BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

Ze Comedy waibuka kama Original Comedy na kuteka nchi October, 17, 2008

Filed under: Burudani — bongocelebrity @ 9:27 AM
Kundi la Original Comedy wakiwa katika Studio za TBC1 wakati wa mazoezi ya onesho lao ambalo limepokelewa kwa shangwe na washabiki wao toka warudi hewani wiki mbili zilizopita. Hivi sasa hakuna anayetumia jina lake alilokuwa anatumia EATV bali sasa wana No-Name 1 hadi 7. Kesho Original Comedy wanafanya onesho lao la kwanza la wazi katika ukumbi wa Diamond Jubilee

Kundi la Original Comedy wakiwa katika Studio za TBC1 wakati wa mazoezi ya onesho lao ambalo limepokelewa kwa shangwe na washabiki wao toka warudi hewani wiki mbili zilizopita. Hivi sasa hakuna anayetumia jina lake alilokuwa anatumia EATV bali sasa wana No-Name 1 hadi 7. Kesho Original Comedy wanafanya onesho lao la kwanza la wazi katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Kipindi cha kwanza cha kundi hilo kilirushwa na televisheni ya taifa TBC1 huku kikionyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kulikuwa na vituko vya aina mbalimbali. Kundi hilo limekuja na sura mpya baada ya majina yote ya wasani hao kubadiliwa huku na jina lakipindi chenyewe likibadilika kutoka ze Comedy hadi Comedy Original. Baadhi ya washabiki wa kipindi hicho wameelezea kufurahishwa kwao na kurejea kwa maonyesho ya kundi hilo na kusema afadhali watapata muda wa kufurahisha pindi wanapokuwa majumbani kwao. Picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com

Advertisements