BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ZIMBABWE:DEMOKRASIA AU UNAFIKI? September, 16, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 10:43 PM

Advertisements
 

23 Responses to “ZIMBABWE:DEMOKRASIA AU UNAFIKI?”

 1. Hashim Abedi Says:

  Wakati waafrika tunafurahia mapatano yaliofikiwa kati ya Muigabe na Tsvangirai , furaha hiyo ni ya matarajio kwamba yaliofikiwa yatasaidia kuikwamua Zimbabwe kutokana na janga la kiuchumi na maafa yanayoendelea kuwakumba raia wake. Lakini tukio hilo ni la hatari na kitisho kwa demokrasia barani Afrika, kwamba sasa unazuka mtindo mpya wa watawala kutokubali kushindwa pale wanaposhindwa na badala yake kuwa tayari kugawana madaraka na washindi na wao wakioshika mpini. Baada ya Kenya sasa ni Zimbabwe sijui itafuata nchio gani nyengine. Zanzibar ndiyo kiboko yao, mgogoro chaguzi tatu zilizopita lakini hakuna suluhisho. Watawala wanaendelea kupiga debe” Mapinduzi daima.” Lakini wanasahao kwa binaadamu hakuna mbabe wa milele.Wako wapi kina Ceucescu, Hitler, Karume ,Bokassa na wengineo ? Haki inaweza kuchelewa lakini huwezi kumnyima mtu daima.

 2. Matty Says:

  uchu wa madaraka/tamaa mbaya/ubinafsi/ufisadi/chuki/unafiki/jeuri/kiburi/utawala wa mabavu ni vitu vinavyomchukiza Mungu!!Iko siku Mungu atasema na wewe Mugabe!!

 3. Wakuvanga Says:

  Hakuna demokrasia yoyote kwa Mbabe jamaa ana miaka 85 bado anataka kuwa rais wa nchi kuna nini pale Ikulu, yeye na Mwai K. hari moja

 4. Dunda galden Says:

  WALIANZA BURUNDI KWA KUPEANA MUDA KWENYE UONGOZI…

  MCHEZO UKAWA MTAMU WA KENYA WAKAFUATA………

  SASA NGOMA INAZIDI KUNOGA KWA WAZIMBABWE NGOMA INAZIDI KUNOGA…KWA WAPENDA AMANI HII NI NJIA NZURI SANA LAKINI KWA WAHUSIKA NI UNAFIKI MKUBWA UWEZI KUMFANYA RAFIKI ADUI WA BABA YAKO….

  JOHN GALAN YALIMKUTA BAADA YA KUTAFUTWA KWA MDA MREFU SASA AKAINGIA KWENYE LAIN
  KWA WENGINE TUSUBILI MUDA MAANA UONGOZI KIVULI UNAULAKINI WAKE

  KWA WENGINE ITAKUWA MCHEZO NI HUO HUO NA KUWASAHUA WALE WALIOMWAGA DAMU NA MISIBA KWENYE FAMILIA ZAO SIJUI SIJUI HUU MCHEZO UTAKUWA HADI LINI YETU MACHO

 5. halima Says:

  Wewe mugabe hivi unayo dini? hata kama huna dini na mungu je humjui? kumbuka kuwa hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha, angalia damu ya watu iliyomwagika basi ipo siku na wewe utalia kilio kama cha hawa mafisadi wetu watanzania, ambao walikuwa wanakula good time, kibao kilipogeuka kuna wengine mpaka walijitangazia kuwa wamekufa . angalia yasije yakakukuta

 6. Hombiz Says:

  Siasa ni mchezo mchafu sana! Kinachonisikitisha mimi ktk muelekeo huu mpya wa siasa za Afrika ni kwamba wengi wanaoathirika na Tabia hii ni wananchi walio wengi ambao wengi wao ni masikini wa kutupa. Hao ndio wanaokufa kwa machafuka, hao ndio wanaoteketea kwa njaa, ujinga na maradhi. Wakati hawa “viongozi batili” (Mugabe, Kibaki, Tsvangirai na Odinga) wao wanaishi maisha bora ya Kikwete.
  Hakuna cha kupigania demokrasia wala nini hapa!. Wote hawa wana uchu wa madaraka tu! Tena si ajabu hao wapinzani wakiingia madarakani ndio watakuwa wabovu zaidi kuliko watawala waliopita. Chiluba si alikuwa akihubiri juu ya democrasia na kuleta maendeleo kwa Zambia wakati alipokuwa akifanya kampeni zake za kugombea uraisi!? Je, alipoingia madarakani nini kilijili!? Aliiba kama mwendawazimu. Mala anunue suti kwa kutumia mamilioni ya $, mala anunue appartment complex nchi za nje, na mambo mengine kama hayo. Na yote hayo aliyatenda kwa kutumia pesa za walipakodi wa nchi yake tena isivyo halali. Hivyo basi, kwa mtazamo wangu mimi, naona wote hawa wanaopiga kelele ni njaa kali tupu! Wanataka madaraka ili wakiyapata wajineemeshe wa ufisadi uliokithili wakati wakiwaacha wananchi walio wengi wakitaabika kwenye wimbi la umasikini uliopindukia, ujinga, na maradhi na vifo vinavyosababishwa na maradhi yanayoweza kudhibitiwa. Nionavyo mimi, Afrika haiwezi kupiga hatua za kweli za maendeleo mpaka walau haya machache yafuatayo yatekelezwe.
  Kwanza, lazima Afrika isiwe na viongozi ambao ni vibaraka wa mataifa yaliyoendekea ambao yanawaendesha viongozi hao kama pia ama Remote Control(wazungu) na TV(Viongozi wa Afrika)
  Pili, Afrika ni lazima iungana na kuwa kitu kimoja na kushirikiana kiuchumi, kisiasa na kiitikadi. Hapo jambo moja kubwa ni kuwa na ushirika wa kiuchumi. Mfano, kuwa na soko moja la Afrika ambalo litapanga bei ya bidhaa zetu ziuzwazo nchi za nje, na sio wazungu kutupangia bei duni ya bidhaa zetu.
  Tatu, muungano wa Afrika hautawezekana mpaka viongozi wenye uchu wa madaraka wasipewe kabisa nafasi ya kuingia Ikulu.
  Jamani eeh!, pia wananchi wengi wa Afrika bado hawana elimu ya kutosha ya kuchanganua mambo mbali mbali kama uchumi na siasa, kutokana na upeo mdogo wa uelewa unaosababishwa na elimu duni. Hii inagusa zaidi wananchi wa vijijini ambao wengi aidha hawakusoma kabisa, au wana elimu ya shule ya msingi tuu. Hebu fikiria, mpaka sasa kuna wananchi nchini Tanzania ambao wanamchagua mtu kuwa mbunge wa jimbo lao kwakuwa kawanunulia pilau, doti za kanga na kuwaambia kuwa wasimchague kiongozi wa upunzania kwakuwa ataleta vita. Wanakubaliana na upuuzi huu kwakuwa uwezo wao wa kuchanganua mambo ni duni, kutokana na uelewa mdogo unaotokana na elimu finyu. Hivyo basi, swala la elimu ni lazima liwe moja ya mahitaji muhimu ya muafrika kokote balani Afrika hivi sasa. Chakula, mavazi, malazi na elimu.
  Hayo ni maoni yangu!

 7. michelle Says:

  Matty kiboko yao ni Mwalimu nyerinyeri tu, kaondoka bila vita na mtu, hakuwa mambo ya kung’ang’ania ikulu. baadae akarest in peace!!!

 8. Mswahilina Says:

  Mie simuamini mzee wa Jongwe.

 9. matty Says:

  Michelle shosti, naipenda Tanzania kwa moyo wote…aisee Mwalimu Nyrr (RIP) alikuwa kiongozi anayefaa kwa kweli lazima tukubali.

 10. Frateline Says:

  Hi Guys kutoka Helsinki-Finland

  Kwa kweli Bara letu la Africa bado safari ni ndefu sana kuelekea ukombozi wa kuichumi na democrasia ya kweli, lakini hakuna kukata tamaa, hila watu wengi msisumbuke sana na kizazi hiki cha wakina mugabe, Museveni na hata kikwete- hiki kizazi cha viongozi waliopo madarakani kimefikia Climax yaani ukomo wa perfomamce yao hakuna jipya na hawataki kuachia madaraka hivyo kusubiri historia ichukue mkondo wake- mimi ninamatumaini sana na imani kubwa sana ya kutisha kuhusu kizazi kijacho miaka ishirini ijayo yaani 2028 kwa wale watakao kuwepo Africa litakuwa bara zuri sana maana kipindi hicho usawa wa kijinsia utakuwa pazuri, democrasia itakuwa na umri wa miaka zaidi ya 30 kwa nchi nyingi za Africa na pia mabadiliko mengine makubwa dunia yakiwepo ya watu weusi kama Obama mtoto wa Kenya kuwa kiongozi wa Taifa kubwa kama Marekani kitakuwa ni jambo la kawaida sio news tena, Hivyo kazi tuliyonayo Waafrica ni kila mmoja wetu kuwekeza katika kizazi kipya kama ni mzazi msomeshe mtoto wako kwa nguvu zako zote, kama ni mwalimu toa mchango wako kwa hali ya juu, lazima tuachane na mawazo ya kukaa kulaumu wakina mugabe ambao pia kwa kizazi chao wanamchango wametoa katika mapambano ya kumkomboa mtu mweusi ingawa wamefeli kiuchúmi, tukumbuke nchi karibia zote za Africa kwa sasa hakuna Democrasia ya kweli- wengi ni wezi wa kura, hivyo mabadiliko lazima yatakuja hivyo ni jukumu letu tuyaandae.

  Mwisho kuhusu hatua ya Mugabe ni hatua nzuri sana katika kuelekea democrasia ya kweli kuanzia kizazi kijacho-2028 na kuendelea, ni uvivu wa kufikilia kwa mtu kutegemea mtoto anayeanza kutambaa kumpeleka katika mashindano ya olimpiki, Kwa mfano Democrasia ya Ulaya na marekani ina umri mkubwa sana- marekani-221 years na ulaya nchi nyingi zaidi ya miaka 100 ya uhuru, hivyo kwa maoni yangu hii hali ya kukubali kugawana madaraka ni hatua nzuri hivyo CCM na CUF huko Zanzibar mnangoja nini? Kumbuka kabla ya hatua hii ya kukubali kugawana madaraka, viongozi wengi wa Africa kwenye vyama vyao tawala walikuwa na kasumba ya kufikili upinzani ni vibaraka wa wazungu na hii inatoka na historia chafu ya ubepari na pia upinzani Africa ulikuwa unatafsiriwa kama uadui na chanzo cha Vita, malipizi kwa vipongozi lakini kwa sasa dhana hizi potofu zinaanza kupotea, hivyo NINAMPONGEZA SANA MPIGANIA UHURU WA ZIMBABWE MZEE WETU ROBERT MUGABE ambaye richa ya mapungufu yake ameionyesha dunia kuwa Mwa Africa anaweza kusema no kwa viongozi wa kizungu wakolofi kama BUSHI au Blair waliopigana vita ya uonevu huko Iraq, na hii inatufundusha viongozi wa bovu wako hata marekani au Ulaya mfano mzuri ni Bushi-unpopular president in USA- deni la nje la marekani sasa ni karibia Trilioni 10, budget deficit ni kubwa ktk historia ya marekani, vita ya kijinga ya Iraq imepoteza maisha ya marekani mengi na marekani wanalipa dola 10 billion kila mwezi sawa na dhamani ya uchumi mzima wa Tanzania.

  Hivyo Africa tutafika-tuwe na matumaini.

  Frateline

 11. Papin Says:

  Huyu kikongwe anaogopa akiachia uprezident watamsulubu kama wenzake wanavyowasulubu,anachokifanya sasa ni kutaka Kufia madarakani. Ubaya wa viongozi wa Africa hawana huruma na wananchi wao ni ufisadi tuu uliowajaa machoni pao.

 12. Mh Lukamba Says:

  Ni kosa kugawana MADARAKA na tsingarai sijui,na upuuzi mkubwa kwa Kikwete kusimamamia mkataba huu.

  Mugabe AGAWANE madaraka na WANANCHI,maana ndo kipimo cha yeye kuwa raisi,na siyo huyo Tsingarai.

  Anaye mchagua raisi ni mwananchi,alafu unaamua kugawana
  madaraka na mtu tu,mwisho itafikia utagawana madaraka ya nchi hata na girl/boy friend wako so far kwamba we umeshikilia nchi.

  Waafrica tuache huu ujinga,Nilitegemea wana harakati watamkosoa Kikwete kwa hili,kwa kusimamia huu ujinga.
  Hakuna elimu inayoitajiwa kwa suala hili,

 13. Donath Says:

  Not to defend anyone, but i trully believe most of these politicians go into politcs with all the best intetions in mind. But we all know that the only the only thing that does not change is change itself. My view in these matters is not broad but its easy to conclude that power can easily corrupt anyone, even those with the best intetions. It is sad that people like Odinga and Tsvangirai cannot stick to their guns and not be so easily lured by power and money

 14. binti-mzuri Says:

  huyu mzee mwenye sura chachu,akitoka madarakani kama bado kako hai dawa yake moja tu..kumfungulia mashtaka kama zambia ilivyomfanyia chiluba.

 15. hombiz Says:

  Frateline!, mimi sioni sababu yoyote ya kumpongeza Mugabe kwa unachokiita kukubali ku-share madaraka. Hayo sio matakwa yake. Hakukubali yeye kama Mugabe. Hilo ni shinikizo la mafisadi wenzake toka kona nyingine za Afrika. Na baada ya yeye kuona maji yako shingoni, ndio kaamua akubaliane na swala hilo kwakuwa hakuwa na jinsi. Na swala la kuniambia 2028 Afrika itakuwa a better place, hilo mimi siamini hata chembe, hayati Nyerere aliwaambia wazungu maneno hayo hayo unayoyasema wewe mara baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Kumbuka Nyerere aliwataka wazungu warudi Tanganyika baada ya miaka 40 ili waone jinsi Afrika itakavyokuwa imeendelea kuliko walivyoiacha wao(wakoloni). Matokeo yake, miaka 40 baada ya uhuru, Tanzania iliharibika kupita kiasi. Barabara ambazo wazungu waliziacha zikiwa bora kabisa, zote ziliharibika vibaya. Huduma za jamii mbovu sana ktk kila sekta. Usafiri wa reli ndio huo kimeo cha hali ya juu. Mala ubinafsiwe na kupewa wahindi mala longolongo kibao. Makampuni yaliyotaifishwa toka kwa watu binafsi walioitwa mabepari yote yaliishia kufa kutokana na uendeshaji mbovu wa watendaji wa serikali. Nyerere huyo huyo alitumia pesa za kuwalipa wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ktk kupiganisha vita ya Tanzania na Uganda. Tena alitumia pesa hizo kwa siri bila hata ya kuwaeleza wazee hawa ambao mpaka sasa wanahangaika kudai pesa zao. Mbaya zaidi wengine wamekufa bila ya kusiona pesa zao. Na wala sitashangaa wengine wakifia kwenye maandamano ya kudai pesa hizo ambazo huko Kenya na Uganda, wastaafu walishalipwa fedha hizo zamaaaaaaaaaaaaaaaaaaani.Nyerere akatumia pesa nyingi ktk kuimarisha mashushushu wake, jeshi, na usalama wa Taifa ili asije kuletewa rabsha na watu waliopinga maamuzi yake mabovu kama azimio la Arusha na sera za vijiji vya ujamaa na kujitegemea ambazo zilipelekea watu kahamishwa ktk vijiji vyao na kupelekwa kwenye mapori ya kuanzisha vijiji vipya. These people felt like they were in the middle of no where!. Some of them lost their lives because of Nyerere`s crazy self! Na ugoro huu ndio uliopelekea Waziri wa mambo ya ndani wa enzi hizo Mzee Ali Hassan Mwinyi na Afisa usalama Augustin Mrema, kujiuzulu nyadhifa zao.Come on peole! Let`s be realistic about these things! Kupambana na ukoloni hata Mkwawa na Kinjekitile walipambana na wakoloni. Japo hawakushinda lakini they did their best. Afadhali ya hawa kuliko hawa viongozi ambao waliingia madarakani kwa njia ya kuikomboa Afrika na baadae wakageuka na kuanza kuikomoa Afrika. Na mpaka sasa bado wanaendelea kufanya hivyo. Halafu unasikia raisi mstaafu Mkapa ambaye ana makashfa kibao eti anawaomba watanzania waache kuongelea maovu yake na badala yake wasali na ili kuidumisha upendo amani na utulivu wa tanzania. Upuuzi wao huu wa kuwafanya watanzania wapumbavu kwa kutumia kigezo cha utulivu, upendo na amani, umeshapitwa na wakati. They need to stop this crazy shit and start being responsible for their actions!. This same mess which happens in Tanzania happens everywhere in Afrika. Ujinga huu wautaisha bila ya kila mtu kuwajibika kiadilifu ktk nafasi yake ktk jamii. Mfano mzuri kwa nchi za Afrika ni Botwana nchi ambayo imeonyesha kukuwa kiuchumi kutokana na sera nzuri za kufata maadili mema ya utumishi na kupinga rushwa kwa gharama yoyote ili. Soma zaidi juu ya nchi ya Botwana kwa kubofya hapa: http://governanceblog.worldbank.org/building-good-governance-local-traditions-botswana-s-former-president-diamonds-and-fight-against-cor

 16. hombiz Says:

  tazama comment hii ya accountant mmoja huko South Africa juu ya kun`gatuka kwa Rais Mbeki
  ROBERT KULOBA, 42, ACCOUNTANT, DURBAN
  Why should people think that by changing leaders they will change the economic and social life?

  Millions still support Thabo Mbeki

  Rather, they should understand that Mbeki has tried to hold this country together for a period of 10 years now and so far, so good.

  Things are not so bad!

  Sure Mbeki was about to go anyway.

  Nowhere is it written as law that he will rule South Africa forever. So why the unnecessary hurry? This is typical African behaviour which leads nowhere!

  People from Zuma’s side think there will be a huge change. They are thinking that because they are poor they will soon be rich now.

  When one government leaves and another comes in there is no change. But the belief in the Zuma cocoon is that if Mbeki is removed then they will socially or economically benefit.

  I say to them:

  Maybe it is better the devil you know than the one you don’t.

  If you look at most of Africa – the countries who gained independence in the 1960s, 1970s but then after eight years everything went zig-zag and such a mess.

  People get in and then do what? Are they trying to satisfy their ego or the national interest?

  Mbeki has tried and he is trying. Things cannot be delivered at once. There is a process.

  South Africans are misguided by the ethos of apathy. They suffered a lot and are traumatised and so now they look to the government to provide everything; just folding their hands and sitting back in their locations and doing nothing.

  It is a problem.

  The effects of apartheid cripple us today – the number of skilled workers are very low. Instead foreigners come to do our jobs. The jobs are there but most people haven’t been properly educated and so don’t know how to do them.

  We know that no government can provide everything. Even in Libya, Gaddafi can’t.

  South Africa’s government is constrained by a lot of problems and the masses have to understand that. They have to add to the effort.

  Because people are uneducated, they are vulnerable.

  Mbeki has not brought poverty to our country – he has handled an economy that was in a very bad way and because of him and his policy of Black Economic Empowerment (BEE) it isn’t anymore.

  It is outrageous to hurry him out. There was no need.

  And it could be very dangerous. No-one can promise everything.

  People lust for power but then when they have it, what will they do?

  Even by unconstitutional means?

  They have hidden agendas to fill their bellies and satisfy their stomachs.

 17. mwwakahajo Says:

  …siku za kuishi kwa mwanadamu alyezaliwa na mwanamke wala si nyingi…. ila nashangaa sana why Mugabe with all oldness+maubaya yake+kiburi na kila kitu kibaya bado Mungu amempa maisha..! sijasahau hili dubwana lilipooa secretary wake,siyo kwamba walianzia hapo ni kwamba alikuwa akizini na huyo sec. kwa muda mrefu,mkewe alipokufa akahalalisha! lina historia mbaya muda mrefu ni vile tu mambo mengi yanafichwa… Mimi namshauri mugabe akumbuke kwamba kuna Mungu,na amheshimu na kumwogopa…maana amedhihirisha kwamba hakuna mwanadamu anayemwogopa sote tunajua. ebu Mugabe wakati siku zako zikielekea ukingon tufanyie kitu kimoja kitakachotusahaulisha ubaya wako!umeumbwaje wewe? kweli shetani siyo lazima awe na pembe, anaweza hata kuvaa suti na miwani!

 18. Amina Says:

  kibiriti billioni moja,chai milioni 3 hotelini,pipi lako tano shilingi ..hahahhahhaha

 19. Amina Says:

  kwani ni lazima useme unatoka finland?maana kila ninaposoma post hi guys kutoka helinski finland…makubwa

 20. BLACKMANNEN Says:

  Hapa sipaachi bila ya kutoa cheche zangu, maana ni patamu sana!!!!

  I’ll Be Back…….This Is Black=Blackmannen

 21. BLACKMANNEN Says:

  “There wil be no majority rule in Rhodesia”. Maneno haya ambayo hayakukanushwa na wala kukemewa na Uingereza wala USA, yalisemwa na kiongozi wa Rhodesia Ian Smith wakati ule – 1974, (Sasa Zimbabwe). Maneno haya niliyanyaka katika magazini ya “The Drum”, 1974, yalinithibitishia jinsi gani wakoloni hawakuwa na mpango wa kuipa uhuru wake Rhodesia (Zimbabwe).

  Waingereza na Wamarekani wakati huo wakiwa katika hali ngumu ya kuyaelewa mapinduzi ya Afrika Kusini yaliyokuwa yamepamba moto chini ya ANC na Jeshi lake la “Enkondo We Sizwe” na Redio yao ya Ukombozi iliyokuwa ikirusha matangazo yake kutoka Radio Tanzania Dar es salaam, vyote viliwaumiza vichwa vyao na kuamua kutoa “Uhuru” wa Zimbabwe kwa kuwekeana makubaliano ya “Lancaster”,

  Mkataba wa “Lancaster” ilikuwa janja ya Waingereza wa kuvuta wakati ili, kusubiri kuona kitakachotokea Afrika Kusini baada ya Waafrika wa huko kushika madaraka ya nchi hiyo, na kama Afrika Kusini, ingekuwa na mwelekeo kama huo huko Zimbabwe. Lakini baada ya kuona mwelekeo wa kisiasa wa Afrika Kusini haukuwa kama ulivyotegemewa na wengi, Waingereza walianza kuupindisha mkata wa Lancaster huko Zimbabwe. Kwa vile sipendi kuandika mengi juu ya hili, naona nizumnguzie jambo letu la Mugabe na Tsvangarai.

  Makubaliano ya watu hawa ni aibu kubwa sana kwa sisi wanamapinduzi wa Afrika na watetea haki za watu weusi duniani. Kijana Tsvangarai ni kibaraka wa watu weupe wanaotumia upeo wake mdogo wa kuelewa mambo, na pia weupe hawa, wanatumia tekinojia yao kubwa ya mawasiliano, kuwarubuni kwa njia ya redio wananchi wengi wa vijijini, kwa kutumia lugha za wananchi hao, katika kuwapa habari za kupotosha juu ya mambo halisi juu ya nchi yao ya Zimbabwe na Viongozi wake na makubaliano ya Lancaster.

  Makosa yalikuwapo pia kwa viongozi wa Zimbabwe katika kubweteka kwao na ahadi za uongo walizopewa, walizokuwa wakizilalia milango wazi kwa muda wote wa utawala wao. Lakini hata hivyo sasa nimefurahi kuona kuwa wameamka japo wamechelewa, sasa watakuwa na kazi ya ziada kuinasua Zimbabwe hapo ilipo sasa, maana watakuwa wakila meza moja na adui yao.

  Mungu Ibariki Afrika!

  This Is Black=Blackmannen

 22. BLACKMANNEN Says:

  BC, wengi ya watu waliotoa maoni yao hapo juu, ni vijana wetu wadogo wasioijua historia nzima ya “Ukombozi wa Afrika”, wanarukia mambo ya Haki za Binadamu na utawala Bora katika nchi za Afrika bila kufahamu kuwa waimba nyimbo hizo ambao ni Wazungu wa Uingereza na Marekani , wanasema hayo kwa katika nchi za Afrika kwa manufaa yao.

  Nchi zetu za Afrika Tanzania ikiwa mojawapo hatukuhitaji vyama vingi vya siasa. Lakini, ili kuwaridhisha vibweka hao, tuliridhia Tanzania kuwa na vyama vingi vya siasa.

  Mbwa hawa, wapinga maendeleo ya Afrika wanawanunua ndugu zetu (Vyama vya Upinzani) ili wavuruge Amani ya Afrika. Angalia DRC, Kenya, Zimbambwe, Afrika Kusini na Mozambique, na hata Tanzania yenyewe.

  Hayan yote ilikuwa ni kuuyumbisha Uhuru wa Mwafrika na kuurudisha katika mikono yao ya Ukoloni – kwasasa unaitwa “Ukoloni Mambo Leo”.

  Mashujaa wetu wa Ukombozi wa Afrika Mwl. J.K Nyerere, Kwame Nkrumah, Nasser, Samora Macheli, Abeid Aman Karume na wengine wengi, kama wangekuwepo leo hii wasingeyakubali maneno ya wakoloni hawa ya vyama vingi.

  Tuwe makini, kwa kuyatafakali kwa undani matakwa ya wenzetu hawa weupe , kwa kile wanachokitaka sisi tukifanye kabla ya kurukia bila fikra.

  This Is Black=Blackmannen


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s