BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PROF JAY KATIKA “THE MTV MAKING OF THE VIDEO” October, 2, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:06 AM

Hivi karibuni msanii maarufu wa Hip Hop nchini Tanzania,Professor Jay amekuwa akizuru nchini Ghana mara kwa mara ikiwa ni kufuatia kuteuliwa kwake na MTVbase katika ile project maarufu ya “The MTV Making of The Video Part II“.Hiyo ni kutokana na kukubalika kwa Prof.Jay miongoni mwa wana-Hip Hop wa barani Afrika.

Huko Ghana,pamoja na kufanya maonyesho mafupi mafupi kadhaa,Prof alikwenda kutengeneza video iitwayo “Who You Be” akiwa ameshirikiana na msanii maarufu wa nchini Ghana aitwaye Kwaw Kesse(pichani juu ni Prof na Kaw Kesse).Video hiyo itaonekana hivi karibuni kupitia MTVbase na TBC.Stay Tuned!Hongera Prof Jay kwa kuwakilisha Tanzania na mafanikio yako katika muziki.

Prof Jay(kushoto) akiwa na Director maarufu wa video,Anthony ambaye ndiye ame-direct “Who You Be’

Advertisements
 

17 Responses to “PROF JAY KATIKA “THE MTV MAKING OF THE VIDEO””

 1. jezi ya J wa mitulinga imetulia. Uzalendo full.. hatubipi heheh (N umenielewa nadhani)

  Joseph Haule ni mmoja ya maMc nilitokea kuwakubali sana ktk B’flava toka enziz ile. Niliikubali kazi yake kisanii kuanzia mashairi na mpaka ujumbe. Nikakubali biti zake na miondoko yake ya kisela katika matamasha na video. Ila ni9kaja kukubali akili yake kumkichwa… hapa nazungumzia ya street sio ya studio nilipooma kibanda chake Mbezi Louis,…
  big up kaka. Mola akuzidishie

 2. xxx Says:

  aisee mzuxxx mtu wetu..mi nakupendaga sana we prof jizee kwakuwa unajituma and ur a good ambassador of tz. wewe na lady jaydee peke ake ndo mna repp tz wengine wote ni ma bishooo tu !

 3. KBC Says:

  Eeebwana JAY Hongera sana..sasa hizi Video zenye VIWANGO vya MBELE..ziendelee kama ALUTA..
  WORK HARD and PLAY HARD..like HARD BLASTERS..
  Its ya Boy!..KBC from K.U.

 4. Hombiz Says:

  Good JOB! Hard work rewards most of the time!.
  Stay strait!

 5. halima Says:

  Katika wanamuziki wa hip hop afrika mashariki basi mshikaji yupo juu sana kuanzia enzi zile za chemsha bongo mpaka sasa nang’atuka. BIG UP!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 6. SaLaMa Says:

  Duh shavu hilo mwanangu usipime hongera sana mtu wangu

 7. Matty Says:

  kumbuka nilikutoa kijijini sitimbi ukiwa na furushi la magimbi hahahahahahaha i like da song!
  Profesor J upo juu babake nakumbuka that day tulimeet somewhere transit motel kwenye msosi ukambeba ma daugher ukamwambia utakuwa ladyj d wa baadae aisee mwanangu ashakumaki mwanawane mziki wako ukipigwa anasema J profesa.
  Haaa Nalitolela Ps..huyu mwanangu ni mmojawapo wa wasanii wenye mafanikio na mziki wao ni kweli anabanda pale mbezi luis kanisani ni jirani yangu.
  All the best bro!

 8. Mbongo Says:

  Prof. J is the best in TZ
  watoto waimbe wakimbie ila yeye is the best
  Keep it up bro

 9. nenet Says:

  Hommie umependeza sana.Lakini huyo mwenzako anataka kupigana na nani ? au ndiyo pozi ? Mwambie bongo tunajua
  peace kama wewe unavyoonekana kwenye picha siyo kupigana…………
  MUCH LOVE HOMMIE….

 10. Msanii Says:

  Profesa ngoma chini. Manyanga juu. Hakuna zaidi. Ila kwa maoni yangu ningekushauri uachane na fake hip-hop imagery. Una kipaji, ujumbe, na akili. You are a legit tanzanian artist. You should stay way above the fray. If anything, you are more of a Jay Z than a T.I. Where are you D&G suits? Put those on!

 11. eve Says:

  yaanii! wewe kipaji unacho ila mapepe na ubabe vilikuponza kwa kumpiga mwenzio mr Nice vilishusha chati yako ulifanya mambo ya kizamani mshikaji hauvumi tena hata ukitoa wimbo unafagiliwa wiki moja tu! kutokana na tabia uliyoionyesha unatakiwa ukuwe mzee!

 12. Hombiz Says:

  eve Jay sio Dudubaya! Usichanganye wasanii hapa! Dudubaya ndio aliyempiga Mr Nice na sio Profesa Jay!. Are you in your own world or what!?

 13. jay's fan Says:

  jay una akili na lyrics zako zina maana saaana. lakin jambo moja mkuu jaribu sana kupunguza pombe, zinakurudisha nyuma saana. Labda ni vigumu kutokana na group yako lakini kwa ushauri wangu ukitaka kuendelea lazima ujaribu kutafuta watu wa maana kuwa nao karibu zaidi. Kwani maisha ya U mc unaisha, lazima uangalie baada ya hapo unaelekea wapi??? group yako sio nzuri. hiyo ni advice yangu. otherwise I am your number one fun.

 14. halima Says:

  we eve jay alimpiga Mr nice wapI? usijeukatuchanganyia mada hapa. au wadau nyie mnajua kuwa jay alishawahi jupigana na mr nice?

 15. halima Says:

  samahani nimekosea ni kupigana

 16. sellanda Says:

  Na wewe eve usikurupuke toka usingizini tu hapa ukatuandikia vitu havina miguu wala kichwa uliza kwanza ndio utoe hizo comments zako.

 17. Matty Says:

  pole sana eve, next time soma kwa uangalifu na udadavue picha kwa kina!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s