge sema tukupeleke kunako siyo ulete mbwembwe kama Mwakyembe.

 9. kokoliko Says:

  Uchunguzi wangu wa haraka haraka unaonyesha kuwa huyu Mashaka ana lake jambo. Ukweli utafichuka muda si mrefu. Yangu macho.
  Kokoliko-kooooooooooo!

 10. mdada Says:

  Am not sure if the guy is just helping may be he wants something else.

 11. Zafanana Says:

  Huyu bwana, ni sawa sawa na westerns who are using African problems to make a living for themselves not for Africans he has just set up “The John Mashaka Charitable Foundation” you can Google to get his website, Fanya wema nenda zako, kuna wabongo wanafanya mazuri and never even seen. Picha, na video is to be used for fundraising purpose, Mashaka just be Mashaka, Kijijini kwanu wanahitaji maji, to mention few..

  Ok mewapa Unga bulanketi, vikiisha je? …. AFRICA DOES NOT NEED AID, WE NEED TRADES TECH THEM HOW TO FISH…. Amen

 12. matty Says:

  Haya semeni nyie leo nikisema mimi ohhhh, ehhh ahhhh, ukweli ndo huo msaada mpaka uite mediaaaaaaaaaaaaaa??????????????wapo wengi wanatoa without those mass media kama hamjui!

 13. Muga Raymond Says:

  It is written in a Bible that “repant and be slow to judge” i guess what am tryin to say is, p’ple must stop condemnation toward this dude, b’coz what Mr Mashaka is doin in his society is something that any tanzanian who’s capable of helpin the needs should do so, and its tym people should stop thinkin negatively, instead we’ve got to support en encourage p’ple like mashaka to continue helping the needs. Also i would like to advise Mr: Mashaka to like share his tacit knowledge by teaching people what to do to overcome problems such as poverty etc, this will uplift p’ple’s capabilies of creating wealth, i mean the concept is to build an independent nation.
  GOD BLESS YOU MR MASHAKA, DON NOT LET PEOPLE STOP YOU FROM WHAT YOUR DOING, B’COZ WHAT YOUR DOIN IS WHAT THE LORD SENT YOU DO ON EARTH.

 14. Stive C Says:

  I TRUST MR MASHAKA SHALL JUST HAVE A CHOICE IN WHICH WAYS HE SHOULD WANT SHOW OFF AND SOME PEOPLE LIKE TO SUPPORT SMALL AND MAKE ENTERTAINMENT LIKE WHAT HE DOES AND SOME PEOPLE LIKE BAHRESA GOES TO GIVE FUTARI, PAY BILLS ZA WAGONJWA AT THE HOSPITAL WITHOUT CALLING THE MEDIA AND GUYS DONT BLAIM MASHAKA BECAUSE SHOW S OFF IS HIS TRIBE NATURE WHICH WE CANT CHANGE IT WE SHALL JUST RECEIVE HIS AID AND REMAIN QUET JUST FRIENDS WHO NEED TO JOIN HIM SHOULD BE AWARE OF WHATS HE S DOING BECAUSE ONCE HE MESS UP TOCHI YA EPA ITAMULIKA THEN PEOPLE WITH THEIR PROFESSIONAL WILL LIKE WHAT EPA COMMUNITY LOOK RIGHT NOW, BECAUSE WITH EPA GUYS IS A GOOD LESSON WE COULD IMAGINE WALOKOLE NAO WALIJIKUTA NDANI YA GUNIA LA EPPA,
  Stive C

 15. Mama wa Kichagga Says:

  Muga you are right & I support U 100%.

  We need people who care about others! and who fear God in their doings knowing that in this globe we are on transit!

 16. BALTAZAR Says:

  FAMOUS MASHAKA JOHN.

  NDUGU ZANGU WATANZANIA TANGU KIJANA HUYU AINGIE KATIKA BLOG NA WEB SITE MBALIMBALI NILITENGEMEA WATANZANIA WENZANGU WANGEJITAHIDI SANA KUMPA KIJANA HUYU MAWAZO KWENYE MAZURI NA MAPUNGUFU YAKE ALIYONAYO KAMA MWANADAMU WA KAWAIDA NIMEONA KIJANA HUYU AMEJITAHIDI SANA KATIKA KUJITOLEA KUSIMAMA KWENYE MAJUKWAA KUZUNGUMZA MENGI ALIYOTAKA KUZUNGUMZA KUNA MAPUNGUFU AMBAYO KILA MTANZANIA ANAONA KATIKA KONA MBALIMBALI KILICHOTAKIWA HAPA NI KUTOA MAWAZO TOFAUTI YENYE MSINGI WA KUKOSOA KWA KUTUMIA LUGHA ZA KISTARABU KABISA ZITAKAZOMSAIDIA.

  KWA UZOEFU WANGU NAELEWA UNAPOKUWA KIONGOZI HUWEZI KUELEWA KAMA WANANCHI WAKO WANAKUFATA AU WANAKUMBIZA. NILIVYOMULEWA MASHAKA ALICHOTAKIWA

  (1) NI FANYA STUDY ZA KUTOSHA KABLA YA KUPANDA JUKWAANI KWAMBA WATANZANIA WANAHITAJI NINI,

  (2) KUWA MUWAZI ZAIDI KWA WATANZANIA KUJINADI KWA SERA ZA UKWELI NA UWAZI ILI JAMII IELEWE KWAMBA UNATOA MISAADA INATOKA WAPI NA NI KWA NIA GANI

  (3) KAMA KIONGOZI NAKWENDA KUNADI SERA ZANGU OUTLOOK YANGU IWEJE KWA WATANZANIA.

  (4) KUJUA WATANZANIA WENGI TUNA LEVEL GANI YA ELIMU NA UPEO WA KUELEWA NA KUCHANGANUA MAMBO

  KWA WATANZANIA WANAOPENDA KUMJUA MASHAKA NA KUJUA NI NINI ANACHOFANYA MASHAKA WAKO NA FOUNDATION INAYOITWA JOHN MASHAKA FOUNDATION WAKO BOEARD DIRESTORS WAFUATAO, MASHAKA ,LA TASHA,MARTIN LATONYA NA MARIA FOUNDATION HIYO IKO SUPPORTED NA JAMES, CATHERINE ARNY NA ESTER WOTE WAKO WACHOVIA BANK NDICHO KINACHOPELEKEA YEYE KUPATA WATU WANYE MOYO KUJITOLEA NA KUDONATE WANACHOJISIKIA.

  USHAURI WANGU BINAFSI KWA MASHAKA USISIKILIZE SANA MANENO YA WATU NA KUWA MUWAZI ILI WATU WAKUELEWE MANAKE WATANZANIA HAWAELEWI MARA WENGINE WASEME UNATAKA KUWA RAIS MARA UBUNGE MARA UMAARUFU LAITI UNGEWAPA UKWELI HUU WANGEKUWA NA MAWAZO.
  PILI PUNGUZA KIDOGO SHOW OFF KUWA NA MAADILI YA UONGOZI USIWE NA ATITUDE YA KISANII NA KUJISHOW KWA KWA SISTER DU WATAKUCHANGANYA SANA HASWA HAPA JIJINI
  TATU JINADI KAMA ORGANIZATION NA SIO KAMA MASHAKA JOHN KAMA NINGEKUWA NA UWEZO WA USHAURI NISINGESEMA UJIITE JOHN MASHAKA FOUNDATION KWA SABABU UNAPOKUWA NA ORGANIZATION NI JUMUIYA ONDOA MUONEKANO WA BINAFSI KUNA MAJINA MAZURI TU KAMA LIGHT OF AFRICA, FUTURE OF AFRICA, KOMBOA AFRICA, ETC.

  USHAURI KWA WATANZANIA MSIWE NA JELOUS NA LUGHA MBAYA KAMA KUNA MTU AMBAYE ANGETAKIWA KUTOA LUGHA MBAYA KWA MASHAKA MIMI NINGEKUWA WA KWANZA KABISA KWANI APRIL 2,2008 FIANCEE WANGU BILA KUSHAURIANA NA MIMI ALITOA AHADI LIVE BONGO CELEBRITYKWAMBA ALIFANYA MEETING NAE MWAKA 2007 ATAMSAIDIA IN SETTING UP NGO NA LIVE ALIAHIDI KUMTUMIA MAIL PERSONALLY KUHUSIANA NA MAMBO HAYO.
  KWA HIVYO WATANZANIA TUMUUNGE MKONO KIJANA WETU

  UKITAKA KUPATA HABARI KAMILI KWA FOUNDATION YAKE BOFYAwww.johnmashakafoundation.org

  BALTAZAR
  http://WWW.KIPEPEOTOURS.COM

 17. binti-mzuri Says:

  we baltazar nawe umenichekesha paragraph yako ya mwisho… sasa ungemkasirikia your fiance kisa kaanzisha NGO na anasaidia watu!?

 18. BALTAZAR Says:

  Binti mzuri nimefuhi jamani kukuchekesha hapana bibie mimi sikumkasirikia kimwana wangu kwa kuanzisha NGO ya kusaidia watu na wala hajaanzisha NGO yeyote nilikuwa tu najaribu kuwasazisha watanzania wenzangu na kupiga mioyo yao pasi juu ya suala zima la kijana.

  Mimi kwa kweli sina pingamizi kabisaaaa na suala la kusaidia watu kwani binti mzuri ukitembelea web site yangu http://www.kipepeotours.com alafau uende kwenye volunteering program utakuta tunatoa misaada pia bila kujitangaza sana.

  Siku njema binti mzuri

 19. binti-mzuri Says:

  okay baltazar,ubarikiwe

 20. Jamal Says:

  Mh…nawasiwasi.

  Mi nipo honest, huyu jamaa anatafuta something.

  kwanini anambwembwe hivyo afu full kuwahusisha mapaparazi….kuna kitu. Nyie mtaniambia siku moja.

  walianza hivihivi kina…..sa hivi wengine wanataka ubunge, wengine wamefanya dili la kupatia fedha…. kwani hamjaona wale wenye vituo vya kulelea watoto hewa?

 21. Amina Says:

  mi huyu ndo nilimshtukia siku nyingi

 22. Chachandu Says:

  Hiyo speech lakini kali, kumbe ndo maana, wakina Jovinata hawataki kucheza mbali. Hata mimi ningekuwa msichana ningejaribu bahati yangu. Harufu ya pesa hipo !

 23. JamviKavuTabora Says:

  Bwana Mashaka,
  Duniani tunawahitaji wakina mashaka 400 tu!
  Umenigusa mno, kazi yako nzuri na Mungu akuzidishie maradufu. Makala ya Juzi ya Habari Leo Imetosha

  Sh. Millioni 8.2 siyo mchezo mimi sijawahi kuikamata maisha yangu yote kwa hiyo kazi yako ni kazi ya kipekee, na ni kipaji toka kwa mola

  Usikate tamaa, kwani watu wa aina yako ni wachache sana duniani. Usiwasikie hawa wachovu waosha vinywa wenye wivu. Wamechoka na maisha, wameshindwa kurudi makwao, wameshindwa hata kujenga banda la kuku makwao, kwa hiyo umewashinda ndio maana kila wakikuona wanakuwa matumbo moto na kupagawa kama vichaa.

  Dunia inakuhitaji, vuta subira, vumilia uwafikishe wafuasi wako kanani. Safi sana Bongo Celebrity

 24. xxx Says:

  zafanana i agree wit u..mnatupa goods zikiisha turudi tena kuomba na kungoja misaada…tufundisheni jinsi ya kujitaftia wenyewe bwana!mr mashaka anatafuta umaarufu tu sampuli hizi mbona nyingi sana na tunazijua!tumeshakushtukia wewe mr mashaka ni wale wale mafisadi tu!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s