BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NI WEWE PEKEE-MAQUIS ORIGINAL October, 3, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:02 AM

Pongezi kwa wote mliofunga na kutubu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.Kufunga sio mchezo ati.Yataka imani sahihi na uvumilivu kamili ili kuzikwaa hizo thawabu.Sikukuu ilikuwaje?Ulienda kuifaidia wapi?Ile mialiko wanayopeana wana BC ilikamilika?

Hapa kwetu ni wikiendi nyingine.Wakati wa zilipendwa.Wakati wa kuserebuka kidogo kwa burudani ili sio tu kuenzi miziki ya kwetu bali kukumbushana kwamba muziki sio lazima uwe na maneno “mbofu mbofu” bali yawezekana kabisa kuongea na kuelewana kupitia muziki.Penzi linaweza kudumishwa kupitia muziki.

Leo tunao tena Maquis Original.Wimbo wa leo ni “Ni Wewe Pekee“.Mtindo ulikuwa ni Zembwela.Wimbo huu ni kwa wote wanaopendana.Pata burudani.Wikiendi Njema.


Advertisements
 

10 Responses to “NI WEWE PEKEE-MAQUIS ORIGINAL”

 1. EDWIN NDAKI Says:

  BC na wadau wote binafsi sina uwezo hata wa kusikiliza wimbo huo,kutokana MAAFA ya vifo vya watoto zaidi ya 19 yaliyotokea Tabora.

  Kwanza nachukua nafasi hii kuwapa pole,ndugu jamaa,wazazi na marafiki wa watoto walioaga dunia.Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu wanachokabiliana nacho.

  Inaumiza sana kuona “MACELEBRITY” wa siku za usoni wanakufa kutoka na uzembe wa mfumo usiojali wasionacho.

  Naamini kama serikali yetu ingekuwa makini kutenga na kusimamia maeneo ya wazi ya burudani ya watoto basi vitu kama hivi vingeweza kuepukwa.

  Tunatumia mabilioni ya pesa kwa safari za kwenda ‘kuuza’ sura USA na kumpigia Bush magoti kuomba msaada wakati ..tunarasimali kibao tunashindwa kuzitumia vema.

  Wamefariki watoto zaidi ya 19 kwa sababu ni watoto wa walalahoi kama mimi ‘muheshimiwa’hana muda hata wa kwenda kuwapa pole anatuma ujumbe tu.Wakati ana muda wa kwenda kuangalia ligi ya NBA..Kweli hii serikali ya ‘kishkaji’.

  Mara nyingi ukiona ‘muheshimiwa’ kaenda kumuona mgonjwa muhimbili basi ujue ni katika ‘utashi wa kisiasa’ hakuna jingine lolote.

  Nawapa pole sana tena sana.Nimeumia sana kuona watoto wakipoteza maisha katika mazingira ambayo tungeweza kuwanusuru.

  Ila poa tu..naamini haya yote yana mwisho wake.

  TUTAFIKA TU

 2. Mama wa Kichagga Says:

  Safi sana BC kibao kina beep sakafu ya moyo asante yamenikumbusha mbali sana ila chichemi hapa hahaaaa.

  Wana BC wote Mungu awajalie muifurahie na kuipenda week-end hii. Muwaambie wapendwa wenu kuwa mnawapenda kwani inapendezaga sana. Ukiminya inakuwa ngumu mwenzio kujua kama bado mambo ni mswano.

  Maquis Nawapenda wametulia vema.

 3. Mswahilina Says:

  Ni wewe pekee “BC”.

 4. hombiz Says:

  Aisee!. Hii nyimbo inanikumbusha mbali sana. Njaa ya mchana wakati nasubiri ugali na maharage pamoja na kabichi. Wakati huo “beki tabu wetu” (mtumishi wa nyumbani) alikuwa ni mwanaume. Alikuwa anajua kupika hadi kila mtu alibana ng`eng`e! Na mwanamama akiwa kajaaliwa mambo fulani mtumishi wetu aliita zegembe!. Wanaume wote tulikuwa macho feni. Tukaulizwa tunashaa nini? Tukaambiwa tukashangae feli meli inatembea lakini haina mataili. kwakwali mambo yalikuwa ni danga che dukinaaaa kama sio dole. Uuuuuuwi! Old is gold ma people!
  Give it up to Maquis Big Time!
  Stay up everybody

 5. Matty Says:

  Hv ni mimi tu siwapati BC au???? pls mnanidrive mad aisee mko wapi wadau???sioni maoni kabisa!

 6. EDWIN NDAKI Says:

  Bc wazima mbona mnasua sua..kuna tatizo gani limewasibu..

  nawaombea kila jema

 7. Matty Says:

  Kibao kimenibamba ile mbaya!
  Nakwambia Edo Ndaki hapa labda mimi nikiwa Raisi mambo kama hayo hayatatokea, history inajieleza kabisa maafa yashawahi kutokea hapo ktk ukumbi huo bado tunaruhusu ukumbi huo huo utumike kwa disco, hv tuna akili timamu kweli??kwanini usingefanyiwa uchunguzi kwanza ili ijulikane unatatizo gani kama hauna madirisha basi ungetobolewa ukuta ili hewa ipatikane.
  Pumzikeni kwa Amani watoto wa mungu na marafiki za Yesu!

 8. DUNDA GALDEN Says:

  Home sick waungwana
  NI WEWE KIPENZI NIKUPENDAE KWA JINA UNAITWA NANI NIHII
  Kibao cha nguvu moja kati ya vibao vya nguvu mwageni music
  wa kwetu BC hatua moja uzaa nyengine
  Chai goda

 9. Gervas Says:

  Buzz!!!! ..Buzz!!!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s