BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PROF JAY KATIKA “THE MTV MAKING OF THE VIDEO” October, 2, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:06 AM

Hivi karibuni msanii maarufu wa Hip Hop nchini Tanzania,Professor Jay amekuwa akizuru nchini Ghana mara kwa mara ikiwa ni kufuatia kuteuliwa kwake na MTVbase katika ile project maarufu ya “The MTV Making of The Video Part II“.Hiyo ni kutokana na kukubalika kwa Prof.Jay miongoni mwa wana-Hip Hop wa barani Afrika.

Huko Ghana,pamoja na kufanya maonyesho mafupi mafupi kadhaa,Prof alikwenda kutengeneza video iitwayo “Who You Be” akiwa ameshirikiana na msanii maarufu wa nchini Ghana aitwaye Kwaw Kesse(pichani juu ni Prof na Kaw Kesse).Video hiyo itaonekana hivi karibuni kupitia MTVbase na TBC.Stay Tuned!Hongera Prof Jay kwa kuwakilisha Tanzania na mafanikio yako katika muziki.

Prof Jay(kushoto) akiwa na Director maarufu wa video,Anthony ambaye ndiye ame-direct “Who You Be’

Advertisements