BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JK ZIARANI MAREKANI September, 21, 2008

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 8:09 PM

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini jana (Jumamosi, Septemba 20, 2008) kwenda New York, Marekani, ambako atahudhuria na kuhutubia kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).

Rais amepangiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne ijayo, Septemba 23, 2008 katika nafasi yake pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu, Rais Kikwete amepangiwa kuhudhuria mikutano mingine muhimu kuanzia ule ambao utaangalia Mahitaji ya Maendeleo ya Afrika. Mkutano huo, utajadili ahadi za nchi tajiri kwa Afrika na Maendeleo ya Bara hilo, na kuona ahadi hizo zinatekelezwa namna gani.
Rais pia atahutubia kikao cha ufunguzi cha viongozi ambao watajadili maendeleo ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s). Baada ya kuwa amehutubia kikao hicho, Rais atashiriki katika mijadala kuhusu afya ya Mama na Mtoto, na pia mjadala kuhusu ugonjwa wa Malaria, masuala yote mawili yakiwa sehemu muhimu ya MDG’s.

Ijumaa, Septemba 26, Rais atakwenda mjini Washington, ambako atatoa hotuba muhimu ya ufunguzi kwenye Kikao cha Mwaka cha Wabunge Wenye Asili ya Afrika katika Bunge la Marekani, na pia kuhutubia mkutano wa viongozi wa shughuli za biashara katika Marekani.

Mbali na mikutano ambayo amepangiwa kuhutubia ama kushiriki, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wengi wa shughuli za kisiasa, kibiashara na kiuchumi duniani na katika Marekani.

Miongoni mwa viongozi ambao Rais Kikwete atakutana nao na kufanya mazungumzo nao ni pamoja na Rais wa Iran, Mheshimiwa Ahmedinajad; Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Mheshimiwa Javier Solana; na mfanyabiashara maarufu duniani wa shughuli za kompyuta na teknolojia ya mawasiliano, Bill Gates.

Rais Kikwete pia atakutana na Waziri Mkuu wa Denmark, Mheshimiwa Anders Fogh Rasmussen; na Katibu Mkuu wa Shirika la Kazi Dunia (ILO), Juan Somavia.

Rais Kikwete pia atafanya kikao cha pamoja kati yake, Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon na Makamu wa Rais wa Sudan, Ustaz. Ali Osman kuzungumzia mgogoro wa eneo la Darfur nchini Sudan.

Wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika Sudan mwanzoni mwa mwezi huu, Mwenyekiti huyo wa AU, alimwahidi Rais Omar El Bashir wa Sudan kuwa angefanya kikao kati yake, Katibu Mkuu wa UN, na mwakilishi wa Sudan kuhusu hali ya Darfur wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Kikao hicho kitaangalia jinsi gani ya kuharakisha zoezi la kupeleka askari wa kulinda amani wa UN na AU katika Darfur, na pia jinsi ya kuahirisha, kwa angalau mwaka mmoja, hati ya kukamatwa kwa Rais Bashir iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC).
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Advertisements
 

25 Responses to “JK ZIARANI MAREKANI”

 1. Majita Says:

  …….sijui ataongea nini.Mimi inanipa shida kukimbilia kumpokea Kagame kujiunga na East Africa wakati kesi zoooote za mauaji ya kimbari pale UNICTR Arusha kagame alikuwa anatajwa na kila mtoa ushahidi ama washitakiwa wenyewe kama mhusika namba moja.Mhhh yangu mimi majicho.haya bwn kikwete.Kwa kijita tunasema “Go Kikwete” ila kabla ya go unawela silabi “ye”

 2. jonas Says:

  Rais wetu anafanya kazi nzuri sana kwa ajili ya
  maendeleo ya watu wake safari zake pia zina tija kwa ajili ya manufaa ya wananchi kwa ujumla.Wasiwasi wangu pale baba unapo safiri sana na nyumba kumwachia mama unaweza kukuta watoto wamekuwa manunda na ukaharibu mustkabari wa maisha yao.

 3. MDAU ASWA Says:

  IVI BUSH ANA AJENDA GANI NA KIKWETE.KILA SIKU KIKWETE ANAENDA MAREKAN MBONA NCH ZA ASIA U ULAYA HAKUNA MAMBO AYA.UCHUM UNAJEGWA NA WANANCH WENYEWE NCH ZA ASIA ZILIJUA ILO.NAOMBA RAHIS AWE WAZIRI WA MAMBO YA NJE.WABADILISHANE NA MEMBE.NAMSHAURI KIKWETE ACHUKUE GREEN CARD TUJUE MOJA

 4. Mbarook Says:

  Ukirudi huko, petrol iuzwe elfu 1, diesel 1,200 na mafuta ya taa 500…jk umebakiza miaka 2 tu lkn maisha ndo yanazidi kuwa magumu, umeshindwa kuwashugulikia wahujumu uchumi, migomo katika sekta za serikali zimeongezeka kwa asilia 75% ukilinganisha na awamu ya 3, umeendeleza mikataba mibovu bila kuwashugulikia wahusika. Najua ccm watakupitisha ugombee tena 2010 japo ningefurahi kama ungesema umeshindwa kutuondolea kero zetu na hauwezi kuondoa hata kama ungepewa miaka 20 ili umpishe mwingine mwenye mawazo mapya na ujasiri, panapo majaaliwa maana najua hauna uungwana huo wakunyoosha mikono juu… nisingependa nisikie kauli ya kuomba tena 5yrs ili ukamilishe ahadi zako, Jakaya utachomwa moto siku ya kihama kwa kutupa ahadi hewa, tulikuamini kama tumaini jipya lilikuja kutukomboa lkn ndo kwanza unatuangamiza

 5. RebbyGod Says:

  To much USA’s safari 4 Presidaaaaa!!!!! Am still wondering whats going on between him and Bush!!!!

 6. Ramsfel Says:

  Mwalimu nyerere walikuwa hawamfanyii ubarazuli huu wa kumshika shika mabega wazungu wanasema kuwakiongozi mwezioakikushikamabega ni kukufanya usione mtu wa chini

 7. hombiz Says:

  hawa watu (Bush & Kikwete) hawawakilishi serikali bali siri-kali!

 8. Renee Says:

  Guys!
  This is United Nations General assembly for Africa’s development needs. The best person to attend such meeting is the president of our country, may be if you take interest and visit http://www.un.org you will learn more. Just for your info I quoted this: “The high-level meeting on Africa’s development needs will take place at United Nations headquarters in New York on 22 September 2008. The theme of the meeting is: “Africa’s development needs: state of implementation of various commitments, challenges and the way forward…. In its resolution 62/242, the General Assembly decided that this meeting will be held at the highest possible political level, with the participation of Heads of State or Government, ministers, special representatives”…. etc. etc. Don’t forget JK is also the head of African Union.

  I understand your concern about our president being “the Vasco D…” and frankly speaking I don’t like mr. Pori’s look and petting, it’s diminishing… These two are supposed to be Commanding Chiefs, right? Then why don’t they maintain that stature! Natumai mheshimiwa JK anatumia akili yake anapoongea na hawa majambazi- Being loyal doesn’t work too well when you’re dealing with the capitalist (esp. Americans).

  BC, natumai ujumbe huu utafika kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais. Great job!

 9. trii Says:

  Too much of something is always harmful.

 10. Matty Says:

  mhhh bro punguza kusafiri duuuu daily u & bush!! hv oficin kwako huwaga unapita tu au hata hupapiti???

 11. solange Says:

  mbarook yupo pamoja, jamani maisha yamezidi kuwa magumu hakuna kipya huyu mzee alichokifanya, tabu tabu tupu, safari safari na yeye, hebu tulizana kidogo jamani utatuwe matatizo ya nyumbani kwako kwanza ndio uingie kwa jirani.

 12. Amina Says:

  Haya safri njema

 13. BALTAZAR Says:

  KWELI JK AMEKUWA NA TRIP NYINGI ZA USA TUOMBE MEMA PENGINE AKIRUDI JAMANI ATATUPA HABARI NJEMA HASWA SIE WATU WA UTALIII HAHAHAHA!!!

  MIMI JAMANI I WISH KWENYE TRIP ZA JK NINGEKUWA NA MIMI NA MIMI NAKWENDA KAMA MJASIRIA MALI WA SEKTA YA UTALII HATA NIMWAGE SERA ZA UTALII WETU.

  ILA JK JAMANI ANAPIGA PAMBA HEBU CHEKINI HILO SUTI LAKE NA LA BUSH MPKA TIE HAINA TOFAUTI KABISA.

  CHEERS

 14. Chris Says:

  Huu urafiki wa Vasco da Gama na Bush na hiyo migodi hiyo! Yetu macho! Najua yatafumuka sana atakapoachia madaraka! Tutayasikia tu baadae,tuombe uhai!

 15. wetu Says:

  ameshapewa chake na gorge kichaka ,huyu bwana mheshimiwa,kwa taarifa za chini bush anyo ardhi bongo,na mikataba ya chini kwa chini tayari imeshatiwa ,yaani sisi tulie tu kwani nchi yote imeshauzwa na mwanachi mlala hoi alie tu,ilchobaki sasa watatuuzia mpaka mama zetu wazazi,kweli nyerere alikua na msimamo na nchi yake ,pamoja na makosa yake ,lakini sasa itabidi tumkumbuke…nchi imejaa rushwa na ufisadi wa hali ya juu….kamwe mheshimiwa na wengineo hamtauona ufalme wa mwenyezi mungu kwa dhambi zenu.za kuhijumu tanganyika..hata msali vipi na kutuoa zaka kwenye makanisa na misikiti,mungu hatawasamehe kwa dhambi za kutuzalilisha watanganyika…kheri kutawaliwa na mkoloni kuliko kuongozwa na mtanganyika kwa kero hizi….kamwe kwa binafsi yangu sitampigia kura mtanganyika yoyote katika maisha yangu.unless mitume warudi tena duniani..hakuna mwanasiasa utakae mwamini tanganyika..except nyere na kolimba na sokoine..the rest ni utumbo mtupu..politics of the baboons..guiding monkeys in the jungle….

 16. Pearl Says:

  ndo hivyo tena hata tusemeje ye ndo rais ana power,nyie wote hapa mnapiga kelele tu hamna lolote mtakalobadilisha mpaka hapo kwenye uchaguzi ujao.

  ni rahisi sana kumsema mtu kwa kitu anachofanya na kwa wakati huohuo hata mmoja wetu hapa akipewa hiyo nafasi ya urais hakuna cha ajabu atakachofanya,siku zote watu wanaona mabaya ya mtu na sio mazuri.
  ukifocuss kwenye ubaya wa mtu hata akifanya jambo zuri hutaweza kugundua kwa sababu umezoea kumuona mbaya.
  Kikwete sio mbaya kwa kiwango hicho jamani.

 17. mjomba kaka Says:

  aisee utadhani baba (bush) anamuuliza Mtoto wake (Jk) ‘habari za shule mwanangu?leo mmefundishwa nini shule?’

 18. Mama wa Kichagga Says:

  Hii sasa nahisi ni laani.

  Hivi ni lazima watu tulalamikie kila jambo lipitalo machoni petu? Kwanini badala ya kulalama tusifikirie njia mbadala ya kutatua matatizo yetu?

  Yaani ukiingia humu ni watu kulalamika, kukejeli, kutukana , kudhalilishana nk! Hivi ndivyo mnavyoona inafaa? Hebu kaeni chini na mfikiri kidogo kabla ya kulalama? Jitahidini kujua kazi za Rais na nafasi zake na mjue taratibu za utekelezaji wake, maana kutokujua nako ni taabu nyingine!

  Ukipita huku mara Angela kakataa taji, mara Latoya kakuabisha (kwani ulimtuma?), mara rais kakunyima sijui chakula khaaaaaaa wacheni ujinga na tumieni akili na mjikomboe.

  Nani alikuambia mtawala au MTU FULANI anayetaka kutimiza malengo yake atakutoa kwenye umaskini kama sio juhudi zako? Au ndiyo mambo ya njia za mikatokato hazilipi? Tumia akili zaidi ngudu yangu.

  NARUIA WATU tuBADILISHE MITAZAMO YETU NA NAMNA YA KUFIKIRI. TUPANGENI MIKAKATI NA TUIWAJIBIKIE TUONE KAMA MAISHA HAYATABADILIKA.

  Pia TUKUMBUKE kuwa midomo yetu italiinua ama kuangamiza taifa maana “Midomo huumba”, tukijinenea wema tutavuna mema na tukijinenea mabaya tutapewa mabaya na ziada.

  Tujifunze kuongea na kushauri mazuri ili tuweze kufanikiwa kwani mara nyingi sana hata mtoto anayefeli shuleni ukimuandama sana ujue ndio unamuharibia zaidi ila ukimpa moyo na mbinu mbadala za kujifunza hubadilika na kufanya vizuri zaidi ya hata wenzake darasani.

  TUJIFUNZENI KUWAELEWA NA KUWAHESHIMU WENZETU KAMA WALIVYO MAANA TUNATOFAUTIANA KIMTIZAMO, KUFIKIRI NA HATA KIUTENDAJI.

  USIENEZE SUMU, ENEZA UPENDO. TUTAFIKA TUU.

 19. Matty Says:

  Ndio mwanasiasa mkereketwa sema usikike hahahahahahha litakayemchoma ndo yeye na limemgusa!!
  swali langu bado liko pale pale oficn bro hakai??

 20. binti-mzuri Says:

  haya mtalii, niletee zawadi

 21. Malikville Says:

  Mzee mkubwa ni ajiulize lini marekani alikua na rafiki wa kudumu?

  Kaa chonjo mzee mkubwa baada ya kukutumia na kupata wanachokitaka hubadilika hao mabwana. Na mifano iko dhahiri.

  Take care!

 22. mwwakahajo Says:

  nakuunga mkono MDAU ASWA, Its now too much!!! i think there must be something cooking around!!

 23. Olive Says:

  Tehe tehe tehe tehe tehe tehe………. First World and Third World,wachina tunalala nao tandale…….!

  Kazi kweli kweli

 24. Mtu Says:

  AIBU, AIBU

  Ondoeni hiyo picha. Bush anamwangalia Rais kama mtoto aliyeanguka. AIBU, AIBU. I would say to the president, don´t go there again!

 25. TIANDRA JONES Says:

  JAMANI BUSH NI MFANYA BIASHARA NA HAPO AKIRETIRE TUU . MTAMWONA SANA TANZANIA . OBAMA HANA TOFAUTI NA WATANZANIA WALIOZANI KIKWETE ATAWASAIDIA AKIWA RAISI MKIPGA KURA MSIANGALIE SURA MARA BOYS TWO MEN , MARA MREFU . CABINET YOTE NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WAMESOMA NA KIKWETE DARASA MOJA AU MWAKA MMOJA NYUMA AY MBELE THATS IT . NENDA CHUO KIKUU CHA DARESAALAAM TAFUTA LIST YA WATU WALIOMALIZA 1975 NA 1974 UTALIA MANAAKE WAMEJAZANA NA KUENDELEA . WAANDISHA WA HABARI MTAENDELEA KUPEWA RISHWA NA HAMTO FANYA UCHUNGUZI POLENI SANA NA MSIOMBE RAISI AJAE AWE MWANDOSYA MTALIA MAANA YAKE . WALEWALE MTAWAONA.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s