BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WANAMUITA MR.BLUE September, 28, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 10:58 PM

Wimbo uliomtoa ulikuwa ni ule uliokuwa ukiinadi rangi ya blue.Pengine ndicho chanzo cha yeye baadaye kuja kujulikana kama Mr.Blue.Pamoja na hayo wimbo wake ulioitwa “Mapozi” ndio ulikuja kutamba kwa staili ya aina yake.Baada ya hapo ikawa ni mapozi nawe,mapozi nawe.Lakini kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya anabakia kuwa Mr.Blue.Hivi karibuni alikuwa katika ziara ya muziki nchini Uingereza.Ni miongoni mwa vijana walioko katika fani ya burudani kupitia muziki nchini Tanzania ambao wanaweza kusema “wanafanya vizuri” katika wanachokifanya.

Mcheki hapa chini katika wimbo wenye ahadi nzito nzito za kurejea kulifuata penzi.

Photo courtesy of Abdallah Mrisho

Advertisements
 

74 Responses to “WANAMUITA MR.BLUE”

 1. kahindi Says:

  Jamani kajamaa kametulia alafu kana kipaji somehow…hivi BC nilickia ati aliacha shule kwa ajili ya umaarufu…je hebu niambie amerudi school?kama bado namuomba amuige mwana fa plz…vinginevyo mimi namkubali na haswa kwa ule wimbo wake wa MAPOZI NAWE WE NA MAPOZI NAWEEEEE….

 2. EDWIN NDAKI Says:

  selebrity wa leo bahati mbaya ni mgeni kwangu.SIMFAHAMU mchango wake katika game.Ila inaonekana anakuja vema vema.

  Achilia mbali picha aliyopiga imejitahidi kunipa picha…yupo katika kundi la ‘umri’ gani na hata mtazamo wake kimaisha unaweza kuwa katika ‘umri’ gani.

  Kwa wadau wengine wote wa tz..poleni sana kwa sisi tusikuwa na umeme.Najua sehemu kubwa ya nchi ipo kwenye giza tororo sijui na bongo wameingia kwenye kipindi cha ‘otumu’.

  Najua kuna wadau wengine maoni yao tutayakosa kwa muda huu wa mgao ..ila Inshaalaah Mungu atasaidia umeme utarejea karibuni.MAISHA BORA NDIYO HAYO.

  Tupige kazi kwa bidii,wa kusoma wakamue kwa bidii..ipo siku nawaambia ..TUTAFIKA TU kwenye ile nchi yetu ya ahadi..ila sio kupitia hawa wanasiasa.

  Siku njema

 3. mtajiju Says:

  Ndugu yangu hiiyo ni tatoo au umechora na peni msuli huna basi kichekesho mtindo mmoja

 4. Matty Says:

  kipaji unacho …but, u need to go back to school kijana!!

 5. Gervas Says:

  Bado safari ni ndefu…..na sijui kama tutafika. Labda wasanii/producers wajaribu kumix beats na style za mziki wa kiasilia na huu wa kizazi kipya. Lakini miziki hii tuliyonayo inakuwa na market ndani ya nchi tu and not beyond that. Wasouth Afrika ndiko walikoibukia. Mfano Saida karoli alianza na idea hiyo, sijui kaishia wapi. Wasanii wetu wanakalia tu kulundika albam, mwingine kwa miezi mitano anakuambia ana albam tano na kulalamika kuwa watanzania hawanunui kazi zao….. tujiulize miziki yenyewe inauzika?

 6. Ed Says:

  Thanks God ubalozi wa Marekani unakatalia visa hawa watu. Hebu imagine hawa watoto wangekuwa wana hang kwenye suits za ATL au Htown?
  Hizi Hardcore tattoo kama mwizi… For god sake what is wrong with youngstars in Tanzania?
  When i see that i feel like throw up…..

 7. usinijue1 Says:

  hivi huyu bwana mdogo shule ndio basi tena ama vipi,maana sijawahi kusikia swala la kujihusisha na elimu

 8. 1st lady Says:

  Thanks BC u made my day,nampenda sana huyu kijana,go blue

 9. Mzanzibar 100% Says:

  Waswahili wanasema ” Ujana ni nyonjwa, kila mtu huonja…” Huyu naye (Mr Blue) anauonja ujana kwa “style” yake! Maana wengine husema ujana ni nusu ya uchizi.. huyu naona ni robo tatu (3/4)ya uchizi! Ndio ujana ni maji ya moto ukiyachezea yatakuchoma, huyu mwenztu hayako mbali kumchoma, kama hayaja mchoma…! Ameacha shule kwa ajili ya kubana puwa (kuimba), mziki wenyewe wa bongo una ng’ara msimu mmoja msimu ujao uko nje ya game, ukishindwa kujipanga vizuri ndo ntolee tena..!

  Huyu anahitaji mshauri kabla mambo hayajazidi kumharibikia…!

 10. Edwin NDAKI Says:

  BC chonde chonde.

  nakuomba unisaidie au mtu yoyote anipatie wasifu wa huyo dogo.

  naona wadau wameanza ooh..kaacha skuli kafuata umaarufu..SIAMINI KAMA KWELI KIJANA KAMA HUYO ANAVYOONEKANA NA UPEO MKUBWA aamue kuacha shule kwenda kubongoka flava.

  kama kweli dogo rudi shule..plz BC NAOMBA MAHOJIANO ya MR BLUU kama yupo tayari kutoa ushirikiano.

  kila la kheri mr bluu

 11. Habasoda Says:

  kijana aende gym atengeneze mwili asiwe kama dem, miili hutengenezwa haiji yenyewe.

 12. Dinah Says:

  Enzi zetu miaka ya 70s kwenda shule au kusoma ikuwa ni wajibu (labda kwa vile Elimu ilikuwa bure) tofauti na siku hizi.

  🙂 nilisikia wazazi wa Kibongo wakilaumiwa kuwa wanawalazimisha watoto wao kusoma au somea masomo fulani hata kama watoto hao hawapendi shule.

  Ikadaiwa kuwa “wazungu” (kitu ambacho sio kweli)huwaachia watoto wao wachague wanataka kufanya nini kwenye maisha yao hali inayowafanya watoto hao kuwa na maendeleo (inategemea anafanya sanaa gani) sasa basi huenda wazazi wa huyu kijana wamejaribu kuwa “wazungu”.

  Nakubaliana na wote wanaoshauri dogo arudi shule, lakini napenda kusema kuwa anajitahidi sana kwenye sanaa anayoifanya.
  Eid njema….

 13. DAYDREAMER Says:

  Dogo babu namkubali ….mbona mzuka..hana magumashi wala nn!!!!makamuzi yake n mwendo wa kujimwaga tu.
  kip it Blue…

 14. tongenyama Says:

  Bwa’ mdogo anaimba vizuri, anachoniboa tu ni kwamba hataki shule. Nenda shule mdogo wangu utrakapo zeheka hakuna atakaye nunua mziki wako, utabaki umechoka kama shaban dede.

 15. kekue Says:

  Anajitahidi sn, ila rudi shule coz ni muhimu u still young bwa mdogo.

 16. Winnie G Says:

  kaka Ed na MAtty,

  Mimi nashukuru kwa comment zenu. Unajua mimi nacheka sana nikirudi home na nikiona vijana wanavyojaribu kuiga MAblack Americans; mimi naishi Europe ila naenda sana USA na najua matatizo ya Black Americans moja wapo hawaendi shule na pia ni masikini WA KUTUPWA JAPO sio wote but the majority..

  sasa vijana wetu wakiweke Tatoo ndio wanajiona ma nigger sana it makes me so sick…

  kaka yangu na mimi pia nashukuru kwamba US embassy haiwapi visa maana hata kama wanascholarship wakifika USA wataingia mtaani na kuwa majambazi na kuuliwa na polisi kama manigger wanavyokufa..

  Kuhusu huyu mwimbaji;

  mdogo wangu nenda shule, take an example ya waimbaji wenye degree zao wale wa jirani hapo Kenya..kumbuka muziki wa Bongo haulipi kabisa…pole kwa comment yangu ya wazi..

 17. sisterTZ Says:

  Mimi nimechoka kuona vijana ambao shule hawataki ndio wanaingia kwenye fani ya muziki kwa mtindo huo ndugu zangu muziki wa bongo hauwezi kuendelea kabisa..

  hao mapromota wenyewe ndio matapeli kabisa.. sijui kama tutafika. Namkumbuka sana dada Saida Karori jamani huyu dada anakipaji lakini sijui ilikuwa walimtapeli mpaka sasa hatujui yupo wapi…

 18. r.k togolai Says:

  hivi jamani jina lake halisi ni nani !

 19. Olive Says:

  Shule muhimu..but u r gud!

 20. Matty Says:

  Wabilah Toufiq! barakatu la idd all of you guys! am taking this opportunity to wish you all the very best in all your endeavours,though BC umetunyima kibao cha idd.members pls receive greetings from me!
  Any,
  Amina,
  Kekuu,
  Mama wa Kichagga,
  Pearl,
  Olive,
  Halima,
  Binti-Mzuri,
  Ramla,
  Queen,
  Pendo,
  Kahindi,
  E.Ndaki,
  Chris,
  Nalitolela ps.
  Black manenn,
  Mzanzibar 100%,
  Gervas,
  Hombiz,
  mtajiju,
  Majita kidogo nikusahau hahahahahaha najua ungedai salamu za Idd tu
  BC WENYEWE PIA

  Jamani niliowasahau so sorry nina haraka sana!

  May Allah Subhanahu bless you all with joy, health, peace, prosperity and the warmth & love of all dear ones always.

 21. kekue Says:

  Wana BC wooooooooooote nawatakia idd njema, mshereheke kwa kiasi, lile jungu lililovunjwa lijengwe upya, hahahahaaaaa bc umetusahau na sie ungetuwekea japo kaswida tuselebuke na idd!!!!!!!!!!!!

 22. EDDY Says:

  WIMBO NI MBOVU, KWANZA HAENDI NA BITS NA KISWAHILI KIBOVU, HILO NI TATIZO LA KUTAKA KUMALIZA KUYATAMKA MANENO YOTE KATIKA WIMBO KITU AMBACHO WABONGO WENGI WANAKOSEA SI LAZIMA UTAMKA NENO LOTE KATIKA MUSIC, MUSIC NI SANAA, AND ENTERTAINMENT, LAKINI HAPO AMEIMBA VIBAYA SANA NI MBOVU SIJAPATA ONA

 23. xxx Says:

  tattoo ya korosho hiyo..kwi kwi kwi!

 24. hombiz Says:

  he needs to go back to school! He better waste no time neither!

 25. Majita Says:

  Matty kidooogo nibomoe hii screen kwa kichwa coz kusahaurika tena ingekuwa noma.Nilikodoa “mimajicho” roho ikawa inapwita ninajisemaea rohoni “nimesahaurika” hahahaha

  Haya wewe dogo watu wote tunasema S H U L E.

 26. Bob Sambeke Says:

  Oya Mbona wote mmechangia ande shule! Me naenda Tofauti kidogo…Me Namwambia Ajitahidi kufikiri baada ya miaka kumi atakuwa vipi? Akipata Jibu Ndo Alifanyie Kazi..Unaweza Ukaenda Shule Ukawa na maisha ya kawaida..Mr.Blue Yupo Darasa La Saba Lakini Ananipita Hata Mimi kwa hela wakati me nina Degree! Mbona Prof.Jay hana Degree,Lady Jay-Dee Mbona Form 1V Lakini Ana Hela Zaidi Ya MILLION 500Tsh,Ambazo Nynyi Wabeba Box Hamtozipata Mpaka Mnakufa na Midegree Yenu Hiyo,cha msingi tumshauli kwamba achukulie mziki kazi ili aje kufanikiwa..Duniani Kote wenye hela ni watu wa mabizness na co wenye elimu 2 kazi kusubiria mshaara,mshaara wenyeye Gros 900,wakikata kodi na nsss unabaki na laki7,hiyo laki7 unaweza kupush vogue?
  Acheni ushamba nyie…Aende Shule akajiendeleza na co kama aciposoma ndo hatafeli maisha..Mbona anamaisha mazuri 2,,Ana gari 2,ana nyumba yake fresh..
  Habari ndio hiyo Haters

 27. Bob Sambeke Says:

  E bwana cha msingi mtu uwe na hela.Mbona Maprofessor Wengi Wapo Na hawana hela wanayo hela ya kula tu?

  Hivi Unaweza Kumlinganisha Professor Luanga na Lady JD kwa Hela?

 28. Hombiz Says:

  Bob Sambeke kweli wewe ni kichwa cha panzi! Hivi bado tu haujafahamu kuwa “mali bila daftari huisha bila habari!”. Elimu ni hazina ya aina yake. Elimu unaweza kuifafanua kwa kauli nyingi zenye kuleta maana. Kwa mfano:
  1. Elimu ni ufunguo wa maisha
  2. Elimu ni ujuzi unaomuwezesha binaadamu kuyakabili na kuyabadili mazingira yaliyomzunguka ili yaweze kuwa bora zaidi
  3. Elimu ni kitegauchumi
  4. Elimu ni siraha ya kupambana na njaa, ujinga, na maradhi.
  Hizo ni baadhi tu ya definition za haraka haraka juu ya elimu.
  Kumbuka wachumi walisema “life is full of uncertainty. You never know what will happen to you”. Even if you have billions of money in the Bank, you still need some type of security (education) in case anything happens to your finance. Mfano mzuri ni hii hali ya kuharibika kwa uchumi wa marekani hivi sasa. Watu wengi waliokuwa matajiri wamepoteza pesa zao, nyumba zao na sasa ni malofa wa kutupa. Sasa wale walio na elimu zao kichwani, zitawasaidia kuanza tena kupambana na maisha from the scratch kwa kutafuta kazi na wakizipata kuzifanya kiufasaha. Lakini kwa yule aliyekuwa na pesa nyingi bila elimu, huyo itakuwa vigumu sana kuyaanza maisha from the bottom all the way up. Vile vile kumbuka, vipaji vya sanaa (muda mwingi) havidumu milele. Wasanii huvuma sana na baada ya muda Fulani huchuja na kupolomoka. Ni wachache sana wanaovuma for the life time. Therefore, education is important. Tazama Mr 2. Alivuma na mwisho akachuja na sasa yuko marekani anaitafuta elimu ambayo hakuwanayo hapo awali. Sasa heri yake yeye aliyeweza kupata nafasi hiyo ya kusoma hivi sasa. Na pia at least alikuwa na pa kuanzia kwani tayari alikuwa na elimu kidogo. Sasa anngekuwa hana kabisa, sijui ingekuwaje.
  Come on Bob Sambeke! Be realistic about these things dude!

 29. majita Says:

  Kwako BOB SAMBEKE,
  baada ya kusoma bandiko lako hapo juu,nimegundua kuwa ama hujui maana ya Elimu au maana ya tajiri au kuwa na hela.
  Mifano yako unayotoa ya profesa sijui nini mwenye hela ni mfu.
  Tunapokuwa tunasema mtu fulani ana hela nyingi maana yake ni kuwa kuna uwiano wa hela yake na mahitaji yake.Hakuna kiwango chochote duniani ambacho kimewekwa ili mtu akikifikisha basi na yeye anajulikana kama tajiri.

  Bob Sambeke,nakupa mfano:- Nilipokuwa mdogo kule kijijini kwetu Majita kulikuwa na tajiri SANA.Alikuwa anamiliki vitu vingi hadi akawa amenunua baiskeli yake ya Phoenix mpya na watoto wake wote walikuwa na baiskeli za swala.Tulimuona tajiri sana na duka lake pale kijijini.SIFA zikamulewesha,akaenda Musoma mjini.Guess what??nafikiri unajua jibu.Yaani baada ya kufika Musoma mjini yeye na baiskeli zake alikuwa kati ya watu masikini.Hapo Musoma akatokea tajiri mwingine tena.Yeye alikuwa na gari zake.Nae akaondoka akaenda Dar,ile kufika tu Dar wala hakuhesabiwa kati ya Matajiri.Sasa endeleza huo mlolongo hadi ulipo na ulinganishe na tajiri wako.

  Tunapozungumzia ELIMU kwa huyu bwn mdogo ni ili tumsaidie awe na upeo wa kuelewa mambo.Bob Sambeke una-sound kama uko nje ya nchi.Hebu nambie mwanamuziki wa kimarekani ambae ana Elimu kama ya huyu bwn blue.Kwa bandiko lako hili naku dadicate mwimbo wa “GRADUATION” wa Kanye West.
  Pia sikuachi hivi hivi,nakupa kazi ya ziada ya kutafuta maana ya neno Elimu na Tajiri.
  Wasalaaamu.
  Majita

 30. Bimkubwa Says:

  Hombiz, Umenena!!! Nashukuru kwa kuandika ujumbe huo. Vijana wengi sana bongo wamebaki kujifananisha na black americans na kujipa false hopes in the amount of money they have in the bank.
  Yardsticks wanazotumia kwa kujipima maendeleo nazo ni hoi vilevile.
  Bob Sambeke usimdanganye mtoto wa watu. Uwezo wake ni mdogo sana kuhimili mabadiliko ya uchumi na maisha kwa ujumla. The poor boy has a backbone which can only last him 5 more years if he is lucky. What next?? the boy ain’t 25 years old even !! Do you think those 2 used vehicles and a house will secure his future? The future of his family? Think again.
  Lady JD and mr Blue are in two different leagues. JD has corporate support and power, Mr Blue has none of that. Let him go back to school and polish the minute knowledge he has.

 31. Mina El Faidhina Ustaadhi Matty. Na kwa wote mliobaki… Eid pilau kwangu bwana (kama unakujua na unaweza kufika)…. vinginevyo mkono wa Eid nitawapa tukikutana hahaha.

  Edo naona uliondoka kitambo na bado hujarejea ku nyumba. Dogo huyu bwana ni bwana mdogo sana, kiumri na kifani.. si wa zamani. Alianza kuwika kipindi sipo Bongo.. nikaenda likizo 2004 nikakuta yupo juu na kibao BLUE BLUE. Niliikubali kazi si kitoto mzee. Mara akaja na mapozi, then Nipo, n.k.

  Kwa ushauri.. uwe unafuatilia youtube track mpya na pia waulize ndugu jamaa na marafiki popote walipo Tz.

  By the way waungwana… nimekumbuka kipindi cha KLABU RAHA LEO… SHOOOWWWWWWWWW!!!!!!!!!! hahaha.. old skool eh?

 32. sexycecy Says:

  BOB SAMBEKE INAONEKANA NA WEWE HAUJASOMA
  COZ HAUWEZI KUTETEA UJINGA KAMWE HUWEZI
  MLINGANISHA MTU MWENYE ELIMU TENA PROFFESOR
  NA LADY JD PESA SI KILA KITU KATIKA MAISHA
  UKIWALINGANISHA WATU WAWILI KAMA HAWA
  NI KAMA UNAKUWA UPOTEVU WA NIDHAMU
  PROFFESOR NI PROFFESOR
  HUYO LADYJD NA PESA ZAKE KUNA MAMBO MENGI
  YUPO NYUMA KIMAISHA PESA CANT BUY YOU THE WORLD!
  MTAKE RADHI PROFESSOR LUANGA

 33. Mh Lukamba Says:

  Kumbukeni UFUNGUO una FUNGA na KUFUNGUA,Huu usemi wa kusema elimu ni ufunguo wa maisha !!!!
  wengi wemefungiwa na fungo Elimu,kwahiyo ni kijana kujipanga tu,ukiwa na hela unaajiri wasomi waprogram maisha yako!!!!
  wabeba box wako wengi na degree zao,Pata hela,tangaza ajira uone,watakavyomimina mibarua,wote wamechoka na kazi za box

 34. Pearl Says:

  matty shosti asante kwa salaam za idd

 35. Mimi Says:

  Oh God help these people from Ignorance. Humu wamo wasiojua wanachokisema na wengine wanosema mambo coz ndivyo yasemwavyo na wengine.

  Guys you need to understand what you are looking for in life kabla ya yote. Kama unataka kuwa daktari lazima uende darasani mana udaktari si kipaji ni shulee, vivyohivyo kama wataka kuwa na fani nyingine. But it does not mean lazima kila mtu awe na degree duniani!!! Huo ni ulimbukeni na ushamba wa mambo. Waloenda shule wakapata fursa ya kusoma falsafa watakuwa wanajua kuwa Aristotle alishasema kila mwanadamu anatafuta furaha. Happiness ndio ultimate goal ya kila mtu. So ni njia gani utaipata ni kupitia mambo mengi lakini dunia imeamini usipokuwa na pesa huwezi kuipata. So money is just a means to achieving happiness. Sio shule sio kuishi ulaya.

  In other words i support what this young guy did as long as yuko fucused. Kuna wajinga wengi tu wanasoma coz baba ana ada ya kumlipia lakini hana dira, na at the end of the day maisha ni misery kwake tu. But wapo wengi wamefanikiwa bila kwenda vidato viiingi maadamu wamepata universal primary education ya kuwaongoza maishani.

  Kuna mwehu mmoja hapo juu anasifu marekani kuwanyima visa na anashoboka na mitaa ya US as if kwao..sasa mtu kama huyo atamshari vipi Blue kusoma wakati kama yeye amesoma ndo akili yake imeishia hapo??? Jacko Wacko alianza music at 13 years sijui kama alikuwa ashagraduate by then na sijui kama graduates wa kibongo kuna anayemzidi hata housegirl wake kipato.

  Acheni ufinyu wa mawazo tuliosoma its for us and our children, waliojaliwa vipaji they have equal chances to win better life. Huyo anayejidai kasoma na yuko US kubeba box na kuosha vyombo hotelini hawajui akina Lil Wyne na Cash money nzima, 50cent, wote waliokimbia shule but wanaishi kama wafalme???

  Blue you keep yo head up …you have a bright future son.

 36. any Says:

  Bob Sambeke ungekuwa jirani ningekupa lager mbili! kila mtu kakomalia shule shule, si kila aendae shule ana mafanikio, wapo walioenda shule na wanasaga lami mtindo mmoja, kutwa kucha wamebeba tumifuko twa karatasi tuna CV ndani, kama yeye kachagua mziko ni his option! matty uko wapi na personal decision ya mr blue. haaaaaaaaaaaaa. weekend njema.

 37. machame Says:

  kijana anajitahidi lakini kitu muhimu ni kumix ngoma za kinyumbani na za kisasa na pia kuacha kujiweka kimarekani maana wamerekani hawatanunua nyimbo zako lakini sisi wa nyumbani tutanunua. Kama shida yetu ni kusikiliza wasanii wanaofanana na wamarekani basi hatuna haja kusikiliza wenzetu bali wao wenyewe.

 38. any Says:

  Matty asante kwa salam za idd, nashukuru nimekuwa wa kwanza kutajwa kwenye list, thanks mami

 39. neema Says:

  mdogo wangu umependeza sana .but do me a favour….. go back to school get your GED……..We love you hommie dont think we hates you…. No matter what go west or south.. Diploma fir…………..st……….., No body going to ask you about
  tatoo,the gona asking you where the white paper not tatoo.
  where are you now, wake up hoooommmmiiiiieeeee
  Much love hommie

 40. hombiz Says:

  Shule inabaki kuwa ni jambo muhimu hapa!. Nyie wote mnaopinga swala hilo vigezo mnavyovitumia, haviingii akilini kwangu hata kidogo. Kama nilivyotanabaisha hapo awali, elimu ni jambo muhimu sana ktk maisha ya mwanadamu. Mchangiaji # 30(mimi),hapa kinachoongelewa ni umuhimu wa shule kwa hawa vijana wadogo waliojikita kwenye fani ya bongo flavar bila kuipa elimu kipaumbele. Swala la furaha hiyo ni topic pekee inayojitegemea kabisa. Unaweza kuwa apechi alolo na bado ukawa na furaha. Kwa mfano, kuna documentary niliangalia kwenye TV ambayo ilionyesha maisha ya bush man ambao hawajasoma kabisa lakini wanafuraha na maisha yao ile mbaya huko polini. Ila wangekuwa wamesoma, pamoja na furaha yao, elimu ingewasaidia kuyakabili na kuyabadili mazingira yao na kuwa bora zaidi kulingana na wakati. Pia kwa taarifa yako Michael Jackson yuko kwenye matatizo makubwa sana ya kifedha kutokana na matumizi mabovu ambayo bila shaka yanachangiwa na ufinyu wa elimu yake. He has a billionaire’s spending habit, but a millionaire’s budget. Michael is” a “spendaholic” who racked up $35 million in annual bills while earning just $12 million a year. Sasa angekuwa na elimu nzuri kweli angefanya ujinga huu wa mali bila daftari?.
  Kwa mdau aliyezungumzia visa ya marekani, huyo sijui ana maana gani. Nnavyofahamu mimi ni kwamba ubalozi wa marekani haumnyimi mtu viza kwa ajili ya kuwa msanii wa bongo flavar na sababu nyingine zisizoleta maana. Sababu pekee wanayompa mtu visa ni kutimiza matakwa yao. Kama hutimizi matakwa yao, basi hawampi muombaji viza. Huo sio ukweli hata kidogo.
  Wakati huo huo mchangiaji namba 30, sio kuwa kila mtanzania aliyesoma anayeishi marekani, anaosha vyombo hotelini kwa wazungu na kubeba box. Kuna watanzania wengi wasomi wako Marekani Kaskazini ambao wamesoma vizuri na wana kazi nzuri sana zinazowalipa vema kabisa.
  Swala la kina Lil Wayne na wasanii wengine wengi ni kweli ma-milionea. Lakini kwakuwa shule haipo kichwani, basi na matendo yao yanalingana na uwezo wao waufahamu. Ndio maana wengi huishia kwenda jela kwa uhalifu wa kijinga na wengine hufilisika kama Mc Hammer.
  Ngoja niishie hapa kwani siwezi kumaliza hii topic nnayopenda kuitetea kwa nguvu zote.

 41. Matty Says:

  mhh hii kali!
  Any nipo mamangu wewe tena lazima uwe wakwanza kwenye salamu zangu aisee, ila hz personal decision za MR.BLUE NI BALAAA!!ngoja kwanza na mimi nimtapikie bob sambeke!
  anyway BOB SAMBEKE umeraruaraua hasira zako lakini mshamba ni wewe unayeropoka tu sijaona point hapo, hv ingekuwa ni mwanao huyo ungemshauri afocus mbele ipi??without education?au kwa kuwa ni mwana wa mwenzio??
  Tunachosema umri mdogo anatakiwa arudi shule, mambo mengine baadae KAMA kitabu kikidunda poa tu atasaka life kwa kubana pua, suala ni kuwa AMEACHA SHULE SABABU YA KUFLOOOOOOOOOOOOOOO (MZIKI)
  HOMBIZ umemaliza KAKA! Bob Sambeke get a life!

 42. trii Says:

  watu wanavyo jifanya kuijua US hatari,utadhani walizaliwa huko.mr blue we kamua,kama muziki unauwezo wa kukupa hela za kujenga/kununua nyumba,mlo wa kila siku,kuwa na kagari kamoja ka kuzungukia hapa na pale,kwa kifupi maisha mazuri,we endelea,kama show 1 inauwezo wa kupata mfano Million 4 poa sana, mtu unafanya kazi mshahara kwa mwezi laki 2,hiyo M 4 itafika lini si miaka?

 43. trii Says:

  unaweza pia kusoma ukiwa home na siku ya paper unaenda kufanya au hadi uvyae uniform ndo wajue unasoma?watu wote tuna tafuta pesa,cha muhimu uweze kusoma+kuandika+kuelewa.kama muda huu ndo channel za pesa zipo wima sasa plzzz bora utafute kwanza, elimu haina mwisho kama unania ya kusoma utasoma tuu hata gumbaro. pesa tafuta ukiwa kijana,uzee kupumzika.

 44. Frank Says:

  huyu bwana mdogo kwa nini katika kila picha anayopiga ni lazima abetue midomo…mara ajing’ate, mara arambe ulimi, mara sijui afanye nini…..mimi sijui kwanini labda waungwana mnielimishe kwamba ameshauriwa afanye hivyo kwani ndio anapendeza au vipi……

 45. Bob Sambeke Says:

  CHUKUA HII

  1.Habari Zenu Wabeba Box,Hombiz,Majita,sexycecy,bimkubwa,matty na wengine wanaonidiss me kwenye comments na kumdiss

  blue kwa uamuzi wake
  2.Big Up Mh Lukamba,Mimi na Any kwa kuwa na mtazamo mkubwa wa maisha wa kuangalia pande zote za shilingi na co ao

  wenye mitazomo ya mwaka 47.
  3.Nyie watu kumbukeni Elimu ni pana sana na co mnavyofikiria.Kuna 4mal and in4mal education nadhani mlitambue hili

  wazeya.inawezekana kabisa mr blue asiwe na 4mal education hiyo mnayong’ang’ania ya kukariri madesa but akawa best kwenye

  in4mal education ambayo inamuwezesha kukabiliana na mazingira halisi kumbuka hata charles Darwin alisema kwamba “It is not

  the strongest of the species that survives, nor the most intelligent, but the one most responsive to change” kama wewe unafikiri

  kwamba ukisoma ndo maisha utayaweza kweli wewe utakuwa una upungufu wa kufikiri kichwani(UKUKI) hata mari andrreti

  anakwambia “If things seem under control, you’re just not going fast enough.”,Life its all about challenge and how you overcome

  those challenge me nampa 10 na co 5 mr blue…Keep it on ..hustler
  4.Na wewew hombiz unaongea pumba tu..Ushawahi kumuona m2 anapush vogue kwa kutegemea mshahara wa kila mwezi,acha

  ujinga wa mawazo Kila m2 atafanikiwa endapo atakuwa serious kwa ki2 ambacho anachokifanya,big up mimi kwa kuwaeleza kuwa

  kuna specialization co kila m2 awe na degree ona 50 cent ajaenda shule lakini he the richest rapper ever na anabuni miradi

  mbalimbali sasa anatumia nini kubuni hiyo miradi wakati shule ana? you get my point
  HABARI NDIO HIYO

 46. halima Says:

  matty al faidhina best duuh umeona wadau walivo na hasira? frank ndugu yangu hizo ndo poz za wanamuziki wetu wa bongo flavour, wangekuwa na uwezo wangeng’ata hata masikio.

 47. Matty Says:

  Bomb Sambeke!
  Relax ma dear unakuja kiswahili swahili sana mbona???
  Hakuna nini wala nini dogo arejee shule thats all!hakuna changamoto yoyote ile ya kufikirisha bila kuwa na elimu hasa kwa dogo kama huyu BLUE, labda kama tunasadikika na never hawezi kujifananisha na hao kina 50 cents kimafanikio.

 48. Hombiz Says:

  Bob Sambeke! Tatizo lako ni: “hujui kwamba hujui”. Ingekuwa afadhali kidooogo kama ungekuwa, “unajua kwamba hujui!” Na ni jambo baya saana kumpigia mbuzi gitaaa!. Kwani akitikisa mkia wewe utafikili anafurahia milindimo ya gitaa lako kumbe mbuzi yule anafurahia utamu wa majani.
  Education is the vision for one’s eyes to see the world:
  Education encompasses teaching and learning specific skills, and also something less tangible but more profound: the imparting of knowledge, positive judgment and well-developed wisdom. Education has as one of its fundamental aspects the imparting of culture from generation to generation . Education means ‘to draw out’, facilitating realisation of self-potential and latent talents of an individual. It is an application of pedagogy, a body of theoretical and applied research relating to teaching and learning and draws on many disciplines such as psychology, philosophy, computer science, linguistics, neuroscience, sociology and anthropology. Nashukuru wadau mnaothamini elimu kwa kujaribu kumshauri huyu bwana mdogo. Shukrani zangu ktk hoja hii ziende kwa wachangiaji wafuatao:
  Matty, Usinijue, Mzangibari 100%, Edwin, Ndaki, Dinah, tongenyama, kekeu, Winnie G (ingawa sikubaliani na wewe “Winnie G” ktk swala la kuwanyima viza za U.S.A. vijana wa Tz), Sister TZ, Olive, sexycecy, na neema. Kwa wengine waliotoa hoja za kupinga swala la elimu, nasema “shame on them!”. Natarajia mtalitazama swala hili upya na kuepusha kutokea kwa disfunctional families ktk maisha yenu!
  Always,
  SHULE KWA KWENDA MBELE, HAKUNA KUKIMBIA UMANDE!

 49. Bob Sambeke Says:

  Tatizo nyie wa2 wa madesa mnakasumba nisome nipate kazi niwe na maisha mazuri lkn ukimaliza unasaga lami we mpaka sole zinaisha,mvua na jua lako,kila siku upo barabarani na mifuko ya kaki..Na ukija kupata kazi ,kazi yenyewe gros 200-900usd.Then kwa mshaara huo unaweza ukatoka na maisha haya.kwahyo utaona wa2 wengi wakiajiriwa wanatafuta dili za umo ofcn kwao ili waweze kuinua kipato,ndo wanaanza kuibia mashirika na makampuni mengine.

  Kwa wa2 kama ao elimu inawasaidiaje,we utaibaje kwenye kampuni au shirika unalofanya kazi we auni ndo mwanzo wa kulifirisi shirika?

  Mr.Blue Komaa na gemu,kwani kusoma mpaka uvae uni4m na utangaze kwenye magazeti unasoma kuna open school kibao
  kwahyo we komaa…Dogo unatisha full respect unawapiga bao wa2 kibao wakiwemo wabeba box ndo wanaokudiss sana kama ukichunguza…Inakuwaje we una nyumba wakati wao wanalala chumba kimoja wa2 10..Halafu wanatuma maemail hooo nina maisha mazuri sana huku kiwanja,kumbe hamna ki2 chochote! Kila m2 ana nafasi ya kuwin no matter umesoma au ujasoma?
  Y’ all heard ..Matty na wenzako

 50. Lil Thug Says:

  cn u email me on arianeu94@hotmail.com
  plz!!!!!!!!!!

 51. halima Says:

  Wewe unaejiita bob Sambeka huo ushauri naona kama unawafaa ukoo wenu wote ni vizuri kama utawashauri kizazi chako chote kisiende shule ili baadae waje kuwa kama 50 cent. HABARI NDIO HII

 52. kahindi Says:

  Matty…..aksante kwa salaamu za eid

 53. binti-mzuri Says:

  hhaha kazi kweli kweli!

 54. any Says:

  Matty huenda alishajipima akaona akienda school atazungusha, so akajiwahi sekta ingine! unless kama alifaulu kabisa kuendelea akagoma,. mi simjui background yake, so i cant say much!

 55. nditu Says:

  Dogo, Elimu ni muhimu, pesa utazipata, zitakwisha lakini ukiwa na elimu ni hadhina kubwa. Popote utapokelewa lakini ukiwa ignorant nani atakuchukua?

 56. Amina Says:

  du ishakua soooo

 57. kukuwakienyeji Says:

  Hicho kitoto kimeanza kuota ndevu.tumekilea naona sasa kimeanza na kutunisha misuli.Ila big up dogo.kusoma nini.dodo ame identify mziki kama proffessional na anakipaji.mwacheni aendelee.graduate analipwa shilingi 300,000 take home ktk nchi ya Tanzania.wakati dogo akifanya tamasha moja basi ana uhakika wa zaidi ya 500,000.na halipi kodi.acheni usenge.tatizo mmzoea kwamba kila mtu atatoka na shule.

 58. matty Says:

  Bob Sambeke!
  hahahahahhahahahaa hujui kama hujui tu na utabaki kutojua tu!Hombiz chukua big 5 umemaliza!
  Utaweza iba vipi bila ujanja kichwani hata mafisadi wa EPA, RICHMONDULI pia wamesoma.
  Acha zako wewe bob sambeke dogo arejee skonga tu!

 59. kahindi Says:

  nditu kiswahili sanifu…hazina na si hadhina,upoooo?

 60. mss Says:

  kula 10 mtu wangu halima kweli huo ushauri unafaa kizazi chake chote, naona ameshaanza kwake siunaona hata mawazo yake ni ya mtu ambaye hajaenda shule come again bob sambeka usijeukampeleka shule hata mjukuu wako wote watakuwa nyamihela utakula kiulaini, huku ukiendelea kuota huku unakimbia halafu baadaye utaona maisha yanaendaje.

 61. sellanda Says:

  wewe kuku wa kienyeji acha kutoa maneno machafu kwenye hii blog kumbuka humu kunawatu wenye akili timamu, so jaribu kuwa muungwana sio unatukana watu hapa. Nani umemuona ameshikishwa ukuta hapa? jaribu kuwa mstaarabu

 62. Monica Says:

  Mr blue umekosea mahesabu ungeenda shule halafu mziki, unafata muziki upo tu, ungepiga tu mziki na watu wangeukubali,lakini shule ina inapendeza kusoma ukiwa na umri mdogo yaani bila majukumu, wewe unawaza shule tu, sio kama ukiwa na mke au watoto ambaoo nao wanamatatizo yao, shule haiyendi vizuri.ushauri wa bure ufanyie kazi.

 63. watubwana Says:

  siri ya mtungi aijuaye ngata,blue kaka rudi shule,muziki kwa TANZANIA ni bado sana,JAPO UMEKUA KIDOGO SANA
  si wakuutegemea.NI WA UMAARUFU TU,UKIJIANGALIA MFUKONI HUNA KITU.INABIDI UTUMIE AKILI SANA ILI UWEZE KUISHI NA SI MUZIKI PEKE YAKE.usanii bila shule haufiki popote ndugu yangu.mimi baba yangu nae alikua msanii kama wewe,ila ALIENDA SHULE, alisoma enzizileee,NA ALIKUA MMILIKI WA BENDI KUBWA TU TANZANIA KAMA UNAIJUA SAFARI TRIPERS ILA WENGI WANAJUA ILE BENDI NIYA ……….,YULE ALIKUWA MWIMBAJI TU,ILA MMILIKI NI BABA YANGU,BABA YANGU NDIE ALIEMFUNDISHA MUZIKI YEYE…..KUPIGA GITAA,KINANDAA,NGOMA,KUIMBA NA NK.
  …..ALIKUA AMEAJIRIWA NA BABA YANGU.BABA YANGU ALIPEWA NA BABU YANGU MTAJI WA KUANZISHA BENDI.WALINUNUA KILA KITU KINACHOHUSIANA NA BENDI YA MUZIKI,AMBAVYO VITU VYOTE HIVYO VIPO NYUMBANI KWETU…… HADI LEO HII.HAJAUZA HATA KITU KIMOJA.BENDI ILIPOKUFA,ALIPOANZA KUUMWA,HAKUWEZA KUENDELEA NA MUZIKI.KISOMO NDICHO KILICHOKUA KINAMSAIDIA.KIPINDI HICHO ALIKUA NAKAZI YAKE NZURI TU.HADI ALIPOZIDI KUUMWANA KUACHA KAZI.
  WANAMUZIKI WENGI WA TANZANIA HAWAPENDI KUWAPA UMAARUFU WALE WALIOWAFUNDISHA MUZIKI.MARA NYINGI WANAMUZIKI WAKIHOJIWA WANASEMA OHHH MI NILIANZA KUPIGA GITAA,KINANDA TOKA NIKO MDOGOOO.NI UONGO WA HALI YA JUUU.HATA MUNGU HAPENDI.KUWENI NA UPENDO KWA WENGINE.HAKINA MAREFU YASIYO NA NCHA

 64. halima Says:

  Aiseee!!!!!! mbona baba yangu zimekuwa nyingi hapo duh sielewi wajameni mada imetoka out imekuja baba yangu insha mhh na hiyo methali hapo mwisho mhhh iko sawa kweli?

 65. hombiz Says:

  mchangiaji “watubwana”. Umetoa comment nzuri sana!. Natumaini itasaidia kuleta mabadiliko chanya kwa wasanii wengi wa muziki wa bongo flavor!

 66. watubwana Says:

  nashukuru sana hombiz kwa kunielewa,asante sana.

 67. watubwana Says:

  blue nenda shule,kinacho hitajika katika maisha ni DESTINATION yaani kule unakoelekea,FUTURE na si sasa,sasa hivi utakua maarufu na kupata pesa,je unainvest sehemu?zitaweza kukusaidia hapo baadae?elimu ndio ufunguo wako,nenda shule.nakumbuka kuna wimbo kabisa uliimbwa unaitwa ROZA NENDA SHULE,kama unasikilizaga zilipendwa.

 68. rendezvour Says:

  lil wayne yupo university of houston longtime since when he was promoted CEO of his label CASH MONEY so man dont just run ur mouth…u got do lil research b4 u drop some lines dont mislead peeps

 69. hombiz Says:

  one love, watubwana!
  stay up, always

 70. hilly Says:

  kuna watu wanatoa hot point mpaka basi yaani,na sababu hii inawafanya wajenge uadui na wenye point pumba. but worry not,keep it up! blue just go back to school,hao wanaosema usiende shule ukichunguza sana wana biashara za ajabuajabu tu hawana future direction. siku zote mtu aliyekwenda shule anakupa shauri mzuri. Hao wanaosema eti kuna watu wamesoma na wanasaga lami hawana target ya maisha na wanaagalia kitu kimoja, i mean hawana alternatives to their future. Sasa we mtu labda kasomea science,may b ana ndoto ya kua engineer akashindwa(fail) mitihani,sasa kama huna alternatives to your future lazma utasaga lami na kusema elimu haina mpango. Kumbe wewe ndio huna mpango. Mtu unaweza kuamua hata kwenda ualimu,japo haulipi ila unaweza ukawa na tution inakuingizia kipato,sio muuza vocha anaewaza utajiri. La unaweza kuamua kujiunga na upolice kutokana na level yako ya elimu,japo pesa ndogo ila mwisho wa mwezi unaingiza,kusoma sio lazma upate mamilioni acheni mawazo ya kitoto. Kwa sababu polisi huwezi kumfananisha na muuza mitumba anaefukuzwa na mgambo kila siku.Zipo mbinu nyingi za kufanya kufight life hata kama umefanya vibaya shuleni ila ukikata tamaa lazma usage lami uje sema elimu haina mpango.Watu wengi wenye mafanikio sio kwamba walipata a kwenye vyeti vyao.Huwezi ukaishi kwa kutegemea entertainment wakati kuna competition ya ajabu inayokuja nyuma yako,wanamziki kila siku tunawasikia wanajiita maandagraundi, Sikia kitu chochote ambacho ni participated by society kinakua competitive,na lazma uwe competent.Ndio mana msanii leo kavumaaaa,kesho kaingia mitini maana hawezi huo ushindani.Akina mr nice walikua na pesa sana tu,mbona alifilisika,low knowledge.Ukiwa na elimu bwana hata kama hauna pesa ur still the best!Nchi yetu bado inaendelea msije kujifananisha na nchi za wenzetu walioendelea ambako hata mtu ukiwa huna kazi basi utaclaim benefit unaishi kwa kulipiwa nyumba na kupewa pesa ya chakula. Wasanii wa bongo wanatakiwa waishi kama wako kwenye developing country na sio developed ones,mkifanya hivyo lazma mtapoteza.Mambo ya kufananisha tz na america mnakosea sana jama,hivi america wametuacha nyuma mile ngapi?tchao

 71. watubwana Says:

  i up grade u hilly.thanx 4 the comment.

 72. charonaire Says:

  du!imeshakuwa topic

 73. LILFUE Says:

  BLUU USIWASIKILIZE WAJINGA WOTE WANAOKUSILIBA UNAJUA NA UNAWEZA ENDELEA HIVYO HIVYO MAISHA KOKOTE SIO UKISOMA NDIO UTAWINI MTU UKISHAJUA KUTAFUTA ELA TU KUSOMA INAKUWA MTIHANI AU HAWAJUI TAKE CARE HAPPY VALENTINE MAN………………………………….LILFUE

 74. LILFUE Says:

  MR BLUU UNAJUANUSIWASIKILIZE WAJINGA WANAOCHONGA OHH SHULE HATA MZIKI SHULE HAWAJUI NINI?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s