BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ZE COMEDY:NDIO IMETOKA AU? September, 15, 2008

Filed under: Burudani,Comedy/Vichekesho,Sanaa/Maonyesho,Television — bongocelebrity @ 10:43 PM

Kama kuna kitu ambacho kilitokea katika upande wa burudani nchini Tanzania hivi karibuni na kuteka hisia za watanzania wengi,bila shaka kitu hicho ni kundi lililokuwa linajulikana kama Ze Comedy.Tunasema lililokuwa linajulikana kama “Ze Comedy” kwa sababu mpaka sasa kuna utata au kesi kuhusiana na haki miliki ya jina hilo!Kesi iko kwa pilato.

Ilifikia kipindi ukimtafuta mtu siku ya Alhamisi jioni(wakati kipindi cha Ze Comedy kipo hewani) usipompata yawezekana kabisa yupo mbele ya luninga yake akiwacheki Ze Comedy huku simu yake akiwa ameiweka katika mtetemko(vibration) katika kumaanisha kwamba “hataki usumbufu”.

Wakati kundi hilo likizidi kujipatia umaarufu mara ghafla zikaja habari kwamba Ze Comedy wanakwenda “mapumzikoni”.Pamoja na kwamba tangazo hilo liliwasikitisha watu,ilieleweka kwamba mapumziko ni jambo muhimu kwa kila binadamu kwa hiyo watu wakaelewa!

Tatizo lilikuja pale mgogoro ulipofumka baina ya Ze Comedy na uongozi wa kituo cha EATV ambacho ndio kilikuwa kinarusha kipindi cha Ze Comedy kila siku ya Alhamisi saa moja jioni.Mapatano ya mezani yakashindikana.Kesi ikaenda mahakamani(bado ipo).Siasa nazo zikaingilia kati.Vigogo wa nchi wakaingilia lakini wapi.

Leo hii watu wengi wanajiuliza,je Ze Comedy watarudi? Na wakirudi watarudi kwa namna gani,kwa kutumia jina gani?Unadhani watakamata tena?Unadhani kilichotokea mpaka hivi sasa kinatoa mafunzo gani kwa vikundi vingine na washika dau wote wa fani ya burudani nchini Tanzania?

Kuna habari ambazo bado hazijaweza kuthibitishwa zinazosema kwamba vijana hao mahiri kwa kuvunja watu mbavu huku wakielimisha jamii wana mpango wa kufanya ziara kabambe nje ya Tanzania.Tunasubiri.

Advertisements
 

40 Responses to “ZE COMEDY:NDIO IMETOKA AU?”

 1. wakuvanga Says:

  Pole sana ndugu zangu zecomedy sasa mjifunze make bongo swala likishakuwa la njuru nyingi basi ufiki mbali, jaribu kuwa na mikataba yenye akili sio unaambiwa njoo hapa nawe unakuja uliza nikija kesho itakuwaje??????????………………………………………………….Mambo ya pesa noma

 2. Melisa Says:

  Yaani nyinyie vijana manaonekana werevu sanaa, lakini kwa nini mnataka kupishana na wagogo kuhusu jina? kwa nini msitafute jina lingine mwendelee na comedy yenu,mnazidi kupoteza muda na mtasababisha watanzamaji kuwasahau bure, mbona majina yapo mengi tu? ) wao si hawataki mtumie (Ze comedy) then Go for (ze komedi) , muwe creative na proactive jamani, acheni malumbano na watu, mtakuja kufa bureeee, kisa jina. we miss u guys

 3. aisha rubama Says:

  kwa kweli inasikitisha sana..halafu mbaya zaidi hapa walipofikia ze comedy inawafanya wasanii wengine wachanga wakate tamaa kabisa na kufanya sanaa.,ambacho ni kitu kibaya saana.ze comedy ni kundi linalo jiamini nami nawapongeza kwa kila nyanja (kazeni buti makaka) kuna msemo wa waswahili usemao penye riziki hapakosi fitna ingawa sielewi vizuri mgogoro wao lakini nahisi kuna kubaniwa kwa hali fulani.siku yeyote ile mtakapo maliza mgogoro lianzisheni libeneke maana vipaji vyenu havitachakaa…msikate tamaa hata siku moja.

 4. EDWIN NDAKI Says:

  Nimerejea kutoka ze comedy(na maanisha mapumziko)…tee teee
  Kisiasa:
  Vijana walirubiniwa na mdosi “Manji” wampige chini Mengi baada ya kuona wanaanza kupata mafanikio kupitia EATV.Kwani ni suala ambalo liko wazi kuwa hao wakubwa wawili wana “bif” katia yao.Mmmoja akililia walalahoi mwingine akililia wanaokula mpaka HOI.

  Kiuchumi:
  Vijana walikuwa wanajiongezea kipata cha na pia patao la taifa na kusaidia hizoooo ajira milioni moja kila mwaka ziwekane.Hivyo kuwasimamisha ni kuwauwa WAJASIRIAMALI hawa.

  Kijamii:
  Walifanikiwa sana kukubalika na kufikisha ujumbe na burudani kwa asilimia kubwa.Pia serikali ilibidi wacheze dili la kuwavuta ili KUWAFUMBA mdomo maaana walikuwa wanawasaidia wananchi kuelewa “hard news” katika lugha rahisi.Kuwaamsha walio lala.Hivyo kuwavuta TBC ilikuwa njia ya “mpe mchawi akulele mwana”

  USHAURI:
  Naami hawa vijana wanavipaji.Ila kwa vikundi vingine na watu wengine.Ni vema kabla hujafanya maamuzi magumu kufikiri nini kitatokea.Ukipata umaarufu utumie vema

  WAHENGA WALISEMA:
  MILUZI MINGI UMPOTEZA MBWA:

  Nawamiss sana Ze comedy..kila la kheri muwe mswano mrejee kwenye game sio lazima kideoni hat akwenye RTD..utani

  TUTAFIKA TU

 5. Pandu Says:

  NGOMA IKILIA SANA………………

 6. Gervas Says:

  Mbali na sababu za kisheria zinazosimamia mgogoro huu, mimi nafikiri mgogoro huu umejificha katika swala la kisiasa au kibiashara au watu wawili tu wachache ambao wameamua kuonyeshana ubabe. Nikweli mgogoro umeshindikana kutatuliwa kwa njia za mezani? (kirafiki), in fuakti walikuwa wana make mai dei/week. I cant imagine watoto wanawamiss namna gani. Halafu hiyo haki miriki ni miriki ya jina pekee (ze comedy) au na perfomance yenyewe (manjonjo), maana kama ni jina tu si wabadili na waendeleze libeneke?……. Edwin Ndaki, jamaa zako wale wanaotaka kupiga Arua Ulaya kugonga Enjili bila ya visa wala tiketi umeshawaandalia majukwaa ya kufanyia hayo mahubiri? nasikia malibwa, jenenge, ma-Abel wote wamo !! teh-teh-teh

 7. Matty Says:

  Guys have talents, Mengi dear refrain pls, u better leave them alone, wat u did is unacceptable infront of GOD.

  That is me and not anybody..pls don’t touch my opinion guys!

 8. Dunda Galden Says:

  Hakuna kukata tamaa na zile zama za methali ya Ngombe wa masikini hazai akizaa dume na hakichukui mda linakufa sasa hakuna na kama zipo basi njia muafaka ni mapambano y hali na mali kwani dhulma za haki zinajengewa misingi ya kisheria kama haujaamka mwanzoni ngumu kuelewa maoni yangu……nilitafakali kwa kina sana
  POLENI ZE COMEDY ALUNTA KONTUNUA MSIBWETE
  chaidoga

 9. binti-mzuri Says:

  haha comment ya edwin ndaki imenichekesha

  ze comedy i miss uuuu!!! mi nilikua nawavizia youtube au eastafrican tube ila naona hata siku izi watu hawaupload.

 10. Chris Says:

  Mbona unajihami Matty! Hahahahaaa!

  Mliotangulia mmeongelea niliyotaka!

  Naamini mkataba watakaofanya baada ya hili sheshe walilo nalo hautakua kama uliopita! Mkataba ni kitu muhimu sana hususani kwa wasanii ambao kila leo wanaumia! Refer mahojiano na K-Singo! Wasanii wanajiua wenyewe! Hawako makini na ni kwa sababu ya tamaa ya fedha kidogo ambazo wanaahidiwa mwanzoni na wao huenda by then wanakuwa wako kijiweni!

  Mkataba mzuri hautaingiliwa na siasa ambazo zimeongelewa na wachangiaji waliopita!

  These guys are talented! Hizo (political) conflicting interests zinazoendelea ni kwa sababu ya vipaji walivyokuwa navyo hawa jamaa! Wish them the best on this hard road through!

 11. Frateline Says:

  Hi Guys kutoka Helsinki-Finland

  USHAURI WA BURE KWA ZECOMEDY

  Hawa jamaa kwa kweli wanakubalika, tatizo wanapoteza muda kugombana na MENGI ambaye alikuwa anawatumia kupata faida na matangazo ktk TV zake, Sasa nyie vijana ebu fanya mambo yafuatayo;
  1. Tafuta majina mengine hata ikibidi ikigiza kama viziwi bila kutaja neno comedy wala zecomedy, wala masanja, wala joti au mpoki achana na haya majina- sura zetu tiyari ni trade mark-nyie mnayo social capital tiyari, mkifika ktk TV siku moja basi tiyari kila mtu atajua

  2. Mimi ninakumbuka mwaka huu january nilikuwa bongo siku ya Zecomedy watu wa rika zote wanakimbia haraka nyumbani kuwahi kipindi- kuna watu wawili ninawaheshimu sana mmoja ni profesa(jina nalihifadhi) na mwingine ni mwenyekiti wa Taifa wa chama kikubwa cha Siasa kwa nyakati tofauti walikili mbele yangu kuwa wao ni wapenzi wa zecomedy- sasa nyie vijana kwa nini unafanya watanzania wawamiss kiasi hicho eti kwa sababu ya tamaa za mengi na mhavile-achana nao hao

  3. Jiite machina tofauti kwa muda wakati mambo ya kesi yanaendelea- hata mkiwa na majina yetu halisi kwa muda

  4. ITV na East Africa TV wanapenda kunyonya wasanii, wakina mambo hayo wako wapi? wangapi wamepita hapo wakijua haki zao , mengi na mhavile wanawafukuza, msikubali hata kidogo kurudi East Africa- nyie lazima mjisimamie- na hii italeta heshima kwa wasaa wachanga na nyie mtakuwa na pesa kama wasanii wa ulaya, usikubali kutumiwa.

  5. wakati huo huo mnaweza kukuanza kujiendeleza kimasomo hapo hapo Bongo vikozi vidogo vidogo msilewe masifa- nyie kazi ni mtindo mmoja hakuna kulala.

  6. msijipendekeze sanaaaaaaaaa kwa baadhi wa watu wanaojifanya wanaipenda sana CCM wakati hata CCM yenyewe wanahisaliti, wanawaogopa msije waumbua, kama mnataka muendelee kukubalika lazima muwe huru kama mwanzo

  Mwisho ninawatakia maisha mema, mimi siwamiss maana nipo nje ya bongo niliwaacha mnatesa nakumbuka mara ya mwisho kuwaona live ilikuwa mnazi mmoja ambapo umlimfunika makamu wa Raisi- nyie mlikuwa mnatisha, you were really great bongo celebrities.

  God bless you guys

  Frateline

 12. Mswahilina Says:

  Edwin umesema kweli.
  Pia hawa vijana walilewa sifa.

 13. msukule Says:

  Huyo mchaniaji namaba mbili namuunga mkono na miguu.
  Lazima wawe creative hata kama kuna watu watatumia jina ilo,wananchi hawana inrest na jina wana interest na comedy yenyewe.
  Funzo kwa vijana ni kuwa kabla ya kufanya maamuzi ni lazima wachunguze na wawashirikishe wajanja.
  Pili,mliondoka na maneno ya kejeli bila kujali nani kawafikisha hapo.

 14. BALTAZAR Says:

  NGUGU ZANGU ZECOMEDY POLENI SANA NAFIKIRI ALIYEWASHAURI MFUNGUE KESI KISA ETI NI HAKI MILIKI LA JINA AMEFANYA KOSA KUBWA SANA NDIO MAANA JAMANI WATANZANIA WENZANGU KILA MARA MIMI NAWASHAURI SANA ACHENI KABISA KUWA NA MARAFIKI AMBAO SI WA KWELI.

  MIMI LEO HII NINGEKUWA ZECOMEDY NINGEBADILI JINA NA NINGEPIGA KAZI KAMA KAWAIDA MFANO MDOGO TU CELTEL TO ZEIN SI UNAONAONA KAZI WANAPIGA KAMA KAWAIDA JINA WALA HALIKUPUNGUZII CHOCHOTE NI UHABA WA MAWAZO KWA KWELI KAMA KUNA UWEZEKANO NINGEOMBA MUWAACHIE EATV JINA WABAKI NALO NYIE PIGENI KAZI.

  PIA VIONGOZI WETU WA SERIKALI WANGEINGILIA KATI SWALA HILI KWANI HAWA ZECOMEDY JAMANI WALIKUWA WANAFURAHISHA MNO HATA KAMA MTU AMENUNA SIKU NZIMA LAZIMA KWA ZECOMEDY UNACHEKA SASA, KESI HII KWA KWELI INAONEKANA KWAMBA KUNA UBABE WA MATAJIRI WAWILI AMBAO INASABABISHA WATANZANIA WANAKOSA UHONDO.

  KAMA KUNA UWEZEKANO NAOMBA NIPATE CONTACT ZA MWENYEKITI WA VIJANA HAWA ILI NIWEZE KUWAPA USHAURI MZURI AMBAO UTAWAFIKISHA MBALI SI KUWA NA TABIA YA KUPENDA KESI.

  BALTAZAR ATHANAS
  http://www.kipepeotours.com

 15. Pearl Says:

  jamani kama ni hilo jina si mumuachie huyo muhusika!!!! kwa sababu kama ni kweli yeye ndo ana hatimiliki sasa nini
  makelele!!!!!?????

  tungine jina lenu jingine, angalieni wale “FUTUHI” wa Star tv wameigiza muundo mzima wa “ZE COMEDY” ila ni jina tu ndo wametofautisha.

 16. Matty Says:

  Chris mtani wangu si unajua watu hawakawii kuninyoshea kidole haahahahahahhaa!!! ila nimewaweza hakuna aliyetouch my opinion aisee!
  Edwin Ndaki tutafika kweli kwa mtindo huu wa kukandamizana????

 17. Mama Maureen Says:

  jamani ze comedy msiendelee kupoteza muda angalieni usawa mwingine kama ni kubadilisha jina muendelee kuburudisha jamii.mjue muda ni pesa,fanyeni linalowezekana mrudi hewani!!!

 18. Anonymous Says:

  Hawa mabwana wadogo walifikia hatua ya kututukana sana baadhi yetu tuliowapa hizo kazi za pembeni (private jobs). Katika mojawapo za kurushiana maneno, tuliwaasi wasiwe na kiburi, na kwa maneno makali tukawaonya kuwa hayo mapembe yao walizozikuza kwa kiburi zitakuja kukatwa siku moja! Sijui hiyo siku ndo imetimia au? Mengi atawabana mpaka basi…. Lakini kwa hilo, inabidi mjifunze ili mkipata nafasi nyingine ya kuwa ma star tena, msitudharau wakubwa wenu….. dont hurt and spit on people as you climb the ladder of life, because you dont know when you will come down…..

 19. real-TZ Says:

  Nianze kwa kushukuru Edwin Ndaki, comments zako ni full ukweli, then niendelee na huyu Matty(mzungu wa kibongo) sijakubaliana nae, kwanza nam ignore coz haelewi mchakato mzima….amedakia mada.

  Narudi kwa maoni yangu
  hawa vijana ni kweli wazuri lakini walichemka kukurupukia mkataba mnono wa TBC bila kujua ni nini chanzo cha wao kuupata mkataba mnono kama huo.

  kila kitu kina reason, wakatae wakubali bifu la wakubwa wawili ndilo chanzo. huyo wa pili alitaka kumkomoa mwingine ambae kwa bahati mbaya ndie mtu mwenye IMAGE nzuri tanzania(mpigania walalahoi). ambae hata utajiri wake ni wakuutolea jasho c wakuukuta kama huyu mwingine. na ndomana huyu mwingine aliewachukua washikaji huwa hana uchungu na hela zake. Hata misaada yake huwa hailengi kusaidia jamii kama mwenzake bali ni kujipa MIJISIFA isiyo ya maana.

  so: kwasababu mlishakosea, nyie jishusheni mtafute jina lingine then muendelee na kazi yenu, ila muwe makini. Hatutegemei kama mtaacha kuwakosoa MAFISADi kisa eti mmesaini mkataba na………………

 20. mililindi Says:

  Hii ni aibu kwa kituo kinachomilikiwa na mtu mpenda amani kama Mheshimiwa Mengi kuwazibia riziki vijana wa Ze comedy kisa kuthaminiwa na Manji,Mheshimiwa Mengi ingilia kati waweke huru vijana ili wapate kupata mkate wa kila siku ninajua umepata hasara kwa kukosa pesa za matangazo kwenye kipindi hiki na wewe una vyanzo vingi vya pesa hata kama ni sheria kumbuka kuwa hata ukipata wana comedy wengine na kukiita kipindi The comedy na kuwaita hao watu Masanja Mkandamizaji,joti mpoki wakuvuanga na nk. hawatapendeza kama the comedy yenyewe original.Mengi ingilia kati kwa huruma yako uwaache hao vijana waendelee na kazi wewe Mungu atakupa zaidi na zaidi na kama na wao kupata fundisho kwa sasa wamepata fundisho la kutosha hawawezi kurubunika tena kirahisi.EATV futa kesi waruihusu vijana waendelee.

 21. halima Says:

  Ze comedy wanawane, nyinyi mnatisha hakuna anaebisha, siku zote binadamu usfanya kitu kwa kumuogopa mtu hautafanikiwa milele, fanya kitu roho inataka, Kwa hiyo mengi labda kama angekuwa amewapa hiko kipaji ndio ingekuwa big tatizo lakini mmezaliwa nacho wala msijali wanawaneeee. kama ni jina badilisheni muendelee kutupa mavituuz

 22. mariorossen Says:

  I like that,…bicause I have joke too

 23. Hombiz Says:

  Jamani eeeeh!. Kwanini kila penye kula pana mbwembwe kiasi hiki? Kweli Bongo songombingo!

 24. nammy Says:

  malindi cku zote msema ukweli lazima abaniwe,kwan huijui nchi yako ?

 25. Mswahilina Says:

  Hawa vijana warudi tu EATV wakaombe msamaha na kuendeleza libeneke la kukandamiza.

 26. jonas Says:

  Poleni the comedy,lakini muda bado upo, mi nawashauri,badilisheni jina ingieni kazini.Nyie ni wabunifu hata hizo mtabuni nyingine,nawaamini.

 27. Matty Says:

  Real-Tz,hata mimi nakuignore vilevile wewe mwenyewe hujui unachoongea so ndo maana nikasema pls don’t touch my opinion!!!
  Hayo uliyoongea si mageni na hayatokuwa mageni masikioni pa mtu yeyote yule….mtizamo wako ni wako na wangu ni wangu.
  pls Relax Real-Tz!

 28. kindo Says:

  kuvunja mkataba na kuingia mkataba mwingine si tatizo…lakini tatizo ni upambe uliojitokeza baada ya mkataba wa kwanza kuvunjika. Mpambe hakujulikana katokea wapi na kwasababu zipi na wala hahusiki kabisa na mambo ya habari na burudani. sababu hii inafanya mafahali hawa ambao siku zote wanatofautiana katika anga za biashara wazidi kupigana kutumia migongo ya vijana hawa ambao wao bila kujua wanaumia. mwisho wa siku sisi tutawasahau na hao mafahali watachoka/watawachoka. la muhimu waachane na wote wapasue kivyaovyao. watafute wanasheria ambao watawasaidia ktk kuangalia mikataba iliyopo na kujua wataanzaje upya…..wakumbuke kuwa fani ya burudani inakwenda na muda, jinsi wanavyochelewa ndivyo na watazamaji wanavyozidi kuwaondoa akilini…nasikia kuna kikundi huko mwanza kimeanza kuwaiga ….sasa hivi litaibuka kundi jingine, litakalo vuta hisia za watazamaji kiaina and ze comedy will be no more….hangaikeni vijana wakati ndio huu!

 29. kazingoma Says:

  mwana wane sasa sijui wamejikandamiza wenyewe au wamemkandamiza mtu…! any way jamaa tumewamisi sana. La msingi watoke kivingine tu kuku si kuku tu jogoo jina, wongo mazee1

 30. ISMA KABENGO Says:

  WEWE MSWALIHINA UNAKOSEA KABISA HAKUNA CHA KURUDI ITV KUOMBA SAMAHANI,ITV WANAFIKIRIA KUWAKOMOA TU,HAWA BADO VIJANA WADOGO SANA WANAHARIBIWA MAISHA YAO NA UBINAFSI WA ITV,KWA MANUFAA YA EATV SASA HUYO MENGI ANAYESEMA ANAWAJALI WAZAWA KUJIWEZESHA ANAWEZESHA AU KWA MANUFAA YA MAKAMPUNI YAKE?????///LAKINI NATAKA KUJUA MWENYE HATI YA USAJIRI NI NANI????ALIYENAYO MKONONI???? EATV AU HAWA JAMAA????

 31. khalid Says:

  wasirudi tena hao takataka walikua wanaona raha kujifanya kuiga kuran tukufu!!!
  ndio nimewatokea puani sasa.
  mr nice chalii,nani sijui chali sasa ze comedy chali chali chali x 100.

 32. mbowe alirehema Says:

  Mengi ni mnafiki hana cha kusaidia walala hoi wala nini, eti utajiri kautolea jasho! hakuna mtu anaweza kukueleza chanzo cha mafanikio yake, kila mtu atajaribu kutia chumvi jinsi gani ametajirika, hawa ni watu walioua NBC kukopa na kuto lipa mkopo, ni mnafiki mkubwa tu ndo maana anajipendekeza kwa serikali, ana ujanja wa nyani tu, hata misaada anayotoa si pesa zake ni za wafadhili lakini hataki kuweka wazi kwa vile ni mpenda sifa mkubwa, sasa anasaidia niaje kwa kukandamiza hawa watoto. alikuwa na makapuni mengi ya franchise anasema yake kumbe ni ya watu yeye ananunua jina na kupata pesa toka kampuni mama na ku-kick off the business, hata mengi ya makampuni yake ya habari ni yanje, hana akili wala ubavu wa kuanzisha chake, kwanza hakuna biashara rahisi kufanya kama ya habari hata kipofu anaweza kufanya.

 33. kazingoma Says:

  Aaah! mazee si kihivyo.
  Khalid:
  Ni kweli unadiliki kuwafukuzia mbali jamaa ati kwa vile waliwahi kuiga au kuigiza Quran Tukufu.Mbona kuna visa kadhaa wamekuwa wanaigiza Biblia Tktf,mfano kuigiza maombi kwenye barabara mpya ya Sam Nujoma kama utakumbuka n.k isitoshe visa vilivyowahusu watu binafsi,makundi ya watu n.k wote sie tungewalaani sasa ingekuwaje tena umaana wao.

  Any way sikumbuki hicho kisa kilichokugusa kivile mpaka ukaona hawafai na wakafie mbali zao,e bwana.

  Baltazar:
  Huenda unajua zaidi nisamehe ktk hili, sidhani kama tatizo ni jina tu kati ya hawa jamaa na eatv, lazima yapo mengine sambamba na hilo ili wawe “totally different entity” na hiyo ze comedy, e bwana, ndiyo kusema subira inaahitajika hasa kwa wao wenyewe na hasa kwa vile issue imekuwa ya kisheria zaidi.tacare mazee!!!!!

 34. ze-majuuz Says:

  Khalid wewe ni taraban nini? Itabidi na wewe ukapotelee pangoni huko Afganistan. Ule wako Obama akutie machoni, utajuta! teh-teh-teh!

 35. tally Says:

  1-vijana walikuwa fresh sana umeona but hawataki kujifanya wajinga ili wapate hela kwani kubadilisha jina kuna chukua muda gani?
  2-washkaji baada ya kutoka EATV na mabifu yale wakajidai kwenda ku colaborate na MANJI na ndio ili mpain sana MR.MENGI hata hivyo mengi yeye hausiki bali ni TV presenter na producer ndio kazi zao yeye anafanya kazi ya kusimamia kampuni yake.
  3-vijana wanaongopewa na viela wanavyohongwa na MANJI mwanaume haongwi then kuombaomba c o kuzuri coz washkaji MANJI hana future nao yoyote yeye anataka wamuombe hela tu mwisho wa siku anawatema tu jamaa nackia walikuwa wanalipwa hela nzuri kwanza walikuwa wanalipwa per episode watakayofanya na kwa mwezi wanalipwa tena, wangapi waliokuwa wavumilivu wametoka ITV m2 kama betty mkwasa(mkuu wilwya), hamedi kipozi etc
  NI HAYO TU

 36. Amina Says:

  we khalid umenichekesha

 37. Olive Says:

  Mungu atawatangulia tu,penye jema hapakosi baya,kama kuna mahali ZE COMEDY walimkosea mtu jamani muwasamehe,kumbuka nawe huwa unakosea na unasamehewa,Mungu pia amekusamehe wewe mangapi tangu uzaliwe?

  We Khalid Quran haikufundishi laana na visasi okk??????

  Frateline NO.11 i salute ur comments,za kiwango sanaaaa,high que yako imejionyesha.Tek care

  Otherwize i miss u ol ze comedian,jamani we are praying to c u back and having funny from u guyz,mpo juu na u r unique hakuna kama nyie TZ mnafunika.

  Mtatoka tuuuuuu,riziki ya mtu haipotei inacheleweshwa tuuu.

  Ze majuuz umenifirahisha mnooooooooo!!!!

  Tehe tehe tehe

 38. BigThinker Says:

  Nyie mnaoponda mengi, mnaweza kuniambia anahusikaje? Hivi ni nituko, Mengi anadili za maana za kumkip bize…who are ZE COMEDY anyway?

  Kwanza walikua wanapotosha jamii kwa maneno yao ya matusi na kufikia kuigiza maneno matakatifu kihuni, wale kona.

  Umaarufu gani waliokuwa nao mpaka wambabaishe mengi, na huyo bosi wao(seki) amesahau alipotoka, bila huyo Mengi mnaemponda nani angemjua? Je angekua anadhulumiwa mbona amechelewa kuondoka?

  Think Big kabla ya kuanza kutoa Comments za kizushi

  Enjoy!

 39. Jamal Says:

  Namsaport huyo BIGTHINKER, its true vyote ulivyosema. wabongo tuache ushabiki…tujifunze kufikiria kabla ya kuropoka.

  Kila mtu hakosi maadui ila nenda mbele rudi nyuma MENGI ataendelea kuwa mtu mwenye kuheshimika maishani yake yote.

  amekua akisaidia jamii kwa mda mrefu sana, huyu MBOWE ELIREHEMA anaesema mengi ni mnafiki, misaada anayotoa siyo ya kwake….nataka kumuuliza swali moja.

  TUNA MATAJIRI WANGAPI TZ? WANGAPI WANAJISHUGHULISHA HATA KWENDA KUOMBA HIYO MISAADA KWA WATU WENGINE ILI WAWASAIDIE WABONGO?

  Sasa kama hawafanyi hivyo kwanini tusimkubali MENGI?

  Tuache ubinafsi hata wa shukrani.

  ThinkBig!

 40. sifeni Says:

  Na hao vigogo hawataki kundi hilo liendelee kwa sababu walikuwa wanaongea ukweli kuhusu matendo yao wanayo yafanya ambayo ni kuwatapeli wananchi.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s