BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MPENZI LUTA- MAQUIS ORIGINAL September, 18, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:05 PM

Mwisho wa wiki maarufu kama wikiendi ndio ushapiga tena hodi.Lakini kwa sababu wengi tupo kwenye mfungo wa Ramadhan,mwisho wa wiki bado unakuwa umepooza.Inaeleweka,ni mwezi wa toba!

Pamoja na hayo zipo jadi ambazo hazina budi kuendelezwa.Mojawapo ni hii ya kupata burudani kidogo kupitia hapa BC.Ni wakati wa Zilipendwa,wakati wa kukumbushana kwamba muziki ni ujumbe,muziki ni mpangilio wa vyombo vya muziki na sio kelele zisizo na mpangilio.Ni wakati wa mawaidha kupitia burudani ya muziki.

Leo tunao Maquis Original.Bendi hii ilikuwa na makao yake makuu pale ilipokuwa Lang’ata Social Hall-Kinondoni jijini Dar-es-salaam.Lakini Maquis Original haikuanzia nchini Tanzania bali huko Mashariki mwa iliyokuwa Zaire katika mji wa Lubumbashi mnamo mwaka 1970.Miongoni mwa wanamuziki waanzilishi wa bendi hii ni kama vile Mbuya Makonga “Adios”, Tshimanga Asosa na mwanamuziki anayetumikia kifungo cha maisha hivi sasa,Nguza Mbangu “Viking”.

Wimbo wa leo unaitwa Mpenzi Luta.Hapa unaweza kusikia vizuri gitaa la Nguza.Mtindo wa Maquis wakati huu ulikuwa unaitwa Zembwela.Kama utakumbuka Maquis waliwahi pia kuwa na mitindo kama Kamanyola bila jasho,Ogelea Piga Mbizi nk.Sikiliza kwa makini ujumbe uliomo katika wimbo huu.Pata burudani.Ijumaa Njema.Wikiendi Njema

Okay na vijana wa juzi sijawasahau.Unakikumbuka hiki kitu?Bobby hawa jamaa bado wapo kwenye muziki hapo Bondeni?Sikiliza

Advertisements
 

28 Responses to “MPENZI LUTA- MAQUIS ORIGINAL”

 1. Mama wa Kichagga Says:

  Mimi chichemi le Jeff! Nachek TUU HAHAA

 2. Classic Show Says:

  Mwanamziki ngwiji mpiga Gitaa la Solo wa ex.Maquis Original ya mjini Dar-Es-Salaam Kahanga Dekula”Maestro Vumbi”
  Anatarajia kuwasili Dar tarehe 02.Oktoba kwa mwaliko wa Kampuni Clouds Ent. ya mr.Joseph Kusaga kwa Show “Classic”.
  Maestro Vumbi ataungana na mangwiji wenzake akina Kanku Kelly,Tshimanga Assosa,Mafumu Bilali,Keppy Kiombile…n.k
  na kutoa Burudani hiyo tarehe 10-11. Oktoba 2008 katika Ukumbi wa Police Officers Messe Osterbay Dar-Es-Salaam.
  Maestro anatajia kufurahisha wapenzi wake na mitindo mipya naya zamani; Kamanyola,Ogelea piga mbizi,Zembwela,
  Sendemaa,Washa-Washa,Sultan Qaboos na uzinduzi wa CD yake mpya”RUMALIZA”.kaa chonjo… mcheza kwao utunzwa.

 3. mkandarasi Says:

  Mwenye habari za uhakika kuhusu waliko wakina Nguza na wanae kwa hivi sasa tafadhali naomba aweke hadharani hapa kupitia Bongo Celebrity.Kama bado yuko jela ni jela gani.Na kuna utaratibu gani wa kwenda kumtembelea.Mimi ni mmoja wa wapenzi wake wakubwa wa muziki hapa nchini.Yeye na familia yake kutokuwepo katika fani ya muziki kunaniuma sana.Much as I sympathise with the Nguza Family!Nisaidieni jamani.Hakuna Kosa au siyo?

 4. matty Says:

  hapo sawa!!! kama kawa bila mziki no wknd!! hiyo ipo daima aiseee!
  Wknd njema WADAU WA BC wote na wewe mwenyewe JEFF!!

 5. halima Says:

  Mhhh!!!!!!!!!!!

 6. binti-mzuri Says:

  watu wengine bwana..kinawauma ngusa viking kutokuwepo mtaani,what about the kids who have lost their virginities to the rapist?wao ndo tusemeje. E bwana e, May you Perish Nguza Viking and your clan huko segerea..maana mi nikikuona mtaani,nakuvisha tairi la moto.

  Thanks for the music once again.. enjoy the weekend yall

 7. Edwin NDAKI Says:

  Matty mambo vipi? KWA DANI KAMA kawa mida mida ila mi nitachelewa kidogo .Vipi baada ya hapo wapi sasa.

  wadau wote nawatakia ijumaa njema.

  GERVAS mi nawahi magorombe..

  TUTAFIKA TU

 8. TEACHER-DENMARK Says:

  Ahaaa jamani umenikumbusha mbaliiiiiiiiiiii nikoshule ya msingi nimewakumbuka pia ambao hawako duniani nilioishi nao kama jirani na marafiki ….maisha mara moja

 9. Dullah Says:

  Hapo BC Mmcheza, maana nilijua mmeishiwa. Thanks a lot and God bless BC.

 10. Mswahilina Says:

  Asante kwa kutukumbushia ujana wetu mkuu BC (Jeff) kwa wimbo wa “Mpenzi Luta”

 11. Semeni wananchi, I know I have been missing in action the last few days… hope each and everyone of you had a fabulous weekend.. I know I did!!;-) ..na sherehe bado inaendelea.. after all, b’days come but one a year 😀

  Salamu kwa wadau, Edo, Matty, Binti-Mzuri, Matty, Mama wa Kichagga, Blackmannen na wengineo wote!!

 12. DEVOTA Says:

  Yaani jamani mambo ya bongo ni mswano tu wikiend ikifika si mchezo enzi hizo za mpenzi luta lakini kwa sasa wimbo unawika wiki mbili tu maneno kwisha

 13. hombiz Says:

  Nguza kama kweli ulifanya mchezo mchafu unastahiri adhabu hiyo( reap what you sow. Lakini kama uliuziwa kesi kwakweli waliokufanyia kitu hiyo mbaya need to rot in hell!

 14. Matty Says:

  Edwin Ndaki aaaah wewe nae na mfungo huu ndugu yangu kwa Dan au unataka kunifungulisha???
  Thanx Nalitolela .P.S kwa salamu, halafu kuna Matty wangapi hapa BC naona umetuorodhesha wawili…..hahhahahahaha ila mimi ndo dada yenu Matty originaliiiiiiiiiii
  Tutafika!

 15. Amina Says:

  Jamani msinikumbushe papii naweza kulia nilikua nampenda sana kati ya wazsaire wote wa hapa bongo..matty nimerudi

 16. Jamal Says:

  binti-mzuri kila siku huwa nakwambia hufikirii wala hujui mambo yanavyoenda mjini, we ni wapi wewe ha?

  kwa faida yako
  Nguza na familia yake hawakubaka chochote ni ishu ya kupika tu ili wajingawajinga kama wewe mfikirie hivyo.

  “Mbabe akitaka kupita mpishe…” hiyo ndo formula ya maisha hapa bongo, ukikiuka hiyo yatakukuta yaliyowakuta wakina NGUZA.

 17. Matty Says:

  Amina shosti wangu welcome back!!Mony hajambo?umemsikia Jamal alivyosema?

 18. binti-mzuri Says:

  Jamal na wewe umeyajua hayo kwakua ni mkuu wa kitengo cha upelelezi au???

 19. Jamal Says:

  binti-mzuri Hayo ni mambo madogo sana kwangu na kwa mtu ambae ni mwanaharakati.

  Inavyoonyesha wewe umekalia kuangalia tamthilia tu lakini hujishughulishi nakujua wapi jamii yetu inapoelekea…

  ooops i fill sory for you pretie.

  “THAT IS THE FACT” one more thing utapoanza kujihusisha na mambo ya kijamii TAFADHALI usigushe isue za wakubwa wako wa nchi SAWA?

  Enjoy!

 20. Sultan Says:

  Jamal Niko pamoja na wewe!!
  Nilikuwa sifikirii kama kunaweza kupatikana watu wenye upeo na wanaharakati wasema ukweli kama wewe hivi sasa hapa Tanzania!! Muulize huyo anayejiita Binti Mzuri yeye alikuwepo wakati hao watoto wanabakwa??!! ama shahidi yoyote aliyekuwepo alichukua hatua gani??!! Na mwalimu ambaye nae alihusika katika issue hiyo ilikuwaje akaachiwa huru??!! Asifungwe hata mwezi mmoja??!! Hakimu aliyehukumu ile kesi amemfuatilia kujua yupo wapi?? na Kwanini amestaafu??
  Kwa wasiofahamu maisha ya Nguza pale kwake kila siku hawapungui wageni zaidi ya 20 mchana, na ndio muda ambao kosa linakisiwa kufanyika licha ya wageni kuna bendi yake mwenyewe ambayo hufanyia mazoezi hapo! Mwanae mmoja Nguza yule Mbangu wa kwanza wa kiume huwa haishi pale(amepanga). Papii huwa hata hashindi pale sababu pia yeye na kaka yake walikuwa bendi nyingine ya FM Academia. Kuanzia kubanwa na shughuli za bendi yao mpaka shughuli zao binafsi na mambo mengine ilikuwa ni vigumu kuja nyumbani kwao na kumkuta Papii yupo pale(pia alikuwa Solo artist), kwake ilikuwa ni heri akakae kijiweni na marafiki kuliko kushinda nyumbani. Tatu kwa ufafanuzi zaidi, mimi nijirani pale kwao na wakati matatizo yanatokea Mimi nilikuwa Nairobi na Papii alikuwa Arusha na fiesta nilikuwa nikiwasiliana nae.
  Nakumbuka Papii alikuwa akijua kwamba Baba na kaka yake wameshikwa lakini alikuwa hajui sababu nini nadhani angejua kwamba alikuwa ni mkosaji asingejisumbua kurudi Dar! Angetorokea hata Nairobi kwenda Congo! Tulikuwa tukiwasiliana nae mara kwa mara. Matatizo humkuta kila mtu na huwezi kujua ni yapi yatakayo kukuta na ni kwa muda gani yatakujia! Kwa kukusaidia kaka Jamal mjinga huwa hajijui kama yeye ni mjinga! Kwahiyo akiropoka kitu asichokijua muache aendelee na ujinga wake. Mimi ninachosema pale sio mwisho wa ile kesi hukumu ipo tu na Mungu ndio atatoa hukumu ya haki. Ningemfafanulia huyo binti vizuri kama alikuwa mtu anataka kujua lakini sababu anamdomo mchafu wacha aendelee na domo lake alafu tuangalie kama litamsaidia. Sijui hata kama shule ameenda maana IQ yake inaonyesha anaupeo mdogo sana wakufikiri. Nikama ulivyosema Mr. Jamal huyo dada akisha shiba basi yeye ni tamthilia tu za fulani kampenda fulani zimemjaa kichwani.
  Wasalaam.

 21. Matty Says:

  salutations to you guys no. 20 & Jamal habari ndo hiyo!

 22. Jamal Says:

  Nashukuru Sana Bro Sultan

  Nimefarijika sana kujua kumbe kuna watu wenye jicho la tatu kama wewe, infact umeeleza vizuri kutosha kwa mtu mwenye IQ ya kawaida kabisa kuelewa.

  Yani umetumia ushahidi wa kawaida kabisa(wa kimazingira) kufafanua. Mi nachoamini One day else Tutajua Ni nani atoae madaraka, kama Si binadamu basi hakutakuwa mtu awaye yeyote atayeweza kuupindisha ukweli wa mambo. Bila kuzingatia cheo alichonacho au madaraka aliyonayo.

  Nakutakia Heri na Furaha katika sikukuu hii……

  IDD EL-FITRI Nguza n Your Family, We love you!

 23. binti-mzuri Says:

  hahahah .. ebwana mie IQ sifuri Jamal..lakini haka ka IQ kamenipa ka masters bwana,so am not complainin. domo langu chafu,limeniletea familia..matter of fact,am having a nice life and following the LAW…ndio maana nipo hapa relaxed with the fact that nguza viking will perish in jail,and i wont have to worry about him ever attacking my children. that thought itself is enough for me,further details dont interest me… i believe a bunch of 15 7 year-olds than wazee kama nguza viking who had time to sit with their lawyers and make up their stories..from him not being able to have sex,to papii being married etc,SIJUI SIJALI..nyie wapenzi wao ndo mtajijuu..wapelekeeni juisi za machungwa pale segerea waongeze protini..habari ndio hiyo!wako jela..and as long as am alive and theres law in this planet..FOR A VERY LONG TIME.. yessaaaah. yani mibongo iko shalo shalo,no wonder li nchi haliendelei..embu nijitokee mie humukabla sijawa ka nyie … AM OUT KWA NGUVU ZOTE!

 24. Sultan Says:

  Thanx ya all! Matty and Jamal. You need to grow up girl! “TANZANIA KUNA MAFIA HATARI SANA” You ll’ see a lot of things some to come days to prove what I’m saying. Peace & Love.

 25. Sultan Says:

  Sorry I meant you will see a lot things some days to come

 26. Jamal Says:

  kweli binti-mzuri ni KILAZA, aliekuambia masterz inahitaji IQ ni
  nani…..we wa wapi wewe? Em jichek kabla ya kukurupuka na kuropoka….watu au hata hausikii watu wanamasters kwa vyeti feki? N abt Kuwa na amani kwa kufwata sheria..ni nani aliekwambia hiyo ndo formula ya maisha ni nani, do u know that co wote waliopo gerezani ni wakosaji? so what r u talking abt, Mawazo kama hayo ni ya waru wenye AKILI ZA KUSHIKIWA…where ru lady….? Do u really have masters or ur ndo yaleyale ya vyeti FEKI…..?

 27. Jamal Says:

  kweli binti-mzuri ni KILAZA, aliekuambia masterz inahitaji IQ ni
  nani…..we wa wapi wewe? Em jichek kabla ya kukurupuka na kuropoka….hausikii watu wanamasters kwa vyeti feki? N abt Kuwa na amani kwa kufwata sheria..ni nani aliekwambia hiyo ndo formula ya maisha, do u know that co wote waliopo gerezani ni wakosaji? so what r u talking abt, Mawazo kama hayo ni ya watu wenye AKILI ZA KUSHIKIWA…where ru lady….? Do u really have masters or ndo yaleyale ya vyeti FEKI…..?

 28. MASUMBUKO Says:

  Maskini nguza. Pole baba. MUNGU atawajalia. Tunawaombea sana mtoke. ili muendelee kutupa raha.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s