BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JENERALI ULIMWENGU September, 30, 2008

Filed under: Magazeti,Uandishi — bongocelebrity @ 10:03 PM

Pichani ni Jenerali Ulimwengu.Huyu ni miongoni mwa waandishi wa habari nchini Tanzania walio na uwezo wa aina yake katika kujenga na kubomoa hoja iwe ni katika maandishi au maongezi.Makala zake siku hizi zinapatikana katika gazeti la Raia Mwema.

Photo/Bob Sankofa

Advertisements
 

37 Responses to “JENERALI ULIMWENGU”

 1. EDWIN NDAKI Says:

  nafungua computer naona sura ya mtu ambae kwenye maisha yangu ana mchango mkubwa sana.

  Nilimfahamu huyu baba miaka mingiu iliyopita.Nilipenda sana kazi zake.Nilizidi kuvutiwa zaidi alipokuwa anaandika ‘RAI YA JENERALI’ kwenye gazeti la ‘Rai’ lilipokuwa ‘hai’

  Katika umri mdogo nilijikuta nanunua gazeti la rai badala ya kununua magazeti “pendwa”(udaku).

  Ulimwengu alinivutia nikajikuta naipenda fani ya habari pamoja na bwana mmoja kutoka uganda ambaye kwa sasa kajikita USA..Shaka Sali(sina uhakika na jina kama nimeliandika vema)anayeendesha kipindi cha straight talk africa.

  Ulimwengu ni mwanahabari mzuri sana.Nakimis sana kipindi chake cha jenerali on maonday chanel ten.

  Mola akupe afya njema ..wewe ni really BONGO CELEBRITY.

 2. Kama usemavyo BC. Huyu jamaa ni zaidi ya Talk Show hosts wengi tuwaonao. Ana upeo wa ajabu na anatambua, kuchambua na kuchanganua mengi saana awapo kwenye kipindi (na hata katika makala zake).
  Naheshimu saana kazi zake na naamini kwa wenye upeo mwema wanaweza kulitambua hili na wale wasiopenda ukweli na uchambuzi makini wataendeleza jungus zilizomfanya aambiwe si raia.
  Blessings Jenerali

 3. Hombiz Says:

  Edwin Ndaki & Mzee wa Changamoto, nakubaliana na nyinyi kabisa. Jenerali Ulimwengu, hiki ni kichwa!. Nimesoma makala zake nyingi sana ktk Gazeti la Raia mwema na kumkubali sana huyu mtaalamu. Anapembua mambo kiyakinifu na ananyumbulika kulingana na mazingira. Nafagilia sana wasifu wake wa nje!. Endeleza lieneke kaka, una haiba tosha kabisa ya kuwa muandishi wa habari..
  Be easy bro!

 4. majita Says:

  Sawa kabisa.Huyu bwana ni nguli wa habari na mimi nilikuwa mmoja wa wapenzi wa gazeti la RAI kabla halijabadilisha sura yake ya cover hapo miaka ya 2007.Ila swali langu na hofu yangu ni kuwa:-
  Hili gazeti wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (aliyepatikana Kikwete) lilikuwa linaandika habari nyingi sana za ku-critisize serikali na kuanika uliokuwa unajulikana kama “uozo” wa serikali,sasa je hatuoni kuwa hizi zilikuwa ni chuki binafsi kwa mh.Mkapa vs ulimwengu pia walilitumia kama kampeini ya kumuuza kikwete jambo walilofanikiwa na sasa tunaonja joto ya jiwe ya wanahabari hawa?????

  Kama hii wasiwasi yangu ni ya kweli bwn Ulimwengu ulisaidia kumuweka kikwete hapo alipo na ahadi zake za ari,nguvu na kasi mpya baaasi “Maisha bora kwako utayaona uko siku za usoni pako.”

 5. usinijue1 Says:

  huyu jamaa unapozungumzia uandishi wa habari basi yeye anastahili sifa zote,nakumbuka katika makala zake za miaka ya nyuma alipokua akikosoa ama ukuwafumbua watz juu ya mabaya yafanywayo naviongozi wetu wa serikali kuu basi akasingiziwa kesi ya kuwa si raia wanchi ili afukuzwe, sasa sijui iliishaje maana niliondoka lakini namuona yupo anaendeleza libeneke la uandishi, mungu amzidishie

 6. nakubaliana na wadau waliotangulia, Jenerali is a class apart katika suala la uandishi wa kalamu na pia mahojiano ya televisheni. Kila ninapokuwa Tanzania najitahidi sana niangalie Jenerali on Monday. Navutiwa na Bwana Ulimwengu alivyo mpembuzi mzuri wa mambo mbalimbali ikiwamo siasa, uchumi, mahusiano ya jamii, n.k. Ni mcheshi na mchangamfu na ana ufahamu na uelewa wa mambo mbalimbali. Kabla hajaja katika ulimwengu wa luninga tulikuwa tunapata makala yake ya kila wiki ya “Rai ya Jenerali Ulimwengu”katika gazeti la Rai, ambapo sasa makala hiyo imehamia gazeti ya Raia Mwema na inaitwa “Rai ya Jenerali”.

  Ndaki amemtaja mtu mmoja wa maana sana pia. Shaka Sali. Star TV walikuwa wanarusha kipindi chake toka VoA

 7. Matty Says:

  hiki ndo kichwa aisee nampenda sana huyu baba walai!

 8. Christabell Says:

  Safi sana! Hiki ni kichwa haswaa! Fani iko ktk damu. Hakulazimishwa kuwa mwana habari. Endeleza libeneke!
  Nakupa heshima zote maana huna na huandiki majungu!

 9. Mwalimu Zawadi Says:

  Nadhani huyu anaweza kuitwa mwandishi-nguli mwandamizi, gwiji wa uchambuzi, mtaalamu aliyebobea, mwenye upeo wa juu katika habari Tanzania. Huandika na kusema anachokiamini kwa nadharia yakinifu. Tunahitaji vijana watakaoweza kuendeleza libeneke kama yeye.

  ubarikiwe Jenerali, kalamu yako idumu milele

 10. any Says:

  Briliant man, ana upeo mzuri sana!
  pia ni handsome, is he single? was just wondering.

 11. joseph Mwita Says:

  Jenerali Ulimwengu ni kati ya waandishi wachache ambao bara la Afrika linatakiwa kujivunia.Ni watu wachache wanaweza kuwa na kipaji kama cha Jenerali.Mimi namfananisha na Charlie Rose wa PBS hapa USA.

 12. Chris Says:

  Ni kati ya watu walio objective na kazi zao! Hajavamia fani ya uandishi! Ulimwengu ni zaidi ya muandishi! Ni mwanataaluma alietukuka katika uandishi na uchambuzi wa mambo mbalimbali.

  Si mtu wa kukurupuka! Makala zake zimeenda “shule” haswa. He’s so inspirational kwa kweli!

 13. Frateline Says:

  Hi Guys kutoka Helsinki-Finland

  Kwa kweli hata mimi ninamkubali Bwana ulimwengu, nimekuwa nafuatilia sana Siasa za Marekani tokea march, 2008 mwaka huu, nimependa sana waandishi wa habari wa Marekani kama Chris Methew, Davi Gregory, Rachel, Todd Chuck na wengine wengi ambao wanajulikana kama News analysts na wengine wako NBC political news analysts, kwa kweli hawa watu wanaonyesha uwezo wa kupambanua hoja mbali hasa hasa kuhusu kampeni za marekani, sasa kwa upande wa bongo ni waandishi wachache wenye uwezo kama ulimwengu, maana fani ya uandishi wa habari nchini bongo bado imevamiwa na waandishi wanaojulikana kama Kanyanga ambao wengi ni waandishi wa habari wasio na sifa wala Elimu ya uandishi wa habari. Lakini tatizo jingine bongo wamiliki wa vyombo vya habari ni wanyonyaji wanapenda kulipa pesa kidogo na kuajili watu watakao kubali mishahara ya kinyonyaji, ndiyo maana mtu kama ulimwengu amejiajili, mwenyewe

  hongera ulimwengu

  stay blessed

  frateline

 14. Matty Says:

  Any, naona umekuja na nguvu mpya ngoja asikie mkewe hahahahahahahahaha mimi namuona kazeeka lakini!

 15. thomas Says:

  jenerali ulimwengu na wenzake na gazeti lao la Rai. ya dhamani zile ndiyo walionifanya nianze kupenda kusoma habari za uchunguzi, na mpaka leo sijaacha.
  jenerali unastahili hongera kwa makala zako nzuri na zenye kujenga na ambazo huwasaidia watawala kuangalia mienendo yao. hongera mzee jenerali.
  Mzee jenerali elewa kwamba umma wa watanzania unakupenda na umekuwa mmoja kati ya watetezi wakubwa katika jamii hii.
  Mimi nakuomba urudishe ujasiri wako wa zamani.jenerali wa sasa nikama umebadilika kidogo na unaonesha kuwa muoga,generali wa sasa hivi,hajakemea richmond wala Eppa? na unaongea kwa mafumbo sana.
  Nilizisoma kwa makini barua zako za wazi kwa rais mpya katika gazeti lako la zamani.kwa jinsi ulivyokuwa unaandika ilionesha kwamba ulikuwa na imani kubwa sana na serikari iliyoingia madarakani na ukadhani mzigo umetua na wakati wa kupumzika hata uandishi sote tuliamini hivyo.
  baada ya kuona mambo yanaenda tofauti na ulivyotarajia umerudi tena lakini safari hii unaonekana muonga. yawezekana ni mtazamo wangu tu.
  katika yote tunakuunga mkono na gazeti la Raia mwema ndilo gazeti letu makini
  kila laheri mzee jeneral.

 16. Bwaya Says:

  Nimeanza kumsoma Jenerali miaka ipatayo kumi sasa. Sasa hivi nikizikosa makala zake huwa sipati amani. Najisikia kuumwa.

  Naomba Bongo Celebrity mtupatie mahojiano ya watu kama hawa. Nadhani kuna mengi sisi vijana wa leo twaweza kujifunza kwao. Vichwa kama Padri Priva Karugendo, akina Ryoba ni muhimu vikatafutwa viseme na kizazi cha leo.

 17. DUNDA GALDEN Says:

  Hekima na busara zako ndizo zinazo weza kuliongezea ili taifa letu wale wanao elewewa nini maana ya kile unachikiandika,moja kati ya Nakala zako zinafundisha nusu ya kizazi kipya manufaaa makubwa ya leo na kesho

 18. Hombiz Says:

  Frateline, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kuhusu waandishi wa TZ. Lakini pamoja na baadhi yao kuvamia fani na wengine kuwa kanyaga twende, still wapo waandishi wa kweli na wasiopenda kuyumbishwa kama bwana Generali Ulimwengu.
  Kuna jambo jingine kubwa ambalo mwenyekiti Maggid Mjengwa wa http://mjengwa.blogspot.com/ aliwahi kuliongelea kwenye makala zake. Jambo hili linahusu selikali kuwabania waandishi ktk swala zima la kuwapatia ruzuku. Alitoa mfano kwa kusema, utakuta muandishi wa habari anaambatana na mkuu wa Wilaya ktk msafara wake wa (ziara)kwenda kuhutubia sehemu fulani. Ktk msafara huo, muandishi anamtegemea mkuu wa Wilaya ndiye amlipie nauli ya kwenda na kuludi. Sasa unategemea muandishi huyo atakuwa huru kuandika vibaya kuhusu mkuu wa wilaya iwapo atafanya vibaya ktk ziara yake? Pengine anaogopa kuwa akiandika vibaya, mkuu wa wilaya anaweza kumwambia kuwa sikulipii nauli ya kurudi, na mambo kama hayo. Huu ni mfano mmoja tu, lakini ipo mingi kwakweli. Inaniuma sana ninapoona waandhishi wa kweli wanateseka na kufanya kazi ktk mazingira magumu kama haya. Wengine hufikia hatua ya kuhatarisha maisha yao kv kumwagiwa tindikali ama kuuwawa kabisa mithili ya Stan Katabalo aliyekuwa mwandishi wa kipelelezi, aliyefuchua kashfa ya roliondo iliyowahusu vigogo wa juu serikalini. MOLA amrehemu Katabalo. S. Inapendeza sana unapoona kuwa waandishi wa kweli wanaweza kujikwamua kutoka ktk ukilitimba wa kuendeshwa na waajili wao na badala yake kuweza kujiajili na kufanya kazi zao binafsi (za kiandishi) kwa uhuru wa kutosha.

 19. Frateline Says:

  Hi guys kutoka helsinki

  Bwana Hombiz kwa kweli nikupata hoja zako za msingi kabisa, ndiyo maana kwenye comment yangu nimewalaumu wamiliki, waandishi wa kweli wapo ndiyo ila mazingira ya kazi bongo ni mabovu sana,je tutafika?

  Frateline

 20. Unapozungumzia waandishi wa habari,basi mzee jenerali ulimwengu,si mwandishi bali ni nguli wa waandishi wa habari ambaye anaijua taaluma hiyo vilivyo na kuheshimu miiko ya uandishi,acha waandishi wengine ,ambao wananunulika kama dagaa sokoni,ukitaka kujua kichwa cha huyu mzee ulimwengu ni hazina ya nchi,basi soma makala zake kwenye gazeti la raia mwema ndiyo utamjua huyu jamaa ni nani ktk uaindishi,mzee ulimwengu MUNGU akupe afya njema na akubariki ktk shunghuli zako
  asante baba

 21. any Says:

  Wee Matty, temea chini kabisa, kazeeka wapi! mi namwona bado kabisa.

 22. kahindi Says:

  we Matty.hata kama kazeeka.lakini kumbuka kuwa ujuzi hauzeeki,alafu kuzeeka kwake we kunakuhusu nini?

 23. kapisi Says:

  mi namkubali kwa pamba zake…

 24. Amina Says:

  kwani ni lazima useme umetoka finland?makubwa…….namimi hi guys im fom kijtonyama dar hahhahhahhha

 25. hombiz Says:

  mmmmh! Frateline, sijuwi kama kweli tutafika kwa mwendo huu ndugu yangu! Kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa ki-imla hivi sasa, sipati matumaini sana!
  Let`s keep our heads up and see what happens!

 26. matty Says:

  lakini kweli Any si ndo kama ule mpasho wa shosti wetu Malkia wa mipasho aluuuuuuuuuuu eti ng’ombe hazeeki Maini….walai yule mama kiboko hahahahaha!

 27. anonymous Says:

  majita acha uzushi

 28. any Says:

  Matty mi nampenda bwana, ivi si mnatoka nae kijiji jirani niunganishie basi.

 29. Mwana wa mkulima Says:

  Hivi wadau mnajua kwamba kitaaluma JENERALI ULIMWENGU SIYO MWANDISHI WA HABARI?

  HUYU BWANA KITAALUMA NI MWANASHERIA. ALISOMEA PALE UD. ILA UANDISHI NADHANI NI KIPAJI CHA DAMU. HONESTLY, MIMI SIKU NILIPOGUNDUA KWAMBA ULIMWENGU HAKUSOMEA UANDISHI DARASANI SIKUAMINI.

  ANYHOW HE KNOWS WHAT HE DOES. MUNGU AMZIDISHIE BARAKA TELE.

 30. Matty Says:

  Any, kwa hilo tu usijali nitaunganisha shosti!

  Kahindi bibie nipishe nipite ujumbe wangu unakuhusu nini?? ulijuaje kama si……………………..

  BC unabana sana mwanangu sikuhz!

 31. binti-mzuri Says:

  WE MATTY UMEANZA KUSHUSHUANA LINI,WE SI ULIKUA UNAJIFANYA MTU MWEMA

 32. kahindi Says:

  HAYA MATTY…PITA BIBIEEEEEEEEEEEEEEE…ILA MI NAMUONA HAJAZEEKA.

 33. kahindi Says:

  BINTI MZURI…HABARI ZA SIKU SHOSTI?

 34. Matty Says:

  Binti Mzuri Mimi ni mwema siku zote ulikuwa hujui??? jibu la swali lako kuwa nimeanza lini kushushuana ni hili (kushushuana nimeanza tangu nipo nasery school!!!!!!)

  Kahindi Bibie asante kwa kunipa njia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 35. bdo Says:

  heko Jenerali Ulimwengu, as your names appear – wewe ni General wa Ulimwengu wa Habari, kama kweli mwana wa mkulima anasema ukweli kuwa haujagusa hata darasa la habari, sasa sijui ungetia mguu ingekuwaje….ila sometimes ukae na hawa “Auxiliary mgombo” wa habari waache kunuka rushwa za kupamba watu, akipewa 500 anakuandika vzr, ukimnyima 100 ya nauli anakundika vibaya

 36. Sado Says:

  JENERALI ULIMWENGU gwiji la habari,mwanasheria,mwanafalsafa,mzalendo wa kiafrika,mjamaa,kamaradi,mfuasi na mtoto wa MWL JK,amewahi kua katibu mkuu wa vijana afrika,mkuu wa wilaya na mbunge.ameshiriki vita kumtoa mkoloni msumbiji,anaijua vizuri afrika anayoipenda mno.lkn pia anaijua dunia,ni mtu wa msimamo usioyumba ktk mambo ya msingi anayoyaamini,yeye ni daraja la watukufu wachache nchi hii imewahi kupata km vile dk salim a.salim,warioba,issa shivji,othman haroub na wengineo.kama kuna dhambi kubwa nchi hii imepata kufanya ni kuwabagua wa tz hawa wazalendo salim na ulimwengu na dhambi hii imeanza kututafuna na km hatutatubia na kubadilika itatuangamiza kabisa km taifa,jamani ulimwengu ni tembo na mimi kipofu nimeeleza sehemu nilizopapasa nawaachia wenye macho na walio karibu nae (niko kijijini msalala-geita)watuelezee zaidi,kwa mwenye kuhitaji makala zake za nyuma kipo kitabu cha makala zake kinaitwa RAI YA JENERALI ULIMWENGU.namwombea MUNGU ampe maisha marefu na yenye baraka.

 37. bilabaye kwigeza Says:

  Kitu pekee kinachokuja bila juhudi ni Umri. kinachokuja kwa haraka ni Makosa, na kinachokuja mwisho ni Majuto. Wao hawatambui ni kipi cha kwanza na kipi cha mwisho. Lakini kipindi cha ukombozi wa kweli kupitia vijana wazalendo wa nchi hii wakiongozwa na maazo ya wazalendo wasiotiliwa shaka wa nchi hii kama Ndugu JENERALI ULIMWENGU, ni katika kipindi hiki watakapo tambua maana ya msemo huu. Mapinduzi Daima.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s