BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BAADA YA USHINDI,MANJI AUGUA October, 28, 2008

Filed under: Michezo,Wadhamini/Sponsors — bongocelebrity @ 10:25 PM

Siku moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu. SIKU moja baada ya kuishuhudia Yanga ikiichapa Simba bao 1-0, mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Pichani ni Mfadhili huyo,Yusuf Manji(kulia) akiwa na Rais Mstaafu wa Yanga,Francis Kifukwe(kushoto).Hii ilikuwa kwenye hafla ya kutiliana mkataba wa udhamini kati ya club za Yanga na Simba na kampuni ya bia nchini.TBL miezi michache iliyopita.

Picha na Issa Michuzi

Advertisements
 

18 Responses to “BAADA YA USHINDI,MANJI AUGUA”

 1. binti-mzuri Says:

  mh!ila BC na wewe bwana,kwahiyo jamii ina suggesti nini,kwamba karogwa?? wadau plz comment,mi nicheke leo,

 2. halima Says:

  Hakuamini kama ile kazi aliyomtuma yule refa amefanikisha kwani kama kuwa beba yanga aliwabeba sasa kile kipindi cha pili simba walipokuwa wamecharuka basi ndio pressure ilipoanzia pale duuh!!!!!

 3. DMX Says:

  Jamaa alifikiri ndala itatafunwa na mnyama ili asevu hela zake. kumbe watu wakafanya kweli maana akiondoka manji basi njaa imeingiya jangwani.

 4. Matty Says:

  kambi zenyewe za mazoezi zilikuwa Pemba vs Tanga kunani unasemaje hapo shosti Binti-mzuri??????
  Pole sana mdhamini Manji ugua pole!

 5. hombiz Says:

  I wish you a fast recovery ndugu Manji

 6. binti-mzuri Says:

  haha matty,speechless!

 7. EDWIN NDAKI Says:

  Pole Manji ndio marefa wa Tanzania yani milioni 20 mlikubaliana magoli mawili yeye kawapo goli moja na kutoa wachezaji wawili badala ya kumtoa na kipa..

  pole sana ndio watz..

 8. BLACKMANNEN Says:

  Kuugua ghafla kwa Manji, ni sawa na kuugua mtu yeyote. Msianze kuleta teoria au nadharia za mawazo ya kuzua hapa.

  Hongera Wana Yanga kwa ushindi wenu dhidi ya watani wenu Simba. Katika mashindano, ni lazima mshindi apatikane.

  Black=Blackmannen

 9. kahindi Says:

  mhh…kapigwa jinii….maskini manji,pole sana.

 10. Matty Says:

  Binti Mzuri na Kahindi mmemsikia BLACKMANNEN anvyosema???

 11. kahindi Says:

  matty nimempata…

 12. eve Says:

  Longo longo zote hizo ni simba tu kila anayetia doa lake baya ni simba mmeshindwa mnaanza maneno kwani mtu akiugua haponi nyie vip mtaishia kuuza maji ya viroba tu!!!!! mkalale hamna lolote mlienda uwanjani kuharibu nyasi zetu tu!!!!!.ugua pole bwana manji ndo upime akili za watz zilivyo kama gogo! ndo zao.usimaindi wala nini?

 13. halima Says:

  Baadhi ya wabunge wanataka mh. manji achunguzwe hizo hela anazowahonga yanga zinapatikanaje isijekuwa nayeye anaukoo na mafisadi baada ya kusikia hayo pressure ndipo ilipopandia hahahah

 14. binti-mzuri Says:

  hahahhaha!! blackmannen i agree with you, ila kwa jinsi kichwa cha habari kilivyowekwa.. na ndugu zetu huko nyumbani kwa kuzua…. hapo mtaani watu watakua wanasema karogwa tu huyo..haha ila nimecheka!

  kahindi bibie vp? katupiwa jini? LOOOL

  mi ngoja nicheke

 15. Bob Sambeke Says:

  E bwana c mchezo kuumwa kwa m2 ni kawaida,kwahyo no comment on that,get well soon,Billgate wa Bongo

 16. msema kweli Says:

  mkono wa mtu!

 17. michelle Says:

  wanataka kumnyorosa watchout now!!!!!!!!!!!!

 18. papuu Says:

  MNAOSEMA KAROGWA,MTAKUA MLIROGA NYIE


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s