BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BAADA YA USHINDI,MANJI AUGUA October, 28, 2008

Filed under: Michezo,Wadhamini/Sponsors — bongocelebrity @ 10:25 PM

Siku moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu. SIKU moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Pichani ni Mfadhili huyo,Yusuf Manji(kulia) akiwa na Rais Mstaafu wa Yanga,Francis Kifukwe(kushoto).Hii ilikuwa kwenye hafla ya kutiliana mkataba wa udhamini kati ya club za Yanga na Simba na kampuni ya bia nchini.TBL miezi michache iliyopita.

Picha na Issa Michuzi

Advertisements
 

NDOA HAINA DOA-INSPEKTA HARUNI

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 6:39 PM

Ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao hivi leo wanaweza kujiita “wakongwe”.Kwa miaka nenda rudi wamekuwepo katika “game”.Jina lake anaitwa Inspekta Haruni…jina la kisanii likiwa limelifunika jina lake halisi la.Tangu enzi za Gangwe Mob(pale alikuwa na mwenzake Luteni Kalama)

Hivi karibuni ametangaza kujitoa katika kundi la Wanaume Halisi lililo chini ya Sir Juma Nature.Lakini kabla ya kujitoa gumzo kuelekea upande wake lilikuwa kuhusu wimbo wake wa hivi karibuni uitwao Ndoa Haina Doa.

Wimbo huu ni majibu ya wazi kwenda kwa MwanaFA ambaye hivi karibuni umekuwa sio tu msemo maarufu bali “kisingizio” cha vijana wengi kuhusu ndoa au mahusiano ya kudumu.Wimbo wa MwanaFA unaitwa Bado Nipo Nipo akiwa amemshirikisha mrembo Flaviana Matata katika kiitikio(chorus).Unaweza kuusikiliza wimbo wa MwanaFA kwa kubonyeza hapa na kisha kuusikiliza wimbo wa Ndoa Haina Doa kwa kubonyeza player hapo chini. 

NYOTA NJEMA YAANZA KUMUANGAZIA MIRIAM ODEMBA

Filed under: African Pride,Sanaa/Maonyesho,Urembo — bongocelebrity @ 9:39 AM

Mrembo Miriam Odemba(pichani) ambaye yuko nchini Philippines akiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth amefanikiwa kuingia katika tano bora katika shindano la kutafuta mrembo aliyependeza katika vazi la ufukweni katika kundi lake.

Mashindano haya yalijumuisha baadi tu ya warembo 90 ambao wanashiriki katika mashindano ya Miss Earth 2008 kwani fainali ya mashindano ya vazi la ufukweni yatafanyika tarehe 1 Novemba. Katika kundi lake, Miriam aliweza kuwapiku warembo wenzake takriban 30 kwa kupita jukwaani kwa kujiamini katika vazi hili la ufukweni.

Washindi wengine ni Columbia, France, Greece na Canada. Mshindi wa kwanza alikuwa Canada ambaye alijinyakulia zawadi ya dola 1,500.

 

WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAANDAMANA

Filed under: Watu na Matukio — bongocelebrity @ 5:57 AM

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wameandamana leo asubuhi jijini Dar es salaam,maandamano hayo yalianzia mtaa wa Lugoda na kuelekea wizara ya habari utamaduni na michezo,ambako walikabidhi barua kwa Waziri wa wizara hiyo Mh George Mkuchika,aidha madhumuni ya maandamano hayo yalikuwa ni kupinga kufungiwa kwa gazeti la mwanahalisi na serikali kwa muda wa miezi 3 na pia kuishinikiza serikali ifanye marekebisho ya sheria ya uhuru wa vyombo vya habari ya mwaka 1976