BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

VODACOM NA HUDUMA KWA JAMII October, 22, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 9:06 AM

 

Mojawapo ya makampuni nchini Tanzania ambayo yanafanya kazi nzuri ya huduma kwa jamii (corporate social responsibility) ni Vodacom kupitia kitengo chao cha Vodacom Foundation.Hivi karibuni BC ilishuhudia uzinduzi wa mradi wa “Voda Kompyuta” kwa shule za sekondari Tanzania ambapo walikabidhi kompyuta 22 kwa Meya wa Arusha-Lawrence Hedi.Hizo ni kwa ajili ya kompyuta mbili za sekondari mkoani Arusha.

 

Pichani juu ni Mkurugenzi wa Utawala (Africa) wa Vodafone,Bob Collymore akimkabidhi Meya wa Arusha,Mh.Lawrence Hedi kompyuta hizo.Kwa habari kamili kuhusu tukio hili endelea kusoma hapo chini.BC inaunga mkono vitu kama hivi.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

 

Tarehe: 20.10.08.

 

VODACOM FOUNDATION IMEZINDUA MRADI WA ‘VODA KOMPYUTA’ KWA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA NA KUKABIDHI KOMPYUTA 22 KWA MEYA WA ARUSHA – LAWRENCE HEDI KWA AJILI YA SHULE MBILI ZA SEKONDARI MKOANI ARUSHA.

 

 

Vodacom Foundation, kitengo cha huduma kwa jamii cha kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, imezindua rasmi mradi wa kutoa misaada ya Kompyuta katika shule za sekondari nchini na hasa zile zilizo vijijini na maeneo yaliyonyuma na duni zaidi ki maendeleo na uchumi. Yote hii ni katika mwendelezo wa kusaidiana na serikali yetu ya Tanzania yenye nia ya kuboresha Elimu.

 

Mafunzo ya kompyuta ni sehemu ya mtaala wa elimu ya sekondari nchini Tanzania, lakini baadhi ya shule hazina somo hili kwa ukosefu wa vifaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maabara ya kompyuta. kwa kuligundua hili Vodacom Foundation inazindua rasmi mradi wake wa Voda Kompyuta kwa minajili ya kutoa misaada ya kompyuta kwa shule za sekondari nchini Tanzania.

 

Mradi wa Voda Kompyuta.

Mradi huu ni sehemu ya mradi mkubwa zaidi wa taasisi ya Vodafone Group Foundation, (kitengo cha huduma kwa jamii cha kampuni ya simu ya kimataifa ya Vodafone), wa kutoa misaada ya kompyuta katika shule za sekondari barani Afrika. Tanzania kupitia Vodacom Foundation imebahatika kuwa sehemu ya mradi huo na awamu ya kwanza inatazamia kutoa Kompyuta zisizopungua 168 katika shule zisizopungua 20 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2008.

 

Vodacom Foundation inashirikiana kwa karibu na TEA – Tanzania Education Authority kwenye eneo la kutambua shule zenye vigezo vya kupata misaada hii kwa mujibu wa taratibu za Vodacom Foundation na Vodafone Foundation.

 

Uzinduzi rasmi wa mradi huu ulifanyika Ijumaa ya tarehe 17 mwezi Oktoba saa tano asubuhi katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok, ilio nje kidogo ya mji wa Arusha. Uzinduzi huu uliambatana na mgao wa kwanza wa kompyuta kwa shule mbili za mkoa ya Arusha, ambazo ni;

1.    Kipok Sekondari.

2.    Arusha Sekondari.

 

Shule hizi mbili  zitapata kompyuta 11 (kumi na moja) kila mmoja.

 

Kompyuta hizi zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Utawala barani Africa wa kampuni ya Vodafone, NDUGU BOB COLLYMORE.

 

Meya wa Arusha nae alitoa shukurani kwa Vodacom Foundation na kuwapongeza kwa jitihada zao za kuchangia maendeleo ya jamii ya Tanzania. Aliwasihi kutokuchoka kuisaidia na kumwomba Bob Collymore akiwa kama mwakilishi wa Vodafone akawaombe Vodafone Foundation wasisite kutoa awamu ya pili na ya tatu ya msaada wa mradi wa Voda Computer. Aliwasii pia wanafunzi na walimu wa shule ya Kipok kutunza msaada huo ili waweze kuvitumia kwa muda mrefu!

 

Nae Meya wa Arusha Mh. Lawrence Hedi alitoa shukurani kwa Vodacom Foundation na kuwapongeza kwa jitihada zao za kuchangia maendeleo ya jamii ya Tanzania. Aliwasihi kutokuchoka kuisaidia na kumwomba Bob Collymore akiwa kama mwakilishi wa Vodafone akawaombe Vodafone Foundation wasisite kutoa awamu ya pili na ya tatu ya msaada wa mradi wa Voda Computer. Aliwasii pia wanafunzi na walimu wa shule ya Kipok kutunza msaada huo ili waweze kuvitumia kwa muda mrefu!

 

Wakati huo huo…

Mkurugenzi wa Utawala wa Vodafone barani Africa, Ndg Bob Collymore ambae alifanya ziara fupi ya miradi ya Vodacom Foundation nchini. Alipeleka  msaada wa vitanda na magodoro katika kituo cha kulelea watoto Yatima cha Msongola kilichomo Mbagala na kinacholea watoto 50 hadi sasa. Thamani ya vitanda na magodoro vilivotolewa na Mkurugenzi Bob Collymore ni zaidi ya shs 2,000,000 (Milioni Mbili).

 

Vile vile alitembelea vituo vingine viwili ambavo vimeshapata ufadhili na misaada kutoka Vodacom Foundation vya Kurasini Center, Yatima Trust Fund, Manzese Rehabilitation Center  na Temeke Sekondari.

 

Kwa taarifa zaidi kuhusu hafla hii pamoja na mradi huu wa Voda Kompyuta tafadhali usisite kuwasiliana na Mkuu wa Kitengo – Bi Mwamvita Makamba.

 

Ahsante.

 

Maelezo Mafupi:

 

Bob Collymore:

Bob Collymore ni Mkurugenzi wa Utawala wa Vodafone barani Africa. Bob Collymore ni mkurugenzi wa bodi mbali mbali zikiwamo za Vodacom Group, Vodacom Tanzania, M-Pesa (Kenya na Tanzania), Mozambique, DRC na vile vile ni mwangalizi/msimamizi wa hisa za uwekezaji za Vodacom Africa ya Kusini. Sehemu ya kazi yake pia ni kusimamia jina la Vodafone na uwekezaji wake barani Africa. Ndg Bob alikuja ziarani nchini Tanzania kwa siku nne (4) amabapo alitembelea miradi mbali mbali ya Vodacom Foundation ambayo hupata misaada ya kifedha kutoka katika Vodafone Group Foundation (ambapo yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi yake). Amezindua rasmi programu ya Voda Kompyuta na kuumkabidhi Meya wa Mkoa wa Arusha Mh. Lawrence Hedi kompyuta 22 kwa ajili ya shule mbili za Kipok na Arusha Sekondari.

 

 

 

 

 

 

Advertisements
 

7 Responses to “VODACOM NA HUDUMA KWA JAMII”

 1. kahindi Says:

  huyu ni kapuya na chiligati?????????????

 2. mleba Says:

  Mmhh ….. meyeyusho tu.

 3. Hombiz Says:

  What Vodacom is doing is alright. But, in my opinion, I feel like these phone companies “including vodacom” charge too much for their services. They make exorbitant profit by exploiting tax payers who spend a lot of money in order to consume their services. The government needs to do something about that. They should not use their Vodacom Foundation as a tactic of getting away with what they do to exploit the blood of innocent citizens. That`s how i feel!

 4. sellanda Says:

  ndio hao hao wala ujakosea maana intoduction hujaiona

 5. Gervas Says:

  Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa ku-charge gharama ya juu simu za mikononi, ndo maana unaona makampuni yanamiminika bongo kuzoa mapene ya bure. Hawa watu wanachokifanya saizi ni mchanga wa macho tu na vijizawadi hivi sijui foundation sijui fasta, wanatengeneza pesa nzuri tu ndo usishangae hata marketing yao ni ya mabilioni ya pesa. Yaani unaongea na mtu huwezi hata kum-hold ufanye kitu kidogo..umeumia. Anyway nasikia kampuni zingine bado zinamiminika bongo kuvuna. Edwin, hata tukifika tutakuwa tumekwisha au hatufai

 6. kahindi Says:

  sellanda unasemaje?

 7. binti-mzuri Says:

  mh


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s