BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAYALLA IS DOING ALRIGHT September, 16, 2008

Filed under: Watangazaji — bongocelebrity @ 10:34 PM

Paschal Mayalla(pichani) mwandishi na mtangazaji maarufu hajambo na tayari yupo tena mitaani kuendelea na shughuli zake ingawa kidogo mkono bado unamsumbua.Hiyo ni kwa mujibu wa blog ya Mzee wa Sumo.

Kama mtakumbuka hivi karibuni Mayalla alipata ajali mbaya ya pikipiki alipokuwa akisafiri kuelekea Dodoma akitokea Dar-es-salaam Pichani ni Pascal Mayalla akikatisha katika mitaa jijini Dar-es-salaam kama alivyonaswa na Mzee wa Sumo.BC inaendelea kumtakia Mayalla afya njema.

Advertisements
 

14 Responses to “MAYALLA IS DOING ALRIGHT”

 1. Matty Says:

  Pole sana Paschal Mayalla, inshallah Mungu akuponye huo mkono uendeleze libeneke!

 2. halima Says:

  Pole sana Paschal Mayala ndugu yangu lakini angalia hiyo pikipiki itakutoa roho ndugu yangu all the best

 3. Hombiz Says:

  Pole sana Paschal Mayalla. Life is never fair!. Mtangulize MUUMBA mbele and everything else is gonna be O.K.
  Ushauri wangu ni kwamba achana kabisa na mambo ya pikipiki. Take that as a warning sign hommie!
  Stay up Bro!

 4. Pearl Says:

  sasa haya mambo ya kusafiri na pikipiki ndo nini tena we mayalla!!!!???? si unaona umeumia sasa!!!!! haya usirudie tena

 5. EDWIN NDAKI Says:

  Ni habari njema kwamba mapambano bado yanaendelea.

  Binafsi nilianza kumfahamu na kuvutiwa na kazi za huyo muheshimiwa pale alipokuwa ITV.

  Pascal anakumbuka alikuwa na kipindi kizuri sana.Nakumbuka alikuwa na kipindi kilikuwa kinaitwa “KITIMOTO” sio mfugo bali kifaa kinawaka.Matty upo hapo kwa Dani.

  Nilikuwa napenda jinsi alivyokuwa akiwaalika watu mbali mbali maarufu na kuitwa washiriki wawaulize maswali.Kile kipindi kilikuwa bab kubwa.Nina hakika vipindi kama vile vingituwezesha kujua mengi.

  Mfano mambo ya EPA,RICHMOND au mzee wa KIWIRA aka Mzee Lupaso naye tungemuita tungemwambia japo atupe dodosa kuhusu maendeleo ya MRADI wake wa kiwira.

  Kila jema Pascal Mola yupo naye upone haraka ili tuendelee na safari ndefu ya kufika nchi ya asali .

  TUTAFIKA tu haijalishi miaka mingapi

 6. Triple S Says:

  Pole sana kaka Mungu akubariki pikipiki tafadhali jaribu kuiweka pembeni ikiwezekana kaka, najua ina historia ndefu lakini…Take care. Inshalaah Mungu akulinde.!

 7. Debora kiaka kizuguto Says:

  Pole sana Pascal Mayalla mungu ni mwema aliyekuponya na kukutetea katika ajali ya pikipiki acha kabisa kutumia pikipiki katika safari ndefu, Usimjaribu mungu. Ukasema ni shetani kumbe wewe mwenyewe, kukinga ni bora kuliko kutibu.
  Debora

 8. kazingoma Says:

  Pole sana Bro! wewe ni mtu makini sana kt.safu hiyo muhimu,nafeel sana kazi zako toka enzi za ‘kitimoto’ 7-7 shows, ushereheshaji (Mc) n.k.Get well mkuu huo mkono na sio vema kutumia ‘sekeni’ kwa safari ndefu kama hiyo kiafya ni hatari licha ya kudondoka. stay alright Bro! God is Great.

 9. binti-mzuri Says:

  yani kasafiri na pikipiki kutoka dodoma to dar.. duh..si angepanda basi!..

  ajali ajali tu… hata asipopanda pikipiki anaweza pata ya gari..the thing here ni kumuasa awe mwangalifu,kumwambia aweke pikipiki pembeni i dont think it solves matter.maybe thats the only mode of transport hes got..aache kwenda safari ndefu na pikipiki though..ndani ya jiji thats fine,ila from dodoma to dar thats a no-no

 10. Monica Says:

  Pole ndugu inaelekea MUNGU anakupenda sana mara ya pil sasa unanusulika kufa na ajali.
  Yaani toka nizaliwe nina miaka 32 sasa, kwakweli sijasikia kama kuna watu huwa wanasafiri umbali mrefu kama huu wa Pascal Mayalla alivyofanya natumaini wote akili zao si nzuri.Nasafirigi na gari ndogo mpaka kwetu Tanga huwa magari makubwa nikiliona tu linakuja napark kando lipite kwanza ndio niendelee na safari, leo yeye pikipiki yaani kweli kuna watu wamedata, na kudata si mpaka uvue nguo kweli nimeamini usemi huo,

  Mdau Swiss, Geneva

 11. Mpogoro, Cardiff Says:

  Sasa na werafiki yangu Pakali, yaani umekuwa bahili hivyo umeshindwa kuongeza milini moja tu ukanunua hata ka-corolla mpaka unadiriki kusafiri na pikipiki kwenda Dodoma. Acha kujaribu Muumba wako. tunajua serikali wanakupa hela nyingi sana kwenye maonesho na mikutano na masherehe yao unayowafanyia kazi. Please, bado tunakuhitaji

 12. Angeline Says:

  Pole na hongera kwa kuendelea vyema.

 13. kibwega Says:

  Nyie mnashangaa pikpiki. Mwaka fulani nilikutana na wazungu wanatoka europa na baiskel wanaenda south halafu kwa meli mpaka S. amerika the north amerika then by flight to europe. Endelea na pikipik ila uje madreva wengi ni vichaa sana hawajapimwa unapoona vyombo vyao unawapisha.

 14. MARY-WASH.DC Says:

  POLE SANA KAKA KWA AJALI ILIOKUKUTA.NATUMAINI UNAENDELEA VIZURI.NA BWANA MUNGU AKULINDE NA AKUBARIKI.AMEN


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s