BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“WASANII WAJIELIMISHE,WAPENDANE NA WASIDANGANYANE”-KBC September, 14, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Single/Mpya,Tanzania/Zanzibar,Watangazaji — bongocelebrity @ 7:47 PM

Kabla ya makundi ya muziki kama vile Wanaume TMK,Das Nundaz,Nako2Nako,East Coast na mengineyo kuibuka au hata kutambulika kwenye anga za muziki nchini Tanzania yalikuwepo makundi ambayo hivi leo wengi tunakubaliana kwamba hao ndio waanzilishi wa kinachoonekana hivi leo kuwa kama vuguvugu la vijana katika kupigania haki yao ya msingi ya kujielezea(freedom of expression) katika jamii kupitia sanaa ya muziki.

Miongoni mwa makundi hayo ni lile lililotamba sana na kujulikana kama Kwanza Unit.Miongoni mwa wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo ni KBC au KSingo(pichani) kama alivyojulikana wakati ule na hata hivi sasa.Mbali na Kwanza Unit,wengi bado mtakuwa mnamkumbuka kama mpigania haki za Wana Hip Hop na pia miongoni mwa wanamuziki waliojitolea sana katika kuhakikisha kwamba Hip Hop ya Tanzania inaeleweka na kukubalika.Pia wengine mtamkumbuka kama DJ pale Clouds FM katika Dr.Beat.

Tukiwa bado katika kuhakikisha kwamba historia ya vuguvugu hilo na kwa ujumla historia nzima ya muziki tunaouita “wa kizazi kipya” hivi leo,haipotei na inawekwa vyema mtandaoni,hivi karibuni tulifanya mahojiano na KBC kama utakavyoyasoma hivi punde.

Je unakumbuka Kwanza Unit ilianzishwa mwaka gani?Nini yalikuwa malengo ya mwanzoni?Leo hii KBC akiangalia nyuma anaona tofauti gani au maendeleo ya aina gani katika muziki wa kizazi kipya?Nini ushauri wake kuhusu masuala ya haki miliki na utawala wa biashara ya muziki?Kwa maoni yake,nani anachangia kudidimiza muziki?Ni producer au Radio DJ?

Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo ambayo pia yana Swanglish ya aina yake katika kuleta au kuchanganya ladha kiaina;

Kwanza Unit:Then and now!

BC: Shukrani na karibu sana ndani ya BC.Mambo vipi?


KBC:What up Jeff!! It’s OBAMA 08 and I like this BC atmosphere,..Tunaendelea Kupambana..That Hasheem Thabeet interview was GREAT!!

BC: Kwanza kabisa nadhani wapenzi wengi wa fani ya muziki nchini Tanzania na duniani kote  wangependa kufahamu;uko wapi na unajishughulisha na nini hivi sasa?Bado unafanya shughuli za muziki?Kama hapana,imekuwaje ukaachana na muziki?

KBC:Well at the moment im “PassPort Pimpin”..In and Out of Bongo..Si Unajua tena siku hizi dunia kijiji cha ujamaa??I’m Graphic Designer by Profession..Mfanya Biashara and a B.BOY GENTLEMAN..In Bongo im a Hip Hop Veteran..Sitoweza kuacha music..I still write alot.

BC: Kumekuwepo na mijadala mbalimbali kuhusiana na historia nzima ya kundi la Kwanza Unit. Ndani ya mijadala hiyo kumekuwepo na kutofautiana kuhusu historia nzima ya kundi hilo.Unaweza leo kutuambia kwa mlipoanzisha kundi la Kwanza Unit mlikuwa wangapi, kina nani na mlikuwa na malengo gani hasa?Mwamko wenu ulitokana na nini?


KBC: First and foremost let me start by giving Thanx to All the Kwanza Unit supporters All over the world,from the early days till now..

Kwa kweli tumeshuhudia mijadala mingi kuhusu historia ya Kwanza Unit lakini tatizo watu wengi huitazama Kwanza Unit kama kundi la muziki tuu..while Kwanza UniT is/was a MOVEMENT. That’s bigger than Music…bigger than the number of Emcees in it..

The Movement started in 1992.Malengo yalikuwa ni kwanza kutambulisha na kuelimisha jamii kuhusu utamaduni huu wa HipHop..Pili ni kutumia Hiphop kama chombo au kitendea kazi cha kuelimisha na kuangazia mazuri na mabaya yanayotokea katika jamii zetu za TZ..Long story short EDUTAINMENT..

BC: Ni changamoto gani(kiutendaji na kijamii) ambazo mlikumbana nazo kipindi mnaanza ku-rap?


KBC:Changamoto ilikuwa to follow the VISION that we had collectively..to Document whats happening Around our Jamii,..The Struggle,The Good times,the joys and Pains..so we became the Voice of the urban Bongo Youth.

Kwanza Unit 1994:Kutoka kushoto kwenda kulia Eazy -B, D-Rob (RIP), Rhymson(now Zavaara),Fresh-G and Y-Thang.

BC:Ni wazi kwamba muziki wa rap/hip hop nchini Tanzania umeshapitia vipindi kadhaa muhimu.Hapa nazungumzia tangu kuanzishwa kwake mpaka hapa ulipo hivi leo.Sasa ukilinganisha na “enzi zenu” na jinsi mziki ulivyo hivi leo nchini Tanzania,kuna tofauti gani za kimsingi ambazo unaziona?Ni tofauti nzuri au mbaya?Kwanini?


KBC:“Enzi Zetu” huh?..ha haa..we not that old Jeff! HipHop Culture inatambulika zaidi kwa watanzania siku hizi.Thanx to Programs like WAPI chini ya usimamizi wa ZAVARAA a.k.a CHIEF RHYMSOM,kwa kuelimisha vijana kuhusu Hiphop Culture and its elements.

Lakini Bongo HipHop music bado unapata vikwazo vingi siku hizi kutokana na mafanikio ya muziki wa BONGO FLAVA. Watanzania wengi Bado hawajui tofauti kati ya HipHop na Bongo Flava..hata wale Radio DJ ambao ni kiungo kati ya msanii na mashabiki wa Muziki wa TZ.

Siku hizi Everybody RAPs..Even RnB singers Rap nowadays..lakini ukweli ni Kwamba just cos you Rap.. it doesn’t make you HipHop artist.Ni kama wale watalii wazungu wanaweza kujifunza kuongea Kiswahili vizuri tuu..lakini hawawezi kuwa waswahili..vivyo Hivyo kuna wasanii wengi wa BongoFlava wanao Rap lakini sio Wana HipHop.

BC: Pia kumekuwepo na habari au taarifa tofauti tofauti kuhusu muanzilishi au waanzilishi wa muziki wa kufoka foka(rap) nchini Tanzania.Kwa unavyokumbuka au kuelewa wewe,nani unaweza kumuita mwanzilishi wa rap nchini Tanzania?Ilikuwaje?


KBC: No Disrespect Jeff,but the word KUFOKA FOKA is offensive to an artist as the ‘N’ word to a Black person..that word was invented by ignorant TZ journalist who did not know anything about Rap music,and even when they were informed about it they refused to call it what it is..RAP MUSIC..so they called it KuFOKA FOKA..

Now you see what we had to go thru “Enzi Zetu”..we had to fight for everything..Most press and media people at that time found it hard to be informed about this new artform by these Urban Bongo youngsters.Most of them wrote their own version of our story and that’s why you have too many contradicting stories.

BC: Kama ilivyo kwa mambo mengi katika jamii,muziki wa kizazi kipya ni eneo mojawapo ambalo linapingwa,kubezwa na kupewa shutuma mbalimbali.Miongoni mwa shutuma zinazoambatana na pingamizi kadhaa ni ile ya kwamba hivi leo vijana wengi wanafanya muziki sio kwa sababu wana vipaji bali ni katika minajili ya kuganga njaa tu.Unasemaje kuhusu shutuma kama hizo?Unadhani zina ukweli wowote?Kama ndio,hali hiyo unadhani ina mchango gani katika maendeleo ya muziki?


KBC: Muziki sio kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya,kwa kizazi kipya au Zilipendwa..The Problem is not doing it for the money or for the love..the issue is do these so called Wasanii know music??..

Ukweli ni kwamba hata kama una kipaji cha muziki ili watu wakusikie utahitaji kurecord professionally. Hapo itabidi ulipe studio fees,mashabiki wa muziki ni wengi itakubidi kujipromote..itabidi utengeneze copies of your demo..itakugharimu..Hata kama unataka kutoa muziki wako bure itakubidi utengeneze copy nyingi ili kila mtu akusikie nk

Sasa kwa wale wanaoweza muziki na wana uhakika na vipaji vyao kutokana na demand ya mashabiki wa muziki,wameingia kwenye “Biashara ya Muziki”..watu wengi wanaotoa shutuma Hizo inabidi wafanye mahesabu ya gharama za kurecord+Kupromote. Studio owners dont care kama una kipaji or Not..All Money is good Money,its bizness,they have bills to pay too.If it was Free then we could critisize.Halafu kila mtu ana haki ya kujitafutia.Si ni bora
wafanye Muziki kuliko kwenda kukaba na kutumia madawa ya kulevya..au sio?

BC: Katika muendelezo huo huo wa shutuma na lawama,limekuwepo suala la producers kuonekana kama chanzo cha kuzorotesha ukuaji na umakini wa muziki wa kizazi kipya.Wanaosema hivyo wanasema kitendo cha producers kukubali kumuingiza mtu yeyote studio ili arekodi nyimbo bila kuzingatia kipaji alicho nacho mtu bali hela aliyonayo tu kinaua kabisa fani.Unasemaje kuhusu hilo?Unashauri nini kifanyike?


KBC:Tatizo sio Music Producers Jeff..kusema kurecord wasio na Talent ni kuua fani ni sawa na kusema Kufundisha wanafunzi wajinga ni kuua elimu..Tatizo ni Radio Dj’s wasiojua Muziki,wanaopokea pesa na kupromote yeyote yule mwenye pesa..sisi wana Hiphop tunaziita WACK SONGS.

Kwa mtindo huo huwapa nafasi wasio na vipaji kwenye chart za muziki..so every other kid thinks music is easy..so they go to the studio too..more money to the Producer-More money to Radio Dj’s..More money kwa Muhindi anayeuza kanda(cassettes) na kuwaibia wasanii..RADIOs KILLED GOOD MUSIC!!

Kwanza Unit.Hapa ilikuwa ndani ya Lang’ata(siku hizi FM Club) 1994


BC: Leo hii ukiangalia jinsi ambayo muziki unaoitwa wa kizazi kipya umepata umaarufu kiasi kwamba ndio umekuwa kimbilio la vijana wengi katika kutaka kujiajiri na mambo kama hayo unajisikiaje?

KBC: It really feels like Graduation day..Job Well Done..Juhudi zetu na malengo yetu yametimia,nguvu zetu hazikupotea bure..TZ artist can live off music now..Vijana wa kitanzania wanatumia sauti zao na uwezo wao wakisanii kujiajiri na kutangaza utamaduni na maisha ya jamii yetu ya Kitanzania..ProF Jay on tour Europe+USA..Juma Nature getting nominated for MTV awards…Lady JayDee performing at Nelson Mandela’s Birthday nk. Enzi zetu wengine walituita wahuni lakini hatukukata tama.Leo hii hata President Jakaya Kikwete ni mshabiki wa muziki huu wa kizazi kipya.1994 People were amazed of what KWANZA can do..today Im amazed of what FID Q can do..”it feels really really Good”..

BC: Ni wanamuziki gani nchini Tanzania hivi leo wanaokuvutia kutokana na kazi zao?Kwanini?

KBC:Unajua Muziki wa Vijana TZ umegawanyika,I have alot nitataja wachache..
HASHIM a.k.a Dogo,FID Q,JUMA NATURE,SALU T,Professor JAY,J-Mo,MChiZi Mox,CHIDI BENZ,NAKO2NAKO,BaBUU,KURASSA,LANGA,BOB-Q na BK,..aaaah Man! JeFF I got many..LADY JAYDEE,NURUWELL,DAZ NUNDAZ,MASHARIKANZ,Giz MABOVU,Mjomba NASH..i can feel up a room Jeff let me stop..ha haaa

BC: Je mna mpango wowote wa kujumuika siku moja kama Kwanza Unit na kufanya japo onyesho moja na pamoja?Mawasiliano yenu yakoje?


KBC: Yeess!!Mpango huo upo na ulikuwepo..Tulitarajia kujumuika pamoja mwaka huu kwa Kishindo Kikubwa ile siku ya 08/08/08..Lakini Mikataba ya Kibiashara ikaingiliana..lakini yote Heri..Tegeni Macho na Masikio 2009!!..its gonna be BIG!!

BC: Matatizo ya haki miliki na wasanii kuibiwa kazi zao yamekuwepo toka enzi na enzi.Unadhani kwanini inakuwa ngumu kuyapatia ufumbuzi?Unadhani hiyo ni vita isiyo na mwisho na ambayo mshindi hawezi kupatikana kamwe?

KBC: Haki Miliki itapatikana pale wasanii watakapo funguka macho kuhusu biashara ya Muziki..TZ music industy set up needs to be restructured.Tunahitaji Music Business ya kweli.Msanii anahitaji kuwa na lawyer,Msanii anahitaji Kuwa na Contracts na Recording Labels..sio radio DJ’s.

Haki za msanii na makubaliano ya kibiashara yawe wazi kwenye Contract wakiwakilishwa na Lawyers wao.Kwa wale wasanii wakubwa wanaohitaji Meneja..inabidi wawaajiri..Msanii ni boss wa meneja wake sio vice Versa..

Record Label ndio zigharamie studio fees na promotion cost..we all know alot of money is generated in Entertainment industry,more Tax money for our serikali.Ingekuwa vizuri kama serikali ingesaidia kulinda haki miliki za wasanii hawa..Kwa kweli inabidi wanamuziki wa TZ waende na wakati..”2008 World SuperStars like Jay-Z,50 Cent,Shaggy,Akon,KC n JOJO,etc wanafanya shows Tanzania..na tunawalipa pesa nyingi tuu..Mamillioni!! kwanini hatuwezi kuwalipa wasanii wetu wenyewe??

BC: Mwisho ungependa kutoa ushauri gani kwa vijana ambao hivi leo wapo kwenye “game”?

KBC:Kuheshimiana,kushirikiana,kupeana support.Nimewahi kwenda show mbali mbali za wasanii wa siku hizi..ni vigumu kuwaona wasanii wenzao kuja ku support..kama kila msanii wa kizazi kipya atahudhuria show ya mwenzao basi wote watatengeneza chakula kizuri.

Nawashauri katika Fani yoyote ile..Bring your “A game”..work hard on it..give it 120%..wasitegemee misaada.Business is never personal.Wasanii wajielimishe,wasidanganyane na mafanikio ya hapa hapa nyumbani. Wajitayarishe kama kama wanariadha kabla ya Olympics.Wana jukumu la kuiwakilisha Tanzania kisanaa.Pia nawaomba wasanii wote wawashauri Wanaume Family(Ze Original) kurudiana…their shows were AMAZING!!Vile vile Kumshauri HASHIM “Dogo” kurudi kwenye Muziki..tunahitaji sauti yake..Hata Album moja tuu..He is the Best TZ HipHop artist thats never been heard by many.

BC: Asante kwa muda wako na tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.


KBC: Yo! Jeff shukrani sana..its been REAL,Keep up the Good work with the Blogg..Here is a gift to All Kwanza Unit and Bongo Celebrity Fans.
my song called “GRINDING”-KBC feat Fid-Q n RoZe PeTaL..Enjoy!!

Advertisements
 

23 Responses to ““WASANII WAJIELIMISHE,WAPENDANE NA WASIDANGANYANE”-KBC”

 1. Alias B-Man Says:

  Big up rispekt KBC, you’ve always been tru to HIP HOP nakumbuka my first radio interview ever was with you on Dr. Beat 1999. You make an excellent ambassador of TZ HIP HOP na I believe you and Zavaara can do great things with WAPI and even much more. Let’s network and see what else we can do together, najua the past few years have been busy for us all but I have a few ideas we can put together…it’s never too late…holla at me bro…rgmongi@hotmail.com..Y- Thang where yu at bro!!! LOL!! Kwanza Unit and Hip Hop 4 life!

 2. hombiz Says:

  Big up K Singo. Ushauri uliotoa una akili tosha kwa vijana wasanii wa Tanzania. Kila la kheri ktk shughuli zako. Stay up Bro!

 3. binti-mzuri Says:

  ah! haya

 4. mandingo Says:

  check this out from one of former members of kwanza unit bugzymalone now known as king jaffi, you can watch his video on youtube just type king jaffi and you will see the title of the song FALLEN ANGEL, he is currently reside in columbus ohio in USA. thanks everybody.

 5. Leo Faya Says:

  KBC – Kibacha.. hit me up its been years since we met up… But always good to read and hear from you.. Stay up.

  Leo

 6. Pamela B. Says:

  Very Impressive!!

 7. "Mzalendo" Says:

  Ndio KBC wapeleke shulee!!..Hawa wasanii wa Bongo Flava inabidi wajiendeleze zaidi ya Muziki..Waende shule..kama Mwenzao Mwana FA..Washirikiane kkt Fani zao..tumechoka kusia NGUMI kila siku..BEEF kila show..Mara KIKOSI kampigana NAKO2NAKO,mara WANAUME wamegawanyika..Mara TID kampiga Mshabiki..mambo hayo ndo yatakayo kwamisha juhudi zao za kisanii..KWANZA UNIT na nyie Mtarudi kwenye GAME lini??

 8. "Mzalendo" Says:

  Haya Bongo FLava kazi kwenu..wakongwe bado wanayakusema

  KBC-Verse 2:

  WELCOME TO THE MOTHERLAND
  HOME OF THE BROTHERMAN
  STONE COLD GUTTER MAN
  POVERTY STRIKEN,POLITICIANS SICKENING
  THEY’RE KILLING MY PEOPLE..GUNS ON THE STREETS MAN,
  TAXES IS HIGH, THE BUDGET IS LOW
  WE TRYING TO GET BY LIKE HUSTLE AND FLOW
  WE PRAY TO ALLAH.. THEY’RE STARTING THE WAR
  TELLING LIES WITH DEMOCRACY
  THEY’RE PUSHING THE DOCTRINE ALL OVER THE WORLD..

  Duuuu!!..Haya wale waliosema hawa wanaMuziki ni wahuni wako wapii?..NUFF Respect to KBC lakini FID Q is THE FUTURE..TZ HIPHOP4LIFE!!

 9. Stiggo (DE-PLoW-MaTz) Says:

  Big Bro,U always do big things,i got non but a respect 4 u n all KU crew without u guys i dont know where this bongo flava would be,I remember back then,no a lot studios,no a lot producers but u guys made non but classics.I like the point of saying bongo artists should love each other that sounds like nothing but the truth is those simple words mean a lot,N thats y u r…. n u’ll be on top of the Game forever even if u not making music any more,by the way i believe u still got some left,u gotta do 1 for fun!!!!,Holla at ur Boy,stiggo2@yahoo.com,
  Stiggo-New York City

 10. Hewa Says:

  Nice words Kibacha,ni vizuri uwaelimishe wasanii wa sasa wengi hawajui mambo yalianzaje na walikuwa wadogo wakati ule.msalimie wifi

 11. Matty Says:

  i understand nothing on those comments above! naona ni mwendo wa hiphopverse tu!

 12. Triple S Says:

  Mzee wetu K Single kazi nzuri nimependa mawazo yako na umenikumbusha mengi ya enzi zetu..! Hii cut ya Grinding ina “make sense” nasubiri perfomance ukija unyamwezini kwenye Bongo Flavour Expolsion.Keep it up. Amani.

 13. binti-mzuri Says:

  matty mi ndo mana commenti yangu ikawa kama vile!

 14. Stiggo (DE-PLoW-MaTz) Says:

  Hot song,i love it!!!,Holla at me.1

 15. Mwalimu Zawadi Says:

  KBC hilo ulilosema kuhusu redio kuua muziki mzuri Tanzania, umesema ukweli. Nimefurahi kusikia msimamo wako katika hilo. Endelea kuwaambia wasanii wa muziki mpaka wasikie. big up

 16. nylene Says:

  mandingo
  asante for ur comment nimeangalia hiyo video ya bugzymalone aka king jaffi bomba sana, jamaa anajitahidi sana tanzania tunaweza kupata akon wetu, ila inabidi jamaa apate hits nyingi sana kwenye youtube labda anaweza kupata record contract. vile vile ningeomba BC waweke hiyo video hapa itapata hits nyingi kwa vile bado zitakua zinaingia youtube. if you are interested read comment# 4 from mandingo

 17. nylene Says:

  ze-majuzi
  that is not the right video, check this one out
  http:/www.youtube/results?search_query=king+jaffi&search_type=&aq=0

 18. Jemedali Says:

  Basi mi na cmatani ni kama mkosi// twalenga na hatukosi// mawe baada ya mawe tumebarikiwa wee…….

  KBC heshima kubwa na muongozo wako wa nguvu. Hip hop ipo na itaendelea kuwepo. Najaribu kuja na project inayo consist Mimi (Jemedali), KBC, Fid Q na Hashim aka Dogo… we gatta keep it moving… unaonaje?

 19. Kaka Poli Says:

  Maneno matamu,
  kusoma hayanishi hamu,
  umefika wakati wa kushika hatamu,
  mjomba tuma salamu,
  kamweleze kikwete,
  tumechoka na ubwete,
  tunataka mahindi si mabua wala matete,
  sisi so maskini kama wanvyolazimisha iwe,
  sera zetu ni uhuni wanatuona wasaka mawe,
  wezi wetu vibopa, si majambazi wa duka waliochoka,
  hata waipore ikulu majina hayatochomoka,
  mikataba ya madini, rasilimali ya nchi, utajiriwa masikini unasainiwa nyumbani,
  ……………………………
  E-n-d-e-l-e-a!!!!!

 20. KBC..YO FAM..ITS BEEN A MINUTE..BUT much respect i like every single line on this article i hope somebody in this music industry esp…TZ ARTISTS CAN USE IT TO MAKE BETTER CHOICES AND AT THE END OF THE DAY A REEL TALENTED INDIVIDUAL CAN GET WHAT HE/SHE DESERVE…!!!!!!YES THERE IS A LOT MONEY IN TANZANIA THAT CAN PAY THE ARTIST WHAT THEY DESERVE..IN BUSSINESS…PEOPLE GET PAID WHAT THEY AGREED ON THE CONTRACT AND NOT””” WHAT THEY DESERVE…HOLLA AT YOUR BOY I LIKE THE TRACK…KEEP GOOD MUSIC COMIN I LOVE GOOD MUSIC..DJJOE..

 21. "Mzalendo"..a.k.a KBC. Says:

  Asante JeFF kwa Mahojiano haya..Nashukuru wale wote walionufaika na Hayo Madini Machache..Shout out to everybody who show their support every day for Bongo Music..Stiggo,Mongi ,Leo i ma Holla soon..Dj JOE thanx for reppin BONGO onna DJ tip..yu doing it BIG..Jeff you need to Interview this guy..He started just like any other Bongo kid who love Music..Now American Superstaers need his help to Promote their Music..For those in UK..MWANA FA will be in your Area for Sikukuu ya IDDI..show ya Support..Peace and Blessings…One!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s