BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

LATOYA NJE YA BIG BROTHER AFRICA! September, 21, 2008

Filed under: Burudani — bongocelebrity @ 8:12 PM

Mwakilishi wa Tanzania katika shindano maarufu la Big Brother Africa,Latoya, amekuwa mshiriki wa kwanza kuondolewa ndani ya jumba la Big Brother Africa!Kwa maana hiyo Tanzania safari hii imeambulia patupu baada ya kuonekana kuwa tishio katika misimu miwili iliyopita ya shindano hilo.Kama mtakumbuka Mwisho aliibuka mshind wa pili na Richard akaibuka namba moja.

Nini kimetokea?Unadhani kwanini Latoya ameishia hapa?Kuna yepi ambayo Mwisho Mwampamba na Richard Bezuidehout waliyafanya ambayo Latoya hakuyazingatia?Mjadala u-wazi.

Advertisements
 

123 Responses to “LATOYA NJE YA BIG BROTHER AFRICA!”

 1. Some more Says:

  Nilijua…..nilijua tu,M-net wa Tanzania mmepeleka kachangu,yani nimereka kweli.Unajua next time ni lazima muangalie watu wa kuwapeleka sio lazima wanaume kila siku hata wanawake lakini wenye upeo si kwenda kulala na kila mtu.Yani huyu binti siku niliyosikia kachaguliwa kwenda kutuwakilisha watz niukajua ni shoti hebu muangalie kwanza sijui atakuja kutupa sababu gani manake saa hizi kama namuona anatunga sababu za kuja kutupa me naomba kama utapitia hii BC usije na sababu wewe kaa kimya na wala huji kupokewa labda familia yako tu.Yani wewe binti umeharibu jina kabisa yani itaonekana kuwa Tanzania hatuna wanawake ambao wanasifa ya kutuwakilisha kumbe wako wengi tu ila ni UMAPEPE,USHAMBA,UMUCH KNOW na mengine yani naishiwa hata na maneno.Jamani mabinti wenye sifa jitokezeni next time muende ili mkasafishe jina sio kama huyu aliyeenda kutoa nuksi.I wish ningekuwa karibu yani.BC naomba kuwakilisha

 2. Some more Says:

  mnaomba nafasi na mnapopata hamjui kuzitumia ipasavyo liangalie kwanza alijua angekuwa kama Tatiana kumbe aaahh wapiiii umeula wa chuya na mawe kwa kwa kujifanya unajua.Pole Seven na crew yako nzima ya Mnet kwa kupeleka hasara manake amewatia aibu

 3. Majita Says:

  Mmmmh hapa sitii neno.inawezekana kuna mambo mawili.Ila jambo kubwa ni kuwa,kama Richard alikuwa mshindi kisa alipigilia misumari watoto wa wenzake na mwisho nae alikuwa mshindi wa 2 kwa tabia kama ya Richard basi tuseme kuwa huyu binti kashindwa kwa sababu hakataka kuwa na Tabnia kama za waliomtangulia.hahahahahahahaha.Matty vipi??

 4. ISMA KABENGO Says:

  VERY LAZY,NO BRAIN,

 5. samata Says:

  Tatizo la Tanzania ni haka ka ugonjwa kanakoitwa ’50/50 JINSIA’. Najua multichoice hawakuchagua mtu kulingana na sifa bali safari hii walisema tupate mwakilishi mwanamke.
  Si unasikia hata mambo yanayoendelea eti mjadala wa uwakilishi!!!
  Nina hakika akina Lucy kihwelu wakati huo waliamua au walipata shinikizo lazima aende mwananmke kutoa nafasi sawa. Mimi nasema kama mwanamke ana uwezo apewe na kama ni mwanaume apewe. lakini si kuchagua mtu amabye from day one wana BC walisita sana.
  Haya sasa kaenda kufanya madudu aibu tupu.

 6. raphael Says:

  Hata mimi nilijua tuu tangu mwanzo aliingia na mapepe ya manzese uwanja wa fisi sasa matokeo yake ndio hayo nimejitahidi kumtetea huko kwenye forum ili kubadilisha mawazo ya watu nimetukanwa mpaka nimekoma ila haikusaidia maana alishaharibu ameingia na bad strategy alitakiwa awe mwenyewe sio kuiga watu nilimpenda tabia yake ya kumind her own business na alikuwa hana wivu ila kitendo cha yeye kuwachanganya wale wanaume kwa muda mfupi ndio hicho kimemuharibia sasa ana majina kibao, bitchy, slut yote hayo ni yeye but all in all watanzania tunatakiwa kukumbuka kuwa hii ni game na haikuwa bahati yetu this season so msimseme sana ingawaje kachemsha but sasa atajifunza na wengine watajifunza kupitia kwake na I hope my friend Seven hajawa too much disappointed, take it easy gal next time uwe makini kutafuta mwakilishi kwenye game kubwa kama hiyo. I will have more to talk now am sad for wht happed, I lv the game bt now the appetite is gone b’se mwakilishi wangu katolewa ni mapema sana anyway its a game and I tell you I will make sure Mimi na Lucille their Next they gossiper na walikuwa hawampendi Toya na their big pretenders and backstabbers, they have to start packing their things vry soon, see ya’ guys in forum

 7. hellen Says:

  yaani mimi toka mwanzo tu nilijuwa mwaka huu atuna kitu jamani m net yani katika wale wote mliona huyu dada ndo anawafaa jamani ametutia aibu sana yani jana nilikuwa natamani nipasue tv kwa sababu alikuwa anatukera sana kaenda kuboronga tu uko .mshamba kweli tena ana ataaibu eti najuwa nimeshakuwa super star kwaiyo yeye alichotaka nikutoka nakuwa mtu maarufu .mjinga kweli tena umetuaibisha ma dem wabongo tu naonekana wahuni tu

 8. kekue Says:

  Kyeleuwiiii maskini dd yetu, no msimlaumu sn coz aliona style aloingia nayo ingemfikisha mbali, maskini ya mungu anyway haya njoo uendelee kuuza vipuri !!!!!!!!!!!!!!!

 9. Matty Says:

  Heee ngoja waosha vinywa wafanye kazi yao!karibu home Latoya ulichetuka sana huko south shosti lol!

 10. Pwagu. Says:

  Nimefurahi sana kusikia umetolewa, nilikuwa naona aibu sana nilipokuwa naangalia, ulianza moto sana, siku uliyovua nguo ndio ulinichefua kabisa, nikasema lazima tukupingie kula za kutoka.

  Hv nyie M-net mnataka kutuambia ni hao machotara tu ndio wana sifa ya kushiriki hiro shindano lenu, kwani ni kasoro gani mmeiona kwa sisi mandingo. achani kutunyanyapaa nyie mnachangua machotara wenu harafu mnaanza kutuhamasisha mandigo tupige kula.

 11. mkereketwa Says:

  Kwa kweli binti huyu ametutia aibu watanzania, tabia alizokuwa anazionyesha kwenye jumbe hilo hasa mimi ilinisikitisha, tatizo ni kwamba wengi wa wao wanaiga tabia za mtu fulani fulani ambazo hazipendezi. Umetuangusha mno sijui utakuja kusema nini kwa watanzania. Hatutahitaji uongo wakutueleza. Hata hivyo tunashukuru kwa kutolewa kwa maana ungeliaibisha taifa na matendo yako kwenye Jumba.

 12. jonas Says:

  Huyu binti ametia aibu sana yaani yeye alifikiri
  mchezo huu ni mapenzi tu.Anagalia sasa anarudi mapema aibu tupu watu sasa hivi hawahusudishi mambo yake ndo maana katoka mapema asiendelee kutia iabu.Hii pia ni fundisho kwa washiriki wengine wafahamu kwamba mchezo huu hauhusishi mambo ya ngono tu bali unaangalia tabia yako na utashi wako kama wewe ni binadamu jinsi unavyo jitofautisha na wanyama!

 13. naj Says:

  mi nashaangaa wa tz wanapopiga kura kumchagua mtu sijui wanakuwa usingizini huyu latoya hafai na hatofaa kwenye lolote mbona wanawake wenye sifa wapo wangechaguliwa tunalitia doa baya jina letu TANZANIA….hafai hata kwa kidole bora hata alivyotolewaa maana angezidi kutuaibisha

 14. lijenga Says:

  Yaani hapa hata la kusema sina huya mdada kavuna alichopanda,nahisi alikuwa anatafuta umaarufu akidhania umapepe unalipa kumbe kaingia mkenge,pole sana kwa washauri wake waliomwongopea kama angewza kuwa kama Tatiana,ametutia haibu sana b,bora basi angekuwa hata na katabia kazuri,bora arudi akajichimbie zake huko Arusha na akajibu mashtaka ya boy frind wake,namtakia safari njema ya kurejea nyumbani,amekipata alichovuna.

 15. ally sabu Says:

  tusimlaumu sana haya ni kama mashindano so kuna kushindwa na kushinda.na wala tusitumie jinsia yake kumdhalilisha eti kisa wanaume walifanya vizuri.kama kuwa na wapenzi hata mwisho na richard pia nao walikuwa na wapenzi..tusitegemee kila leo sisi tutakuwa washindi tu

 16. ann Says:

  evyone deserve a chance na latoya amepata chance kaitumia vilivyo.wivu wa baadhi ya nchi kuona kua watz tunafanya well zaidi yao na kwakweli lato angeingia final 2ngeshinda tu kwanza she is so talent na alipotolewa na kuwekwa ktk another house big brother ilikua sinaboa.ok na hao watakua majirani zetu tu apo coz always wanafanya maloloso tu.ok lato upo ktka new lne nw. big up tanzania

 17. hiki kibinti kichangu nani alimwambia kufanya ngono ovyo ovyo ndio ushindi .lkn huku kuchaguana kwa kujuana mpaka lini? naamini wasichana wenye vipaji wapo msiangalie huyu mtoto wa fulani. atasema sababu gani?au atasema maandalizi mabovu .oooo wanawake hatuthaminiwi namna hii nani atawathamini au nani atakubali kupata hasara next time angalieni watu wa kuwapeleka habari ndio hiyooooooooo

 18. Laura Says:

  Nimeona bora atoke tu, sababu angeendelea kubaki BBA House, tungezidi kupata aibu, kwani aibu si kwake tu ni kwetu sote wasichana wa kitz, maana yeye alifanya mambo kwa kutaka umaarufu wa haraka haraka, angesoma watu walivyo kwanza, kuchangamka kungefuatia, mfano mzuri ni bint wa kinamibia Lucille, alikuwa kama anabore mwanzoni kumbe alikuwa anasomea watu, sasa yupo okay na anavutia, mdogo wetu Latoya umaarufu wa haraka hauji kwa kujishaua kwa wanaume, na kuvua kuvua nguo si maadili ya wasichana wa bongo, sister seven next tym wapeni maadili kwanza utanzania wetu usiabishwe na wasichana wachache, kuwa nawapenzi wawili nyumba moja kwa msichana ni jinsi gani hana heshima dada Latoya, ULitutia hasira sana, umetoka mapema bora kuepusha mengine, maana ungeenda paint house na sijui Rico au Morris ungeachia LIVE!!! Karibu Home!!!!!

 19. DEVOTA Says:

  Hi jamani haya yanawezakutokea popote pale kwani hawo waliotoka mwanzo miaka iliyopita si ni watu kama latoya?

  Kwanaz tushukuru mungu tanzania kuwa kwenye top 3 miaka iliyopita this is like a game kuna kushinda na kushindwa

  ni hayo tu kwa leo

 20. naila Says:

  siku ya kwanza alivyoingia nikaona mh!hapa sijui!she was too atifisho,trying so hard,mjuzi mshamba!shangu si changu basi hata sikuweza kulelwa ni kitu gani!
  ati” i wanted to be famous” femasi my foot!

 21. Hivi we Latoya umekulia Arusha au Machame? Cos mabint wa Arusha hatuna tabia hizo.Mi nahisi ulidhani bado upo nyumbani kwa mzee Lyakurwa.Mule ni BIG BROTHER HOUSE AND PEOPLE ARE THERE ONLY FOR THE BIG DON na sio kwa umaarufu wa kijinga kama ulio taka wewe.Inaonyesha ni jinsi gani hauna malengo ila umetawaliwa na ushamba. HUFAI KABISA NA USIPENDE KUIGAAAAAAAAAA!

 22. sellanda Says:

  Ndugu some more laiti kama latoya angekuwa ameshinda basi wewe ndio ungekuwa wa kwanza kumpongeza lakini kwa sababu ameshindwa lazima umponde. Mimi sijaona baya lolote alilofanya latoya hayo ni matokeo wewe ulitegemea kila siku tanzania ndio washinde ina maana hao wengine hawataki kushinda?

 23. Hassana Says:

  Huwezi amini, mimi nilikua ni mmoja kati ya watu waliokua na hamu ya kumtoa yule binti.
  Jamani alishaanza kunichefua.
  Alizidi kujirahisisha.
  Bora ametoka mapema.

 24. Bob Sambeke Says:

  BORA KATOLEWA MAPEMA MAANA ALISHAANZA KUALIBU MARA KAMCHUKUA HUYU MARA YULE! AFADHARI ANGETUAIBISHA SANA KWA MAMBO YAKE YA KUPENDA NGONO BORA WALIVYO MTOA MTOTO KICHECHE SANA HUYU.NA WANAOPITISHA AHO WA2 HUKU KWETU PELEKENI WATU AMBAO WANAJUA WANAFANYA NINI CO MNAPEKEKA MALIMBUKENI! NDIO MAANA KAENDA KUTUAIBISHA TU! SHAME ON HER!

 25. Pandu Says:

  Du! maana sijui nianzie wapi. Mimi naona akirudi asitoe sababu yeyote zaidi ya kutuomba radhi wadanganyika kwa uwakilishi wake mbovu usio na tija. Watu wamemmega harafu katoka patupu…na nyie multi choice japo lucy kihwele amesepa ili msala huu usimkumbe, lengo lenu la kumpeleka huyu mama huruma ilikuwa kuweka usawa flani kijinsia lkn choice ilikuwa mbovu kupita maelezo na nyie mtuombe radhi kwa kutuchagulia kimeo, sijamind walivyomtoa ila nimemind alivyokuwa akigawa uroda kwa kufikiri ndo njia pekee ya kumsongesha mbele kumbe sivyo.

 26. nice2 Says:

  Mnamlaumu dada wa watu bure, alikua anajaribu kuchangamsha tu na kutoka imekua ni bahati mbaya kwa sababu nchi zote zilimpigia kura kwa ajili ya wivu juu ya Tanzania tu, wala msitake kumshambulia dada wa watu bureee, muacheni!!! angekuja na hela hapa wote mngemchekea, lakini kwa ajili ametolewa wa kwanza mnajifanya kumponda, watanzania bwana!

 27. Bennie Says:

  Hakuna kitu kibaya katika maisha kama kuishi maisha yasiyo ya kwako yaani maisha ya mtu mwingine na ukijaribu kufanya hivyo siku zote huwezi kufanikiwa. Latoya alitaka kuwa kama Richard alivyokuwa akasahau kwamba yeye ni mwanamke, akasahau hata Richard mwenyewe alibadilika kadri siku zilivyokuwa zinaongezeka ndani ya BBAII na hakuwa na pupa wala ujuaji katika kuhakikisha anapata ushindi. Pia kupata ushindi si lazima uwe mapepe sifa ya mwanamke ni utulivu na uelewa wa kutosha(Tuliyaona hayo kwa Cherise na alishinda). Sisi tumeula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua. Pole Latoya lakini umevuna ulichopanda.
  Wadau naomba kutoa hoja.

 28. Dunda Galden Says:

  Anti mtalii haman noma ludi nyumbani usijali asie shindwa si mshindani hahahaha kwenu watalii sababu haziishi………BINTI-MZURI kuja kufuturuu nimechemsha mimi nakuja siku ya Idd El Fitriiiiiii kama mualiko utakubarika
  chai goda

 29. linda Says:

  Ujinga mtupu!

 30. Simson Says:

  Jamani haya ni mashindano, na katika mashindano kuna kushindwa na kushinda ila kwa sisi watanzania mtu akishindwa tu katika shindano lolote watampa lawama mpaka ambazo hazifai kuandikwa kwenye vyombo vya habari. Swali linakuja “ANGESHINDA INGEKUWAJE” Mbona hata hao wliopita walikuwa wanafanya huo ufuska? KWANI HIZO NCHI ZINAZOKUWA ZA KWANZA KUTOKA UNAFIKIRI HATA WAO HAWATAKI KUWA WASHINDI?
  Jamani watanzania tuwe tunakubaliana na matokeo ya pande zote mbili sio tupende upande mmoja tu

 31. halima Says:

  Hivi amefanya nini cha ajabu? hayo ni matokeo tu lazima tukubaliane nayo, alipokuwa ameshinda richard hakuna mtu ambae aliona huwo mnaoita umalaya, alikuwa anafanya nini na tatiyana? au ule sio umalaya? au kwa sababu alishinda? acheni hizo, siku zote watanzania hatukubali kushindwa na tunataka siku zote tushinde tu. mimi sijaona cha ajabu habari ndio hiyooooo!!!!!!!!!! matty upo mwanawane

 32. Lolita Says:

  Well what i can say…ths z a shame both to TANZANIA n her(Latoya)….i mean she ws putin herself in someone’s shoes..
  she wasnt her..she thought by jigin wth everyone ws makin herself famous,,what a bullshit….

  Nweiz…ths z smthn to learn..hope next BBA…ths wont happen..either a he or she who will be representn TZ…wont go n do the same shit..

 33. EDWIN NDAKI Says:

  Naenda kuchunga ng’ombe wangu.Nikirudi nitakuja kutoa maoni ingawa hayatakuwa tofauti sana na yale niliyoyatoa siku ALIPOTEULIWA kwenda kuwakilisha Tz.

  Nilikuwa mkweli na nitaendelea kusimamia katika kile nilichosema.

  Mida mida narudi watu wangu

 34. ISMA KABENGO Says:

  WEE NICE2 UNAKOSEA,MIMI NILIANGALIA TANGU SIKU BB3 ILIPOANZA,SIKU YA KWANZA TU NIKASEMA TANZANIA SAFARI HII WAMEPELEKA BOMU KWA KUWA SIKU YA KWANZA TU ALIANZA KUWA MAPEPE KAPAPATIKIA KULALA NA WAVULANA HATA HAO AKINA RICHARD ILICHUKUA SIKU ZAIDI YA WIKI MWEZI KUZOEANA NA WANGINE,UKWELI UNABAKI PALE PALE ALICHEFUA SANA JANA WAKATI ANATOLEWA ANASEMA ALIKUWA ANATAFUTA UMAARUFU NA SASA NI MAARUFU NA USECRETARY BASI .SASA HUYU KWELI MSHINDANI??? HILI NI BOMU HARAFU KIBAYA ALIKUWA MVIVU HAJISHUGHULISHI KIJISHAUA KWA WAVULANA TU HII N I KALI YAKE KABISA ALIPONIACHA HOI NA MIMI NLIONA HAKI KABISA ATOKE MAPEMA

 35. hombiz Says:

  she needs to go sit down somewhere.

 36. Kokubanza Says:

  Mh. Latoya pole mdogo wangu lakini hayo ndio maisha songa mbele. Kuna mambo mawili uliyotakiwa uzingatie wakati unakwenda BBA 3. Kwanza, kama ulivyosema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika shindano hili. Shindano la kwanza Mwisho alikaa siku zote 91 na ingawa hakupata burungutu aliibuka mshindi wa pili. Kwenye shindano la pili Richard akaingiza bao la kisigino. Kwa historia hiyo bongo ni tishio kwa hiyo mshiriki wa bongo anakuwa kwenye darubini akienda tenge kidogo tu anatolewa kupunguza ushindani. Pili wanaongia kwa speed kwenye hilo jumba la big brother huwa hawafiki mbali. Speed yako ilinitisha sana maana ulimzidi hata Merily. The last nail in your coffin was the day you crossed over from Morris to Ricco. Pole umetolewa wiki ambayo Ricco alikuwa na uwezo wa kukusaidia angalau ungetoka wa pili ama wa tatu utupunguzie aibu watanzania. Anyway kuteleza sio kuanguka. I hope umejifunza kitu. Mwanamke jisimamie. Do not sleep you way up!

 37. eva Says:

  that girl is chav

 38. POTI Says:

  kuna yule jamaa aliye kuwa anajiita (mzalendo) sijui kajificha wapi.tulikuwa tuna hamu ya kujua ana semaje na huyo latoya wake wa kikenya.

  Latoya wenu akishindwa msikimbie jamani.

 39. kwerekwere Says:

  mamaeeeeeeeeeeeeee nipo sauz jamaaaa wananiambiaa wewe dada zako kumbee mama wa huruma aibuuuuuuu mie sisemi lolote hata bar yangu nimehama sasa jmos nipo gado tuu sina raha wala usemi nikichema tu aaaah dada kalambwa na midume kibao

 40. dinna Says:

  Latoya ni binadamu kama nyie mnaochangia. Inawezekana baadhi yenu mnao mponda ni wenye tabia chafu na wapenda ngono kuliko yeye. Sikuona kibaya alichofanya mtoto wa watu na hili ni gemu na lazima atoke mtu. Kutoka kwake mapema ni wivu tu wa nchi nyingine kuona Tanzania kila mwaka iko juu thats all. So give her a break plse!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Na kwa jinsi alivyo hana presha kwa kutokuwa mshindi kwani hata wakati anatoka she was so happy. I believe she will do more in her life. Latoya welcome home baby!

 41. sifa Says:

  Afadhali ametolewa kwasababu alikuwa anatudhalilasha watanzania na kuvunja mila na desturi zetu kutokana na ujinga aliokuwa akiufanya tatizo ni ulimbukeni uliomjaa.

 42. michelle Says:

  JAMANI HUYU BINTI SI CHOTARA NI MCHAGA WA ROMBO WAZAZI WAKE WOTE WALIKUWA WAROMBO, BAHATI MBAYA WALISHATUTANGULIA LAKINI MSIDANGANYIKE HUYU NI MSWAHILI WAKUTUPWA.

 43. baker Says:

  mbona fujo wanampaka! yeye kama yeye jamani kafanya aliyoyaona kuwa ynafaa kiupande wake! kwahiyo ndoishakuwa ivyo nikupiga kimya, kwani sikila m2 na life yake jamani mbona mnakandia kihivyo, mambo ayo yakizamani washakji. Hambadilikagi tu!
  Latoya big up kwani ni exprnc vile vile, rudi home uendelee na maisha yako haya madongo ni yakupita tu.

 44. any Says:

  Haa, mnachekesha, katuaibisha watanzania? i dont buy that. Kajiaibisha mwenyewe maana mimi kama mtz sidhani kama alikuwa ananiwakilisha, maana watanzania hatufanyi alichokuwa anakifanya yeye hadharani. Tunafanyia vyumbani au ukizidiwa kwenye gari naamanisha tunajifichaga. haaaa.

 45. trii Says:

  sawa tumekubali matokeo.

 46. muhsin Says:

  I HAVE NEVER BEEN ASHAMED LIKE i HAVE BEEN THIS TYM. iTS ALL BECAUSE OF HUYU LATOYA.THE STRATEGY AMBAYO INAWEZA KUKUFANYA UWE SUCCESSFUL IN BBA NI KUWA REAL. HUYU DADA WAS FAR FROM BEING REAL KATUTIA AIBU NA ANASET IMPRESSION MBAYA KUHUSU MADADA ZANGU WAZURI MA KIBONGO.MULTICHOICE MNATAKA KUNIAMBIA BBA NI KWA AJILI YA MAHAFKASTI TU? GIVE US A BREAK WILL YOU?

 47. mwwakahajo Says:

  haka kasichana kametutia aibu ni lazima tukubali.kuwa na mpenzi haikatazwi hasa kulingana maumbile na ubinadamu kamili. tatizo ni pale ubinadamu wako unapoukataa na kujifanya mnyama sawa kama mbwa! dogo umechemsha kwa kuchojoa nguo ovyo kwa wanaume zaidi ya mmoja kwa kipindi kifupi sana.hata kama ulibanwa sana wakati unaingia kwenye hilo jumba basi ungeamchukua mmoja.yaani we uko kama kuku,akirukiwa hapa na jogoo mmoja atarukiwa pale na jogoo mwingine kazi yako kukaa chini tu ”wajipandiage tu , sambi sao” hopeless kabisa! na hii ni tabia yako si kwamba umeenda kujifunzia huko. muwe makini nako kakirudi hakajaanza leo hako…. wengine mjifunze mkienda muwe na adabu.hii ni game sawa, lakini haimanishi inakuondoa katika nafasi ya utu na ubinadamu. hovyo kabisa latoya!

 48. mwwakahajo Says:

  kiukweli kabisa kama angekuwa na ka boy friend kako kamoja i would have no comment !! kwani kushinda ama kushindwa ni matokeo…. ila kwa hiyo tabia yako uliyoifanya latoya nahisi M-net walikutoa mtaa wa ohio au kule kinondoni kwa wezio wasiothamini miili yao na kuifanya kama viwanja vya kujaribishia magari mabovu. kwenda zako latoya!!

 49. nkyeku Says:

  Mie naona afadhali katolewa mapema maana angeweza hata kumuomba Big Brother Ngono…

 50. dennis vitus Says:

  MWATAKA NISEME NINI?LABDA MAPAJA YAKE HAYANA MVUTO AU MIUNOMIUNO YAKE HAICHENGUI,DOOOOO MTOTO AAMECHEMKA MBAYA RUDI NYUMBANI 2ENDELEZE LIBENEKE LILELILE ULILOLIANZA BIG BROTHER ,NI HAYO 2 MTOTO WA KICHAGA

 51. Philip Says:

  But hata Richard nae kama nakumbuka vizuri alifanya vitu vya aibu atleast I gathered that kutokana na comments za watu!! N he won!! Wouldn’t blame her to try the same thing if it means winning! In a game like BBA you do what yo gotta to get them 100,000 usd!!

 52. kindo Says:

  kwenye kila mchezo kuna strategy. kila strategy inaweza kuleta ushindi au kushindwa. bahati mbaya sana strategy ya Latoiya haikuleta ushindi kwasababu hakutulia kusoma nyakati. wenzie wote initial strategy yao ilikuwa ni lay back attitude ili kuweza kuwasoma ma-housemates wengine na system nzima ndani ya jumba la BBA. pili, strategy ya Richard ambayo Latoiya alijaribu kuitumia kwake yeye isingelipa kutokana na mfumo. kwamba sisi ni waafrika na mfumo dume ndio unaotawala. alitakiwa alione hilo mapema sana. tatu, throughout the game she was not herself she was trying too hard …..kuna wakati alionyesha kuchoka, kwasababu when you try so hard you tend to get tired easily… hata angebaki asingefika mbali kwasababu si mwepesi wa kusoma situation na kubadili game….lakini ndio hivyo…asiyekubali kushindwa si mshindani. karibu uswazi bibie!

 53. Bhuinda Says:

  Hamna lolote mnaomusaga, msiseme wakati hamjui kilinachoendela huko ndani ya jumba, kafanya kipi amabacho richard hakufanya na ambaye alikua kaoa, wazushi tu.
  Latoya ana sifa ambazo ninyi hamna ndo maana kachaguliwa, kwani hao waliokua wanatoka mwanzo hawakua watu?
  Latoya mama achana na maneno ya wenye wivu walitamani wawe wao ndo kama hivyo.
  Latoya mama big up wala huna wa kumuomba radhi, wanafanya mangapi wao hadi wewe ndo uombe radhi, mamiss wanaboronga kila leo walishaomba radhi? wansoka? wazushi, wala usiomuombe yeyote radhi kama unaamini ulichofanya kilistahili kwa ajili ya kupata ushindi, si kila strategy ita-work out zingine zinagoma, kama yako, so what,
  Muacheni dada wa watu aanze maisha yake mapya.
  Alichotaka according to yeye ni umaarufu na tayari anao so hayo mengine mwasema ninyi, hao akina richard wamesaidia nini watanzania tangu mje.
  Mmekosa uzalendo wenyewe, wengine nchi zao hata kama washiriki wanaboronga bado wako positive nao, ninyi hapa na viingereza vyenu na kujidai mwajua saaana mkawa negative what do you expect from the rest of Africa kama nchi yake yenyewe iko negative.
  Ninyi ndo mnatakatiwa kumuomba radhi kwa kutokua wazalendo.
  kazi kulalala tu…

 54. Amina Says:

  DU HATARI MATTY HALAFU NAONA KUNA MEMBERS WAPYA HUMU WAMEIINGIA…..

 55. Amina Says:

  Bi shost kalikoroga atalinywa

 56. V.E.S. Says:

  Suala sio kukurupukia mapenzi wala nini, ni kweli richard alifanya hilo lkn kumbuka hakukurupuka and that came naturally sasa yeye kuigaiga akidhani coz it worked for richard it will for her to… no no noooo…. you are very wrong Latoya. Pale ni utashi wako ulitakiwa uishi maisha yako na sio kuiga, ama utatuambia hata huku nje ndivyo unavyoishi kurukia rukia wanaume leo huyu kesho huyu, unachuna uyu unalala na yule is it TOYA????? The shoes fitted Richard will never fit you, ulikurupuka mno ungetulia usome watu yaani wee mwenzangu bure kabisa huoni mbele wala nyuma pole sana. You had nothing else to offer than kurukia wanaume.

  Harafu ulivyotoka ati wasema ulitaka umaarufu, did you really listen to yourself, aren’t ashame of yourself? Hata kama that is what you wanted huwezi kuropoka kwa hadhira hivyo unaonekana limbukeni na mshamba with no brain my dear, watu wanashindania $100,000 wewe unashindania umaarufu. sasa subiri uone huo umaarufu wako utakapo kufikisha, magazeti yatakuandika hadi utaomba msamaa, omba mungu upate kamkataba uko south laa sivyo utatokota.

 57. kikapu Says:

  Layoya hakufanya cha ajabu zaidi ya Richard ila Latoya tayari alionekana ni tishio na ndio maana aliondolewa mapema na ushindani wake ndio uliomfnaya hata Big ampe nafasi ya upendeleo kumuweka kwenye penthouse. mfumo dume wa watanzania ndio unaona kama latoya amekosea wamesahau finger gate ya Richard na Ufuneka.

 58. Maneno Mpina Says:

  Well, its big lesson and challenge for all stakeholders who believe in winning at the right hand and for the right and acceptable characters! Karibu nyumbani dada!!!!!!!!!

 59. uejfuewthfiu Says:

  Huo ulikuwa ni ushindani tu. Someone had to win and someone had to loose. So either way ilikuwa ni lazima aangukie kwenye moja wapo. Mi nashangaa majungu ya nini. She was her self. Hakuiga tabia ya mtu, thats just the way she is. Kama alionyesha umalaya, basi ndivyo alivyo kuliko ange-fake then siku ya siku asahau aaribu zaidi.
  Love u Latoya. To me u r still a winner.

 60. kikapu Says:

  Namshangaa sana huyo Sifa anayesema Latoya alikuwa anatudhalilisha. vp Richard hakukudhalilisha???? au kwa kuwa alishinda??? na vp kuhusu mkewe wakati dunia nzima ilijua Richard kaoa na alikuwa na Tatiana? achanei mfume dume. mwanaume akifanya Rijali ila mwananmke akifanya ni malaya. haya ni kipi cha ajabu alichokifanya ambacho wewe hukijui wala hujawahi kufanya. ule ni mchezo na Tanzania tuna tisha kwa hiyo hiyo ni campaign ya nchi nyingingine tusishinde tena. amkeni watanzania mwacheni mtoto wa watu.

 61. uejfuewthfiu Says:

  We anonymous hapo juu, wazazi wa Latoya hawajatutangulia. Ni ma ayake tu ndio aliyetutangulia lakini baba yake yupo hai na alihojiwa. We vipi wewe…..mbona unapenda kusingizia kifo. Mi Latoya hata kama hajashinda, to me she is still a winner. Alikanyaga in that house, thats all that matters.

 62. halima Says:

  Hivi huo udhalilishaji mnaodai ni upi? Na uliza tena richard alikuwa anafanya nini mule ndani? mbona tulikuwa tunashangilia tu. tushangilie na hili. Latoya my baby usijali achana na wabeba maboksi waoshe vinywa.

 63. Matty Says:

  Majita mkuu nipo nilikuwa nangoja wenye kichefuchefu watapike kwanza kisha nije nisawazishe!

  Halima shosti nipo!!ngoja kwanza niwaweke sawa wadau pamoja na yeye mwenyewe shosti Latoya.

  Mbona nilijua zimekuwa nyingi sana washkaji???muacheni kwanza apumzike, halafu mbona tunakuwa wa kwanza kulaumu tu hivi tungepelekwa sie MALAIKA tungeweza???haya litakaemchoma limemgusa!!

  SHOSTI LATOYA,
  sawa umechemka kule south sasa suala la kusema ulitaka uwe femasi ndo nini???na wewe nae ndo maana wenzako wanadai ni bishororo,limbukeni n.k inahusiana nini na mchakato mzima wa shindano hilo??

 64. bdo Says:

  Namshuru Mungu kwa hatua aliyofikia, maana tushukuru kwa hili la kutoka mapema maana tungeshudia makubwa zaidi – ya aibu endapo huyu binti angeendela kushiriki, asante Mungu

 65. dina Says:

  Inawezekana kuwa strategy aliyoingilia haikuwa yenyewe, and looks like she was not being herself, nafikiri hapo ndio palipom-cost her chances in BBA3. Ila kitu kingine nilicho-note ni kwamba some issues if are done by akina baba ..It’s ok (and they receive a pat on the back!), lakini wakifanya akina mama, the utamaduni, desturi na mila things pops up! Kwani alichokuwa anafanya Richard kwenye BBA2 ndio kilikuwa mila na desturi zenu? He ended up being rewarded the moola….

 66. Semasema Says:

  Pole mwaya weeee mlupo huoooo…

 67. Anna wa Moshi Says:

  Pengine Latoya hakuelewa anakwenda kushindania nini, alidhani anakwenda kwenye mashindano ya ngono ……..na alikuwa na shauku na kutamani kuonja……. kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
  Ila ametuaibisha mnooooo…..

 68. Sheila Says:

  Jamani jamani Watz!! Mbona mnapenda kuaibishana? Kuna mtu hapo juu kasema ati Latoya katoka machame au Arusha; kwani huko machame ndo kuna washamba sanaa au? Hebu angalia jinsi mnavyokuwa mnatoa maduku duku yenu. Makabila hapa hayausiani na tabia za watu. Na kuhusu Latoya kutolewa naona mbona ni sawa tu, everyone has their own choice in life. So whatever she does its her own choice. Msimseme mdada wa watu wakati nyie pia wachafu kwa njia moja ama nyingine. Watz kabla hujamnyooshea mwenzako kidogo umejaribu kwanza kuangalia boriti lililopo kwenye jicho lako?

 69. Mh Lukamba Says:

  Sibadiliki na uzalendo wangu,BB3 siyo shindano la kushiriki mtanzania na kwa mtu mwenye akili timamu na mwenye maadili !!!
  Nawapongeza wote mlikuwa sambamba katika kumpinga Latoya,na katika kupinga hili shindano

 70. latoya Says:

  loh, watanzania hampendi kushindwa! jamani dada wa watu kajitahidi sana , tena bora alivyotoka mapema aendelee na shughulizake maana pale mshindi ni mmoja tu, mtu ukikaa hadi siku ya mwisho na utoke kapa kama mwisho, Ofuneka etc ni kazi bure maana unakuwa umejichora vya kutosha na umepoteza a lot of ur time. I LIKED LATOYA AND SHE DID WHAT SHE COULD DO, IT’S UNFAIR TO COMPARE HE WITH ANYBODY.

 71. Mimy Says:

  Uuups kwa kweli mimi binafsi nimefurahi sana kuona huyu dada ametolewa, kama baadhi ya wachangiaji walivyosema jamani wakinadada wapo wengi tu Tanzania wenye uwezo mzuri tu ni wao tu kujitokeza ili waweze kuchaguliwa. Yesu wangu sasa sijui kwa kweli tutaonekanaje kama Taifa especially Mwanamke wa Kitanzania, kama tena kuna mtu aliwahi kusikia kuwa TZ wana wanawake wenye tabia fulani sasa kwa kumwangalia huyu wa Arusha baaaaaaaaaaaasi ameconclude. Kwa kweli bora ametoka maana ilikuwa BALLAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA na angeelendea kuwepo ingekuwa MBOFU sana. Haya RUDI arusha ukaendelee KUWACHANGANYA WANAAPOLO ndicho ulichozoea inaelekea na kama hiyo ndio tabia yako oooooh basi MANDE is nearby kwa ninavyowafahamu WANAAPOLO. Watakufanya KITU MBAYA, KITU INAFINYA SHAURI YAKO

 72. Rena Says:

  Mie namuonea sana huruma atakavyorudi sijui atasema nini maskini wa mungu je familia ndugu atawaambiaje maana magazeti yote yamejaa story yake hizo aibu atazificha wapi kila mtu anamfahamu na hata boy friend wake atamwacha maskini pole sana na ujifunze ukienda ugenini ujifunze wale watu wanakaaje wanalalaje hiyo ndiyo itakayokusaidia
  ukisharudi we uingia tu ndani ujifungie maana watu wana hasina sana na wewe maskini mdogo wangu poleeeeeeeeeeeee

 73. Olive Says:

  Toya hongera sana,ulifaulu step ya kwanza,zilizofuata umeharibu mwenyewe acha kujitetea eti watazamaji ndo judges u were not aware na ulichokuwa unafanya…! Gosh!

  Pia kumbuka Mwanaume kuwa na wanawake wengi yeye ni LIJALI kwa mwanamke ni AIBU ,coz she waz made for a man n not a man for a woman ndo maana kuna KING MUSWATIIIIII….!Think about it!!!!!

  Pia si vizuri kusema eti haustaili kuwa SECTRETARY u deserve more than that,ni kipi hicho kime replace professional yako in a SECOND???? U will need a recommendation letter kutoka wa muajiri wako kuonyesha we ni mzoefu n its not ur first Appointment ktk employment industry..!!!! Usitupe mbachao kwa msala upitaooo….! Unless kapige more classess utakuwa juu.Ila ukitegemea kuwa among Bongo celebritiez itakula kwako..!!!

  Uzuri wa mwanamke c rangi,sura,nywele n ol meks a woman beuty ni uniqueness yako ktk thinking wise and ol related.

  Think b4 wen addressing entin in Public especially in TZ! Muulize vijisenti!!! NOMAAAAAA !!!!

  We ni mdogo be in ur BEST BEHAVIOUR ,go for classes!!!

  Kijishaua kwenye press ACHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.

  Nilikusikia unasema utafanya Press Conference…fikiria sana utakachokuwa una ongea,kujibu maswali ni everytin,u r now known in every corner.

  Mkumbuke Muumba wako daima.

  Cheerz!

 74. Papin Says:

  Nia yake kama alivyojieleza kuwa kila siku alikuwa anajifikiria jinsi ya kutoka sasa katoka kwa kuliaibisha taifa nyie mwachonga

 75. Chris Says:

  Watu wanaosha vinywa aiseeeeeee! Duuuuh!

  Anyway, her stay in the room proved how jinxed and blank-minded she is! IMO, I see like she thought success is where u stand and not where you’re heading/looking! She wanted to pass on the ways of the previous Richard! That made her to be fake!

  BTW, guys when it comes to butchering our image I think Richard started!

 76. upendo Says:

  pole sana umeabika sana umeabisha taifa ngoja niondoke maana acha wengine waonge

 77. mzalendo Says:

  Nipo poti, nilikuwa busy kidogo naandaa maandalizi ya kumpokea Latoya. Usijali, ule ulikuwa ni mchezo na nadhani Watanzania wengi wemepitiwa kidogo na hilo, “asiye kubali kushindwa sio mshindani” na hii inaonyesha jinsi mlivyo. Richard alichofanya mmemsifia ingawa kila mtu alijua kuwa ameoa, lakini kwa vile alishinda mlimpokea na mikona miwili. Latoya alikua tishio kwa Nnchi zingine za afrika, hata wenzake walivyomnominate hawakumpa majina mlombatiza mtoto wa watu, walisema she is compitition! Sasa nyie majaji dunia mnaotaka kuwagaiwa watu riski wakati wanamaindi maisha yao mkaingila we, na sasa mnasema kawatia aibu, MUNGU AWASAMEHE WOTE! BHUINDA NA WENGINE WOTE MLOELEWA GAME; ASANTENI SANA. Matty big up, nimekuwa nakusoma sana kwenye forum za mnet asante.

 78. Majita Says:

  CONCLUSION.
  Mimi MAJITA kwa mtazamo wangu naona huyu binti kajitahidi SANA.Na ingekuwa ni kutoa tathimini ya ki-nchi Tanzania bado tunaongoza saaaana tu.
  Wewe Fikiria:-Mwisho alikuwa mshindi wa Pili.Richard mshindi wa Kwanza.Na huyu Latoya kawa mshiriki wa KWANZA kutoka.Yaani kwa ufupi tumevunja rekodi hadi sasa.Yaani tuna mshindi wa Kwanza,wa Pili na wa Mwisho.

  Sasa nyie wadau hebu nitajieni ni nchi gani ina washindi wote wenye nafasi muhimu za kuangaliwa katika mashindano as wa kwanza wa pili na wa mwisho hadi sasa????Ni TZ pekee.Hongera Latoya.Unafikiri angekuwa wa katikati huko ningetoa hii comment ya 77 muda huu tu.Si zingeishia 20 au 30 tu.hahahahahahahaha.
  Majita

 79. Nuru Says:

  Jamani Latoya hakufanya ngono mle ndani it was kissing only, au wenzetu mlikuwa na BB yenu tofauti?!!! Kilichomponza Latoya kutolewa kwanza ni kureveal strategy yake ya ku-play with boys minds kwa Biggie ambapo viewers pia wakaipata. Ya pili jamani Tz tishio kwenye BB so nchi zote zenye washiriki walikuwa wanataka atoke tu, Hata kama asingekuwa nominated the 1st time, huko mbele angekuwa nominated wangemtoa tu…

 80. Pearl Says:

  toya toya toya!!!!!! hicho kitu huwa hapewi kila mtu kwasababu kwa kufanya hivyo unajiharibia heshima yako. Kwa kifupi ni kwamba hapo ndo pana utu wako sasa ikitokea unagawa ovyo matokeo yake ndo kama hivyo unakuwa “valueless” na you can even yourself prove from the comments people are making here.

  Umaarufu wako unautafuta vibaya shosti,ungeweza kutumia kiungo kingine kwenye mwili wako lakini hicho ulichotumia kimekuharibia.

 81. Klover Says:

  You people, you are talking tooo much, hivi kwani ni nyie ndio mlimpeleka latoya huko? kwani hata angepata hela angewagawia? je kuna mtu kati yenu kapata japo kasenti toka kwa richard? sasa kelele ya nini, na nyie si muende kama mnataka. Afanye vizuri au vibaya nyie yawahusu nini na yule kaenda kama latoya na wala sio kama tanzania. Loo muwe na aibu na pia waelewa. Inaelekea nyie hata mkiangali sinema pia mtazisema tu wakati mnajua ule ni maigizo tu. Badilikeni watanzania lazima muwe waelewa wa mambo.

 82. EDMUND SAMA Says:

  Achenni kumsema Latoya kwani ndio kiwango chake kilivyo kama mnaona hakuwa na vigezo vya kwenda BBA si mngeenda nyie? vle vlle mnafikiri nchi zingine hazitaki ushindi Tz tu ndio inahitaji sio wakati wa kulaumiana huu

 83. weezy b Says:

  Hakuna aliyeumbwa kama malaika kwamba hata kosea cha kufanya next tym tafuteni m2 anayefaa ndio mumuweke mtoto ni mzuri ila kajichanganya bahati mbaya hao wanaolalamika wajaribu kufikiria.

 84. ma'reen Says:

  Jamani eeh muacheni mtoto wa watu! Her strategy failed her n that’s all. Kuhusu kulala na wanaume wengine nafikiri mnasubiri kusoma magazeti ya udaku ndo mtoe comments. Av bn watching it nikipata mda n almost every girl (except Hazel) has or is sharing a bed with a man. Sijaona au kusikia in highlights kuwa alifanya ngono. The only suspect wa kufanya ngono japo walijifunika sana tukaona movements zisizo za kawaida ni Tawana. So please give the poor girl some break! Kitu negative nilichoona kwake ni kauvivu ambako alikarekebisha huku ishakuwa too late akiwa kwenye dump. Upeo wake wa mambo mbalimbali pia si mkubwa ki-hivyo, bt she’s still young ajitahidi kupandisha book. Otherwise please stop hating on her. Pole sana mdogo wangu welcome back home.

 85. Amina Says:

  mhh hatari mi hiyo big brother sijui ni nini?

 86. Nnana Says:

  Achana na wabongo Latoya ndiyo walivyo wana mfumo dume sana, mi sjaona kibaya ulichofanya mdogo wangu, ukicompare na Richard aliyekua ameacha mke huku nje na vile vituko alivokua akivifanya wewe hata robo hujafikia, au kwa vile Richard alishinda? Toya ulikua unatisha na vile mataifa mengine yameshawaogopa waTz basi ndyo sbb yakawa na kampeni ya kukutoa usije ukashinda tena, Halafu vinyamkera wengine nao huku bongo eti wanakupigia kura za kukutoa yaani waswahili wivu wa nini jamani ndo maana mnaishia kurogana tu hamna jipya la maendeleo nyie ni ndumba tu. Mmepata faida gani sasa baada ya Latoya kutoka? hata mngepelekwa nyie mngeweza basi? Wanawake nao mko mstari wa mbele kumpinga Toya mkoje? mliona akishinda atawazidi pamba au? Karibu nyumbani mdogo wetu hata kama umetoka kwenye jumba bado wanakugwaya. we ulikua huoni hata ukishaoga tu ukajipodoa viwatu vilikua vinakupiga mimajicho ya wivu, vilikua na wasiwasi utashinda tena. Hao wanaosema eti umekiss umefanya nini na Rico na Morris me kwa kweli mi niliona unawachezea tu labda hao wanaosema hawakujui kwa ukaribu ndiyo sbb wanaona kama ulifika bei, na wao wanapokusema hivyo kwani wao ni wasafi sana? hebu usijipe presha, Kwanza hata ulipotoka kwa jinsi ulivojibu maswali na Kb pale nje kichwa kimeonyesha kina akili mdogo wangu! Tunamiss dance zako sana babygal!

 87. caroline Says:

  naungana na wewe halima,kunyas anye bata akinya kuku ……………………………….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!,mpeni maneno mazuri sio kusema mlijua mlijua yapi?????????????????????????????????

 88. noela Says:

  SASA WADANGANYIKA ACHENI KUSIKITIKA MAANA RICHARD ALIKUWA WAKWANZA,MWISHO WA PILI SASA YEYE NI SUFURI KWAHIYO TUNATAKIWA TUHESABABU KUANZIA 0,1,3

 89. Matty Says:

  Amina welcome back shosti! hapa wageni wamekuwa wengi mno nadhani BC NI ZAIDI YA BLOG sijui kama umenipata?halafu sasa wageni wengi hapa hata hodi hawapigi hahahahahahha mgonga kengele nipo around na ukitaka nikuorodheshee wageni naweza.

  Wapendwa mbona hivyo??kejeli, matusi,jazba za nini?Latoya ni latoya na sie ni sie sasa kashachemsha yaishe basi washkaji!

  Mama wa Kichagga sijakusikia kabisa dadangu upo wapi???

  BC ukiweza tunaomba umhoji huyu shosti tusikie toka kwake zaidi maana naona waliowengi wanausemea moyo wake heeee makubwa!

 90. kikapu Says:

  Mashinadano ni mtoano Latoya katoka mnachonga

 91. cnyo Says:

  waosha vinywa osheni, but the girl was in the game! kwani mbona kina richie walikua na wapenzi jamani……….,hebu mwacheni latoya. kwanza hii ni campain toka nchi nyingine kwa kuona kwamba tz kila siku tupo juu, thats why wakaamua kutuua mapema! latoya, ur welcome back mama, ur beautiful is true!!!!!!

 92. Tamu Says:

  mh yetu macho na masikio.
  >amesema u-secretary is a disease na alihitaji awe famous na ameshakuwa celebrity na magazeti yote ya Tanzania yatashine picha na jina lake tu.

  >amesahau kuwa magazeti yanaweza kukuinua na pia yanaweza kukupoteza. na haelewi kuwa kazi ya u secretary ndio ilimfikisha alipo.

  >na haelewi kuwa celebrity kuna gharama.

  anyway kila mtu ana malengo yake ila ya huyu mwenzenu yameshangaza maana hata muhogo mchungu ni famous sasa je yeye anauhitaji wa namna gani?

  ni vyema angekuwa anafikiri kabla ya kujibu maana majibu yake yanaonyesha jinsi alivyo na upeo mdogo wa fikira.

 93. Lily Victor Says:

  kwa kweli mimi binasfi siwezi kumpa hongera Latoya kwani kwenye nyumba la Big brother kumeandaliwa kwa ajili ya kufanya mambo ya ajabu? Kuingia na kuingia tu akaanza kuonyesha makeke yake. ushauri wangu arudi kwao aendelee na kazi za ujenzi wa taifa letu

 94. Matty Says:

  Majita kichwa chako kinahitaji clorokwini nimecheka mpaka basi jamani hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 95. Majita Says:

  Matty unafikiri???Hapo ndo penyewe.Idha way kusingetokea matokeo tofauti na hayo.Hahahahahahaha matty kama uliota vile niko na dozi ya krolokwini.Chungu hizoo!!halafu nanywea malimau eti nisijikune/zisiniwashe.hahahahahaha.krolokwini bwana kaaazi kweli kweli.

 96. michelle Says:

  Kama nasingizia mbona unasema mama yake kafa,wee vipi, huyo aliyehojiwa ni bb mdogo wake, kwisha maneno.

 97. michelle Says:

  Matty shost sijakusikia muda hata salam wangu? umenisahau nini? basi mimi nakusalimia kwa jina la yule alieko upstairs.

 98. Chachandu Says:

  Hau na wewe, umerudi kumuandikia John Mashaka? Yule ni superstar Msomi, haumuwezi.

  Wewe ni bora ukauze sure posta mya, nadhani kempiski haukubaliki

 99. mtajiju Says:

  kwani hii ni sehemu ya kusalimiana na kupeana stori zenu? nazani hii ni sehemu ya kutoa maoni kuhusiana na latoya sio mambo binafsi,wewe matty na amina na majita zamani mlikua mnatoa maoni mazuri yenye mvuto sasa ivi mmekuaje?mnasalimiana tuu hata sipati maoni yenu

 100. Matty Says:

  Majita ndugu yangu ila tuache utani krolokwini chungu aisee sasa na hayo malimau inakuwa vipi??hahahahaha
  Michelle shosti asante kwa salamu, na mimi nakusalimu ktkt jina la bwana!
  Halafu shosti Latoya anatafuta umaarufu kihivyo atalia walai nvyoijua bongo jamani udaku ni sooo!!

 101. mwwakahajo Says:

  we klover nina wasiwasi na uelewa wako? unaposema latoya alienda kama latoya unamaanisha nini? ina maana kwa akili yako unadhani kuna siku utakutanana na mtu anyeitwa Tanzania?USITUTIE HASIRA WAKATI Hako kabinti kameshatuudhi.. PEARL NIMEKUFAGILIWA KWA MSG YAKOnafaa kuwa mtoa ushauri nasaha.

 102. hawa msangi Says:

  mmhh nadhani next time wakati tunatafuta mwakilishi wa kutuwakilisha tujaribu kupima uwezo wa kufikiri wa mshiriki.huyu hakuwa anajua kitu chochote kama tutamlaumu tutakuwa tunamuonea

 103. grace Says:

  latoya wamemuuonea 2,its not fare kwani wote waliopita walikuwa hivyohivto

 104. viveca Says:

  Hivi Watanzania hamna kazi, EPA hamjalipwa dada sa kakopwa.

 105. binti-mzuri Says:

  we dunda galden namba 29,karibu eid.

  kweli humu ndani kuna waosha vinywa,haya sukutueni. i guarantee that if latoya had won,comments would have been different here regardless of what she did. kila mtu na maisha yake,kama yeye kaamua kuishi yake hiyo,wewe ishi yako vile unavyoona inakufaa. that life works for her,your life works for you..leave her alone. you cant chnge people,accept them as they are, na next series,nenda ka apply.

 106. Frateline Says:

  Hi Guys kutoka Helsinki-Finland

  Mimi sio mpenzi wa BBA lakini wachangiaji wengi wanamshambulia huyu dada na mimi wala sitaki kumtetea ila natoa hangalizo, kwa nini umalaya unaonekana kwa wasichana na wanawake tu? mbona wanaume kama richard na mrisho walikuwa wauni na malaya, mbona watu hawajawasema? mimi nasema umalaya ni umalaya uwe mwanamme au mwanamke, halafu BBA ni mchezo wenye mazingira ya ngono ngono hata washiriki wanashawishiwa lazima kufanya mapenzi ndiyo unashindwa hata waliotangulia na kushinda walikuwa hivyo hivyo, ushauri wa bure kama Dada unajiheshimu usishiriki ktk mchezo huu hafadhali Tanzania ikawakilishwa na wanaume tu maana sio vizuri kuwaona dada zetu wanadhalilika hovyo na hii ni kutokana na utamaduni wa mwaAfrica-polygamy is allowed for men not for women.

  Frateline

 107. mzalendo Says:

  Nakufagilia binti-mzuri, wale wajuaji na vinywa vichafu chukueni fomi next season.

 108. mwwakahajo Says:

  hata mimi wananiboa sana hao wanaoigeuza hii safu kama sehemu yao ya kuchat issue zao! mkoje nyie?si mtumiane sms kwa simu zenu.mada ni tofauti kabisa na nyie mnaibua mada zenu za kitoto! twamzungumzia latoya kama mmesau sio kutuletea issue zenu za jikoni.. mara krolokwini ….mara malimao…ovyoooo!! mnataka tuwaeleweje?

 109. Nuru Says:

  Mnaoponda Latoya, there is next time chukueni form mkatuwakilishe tuone mtakuja na nini, nahisi hata kwenye fake nominations mtapata votes toka kwa all fellow housemates. Get a life..

 110. Matty Says:

  Mtajiju heeee kumbe linakuchoma watu kutumiana salamu??pole ndugu yangu salamu zikufikie popote pale ulipo.
  Haya maoni yangu ni kuwa jamani give her a break its enough sasa washkaji mhhh mwenyewe ashasema hana hata boifrend hahahahahahahahahah (anatafuta i gues)sasa mbona mnamsakama mtoto wa mwenzenu?????

 111. Emie pesh Says:

  Huyo kachemka!!! I thinks she only wanted to be a star!alikuwa too mshamba ila kujifanya wa kisasa.it is good that you are out.

 112. BLACKMANNEN Says:

  He he he he he heeeeeeeeeeee! Duh, wanachama wenzangu wa BC, mna mambo nyieee, he he he he he heee! Jamani tuendeleze UPENDO wetu kati ya Watanzania wote!

  Nimo njiani, nitashuka na maoni yangu kuhusu “Mwakilishi Wetu BBIII Afrika, Bi. LATOYA” au “Lato” na wengine wanamwita “Toyota”!

  I’ll Be Back……..This Is Black=Blackmannen

 113. BLACKMANNEN Says:

  Hi Bi. Latoya!

  Karibu nyumbani dadaangu! Ulichofuata BBAIII, kimeishia hapo ulipokiona mwenyewe. Yote hayo yasikupe taabu dadaangu, kwani katika mashindano yo yote, lazima kuwe na mshindi na mshindwaji. Lakini kitu hicho usikiache bila kukitumia katika kujielewa wewe mwenyewe kwanini umeshindwa katika hatua za mwanzo.

  Soma mtiririko wa maoni yetu ya tangu ulipoingia katika jumba la BBAIII na leo hii katika chati hii, kweli tumekusema mengi sana, lakini pengine katika uchambuzi wako utaona machache ambayo yanaweza kukusaidia kimaisha.

  Mimi katika maoni yangu sijaliona kosa lako wakati ukiwa jumbani humo, kwa sababu, mimi naamini uliyokuwa ukiyafanya humo ndiyo tabia yako halisi uliyonayo nyumbani Latoya wetu. Huwezi kumridhisha kila mtu kwa tabia ulizozaliwa nazo dadaangu, kila mtu na tabia yake, kama hawakuzipenda za kwako, nadhani na wao wataingia ili kuzionyesha za kwao ili waambiwe kama ni nzuri, maana kila mtu ana amini ana tabia nzuri kuliko mwenzake, lakini watu wa nje ndo waamuzi.

  Wana BC wenzangu, nawaomba tuwe na huruma kwa dada yetu, hata kama utaona alikuwa anakukera moyoni mwako, mpende kama Mtanzania mwenzako mwenye tabia isiyofanana na ya kwako. Mbona wanariadha wetu hawajaleta medali kwa miaka mingi mbali ya kwenda mashindanoni kila mara, hatuwaandami kama dada yetu huyu? Mbona Ma-Miss wetu kila mtu hawatuletei taji, mbona hatuwaandami kama mnavyomwandama Lato wetu? Mbona sioni matusi na majina ya ajabu kwa Taifa Star, ambao kila timu inayocheza nao inawafunga, ambapo hadi Rais wetu ameamua kuachana nao?

  Mara nyingi watu wasiokuwa katika mashindano ni wataalamu wa kusema kama mimi ninavyoona hapa kuwa, kama ningekuwa Rais wa Tanzania ningefanya mengi kwa Watanzania, kwa kuwafunga jela mafisadi wote haraka, bila kuwafikisha mahakani kujitetea na kumfunga jela Mkurugenzi wa Tanesco kwa kuleta za kuleta eti, mgawo wa Umeme, na pia, kuamuru kunyongwa kwa Zombe na Bageni, kutokana na mauaji waliyoyafanya huko Pande- Mstuni na waliobaki kufungwa maisha na wengine kufungwa sio chini ya miaka kumi kwa ushiriki wa mauaji bila kutoa taarifa za mauaji hayo serikalini.

  Latoya, Toya, Lato au Toyota, karibu sana nyumbani, tunakupenda, hapa ndipo nyumbani, sisi tunakuthamini kuliko mtu mwingine duniani, na TUNAKUPENDA SANA Latoya wetu!

  This Is Black=Blackmannen

 114. lawrence Says:

  latoya kawaida, ila please ongea kiswahili kama mswahili na sio mgiriki anayejifunza kiswahili

 115. cheche Says:

  Mwee! huyu dada kaitahidi,ila inabidi ashiriki kwenye shoo ya TEQUILA au i love new york ya hapa marekani! tusimkandie sana ila inabidi tu learn through mistakes thats it!
  cheche

 116. Ngwale Says:

  Hahahahaha!!! Watanzania tuamkeni sasa mambo tunampa umiss au tumpeleke muwakilishai wa BB kwa sababu ni kipotable au mtoto wa fulani matekeo ndio hayo. Kumpeleka Huyu binti lilikuwa ni kosa kubwa mapepe shangingi na mkosa haya na adabu kasingiziwa.

  Pelekeni watu wanaojua challenge na wanaojua wanatafuta nini. POLE KIDADA MAPEPE NINAMSHAKE KIMETOKEA BOMANG’OMBE SIO ARUSHA.

 117. xxx Says:

  ivi hiyo bigi blaza wanachaguliwaga machotara tu?au ngozi nyeupe nyeupe..we ona mwisho, richie na huyu latoya..mbona weusi km mpoki ivi hawachaguliwi..huu ni ubaguzi

 118. mwwakahajo Says:

  nadhani hii mada sasa iishe. BC tafadhari bwana hii muda wake umeisha. we need other current issue, toa hii mada ya “chotara ndizi” huyu aliyezoea kufanya mapenzi migombani kule arisha akadhani anaweza ku – apply the same mahali popote…toa tafaDHARI.

 119. No name five(Violet) Says:

  dada katutia aibu kwa tabia zake lakini tusimlaumu kwa kushindwa. kwani wanaoshindwa ni akina nani na sisi watz tuwe washindi tu? ukiingia mashindanoni kubali matokeo mawili ya kushinda na kushindwa.
  byeee!!

 120. Mary Mkwaya Malamo Says:

  aah! sio issue watu wangu, kama vipi mwakani mmoja wetu aende kwenye jumba lile tuone atatoka wangapi? sister kutoka wakwanza sio issue masela…. tusimaindiane ki- hivyo. Latoya sister hongera umecheza nafasi yako sema tu hukuwa na tekniki nyingi mwana.

 121. shantell Says:

  acheni majungu jman…………..
  Latoya dear kila mtu huwa ana anguka kwenye sehemu tofauti,juz like mum alivomuambia dada ako Scolaa, ukianguka sio mwisho stand up, wipe urself remove the dust n move forward sweetheart!!Shiit happens!!!, we all go wrong so worry out n move on, yote maisha haterz will talk shit buht they aint got nuthn on u n watakaa kimyaa hata kama nii miaka kadhaa ijayo ila haya yote yatapita!
  welcome home girl n hope to see u around zaile area za kawa.
  1luv

 122. Neema Says:

  LATOYA YOU ARE THE WINNER,……wabongo muache majungu na uongo, Latoya hakufanya ngono alikiss tu na hao vijana wawili, na alimuacha mganda kwasababu mganda alikuwa anammisstreat….kama mnafuatilia mchezo Latoya anakumbukwa sana na tokea atoke mchezo umekuwa unaboa…show inaboa sana…na Latoya wamemtoa kwasababu Tanzania imekuwa ikishinda mara kwa mara so waliona wasipomtoa Tanzania itashinda tena….Yule mbotswana aliyekuwa nae kwenye rubbish dump ndio anakobolewa kila kukicha…..halafu mnasema Latoya malaya…..Ricco mwenyewe (Angola) anayetegemea kushindwa juzi alisema Latoya yupo juu mara tatu ya kwake na anashangaa kwanini viewers wamemtoa…..Huu mchezo umegeuka umekuwa politics…HABARI NDIO HIYO…….


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s