BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NGAPULILA-VIJANA JAZZ BAND September, 25, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 10:33 PM

Jinsi miaka inavyokwenda ndivyo hata mipangilio ya mwisho wa wiki inavyobadilika. Kuna nyakati watu walitumia muda mwingi wa mwisho wa wiki wakiwa feri wakijipanga vyema kwa mipango kabambe kuhusu namna ya namna ya kuzamia melini wakaibukie Greece kusaka maisha.

Hizo ndio nyakati ambazo nchi kama Marekani zilionekana za wazee na wenye pesa (kama alivyosema Sugu) huku vijana wakiamini kuwa maisha yanaanzia kwenye nchi ambazo zinafikika kwa meli hasa Greece. Bahati mbaya wapo walioishia majini na wengine kuteseka mpaka kufa kwa kukosa chakula. Unakumbuka nyakati hizo? Nyakati za kuamini kuwa huwezi ku-win maisha Bongo?

Hapa tunao Vijana Jazz Band enzi za “Pambamoto Shambulia” wakiwa na safu kamili na stadi ya kina Hayati Hemedi Maneti “Chiriku” , Eddie Sheggie “Fast Mover”, Shabani Yohana “Wanted”, Super Sax Rashid Pembe na wengineo wakielimisha jamii juu ya athari za uzamiaji kama aliokuwa akitaka kuufanya Ngapulila.Wimbo unaitwa Ngapulila.Pata Burudani,wikiend njema.

Ujumbe na burudani ya leo imeletwa kwenu na blogger mwalikwa,Mubelwa Bandio, anayeblog kupitia www.changamotoyetu.blogspot.com.Mtembelee.

Advertisements
 

21 Responses to “NGAPULILA-VIJANA JAZZ BAND”

 1. nchekube Says:

  mmmmmh! napata home sick jamani hebu siku ziende nirudi kwetu,R.I.P Manet.

 2. Pearl Says:

  matty,gervas,dunda galden,mama wa kichaga mie nawatakia wiki endi njema.
  any uko wapi mtu wangu husikiki jamani mpaka nakumiss shosti.
  binti mzuri,majita,edwin ndaki na wana BC wote natumaini mtaifurahia wiki endi yenu,tchao.

 3. EDWIN NDAKI Says:

  Kwanza kabisa namshukuru Mola kwa kuendelea kutujalia wote uzima na kuiona siku ya leo.

  BC kazi nzuri sana kutuleta kitu kutoka kwa Vijana Jazz Band ambao nakumbuka walikuwa wakisumbuana sana miaka hiyo na bendi kama Washirika Stars”watu njata njata”

  Ni kweli zamani watu walikuwa wakipa mishe mishe kuzamia Ugiriki na baadaye watu wakabadili upepo wakaanza kushuko bondeni ‘SAUZI’.

  Nawapongeza asilimia kubwa ya miziki ya zamani ilikuwa inahusiana na matukio yanayotokea katika katika jamii.Mfano mdogo kuna nyimbo zina hamasisha kuhusu kwenza ‘GEZA ULOLE’..mambo ya kuanzisha vijiji vya ujamaa badala ya kukaa vijiweni.

  Leo hii tuna mambo kibao yanayotukabili..asilimia kubwa ya wasanii wetu wanakuwa ‘bubu’ au waoga kutungia nyimbo sijui wanaofia nini?

  Mfano nilitegemea baada ya sakata la RICHMOND,EPA na ufisadi kwa ujumla nisikie lolote.Au nilitegemea baada ya mauaji ya aaibu ya wenzetu Albino wasanii waje na mipini ya kuelimisha jamii.Lakini matokeo yake asilimia kubwa wamekalia kuimba wamebana ‘pua’..(sio wote)

  Ila naamini bado tupo safarini wasanii wanakazi kubwa ya kuwakumbusha wananchi japo wajue tumefika kituo gani au ndio mwisho wa SAFARI.

  Nawatakia kile jema katika mapumziko ya wiki.Natumaini kesho MAN UTD watatupa faraja mashabiki wake..aaa aaaa lol..

  Binti Mzuri.Gervas,kekuu,mswahilina,Frateline,MzalendoMajita mwisho mwema wa juma.

  Matty baadaye basi kama saa kumi tuonane kwa Dani.

  Wengine ambao majina yenu hayajatokea hapa nawajali sana naninawatakia mwisho mwema wa juma

  TUTAFIKA TU

 4. Naam, BC haap ndio penyewe. Unanikumbusha mashindano ya bendi yalikuwa 1988 kama sikosei; nilikuwa mpenzi mkubwa wa Vijana Jazz wakiongozwa na Marehemu hemedi Maneti. Nilikuwa namkubali sauti ya Zeze Adam Bakari and Ngapulila was my favorite song… still one of my favorite songs ever. Aisee Jeff itabidi huu unitumie katika email.

 5. Edwin NDAKI Says:

  Pearl asante kwa ujumbe wako.

  nakutakia nawe mapumziko au libeneke jema la mwisho wa wiki.
  ..Mama wa kichaga,Dinah siku njema..

  Chris upo mbona KIMYA sana kama ANY?

  tutafika tu

 6. usinijue1 Says:

  sikia sauti ya maneti na shegy wakati kwambali kwenyekiitikio sauti ya adam bakari sauti ya zege ikisikika,ya old is gold nakubali nyimbo nzuri ujumbe wamaana kwa wale waliokua wanataka shortcut ya maisha enzi hizo…….hivi hizi bendi zasikuhizi hazisikilizi recodi za zamani maana wameng’ang’ania mapenzi tuuuuuuuuuuu na majisifu wakati jamii inapotoka

 7. Majita Says:

  Jamani wakuu wote,
  Nashukuru kwa salaamu za mwisho wa wiki na Ngapulia eeeh baba una hatari.
  Mimi mwisho wa wiki hii hasa Ijumaa hii kwangu ni ngumu kweli.Kuna litanzania lenzangu hapa nilipo limenikomalia eti Mccain kafanya vizuri kwenye debate wakati polls zinaonyesha Obama kafanya BORA zaidi.Yaani tumeshabishana hadi nafikiri hata nyie hapa mnasikia tuu hii sauti ya mabishano.Nimemkosa kosa kumtia kwenzi la kisogo lakini yeye bado tuu.Sasa ngoja niiendelee kukodoa mecho na majicho kwenye TV halafu nikitulia nile Ngapulila na kesho nirudi hapa nitoe komenti nzuri kabisa.Aidha wadau wote kwa sasa nawatakia week nenda kwa usalama.
  Ndaki,Pearl aka lulu,matty mama mkwe wa kichaga,binti “muzuri” na wengine wote tutawasiliana hapa hapa kijijini kwetu tulisakate rhumba

 8. Matty Says:

  Pearl shosti asante kwa kunitakia wknd njema!na mimi nakumwagia salamu zangu kuwa enjoy the wknd!

  Edwin Ndaki asante na wewe pia kwa salamu lakini tatizo lako kubwa ni kwamba umebadili no. au uneona watu wanabip sana nini???hahahahahahahaha!

  Asante sana BC kwa kibao mororo, pia nina ombi binafsi ukipata wasaa tutafutie msanii Marlow na vibao vyake kama Rita/bembeleza umhoji na utuachie sebene tuburudike maana mimi namzimia ile mbovu sasa sijui kama ombi litakubaliwa.

  Any shosti uko wapi??tunakumisi sana tu!

  Ujumbe wa leo!!!!!!!Wknd njema wote!!!

 9. Gervas Says:

  Jamani weekend ni nzuri na ndefu, maana ni mwisho wa mwezi afu ni Idd, Pearl asante na ninaomba uje na Edwin, Binti mrembo (mzuri), Matty na warembo wengine wote wa room hii. Maana sisi watu wa kule uswahilini siku ya sherehe lazima tuende baharini (Ocean Road) kuangalia bahari na kushangaa Melikebu.

  Frateline…tukutane pale Baraza basi, Mswahilina usisahau kuja na ndizi maana mambo ya mpunga si unajua tena. Bc na squad lake lote wakarishwaa…..

 10. EDWIN NDAKI Says:

  usinijue 1 unachosema ni kweli ..asilimia kubwa za bendi za leo ukisikiliza nyimbo zimejaa majina ya ‘mapedeshee,bar nk..

  Ndio maana mzee mzima Komandoo Hamza Kalala akatoa wimbo wake..Ngozi ya kitimoto haibwi ng’ombe

 11. Dunda Golden Says:

  Home sick BC.Pear salam zimefika nawe pia wiki njema pia nanyi Binti mzuri,Matty,Edwin wa Ndaki,Pandu na wengi wengineo.
  mwimbo huu unanikumbusha jirani yangu mmoja alietaka kuja ulaya lakini akawa muoga mala nyingi alikuwa akimulia yalimfika kaka Ngapulila wengi walifika na walioishia njiani walijitahidi safi sana kila la kheri maisha kokote maana hata Bongo mambo yanakuwa chicha si lazima uku….
  chai goda

 12. aisee ninasikiliza hiki kibao kwa mara ya 100 wikiendi hii n I can’t get over it. Next Jeff naomba Wanaushirika… Watu Njatanjata… Nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa vijana na Wanaushirika ndio walikuwa direct descendants wao; kina Sheggy, Kida… raha tu raha tu!!
  Shemeji yangu Ndaki inakuaje? Matty.. Blackmanne, Binti Mzuri (aisee inabidi tukutane dada); Any, mama wa Kimangi 🙂 …wikiendi njema

 13. RebbyGod Says:

  oohh I feel home sick pia!!! halafu huu wimbo umenikumbusha mambo mengi sana. Loh kweli nyumbani ni nyumbani. Thanx BC

 14. EDWIN NDAKI Says:

  Nalitolela,Ps

  Inabidi tukusanye sahihi za kushinikiza BC watafute kwa udi na uvumba wimbo wa washirika stars.

  Maana nakumbuka kipindi kile walikuwa wanatisha.Vibao vyao kama Julie.Kate na vinginevyo vilikuwa vikali sana.

  Natumaini Bc watatusaidia ilo zoezi liweze kukamilika mapema.

  CHAI GODA mi nitakuja kwenye hiyo shuguli nakutakia mwisho mzuri wa juma.

  Gervas yaani siku kuu lazima twende kutembea mtu wangu.Ila si unajua ninavyopenda kula ‘mfugo’ yaani lazima nistue leo.

  siku njema watu wangu..tupeane mialiko sio tunatosana dakika za mwisho.

 15. hombiz Says:

  Nawe..nami…bara mpaka pwani…..pambamoto………..shambuliaaaaaaaaaaaaa!!!!!
  Hii imekaa sawa.
  Uuuuups! Ngalula sijuwi yuko wapi hivi sasa! Sijuwi alisikiliza usia huu ama aliona wanamchanganya tuu akazamia zake. But you know what! sometimes it worth taking risks. Haya maisha ya BONGO ukiyalia “pose”, na maendeleo nayo yanakula “pose” vile vile!.
  Ila sijasema vijana muwe na mawazo ya kuzamia. Fanyeni kazi kwa bidii. Kila mtu awajibike kwa nafasi yake.
  TUTAFIKA TU!

 16. Ras Twin Says:

  Thanx BC. Hii ni njema saana

 17. Matty Says:

  Asanteni sana wote mlionitakia wknd njema, actually ilikuwa nzuri mno.
  Jamani IDD ndo hiyo tualikane washkaji!
  Amina vipi mwaliko nitapata???

 18. DUNDA GALDEN Says:

  Hamna noma mwana Ndaki unakaribishwa

 19. binti-mzuri Says:

  heh jamani,i havent been around..thanx wote kwa salamu!much appreciated!!!!.. weekend njema

 20. nyimbo ni ka hizo.wakati wa mwisho wa wiki nikiwa mombasa 1999,saba saba club.
  Obama tunakuombea kila kujao,Mungu wako yuko.

 21. peter raphael Says:

  nitaomba baadhi ya nyimbo nyingine za vijana jazz, kama ogopa tapeli, magaidi wa msumbiji, unijali kwa chumvi,

  nitashukuru kama nitatumiwa kwa email hiyo


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s