BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

flaviana aendelea kutesa afrika ya kusini October, 23, 2008

Filed under: Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 8:11 AM

Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2007, Flaviana Matata ambaye hivi sasa yuko nchini Afrika ya Kusini ameendelea kupanda chati baada ya kunyakua tangazo katika jarida la True Love.
Flaviana ambaye anaonekana amevaa mavazi mawili tofauti ukurasa wa 73, ameweza kupata mkataba huu.

Akieleza mkataba huu wa kutangaza nguo Flaviana alieleza,” Huu ni mkataba mmoja tu, na hivi punde natarajia tangazo langu la televisheni pia lianze kuonekana hapa South Africa na bara la Afrika”.
Flaviana hakuwa tayari kuzungumzia mkataba wake mwingine hadi itakapoonekana lakini alieleza wazi kuwa hivi sasa anaendelea kupata mialiko mingi ya kazi (casting).
Flaviana Matata aliwakilisha nchi yetu kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Miss Universe nchini Mexico ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya 6. Hivi sasa yuko nchini Afrika Kusini akifanya kazi ya uanamitindo.
BC inamtakia kila la kheri mlimbwende huyo kwa mafanikio hayo.

Advertisements